Nyumbani » 31/03/2017 Entries posted on “Machi, 2017”

Miili ya wahudumu wa misaada ya kibinadamu kutoka Kenya waliouawa Sudan Kusini kusafirishwa

Kusikiliza / Eneo walikoshambuliwa watoa huduma huko nchini Sudan Kusini.(Picha:Isaac Billy/ UNMISS)

Waziri wa mambo ya nje wa Kenya Bi Amina Mohamed Ijumaa ametangaza kwamba miili ya wahudumu wa misaada watatu kutoka Kenya waliouawa mwishoni wa wiki iliyopita nchini Sudan kusini itasafirishwa kesho Jumamosi kutoka Juba na kurejeshwa nyumbani Kenya. Ubalozi wa Kenya Juba na ubalozi wa Sudan Kusini Nairobi wanashirikiana kuratibu zoezi hilo. Wahudumu hao ni [...]

31/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa kifua kikuu, changamoto na tiba

Kusikiliza / TB ni ugonjwa ambao unaambukiza na kinga ni muhimu.(Picha:UNifeed/video capture)

Kifua kikuu au TB!Gonjwa lililoorodheshwa na shirika la afya ulimwengni WHO kuwa miongoni mwa magonjwa 10 yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani. WHO inasema mathalani mwaka 2015 watu milioni 10.4 waliugua ugonjwa huo, milioni 1.8 walifariki duniani, wakiwemo takribari watu Laki tano ambao walikuwa na virusi vya Ukimwi, VVU. Miongoni mwa waathirika ni kundi la wahamiaji [...]

31/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanamuziki wapazia kilio cha Yemen

Kusikiliza / Makala-2

Nchini Yemen, mapigano yaliyoanza miaka miwili iliyopita, yamekuwa mwiba siyo tu kwa raia bali pia kwa wale wanaotumia nchi hiyo kama njia ya kupitia kuvuka ghuba ya Aden na bahari ya Sham kwenda nchi nyingine. Wakimbizi na wahamiaji wanakumbwa na majanga kama vile kutekwa, kutumikishwa na hata wengine kukosa chakula na huduma za msingi. Wengine [...]

31/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Muda wa MONUSCO waongezwa hadi 2018, askari wapunguzwa

Kusikiliza / Mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley akihutubia kikao hicho.(Picha:UM//Rick Bajornas)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloongeza muda wa ujumbe wa umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO hadi tarehe 31 mwezi Machi mwakani. Pamoja na kuongeza muda wa ujumbe huo, azimio hilo limegusia suala nyeti lililokuwa linajadiliwa kuhusu kupunguza idadi ya askari, ambapo sasa imepunguzwa [...]

31/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa Israel kuhusu makazi mapya ya walowezi umenisikitisha-Guterres

Kusikiliza / Ujenzi na Israel katika maeneo yanayokaliwa ya Palestina umeongezeka.(Picha:Annie Slemrod/IRIN/maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres amesema amesikitishwa na kutiwa shaka na uamuzi wa Israel wa kujenga makazi mpaya ya Walowezi kwenye eneo linalokaliwa la Wapalestina. Kupitia ujumbe uliotolewa na msemaji wake Ijumaa, Katibu Mkuu amekuwa akisisitiza kila wakati kwamba hakuna mpango mbadala kwa Waisrael na Wapalestina kuishi pamoja kwa mani na usalama. [...]

31/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wenye usonji wanakosa haki za msingi za binadamu

Kusikiliza / UNICEF inafadhili miradi ya kutoa huduma kwa watoto wenye usonji.(Picha:UNICEF)

Kwa kuzingatia haki za msingi za binadamu kwa watu wenye usonji, dunia inaishi kizani , kwa mujibu wa mtaalamu wa masuala ya usonji. Akizungumza Ijumaa katika tukio maalumu la kuadhimisha siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu usonji kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, profesa Simon Baron-Cohen mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa usonji kwenye [...]

31/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

DRC inahitaji usaidizi zaidi bajeti sasa kuliko wakati mwingine: Balozi Mahiga

Kusikiliza / Mahiga-Barazani2

  Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki  wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuhakikisha bajeti kwa ajili ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC, MONUSCO inaongezwa ili kuhakikisha uimarishwaji wa amani katika ukanda huo. Katika mhojiano na idhaa hii, saa [...]

31/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji 655 wafariki wakisaka hifadhi-IOM

Kusikiliza / Picha:IOM

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM linasema wahamiaji na wakimbizi karibu 700 wamefariki katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu wa 2017 wakati wa safari za kusaka hifadhi sehemu mbalimbali. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo msemaji wa IOM Joel Millman amesema idadi hiyo hata hivyo bado haijavuka [...]

31/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Misele

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia matumizi yasiyo sahihi ya neno Misele Mchambuzi wetu  Nuhu Zuberi Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA anasema neno misele ni aina ya dawa lakini linatumika kumaanisha kutia nakshi lakini hiyo si sahihi kwani hamna usanifu na lnatumika [...]

31/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupitishwa kwa Baraza la mawaziri Somalia ni hatua chanya- UM

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya Bunge la Somalia kupitisha Baraza la Mawaziri.(Picha:UNSOM)

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya Bunge la Somalia kupitisha Baraza la Mawaziri lililoteuliwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khaire mapema mwezi huu. Baraza hilo lina mawaziri 27 ambao sita kati yao ni wanawake, hatua ambayo Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa umoja huo nchini Somalia, Michael Keating amesema ni chanya katika [...]

31/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wahitajika zaidi hivi sasa kusaidia raia huko Mosul- Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alipotembelea kambi ya wakimbizi ya Hassan Sham, Iraq.(Picha:UM/Twitter)

Akiwa bado Mashariki ya Kati kwa ziara katika ukanda huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo ametembelea kambi ya wakimbizi ya Hassan Sham, kaskazini mwa Iraq. Guterres amepata fursa ya kuzungumza na wakimbizi wa ndani pamoja na watu wa kabila la Yazid, wakati huu ambapo mapigano ya kukomboa mji wa Mosul yameingia [...]

31/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makabila madogo Somalia yaomba serikali izuie ubaguzi

Kusikiliza / Makabila madogo wakihudhuria mkutano. Picha:AMISOM

Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM pamoja na serikali ya Denmark, wamehitimisha mkutano wa ngazi ya juu wa siku tatu mjini Mogadishu, Somalia, uliojadili ujumuishaji na ukuzaji wa makabila madogo katika masuala ya nchi kwa lengo la kukuza amani na utulivu. Amina Hassan na ripoti kamili. (Taarifa ya Amina) AMISOM imesema mkutano huo [...]

31/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wasio na chakula duniani yaongezeka- Ripoti

Kusikiliza / Mkimbizi wa ndani aliyefurushwa akipika mlo ambao ni mgao wake wa mwisho.(Picha:FAO/Sudan Kusini)

Ripoti mpya kuhusu hali ya janga la chakula duniani imesema idadi ya watu wasio na uhakika wa kupata chakula iliongezeka mwaka jana na kufikia watu milioni 108, ikilinganishwa na milioni 80 mwaka 2015, licha ya jitihada za kimataifa za kuhakikisha watu wana chakula cha kutosha. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Ikiwa imeandaliwa [...]

31/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sasa tuna uwezo wa kutuma haraka kikosi imara- Ladsous

Kusikiliza / Ulinzi wa amani2

Mkutano wa viongozi uliofanyika miaka miwili iliyopita kuhusu ulinzi wa amani uliboresha operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Hervé Ladsous, mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya umoja huo, wakati huu ambapo anamaliza muda wake hii leo tarehe 31 mwezi Machi. Amesema [...]

31/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umuhimu wa vyandarua katika kujikinga na malaria

Kusikiliza / Mtoto akiwa amelala ndani ya neti.(Picha:UM/Logan Abassi)

Shirika la afya ulimwenguni, WHO kwenye ripoti yake ya mwaka 2016 iliyotolewa Desemba 13 kwa ajili ya malaria linaeleza kuwa watoto na wanawake wajawazito barani Afrika wana fursa ya kudhibiti Malaria.  Miongoni mwa mbinu za kukabiliana na ugonjwa huo hatari ni kutumia vyandaraua. Nchini Tanzania juhudi za kukabiliana na malaria kupitia mkakati wa kitaifa zinaendelea [...]

30/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

ITU yaunda kikosi cha kuboresha miji.

Kusikiliza / ITU FORUM 1

Shirika la Umoja wa Mataifa la teknolojia ya taarifa na mawasiliano ITU limeunda kikosi lengo kwa ajili ya kutafiti uchakatuaji wa taarifa na usimamizi katika muktadha wa miji erevu, ili kufikia kiwango cha ITU. Taarifa ya ITU inasema kwamba kundi hilo li wazi katika ushirikiano na kundi lolote linalohitaji kufanya hivyo ili kufanikisha ujumuishwaji wa [...]

30/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Syria ondoeni vikwazo vya kiutendaji ili misaada ifike- UM

Kusikiliza / WFP yasambaza msaada mjini Aleppo. Picha: WFP

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo wamepokea taarifa kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria ambapo wameelezwa kuhusu vizuizi vinavyoendelea kukwamisha misafara iliyobeba misaada ya kibinadamu. Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa Machi, Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ameeleza hayo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao kilichohutubiwa na [...]

30/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mgogoro wa wakimbizi wahitaji wajibu wa pamoja-Hendricks

Kusikiliza / Balozi mwema wa heshima ya maisha wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Barbara Hendricks. Picha: © UNHCR/G Kovacs

Balozi mwema wa heshima ya maisha wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Barbara Hendricks ametoa wito kwa Muungano wa Ulaya kukumbuka maadili ya kuanzishwa kwake. Akizungumza kwenye bunge la Muungano wa Ulaya kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya mkataba wa Roma ametoa wito kwa nchi wanachama kutimiza wajibu wao katika kushughulikia [...]

30/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ahadi ya kupatia makazi wakimbizi wa Syria yasuasua- UNHCR

Kusikiliza / Familia ya Mahmut ambao wameanza maisha mapya Ottawa, Canada.(Picha:UNCHR)

Wakati idadi ya watu wanaokimbia Syria ikivuka milioni 5 kutokana na vita vilivyodumu miaka sita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetaka jamii ya kimataifa ichukue hatua zaidi kuwasaidia wapate hifadhi. Kaminshna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema bado kuna safari ndefu kupanua wigo wa makazi kwa wakimbizi hao wanawake, wanaume na [...]

30/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ziara yangu Iraq ni kuonyesha mshikamano:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kushoto) akiwa na Rais wa Iraq. Picha: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema yuko nchini Iraq kuonyesha mshikamano wake na watu na serikali ya taifa hilo lililoghubikwa na vita. Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja na waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abdi, amesema ana matumaini mji wa Mosul utakombolewa kabisa hivi karibuni na ameipongeza serikali kwa juhudi zake [...]

30/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Njaa yaongeza madhila kwa watoto Somalia-UNICEF

Kusikiliza / Nalo Nuura Musdhaf, 26, anayeishi katika kambi na wanae.(Picha:UNifeed/video capture)

Amkani, si shwari tena Somalia! Ndivyo ilivyoanza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, ikionya kuwa kuongezeka kwa njaa nchini Somalia kunaongeza idadi ya watoto ambao wanakabiliwa na utapiamlo na kipindu pindu. Flora Nducha na taarifa kamili. ( TAARIFA YA FLORA) UNICEF inasema kwamba watoto nchini humo wanakabiliwa na aina mbili [...]

30/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yasifiwa kuondoa vizuizi barabarani

Kusikiliza / Sudan Kusini yasifiwa kuondoa vizuizi barabarani.(Picha:UNMISS)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, David Shearer, amepongeza mamlaka ya mji wa Gogrial, nchini humo kwa kuondoa vizuizi 7 kati ya 9 barabarani kuanzia mwezi Februari mwaka huu ili kurahisisha upitishaji wa misaada ya kibinadamu nchini humo. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Bwana Shearer ambaye [...]

30/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yamtunuku mwandishi Dawit Isaak mzaliwa wa Eritrea

Kusikiliza / Dawit Isaak nchini Sweden Picha: UNESCO_© Kalle Ahlsén

Dawit Isaak, mwandishi wa habari mzaliwa wa Eritrea mwenye uraia wa Sweden ambaye sasa yuko kifungoni, amechaguliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO , kupokea tuzo ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mwaka 2017 ijulikanayo kama UNESCO/Guillermo Cano World Press Freedom Prize. Bwana. Isaak alikamatwa katika [...]

30/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IRRI na FAO wasaidia kilimo endelevu cha mpunga

Kusikiliza / Wakulima wavuna mpunga Vietnam. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO na taasisi ya kimataifa ya utafiti wa mpungu IRRI , wameafikiana kushirikiana kwa karibu zaidi kusaidia uzalishaji endelevu wa mpunga katika nchi zinazoendelea ili kuimarisha uhakika wa chakula na maisha ya watu huku wakilinda mali asili. Muafaka uliiotiwa saini Alhamisi una lengo la kukusanya ujuzi wa kisayansi na teknolojia [...]

30/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kubiš alaani vikali shambulio la kigaidi Yousufiyah Baghdad

Kusikiliza / Ján Kubiš.Picha ya UNAMA

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ján Kubiš, amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea Yousufiyah Baghdad nchini humo Jumatano jioni, ambapo watu kadhaa wameuawa au kujeruhiwa. Bwana Kubiš amesema shambulio hilo la kinyama ni la pili kuilenga Baghdad chini ya siku kumi na limetekelezwa na magaidi wenye lengo la kulipiza [...]

30/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwelekeo wa usajili wa watoto Tanzania una nuru- UNICEF

Kusikiliza / Ramani ya Tanzania ikionyesha usajili wa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa. (Picha:UNICEF Twitter)

Nchini Tanzania kampeni ya usajili watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano iliyoanza mwaka 2013, imesaidia kusogeza huduma za usajili karibu na jamii na hivyo kupunguza gharama zilizokuwa zinazuia baadhi ya wazazi kutotilia maanani mpango huo. Kampeni hiyo inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali [...]

30/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

David Beasley Mkurugenzi Mtendaji mpya wa WFP

Kusikiliza / Picha: WFP/David Gross

Shirika la Mpango wa Chakula, WFP pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wamemteua Bwana David Beasley wa Marekani kuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, akichukua nafasi ya Etherine Cousin ambaye anamaliza muhula wake wa miaka mitano Aprili 4 mwaka huu. Taarifa ya WFP imesema Bwana Beasley ambaye ni Mwenyekiti wa kituo [...]

29/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yapongeza sheria ya Zampa nchini Italia

Kusikiliza / Watoto wakimbizi kuto Syria waliokolewa boti yao ilivyozama. Picha: © UNHCR/Andrew McConnell

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema sheria ya Zampa iliyopitishwa nchini Italia ni ya kihistoria katika ulinzi wa watoto wahamiaji na wakimbizi. Watoto hao ni wale wanaokuwa wanasafiri wenyewe kuelekea Ulaya kusaka hifadhi ambapo UNICEF imesema ni ya kuigwa barani humo. Mathalani sheria hiyo inataka kuwepo kwa msururu wa mikakati ikiwemo [...]

29/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa iamke dhidi ya uvunjifu wa haki- Bachelet

Kusikiliza / Rais wa Chile Michelle Bachelet.(Picha:UM/Jean-Marc Ferré)

Akilihutubia baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi hii leo, Rais wa Chile Michelle Bachelet amesema janga la watoto wakimbizi wa Syria na kuongezeka kuwa hotuba za chuki dhidi ya wageni lazima vikomeshwe kwa ushirikiano baina ya jumuiya ya kimataifa. Bi Bachelet ambaye nchi yake inatetea kuteuliwa tena kuwa mwanachama [...]

29/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen yazidi kutwama- Baraza

Kusikiliza / Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza akizungumza na waandishi wa habari New York.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Hali nchini Yemen inazidi kuwa mbaya na ya machungu huku raia wakilipa gharama ya mapigano yanayoendelea kwa miaka miwili sasa. Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Machi, Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari hii leo baada ya kikao cha faragha cha baraza [...]

29/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa unaozuia uwezo wa watoto kujifunza, “Down syndrome” haupatiwi kipaumbele Uganda- Omwukor

Kusikiliza / Mtoto aliye na Down syndrome. Picha: UM

Uganda kama ilivyo katika baadhi ya nchi za Afrika uelewa wa tatizo la ugonjwa unaoathiri uwezo wa kujifunza au Down Syndrome ni mdogo, hali inayochangia hata lisipewe uzito unaostahili. Je nini kifanyike kuhakikisha mwangaza unang'aa katika tatizo hili Uganda? Ungana na Flora Nducha katika Makala hii.

29/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mdudu hatari anayeshambulia minazi na mitende aleta changamoto- FAO

Kusikiliza / fao

Mdudu hatari alaye mimea ya minazi na tende amesababisha shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kuitisha mkutano wa siku tatu huko Roma, Italia ili kujadili mpango wa kimataifa wa kuzuia kuenea kwake hususan Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini. FAO imesema mkutano huo utakaoutanisha wanasayansi, wataalamu wa kudhibiti wadudu, mawaziri wa kilimo na [...]

29/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za kiarabu badilisheni mwelekeo ili msigeuzwe mtaji- Guterres

Kusikiliza / Guterres-ArabLeague-29MAR17-350-300

Umoja wa Mataifa umesihi viongozi wa nchi za kiarabu kuundwa kile ilichoita ulimwengu mpya wa kiarabu utakaowezesha nchi hizo kumaliza tofauti zao kwa njia ya mashauriano na mazungumzo. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Ikiwa ni ziara yake ya pili huko Mashariki ya Kati ndani ya mwezi wa tatu wa uongozi wake wa [...]

29/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na mkakati wa kupunguza madhara ya makosa ya matumizi ya dawa

Kusikiliza / Dawa WHO 1

Shirika la afya ulimwenguni WHO kupitia kitengo chake cha kimataifa cha usalama na changamoto kwa mgonjwa, linanuia kukabiliana na madhaifu katika mfumo wa afya ya makosa katika matumiziya dawa yanayosababisha madhara kwa watumiaji. Grace Kaneiya na taarifa zaidi. ( TAARIFA YA GRACE) WHO katika maelezo yake inasema marekebisho ya mfumo huo yanalenga kuimarisha matumizi ya [...]

29/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabaki ya miili ya wataalamu DRC yapatikana, UM kuchunguza

Kusikiliza / Maandamano huko DRC mwezi Disemba mwaka 2016. (Picha:MONUSCO)

Hatimaye Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa mabaki ya miili yaliyopatikana huko Kananga, jimbo la Kasai Kati nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni ya wataalamu wawili wa kimataifa waliotoweka wiki mbili zilizopita. Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema walinda amani wa umoja huo walibaini mabaki hayo siku ya [...]

29/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 27 katika nchi nne za Afrika hawana maji safi na salama- UNICEF

Kusikiliza / Msichana katika foleni ya kusubiri maji.(Picha:Phil Hatcher-Moore/UNICEF)

Uhaba wa maji, ukosefu wa huduma za kujisafi na tabia zisizo sahihi za kujisafi zinaongeza tishio kwa watoto ambao tayari wanakabiliwa na unyafuzi huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema hayo hii leo likiongeza kuwa takribani watu milioni 27 katika nchi hizo nne [...]

29/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Raia wengi wameuawa kwenye ukombozi Mosul: Zeid

Kusikiliza / Familia inaonekana hapa na mizigo nje ya nyumba yao iliyoharibiwa huko Mosul.
Picha: UNHCR/Ivor Prickett

  Wito umetolewa hii leo kwa vikosi vya ulinzi na usalama nchini Iraq kuchukua “tahadhari kubwa”iwezekanavyo katika kampeni zao za kuikomboa Mosul kutoka kwa wanamgambo ISIL huku kukiwa na taarifa kwamba mamia ya raia wameuawa katika mashambulizi ya anga. Ombi hilo limetolewa na ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vimbunga Matthew na Otto vyastaafishwa: WMO

Kusikiliza / Kupanda kwa viwango vya bahari. Picha: OCHA/Danielle Parry

Ni kawadia kusikia watu wakistaafu baada ya kufuikia umri fulani kwa mujibu wa sheria za nchi! Hii imekuwa tofauti kwa binadamu, vimbunga Mathew na Otto ambavyo vimesababisha madhara makubwa yakiwemo vifo na uharibifu wa mali na pia madhara ya kiafya, vimestaafishwa rasmi leo na shirika la kimataifa la hali ya hewa WMO. Majina ya vimbunga [...]

28/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nyukilia itumike kwa maendeleo sio silaha-Tanzania

Kusikiliza / Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, Balozi Modest Mero (kulia). Picha: UN Photo/Mark Garten

Tanzania imesema inaunga mkono maendeleo ya teknolojia ya nyuklia katika kutibu magonjwa yasiyoambukiza kama vile saratani na utunzaji wa chakula dhidi ya uharibifu, lakini ikasisistiza kwamba matumizi ya silaha za nyukilia ni jinamizi kwa kila mmoja. Hiyo ni sehemu ya tamko la serikali ya nchi hiyo katika mkutano uliofanyika hii leo katika makao makuu ya [...]

28/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNODC, Kenya wazindua muongozo wa kukabalina na ugaidi.

Kusikiliza / Muongozo wa kuzingatia haki za binadamu na kushugulikia uhalifu wa kigaidi nchini Kenya. Picha: UNODC

Ikiwezeshwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC, serikali ya Kenya kupitia ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali, leo wamezindua muongozo wa kuzingatia haki za binadamu na kushugulikia uhalifu wa kigaidi nchini humo. Hatua hii ni sehemu ya juhudi za mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kukabliana na ugaidi duniani, unaosisitiza [...]

28/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ndoto za wananchi wa Sudan Kusini kuwa taifa lao huru litaimarika

Kusikiliza / Nyanya shambani. Picha: UM

Kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa Machi, Mwenyekiti mpya wa kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU Moussa Faki Mahamat alikuwa ziarani nchini Sudan Kusini kujionea hali halisi wakati huu ambapo janga la kibinamu linazidi kupanuka, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu tangu mzozo wa wenyewe kwa wenyewe uibuke nchini humo. Ndoto za wananchi [...]

28/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Muda unayoyoma kwa watoto wanaokabiliwa na baa la njaa, ukame na vita

Kusikiliza / Mfanya kazi wa UNICEF Judy Jurua Michael (kati) anapima mtoto Alakaii kituoni Gabat nchini Sudan Kusini. Picha: UNICEF/Mackenzie Knowles-Coursin

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto hawawezi kusubiri, na dola milioni 255 zinahitajika haraka ili kukabiliana na mahitaji kaskazini mashariki mwa Nigeria, Somalia, Sudan Kusini na Yemen. Mkurugenzi wa Mipango ya dharura wa UNICEF Manuel Fontaine amesema kutokana na funzo walilopata mwaka wa 2011 nchini Somalia ni kwamba muda waliotangaza [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunaalani vikali mauaji ya polisi 40 wa serikali DRC: UM/AU/EU

Kusikiliza / Maafisa wa Umoja wa Mataifa na raia wa DRC wasikitishwa na mauaji wa polisi. Picha: MONUSCO

Umoja wa Mataifa, Muungano wa Africa, AU pamoja na Muungano wa Ulaya, EU wamelaani vikali ripoti za mauaji ya polisi 40 wa serikali yaliyotekelezwa na waasi wa Kamuina Nsapu katika wilaya ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mwezi Machi. Taarifa kamili na Rosemary Musumba (TAARIFA YA ROSEMARY) Mauaji hayo yaliyofanyika katikati mwa [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Surua yashambulia kwa kasi Ulaya: WHO

Kusikiliza / Mtot wa kike anapewa chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua huko Ulaya. Picha: UNICEF_EPA/E. Oudenaarden

Kama ulifikiri surua inashambulia bara Afrika pekee, lahasha! Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema zaidi ya visa 500 vimeripotiwa barani Ulaya ifikapo jana Januari 27 huku ugonjwa huo unaoathiri watoto ukidaiwa huenda ukisasabisha mlipuko mkubwa zaidi kutokana na kupungua kwa chanjo kwa asilimia 95. WHO inasema katika taarifa yake ya leo kwamba kwa kipindi cha [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF na wadau wasaidia zaidi ya 145,000 kwenye baa la njaa Sudan kusini:

Kusikiliza / Mfanya kazi wa UNICEF Judy Jurua Michael (kushoto) anamhudumia mtoto akiwa na mamake Iman Diing. Picha; UNICEF/UN056592/Knowles-Coursin

Mwezi mmoja tangu kutangazwa kwa baa la njaa katika baadhi ya sehemu nchini Sudan kusini , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa pamoja na lile la mpango wa chakula WFP na washirika wengine wamefikisha msaada wa kuokoa maisha kwa watu 145,000 wakiwemo watoto 33,000 wa chini ya umri wa miaka mitano. [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni wakati wa washawishi wa mzozo Syria kuweka kando tofauti zao:Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na wanafunzi kambi ya wakimbizi ya Zaatari nchini Jordan. Picha: Stephane Dujarric.

Wakati mazungumzo ya amani ya Syria yameanza tena Geneva naziomba pande zote katika mzozo na hususani nchi zenye ushawishi kuelewa kwamba ni lazima kuleta amani Syria. Amina Hassan na taarifa kamili (TAARIFA YA AMINA) Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António  Guterres alipozuru kambi ya wakimbizi ya Zaatari nchini Jordan mapema Jumanne. [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

YWCA yaazimia kuinua wanawake Tanzania: Dk Grace

Kusikiliza / YWCA TZ 6

Mkutano wa 61 wa hadhi ya wanawake CSW 61 ukiwa umemalizika mjini New York, shirika la wasichana Wakristo nchini Tanzania YWCA  limesema lithakikisha linatekeleza maazimio ya kuwaendeleza wanawake katika nyanja kadhaa ikiwamo uchumi. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Katibu Mkuu kitaifa wa YWCA Dk Grace Soko aliyehudhuria mkutano huo amesema maazimio yaliyofikiwa yameondoa vikwazo [...]

28/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuna matumaini na mjadala wa kitaifa nchini Gabon – UM

Kusikiliza / François Fall Louncény mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa UM kwa Afrika ya kati, UNOCA
Picha: UNOCA

Wakati Gabon inajiandaa na mjadala wa kitaifa kesho Jumanne, Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kwa Afrika ya kati, UNOCA, Francois Louncény Fall amesema wana imani kubwa kuwa mjadala huo utaendeshwa kwa amani, utulivu na utakuwa jumuishi. Taarifa ya UNOCA imesema kwa miezi miwili sasa Bwana Fall ameimarisha juhudi za kufanya majadiliano [...]

27/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanyamapori wainua vipato na elimu Uganda.

Kusikiliza / Tembo wa Afrika. Picha: World Bank/Curt Carnemark

Takwimu  za benki ya dunia za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa Sekta ya utalii nchini Uganda huiliingizia taifa asilimia 3.7 ya pato la ndani  . Uwepo wa mbuga za wanyama ni sehemu ya mchango wa pato hilo. Mbuga hizo za wanyama zimekuwa na manufaa kwa wakazi nchini humo hususani wale waishio jirani na mbuga za wanyama. [...]

27/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yazindua kitabu cha mwongozo waandishi wa habari za ugaidi

Kusikiliza / Kitabu cha mwongozo ya waandishi wa habari za ugaidi. Picha: UNESCO

Shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO limezindua kitabu cha mwongozo kwa waandishi wa habari ili kuongeza uelewa wao zaidi katika kuandika habari kuhusu ugaidi. Taarifa ya UNESCO imesema kitabu hicho kilichoandikwa na Jean-Paul Marthoz kitawezesha wanahabari kutekeleza majukumu yako ya kuhabarisha umma bila kuwapatia fursa magaidi ya kufanikisha lengo lao [...]

27/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Harakati za kutokomeza nyuklia zaanza, nchi 40 zasema hazitoshiriki

Kusikiliza / Jaribio la nyuklia uliofanywa na Marekani katika Enewetak Atoll, Visiwa vya Marshall, Novemba 1, 1952. Picha: US Government

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limeanza awamu ya kwanza ya mkutano wake wa kujadili mbinu yenye nguvu kisheria ambayo itawezesha kutokomeza silaha za nyuklia ulimwenguni. Akifungua mkutano huo, Mwenyekiti wa kikao hicho kitakachomalizika tarehe 31 mwezi huu, balozi Elayne Whyte Gomez wa Costa Rica amesema amani ni lazima iibuke mshindi dhidi ya silaha [...]

27/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Milio ya risasi na mabomu yaendelea kunguruma Yemen licha ya juhudi za kimataifa

Kusikiliza / Watoto ndio waathiririka zaidi migogoro nchini Yemen ikiingia mwaka wa tatu. Picha: UNICEF

Licha ya juhudi za kimataifa za kuleta suluhu ya kudumu ya kisasa Yemen, milio ya makombora, mabomu, risasi na vifaru sasa imekuwa ada katika maisha ya kila siku nchini humo. Amina Hassan na ripoti kamili. (Taarifa ya Amina) Hayo yamesemwa na Stephen O'Brien msaidizi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu [...]

27/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan yafungua njia salama kukabili njaa Sudan Kusini

Kusikiliza / Picha:WFP/Peter Testuzza

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibindamu, OCHA imekaribisha hatua ya serikali ya Sudan ya kufungua njia mpya na salama kwa ajili ya kupitisha misaada ya kibinadamu, hatua ambayo itaokoa maisha ya watu 100,000 wanaokumbwa na njaa kali nchini Sudan Kusini. Barabara hiyo ya urefu wa kilometa 500 yenye kuanzia El Obeid [...]

27/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa Zambia unakua lakini yahitaji marekebisho ya sera- IMF

Kusikiliza / Watoto nchini Zambi. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Shirika la fedha duniani, IMF limesema Zambia imechukua hatua ili kuwezesha shirika hilo kusaidia mipango ya uchumi. IMF imesema hayo kufuatia ziara ya wiki mbili nchini humo iliyoongozwa na Tsidi Tsikata. Mathalani imetaja mipango hiyo kuwa ni pamoja na mipango ambamo kwayo inahakikisha fedha za umma zinatumika ipasavyo na kiuendelevu pamoja na malipo ya malimbikizo [...]

27/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viongozi Sudan Kusini zingatieni amani- Mahamat

Kusikiliza / Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU, Moussa Faki Mahamat (kulia) akihutubia waandishi wa habari Unity nchini Sudan Kusini. Picha: UNMISS/Isaac Billy

Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU, Moussa Faki Mahamat yuko nchini Sudan Kusini ambako ametoa wito wa utekelezaji wa mkataba wa amani ili kumaliza machungu yanayokabili wananchi. Akizungumza huko Ganyiel, kwenye jimbo la Unity Kusini, Bwana Mahamat amesema kiwango cha machungu ni cha kupitiliza na zaidi ya yote janga la kibinadamu. Amesema aliguswa [...]

27/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Licha ya juhudi za kimataifa , milio ya risasi na mabomu yaendelea kunguruma Yemen:O'Brien

Kusikiliza / Stephen O'Brien msaidizi wa Katibu mkuu katika masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura ichani na watoto nchini Yemen. Picha: OCHA

Licha ya juhudi za kimataifa za kuleta suluhu ya kudumu ya kisasa Yemen, milio ya makombora, mabomu, risasi na vifaru sasa imekuwa ada katika maisha ya kila siku nchini humo. Hayo yamesema na Stephen O'Brien msaidizi wa Katibu mkuu katika masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, katika taarifa yake kuhusu miaka miwili baada ya [...]

27/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanigeria waliokuwa Libya warejea nyumbani kwa wimbo:IOM

Kusikiliza / Wanageria waliokuwa libya wakirejea nyumbani. Picha: IOM

Zaidi ya wanigeria 150 baadhi yao wakibubujikwa na machozi , waliimba kwa furaha wakati ndege inatua nyumbani Lagos, Nigeria baada ya kukwama Libya kwa miezi mingi wakisubiri kujaribu kuingia Ulaya. Rosemary Musumba na ripoti kamili. (Taarifa ya Rosemary) Nats.. Kibao hicho I am coming home.. yaani narudi nyumbani kikiimbwa na raia wa Nigeria wakiwa ndani [...]

27/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirika imara ni muhimu kwa suluhu endelevu ya wakimbizi Ugiriki:UNHCR

Kusikiliza / Watoto wachukua picha katika kituo cha malazi cha Kara Tepe. Picha: © UNHCR/Achilleas Zavallis

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Jumatatu limesema juhudi za pamoja na kuimarisha ushirikiano ni muhimu sana katika kuboresha hali kwa waomba hifadhi na wakimbizi nchini Ugiriki na limetoa mapendekezo manane ya kusaidia kuhakikisha msaada endelevu kwa wakimbizi nchini humo. Kamishina mkuu wa wakimbizi Filipo Grand amesema , UNHCR inajihusisha kikamilifu kutafuta [...]

27/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vita vikiingia mwaka wa pili familia Yemen zageukia hatua kujikimu: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto wa kike anatibiwa katika hospitali ya Al-Sabeen, Sana'a, Yemen. Picha: © UNICEF Yemen/2017/Farid

Baada ya miaka miwili ya vita, familia nchini Yemen zinageukia hatua kali ili kukidhi mhitaji ya watoto wao, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika ripoti yake iliyotolewa Jumatatu. Ripoti inasema njia za kujikimu zimesambaratishwa na machafuko na kuigeuza Yemen kuwa moja ya nchi zenye tatizo kubwa la uhakika wa chakula [...]

27/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vita na migogoro ya muda mrefu ni kikwazo katika kutokomeza njaa:FAO

Kusikiliza / Picha: FAO/Giulio Napolitano

Uhakika wa chakula na viwango vya lishe Mashariki ya mbali na Afrika Kaskazini vimedorora kwa haraka katika miaka mitano iliyopita , vikitishia hatua zilizopigwa kabla ya 2010 ambapo hali ya lishe duni, kudumaa, matatizo ya upungufu wa damu na umasikini vilikuwa vinapungua, imesema ripoti mpya ya shirika la chakula nakilimo FAO iliyotolewa Jumatatu. Ripoti hiyo [...]

27/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

KNCCI yanufaisha wanawake wafanyabiashara Kenya

Kusikiliza / KNCCI inasaidia wafanya biashara wanawake ikiwemo wachuuzi wa vyakula.(Picha:UM/Tobin Jones)

Chama cha wafanyabiashara na wenye Viwanda nchini Kenya, KNCCI, kimesema kimepatia kipaumbele wanawake upande wa biashara na sasa asilimia 90 ya wanufaika wameweza kuinua jamii zao. Naibu Mwenyekiti wa chama hicho Rukia Rashid amesema hayo akihojiwa na Idhaa hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, Marekani. Amesema mipango ya usaidizi ni [...]

27/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yalaani vikali mauaji ya wahudumu sita wa misaada Sudan Kusini:

Kusikiliza / Eugene Owusu, Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa OCHA nchini Sudan Kusini, akilaani vikali mauaji ya wahudumu sita wa misaada ya kibinadamu huko Pibor. Picha na UNMISS.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa shirika la Umoja wa Mataifa OCHA nchini Sudan Kusini Eugene Owusu, amelaani vikali mauaji ya wafanyakazi sita wa misaada yaliyofanyika Jumamosi Machi 25 wakiwa safarini kutoka Juba kuelekea Pibor. Katika taarifa yake Bwana Eugen Owusu amesema amesikitishwa na kughadhibishwa na mauaji hayo ya kinyama , katika wakati ambao mahitaji [...]

26/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini ichunguze na kushikilia wauaji wa wahudumu wa misaada:UNMISS

Kusikiliza / Mtu mwenye silaha mjini Pibor, jimbo laJonglei Sudan Kusini. Pibor imeshuhudia machafuko ambayo yamesababisha maelfu kukimbia, na uharibifu mkubwa wa mali na maisha. Picha na OCHA/Cecilia Attefor

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini , David Shearer ameitaka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza na kuwashilikilia wauaji wa wahudumu sita wa misaada ya kibinadamu. Wafanyakazi hao kutoka shirika la kitaifa lisilo la kiserikali waliripotiwa kushambuliwa katika gari lao kwenye eneo linalodhibitiwa na serikali katika barabara ya Upper Juba-Pibor [...]

26/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko mapya Damascus na kwingineko yatia hofu: De Mistura

Kusikiliza / Staffan de Mistura, mwakilishi maalumu wa UM kwa ajili ya Syria, anatiwa hofu na machafuko mapya Damascus na kwingineko Syria. Picha na UM.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria, Staffan de Mistura, amesema anatiwa hofu na mapigano ya karibuni Damascus, Hama na kwingineko Syria. Amesema ukiukwaji unaoongezeka hivi karibuni unatishia mustakhbali wa amani uliojadiliwa kupitia mikutano ya Astana, ukiwa na athari mbaya kwa usalama wa raia wa Syria , fursa za misaada ya kibinadamu [...]

25/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni saa moja ya kujali mazingira duniani:Guterres

Kusikiliza / Nembo ya saa moja ya kuzima taa kujali mazingira. saa hiyo itakuwa saa 8:30 usiku kote duniani. Picha na UM.

Kwa mara ya Kumi, leo Jumamosi jioni, watu kila mahali watashiriki katika "saa moja ya kujali mazingira ulimwenguni" kama ishara ya kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Katika ujumbe wake kuhusu tukio hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuhatarisha maisha na vipato duniani kote. Mwaka jana [...]

25/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatoa wito IGAD wa msaada Zaidi kwa Somalia:

Kusikiliza / Wakimbizi wa Somalia wakiwa Ethiopia moja ya nchi wanachama wa IGAD wakisubiri msaada. Picha kwa hisani ya UNHCR.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR,limetoa wito wa msaada kwa juhudi zenye lengo la kuleta utulivu ndani ya Somalia na kwa nchi zinazohifadhi wakimbizi wa Somalia. Akizungumza kwenye mkutano maalumu wa wakuu wa nchi za shirika la kikanda la mendeleo IGAD unaofanyika Nairobi Kenya, kwa lengo la kusaka suluhu ya kudumu kwa [...]

25/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tukiwakumbuka wanaoshikiliwa au kutoweka, tunaimarisha ulinzi kwa wafanyakazi:UM

Kusikiliza / Hayati Alec Collett , aliyekuwa mwanahabari shirika la Umoja wa Mataifa la UNRWA, alitekwa mwaka 1985 na maiti yake ilikutwa bonde la Beeka Lebanon mwaka 2009. Picha na UM / Milton Grant

Hadi kufikia Machi 15 mwaka 2015 wafanyakazi 33 wa Umoja wa Mataifa na wanaohusiana na Umoja huo wanashikiliwa na mamlaka za nchi 15. Mfanyakazi mmoja ametoweka na hajulikani haliko huku makandarasi wawili wa Umoja wa mataifa bodo wanashikiliwa na waliowateka nyara. Siku ya kimataifa ya mshikamano na wafanyakazi wa Umoja wa mataifa wanaoshikiliwa au waliotoweka [...]

25/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakati baadhi ya mifumo ya utumwa imetokomezwa mipya inaibuka-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihutubia CSW61.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Wakati baadhi ya mifumo ya utumiwa ikiwa imetokomezwa mingine inaibuka na kuleta athari kubwa duniani ikiwemo usafirishaji haramu wa binadamu na kazi za shuruti, na hivyo kukumbusha kwamba tuliyojifunza jana inamaanisha kuyatumia kukabili madhila ya leo. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hafla maalumu ya kumbukizi ya kuwaenzi [...]

24/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa ndani Gambella Ethiopia wanufaika na msaada: IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Eritrea walioko nchini Ethiopia wansafirishwa na IOM kuelekea kambi za wakimbizi. Picha: © IOM 2015

Wakimbizi wa ndani 332 walio kwenye mazingira magumu wamenufaika na msaada kutoka shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM nchini Ethiopia ikishirikiana na Ofisi inayoshughulikia maafa na uhakika wa chakula katika mkoa wa Gambella DPFSA. Msaada huo ulikuwa wa vifaa muhimu na kusaidia kaya, fedha ili kukidhi mahitaji yao ya msingi. Taarifa ya IOM imesema kuwa [...]

24/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umuhimu wa misitu ni dhahiri na hivyo inahitaji kulindwa

Kusikiliza / Keith Bitamizire akiwa katika mahojiano na John Kibego katika msitu nchini Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/John Kibego)

Kila Machi 21, dunia haudhimisha siku ya misitu. Misitu ni uhai! Huu ni usemi ambao hutumika mara nyingi ukipigia chepuo umuhimu wa rasilimali hiyo ambayo huhifadhi maji, husaidia upatikanaji wa chakula, hewa safi na kwa ujumla mazingira bora kwa vizazi, hasa wakati huu ambapo uharibifu wa mazingira unaathiir mustakhbali wa sayari dunia. Umuhimu huo ndiyo [...]

24/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Japo kuna changamoto, ulinzi wa amani umeokoa maisha- Ladsous

Kusikiliza / Hervé Ladsous katika ziara yake ya mwisho Mali anawasalamia walinda amani wa Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Sylvain Liechti

Baada ya miaka sita ya kuhudumu kama Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous anahitimisha jukumu hilo akisema ingawa kulikuwa na changamoto bado wamepata mafanikio ikiwemo kuokoa raia. Akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani kabla ya kumaliza mkataba wake tarehe 31 mwezi huu, Bwana Ladsous ametaja [...]

24/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Biashara ya utumwa yaacha alama Amerika Kusini

Kusikiliza / Muziki wa Cuba wenye mvuto wa Afrika. Picha: UM/Video capture

Tarehe 25 Machi kila mwaka kunaadhimishwa  siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa. Mwaka huu kumbukizi hizo zinaangazia jinsi wahanga wa biashara ya utumwa wanavyoendelea kuchangia na kuleta mabadiliko katika jamii duniani kote.  Katika makala hii Amina Hassan anaangazia jinsi biashara hiyo inavyoendelea kuvutia utamaduni katika jamii fulani Amerika [...]

24/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni azimio la kihistoria kulinda urithi wa dunia dhidi ya ugaidi

Kusikiliza / Uharibifu katika kituo cha urithi wa dunia wa Palmyra nchini Syria. Picha: ©UNESCO/Francesco Bandarin (maktaba) 26979

Baaraza la usalama la Umoja wa mataifa Ijumaa limepitisha azimio la kihistoria kulinda urithi wa kitamaduni wa dunia dhidi ya makundi ya kigaidi wakati wa vita vya silaha. Azimio hilo litashughulikia masuala muhimu ya usafirishaji haramu wa bidhaa za kitamaduni kama chanzo cha fedha za ufadhili wa ugaidi na pia linaweka bayana njia za kulinda [...]

24/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki- Sifongo

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Wiki hii tunaangazia neno "Sifongo" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema kwamba msamiati huu unafahamika kutokana na kuandikwa sana katika vitabu takatifu. Anasema sifongo ni kama kitu yavu yavu kinachosharabu maji na kina uwezo wa kukaa na maji lakini pia kinayaachia [...]

24/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yawapa fidia wahanga 297 wa uhalifu wa Katanga

Kusikiliza / Germain Katanga.(Picha:ICC)

Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC leo imetoa amri ya kuwafidia wahanga 297 wa uhalifu uliofanywa na Germain Katanga katika wilaya ya Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo Februari 24 mwaka 2003. Taarifa kamili na John Kibego. (Taarifa ya Kibego) Mahakama imesema fidia hiyo si toshelezi kwa madhara waliyoyapitia waathirika bali ni ishara [...]

24/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tatizo la kifua kikuu bado ni changamoto duniani-WHO

Kusikiliza / Utoaji huduma kwa mgonjwa wa kifua kikuu.(Picha:UNifeed/video capture)

Ugonjwa wa kifua kikuu au TB bado ni changamoto kubwa duniani na kwa kulitambua hilo shirika la afya ulimwenguni limetoa muongozo mpya wa kimaadili likiadhimisha siku ya kifua kikuu ambayo hua Machi 24 kila mwaka. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Baadhi ya mambo yaliyojumuishwa katika muongozo huo wa WHO ni masuala ya [...]

24/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jopo latumwa Myanmar kuchunguza ukiukwaji wa haki

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la haki za binadamu. Picha: UN Photo/Pierre Albouy

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio kuhusu Myanmar ambalo pamoja na mambo mengine linaridhia kupelekwa kwa tume huru ya kimataifa nchini Myanmar ili kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo, hususan kwenye jimbo la Rakhine. Wajumbe wa jopo hilo watachaguliwa na Rais wa Baraza hilo ambapo watachunguza madhila [...]

24/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Matumizi bora ya fedha za umma yataimarisha kilimo Afrika

Kusikiliza / Mkulima huyu na miche ya Acacia akiwa kijiji cha Launi, Aguie, Niger.(Picha:IFAD)

Benki ya Dunia imetaka nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara zifanyie marekebisho mfumo wake wa matumizi ya fedha za umma ili kupatia kipaumbele sekta ya kilimo. Katika ripoti yake kuhusu Kuvuna faida zaidi:Vipaumbele vya matumizi ya umma Afrika kwa ajili ya tija kwenye kilimo, benki hiyo imesema kwa sasa bajeti za serikali [...]

24/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuwezesha vijana katika afya ya uzazi-UNFPA Tanzania

Kusikiliza / Picha: Amua/Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania, limezindua mradi maalum wa mafunzo kwa ajili ya kuwawezesha vijana katika kuibua suluhu bunifu zinazohusu masuala ya afya ya uzazi. Mradi huo wa miezi sita uitwao Amua, unatarajia kutumia teknolojia ya habari na mawasiliao TEHAMA na utawawezesha vijana wajasiriamali, kwa kuwapa mafunzo ya ujuzi [...]

24/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni mpya ya UM inatarajia kutokomeza Polio Afrika

Kusikiliza / Mhudumu akiwapa watoto chanjo katika eneo la Guéckédou, nchini Guinea. Picha: UNICEF/UNI183271/Bindra

Kampeni ya chanjo ya aina yake kuwahi kufanyika katika bara la Afrika dhidi ya polio itatoa chanjo kwa watoto milioni 116 wiki ijayo katika nchi 13 za Afrika Magharibi na Kati limesema Shirika la Afya Duniani, WHO na Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Kampeni hiyo ambayo itafanywa kwa wakati mmoja na wahudumu wakujitolea 190,000 kwa [...]

24/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mikopo yalenga kukwamua wanawake kiuchumi nchini Tanzania

Kusikiliza / Mfanya biashara nchini Tanzania.(Picha:WorldBank)

Umaskini uliokithiri umepunguzwa zaidi ya maradufu katika nchi mbali mbali duniani tangu mwaka 1990. Wakati hii ikiwa ni hatua kubwa, bado yaelezwa kuwa mtu mmoja kati ya watano katika nchi zinazoendelea anaishi kwa kutumia chini ya dola moja na senti ishirini na tano kila siku na kuna mamilioni wengi ambao wana kipato kidogo zaidi tu [...]

23/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwa kila uasi unaofanyika Sudan Kusini unachagiza kisasi-Guterres

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres wakati wa kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Manuel Elias)

Kwa kila mtoto anayekufa, kwa kila mwanamke au msichana anayebakwa na wahusika kukwepa sheria, na kwa kila mvulana anayeingizwa vitani na kulishwa dhana za chuuki , kumbuka kuna mzazi aliyejawa na gadhabu, mume au baba aliyeghubikwa na huzuni na kutumbukia katika kusaka ulipizaji kisasi. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres [...]

23/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto Syria taabani-UNICEF

Kusikiliza / kijana mdogo mbele ya jengo lililoharibiwa mjini Homs Syria
Picha: WFP/Abeer Etefa (file)

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Geert Cappelaere amesema ripoti ya kwamba makumi ya watoto ni miongoni mwa watu 53 waliouawa jana jumatano kufuatia shambulio kwenye shule moja huko Syria, zinakumbusha ulimwengu kuwa jamii ya kimataifa inawaangusha watoto wa nchi hiyo. Akizungumza [...]

23/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mshikamano wa Baraza utumike kukwamua Somalia- Keating

Kusikiliza / Keating

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu Somalia ambapo wajumbe wameelezwa kuwa janga la kibinadamu nchini humo linaweza kuepukwa iwapo fedha zaidi zitakapatikana kukidhi mahitaji yanayotakiwa. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema hali inazidi kuwa mbaya kwa kuwa [...]

23/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maadhimisho ya Siku ya TB Duniani yasisahau wahamiaji-IOM

Kusikiliza / Wafanya kazi wakimbizi huko Mawlamyine nchini Myanmar. Picha: IOM

Tukielekea siku ya Kifua Kikuu Duniani, Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM imeungana na Shirika la Afya Duniani, WHO na washirika wengine kuongeza maradufu juhudi za uelewa wa umma kuhusu kifua kikuu ama TB na madhara yake kwa jamii zilizo hatarini zaidi kama vile wahamiaji. IOM imesema ugonjwa huo ambao WHO imesema unatibika, husababisha unyanyapaa [...]

23/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna changamoto lakini hatua pia zinapigwa kukabili mabadiliko ya tabianchi-Guterres

Kusikiliza / Athari za mabadiliko ya tabianchi mashinani picha: UN Photo/Albert González Farran

Mabadiliko ya tabianchi ni makubwa na tishio kwa amani, ustawi na malengo yote ya maendeleo endelevu na kwamba kukabili mabadiliko hayo ni fursa ambayo dunia haitomudu kuikataa. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres katika mjadala wa ngazi ya juu Alhamisi kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa ukijikita katika [...]

23/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 20 zahitajika kusaidia wahanga wa kimbunga Enawo, Madagascar

Kusikiliza / Jiji moja nchini Madagascar baada ya kimbunga Enawo. Picha: UNICEF

Umoja wa Mataifa na wadau wake wametoa ombi la dola milioni 20 ili kukabiliana na athari za kimbunga Enawo kilichopiga Madascar mapema mwezi huu. Kimbunga hicho kikiambatana na upepo mkali na mvua iliyosababisha mafuriko, kilipiga maeneo ya kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo na sasa watu takribani laki mbili na nusu wanahitaji misaada ya dharura kuokoa maisha [...]

23/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kusambaratika kwa mfumo wa afya Yemen kwatishia uhai wa wajawazito- UNFPA

Kusikiliza / Muuguzi Rasheeda akihudumia mtoto wa mama Ayisha ambaye amebebwa na dadake Ayisha.(Pichaa: UNFPA Yemen )

Miaka miwili ya mapigano nchini Yemen, imekuwa mzigo mkubwa kwa afya ya wanawake na wasichana nchini humo. Makala iliyochapishwa katika tovuti ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA inasema kuwa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe yaliyoanza tarehe 26 mwezi Machi mwaka 2015, yamesambaratisha vituo vya afya, na sasa wanawake wajawazito [...]

23/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaada kwa wakimbizi wa Sudan kusini wahitajika haraka-UNHCR/Uganda

Kusikiliza / Mzigo wa kuwahifadhi wakimbizi walioko Uganda unazidi kuwa mzito, ombi la msaada limetolewa na Uganda/UNHCR.(Picha:UNHCR)

Serikali ya Uganda na kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR,  Filippo Grandi  leo Alhamisi wametoa ombi la pamoja kwa jumuiya ya kimataifa kutoa haraka msaada kwa maelfu ya wakimbizi wa Sudan Kusini wanaoendelea kuwasili Uganda kila siku  wakikimbia vita na sasa uhaba wa chakula. Taarifa kamili na Rosemary Musumba. [...]

23/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

SheTrades yafungua milango Rwanda, wanawake wazungumza

Kusikiliza / SHE TRADES2

Mpango wa SheTrades wa kuwezesha wanawake kupenya katika masoko ya kikanda na kimataifa umefungua milango yake huko Rwanda ambapo Mkurungezi Mtendaji wa kituo cha biashara cha kimataifa, ITC, Arancha Gonzales amesema ni fursa mpya ya kuimarisha harakati za nchi hiyo kumkomboa mwanamke. Akizungumza kwenye uzinduzi huo mjini Kigali, Bi. Gonzales amesema ni kwa mantiki hiyo [...]

23/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuelekea uchaguzi mkuu Kenya, wanawake wajengewa uwezo wa mawasiliano

Kusikiliza / Kenya-2

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya mwezi Agosti mwaka huu, serikali imechukua hatua kujengea uwezo wanawake wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi ili kufanikisha usawa wa 50 kwa 50 kwenye ngazi ya uamuzi ifikapo mwaka 2030. Akihojiwa na Idhaa hii kando ya mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake duniani, CSW61 jijini New York, [...]

23/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukaji wa haki za binadamu DRC umeongezeka asilimia 30: UM

Kusikiliza / Walinda amani wa umoja wa mataifa kutoka india wakizungumza na raia na askari wa DRC. Picha: MONUSCO

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour ameesema ukiukaji wa haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa mwaka jana uliongezeka kwa asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia. Bwana Gilmour meyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea huko Geneva, Uswis akiongeza [...]

22/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado kuna mapungufu makubwa katika kukabiliana na haki za binadamu Guinea: UM

Kusikiliza / Picha: OHCHR

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, Andrew Gilmour akizungumza kwenye kikao cha haki za binadamu katika mjadala kuhusu Guinea, amesema licha ya ahadi ya serikali baada ya kuwasilishwa kwa ripoti ya mwisho ya mashauriano ya kitaifa ya Juni 29 kuweka kipaumbele katika mapambano dhidi ya uonevu, bado kuna mapungufu [...]

22/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa muongozo wa maadili ya kulinda haki za wagonjwa wa kifua kikuu

Kusikiliza / Mgonjwa wa kifua kikuuu. Picha: UNICEF/G. Pirozzi

Muongozo mpya wa maadili kwa ajili ya kulinda haki za wagonjwa wa kifua kikuu au TB umezinduliwa leo Jumatano na shirika la afya ulimwenguni WHO , ukiwa na lengo la kusaidia kuhakikisha kwamba nchi zinatekeleza mkakati wa kutokomeza TB zikizingatia maadili ya kuwalinda wote walioathirika na maradhi hayo. Kifua kikuu moja ya maradhi makubwa ya [...]

22/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa maji Pangani waleta mtafaruku wa ndoa na jamii

Kusikiliza / Uhaba wa maji husababisha wanawake kupoteza muda mwingi iwe bombani au kisimani. (Picha:© UNICEF Tanzania/2015/Beechey)

Ukosefu wa maji wilayani Pangani huko mkoani Tanga nchini Tanzania sio tu kwamba unahatarisha afya za wakazi wa wilaya hiyo, bali pia unasababisha mafarakano miongoni mwa wanajamii wanadoa na kuzorotesha maendeleo. Maajabu Ally wa redio washirika Pangani Fm ya mkoani humo anaangazia adha hiyo inayokupa visa na mikasa ikiwamo kukesha kusubiri maji huku mama mmoja [...]

22/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu yazidi kuzorota Somalia-UM

Kusikiliza / Mama na mtoto wake ni miongoni mwa raia wa Somalia wanaokumbwa na uhaba wa njaa
Picha: UN/OCHA

Wakati tishio la baa la njaa likizidi kunyemelea Somalia, hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota nchini humo, umesema Umoja wa mataifa Jumatano. Takribani watu 257,000 wametawanywa nchini Somalia tangu Novemba 2016 hadi Februari mwaka huu, huku wengine zaidi ya elfu nne wakivuka mpaka kuingia Ethiopia . Ombi la msaada halijafikia hata nusu na gonjwa la kipindupindu [...]

22/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majitaka ni mweleko mpya wa kukabili uhaba wa maji- WHO

Kusikiliza / Wavuvi na wakulima wa Kalkata wanatumia maji taka. Picha: WHO

Leo ni siku ya maji duniani ambapo shirika la afya ulimwenguni, WHO linasem majitaka yanaweza kuwa suluhu ya uhaba wa maji unaokabili binadamu hivi sasa. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Itakuwa vipi tukibonga bongo kuhusu matumizi bora ya majitaka kutoka majumbani, mashambani na viwandani, majitaka yanayoelekezwa katika mazingira kila uchao? Hivyo ndivyo [...]

22/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICC yamuongezea Bemba mwaka mmoja jela kwa rushwa

Kusikiliza / Jean-Pierre Bemba. Picha:ICC

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC huko The Hague Uholanzi imemuongezea Jean-Pierre Bemba hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kosa la rushwa. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Bemba ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ameongezewa kifungo hicho wakati huu ambapo tayari anatumikia kifungo cha [...]

22/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majitaka yaweza kuwa raslimali muhimu kwa kilimo-FAO

Kusikiliza / Miti iliyopandwa karibu na mitaro ya maji taka.(Picha: FAO)

Maji ni raslimali muhimu sana katika kufanikisha ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Katika kuadhimisha siku ya maji duniani ambapo kauli mbiu mwaka huu ni "majitaka" upunguzaji na utumiaji tena wa maji hayo,  FAO imesema  kimataifa zaidi ya asilimia 80 ya maji taka yanayozalishwa na jamii hurejea [...]

22/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa IAEA Sudan kusaidia ufadhili wa saratani

Kusikiliza / Cancer general 1

Mkutano ulioandaliwa kwa ushirikiano na shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA kusaidia ufadhili wa miradi ya kukabiliana na saratani katika nchi zilizolemewa na ongezeko la maradhi hayo umemalizika leo Jumatano nchini Sudan. Mkutano huo wa siku mbili uliofanyika mjini Khartoum umetathimini mapendekezo ya kutoa huduma ya saratani kwa wakimbizi na kuongeza ufadhili kwa [...]

22/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Takriban watoto milioni 600 wataishi kwenye uhaba wa maji ifikapo 2040-UM

Kusikiliza / Somali visit

Takriban watoto milioni 600 au 1 kati ya 4 kote duniani wataishi katika maeneo ambayo yana uhaba mkubwa wa maji ifikapo mwaka 2040 kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  UNICEF iliyotolewa Jumatano  katika siku ya maji duniani. Ripoti hiyo 'kiu kwa siku za usoni:maji na watoto katika mabadiliko [...]

22/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila kwa wajawazito Lubumbashi DRC ni mengi:Dr Tshanda

Kusikiliza / Dr Micrette Ngalua Tshanda, mtaalamu wa masuala ya wanawake Lubumbashi DR Congo. Ameanzisha hospitali ya kina mama na watoto inayotoa huduma bure.Picha na UN News Kiswahili

Waswahili husema asifiaye mvua imenyea, au siri ya mtungi aijuaye kata. Kwa kila mama wajawazito mjini Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, adha ya kukosa huduma muhimu kwa kutokuwa na fedha imekuwa kawaida, maisha yao na watoto wao yakiwa hatarini kila uchao. Lakini sasa wameanza kupata matumaini baada ya Dr Micrette Ngalula-tshanda ambaye pia [...]

21/03/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Upekee wa ushairi ni kwamba hutumia maneno teule-Walibora

Kusikiliza / Ken Walibora, mshairi na mwandishi wa vitabu mashuhuri kutoka Kenya. (Picha:Kwa hisani ya Ken Walibora)

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya ushairi, shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni,  UNESCO limesema kwamba ushairi unalenga ubinadamu na maadili ya watu wote na kwamba kubadilisha shairi jepesi kuwa kichocheo thabiti kwa ajili ya kuibua majadiliano na kuleta amani. UNESCO inasema kuwa ushairi kama fasihi, ni dirisha linalotoa fursa ya [...]

21/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Elimu , msaada na upendo ni muhimu kwa wenye down syndrome:

Kusikiliza / Watoto wanafanya mazoezi katika chummba cha mazoezi, wengine wao wakiwa na down syndrome. Picha: UNICEF/Giacomo Pirozzi

Leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa unaoathiri uwezo wa kujifunza au down syndrome. Kauli mbiu mwaka huu ni "sauti yangu, jamii yangu" lengo likiwa kuwawezesha watu wenye ugonjwa huo kupaza sauti zao, kusikilizwa na kushawishi sera za serikali na hatua za kujumuishwa katika jamii. Akizungumza katika mjadala maalumu wa kuadhimisha siku hii kwenye makao [...]

21/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kikosi cha kikanda kuwasili Sudan Kusini- Ladsous

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous akiwasili huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini.(Picha:UNIfeed/Video Capture)

Umoja wa Mataifa umesema kuwa kikosi cha kikanda cha ulinzi kitaanza kuwasili Sudan Kusini wiki chache zijazo, ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Baraza la Usalama la umoja huo. Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema hayo leo huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini alikokuweko ziarani kwa [...]

21/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mvutano wa nani awe Waziri Mkuu DRC ndio kikwazo- Ripoti

Kusikiliza / Walinda amani wa Malawi walioko nchini DRC wanapiga doria katika maeneo ya Oicha and Erengeti huko Ben. Picha: MONUSCO/Anne Herrmann

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limejulishwa utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, bado umekwama, ikiwa ni miwili tangu yatiwe saini. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, kuhusu DRC, ripoti iliyowasilishwa na mwakilishi wake maalum nchini DRC, Maman [...]

21/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushairi unatupatia matumaini katika wakati huu mgumu-UNESCO

Kusikiliza / Siku ya ushairi duniani. Picha: ©Shutterstock/UNESCO

Ushairi unatupa matumaini limesema shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO, katika kuadhimisha siku ya ushairi duniani , likipongeza uwezo wa aya kutupumzisha na misukosuko ya maisha ya kila siku na kutukumbusha uzuri wa wale wanaotuzunguka na muhimili utu wa pamoja. Katika ujumbe maalumu wa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO [...]

21/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baadhi ya nchi mke anahitaji kibali cha mume kufanya kazi- Ripoti

Kusikiliza / Picha:UNDP

Ripoti mpya ya maendeleo ya binadamu duniani kwa mwaka 2016 imezinduliwa huko Stockholm, Sweden ikionyesha kuwa katika miaka 25 iliyopita kumekuwepo na mafanikio licha ya changamoto za baadhi ya watu kuendelea kuenguliwa. Nats.. Uzinduzi wa nyaraka hiyo iitwayo “Ripoti ya maendeleo ya binadamu na nani ameachwa nyuma?” huo ulienda sambamba na uonyeshwaji wa video kuhusu [...]

21/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatiwa hofu na kurejeshwa kwa wakimbizi wa Nigeria kutoka Cameroon

Kusikiliza / Yacoubou, 6, na nyanya yake Rahia ambao walinusurika mikononi mwa Boko Haram na kukimbilia Cameroon walioko katika kambi ya Minawao.(Picha:UNHCR/Alexis Huguet)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limesema linatiwa hofu na kuendelea kulazimishwa kwa mamia ya wakimbizi wa Nigeria walioko Cameroon kurejea nyumbani Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, licha ya kutiwa saini hivi karibuni kwa makubaliano ya pande tatu ambayo pamoja na mambo mengine yana lengo la kuhakikisha wakimbizi wanarejea kwa hiyari. Shirika hilo [...]

21/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubaguzi na ghasia kwa misingi ya rangi vinaongezeka-Guterres

Kusikiliza / Wafanya kazi wa MONUSCO wajiunga kuadhimisha siku ya kutokomeza ubaguzi wa rangi. Picha: UN Photo/Abel Kavanagh

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  António Guterres amesema siku ya leo ya kutokomeza ubaguzi wa rangi inakumbusha machungu ya mwaka 1960 nchini Afrika Kusini ambapo waandamanaji 69 waliuawa kwa misingi ya kibaguzi wakati wa uatawala wa makaburu, lakini miaka 57 baadaye inaonekana dunia ipo katika ongezeko la hali ya kutovumiliana na mgawanyiko mkubwa, huku ubaguzi [...]

21/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wazindua kituo cha kuratibu misaada ya kibinadamu Somalia

Kusikiliza / Waathirika wa janga la Somalia.(Picha:OCHA)

Nchini Somalia, Umoja wa Mataifa umezinduzia kituo cha kuratibu operesheni za kukabiliana na ukame ikiwemo usambazaji wa misaada ya kibinadamu kwa ufanisi hususan kusini magharibi mwa nchi. Naibu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Vincent Lelei amesema kituo hicho kipo kwenye mji wa Baidoa na kitakuwa ni muhimu wakati huu [...]

21/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

CSW61 jukwaa la fursa za kuinua wanawake: Mshiriki

Kusikiliza / Maryknoll watoto

CSW61 ni jukwaa la kutupa fursa za kuwaniua zaidi wanawake, amesema  mmoja wa washiriki kutoka shirika la kimataifa la watawa wa kanisa katoliki lifahamikalo kama Maryknoll sisters ambalo lengo lake ni kuwawezesha wanawake na wanajamii wengine katika sekta za elimu, uchumi na mengineyo Felista Wanzagi kutoka Tanzania ambaye ni mtawa katika shirika hilo, amesema mkutano [...]

21/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha ya watu chupuchupu kwenye ajali ya ndege Wau-UNMISS

Kusikiliza / Ndege iliyolipuka kwenye uwanja wa Wau nchini Sudan Kusini,(Picha:UNIfeed)

Mpango wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini UNMIS leo Jumatatu umesaidia kunusuru maisha ya watu baada ya ndege iliyokuwa na abiria 43 kuanguka  kwenye uwanja wa ndege wa Wau na kulipuka. Ofisi ya UNMISS Wau ilikimbiza timu ya dharura kusaidia operesheni za ukozi, ikwa na madaktari, na askari wa zimamoto. Waloshuhudia wamesema ndege hiyo [...]

20/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati yahaki za watu wenye ulemavu kuwa na mwanamke mmoja tu si sahihi

Kusikiliza / Mtoto mwenye ulemavu.(Picha:World Bank/Masaru Goto)

Ukweli kwamba kuna mwanamke mmoja tu aliyechaguliwa na nchi wanachama kufanya kazi kwenye kamati ya haki za watu wenye ulemavu kimsingi sio sawa. Huo ni ujumbe bayana uliowasilishwa na naibu kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Kate Gilmore katika ufunguzi wa kikao cha 17 cha kamati hiyo mjini Geneva, Uswisi. Amezungumza [...]

20/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wa asili wana ujuzi na ukizingatiwa utakuza kipato: Mshiriki CSW61

Kusikiliza / IMG_4425

Katika zama hizi ambazo ajira ni changamoto ya kimataifa, jamii ya watu wa asili na ujuzi wao asilia wanaweza kukuza ajira, amesema Lucy Mulenkei kutoka mtandao wa taarifa kwa watu wa asili IIN, nchini Kenya. Bi. Mulenkei anashiriki mkutano wa kamisheni ya hadhi ya wanawake CSW61 mjini New York Marekani. Katika mahojiano na Joseph Msami wa [...]

20/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yalaani kushambuliwa kwa meli huko Yemen

Kusikiliza / 04-26-2013yemenrefugees-350-300

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeshutumu kitendo cha kushambuliwa kwa meli moja iliyokuwa imebeba watu takribani 145 karibu na pwani ya Hudaydah nchini Yemen. Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo la Alhamisi lilisababisha vifo vya watu 42, miongoni mwao wakimbizi wanawake na [...]

20/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Smurfs waing'arisha siku ya furaha

Kusikiliza / Watoto wa shule huko Monrovia, Liberia waliojawa na furaha.(Picha:UNMIL/Staton Winter)

Leo ni siku ya kimataifa ya furaha, siku ambayo hutumiwa na jumuiya ya kimataifa katika kuchochea amani na utengamano miongoni mwa jamii ili kukuza maendeleo. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Nats! Hao ni vikaragosi wa filamu ya Smurfs wakipatiana ushauri kuwa wasile mgao wote wa chakula, kwani ni lazima kuwa makini katika [...]

20/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya yakabiliana na saratani

Kusikiliza / Matibabu ya saratani kizazi. Picha: GAVI/Olivier Asselin

Mkutano wa 61 wa hadhi ya wanawake CSW61 ukiendelea mjini New York Marekani, mke wa Gavana wa kaunti ya Meru nchini Kenya Phoebe Munya amesema ukosefu wa madaktari wa saratani umekuwa changamoto hususani kwa wanawake jambo lililosababisha kuchukua hatua kunusuru wanawake. Katika mahojiano na idhaa hii Bi Munya amesema afya ya uzazi kwa wanawake ni [...]

20/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatari ya hotuba za chuki inaongezeka-Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Kila mmoja anahitaji kuongeza juhudi katika kukabiliana na ubaguzi wa rangi, hotuba za chuki na uhalifu wa misingi ya kikabila. Huo ni ujumbe wa Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, katika kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi ambayo kila mwaka huadhimishwa Machi 21. Zeid [...]

20/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utawala bora Tanzania umechochea ufadhili wetu- Benki ya Dunia

Kusikiliza / Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim alipokutana na rais wa Tanzania John Magufuli.(Picha:

Nchini Tanzania hii leo, Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim na Rais John Magufuli wameweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu katika eneo la Ubungo kwenye mkoa wa Dar es salaam, moja ya miradi inayofadhiliwa na benki hiyo. Wakati wa kuelekea katika tukio hilo, Rais Magufuli na mgeni wake walisafiri [...]

20/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ueledi ni msingi katika kufanikisha ulinzi wa amani

Kusikiliza / Atul Khare (Picha: UN Photo/Loey Felipe)

Umoja wa Mataifa umeazimia kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kingono vinavyotekelezwa na watendaji wake walio kwenye operesheni za ulinzi wa amani, iwe ni askari, polisi au watendaji wa kiraia. Mratibu maalum wa Umoja huo katika kuimarisha hatua za chombo hicho dhidi ya ukatili wa kingono na unyanyasaji, Jane Holl Lutte amesema hayo akihojiwa na [...]

20/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ILO na wakfu wa Walk Free kuvalia njuga utumwa wa kisasa

Kusikiliza / Utumikishwaji wa watoto nchini Mynmar.(Picha:ILO/Marcel Crozet)

Shirika la kazi duniani ILO na wakfu wa walk Free watashirikiana kutafiti kiwango cha utumwa wa kisasa duniani .Katika ushirika huo uliotangazwa mwishoni mwa wiki, mashirika hayo mawili yataanzisha makadirio ya pamoja ya utumwa wa kisasa kwa nia ya mchakato wa kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs, huku yakijiwekea kiwango cha asilimia 8.7. Makadirio hayo [...]

20/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Licha ya udogo, smurfs wapigia chepuo malengo makubwa ya SDGs

Kusikiliza / smurfs

Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa vikaragosi vya filamu ya Smurfs: The Lost Village wameadhimisha siku ya furaha duniani kwa kuungana na Umoja wa Mataifa kuchagiza kampeni ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Ikipatiwa jina Smurfs wadogo na malengo makubwa, kampeni hiyo inalenga kuhamasisha vijana popote pale walipo kujifunza kuhusu malengo 17 [...]

18/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake CSW61 waangaziwa

Kusikiliza / Washiriki wa kamisheni ya hadhi ya wanawake kikao cha 61 CSW New York.(Picha:UM/Idhaa ya Kiswahili.)

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake umeanza tarehe 13 mwezi huu wa Machi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Asasi za kiraia kutoka sehemu mbalimbali zinazojihusiha na masuala ya ustawi wa wanawake zimewakilishwa huku pia serikali zikituma wawakilishi wake kushiriki katika mikutano mbalimbali ya ndani kuhusu masuala [...]

17/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Calypso yarithishwa kizazi hadi kizazi

Kusikiliza / Wachezaji wa Calypso tamashani El Callao, Venezuela.(Picha:UNESCO/Video Capture)

Fasihi simulizi inaenezwa kutoka jamii moja hadi nyingine kwa njia mbali mbali ikiwemo matamasha. Miongoni mwa fasihi hizo ni utamaduni wa mtindo wa Calypso ambao huweka bayana historia ya jamii hususan ya nchi za Caribea. Mtindo huu umeorodheshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO kama turathi za tamaduni zisizogusika [...]

17/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ijapokuwa hali ya usalama bado ni tete CAR, maendeleo makubwa yamepatikana-Onanga

Kusikiliza / Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati Parfait Onanga-Anyanga.(Picha:UM/JC McIlwaine)

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA, Parfait Onanga-Anyanga, amesema japokuwa hali ya usalama bado ni tete, lakini maendeleo makubwa yamepatikana tangu tangu uchaguzi wa serikali mpya mapema mwaka jana. Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Onanga-Anyanga [...]

17/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Guinea waliokwama Libya warejea nyumbani-IOM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Guinea waliokuwa Libya wakisafirishwa hadi Guinea Conakry.(Picha:IOM)

Wahamiaji 98 raia wa Guinea wakiwemo wanaume 96 na wanawake wawili waliokuwa wamekwama Libya sasa wamerejea nyumbani Conakry kwa msaada wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Ndege ndogo iliyoandaliwa kwa uratibu wa serikali ya Libya na uongozi wa Guinea iliondoka uwanja wa ndege wa Mitiga tarehe 14 mwezi huu, huku shirika la IOM likifanya [...]

17/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki- Gozigozi

Kusikiliza / Neno la wiki-gozigozi

Katika neno la wiki hii leo tunaangazia matumizi yasiyo sahihi ya neno gozigozi. Mchambuzi wetu  Nuhu Zubeir Bakari, ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA anasema neno gozigozi linatumiwa likimaanisha upuuzi au mambo ya hovyo. Lakini kimsingi neno gozi linamaanisha ngozi ya mnyama iliyochunwa na [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Tunahitaji fedha za dharura kusaidia wakimbizi wa Iraq: UNHCR

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa ndani Iraq wanburuta magodoro na vifaa vingine kuelekea makazi yao katika kambi ya Hasansham, Iraq.Picha: © UNHCR/Ivor Prickett

Idadi ya wanaofurushwa makwao ikiongezeka Magharibi mwa Mosul nchini Iraq, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafungua kambi mpya sambamba na wito wa usaidizi kwa wafadhili kuongeza fedha kwa ajili ya ulinzi na malazi kwa wanaofurushwa. Kwa mujibu wa taarifa ya UNHCR, watu 255,000 wamefurushwa kutoka Mosul na maeneo ya karibu tangu [...]

17/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yakaribisha hatua kubwa ya kuwahamiasha waomba hifadhi 10,000 kutoka Ugiriki

Kusikiliza / Suleiman na familia yake walipata walihamishwa kutoka Ugiriki hadi Portugal.(Picha:IOM/2017)

Zaidi ya waomba hifadhi 10,000 sasa wamehamishwa kutoka Ugiriki na kwenda kwenye mataifa menmgine ya Muungano wa Ulaya . Grace Kaneiya na taarifa kamili (TAARIFA YA GRACE) Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM waomba hifadhi hao wamehamishwa chini ya utekelezaji wa mpango wa Muungano wa Ulaya ulioanza mwanzoni mwa Machi wa kuwahamisha [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Janga la wakimbizi wa Sudan Kusini laongezeka, msaada wahitajika-UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini wanaokimbia ghasai nchini mwao hapa wakiwa kambini.(Picha:UNHCR)

Miezi minane baada ya kuzuka upya machafuko Sudan Kusini , baa la njaa lililosababishwa na mchanganyiko wa vita na ukame sasa limefanya janga la wakimbizi nchini humo kuwa moja ya mgogoro wa wakimbizi unaokuwa haraka duniani. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA) Kwa mujibu wa shirik la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi Sudan Kusini wasindikizwa na polisi kufanya mitihani- UNMISS

Kusikiliza / Wanafunzi wa Sudan Kusini wanafanya mtihani yao ya kwawezesha kumaliza shule ya upili. Picha: UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS unawapatia wanafunzi wa kidato cha nne ulinzi wa polisi wanapokwenda kufanya mitihani yao ya mwisho wakati huu ambapo wanafunzi hao walikumbwa na hofu ya usalama. Msemaji wa UNMISS, Daniel Dicknson ameiambia Radio Miraya ya Umoja wa Mataifa kuwa wanafunzi hao ni wale waliopo kwenye kituo cha [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka mmoja baada ya kufungwa mpaka wa Balkan watoto wazidi kua hatarini:UNICEF

Kusikiliza / Watoto waongea juu ya matatiso yanaowakumba ukumbizini. Picha: UNICEF/Video capture

Mwaka mmoja baada ya mpaka wa mataifa ya Balkan kufungwa na Muungano wa Ulaya na serikali ya Uturuki kutoa tamko lenye lengo la kuzuia wimbi la wahamiaji, watoto wakimbizi na wahamiaji wanakabiliwa na hatari kubwa zaidi ya kurejeshwa kwa nguvu, kuwekwa rumande, kunyanyaswa na kunyimwa haki. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna pengo la mishahara baina ya wanawake na wanaume Tanzania: Kigwangalla

Kusikiliza / Dr Hamisi Kigwangalla (kushoto) akihojiwa na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Serikali ya Tanzania imesema injivunia hatua zilizopigwa katika suala la ukombozi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisheria, kiuchumi, kisiasa na hata kijamii. Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia, wazee na watoto, Dr Hamisi Kigwangalla alipohojiwa na idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa kikao cha 61 [...]

17/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usugu wa viuavijasumu ni tisho kwa kwa maendeleo endelevu: UM

Kusikiliza / Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed na Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt Margaret Chan wakizungumza na waandishi wa habari mjini New York juu wa usugu wa viuavijasumu.
Picha: UN/Mark Garten

Usugu wa viuavijasumu au antimicrobial resistance AMR ni tisho kubwa la kutimiza ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu amesema naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed. Amesema hayo hivi leo Alhamisi kwenye makau makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York walipokuwa wakijadili swala hilo na mkurugenzi mkuu wa shirika la afya [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu wa IOM alaani shambulio dhidi ya msafara wa wahudumu wa kibinadamu Sudan Kusini

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing

  Mkurugeni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM William Lacy Swing,  hivi leo amelaani shambulizi dhidi ya msafara wa wafanyi kazi wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini liotokea Machi 14 na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa. Wafanyi kazi hao walivamiwa na watu wenye silaha wasiojulikana walipokuwa  wanarudi Yirol [...]

16/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Heko Rais Touadéra kwa kuanzisha mahakama maalum CAR- Ladsous

Kusikiliza / Herves Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa. Picha: UN Photo/Loey Felipe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu hali ya amani, usalama na kibinadamu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo imeelezwa kuwa mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi,kumekuwepo na mafanikio hasa kurejeshwa kwa utawala wa serikali kwenye mji muhimu wa Bambari. Akihutubia kikao hicho, mkuu wa operesheni za ulinzi wa [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukatili na manyanyaso kazini ni ukiukaji wa haki za binadamu: ILO

Kusikiliza / Wanawake wafanyakazi katika sekta ya nguo nchini Cambodia. Picha:UN-Women/Cambodia/Charles-Fox

Ukatili na manyanyaso kazini dhidi ya wanawake ni tatizo kubwa na la kimataifa limesema shirika la kazi duniani ILO. Akizungumza kwenye mjadala maalumu kandoni mwa kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani uliojadidili ukomeshaji wa ukatili wa wanawake kazini, , Manuela Tomei ambaye ni mkurugenzi wa idara ya hali ya kazi na [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya raia 120,000 wamekimbia madhila magharibi mwa Mosul, Iraq

Kusikiliza / Wakimbizi wanaokimbia vita huko Mosul. Iraq.(Picha:UNHCR/Saif Al-Tatooz)

Tangu vikosi vya kijeshi nchini vianze mapigano ya kukomboa mji wa Mosul mwezi Oktoba mwaka, takribani raia 345,000 wamekimbia makwao, ambapo 275,000 kati yao wanahitaji usaidizi. Amesema mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Bi Lise Grande akizungumza na waandishi wa habari hii leo kwa njia ya video kutoka Iraq. Ameongeza [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shilingi 5,000 zimebadili maisha yangu: Mjasiriamali

Kusikiliza / Nazi ni chakula cha thamani katika nchi nyingi. Picha: FAO

Mjasiriamali kutoka Tanzania Bi Amina Shaaban anasema amefanikiwa kusomesha watoto wake kwa kuanzia na mtaji wa shilingi 5,000 za Tanzania ambapo aliitumia kuuza nazi nakupata faida. Bi Amina ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania Zanzibar, hususani Pemba, ambao wamenufaika baada ya serikali kuelimisha wanawake namna ya kujikomboa kiuchumi ili kukabiliana na chnagamoto ya ajira. Ungana [...]

16/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunawasaka waliotekwa nyara DRC-Dujarric

Kusikiliza / Msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo Stéphane Dujarric akihutubia waandishi habari.(Picha:UM/Mark Garten)

Umoja wa Mataifa umesema unaendelea na msako dhidi ya wataalamu wa kimataifa wawili na wafanyakazi watatu raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC ambao walitekwa nyara na watu wasiojulikana jimboni Kasai nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani msemaji wa Katibu Mkuu wa umoja huo Stéphane Dujarric amesema malalamiko ya [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Guterres azungumzia mapendekezo ya bajeti ya Marekani 2018

Kusikiliza / Walinda amani katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS waadhimisha siku ya walinda amani. Picha: UM/JC McIlwaine

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ameazimia kufanyia marekebisho chombo hicho na kuhakikisha kuwa kinakidhi malengo na kuleta matokeo bora kwa gharama yenye unafuu. Bwana Guterres amesema hayo kufuatia Ikulu ya Marekani kuweka wazi mapendekezo ya bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka wa 2018, mapendekezo ambayo inaelezwa yanalenga kupunguza matumizi kwenye maeneo [...]

16/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahakama ya haki kwa Sudan Kusini ni muhimu zaidi hivi sasa- Mogae

Kusikiliza / Mogae 2

Mwenyekiti wa tume ya pamoja ya ufuatiliaji na tathmini ya hali ya Sudan Kusini, JMEC, Festus Mogae ameshutumu vikali ghasia, mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu unaotekelezwana vikundi vyote vilivyojihami nchini humo. Akifungua mkutano wa wazi wa JMEC kwenye mji mkuu Juba, Bwana Mogae ambaye ni rais mstaafu wa Botswana ametaka wale wote wanaohusika [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yaleta unafuu kwa wanawake wanaofuga kuku Gambia

Kusikiliza / Mwanamake mjasiriamali anakusanya mayai. Picha: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema miradi yake katika nchi za Afrika imeanza kukwamua wanawake wajasiriamali kwa kuwawezesha kuinua vipato na wakati huo huo kuhakikisha upatikanaji wa chakula. Afisa mwandamizi FAO anayehusika na usawa wa kijinsia na maendeleo vijijini Thacko Ndiaye amesema hayo katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Madhila kwa wajawazito ni kama siri ya mtungi ajiuaye ni kata-Dr Tshanda

Kusikiliza / Mama Madeleine Kanku aliamua kujifungua katika kituo cha afya huko DRC.(Picha:UNFPA DRC

Kikao cha 61 cha kamisheni ya hadhi ya wanawke duniani leo mbali na mada zingine kimesikiza taarifa kutoka asasi za kiraia. Miongoni mwa wanaoshiriki kikao hicho ni Dr Micrette Ngalula Tshanda kutoka Lubumbashi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Yeye ni daktari bingwa wa masuala ya wanawake kwa ushirikiano na mumewe wameanzisha shirika lililo [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukwepaji sheria ndio adha kubwa Sudan kusini-UM

Kusikiliza / Huku mapigano yakiendelea baadhi ya watu wanafurushwa makwao kama wakimbizi hawa waliomba hifadhi kanisani huko Wau, Sudan Kusini.(Picha:UNICEF/UN027524/Ohanesian)

Tume ya Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Sudan Kusini, imesema hali ya kibinadamu inaendelea kuzorota nchini humo, huku uvunjaji wa sheria, watu kuswekwa rumande kiholela, utesaji, ubakaji na mauaji vikigeuka kuwa kasumba. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Mwenyekiti wa tume hiyo Yasmin Sooka ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kutia [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani endelezeni usaidizi kwa CAR, hali inadorora

Kusikiliza / Raia na watoto nchini CAR. Picha: MINUSCA

Hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR inazidi kudorora tangu kuanza upya kwa mapigano mwezi Septemba mwaka jana hadi mwezi huu wa Machi. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Kaimu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Michel Yao amesema hayo wakati wa kikao cha wahisani [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili dhidi ya wanawake ni kikwazo katika mazingira ya sasa ya ajira

Kusikiliza / Fundi viatu1

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW61 ukiingia siku ya nne hii leo, mmoja wa washiriki amesema ukatili dhidi ya wanawake unaendelea kuwa kikwazo cha wanawake kushiriki ipasavyo katika mazingira ya ajira hivi sasa yanayobadilika. Akihojiwa na Idhaa hii jijini New York, Marekani kando mwa CSW, Maureen Mukalo wa shirika la [...]

16/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uganda, Kenya zimepiga hatua katika kuwawezsha wanawake:Mawaziri

Kusikiliza / Waziri wa Sicily Kariuki wa Kenya akishiriki vikao vya CSW61.(Picha:Sicily Kariuki)

Kikao cha ngazi ya mawaziri kilichoangazia uwezeshaji wa wanawake na uhusiano wake katika malengo ya maendeleo endelevu SDGs, kimefanyika hii leo ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 61 tume ya hadhi ya wanawake CSW61 unaondelea mjini New York, Marekani. Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wamehutubia kikao hicho akiwamo waziri wa jinsia ,kazi na maendeleo ya jamii [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lajadili jinsi ya kukomesha usafirishaji haramu wa binadamu

Kusikiliza / Wasichana nchini Columbia ambao wamelazimishwa kufanya biashara ya kingono. Picha: UNICEF/Donna DeCesare

barazauhalifu Takwimu bora na ufadhili vitakuwa muhimu sana katika vita vya kimataifa vya kukomesha biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumatano akihutubia baraza la usalama. Mabalozi kutoka nchi wanachama wamekutana kujadili njia za kuzuia mitandao ambayo inafaidika na uhalifu kama kazi za shutruti, uhalifu [...]

15/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake wadhihirisha kuwa kazi ni kazi bora iwe halali

Kusikiliza / wanawake11

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hali  ya wanawake duniani, CSW61 ukiendelea kushika kasi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania wanawake wa mashinani wameanza kuonyesha bayana kuwa zama za kazi fulani ni za wanaume na nyingine ni za kike zimepitwa na wakati. Mathalani udereva wa magari ya abiria, uwakala wa wasafiri na [...]

15/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Imarisheni sitisho la mapigano Syria tufikie walengwa- Guterres

Kusikiliza / Syria-3

Kwa miaka sita sasa, wananchi wa Syria wamekuwa wahanga wa moja ya majanga makubwa zaidi kukumba dunia zama za sasa. Ndivyo ilivyoanza taarifa ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António  Guterres aliyoitoa wakati huu ambapo vita hivyo vinaingia mwaka wa saba ambapo ametangaza maombi mawili ya dharura. Mosi ametaka pande husika kutumia ipasavyo sitisho [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maarifa ni sehemu kubwa ya ukuaji wa uchumi duniani-WIPO

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa WIPO ni Francis Gurry.(Picha:WIPO/ Emmanuel Berrod)

Shughuli za uchumi kote duniani zina kipengee muhimu cha maarifa kuliko wakati mwingine wowote, kwa mujibu wa takwimu za karibuni zilizotolewa na shirika la kimataifa la hati miliki (WIPO). Katika Ripoti yake kwa mwaka 2016 shirika hilo linasema limeshuhudia idadi kubwa ya maombi ya kimataifa ya kulinda masuala ya ubunifu, nembo za biashara na mitindo [...]

15/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Somalia yaanza kutoa chanjo dhidi ya Kipindupindu

Kusikiliza / Utoaji wa chanjo nchini Somalia.(Picha:UNICEF)

Serikali ya Somalia kwa usaidizi wa shirika la afya duniani, WHO limeanza kutoka chanjo dhidi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa watu zaidi ya 450,000 nchini humo. Mwakilishi wa WHO nchini Somalia Dkt. Ghulam Popal amesema watoto wenye umri wa kuanzia miaka miwili hadi watu wazima watapatiwa chanjo hiyo ya matone kwa awamu mbili kwenye maeneo [...]

15/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake wakishiriki katika uongozi huchochea maendeleo

Kusikiliza / wanawake- CSW61-2

Mkutano 61 wa kamisheni ya hadhi ya wanawake duniani CSW, unaendelea  kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, leo pamoja na mambo mengine mjadala unajikita zaidi katika uwezeshaji wa wanawake na malengo ya maendeleo endelvu SDGs. Wawakilishi wa makundi ya wanawake kutoka mashinani hususani barani Afrika wanaeleza changamoto na mafaniko katika [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwakilishi wa wanawake kwenye serikali na bunge wadorora- IPU

Kusikiliza / Mkutano wa kando katika CSW61 kuhusu usawa wa kijinsia kwenye siasa. Picha: IPU

  Idadi ya wanawake walioko kwenye serikali na mabunge kote duniani inadorora licha ya matumaini kuwepo mwaka 2015. Hiyo ni kwa mujibu wa ramani mpya kuhusu wanawake katika siasa mwaka 2017 iliyozinduliwa hii leo jijini New York, Marekani na umoja wa mabunge duniani, IPU na shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya wanawake, UNWomen [...]

15/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto wa Syria na wimbo #Heartbeat wa kuibua matumaini

Kusikiliza / Mtoto Syria

  Miaka sita ya vita nchini Syria ikiwa imetimu, watoto nchini humo wameimba wimbo uitwao Heartbeat au mapigo ya moyo kwa lengo la kutuma ujumbe wa matumaini licha ya madhila wanayokumbana nayo kila uchao. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Nats.. Wimbo unaanza kwa kuonyesha magofu yatokanayo  na mapigano ya miaka sita sasa [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wanawake Kigoma wapewa misaada

Kusikiliza / Sifa na wanae, Riziki na Yamlele, na mjukuu wake katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania.(Picha:UNHCR/T.Monboe)

Wanawake wakimbizi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma Tanzania wamepatiwa misaada ya vifaa vya kujisafi ikiwa ni sahemu ya kuhifadhi hadhi za wanawake ambao hukabiliwa na changamoto nyingi hususani wawapo ukimbizini. Katika mahojiano na Simavu Nangolo wa redio wa shirika Umoja Radio ya Nyarugusu Kigoma, Meneja wa shirika la Twesa Alex Ndondeye, shirika ambalo hufanya [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Yemen yahitaji msaada wa dharura wa chakula- FAO

Kusikiliza / Mwanamke na mtoto wake kijijini nchini Yemen. Picha: FAO/Rawan Shaif

  Uhaba mkubwa wa chakula unatishia uhai wa zaidi ya watu milioni 17 nchini Yemen ambako mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanaendelea kushika kasi tangu mwaka 2015. Taarifa hizo zimo kwenye ripoti ya uchambuzi kuhusu uhakika wa chakula nchini humo, ripoti iliyochapishwa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake wa misaada ya [...]

15/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini imeanza kuwahamisha watu kwa kuzingatia makabila yao

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani katika kitua cha uhamishaji nchini Sudana Kusini. Picha: UNMISS

  Serikali ya Sudan Kusini imeanza kampeni ya kuorodhesha na kuhamisha watu kwa mujibu wa makabila yao amesema mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Yasmin Sooka ambaye pia ni mwenyekiti wa tume maalumu ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa haki za binadamu Sudan Kusini, akizungumza kwenye baraza la haki za binadamu [...]

15/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni wakati wa malipo sawa kwa wanaume na wanawake:UN Women

Kusikiliza / Patricia Arquette mcheza filamu mashuhuri wa Marekani akizungumza katika mjadala wa malipo sawa baina ya wanawake na wanaume kwenye UM New Yoyk . Picha na UN Women Ryan Browm

Patricia Arquette nyota wa Marekani wa kucheza filamu amekuwa miongoni mwa wanaharakati mashuhuri waliotoa wito katika kikao cha 61 ya kamisheni ya hali ya wanawake duniani wa kumaliza tofauti za kijinsia imataifa na kuziba pengo la malipo baina ya wanaume na wanawake. Kikao hicho kilichofunguliwa Jumatatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New [...]

14/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kilimo cha buni chastawisha maisha ya wanawake Uganda.

Kusikiliza / Mama na kijana mvulana wakivuna buni. Picha: FAO

Ujasiriamali ni miongoni mwa mikakati bunifu ya kuwawezesha wanawake kuinuka kiuchumi wakati huu ambapo malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanapigia chepuo uwezeshaji wa wanawake katika kila ngazi. Nchini Uganda, licha ya changamoto kadhaa, Betty ni mfano wa wanawake waliofanikiwa kupitia kilimo cha mibuni. Ungana na John Kibego katika makala ya kumulika mafaniko ya mwanamke huyo.

14/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu wanahitaji msaada haraka baada ya kimbunga kuipiga Madagascar:IFRC

Kusikiliza / Kimbunga Enawo kikipiga Madagascar, kimeua, kuathiri mioundombinu na mashamba pia:Picha na WMO

Maelfu ya watu nchini Madagascar wanahitaji haraka misaada ya kibinadamu baada ya Kimbunga Enawo kupiga kisiwa hicho na kuharibu nyumba huku mafuriko ykiathiri mashamba na jamii ambapo shikisho la chama cha msalaba mwekundu IFRC limeanza kutoa msaada wa dharura. Inakadiriwa kuwa watu kadhaa wamefariki dunia, karibu watu 200 kujeruhiwa na wengine zaidi ya 84,500 kuyahama [...]

14/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ulaya na Asia ya Kati zaingia katika mfumo mpya wa utapia mlo:FAO

Kusikiliza / Picha: FAO

Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo FAO inasema Ulaya na Asia ya Kati inaingia katika mfumo mpya wa utapiamlo, ikiainisha ongezeko la utipwatipwa na maradhi mengine yanayoambatana na hali hiyo. Shirika hilo linasema ukuaji wa uchumi na kuongezeka kwa kipato vimesaidia kuondoa njaa katika kanda hizo lakini pia umesababisha mabadiliko ya mfumo kwa [...]

14/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi mkuu wa IOM azuru kituo cha wahamiaji Niger:

Kusikiliza / Jopo la IOM ziarani NIger. Picha:IOM

Mwishoni mwa juma, Mkurugeni mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, William Lacy Swing ameanza ziara ya siku tatu nchini Niger ambako amekutana na viongozi wa kitaifa na kikanda , na pia kutembelea kituo cha muda cha wahamiaj kwenye mji mkuu wa taifa hilo Niamey. Bwana Swingi amekwenda pia katika mji wa jangwani wa [...]

14/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Syria, janga kubwa zaidi la kibinadamu tangu vita ya kuu ya pili ya dunia: Zeid

Kusikiliza / Mtoto aliye na umri wa miaka 7 anasimama mbemele ya shule yake iliyoboromoka huko Idleb, Syria. Picha: UNICEF

Akilihutubia  jopo la ngazi ya juu la baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi hii leo,  Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa   Zeid Ra’ad Al Hussein, amesema vita vya Syria ni janga baya zaidi la kibinadamu tangu vita pili ya dunia. Taarifa kamili na Flora Nducha. (Sauti ya Flora) Zeid [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Buba waendelea kushambulia watoto duniani: WHO

Kusikiliza / Buba waendelea kushambulia watoto duniani. Picha: WHO

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema ugonjwa wa buba ambao hushambulia zaidi watoto bado unazishambulia nchi 13 duniani, licha ya shirika hilo kutangaza mwaka jana kuwa  India haina tena ua. Taarifa ya shirika hilo kuhusu ugonjwa huo inasema kuwa matibabu yake ni rahisi kwani dozi moja pekee ya kunywa ya dawa iitwayo kwa kitaalamu azithromycin, [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uikukwaji na ukatoili mkubwa unaendelea Libya:UM

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva. Picha: UN Photo/Jean-Marc Ferré

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema Jumanne kwamba imekuwa ikipokea taarifa mbalimbali za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, sheria za kimataifa za binadamu na ukatili kutoka pande zot e za mzozo tangu kuzuka tena kwa uhasama Machi 3 mwaka huu. Ofisi hiyo inasema habari za kuaminika zinaeleza kwamba mauaji ya [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wa kiume badilikeni, wajumuisheni wasichana-Kuria

Kusikiliza / Kelvin Machariya Kuria, Balozi wa vijana kutoka serikali ya Kenya. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Kelvin Macharia Kuria, Balozi wa vijana kutoka serikali ya Kenya, ni miongoni wa washiriki katika mkutano wa 61 wa kamisheni ya wanawake CSW, unaoendelea jijini New York, anasema mitizamo kwa vijana wa kiume kuhusu vijana wenzao wa kike ni nyenzo katika kuwawezesha wanawake kujumuishwa. Kuria ameiambia idhaa hii katika mahojiano maalum kuwa nchini Kenya kuna [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame umeyaweka rehani maisha ya watoto Somalia-UM

Kusikiliza / Ukame uliopo Somalia unahatarisha hali ya watoto.(Picha:UNIfeed/video capture)

Magonjwa yanayohusiana na ukame yamekatili maisha ya watoto 47 katika miiezi miwili iliyopita katika moja ya hospitali inayoendeshwa na serikali mjini Mohadishu Somalia. Rosemary Musumba na taarifa kamili (TAARIFA YA ROSE) Umoja wa Mataifa umetoa onyo kwa dunia kwamba athari za ukame ukichanganya na vita katika taiafa hilo la Pembe ya afrika zinaweza kuwa zahma [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Badala ya kutuhurunmia tuwezesheni watu wenye ulemavu: Seneta Omondi

Kusikiliza / Seneta Omondi ambaye ni mwanamke mwenye ulemavu akiwakilisha kundi la wanawake na wasichana wenye ulemavu. Picha: UM/Idhaa ya Kiswahili

Kikao cha 61 cha kamisheni ya hali ya wanawake kinaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kikihusisha watu kutoka kila kundi kwenye jamii wakiwemo wenye ulemavu. Wakipaza sauti zao wanasema kuwahurumia wanawake na wasichana wenye ulemavu hakuna tija, tuzingatie nmana ya kuwawezesha, hii ni kauli ya mmoja wa washiriki wa mkutano wa 61 kamisheni [...]

14/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC yaanzisha mkakati mpya kupambana na mihadarati

Kusikiliza / Yuri Fedotov, Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, akihutubia wanahabari jijini New York wakati wa kongamano la wadhamini katika kusaidia taasisi zinazopambana na uhalifu wa kuvuka mipala pwani ya Afrika Magharibi. (Picha:Maktaba/ UN /JC McIlwaine)

Mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC Yury Fedotov akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha 60 cha tume inayohusika na dawa za kulevya CND mjini Vienna, Austria ameelezea juhudi za ofisi yake kukabiliana na tatizo la uhalifu wa dawa hizo na kusema wameanzisha mkakati uitwao maendeleo mbadala ili [...]

13/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea Burundi:UM

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la haki za binadamu. Picha: UN Photo/Pierre Albouy

Wajumbe wa tume maalumu ya wa tume ya uchunguzi kuhusu haki za binadamu nchini Burundi, Fatsah Ouguergouz, Reine Alapini Gansou na Françoise Hampson wamewasilisha ripoti yao ya kwanza kwa baraza la haki za binadamu wakisema wana wasiwasi kuhusu kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji mwingine kwa ujumla. Wasema kupitia mfululizo wa mahojiano [...]

13/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Biashara ya vyakula ofisini yaleta nuru kwa Nadine nchini Burundi

Kusikiliza / Mwanamke mjasiriamali atengeneza vitumbua vya kuuza. Picha: UN Women

Malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs yanapigia chepuo harakati za wanawake kujikwamua iwe kiuchumi,kisiasa au kijamii. Matarajio ni kwamba kwa kufanya hivyo maisha ya mwanamke huyo na jamii yake yatakuwa bora na hatimaye ifikapo mwaka 2030 dunia itakuwa pahala salama na bora kwa kila mtu kuishi bila kujali jinsia yake. Nchini Burundi, [...]

13/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

AFD yatoa mkopo wa Euro milioni 200 kwa IFAD kuwekeza maendeleo vijijini

Kusikiliza / Mwanamke mkulima kijijini.(Picha:IFAD)

Wakuu wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo (IFAD) na shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD) leo wametia saini muafaka wa kufanya kazi pamohja ili kuendelea maeneo ya vijijini ambao unajumuisha mkopo wa awali wa Euro milioni 200 kwa IFAD. Akizungunmzia ushirika huo Rais wa IFAD Kanayo Nwanze amesema huo ni muafaka muhimu sana [...]

13/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Keating alaani shambulio la bomu Mogadishu:UNSOM

Kusikiliza / Wazima moto nchini Somalia (mkataba). Picha: UNSOM

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Michael Keating, amelaani vikali shambulio la mabomu katika maeneo mawili tofauti mjini Mogadishu yaliyoripotiwa kuuawa raia kadhaa na kujeruhi wengine wengi mapema Jumatatu. Bwana Keating amesema bomu la kwanza limelipuka karibu na kituo cha mafunzo ya jeshi la taifa cha Dhagabadan, na taarifa za [...]

13/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mazingira safi shuleni ni jukumu letu sote

Kusikiliza / Picha: UNICEF

Shirika lenye kukuza elimu ya msichana Sudan Kusini limejikita katika kutoa mafunzo kwa walimu 2,500 na zaidi nchini kote kwa lengo la kuboresha mazingira safi na kuwafunza wanafunzi kujisafi mashuleni. Akihojiwa na Redio Miraya ya Umoja wa Mataifa nchini humo, Yolanda Elly, Mshauri wa Kijinsia wa shirika hilo amesema ingekuwa vigumu zaidi wao kutoa mafunzo [...]

13/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2016 ulikithiri kwa ukatili dhidi ya watoto Syria-UNICEF

Kusikiliza / Mtoto aliye na umri wa miaka 7 anasimama mbemele ya shule yake iliyoboromoka huko Idleb, Syria. Picha: UNICEF

Ikiwa inaelekea sasa mwaka wa saba tangukuzuka kwa mgogoro nchini Syria, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kwa ukiukwaji dhidi ya watoto nchini humo ulikuwa mbaya zaidi 2016 ikilinganishwa na miaka mingine tangu vita kuanza. Rosemary Musumba na taarifa kamili. ( TAARIFA YA ROSE) Nats! Hao ni baadhi ya watoto wanokabiliwa [...]

13/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pazia la CSW 61, kamesheni ya hali ya wanawake lafunguliwa UM

Kusikiliza / csw 2

Kikao cha 61 ya kamisheni ya hali ya wanawake duniani limefunguliwa hii leo kwenye makao makuu ya umoja wa Mataifa mjini New York. Amina Hassan na maelezo kamili (TAARIFA YA AMINA) Nats…. Mwenyekiti wa kikao hicho cha 61 chenye kauli mbiu " wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika" akikaribisha wajumbe katika mkutano huo. Wanawake kutoka [...]

13/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zaidi zahitajika kukabili umasikini kwa wazee Namibia

Kusikiliza / Mama mzee katika kijiji cha Herero, Aminuis, nchini Namibia.(Picha: Eskinder Debebe)

Namibia imepongezwa kwa ari yake ya kisiasa na mtazamo wa jinsi ya kuboresha maisha ya Wanamibia wote ifikapo 2030 na kulinda haki za binadamu. Hata hivyo nchi hiyo imetolewa wito wa kutimiza ahadi hizo na mtaalamu huru wa Umoja wa mataifa kuhusu kufurahia haki zote za binadamu kwa wazee Rosa Kornfeld-Matte. Rosa ameihimiza nserikali ya [...]

13/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuhitimisha mchakato wa uchaguzi Haiti ni hatua kubwa-UM

Kusikiliza / Uchaguzi nchini Haiti.(Picha:Logan Abassi UN/MINUSTAH)

Mtaalamu huru wa hali ya haki za binadamu nchini Haiti Gustavo Gallón, amehitimisha ziara ya siku nane kisiwani humo katika kutathimini hali ya haki za binadamu baada ya mchakato wa uchaguzi. Mtaalamu huyo amesisitiza kwamba kukamilisha mchakato wa uchaguzi ni hatua kubwa katika taifa hilo, akisifia uwazi, ujuzi na uthibiti wa baraza la mpito la [...]

13/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi mawili ya bomu yakatili maisha ya waSyria 40

Kusikiliza / Watoto wakiendesha baiskeli karibu na nyumba zilizoharibiwa Qara kijijini Damascus nchini Syria.(Picha:UNHCR/Qusai Alazroni)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani mauaji ya watu zaidi ya 40 na kujeruhi wengine katika milipuko miwili ya mabomu yaliyotokea Jumamosi katika mji mkuu wa Syria, Damascus. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa,  wengi wa wale waliouawa walikuwa wasafiri ambao walikuwa wakisafiri kwa basi kwenda katika makaburi takatifu, ambalo [...]

12/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Simulizi ya wanawake Afghanistan itabadilika wakishiriki kwenye uongozi – UNAMA

Kusikiliza / Wanawake nchini Afghanistan wakijadiliana
Picha: UNAMA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao chake kuhusu Afghanistan ambapo mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Tadamichi Yamamoto amesema katika nusu ya kwanza ya kipindi cha serikali ya umoja wa kitaifa, tayari hatua za maendeleo zimepigwa licha ya changamoto zinazotakiwa kupatiwa suluhu siku zijazo. Ametaja maeneo matatua ambayo yameonyesha [...]

10/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi Kigoma waadhiimisha siku ya wanawake

Kusikiliza / Wanawake wakimbizi nchini Tanzania.(Picha:UNFPA/Tanzania)

Maadhimisho ya siku ya wanawake nchini Tanzania yamefanyika sehemu mbalimbali licha ya kwamba kitaifa yamefanyika mkoani Singida. Mkoani Kigoma katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, mvua kubwa iliyonyesha awali haikuwazuai wananchi kujitokeza kuhudhuria maadhimisho hayo yaliyotia fora kwa burudani na ujumbe. Tuungane na Mabamba Mpela Junior

10/03/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Neno la wiki- Jabari

Kusikiliza / Picha:Idhaa ya Kiswahili

Wiki hii tunaangazia neno Jabari na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania. Bwana Sigalla anasema neno hili lina maana zaidi ya moja, maana ya kwanza ni mtawala mkuu wa pekee, maana ya pili ni mtu shujaa asiye na woga na maana ya tatu ni jeuri.

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Kuelekea 2030, wanawake wamejizatiti kufikia #5050

Kusikiliza / Wanawake wanaohsikilia nafasi mbali mbali katika jamii,Afrika Mashariki.(Picha:UM)

Tarehe Nane mwezi Machi, kwa zaidi ya karne moja sasa, imekuwa ni siku  ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Siku hii ikiangazia harakati za kuweka usawa wa kijinsia kwa mustakhbali bora siyo tu wa kundi hilo ambalo ni zaidi ya asilimia 50 duniani, bali pia kwa ulimwengu wote kwani wahenga walisema ukimwendeleza mwanamke umeendeleza jamii [...]

10/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Burudani zasheheni wakati wa kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

Kusikiliza / Wanawake nchini Tanzania katika maadhimisho ya siku ya wanawake. Picha: UM

Wanawake wameshamiri juma hili. Mataifa mengi yameadhimisha siku ya wanawake duniani mnamo Machi nane, siku ambayo huadhimishwa kila mwaka, lengo likiwa kupigia chepuo haki na ustawi wa kundi hilo katika nyanja mbalimbali. Katika makala ifuatayo Assumpta Massoi anamulika namna burudani ilivyotumiwa kufikisha ujumbe hususani nchi zenye mizozo, huku ikiwaliwaza washiriki, wakiongozwa na wanawake ambao ni [...]

10/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya makataba wa amani , machafuko yafurusha maelfu Colombia-UNHCR

Kusikiliza / Soko lilioko San Jose au San Jude jijini Buenaventura nchini Colombia. Picha © UNHCR/Juan Arredondo

Licha ya kusainiwa kwa mkataba wa amani baina ya serikali ya Colombia na kundi la upinzani liitwalo FARC, mwezi Novemba mwaka jana, machafuko nchini humo yanaendelea kufurusha maelfu ya watu, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Mapigano baina ya vikosi hivyo yamedumu kwa miaka 50. UNHCR licha ya kutambua juhudi za [...]

10/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatari zaidi ya Zika kwa nchi zenye mbu Aedes Aegypti- WHO

Kusikiliza / Mbu wa Aedes anayeambukiza virusi vya Zika. Picha ya WHO

Shirika la afya duniani, WHO leo limetoa mwongozo na orodha mpya ya nchi 70 ambazo ziko hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Zika. Mataifa hayo yako katika kanda mbali mbali ikiwemo Ulaya, Amerika, Asia na Afrika ambapo WHO imesema miongoni mwao ni nchi ambako mbu anayeeneza virusi hivyo Aedes Aegypti anapatikana, ingawa maambukizi hayajaripotiwa. Barani [...]

10/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaada wa chakula wawafikia maelfu ya wahitaji Sudan Kusini

Kusikiliza / Wakazi wa Sudan Kusini wapokea mgao wa chakula.9Picha:WFP/Peter Testuzza)

Zaidi ya watu Laki Tatu waliokuwa wanakabiliwa na njaa huko Sudan Kusini wamefikishiwa misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula. Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa masuala ya kibinadamu Jens Laerke amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kutangazwa kwa baa la njaa lililotokana na ukame kwenye maeneo ya Leer na Mayendit tarehe 20 mwezi [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasichana 20 wauawa baada ya jengo la makazi kuteketea Guatemala

Kusikiliza / Msichana anacheza na kna mabati kutoka jengo liloloporomoka nchini Guatemala. Picha: © UNICEF/NYHQ2007-2316/Michael Kamber

Nchini Guatemala, wasichana 20 wameteketea kwa moto baada ya jengo lao la makazi kuungua kitendo ambacho kimehuzunisha shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) UNICEF inasema tukio hili la kutisha pia limejeruhi wengine wengi na imeitaka serikali ya Guatemala na na maeneo ya kikanda kuachana [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Salva Kiir atubu kwa niaba ya taifa lake

Kusikiliza / Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini.(Picha:UNMISS/Isaac Billy)

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, amongoza maelfu ya raia nchini humo kwa ajili ya maombi maalum ya toba. Grace Kaneiya na taarifa kamili. (TAARIFA YA GRACE) Nats! Ni sauti ya Rais Kiir, katika maombi maalum ya toba yaliyofanyika kwenye makumbusho ya kiongozi wa zamani wa taifa hilo John Garang, mjini Juba ambapo kwa niaba [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya Yemen yafurusha maelfu ya watu- UNHCR

Kusikiliza / Raia wa Yemen ambao wamekimbilia majimbo ya Taiz na Al-HudaydahPicha: © UNHCR/Shabia Mantoo

Mapigano mapya kwenye maeneo ya kati na magharibi mwa Yemen yamelazimisha watu zaidi ya elfu 60 wakimbie makazi yao. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mapigano hayo yanaendelea kwa wiki sita sasa na idadi kubwa ya raia wamekimbilia majimbo ya Taiz na Al-Hudaydah. Msemaji wa UNHCR William Spindler amesema wananchi hao [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Faida za wahamiaji za kiuchumi zitambulike: UM

Kusikiliza / Wahamiaji wajasiriamali kutoka Syria walioko nchini Turkey wapata mafunzo ya ufundi stadi kupitia programu ya mshikamano ya kijamii. Picha: IOM

Likizingatia mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi na wahamiaji wa hivi karibuni, baraza la haki za binadamu hii leo mjini Gweneva Uswisi, limekuwa na mjadala shirikishi kuhusu haki za kundi hilo katika muktadha wa kuhama kwa makundi makubwa. Wajumbe wa baraza hilo wamesisitiza kuwa kuheshimu haki za binadamu kwa wahamiaji sio tu hitaji la [...]

10/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usawa hautakamilika iwapo hautajumuisha wanawake mashinani

Kusikiliza / Justine Uvuza. Picha: Idhaa ya Kiswahili/Amina Hassan

Ujumuishwaji wa wanawake mashinani ni dhana isiyokwepeka katika kutimizia dhima ya maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu ambayo ni wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika, inayokwenda sambamba na lengo nambari kumi la maendeleo endelevu yaani SDG’s, ambalo linachagiza ulimwengu kupunguza ukosefu wa usawa. Akihojiwa na Idhaa hii, Dkt. Justine Uvuza wa Shirika la asasi [...]

10/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkakati mpya unalenga kusaidia zaidi waathirika wa ukatili wa kingono

Kusikiliza / Presentation of the Sexual exploitation and abuse report

Umoja wa Mataifa umeweka bayana mkakati mpya wa kuzuia na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono vinavyotekelezwa na wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbali mbali duniani. Mapendekezo hayo yamo kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ripoti ikielezwa kuwa inaangazia zaidi waathirika wa vitendo hivyo. Katibu Mkuu aliwasilisha mapendekezo [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tukipata teknolojia wezeshi tutazalisha maradufu: Wajasiriamali Wanawake

Kusikiliza / Wanawake wajasiriamali nchini Tanzania.(Picha:ILO/Video capture)

Ukosefu wa teknolojia wezeshi unapunguza mapato kusudiwa kwa wanawake mkoani Kagera nchini Tanzania, hii ni kwa mujibu wa wajasiriamali mkoani humo ambao wanasema wakiwezeshwa kiteknolojia watazalisha maradufu. Nicolaus Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya Kagera nchini humo, amevinjari hadi wajasiriamali hao wanawake wanapofanya kazi zao ili kujionea. Ungana naye katika makala ifuatayo.

09/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini ya suluhu Burundi, nitaitisha mkutano wa dharura: Mkapa

Kusikiliza / Msuluhishi wa mgogoro wa Burundi anayewakilisha Muungano wa Afrika AU, Rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa. Picha: UM/Video capture

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo Machi tisa, limejadili hali ya kiusalama nchini Burundi, ambapo imeelezwa kuwa usalama umeendelea kuzorota na hofu imetanda miongoni mwa raia. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, kuhusu kuzuia migogoro Jamal Benomar, ameliambia baraza hilo kuwa ikiwa ni miaka miwili tangu kuzuka kwa mgogoro nchini [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wagonjwa wa figo Yemen wahaha kupata tiba

Kusikiliza / Utoaji wa huduma wa afya kwa wagonjwa wa figo.(Picha:WHO)

Nchini Yemen, mapigano yakiwa yanaendelea kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Houthi miundombinu ya kiafya inazidi kusambaratika ikiacha wagonjwa taabani wakiwemo wale wa figo. Shirika la afya ulimwenguni WHO nchini humo linasema kutokana na mapigano, wagonjwa wa figo hivi sasa wanashindwa kupata huduma ya kusafisha damu katika vituo vingine na hivyo kulazimika kwenda [...]

09/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujasiri wa wakazi wa Ziwa la bonde Chad unatia matumiani -Balozi Rycroft

Kusikiliza / Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ambaye ni rais wa Baraza la Usalama mwezi Machi akihutubia kikao hicho.(Picha:UM/Manuel Elias)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo hapa makao makuu jijini New York kuwasilisha ripoti yake kufuatia ziara yao ya bonde la Ziwa Chad, Amina Hassan nataarifa kamili. (Taarifa ya Amina) Akihutubi kikao hicho Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ambaye ni rais wa baraza hilo mwezi huu wa Machi na pia kiongozi wa [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sitakubali anayepeperusha bendera ya UM atutie aibu- Guterres

Kusikiliza / Moja ya nukuu kutoka ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. (Picha:UN)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasilisha ripoti yake mbele ya Baraza Kuu inayotaja mikakati mipya mahsusi ya kuepusha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono kwenye operesheni za ulinzi wa amani za chombo hicho. Amesema mikakati hiyo ni muhimu kuhakikisha hakuna mtuhumiwa yeyote anakwepa sheria wakati huu ambapo watuhumiwa wa vitendo hivyo [...]

09/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yachukua hatua kuimarisha utoaji wa haki kwa watoto DRC

Kusikiliza / conference-MONUSCO

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kwa kushirikianana asasi isiyo ya kiraia AJEDEC na serikali wameanza ujenzi wa mahakama wilaya kwenye jimbo la Ituri. Mahakama hiyo inalenga kuimarisha usimamiaji wa haki na sheria kwa kesi zinazohusu watoto hususan visa vinavyohusiana na ulinzi wa mtoto. MONUSCO imegharimia [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka wa 7 wa vita, bado Syria iko njiapanda- UNHCR

Kusikiliza / Msichana Wafaa akiwa na mamake, yeye ni muathirka wa vita vya Syria.(Picha:UNHCR)

Wakati dunia inajiandaa kushuhudia vita nchini Syria vikiingia mwaka wa saba tangu vianze, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetaka jamii ya kimataifa iongeze maradufu usaidizi wake wakati huu ambao mamilioni ya raia wanaendelea kukumbwa na machungu. Grace Kaneiya na taarifa kamili. (Taarifa ya Grace) Filippo Grandi ambaye ni Kamishna Mkuu wa [...]

09/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waalimu wa shule wasiwajibishwe kwa mipango ya majanga

Kusikiliza / Jair TORRES, Mtaalamu wa upunguzaji hatari ya majanga kwnye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Picha: UNESCO

Walimu wa shule wana majukumu ya kutosha darasani bila kutarajiwa kuwa wsimamizi wa kudhibiti hatari ya majanga pia. Mtazamo huo ni kwa mujibu wa Jair Torres, mtaalamu wa upunguzaji hatari ya majanga kwnye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO. Akiwasilisha mkakati wa tano wa UNESCO katika upunguzaji wa hatari ya [...]

09/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majanga ya kimya kimya yanayosambaratisha mazao mara nyingi hupuuzwa: FAO

Kusikiliza / jimbo la Tahoua nchini Niger, lililoathirika sana na Ukame na kuzusha hofu ya upungufu wa chakula.(Picha:WFP/Phil Behan)

Linapokuja suala la kulinda mazao na maisha ya kilimo, majanga ya kimyakimya mara nyingi hayaripotiwi na yanaweza kutokea mara nyingi na kufanya uharibifu mkubwa kuliko kimbunga au mafuriko. Hayo yamesemwa na Anna Ricoy, afisa wa shirika la chakula na kilimo FAO katika kanda ya Amerika ya Kusini ambaye ni mtaalamu wa hatari ya majanga. Bi [...]

09/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalaani urushwaji wa makombora wa DPRK

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama walipotoa azimio kulaani majaribio ya makombora iliyofanywa na Jamhuri ya kidemokrasia ya Korea au DPRK
Picha: UN/Rick Bajornas

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha faragha hivi leo na kupokea taarifa ya mkuu wa Idara ya maswala ya kisiasa Jeffrey Feltman kufuatia hatua ya hivi karibuni cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha makombora manne ya masafa marefu. Makombora matatu kati ya hayo yalitua baharini kwenye [...]

08/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwanasiasa msichana chipukizi alonga ''Wanawake msibweteke muhimu ni nidhamu''

Kusikiliza / Zainab Abdallah.(Picha:Z.Abdalla)

Tunapomulika siku ya wanawake duniani leo Machi nane, ni muhimu tumulike wanawake waliopiga hatua katika nyanja tofauti. Kutana na Zainab Abdallah Issa, mwanasiasa chipukizi nchini Tanzania na aliye mkuu wa wilaya mdogo zaidi. Aliteuliwa mwaka jana kuwa mkuu wa wilya ya Pangani akiwa na umri wa miaka 23, hatua iliyoshangaza wengi. Yeye anaiona kama fursa [...]

08/03/2017 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani shambulizi kwenye hospitali mjini Kabul

Kusikiliza / Makao makuu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNAMA 
Picha: UNAMA/Fardin Waezi

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulizi la kigaidi lenye utata lililotekelezwa mjini Kabul  asubuhi ya kuamkia hivi leo ambako wahusika waliovalia mavazi ya daktari walilipua gari la kujitoa mhanga katika mlango wa hospitali  ya Sardar Mohammad Daud Khan na kusababisha vifo na majeruhi ambapo, idadi kamili bado haijulikani. Naibu mkuu wa [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kidole kimoja hakivunji chawa,wanawake waambiwa waungane

Kusikiliza / Jiko 1

Kuwa na virusi vya Ukimwi VVU, haikuwazuia kikundi cha wanawake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC kujiendeleza kiuchumi. Ndivyo unavyoweza kusema ukitafakari juhudi za wanawake katika ulimwengu wa kazi unaobadilika, ambapo licha ya hali zao hizo za kiafya, wanawake katika kikundi kiitwacho GSV jimboni Kivu ya Kusini, wamenufaika kwa mradi wa majiko. Langi Stany [...]

08/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia ni suluhu ya 50/50 ifikapo 2030- UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ujumbe wa video. Picha: UM/Video Capture

Ikiwa leo ni siku ya wanawake duniani ujumbe ukiangazia wanawake katika mazingira yanayobadilika ya kazi, kuelekea usawa wa kijinsia mwaka 2030, Umoja wa Mataifa umetaka ushiriki wa wanawake kikamilifu ili kufanikisha azma hiyo. Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Nats.. Kibao hicho I will rise up kiliporomoshwa na mwimbaji mwenye kipaji Jana Brown kwenye moja ya [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa yaheshimu faragha mitandaoni-UM

Kusikiliza / Picha:UN Photo/JC McIlwaine

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataiafa kuhusu haki ya faragha, Joseph Cannataci, amelaani sheria ya upekuzi na kuyataka mataifa kote ulimwenguni kuheshimu haki ya faragha ambayo amsema ni haki ya kimataifa katika zama hizi za kidijitali. Kupitia ripoti yake aliyowasilisha hii leo mjini Geneva Uswisi kwenye baraza la haki za binadamu, Bwana Cannataci ameeleza kusikitishwa [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake shupavu waenziwa Uganda

Kusikiliza / Picha: UNFPA

Uganda nayo imejiunga na Dunia kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambako wanawake zaidi ya hamsini wamepatiwa medali ya kuwaenzi kwa ushupavu wao katika nyanja mbalimbali. Shuhuda wetu hujo ni John Kibego. (TAARIFA YA KIBEGO) Nats! Miongoni mwa waliopatiwa midali ni mwanajeshi mwanmke wa cheo cha juu zaidi katika historia ye jeshi la Uganda.  Huenda [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa kijinsia ni chachu katika kukomesha njaa na umasikini-UM

Kusikiliza / Mchango wa wanawake wa vijijini katika uhakika wa chakula haupaswi kupuuzwa.(Picha:FAO-WFP/Ricci Shryock)

Shirika la chakula na kilimo FAO kwa ushirikino na mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na shirika la mpango wa chakula duniani WFP, wamechagiza juhudi katika kuhakikisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake hasa wa vijijini, masuala ambayo wanasema ni chachu ya kukomesha njaa , utapia mlo na umasikini. Kauli hiyo imetolewa kwenye [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku moja nitakuwa mwanamke mahiri duniani-Zainabu

Kusikiliza / Zainab Abdallah.(Picha:Z.Abdalla)

Zainab Abdallah Issa ndiye mkuu wa wilaya mdogo zaidi nchini Tanzania akiwa na umri wa miaka 24. Aliteuliwa na Rais wa nchi hiyo kushika wadhifa huo wa ukuu wa wilaya ya Pangani mwaka jana akiwa na umri wa miaka 23. Katika mahojiano na Kelvin Mpinga wa redio washirika Pangani Fm ya Tanga Tanzania, aliyetaka kufahamu [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii zetu zitakuwa thabiti iwapo tutashirikisha wanawake- Guterres

Kusikiliza / Picha: Julius Mwelu - UN Habitat

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema ulinzi wa wanawake dhidi ya ukiukwaji wa haki zao pamoja na umaskini vitawezekana iwapo watapatiwa kipaumbele kamilifu kwenye mipango ya kuwawezesha. Akizungumza mjini Nairobi, Kenya ambako yuko ziarani, Bwana Guterres amesema ujumuishaji huo uhakikishe wamo kwenye taasisi za serikali, siasa na biashara bila kusahau bodi za [...]

08/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika ionekane kama bara la mafanikio sio matatizo tu-Guterres

Kusikiliza / KENYA

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres anayeendelea na ziara yake nchini Kenya amesema anaamini kwamba simulizi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Afrika haijakuwa sawa wakati wote, kwani wakati mwingine imejikita sana katika mogogoro . Akiongeza kuwa ni kweli kwamba kuna migogoro Afrika kama ilivyo barani Ulaya au Asia, kuna migogoro kila kona, akasisitiza [...]

08/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Jumuisha sauti za wanawake kwenye mchakato amani Maziwa Makuu- Djinnit

Kusikiliza / Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Said Djinnit akuhutubia waandishi wa habari. Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Kujumuisha wanawake katika mchakato wa amani kwenye ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika ni muhimu kwa kuwa inaleta maslahi mengi na endelevu kwa jamii na mataifa kwa ujumla. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwenye ukanda huo Said Djinnit ametoa wito huo leo ikiwa ni siku ya wanawake duniani akisema ili kuondoa mzizi wa mzozo [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna kazi ya mwanamke au mwanaume kazi ni kazi

Kusikiliza / Mariana Tarimo (Kushoto) mfanyakazi wa UN Women nchini Tanzania na Mariana Msale dereva wa UN women Tanzania. Picha: UNIC Tanzania/Video capture

Ingawa mabadiliko ya fikra duniani yanaanza kujitokeza sanjari na mabadiliko ya ulimwengu wa kazi, bado kuna dhana kwamba kuna ajira ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume tu na ni nadra kumkuta mwanamke akifanya mathalani kuwa dereva. Lakini dhana hiyo imekuwa potofu kwa Mariana Tarimo anayefanya kazi na shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

Sera zinazojali jinsia zimeleta mafanikio kwa kampuni- UNWomen

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen Phumzile Mlambo-Ngucka nchini Sweden azungumza kuhusu uwezeshaji wa wanawake. Picha: UN Women

Kampuni zinazoajiri wafanyakazi kwa kuzingatia sera za usawa wa kijinsia zimedhihirisha jinsi mwelekeo huo ulivyo na manufaa kwa maendeleo ya kampuni husika. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen Phumzile Mlambo-Ngucka amesema hayo akihojiwa na radio ya huo katika maadhimsisho ya siku ya wanawake duniani hii leo. Amesema [...]

08/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

Kila mtoto anastahili kuishi kwa usalama: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto pekee yake kwenye safari kusaka usalama
Picha: UNICEF/UN030740/Zehbrauskas

  Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Anthony Lake amesema kuwa watoto wakimbizi wanaokimbia machafuko na ugaidi hivi sasa wanahitaji msaada kuliko wakati mwingine wowote. Lake ametoa kauli hiyo kufuatia  amri mpya nyingine ya Marekani iliyotolewa  Jumatatu kuhusu wanaosaka hifadhi na ukimbizi. Amesema watoto ni miongoni mwa watu wanaoishi [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM na AU wazindua ripoti ya haki za wanawake Afrika

Kusikiliza / Wanafunzi nchini Kenya. Picha: OHCHR

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa , Muungano wa Afrika na kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na masuala ya wanawake UN Women, leo wamezindua ripoti kuhusu haki za wanawake Afrika. Hii ni ripoti ya kwanza katika mfululizo uliopangwa kuhusu haki za wanawake katika bara hilo itaklayojikita katika mada mbalimbali. Mashirika hayo [...]

07/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dola Bilioni 2 zahitajika kusaidia Kenya, Ethiopia na Somalia: UM

Kusikiliza / Mama na mtoto wake ni miongoni mwa raia wa Somalia wanaokumbwa na uhaba wa njaa
Picha: UN/OCHA

Zaidi ya dola bilioni 2 zinahitajika kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Kenya, Somalia na Ethiopia mwaka huu wa 2017. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya naibu wa msemaji wa ofisi ya masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Jens Laerke. Kwa upande wa Somalia pekee msemaji huo amekaribisha mchango wa dola milioni [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake Uganda wajitosa kwenye ufundi kujipatia kipato.

Kusikiliza / Wanawake wajasiriamali nchini Uganda. Picha: UN Women/Video capture

Wanawake nchini Uganda kama zilivyo sehemu nyingine, wanajitutumua kukabiliana na changamaoto za kazi katika ulimengu unaobadilika ili kujipatia kipato na pia kutimiza malengo ya usawa wa 50 kwa 50 kifikapo mwaka 2030. Katika pitapita yake kutathimini kazi hizo kuelekea siku ya wanawake duniani Machi nane, John Kibego kutoka Uganda amekutana na mwanamke ambaye ndiye chanzo [...]

07/03/2017 | Jamii: Makala za wiki, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

SDGs bila takwimu haiwezekani: Montiel

Kusikiliza / ASG Stats

Ikiongozwa na kauli mbiu, takwimu bora maisha bora, tume ya takwimu ya Umoja wa Mataifa imeanza kikao chake cha 48 hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika idara ya uchumi na masuala ya kijamii [...]

07/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Amerika himizeni kujihami na majanga: UM

Kusikiliza / Familia katika Idara ya Grand'Anse waliopoteza mali yao baada ya kimbunga Mathew. Picha: © EU/ECHO/J. Torres

Majanga kama vile kimbunga Matthew yaliyokumba bara Amerika miaka ya hivi karibuni, ni udhihirisho wa changamoto zinazokabili dunia katika kufikia malengo ya mkataba wa Sendai wa kupunguza majanga. Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza majanga UNISDR Robert Glasser amesema hayo hii leo wakati akifungua mkutano wa tano kuhusu kupunguza majanga barani Amerika [...]

07/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake waongezeka katika mabunge, kasi zaidi yahitajika: IPU

Kusikiliza / Ripoti ya IPU kuhusu yaliyojiri mwaka jana. Picha: IPU

Hatua zaidi na utashi thabiti wa kisiasa unahitajika, kuwezesha uwakilishi wa wanawake bungeni ili kuendeleza kasi ya maendeleo yaliyofikiwa duniani katikaa kipindi cha muongo mmoja uliopita, umesema muungano wa mabunge duniani IPU. Katika ripoti ya IPU kuhusu tathimini ya mwaka huu iitwayo Wanawake bungeni 2016, iliyotolewa kuelekea siku ya wanawake duniani Machi nane hapo kesho, [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale, SIKU YA REDIO 2017 | Kusoma Zaidi »

Mipango ya Hungary kuwashikilia waomba hifadhi yatia hofu:UNHCR

Kusikiliza / Wahamiaji kutoka Pakistani huko Kos, Ugiriki waonyesha ramani waliyopokea kuhusu kufungwa kwa mpaka wa Hungary na ikipendekeza kupitia Croatia. Picha: IOM

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linatiwa hofu na sheria mpya iliyopigiwa kura jumanne kwenye bunge la Hungary ambayo itafanya kuwa lazima kuwashikilia waomba hifadhi wote wakiwemo watoto kwa kipindi chote cha mchakato wa kuomba hifadhi. Kwa mujibu wa UNHCR hii inamaanisha kwamba kila muomba hifadhi wakiwemo watoto watazuiliwa kwenye makontena [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upinzani dhidi ya haki za wanawake hutuathiri sote- Zeid

Kusikiliza / Wanawake na wasichana katika sekta ya nguo mara nyingi hunyanyazwa na kulazimishwa kufanya kazi masaa mingi kupita ya kawaida bila kulipwa. Picha: ILO/A. Khemka

Inasikitisha sana kuona mafanikio yaliyopatikana kuhusu haki za wanawake, yaanza kurudishwa nyuma katika baadhi ya maeneo duniani, amesema Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein katika ujumbe wake kuelekea siku ya wanawake duniani siku ya Jumatano. Rosemary Musumba na ripoti kamili. (Taarifa ya Rosemary) Kamishna Zeid amesema mamilioni ya wanawake walijitoa maisha [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukarabati wa barabara inayounganisha DRC na Burundi waanza

Kusikiliza / ukarabati wa barabara inayounganisha jimbo la Kivu Kusini na Burundi kupitia Uvira nchini DRC. Picha: MONUSCO

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO umeanza ukarabati wa barabara inayounganisha jimbo la Kivu Kusini na Burundi kupitia Uvira. Ukarabati wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa Sita utafanyika kwa siku 50 na hivyo kumaliza adha ya usafiri ambapo wananchi walitumia nusu saa kwa gari kusafiri [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzizi wa ubaguzi wa wanawake bado unamea- Wataalamu

Kusikiliza / Wanawake wakiandamana jijini New York kwa ajili ya kuchagiza usawa wakijinsia.(Picha:UN Women/J Carrier)

Harakati za kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake zimeendelea kugonga mwamba licha ya mafanikio katika baadhi ya maeneo tangu kuanza kwa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani zaidi ya karne moja iliyopita. Hiyo ni kwa mujibu wa wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wanawake waliokutana leo huko Geneva, Uswisi kuangazia siku ya wanawake itakayoadhimisha [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viuatilifu vinatishia haki za binadamu- Wataalamu

Kusikiliza / Matumizi ya madawa hatari shambani yana athari kwa binadamu.(PichaFAO/Asim Hafee)

Wataalamu wawili maalum wa Umoja wa Mataifa wametaka kuwepo kwa mkataba mpya wa kimataifa utakaodhibiti na kuondokana na viuatilifu au madawa hatari yanayotumika mashambani. Wataalamu hao Hilal Ever wa haki za chakula na Baskut Tuncak anayeangazia masuala ya sumu wamelieleza Baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi kuwa matumizi kupita kiasi ya viuatilifu kwa [...]

07/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Niko Somalia kuonyesha mshikamano wangu:Guterres

Kusikiliza / SG SOMALIA 3

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Somalia, akizuru Moghadishu na Baidoa kwa mara ya kwanza akiwa katika wadhifa huo ili kuonyesha mshikamano na watu wa taifa hilo ambao amesema wako katika hali ya madhila lakini pia matumaini. Flora Nducha na taarifa kamili (TAARIFA YA FLORA) Amesema wako katika madhila kutokana na [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Stadi za kazi kambini zamwezesha mkimbizi mwanamke kujikimu

Kusikiliza / Finess-1

Kuelekea siku ya wanawake duniani tarehe 08 mwezi huu wa machi, mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Burundi ameelezea vile ambavyo stadi za kazi kambini zimemwezesha kuungana tena na familia yake. Mahimana Faines ambaye sasa anaishi kambi ya wakimbizi ya Lusenda nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC amesema anasema kupitia kituo salama kambini Lusenda alipata taarifa [...]

07/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Guterres alaani kitendo cha DPRK kurusha makombora

Kusikiliza / Katibu mkuu António Guterres
Picha: UN/Rick Bajornas

Secretary-General António Guterres. UN Photo/Rick Bajornas

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guterres amelaani kitendo kilichoripotiwa cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha makombora manne ya masafa marefu. Imeelezwa kuwa makombora matatu kati ya hayo manne yametua baharini kwenye ukanda mahsusi wa kiuchumi wa Japan. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Katibu Mkuu akisema vitendo vya namna [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marekani yatoa kanuni mpya za ukimbizi, UNHCR yasisitiza misingi ni ileile

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi .(Picha:UM/Evan Schneider)

Kufuatia amri mpya ya Marekani ilyotolewa leo kuhusu wanaosaka hifadhi ya ukimbizi nchini humo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesisitiza kuwa wakimbizi ni watu wa kawaida wanaokimbia vita, ghasia au mateso na bado wanasalia na umuhimu wa kupatiwa hifadhi na ulinzi. Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema nia inasalia ile [...]

06/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

MINUSMA yalaani ukiukwaji wa kusitisha mapigano Timbuktu Mali

Kusikiliza / Picha: UN video capture

  Vituo viwili vya kijeshi vilivyokuwa vinashika doria vimeshambulia  jana jumapili na kikundi cha waasi wenye silaha huko kaskazini mwa mji wa Timbuktu nchini Mali. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA ambao unasema kuwa vikundi hivi vyenye silaha vinapinga uanzishwaji wa serikali ya mpito ya Taoudenit, [...]

06/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasomali wanahaha kukidhi mahitaji ya mlo kwa familia- O’Brien

Kusikiliza / O'Brian

  Mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien ametembelea makazi ya muda ya wakimbizi wa ndani yaliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu ambako amejionea hali halisi ya njaa inayokabili nchi hiyo. Ameshuhudia jinsi familia zinavyohaha kukidhi mahitaji ya mlo ya watoto wao akisema kwa kujionea mwenyewe, amepata [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makumbi ya nazi huniingizia kipato na kuwasomesha watoto-Bahati

Kusikiliza / Bahati Sudi ambaye ni mjasiriamali nchini Tanzania.(Picha:Maajabu Ally)

Makumbi ya nazi ambayo mara nyingi hutupwa baada ya kufuliwa kwa nazi, na hivyo kusababisha uchafu wa mazingira, yanatumiwa na mjasiriamali mwanamke mkoani Tanga nchini Tanzania, kujinufaisha kwa kipato na hivyo kutunza mazingira. Hii ni sehemu ya shuhuda za wanawake kuhusu namna wanavyokabiliana na changamoto za kazi katika dunia inayobadilika kila uchao, ikiwa ni kuelekea [...]

06/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Haiti inahitaji msaada wa ujenzi mpya-UNISDR

Kusikiliza / Athari za madhara ya Kimbunga Mathew ni dhahiri nchini Haiti.(Picha:Logan Abassi UN/MINUSTAH)

Wito wa msaada wa ujenzi mpya kwa ajili ya Haiti umetolewa jumatatu na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa athari za majanga UNISDR baada ya kimbunga Matthew kuliacha taifa hilo na hasara ya dola bilioni 2.7. Rosemary Musumba na taarifa kamili. (TAARIFA YA ROSE) Msaada huo wa haraka ni kwa ajili ya [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA bado ina hofu kuhusu DPRK

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Dkt. Yukiya Amano.(Picha:IAEA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Dkt. Yukiya Amano ameseam bado ana wasiwasi mkubwa kuhusu mpango wa nyuklia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK wakati huu ambapo vyombo vya habari vinaripoti kuwa nchi hiyo siku ya jumapili imefyatua makombora manne ya masafa marefu. Akihutubia mkutano wa bodi [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania inajitahidi katika vita dhidi ya mihadarati:UM

Kusikiliza / Madawa ya kulevya kutumika licha ya vikwazo.Picha: UNIC/Tanzania

Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania jumatatu wamezindua ripoti kuhusu matumizi ya dawa za kulevya iliyotolewa na bodi ya kimataifa ya kuzuia dawa za kulevya INCB kwa mwaka 2016. Ripoti hiyo imejikita na athari na matumizi ya dawa hizo kwa wanawake,, akiizungumzia mjini Dar Es salaam Tanzania Mratibu mkazi wa Umoja wa [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

EU yapigia chepuo mlo shuleni nchini Burundi

Kusikiliza / Watoto nchini Burundi wanaopokea mlo shuleni.(Picha:WFP/Didier Bukuru)

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limekaribisha msaada wa zaidi ya dola milioni Tano kutoka Muungano wa Ulaya, EU kwa ajili ya mradi wa mlo shuleni nchini Burundi. Mwakilishi mkazi wa WFP nchini Burundi Charles Vincent amesema fedha hizo zitaelekezwa jimbo la Gitega, katikati mwa nchi ambako siyo tu zitaimarisha uwezo wa watoto shuleni, [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wajumuishwe ajenda 2030- Gilmore

Kusikiliza / Ni muhimu watoto kama hawa walioko nchini Mali wajumuishwe katika ajenda 2030.(Picha:UM/Marco Dormino)

Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Kate Gilmore amesema mustakhbali bora wa dunia unawezekana iwapo masuala ya watoto yatapatiwa kipaumbele wakati wowote wa kujadili amani na maendeleo. Amesema hayo wakati akifungua sehemu ya kwanza ya mkutano wa mwaka wa baraza hilo kuhusu haki za mtoto huko Geneva, Uswisi akisema hivi [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uchafuzi wa hewa huua watoto, jihadhari: WHO

Kusikiliza / Watoto nchini Papua Guinea Picha na Y. Shimizu/WHO

Kama ulifikiri magonjwa ndio sababu pekee ya vifo kwa watoto chini ya miaka mitano, sivyo! Mazingira hususani uchafuzi wa hewa ndani au nje ya nyumba , moshi umpatao asiyevuta tumbaku, ni mongoni mwa sababu ya kifo cha mtoto mmoja kati ya watano limesema shirika la afya ulimwenguni WHO. Amina Hassan na maelezo kamili. ( TAARIFA [...]

06/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitisho dhidi ya wafanyakazi wa UM wahudumu wa misaada havikubaliki: UM

Kusikiliza / Vikosi vya kijeshi vya MINUSCA nchini CAR
Picha: UM/Catianne Tijerina

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA wametoa wito wakutokubaliana na vitisho vilinavyotolewa na muungano wa FPRC dhidi ya wafanyakazi wa MINUSCA, watendaji wa kibinadamu na raia. Ujumbe huo umeonya viongozi wa muungano huo kuwa watawajibika mmoja kwa mmoja kwa vitendo hivyo.  Katika taarifa yake iliyotolewa siku ya Jumamosi, MINUSCA [...]

05/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vita dhidi ya boko haram viende sanjari na maendeleo endelevu

Kusikiliza / Wanachama wa Baraza la Usalama wakizungumza na wandishi wa habari mjini Niamey, Niger.
Picha: Amadou Djibo/UNDP

  Wanachama wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa wanaendelea na ziara yao katika bonde la ziwa Chad hivi leo jumapili wamekua nchini Niger kwa mara ya kwanza. Niger ni moja ya nchi maskini zaidi duniani. Balozi Matthew Rycroft wa Uingereza ambaye ni rais wa baraza hilo mwezi huu wa Machi na pia [...]

05/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu milioni 7 wanakumbwa na baa la njaa bonde la ziwa Chad:UM

Kusikiliza / Mwakilishi wa Uingereza kwa UM Balozi Matthew Rycroft mjini N'Djamena na wanachama wa baraza la Usalama kwenye ziara yao ya kwanza katika bonde la ziwa Chad, Afrika Magharibi.
Picha: UNICEF/B.Bahaji

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo liko nchini Chad ikiwa ni sehemu ya ziara yao ya nchi nne kuangazia changamoto zinaoendelea za kibinadamu katika eneo la bonde la ziwa Chad  na kuongeza uelewa wa kimataifa kwa hatma ya watu wapatao milioni 11. Ujumbe wa baraza hilo ukiwa katika mji mkuu N’Djamena umekutana [...]

04/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuepusha zahma Sudan Kusini msaada lazima ufike sasa: O’Brien

Kusikiliza / Mama anamtazama mtoto wake aliye na utapiamlo mkali nchin Sudan kusini
Picha: UNICEF/Sebastian Rich

Mamia kwa maelfu ya watu nchini Sudan Kusini wataathirika zaidi na baa la njaa endapo wafanyakazi wa misaada hawatapata fursa ya kuwafikishia msaada waathirika na fedha zaidi za ufadhili kutolewa ameonya hii leo mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Stephen O’Brien. Amesema hayo baada ya kusafiri hadi eneo la Ganyiel, [...]

04/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tofauti za wakazi wa Timbuktu haziwazuii kukarabati msikiti wao

dua

Nchini Mali kwenye mji wa Timbuktu, wakazi wa eneo hilo wameamua kufanya msaragambo kila mwaka kwa karne saba sasa kukarabati msikiti wao.

03/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kutana na Adian Coker, mwanamuziki anayekataa ubaguzi

Kusikiliza / Mwanamuziki mkazi wa Uingereza. Picha: UNAIDS/Video capture

Burudani na ujumbe! Ndivyo unavyoweza kusema ukitafakari ushairi wenye vina unaeleta hisia za ujumbe kuhusu kupinga ubaguzi wa kila aina. Huu ni ujumbe wa mwanamuziki Adina Coker mkazi wa Uingereza ambaye ameamua kuingia vitani dhidi ya ubaguzi sambamba na Umoja wa Mataifa unaopinga dhana hiyo.Ungana na Assumpta Massoi katika midundo hiyo.

03/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhai wa wanyamapori ni uhai wetu- UNEP

Kusikiliza / Tempo wanaopatikana barani Africa. Picha: World Bank/Curt Carnemark

Tarehe tatu mwezi Machi ya kila mwaka ni siku ya wanayamapori duniani. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kusikiliza sauti za vijana ambao wana fursa ya kuhakikisha urithi wa wanyamapori kwa vizazi vijavyo. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP, kuwaenzi wanyamapori na maliasili ambalo ni jumuku la serikali na sekta [...]

03/03/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Neno la Wiki – Si ndiyo

Kusikiliza / Leo tunaangazia neno la wiki na neno hilo ni "si ndiyo" mchambuzi ni Nuhu Zubeir Bakari kutoka CHAKITA nchini Kenya. (Picha:Idhaa ya Kiswahili)

Katika neno la wiki Februari 3 tunachambua neno si ndiyo, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Bwana Nuhu anasema kuwa “si ndiyo” ni semi ambayo moja ni kikanushi na moja ni ya kukubali, hivyo mtu anapotumia maneno [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki, Neno La Wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wanaotawanywa na machafuko kwa siku Mosul ni 4,000

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani waliotawanywa Mosoul Iraq kutokana na operesheni za kijeshi zinazoendelea dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL. Picha: UNHCR/Caroline Gluk

Idadi ya watu wanaotawanywa kwa siku Mosoul Iraq kutokana na operesheni za kijeshi zinazoendelea dhidi ya kundi la kigaidi la ISIL na hofu ya matumizi ya silaha za ckemikali dhidi ya raia imeongezeka sana. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR sasa watu 4000 kwa siku wanakimbia kutoka Magharibi mwa [...]

03/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tunza sikio kama yai kwani likishaharibika ndio basi- WHO

Kusikiliza / Picha: WHO

Zaidi ya asilimia tato ya watu wote duniani wanaishi na tatizo la kupoteza uwezo wa masikio kusikia, lakini kuzuia tatizo hilo ni rahisi kuliko kuitibu. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni WHO katika ujumbe wake kuhusu siku siku ya kimataifa ya uwezo wa masikio kuiskia duniani . Kauli mbiu mwaka huu ikiwa [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mganga wa jadi na askofu akutwa na hatia ya mauaji ya albino Afrika Kusini

Kusikiliza / Haki za albino. Picha: UNHRC

Nchini Afrika Kusini mganga wa jadi ambaye pia ni askofu wa kanisa amepatikana na hatia ya kuwa kinara wa mauaji ya albino, hatua ambayo imepongezwa na Umoja wa Mataifa. Flora Nducha na ripoti kamili. (Taarifa ya Flora) Ushahidi uliowasilishwa mahakamani ulithibitisha pasipo shaka kuwa kinara huyo Bhekukufa Gumede mkazi wa Kwa-Zulu Natal nchini Afrika Kusini [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubunifu wabadili fikra za wadau wa SDG’s

Kusikiliza / Tamasha la Kimataifa la Fikra jijini Bonn, Ujerumani. Picha: UM

Tamasha la Kimataifa la Fikra linakunja jamvi leo jijini Bonn, Ujerumani ambapo watunga sera, asasi za kiraia na makampuni binafsi wameshiriki katika mchezo wa kidigitali uitwao # 2030 HIVE MIND” ili kusongesha mbele malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s. Mwandishi wetu Amina Hassan anaripoti kutoka Bonn. (Taarifa ya Amina) Ni washiriki wakijikita katika awamu ya mwisho [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Muenzini Maathai kwa kuhifadhi mazingira : UNEP

Kusikiliza / Profesa Wangari Maathai (kati) akishiriki kwenye upandaji wa miti nchini New York. Picha(maktaba): UN Photo/Evan Schneider

Leo ni siku ya mazingira barani Afrika, siku ambayo pia imepewa heshima ya kuitwa siku ya Wangari Maathai,mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya ambaye enzi za uhai wake alipigia chepuo uhifadhi wa mazingira. Kupitia wavuti wake hii leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP, limezitaka nchi za Afrika kuainisha mafaniko katika uhifadhi [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria kali zahitajika kulinda wanyamapori- UM

Kusikiliza / Ndovu-2

Leo ni siku ya wanyamapori duniani, inayotumiwa kukuza uelewa kuhusu wanyama pori na mali asili kwa lengo la kuhifadhi viumbe hao. Kauli mbiu ya mwaka huu ni kusikiliza sauti za vijana. Rosemary Musumba na maelezo zaidi. (TAARIFA YA ROSE) Hawa ni ndovu, moja ya wanyama vivutio duniani, lakini wanyama hawa wanakabiliwa na tishio la kutoweka [...]

03/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila elimu bure sisi tusingesoma-Wasichana Uganda

Kusikiliza / Wanafunzi darasani. Picha: UNICEF

Katika kutimiza lendo namba nne la maendeleo endelevu SDGs, linalotaka uwepo wa usawa katika elimu, Uganda imepiga hatua kwa kuhakikisha elimu bure hatua iliyowezesha wale wasiojiweza kwenda shule. Ungana na John Kibego ambaye amefuatailia upatikanaji wa elimu nchini humo ambapo pia amezungumza na wanufaika wa mpango huo.

02/03/2017 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa jamii za asili Australia wakabiliwa na ukatili mkubwa:UM

Kusikiliza / Dubruvka Šimonović na Christopher Woodthorpe. UNIC Canberra/Julia Dean

Mifumo mkingi ya ubaguzi imechochea kiwango kikubwa cha ukatili unaowakabili wanawake kutoka jamii za watu wa asili nchini austarlia. Hayo ni kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonović . Bi Šimonović ambaye amekamilisha ziara nchini humo amesema wanawake wengi wanabaguliwa kimaumbile na kukabiliwa na ubaguzi wa [...]

02/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mabadiliko ya tabia nchi huathiri watoto zaidi:UM

Kusikiliza / Naibu mwakilishi wa kudumu wa Ufilipino, Maria Teresa Almojuela (kati). Picha: UM/Video capture

Mabadiliko ya tabia nchi yanatoa tishio kubwa kwa watoto, limeelezwa baraza la haki za binadamu Alhamisi. Katika mjadala uliofanyika Geneva, nchi wanachama na wataalamu wa haki za binadamu wameonya kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanatishia mafanikio ya vijana katika fursa ya chakula, maji , afya na elimu. Na suluhu kwa mujibu wa wataalamu hao ni [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kismaayo yapata kituo cha kujenga stadi za vijana

Kusikiliza / Kituo cha kusaidia kuwajumuisha kwenye jamii, DDR, wapiganaji wa zamani wa kikundi cha kigaidi cha Al –Shabaab kinafunguliwa Kismaayo cnhini Somalia. Picha: UNSOM

Hii leo huko Kismaayo ambao ni mji mkuu wa muda wa jimbo la Jubaland nchini Somalia, kimefunguliwa rasmi kituo cha kusaidia kuwajumuisha kwenye jamii, DDR, wapiganaji wa zamani wa kikundi cha kigaidi cha Al –Shabaab. Kituo hicho ni cha nne kufunguliwa nchini humo kama sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuwapatia tiba na kuwalea wapiganaji [...]

02/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mavuno ni mengi lakini baa la njaa lashika kasi- FAO

Kusikiliza / Mkulima anakata mihogo. Picha: FAO

Hali ya usambazaji chakula kote duniani imeimarika lakini upatikanaji wa chakula umepungua kwa kiasi kikubwa katika maeneo yanayokabiliwa na mgogoro huku ukame ukizidi kudororesha uhakika wa chakula katika nchi za Afrika Mashiriki. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani FAO kwenye ripoti yake mpya kuhusu matarajio na mwelekeo [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatutafikia SGD’s iwapo hatutayawasilisha kwa kila mtu

Kusikiliza / Picha: UM

Tamasha la Kimataifa kuhusu Fikra linaendelea jijini Bonn, Ujerumani ambapo mada kuu iliyojadiliwa leo ni umuhimu wa utoaji wa habari na uwasilishaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye idara ya habari na mawasiliano , Cristina Gallach amenieleza kuwa [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wapatiwe tiba sahihi dhidi ya madawa ya kulevya- Ripoti

Kusikiliza / Mwanamke anavuta afyuni nchini Thailand kwa njia ya kidesturi ya kulala. Picha: UN Photo/D Gair

Ripoti ya mwaka 2016 ya Bodi ya kimataifa ya kuzuia madawa ya kulevya, INCB, imezinduliwa hii leo ambapo pamoja na mambo mengine imetaka serikali duniani zihakikishe kuwa sera zinazolenga udhibiti wa matumizi ya mihadarati zinajumuisha wanawake wakati huu ambapo idadi ya wanawake wanaotumia madawa hayo imeongezeka. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) Ripoti [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya Afrika ya mlo shuleni yaadhimishwa Brazzaville: WFP

Kusikiliza / Picha: WFP

Siku ya Afrika ya mlo shuleni imezinduliwa rasmi na kuadhimishwa Machi mosi 2017 chini ya ulezi wa serikali ya Jamhuri ya Congo Brazzavile , ikiwa na kauli mbiu "Ulishaji mashuleni, ni uwekezaji kwa vijana kwa ajili ya kuimarisha mustakhbali wao" Rosemary Musumba na taarifa kamili (TAARIFA YA ROSE) Kwa mujibu wa shirika la mpango wa [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukame ni janga la kitaifa Somalia: Rais Farmaajo

Kusikiliza / Picha: UNSOM

Rais mpya wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmaajo ambaye aliapishwa hivi karibuni ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia taifa lake kukabiliana na ukame ulioathiri zaidi ya raia milioni sita. Akizungumza mjini Mogadishu kwenye mkutano wa ngazi ya juu kwa ajili ya ukame ambao amesema ni janga la kitaifa, Rais Farmaajo ameomba jumuiya hiyo kuongeza mchango [...]

02/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ITC kuinua wanawake kiuchumi Rwanda

Kusikiliza / Kahawa kama hii isiyoongezewa thamani, bei yake iko hatarini kuyumba. (Picha:UN Photo/Martine Perret)

Kituo cha kimataifa cha biashara ITC ambayo ni taasisi tanzu ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD na wadau, hii leo wametangaza ushirikiano mpya ili kusaidia wauzaji wa kahawa nje ya nchi, wasindikaji, na wakulima wa zao la buni nchini Rwanda. Ushirikiano huo unalenga uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ambapo uboreshaji uwezo wa [...]

01/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya Yemen bado ni tete:O'Brien

Mratibu wa Masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Steohen O'Brien. Picha na UM

Hali ya kibinadamu nchini Yemen bado ni tete na mamilioni ya watu wanahitaji msaada wa haraka hasa katika maeneo ya Kaskazini ambako hali ya usalama ni mbaya zaidi. Akizungumza kwa jia ya video kutoka mjini Saana, Mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Stephen O'Brien amesema alipata fursa ya [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi dhidi ya Allepo ni uhalifu wa kivita: Ripoti

Kusikiliza /

Mapigano ya kuudhibiti mji wa Aleppo nchini Syria mwaka jana, yamesababisha mateso makali yanayochochea uhalifu wa kivita wameonya leo wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. Ikitumia shuhuda 300 za picha za setilaiti na sauti nyingine, ripoti ya kamisheni ya uchunguzi imeonyesha jinsi gani ndege za kivita za Syria na Urusi zilivyogeuza Mashariki [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machungu kabla ya kunyongwa ni makubwa- Zeid

Kusikiliza / adhabu

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad al Hussein amesema madhila wanayokumbana nayo wafungwa wanaosubiri adhabu ya kifo ni miongoni mwa sababu tosha za kuweza kuondokana na adhabu hiyo. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi wakati wa kikao cha ngazi ya juu kuhusu hoja ya adhabu ya kifo ambapo sasa Umoja wa [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Soko la nyumba halizingatii haki za binadamu:UM

Makazi-2

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya nyumba, Leilani Farha,  ameonya juu ya ukuaji wa soko la nyumba za kibiashara bila kujali haki za binadamu, halikadhalika ongezeko la gharama zake kiasi cha watu wengi kutomudu. Akitoa ripoti yake ya hivi karibuni kwa Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, [...]

01/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taarifa kuhusu chanjo zinapotoshwa- WHO

Kusikiliza / Chanjo. (Picha: MAKTABA:UN/JC McIlwaine)

  Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema linatiwa wasiwasi na upotoshwaji  wa habari kuhusu kinga kupitia tovuti kadhaa hatua ambayo shirika hilo imeliita hatari na kutaka wadau kupata taarifa sahihi. John Kibego na taarifa kamili. (TAARIFA YA KIBEGO) Katika kuhakikisha taarifa sahihi, WHO imeanzisha wavuti wa kimataifa kuhusu usalama wa chanjo uitwao VSN, ambao hadi [...]

01/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tamasha la Fikra lafungua pazia leo huko Bonn

Kusikiliza / tamasha-2

Tamasha la siku tatu lenye  lengo la kuchagiza mawazo mapya katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDG’s lmeanza leo jijini Bonn, Ujerumani ambako mwandishi wetu Amina Hassan amepiga kambi na ametuletea ripoti hii. (Taarifa ya Amina) Akifungua tamasha hilo lijulikanalo kama “Tamasha la Kimataifa la Fikra” ambalo limeleta pamoja watunga sera, asasi za kiraia, vijana [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyongeza ya dola milioni 130 kusaidia miundombinu Tanzania- Benki ya dunia

vituo2

Benki ya dunia imeidhinisha nyongeza ya dola milioni 130 kwa ajili ya mradi wa Tanzania wa kuboresha miji, TSCP kupitia uimarishaji wa miundombinu. Miji itakayonufaika ni Tanga, Arusha, Mwanza, Kigoma, Dodoma, Mbeya na Mtwara na lengo ni kuwezesha miji hiyo kuendana na kasi ukuaji wa miji. Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za [...]

01/03/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kimbunga Dineo chaathiri maelfu Msumbiji:UM

Kasi ya kimbunga. (picha:Maktaba)

Kimbunga Dineo kiliwasili kwenye pwani ya jimbo la Inhambane Kusini mwa Msumbiji  wiki iliyopita kikiambatana na upepo mkali , na kisha kikaelekea Afrika Kusini na Zimbabwe, imesema timu ya Umoja wa Mataifa nchini humo. Familia zaidi ya laki moja zimeathirika huku 7651 kati yao zikiwa katika hali mbaya. Nyumba zaidi ya elfu 33 zimesambaratishwa kabisa [...]

01/03/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vikosi vya serikali vimekiuka haki za binadamu DRC: UM

Kusikiliza / Vurugu-2

Vikosi vya ulinzi na usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC vilitumia nguvu kupita kiasi, isiyohitajika na hata silaha ili kudhibiti maandamano mwezi desemba mwaka 2016 , imebaini ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa Jumatano. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya ofisi ya pamoja ya haki za binadamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatutashinda kwa kubagua wengine- UNAIDS

Kusikiliza / Pazasauti2

Leo ni siku ya kimataifa ya kupinga aina zote za ubaguzi ambapo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi, UNAIDS limesema maudhi ya mwaka huu yanasihi kila mtu apaze sauti ili kupinga ubaguzi wa aina mbalimbali ikiwemo dhidi ya watu wenye virusi vya Ukimwi, VVU, au Ukimwi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Michel [...]

01/03/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930