Nyumbani » 02/02/2017 Entries posted on “Febuari 2nd, 2017”

Raia wa Ukraine waachwa kwenye madhila makubwa msimu wa baridi: O’Brien

Kusikiliza / rsz_ukraine

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadili hali ya Ukraine kwenye kmakao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Akiwasilisha ripoti yake kwenye kikao hicho msaidizi wa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa kuhusu  masuala ya kisiasa Jeffrey Feltman ameeleza kuwa ni mwaka wa nne sasa vita bado vinaendelea nchini Ukraine [...]

02/02/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuna haja ya kuisaidia Iraq baada ya Daesh-Kubiš

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Wakati operesheni za kuukomboa mji wa Mosul Iraq zikiendelea , jumuiya ya kimataifa, imeombwa kujikita katika siku ambayo mji huo utakuwa huru kabisa kutoka mikononi mwa kundi la itikadi kali la ISILambalo pia hujulikana kama Daesh. Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Ján Kubiš akizungumza katika kikao cha baraza la usalama kuhusu Iraq [...]

02/02/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ICJ yatupilia mbali ombi la Kenya kuhusu kesi yake na Somalia

Kusikiliza / ICJ. Picha: UM

Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetupilia mbali madai ya Kenya ya kutaka kesi ilisowasilishwa na Somalia dhidi yake kuhusu ugomvi wa mpaka wa majini. Katika uamuzi wake mahakama hiyo imesema kuna haja ya kusikiliza madai ya Somalia kuhusu kesi ya mpaka wa majini iliyowasilishwa mwaka 2014 dhidi ya Kenya. Somalia iliyoko Kaskazini mwa [...]

02/02/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO yapatia wakulima nchini Iraq pembejeo za kilimo

Kusikiliza / Mkulima nchini Iraq.(Picha:FAO)

Zaidi ya wakulima 2000 walioathirika na vita nchini Iraq wamepokea tani 750 za mbolea kutoka shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO ili kuongeza uzalishaji wa mazao yao ya ngano katika majira ya baridi. Mwakilishi wa FAO nchini Iraq Dkt Fadel El-Zubi, kila mkulima katika wilaya za Alqosh na Sheikan kwenye jimbo [...]

02/02/2017 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bei ya nafaka imeendelea kupanda licha ya kuongezeka kwa uzalishaji:FAO

Kusikiliza / Picha: NOOR FAO/Sebastian Liste

Bei ya nafaka duniani imeendelea kupanda licha ya kuwepo kwa chakula cha ziada limesema shirika la chakula na kilimo FAO Alhamisi. Kwa ujumla bei imepanda kwa zaidi ya asilimia 16 ikilinganishwa na mwezi Januari mwaka jana , na imeongezeka asilimia mbili ikilinganishwa na mwezi uliopita wa Januari. FAO imesema nafaka zimepanda kwa asilimia 3.4 kutoka [...]

02/02/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Raia wa Norway ajitolea kuwasaidia wakimbizi

Kusikiliza / Bwana Frode, aliyejitolea kibinafsi kuwasaidia wakimbizi anacheza na watoto.  Picha: UNICEF/Video capture

Kulingana na takwimu za Shrika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, zaidi ya watoto milioni 500 duniani wamekimbia makazi yao kutokana na vita na vurugu, wengi wao wakitenganishwa na wazazi wao. Wengi wa manusura wakiweza kutoroka na wazazi wao hukimbilia nchi jirani kusaka hifadhi. Mwaka jana, takriban wakimbizi 140 kutoka Syria na Iraq [...]

02/02/2017 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Warundi walioswekwa DRC warejea nyumbani kwa hiari

Kusikiliza / Warundi walioswekwa DRC warejea nyumbani kwa hiari.(Picha:MONUSCO)

Hatimaye operesheni ya kuwarejesha nyumbani kwa hiari raia 124 wa Burundi walioingia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kinyume cha sheria zaidi ya mwaka mmoja uliopita imekamilika. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO umesema raia hao waliingia wakiwa na raia wengine wa Rwanda ambapo walikamatwa na kuswekwa ndani humo Bukavu. Baada ya [...]

02/02/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Libya si muafaka kwa wakimbizi na wahamiaji-UNHCR na IOM

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Sudan waliokimbia Libya wakiwa nchini Misri.(Picha:UNHCR/F.Noy)

Kabla ya mkutano rasmi wa Muungano wa Ulaya mjini Valletta nchini Malta hapo kesho Ijumaa, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la kimtaifa la uhamiaji IOM wametoa wito kwa viongozi wa Ulaya kuchukua hatua thabiti kushughulikia tishio la kupotea kwa maisha katika bahari ya Mediterranea na mazingira mabaya kwa wahamiaji na [...]

02/02/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zika isipuuzwe, hatua zaidi zaihitajika- WHO

Kusikiliza / Mama na mtoto mwenye Zika.(Picha:UNifeed/video capture)

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema licha ya kwamba virusi vya Zika hivi sasa sio tishio, lakini ugonjwa huo kama yalivyo magonjwa mengine ya milipuko sio ya kupuuzwa, tahadhari kubwa inapaswa kuchukuliwa. Kwa mujibu wa Mkurungenzi Mkuu wa WHO Margaret Chan katika chapisho lake, ikiwa ni mwaka mmoja tangu atangaze ugonjwa wa Zika kuwa dharura [...]

02/02/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tutahakikisha uchaguzi wa wazi na ukweli Somalia

Kusikiliza / Maafisa wa kuoiga kura wakihesabu kura wakati wa uchaguzi Somaliland.(Picha:UM/Atulinda Allan)

Baada ya vuta ni kuvute na dosari katika mchakato wa uchaguzi wa mabunge nchini Somalia, macho yote sasa yanaelekea katika uchaguzi wa Rais utakaofanyika tarehe 8 mwezi huu. Rosemary Musumba na taarifa kamili (TAARIFA YA ROSE) Ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM umesema wagombea 24 watawania kiti hicho cha Rais kwa kupitia kura [...]

02/02/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa chanjo ya HPV ni hatari kwa wanawake

Kusikiliza / Msichana akipokea chanjo ya HPV.(Picha:UN/Sierra Leone)

Bei kubwa ya chanjo dhidi ya virusi vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi, husababisha vifo vya wanawake 250,000 kila mwaka, asilimia 85 ikiwa ni katika nchi za kipato cha chini na cha kati, limesema Shirika la Afya Duniani, WHO leo. Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Taarifa ya Assumpta) WHO inasema ugonjwa huo huzuilika ikiwa wasichana [...]

02/02/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNSOM yawatunuku maafisa kwa kazi nzuri

Kusikiliza / UNSOM yawatunuku maafisa kwa kazi nzuri.(Picha:UM/Omar Abdisalan)

Maafisa wa polisi na jeshi wanane wametunukiwa medali na vyeti kwa kutambua mchango na huduma zao kama washauri kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Somalia UNSOM. Raisedon Zenenga, naibu mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu nchini Somalia akikabidhi medali hizo kwa maafisa kutoka Sweden, Finland, Nepal na Malawi ambao wamekuwa polisi na wanajeshi [...]

02/02/2017 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wabunge waungana dhidi ya itikadi kali na ugaidi:UNODC

Kusikiliza / Mkutano wa kikanda wa wabunge wa nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini MENA ulioanza Aswan Misri. Picha: UNODC

Tishio la ugaidi dhidi ya amani na usalama limeongezeka na kuenea, na linaathiri watu wengi ambao wanarubuniwa kuingia katika ugaidi hasa kupitia mitandao ya kijamii au propaganda za kidini. Hayo yamejitokeza kwenye mkutano wa kikanda wa wabunge wa nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini MENA ulioanza Aswan Misri Januari 31 na unakamilika leo [...]

02/02/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani shambulio dhidi ya watendaji wake Afrika Magharibi

Kusikiliza / Bendera ya Umoja wa Mataifa. (Picha:UN /John Isaac)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio dhidi ya ujumbe wake karibu na mpaka wa Nigeria na Cameroon, shambulio lililosababisha kuuawa kwa watu watano akiwemo mkandarasi huru wa umoja huo. Yaelezwa kuwa shambulio hilo lilitokea Jumatatu karibu na eneo la Kontcha nchini Cameroon wakati wajumbe wa timu hiyo inayofuatilia mzozo wa mpaka [...]

02/02/2017 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ulaghai katika sekta ya madini ukiepukwa Afrika itanufaika zaidi.

Kusikiliza / Madini2

Shirika la fedha duniani IMF, limesema kuwa bara la Afrika laweza kunufaika zaidi na uwepo wa madini ikiwa mapato ya kodi kwa bidhaa hizo yataongezwa na kuzingatia kanuni ya bei za bidhaa. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya kimataifa ya udhibiti wa rasilimali, na kuhusisha mataifa manne ya Afrika ikwamo Tanzania, Guinea, Ghana [...]

02/02/2017 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031