Nyumbani » 06/03/2017 Entries posted on “Machi 6th, 2017”

Guterres alaani kitendo cha DPRK kurusha makombora

Kusikiliza / Katibu mkuu António Guterres
Picha: UN/Rick Bajornas

Secretary-General António Guterres. UN Photo/Rick Bajornas

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani kitendo kilichoripotiwa cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha makombora manne ya masafa marefu. Imeelezwa kuwa makombora matatu kati ya hayo manne yametua baharini kwenye ukanda mahsusi wa kiuchumi wa Japan. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Katibu Mkuu akisema vitendo vya namna [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marekani yatoa kanuni mpya za ukimbizi, UNHCR yasisitiza misingi ni ileile

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi .(Picha:UM/Evan Schneider)

Kufuatia amri mpya ya Marekani ilyotolewa leo kuhusu wanaosaka hifadhi ya ukimbizi nchini humo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesisitiza kuwa wakimbizi ni watu wa kawaida wanaokimbia vita, ghasia au mateso na bado wanasalia na umuhimu wa kupatiwa hifadhi na ulinzi. Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema nia inasalia ile [...]

06/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

MINUSMA yalaani ukiukwaji wa kusitisha mapigano Timbuktu Mali

Kusikiliza / Picha: UN video capture

  Vituo viwili vya kijeshi vilivyokuwa vinashika doria vimeshambulia  jana jumapili na kikundi cha waasi wenye silaha huko kaskazini mwa mji wa Timbuktu nchini Mali. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA ambao unasema kuwa vikundi hivi vyenye silaha vinapinga uanzishwaji wa serikali ya mpito ya Taoudenit, [...]

06/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasomali wanahaha kukidhi mahitaji ya mlo kwa familia- O’Brien

Kusikiliza / O'Brian

  Mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien ametembelea makazi ya muda ya wakimbizi wa ndani yaliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambako amejionea hali halisi ya njaa inayokabili nchi hiyo. Ameshuhudia jinsi familia zinavyohaha kukidhi mahitaji ya mlo ya watoto wao akisema kwa kujionea mwenyewe, amepata [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makumbi ya nazi huniingizia kipato na kuwasomesha watoto-Bahati

Kusikiliza / Bahati Sudi ambaye ni mjasiriamali nchini Tanzania.(Picha:Maajabu Ally)

Makumbi ya nazi ambayo mara nyingi hutupwa baada ya kufuliwa kwa nazi, na hivyo kusababisha uchafu wa mazingira, yanatumiwa na mjasiriamali mwanamke mkoani Tanga nchini Tanzania, kujinufaisha kwa kipato na hivyo kutunza mazingira. Hii ni sehemu ya shuhuda za wanawake kuhusu namna wanavyokabiliana na changamoto za kazi katika dunia inayobadilika kila uchao, ikiwa ni kuelekea [...]

06/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Haiti inahitaji msaada wa ujenzi mpya-UNISDR

Kusikiliza / Athari za madhara ya Kimbunga Mathew ni dhahiri nchini Haiti.(Picha:Logan Abassi UN/MINUSTAH)

Wito wa msaada wa ujenzi mpya kwa ajili ya Haiti umetolewa jumatatu na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa athari za majanga UNISDR baada ya kimbunga Matthew kuliacha taifa hilo na hasara ya dola bilioni 2.7. Rosemary Musumba na taarifa kamili. (TAARIFA YA ROSE) Msaada huo wa haraka ni kwa ajili ya [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA bado ina hofu kuhusu DPRK

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Dkt. Yukiya Amano.(Picha:IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Dkt. Yukiya Amano ameseam bado ana wasiwasi mkubwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK wakati huu ambapo vyombo vya habari vinaripoti kuwa nchi hiyo siku ya jumapili imefyatua makombora manne ya masafa marefu. Akihutubia mkutano wa bodi [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania inajitahidi katika vita dhidi ya mihadarati:UM

Kusikiliza / Madawa ya kulevya kutumika licha ya vikwazo.Picha: UNIC/Tanzania

Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania jumatatu wamezindua ripoti kuhusu matumizi ya dawa za kulevya iliyotolewa na bodi ya kimataifa ya kuzuia dawa za kulevya INCB kwa mwaka 2016. Ripoti hiyo imejikita na athari na matumizi ya dawa hizo kwa wanawake,, akiizungumzia mjini Dar Es salaam Tanzania Mratibu mkazi wa Umoja wa [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EU yapigia chepuo mlo shuleni nchini Burundi

Kusikiliza / Watoto nchini Burundi wanaopokea mlo shuleni.(Picha:WFP/Didier Bukuru)

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limekaribisha msaada wa zaidi ya dola milioni Tano kutoka Muungano wa Ulaya, EU kwa ajili ya mradi wa mlo shuleni nchini Burundi. Mwakilishi mkazi wa WFP nchini Burundi Charles Vincent amesema fedha hizo zitaelekezwa jimbo la Gitega, katikati mwa nchi ambako siyo tu zitaimarisha uwezo wa watoto shuleni, [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wajumuishwe ajenda 2030- Gilmore

Kusikiliza / Ni muhimu watoto kama hawa walioko nchini Mali wajumuishwe katika ajenda 2030.(Picha:UM/Marco Dormino)

Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Kate Gilmore amesema mustakhbali bora wa dunia unawezekana iwapo masuala ya watoto yatapatiwa kipaumbele wakati wowote wa kujadili amani na maendeleo. Amesema hayo wakati akifungua sehemu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa baraza hilo kuhusu haki za mtoto huko Geneva, Uswisi akisema hivi [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchafuzi wa hewa huua watoto, jihadhari: WHO

Kusikiliza / Watoto nchini Papua Guinea Picha na Y. Shimizu/WHO

Kama ulifikiri magonjwa ndio sababu pekee ya vifo kwa watoto chini ya miaka mitano, sivyo! Mazingira hususani uchafuzi wa hewa ndani au nje ya nyumba , moshi umpatao asiyevuta tumbaku, ni mongoni mwa sababu ya kifo cha mtoto mmoja kati ya watano limesema shirika la afya ulimwenguni WHO. Amina Hassan na maelezo kamili. ( TAARIFA [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031