Nyumbani » 01/03/2017 Entries posted on “Machi 1st, 2017”

ITC kuinua wanawake kiuchumi Rwanda

Kusikiliza / Kahawa kama hii isiyoongezewa thamani, bei yake iko hatarini kuyumba. (Picha:UN Photo/Martine Perret)

Kituo cha kimataifa cha biashara ITC ambayo ni taasisi tanzu ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD na wadau, hii leo wametangaza ushirikiano mpya ili kusaidia wauzaji wa kahawa nje ya nchi, wasindikaji, na wakulima wa zao la buni nchini Rwanda. Ushirikiano huo unalenga uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ambapo uboreshaji uwezo wa [...]

01/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya Yemen bado ni tete:O'Brien

Mratibu wa Masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Steohen O'Brien. Picha na UM

Hali ya kibinadamu nchini Yemen bado ni tete na mamilioni ya watu wanahitaji msaada wa haraka hasa katika maeneo ya Kaskazini ambako hali ya usalama ni mbaya zaidi. Akizungumza kwa jia ya video kutoka mjini Saana, Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien amesema alipata fursa ya [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi dhidi ya Allepo ni uhalifu wa kivita: Ripoti

Kusikiliza /

Mapigano ya kuudhibiti mji wa Aleppo nchini Syria mwaka jana, yamesababisha mateso makali yanayochochea uhalifu wa kivita wameonya leo wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Ikitumia shuhuda 300 za picha za setilaiti na sauti nyingine, ripoti ya kamisheni ya uchunguzi imeonyesha jinsi gani ndege za kivita za Syria na Urusi zilivyogeuza Mashariki [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machungu kabla ya kunyongwa ni makubwa- Zeid

Kusikiliza / adhabu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad al Hussein amesema madhila wanayokumbana nayo wafungwa wanaosubiri adhabu ya kifo ni miongoni mwa sababu tosha za kuweza kuondokana na adhabu hiyo. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi wakati wa kikao cha ngazi ya juu kuhusu hoja ya adhabu ya kifo ambapo sasa Umoja wa [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Soko la nyumba halizingatii haki za binadamu:UM

Makazi-2

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya nyumba, Leilani Farha,  ameonya juu ya ukuaji wa soko la nyumba za kibiashara bila kujali haki za binadamu, halikadhalika ongezeko la gharama zake kiasi cha watu wengi kutomudu. Akitoa ripoti yake ya hivi karibuni kwa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, [...]

01/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taarifa kuhusu chanjo zinapotoshwa- WHO

Kusikiliza / Chanjo. (Picha: MAKTABA:UN/JC McIlwaine)

  Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema linatiwa wasiwasi na upotoshwaji  wa habari kuhusu kinga kupitia tovuti kadhaa hatua ambayo shirika hilo imeliita hatari na kutaka wadau kupata taarifa sahihi. John Kibego na taarifa kamili. (TAARIFA YA KIBEGO) Katika kuhakikisha taarifa sahihi, WHO imeanzisha wavuti wa kimataifa kuhusu usalama wa chanjo uitwao VSN, ambao hadi [...]

01/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tamasha la Fikra lafungua pazia leo huko Bonn

Kusikiliza / tamasha-2

Tamasha la siku tatu lenye  lengo la kuchagiza mawazo mapya katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s lmeanza leo jijini Bonn, Ujerumani ambako mwandishi wetu Amina Hassan amepiga kambi na ametuletea ripoti hii. (Taarifa ya Amina) Akifungua tamasha hilo lijulikanalo kama “Tamasha la Kimataifa la Fikra” ambalo limeleta pamoja watunga sera, asasi za kiraia, vijana [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyongeza ya dola milioni 130 kusaidia miundombinu Tanzania- Benki ya dunia

vituo2

Benki ya dunia imeidhinisha nyongeza ya dola milioni 130 kwa ajili ya mradi wa Tanzania wa kuboresha miji, TSCP kupitia uimarishaji wa miundombinu. Miji itakayonufaika ni Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Dodoma, Mbeya na Mtwara na lengo ni kuwezesha miji hiyo kuendana na kasi ukuaji wa miji. Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za [...]

01/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Dineo chaathiri maelfu Msumbiji:UM

Kasi ya kimbunga. (picha:Maktaba)

Kimbunga Dineo kiliwasili kwenye pwani ya jimbo la Inhambane Kusini mwa Msumbiji  wiki iliyopita kikiambatana na upepo mkali , na kisha kikaelekea Afrika Kusini na Zimbabwe, imesema timu ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Familia zaidi ya laki moja zimeathirika huku 7651 kati yao zikiwa katika hali mbaya. Nyumba zaidi ya elfu 33 zimesambaratishwa kabisa [...]

01/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya serikali vimekiuka haki za binadamu DRC: UM

Kusikiliza / Vurugu-2

Vikosi vya ulinzi na usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC vilitumia nguvu kupita kiasi, isiyohitajika na hata silaha ili kudhibiti maandamano mwezi desemba mwaka 2016 , imebaini ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa Jumatano. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya ofisi ya pamoja ya haki za binadamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatutashinda kwa kubagua wengine- UNAIDS

Kusikiliza / Pazasauti2

Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga aina zote za ubaguzi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi, UNAIDS limesema maudhi ya mwaka huu yanasihi kila mtu apaze sauti ili kupinga ubaguzi wa aina mbalimbali ikiwemo dhidi ya watu wenye virusi vya Ukimwi, VVU, au Ukimwi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031