Nyumbani » 03/03/2017 Entries posted on “Machi 3rd, 2017”

Tofauti za wakazi wa Timbuktu haziwazuii kukarabati msikiti wao

dua

Nchini Mali kwenye mji wa Timbuktu, wakazi wa eneo hilo wameamua kufanya msaragambo kila mwaka kwa karne saba sasa kukarabati msikiti wao.

03/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kutana na Adian Coker, mwanamuziki anayekataa ubaguzi

Kusikiliza / Mwanamuziki mkazi wa Uingereza. Picha: UNAIDS/Video capture

Burudani na ujumbe! Ndivyo unavyoweza kusema ukitafakari ushairi wenye vina unaeleta hisia za ujumbe kuhusu kupinga ubaguzi wa kila aina. Huu ni ujumbe wa mwanamuziki Adina Coker mkazi wa Uingereza ambaye ameamua kuingia vitani dhidi ya ubaguzi sambamba na Umoja wa Mataifa unaopinga dhana hiyo.Ungana na Assumpta Massoi katika midundo hiyo.

03/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhai wa wanyamapori ni uhai wetu- UNEP

Kusikiliza / Tempo wanaopatikana barani Africa. Picha:  World Bank/Curt Carnemark

Tarehe tatu mwezi Machi ya kila mwaka ni siku ya wanayamapori duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kusikiliza sauti za vijana ambao wana fursa ya kuhakikisha urithi wa wanyamapori kwa vizazi vijavyo. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP, kuwaenzi wanyamapori na maliasili ambalo ni jumuku la serikali na sekta [...]

03/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki – Si ndiyo

Kusikiliza / Leo tunaangazia neno la wiki na neno hilo ni "si ndiyo" mchambuzi ni Nuhu Zubeir Bakari kutoka CHAKITA nchini Kenya. (Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Katika neno la wiki Februari 3 tunachambua neno si ndiyo, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Bwana Nuhu anasema kuwa “si ndiyo” ni semi ambayo moja ni kikanushi na moja ni ya kukubali, hivyo mtu anapotumia maneno [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wanaotawanywa na machafuko kwa siku Mosul ni 4,000

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani waliotawanywa Mosoul Iraq kutokana na operesheni za kijeshi zinazoendelea dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL.  Picha: UNHCR/Caroline Gluk

Idadi ya watu wanaotawanywa kwa siku Mosoul Iraq kutokana na operesheni za kijeshi zinazoendelea dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL na hofu ya matumizi ya silaha za ckemikali dhidi ya raia imeongezeka sana. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR sasa watu 4000 kwa siku wanakimbia kutoka Magharibi mwa [...]

03/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunza sikio kama yai kwani likishaharibika ndio basi- WHO

Kusikiliza / Picha: WHO

Zaidi ya asilimia tato ya watu wote duniani wanaishi na tatizo la kupoteza uwezo wa masikio kusikia, lakini kuzuia tatizo hilo ni rahisi kuliko kuitibu. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO katika ujumbe wake kuhusu siku siku ya kimataifa ya uwezo wa masikio kuiskia duniani . Kauli mbiu mwaka huu ikiwa [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mganga wa jadi na askofu akutwa na hatia ya mauaji ya albino Afrika Kusini

Kusikiliza / Haki za albino. Picha: UNHRC

Nchini Afrika Kusini mganga wa jadi ambaye pia ni askofu wa kanisa amepatikana na hatia ya kuwa kinara wa mauaji ya albino, hatua ambayo imepongezwa na Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Ushahidi uliowasilishwa mahakamani ulithibitisha pasipo shaka kuwa kinara huyo Bhekukufa Gumede mkazi wa Kwa-Zulu Natal nchini Afrika Kusini [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubunifu wabadili fikra za wadau wa SDG’s

Kusikiliza / Tamasha la Kimataifa la Fikra jijini Bonn, Ujerumani. Picha: UM

Tamasha la Kimataifa la Fikra linakunja jamvi leo jijini Bonn, Ujerumani ambapo watunga sera, asasi za kiraia na makampuni binafsi wameshiriki katika mchezo wa kidigitali uitwao # 2030 HIVE MIND” ili kusongesha mbele malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s. Mwandishi wetu Amina Hassan anaripoti kutoka Bonn. (Taarifa ya Amina) Ni washiriki wakijikita katika awamu ya mwisho [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muenzini Maathai kwa kuhifadhi mazingira : UNEP

Kusikiliza / Profesa Wangari Maathai (kati) akishiriki kwenye upandaji wa miti nchini New York. Picha(maktaba): UN Photo/Evan Schneider

Leo ni siku ya mazingira barani Afrika, siku ambayo pia imepewa heshima ya kuitwa siku ya Wangari Maathai,mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya ambaye enzi za uhai wake alipigia chepuo uhifadhi wa mazingira. Kupitia wavuti wake hii leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP, limezitaka nchi za Afrika kuainisha mafaniko katika uhifadhi [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria kali zahitajika kulinda wanyamapori- UM

Kusikiliza / Ndovu-2

Leo ni siku ya wanyamapori duniani, inayotumiwa kukuza uelewa kuhusu wanyama pori na mali asili kwa lengo la kuhifadhi viumbe hao. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kusikiliza sauti za vijana. Rosemary Musumba na maelezo zaidi. (TAARIFA YA ROSE) Hawa ni ndovu, moja ya wanyama vivutio duniani, lakini wanyama hawa wanakabiliwa na tishio la kutoweka [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031