Naelewa wajibu wangu mpya CAR kama mwendesha mashtaka maalum:Mukimapa

Kusikiliza /

Mwendesha mashitaka maalumu mpya CAR Bwana Muntazini: Picha na Guira FM /MINUSCAR

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu operesheni za ulinzi wa amani Hervé Ladsous ameliambia baraza la usalama kwamba japokuwa kuna hali ya hofu ya usalama katika maeneo ya nchi ya Jamhuri ya Kati CAR, maendeleo pia yamepatikana ikiwemo kuanzishwa kwa mahakama maalum ya jinai na uteuzi Februari 15 wa mwendesha mashitaka maalum Toussaint Muntazini Mukimapa ambaye ni raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Akihojiwa na redio Guira FM ya  mpango wa Umoja wa Mataifa Jamhuri ya Afrika ya Kati ,MINUSCA, Bwana Mukimapa amesema kuwa..

(Sauti ya Mukimapa)

Ninatoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye ameniteua kama mwendesha mashtaka maalum. Naelewa nina wajibu mkubwa kwa sababu itabidi kukabiliana na changamoto kubwa katika nafasi yangu mpya. Ningependa kusema kuwa DRC na CAR zote zinakabiliwa na karibu matatizo sawa. Ni nchi mbili zilizo  katika hali isiyo nzuri baada ya vita na walioathirika ni wengi ambapo kazi yangu kama mwendesha mashitaka maalum haitakuwa rahisi ila niko tayari.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930