Nyumbani » 02/03/2017 Entries posted on “Machi 2nd, 2017”

Bila elimu bure sisi tusingesoma-Wasichana Uganda

Kusikiliza / Wanafunzi darasani. Picha: UNICEF

Katika kutimiza lendo namba nne la maendeleo endelevu SDGs, linalotaka uwepo wa usawa katika elimu, Uganda imepiga hatua kwa kuhakikisha elimu bure hatua iliyowezesha wale wasiojiweza kwenda shule. Ungana na John Kibego ambaye amefuatailia upatikanaji wa elimu nchini humo ambapo pia amezungumza na wanufaika wa mpango huo.

02/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa jamii za asili Australia wakabiliwa na ukatili mkubwa:UM

Kusikiliza / Dubruvka Šimonović na Christopher Woodthorpe. UNIC Canberra/Julia Dean

Mifumo mkingi ya ubaguzi imechochea kiwango kikubwa cha ukatili unaowakabili wanawake kutoka jamii za watu wa asili nchini austarlia. Hayo ni kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonović . Bi Šimonović ambaye amekamilisha ziara nchini humo amesema wanawake wengi wanabaguliwa kimaumbile na kukabiliwa na ubaguzi wa [...]

02/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya tabia nchi huathiri watoto zaidi:UM

Kusikiliza / Naibu mwakilishi wa kudumu wa Ufilipino, Maria Teresa Almojuela (kati). Picha: UM/Video capture

Mabadiliko ya tabia nchi yanatoa tishio kubwa kwa watoto, limeelezwa baraza la haki za binadamu Alhamisi. Katika mjadala uliofanyika Geneva, nchi wanachama na wataalamu wa haki za binadamu wameonya kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanatishia mafanikio ya vijana katika fursa ya chakula, maji , afya na elimu. Na suluhu kwa mujibu wa wataalamu hao ni [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kismaayo yapata kituo cha kujenga stadi za vijana

Kusikiliza / Kituo cha kusaidia kuwajumuisha kwenye jamii, DDR, wapiganaji wa zamani wa kikundi cha kigaidi cha Al –Shabaab kinafunguliwa Kismaayo cnhini Somalia.  Picha: UNSOM

Hii leo huko Kismaayo ambao ni mji mkuu wa muda wa jimbo la Jubaland nchini Somalia, kimefunguliwa rasmi kituo cha kusaidia kuwajumuisha kwenye jamii, DDR, wapiganaji wa zamani wa kikundi cha kigaidi cha Al –Shabaab. Kituo hicho ni cha nne kufunguliwa nchini humo kama sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuwapatia tiba na kuwalea wapiganaji [...]

02/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mavuno ni mengi lakini baa la njaa lashika kasi- FAO

Kusikiliza / Mkulima anakata mihogo. Picha: FAO

Hali ya usambazaji chakula kote duniani imeimarika lakini upatikanaji wa chakula umepungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo yanayokabiliwa na mgogoro huku ukame ukizidi kudororesha uhakika wa chakula katika nchi za Afrika Mashiriki. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO kwenye ripoti yake mpya kuhusu matarajio na mwelekeo [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatutafikia SGD’s iwapo hatutayawasilisha kwa kila mtu

Kusikiliza / Picha: UM

Tamasha la Kimataifa kuhusu Fikra linaendelea jijini Bonn, Ujerumani ambapo mada kuu iliyojadiliwa leo ni umuhimu wa utoaji wa habari na uwasilishaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye idara ya habari na mawasiliano , Cristina Gallach amenieleza kuwa [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wapatiwe tiba sahihi dhidi ya madawa ya kulevya- Ripoti

Kusikiliza / Mwanamke anavuta afyuni nchini Thailand kwa njia ya kidesturi ya kulala. Picha: UN Photo/D Gair

Ripoti ya mwaka 2016 ya Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya, INCB, imezinduliwa hii leo ambapo pamoja na mambo mengine imetaka serikali duniani zihakikishe kuwa sera zinazolenga udhibiti wa matumizi ya mihadarati zinajumuisha wanawake wakati huu ambapo idadi ya wanawake wanaotumia madawa hayo imeongezeka. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Ripoti [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Afrika ya mlo shuleni yaadhimishwa Brazzaville: WFP

Kusikiliza / Picha: WFP

Siku ya Afrika ya mlo shuleni imezinduliwa rasmi na kuadhimishwa Machi mosi 2017 chini ya ulezi wa serikali ya Jamhuri ya Congo Brazzavile , ikiwa na kauli mbiu "Ulishaji mashuleni, ni uwekezaji kwa vijana kwa ajili ya kuimarisha mustakhbali wao" Rosemary Musumba na taarifa kamili (TAARIFA YA ROSE) Kwa mujibu wa shirika la mpango wa [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame ni janga la kitaifa Somalia: Rais Farmaajo

Kusikiliza / Picha: UNSOM

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmaajo ambaye aliapishwa hivi karibuni ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia taifa lake kukabiliana na ukame ulioathiri zaidi ya raia milioni sita. Akizungumza mjini Mogadishu kwenye mkutano wa ngazi ya juu kwa ajili ya ukame ambao amesema ni janga la kitaifa, Rais Farmaajo ameomba jumuiya hiyo kuongeza mchango [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031