Nyumbani » 08/03/2017 Entries posted on “Machi 8th, 2017”

Baraza la usalama lalaani urushwaji wa makombora wa DPRK

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama walipotoa azimio kulaani majaribio ya makombora iliyofanywa na Jamhuri ya kidemokrasia ya Korea au DPRK
Picha: UN/Rick Bajornas

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha faragha hivi leo na kupokea taarifa ya mkuu wa Idara ya maswala ya kisiasa Jeffrey Feltman kufuatia hatua ya hivi karibuni cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha makombora manne ya masafa marefu. Makombora matatu kati ya hayo yalitua baharini kwenye [...]

08/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwanasiasa msichana chipukizi alonga ''Wanawake msibweteke muhimu ni nidhamu''

Kusikiliza / Zainab Abdallah.(Picha:Z.Abdalla)

Tunapomulika siku ya wanawake duniani leo Machi nane, ni muhimu tumulike wanawake waliopiga hatua katika nyanja tofauti. Kutana na Zainab Abdallah Issa, mwanasiasa chipukizi nchini Tanzania na aliye mkuu wa wilaya mdogo zaidi. Aliteuliwa mwaka jana kuwa mkuu wa wilya ya Pangani akiwa na umri wa miaka 23, hatua iliyoshangaza wengi. Yeye anaiona kama fursa [...]

08/03/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani shambulizi kwenye hospitali mjini Kabul

Kusikiliza / Makao makuu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNAMA 
Picha: UNAMA/Fardin Waezi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulizi la kigaidi lenye utata lililotekelezwa mjini Kabul  asubuhi ya kuamkia hivi leo ambako wahusika waliovalia mavazi ya daktari walilipua gari la kujitoa mhanga katika mlango wa hospitali  ya Sardar Mohammad Daud Khan na kusababisha vifo na majeruhi ambapo, idadi kamili bado haijulikani. Naibu mkuu wa [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kidole kimoja hakivunji chawa,wanawake waambiwa waungane

Kusikiliza / Jiko 1

Kuwa na virusi vya Ukimwi VVU, haikuwazuia kikundi cha wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kujiendeleza kiuchumi. Ndivyo unavyoweza kusema ukitafakari juhudi za wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika, ambapo licha ya hali zao hizo za kiafya, wanawake katika kikundi kiitwacho GSV jimboni Kivu ya Kusini, wamenufaika kwa mradi wa majiko. Langi Stany [...]

08/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia ni suluhu ya 50/50 ifikapo 2030- UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres katika ujumbe wa video. Picha: UM/Video Capture

Ikiwa leo ni siku ya wanawake duniani ujumbe ukiangazia wanawake katika mazingira yanayobadilika ya kazi, kuelekea usawa wa kijinsia mwaka 2030, Umoja wa Mataifa umetaka ushiriki wa wanawake kikamilifu ili kufanikisha azma hiyo. Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Nats.. Kibao hicho I will rise up kiliporomoshwa na mwimbaji mwenye kipaji Jana Brown kwenye moja ya [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa yaheshimu faragha mitandaoni-UM

Kusikiliza / Picha:UN Photo/JC McIlwaine

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataiafa kuhusu haki ya faragha, Joseph Cannataci, amelaani sheria ya upekuzi na kuyataka mataifa kote ulimwenguni kuheshimu haki ya faragha ambayo amsema ni haki ya kimataifa katika zama hizi za kidijitali. Kupitia ripoti yake aliyowasilisha hii leo mjini Geneva Uswisi kwenye baraza la haki za binadamu, Bwana Cannataci ameeleza kusikitishwa [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake shupavu waenziwa Uganda

Kusikiliza / Picha: UNFPA

Uganda nayo imejiunga na Dunia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambako wanawake zaidi ya hamsini wamepatiwa medali ya kuwaenzi kwa ushupavu wao katika nyanja mbalimbali. Shuhuda wetu hujo ni John Kibego. (TAARIFA YA KIBEGO) Nats! Miongoni mwa waliopatiwa midali ni mwanajeshi mwanmke wa cheo cha juu zaidi katika historia ye jeshi la Uganda.  Huenda [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia ni chachu katika kukomesha njaa na umasikini-UM

Kusikiliza / Mchango wa wanawake wa vijijini katika uhakika wa chakula haupaswi kupuuzwa.(Picha:FAO-WFP/Ricci Shryock)

Shirika la chakula na kilimo FAO kwa ushirikino na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, wamechagiza juhudi katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake hasa wa vijijini, masuala ambayo wanasema ni chachu ya kukomesha njaa , utapia mlo na umasikini. Kauli hiyo imetolewa kwenye [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku moja nitakuwa mwanamke mahiri duniani-Zainabu

Kusikiliza / Zainab Abdallah.(Picha:Z.Abdalla)

Zainab Abdallah Issa ndiye mkuu wa wilaya mdogo zaidi nchini Tanzania akiwa na umri wa miaka 24. Aliteuliwa na Rais wa nchi hiyo kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya ya Pangani mwaka jana akiwa na umri wa miaka 23. Katika mahojiano na Kelvin Mpinga wa redio washirika Pangani Fm ya Tanga Tanzania, aliyetaka kufahamu [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii zetu zitakuwa thabiti iwapo tutashirikisha wanawake- Guterres

Kusikiliza / Picha: Julius Mwelu - UN Habitat

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ulinzi wa wanawake dhidi ya ukiukwaji wa haki zao pamoja na umaskini vitawezekana iwapo watapatiwa kipaumbele kamilifu kwenye mipango ya kuwawezesha. Akizungumza mjini Nairobi, Kenya ambako yuko ziarani, Bwana Guterres amesema ujumuishaji huo uhakikishe wamo kwenye taasisi za serikali, siasa na biashara bila kusahau bodi za [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika ionekane kama bara la mafanikio sio matatizo tu-Guterres

Kusikiliza / KENYA

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres anayeendelea na ziara yake nchini Kenya amesema anaamini kwamba simulizi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika haijakuwa sawa wakati wote, kwani wakati mwingine imejikita sana katika mogogoro . Akiongeza kuwa ni kweli kwamba kuna migogoro Afrika kama ilivyo barani Ulaya au Asia, kuna migogoro kila kona, akasisitiza [...]

08/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jumuisha sauti za wanawake kwenye mchakato amani Maziwa Makuu- Djinnit

Kusikiliza / Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Said Djinnit akuhutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Kujumuisha wanawake katika mchakato wa amani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika ni muhimu kwa kuwa inaleta maslahi mengi na endelevu kwa jamii na mataifa kwa ujumla. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo Said Djinnit ametoa wito huo leo ikiwa ni siku ya wanawake duniani akisema ili kuondoa mzizi wa mzozo [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna kazi ya mwanamke au mwanaume kazi ni kazi

Kusikiliza / Mariana Tarimo (Kushoto) mfanyakazi wa UN Women nchini Tanzania na Mariana Msale dereva wa UN women Tanzania. Picha: UNIC Tanzania/Video capture

Ingawa mabadiliko ya fikra duniani yanaanza kujitokeza sanjari na mabadiliko ya ulimwengu wa kazi, bado kuna dhana kwamba kuna ajira ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume tu na ni nadra kumkuta mwanamke akifanya mathalani kuwa dereva. Lakini dhana hiyo imekuwa potofu kwa Mariana Tarimo anayefanya kazi na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

Sera zinazojali jinsia zimeleta mafanikio kwa kampuni- UNWomen

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen Phumzile Mlambo-Ngucka nchini Sweden azungumza kuhusu uwezeshaji wa wanawake.  Picha: UN Women

Kampuni zinazoajiri wafanyakazi kwa kuzingatia sera za usawa wa kijinsia zimedhihirisha jinsi mwelekeo huo ulivyo na manufaa kwa maendeleo ya kampuni husika. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen Phumzile Mlambo-Ngucka amesema hayo akihojiwa na radio ya huo katika maadhimsisho ya siku ya wanawake duniani hii leo. Amesema [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031