Nyumbani » 07/03/2017 Entries posted on “Machi 7th, 2017”

Kila mtoto anastahili kuishi kwa usalama: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto pekee yake kwenye safari kusaka usalama
Picha: UNICEF/UN030740/Zehbrauskas

  Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake amesema kuwa watoto wakimbizi wanaokimbia machafuko na ugaidi hivi sasa wanahitaji msaada kuliko wakati mwingine wowote. Lake ametoa kauli hiyo kufuatia  amri mpya nyingine ya Marekani iliyotolewa  Jumatatu kuhusu wanaosaka hifadhi na ukimbizi. Amesema watoto ni miongoni mwa watu wanaoishi [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM na AU wazindua ripoti ya haki za wanawake Afrika

Kusikiliza / Wanafunzi nchini Kenya. Picha: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa , Muungano wa Afrika na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women, leo wamezindua ripoti kuhusu haki za wanawake Afrika. Hii ni ripoti ya kwanza katika mfululizo uliopangwa kuhusu haki za wanawake katika bara hilo itaklayojikita katika mada mbalimbali. Mashirika hayo [...]

07/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dola Bilioni 2 zahitajika kusaidia Kenya, Ethiopia na Somalia: UM

Kusikiliza / Mama na mtoto wake ni miongoni mwa raia wa Somalia wanaokumbwa na uhaba wa njaa
Picha: UN/OCHA

Zaidi ya dola bilioni 2 zinahitajika kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Kenya, Somalia na Ethiopia mwaka huu wa 2017. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya naibu wa msemaji wa ofisi ya masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Jens Laerke. Kwa upande wa Somalia pekee msemaji huo amekaribisha mchango wa dola milioni [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake Uganda wajitosa kwenye ufundi kujipatia kipato.

Kusikiliza / Wanawake wajasiriamali nchini Uganda. Picha: UN Women/Video capture

Wanawake nchini Uganda kama zilivyo sehemu nyingine, wanajitutumua kukabiliana na changamaoto za kazi katika ulimengu unaobadilika ili kujipatia kipato na pia kutimiza malengo ya usawa wa 50 kwa 50 kifikapo mwaka 2030. Katika pitapita yake kutathimini kazi hizo kuelekea siku ya wanawake duniani Machi nane, John Kibego kutoka Uganda amekutana na mwanamke ambaye ndiye chanzo [...]

07/03/2017 | Jamii: Makala za wiki, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

SDGs bila takwimu haiwezekani: Montiel

Kusikiliza / ASG Stats

Ikiongozwa na kauli mbiu, takwimu bora maisha bora, tume ya takwimu ya Umoja wa Mataifa imeanza kikao chake cha 48 hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika idara ya uchumi na masuala ya kijamii [...]

07/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Amerika himizeni kujihami na majanga: UM

Kusikiliza / Familia katika Idara ya Grand'Anse waliopoteza mali yao baada ya kimbunga Mathew. Picha: © EU/ECHO/J. Torres

Majanga kama vile kimbunga Matthew yaliyokumba bara Amerika miaka ya hivi karibuni, ni udhihirisho wa changamoto zinazokabili dunia katika kufikia malengo ya mkataba wa Sendai wa kupunguza majanga. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza majanga UNISDR Robert Glasser amesema hayo hii leo wakati akifungua mkutano wa tano kuhusu kupunguza majanga barani Amerika [...]

07/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake waongezeka katika mabunge, kasi zaidi yahitajika: IPU

Kusikiliza / Ripoti ya IPU kuhusu yaliyojiri mwaka jana. Picha: IPU

Hatua zaidi na utashi thabiti wa kisiasa unahitajika, kuwezesha uwakilishi wa wanawake bungeni ili kuendeleza kasi ya maendeleo yaliyofikiwa duniani katikaa kipindi cha muongo mmoja uliopita, umesema muungano wa mabunge duniani IPU. Katika ripoti ya IPU kuhusu tathimini ya mwaka huu iitwayo Wanawake bungeni 2016, iliyotolewa kuelekea siku ya wanawake duniani Machi nane hapo kesho, [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

Mipango ya Hungary kuwashikilia waomba hifadhi yatia hofu:UNHCR

Kusikiliza / Wahamiaji kutoka Pakistani huko Kos, Ugiriki waonyesha ramani waliyopokea kuhusu kufungwa kwa mpaka wa Hungary na ikipendekeza kupitia Croatia. Picha: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa hofu na sheria mpya iliyopigiwa kura jumanne kwenye bunge la Hungary ambayo itafanya kuwa lazima kuwashikilia waomba hifadhi wote wakiwemo watoto kwa kipindi chote cha mchakato wa kuomba hifadhi. Kwa mujibu wa UNHCR hii inamaanisha kwamba kila muomba hifadhi wakiwemo watoto watazuiliwa kwenye makontena [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upinzani dhidi ya haki za wanawake hutuathiri sote- Zeid

Kusikiliza / Wanawake na wasichana katika sekta ya nguo mara nyingi hunyanyazwa na kulazimishwa kufanya kazi masaa mingi kupita ya kawaida bila kulipwa. Picha: ILO/A. Khemka

Inasikitisha sana kuona mafanikio yaliyopatikana kuhusu haki za wanawake, yaanza kurudishwa nyuma katika baadhi ya maeneo duniani, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein katika ujumbe wake kuelekea siku ya wanawake duniani siku ya Jumatano. Rosemary Musumba na ripoti kamili. (Taarifa ya Rosemary) Kamishna Zeid amesema mamilioni ya wanawake walijitoa maisha [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukarabati wa barabara inayounganisha DRC na Burundi waanza

Kusikiliza / ukarabati wa barabara inayounganisha jimbo la Kivu Kusini na Burundi kupitia Uvira nchini DRC. Picha: MONUSCO

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO umeanza ukarabati wa barabara inayounganisha jimbo la Kivu Kusini na Burundi kupitia Uvira. Ukarabati wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa Sita utafanyika kwa siku 50 na hivyo kumaliza adha ya usafiri ambapo wananchi walitumia nusu saa kwa gari kusafiri [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzizi wa ubaguzi wa wanawake bado unamea- Wataalamu

Kusikiliza / Wanawake wakiandamana jijini New York kwa ajili ya kuchagiza usawa wakijinsia.(Picha:UN Women/J Carrier)

Harakati za kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake zimeendelea kugonga mwamba licha ya mafanikio katika baadhi ya maeneo tangu kuanza kwa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani zaidi ya karne moja iliyopita. Hiyo ni kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wanawake waliokutana leo huko Geneva, Uswisi kuangazia siku ya wanawake itakayoadhimisha [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viuatilifu vinatishia haki za binadamu- Wataalamu

Kusikiliza / Matumizi ya madawa hatari shambani yana athari kwa binadamu.(PichaFAO/Asim Hafee)

Wataalamu wawili maalum wa Umoja wa Mataifa wametaka kuwepo kwa mkataba mpya wa kimataifa utakaodhibiti na kuondokana na viuatilifu au madawa hatari yanayotumika mashambani. Wataalamu hao Hilal Ever wa haki za chakula na Baskut Tuncak anayeangazia masuala ya sumu wamelieleza Baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi kuwa matumizi kupita kiasi ya viuatilifu kwa [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Niko Somalia kuonyesha mshikamano wangu:Guterres

Kusikiliza / SG SOMALIA 3

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Somalia, akizuru Moghadishu na Baidoa kwa mara ya kwanza akiwa katika wadhifa huo ili kuonyesha mshikamano na watu wa taifa hilo ambao amesema wako katika hali ya madhila lakini pia matumaini. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Amesema wako katika madhila kutokana na [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Stadi za kazi kambini zamwezesha mkimbizi mwanamke kujikimu

Kusikiliza / Finess-1

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe 08 mwezi huu wa machi, mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Burundi ameelezea vile ambavyo stadi za kazi kambini zimemwezesha kuungana tena na familia yake. Mahimana Faines ambaye sasa anaishi kambi ya wakimbizi ya Lusenda nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC amesema anasema kupitia kituo salama kambini Lusenda alipata taarifa [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031