Nyumbani » 31/01/2016 Entries posted on “Januari, 2016”

Mazungumzo ya Syria : mjumbe wa Umoja wa Mataifa aendelea majadiliano

Kusikiliza / Staffan de Mistura. Picha ya UM/ Jean-Marc Ferré

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura anaendelea na majadiliano ya ana kwa ana na wawakilishi wa upinzani na serikali ya Syria, mjini Geneva, Uswisi. Lengo la mazungumzo hayo yasiyokuwa rasmi ni kushawishi pande zote mbili zikubali kunzisha mazungumzo pamoja. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na msemaji wa [...]

31/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Afrika waongee na sauti moja kuhusu mabadiliko ya Umoja wa Mataifa: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu akizungumza na waandishi wa habari Addis Ababa. Picha ya UM/Eskinder Debebe.

Mkutano wa 26 wa Muungano wa Afrika ukiendelea mjini Addis Ababa Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza kwamba uwakilishi katika Baraza la Usalama ni moja ya kipaumbele cha Umoja wa Mataifa, lakini ni wajibu wa nchi wanachama kuelewana kuhusu mabadiliko wanayotaka kutekeleza. Bwana Ban amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa [...]

31/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ki-moon azungumzia mzozo wa Burundi na viongozi wa Rwanda na Burundi

Kusikiliza / Naibu Rais wa Burundi Joseph Butore na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Picha ya UM/Eskinder Debebe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemwambia Naibu Rais wa Burundi Joseph Butore kwamba mchakato wa kisiasa unapaswa kuwa jumuishi, endelevu, na kuungwa mkono na jumuiya ya kikanda na kimataifa ili kupata suluhu kwa mzozo unaoendelea nchini humo. Bwana Ban amesema hayo akizungumza na Bwana Butore leo kuhusu hali ya kiusalama, haki za binadamu na [...]

30/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon ampongeza Rais Kenyatta kwa juhudi zake Somalia

Kusikiliza / Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha ya UN/Eskinder Debebe

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia hali ya usalama nchini Somalia na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akishukuru mchango wa Kenya katika ujenzi wa amani nchini Somalia, na kusisitiza umuhimu wa kuwa na mkakati thabiti wa kupambana na mizizi ya itikadi kali na katili. Mazungumzo hayo yamefanyika leo kando ya mkutano [...]

30/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon apongeza viongozi wa Afrika wanaoacha madaraka kwa kuheshimu katiba

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na viongozi wa Afrika kwenye kikao cha 26 cha Muungano wa Afrika. Picha ya UM/Eskinder Debebe.

Akizungumza leo kwenye ufunguzi wa kikao cha 26 cha Muungano wa Afrika, mjini Addis Ababa, Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaomba viongozi wa Afrika wafuate mfano wa viongozi wanaocha madaraka kwa kuheshimu katiba za nchi zao. Ameongeza kwamba uchaguzi ni mtihani kwa utawala bora, huku nchi 17 za Afrika zikitarajia kufanya [...]

30/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ziara ya Baraza la Usalama Burundi – VIDEO

powers

29/01/2016 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

De Mistura aelezea matumaini ya kukutana na upinzani wa Syria Jumapili

Kusikiliza / Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Stafan de Mistura.(Picha:UM/Pierre Albouy

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Stafan de Mistura, amesema leo anaamini kuwa ataweza kukutana na kamati kuu ya mashauriano ya upinzani nchini Syria mnamo Jumapili jijini Geneva, Uswisi. Bwana de Mistura amesema hayo baada ya kukutana na Balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa, Bashar Jaafari na ujumbe wa [...]

29/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM waitaka Marekani kushughulikia ukatili wa polisi na dhuluma za ubaguzi wa rangi

Kusikiliza / Uzinduzi wa Safina ya Marejeo au "The Ark of Return" kwa ajili ya kuwaenzi wahanga wa utumwa. Picha ya Eskinder Debebe/Umoja wa Mataifa.

Alama za utumwa zinasalia kuwa changamoto kubwa nchini Marekani kwa kuwa kumekuwa hakuna ahadi ya kweli kutambua na kuwalipa fidia watu wenye asili ya Afrika, limesema leo jopo la wataalamu wa Umoja mwishoni mwa ziara yao ya pili rasmi nchini humo. Kuanzia tarehe 9 hadi 29 mwezi huu jopo la wataalamu hao kuhusu watu wenye [...]

29/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ki-moon aziomba nchi za Muungano wa Afrika kutumia uongozi wao kuleta amani Burundi

Kusikiliza / Katibu Mkuu akihutubia kikao cha Muungani wa Afrika. Picha ya UN/Eskinder Debebe.

Burundi, Sudan Kusini na Ugaidi ni mada zilizozungumzwa na Baraza la Amani na Usalama la Muungano wa Afrika lililokutana hii leo Addis Abeba, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewapongeza wanachama wa Muungano wa Afrika na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa jitihada zao katika kuzuia ghasia zaidi nchini Burundi. Bwana Ban [...]

29/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Fahamu utamaduni wa dansi India

Kusikiliza / Mcheza danis.(Picha:UNESCO/Video capture)

Utamaduni ni maisha, ndivyo unavyoweza kusema ukiwa unatafakari na kuzingatia uatamaduni wa watu wa India ambapo pamoja na mambo mengine utamaduni wa jamii moja ya watu wa India ambao hucheza na nyoka huwashangaza wengi. Shirika la Umoja la Mataifa la elimu,sayansi na utamaduni UNESCO linapigia chepuo utamduni huu ambao uko hatarini kutoweka. Ungana na Amina [...]

29/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nishati mbadala nchini Uganda

Kusikiliza / Maganda ya ndizi ambayo sasa yemepata soko kwa  wanaotengeneza mkaa.(Picha:Idhaa ya kiswahili/J.Kibego)

Upatikanaji wa nishati kwa wote ni changamoto kwa karne ya 21, wakati ambapo mtu mmoja kati ya watano hawapati huduma za umeme duniani, na Umoja wa Mataifa ukitarajia kuwa mahitaji ya nishati yataongezeka kwa asilimia 33 ifikapo mwaka 2035. Miongoni mwa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs yaliyopitishwa mwaka 2015, lengo namba 7 ni kuhakikisha [...]

29/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Prof. Murenzi wa Rwanda miongoni mwa wataalam wa kuwezesha teknolojia katika SDGs

Kusikiliza / Picha@WIPO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuwa amemteua Prof. Romain Murenzi wa Rwanda, kuwa miongoni mwa wataalam kumi watakaosaidia katika utaratibu wa uwezeshaji wa teknolojia, ambao ulizinduliwa katika mkutano wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, mnamo Septemba 25, 2015. Wengine waliotajwa katika kundi la wataalam hao kumi ni Bw. Peter Bakker [...]

29/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama latiwa mashaka na kuahirishwa duru ya mwisho ya uchaguzi Haiti

Kusikiliza / Wakati wa uchaguzi wa mwezi Agosti, 2015, nchini Haiti. Picha ya UN/MINUSTAH/Logan Abassi

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wamelezea wasiwasi wao kuhusu hali inayoelekea kuahirishwa moja kwa moja duru ya mwisho ya uchaguzi nchini Haiti, ambao awali ulikuwa ufanyike Disemba 27, kisha ukaahirishwa kwa mara ya pili hadi Januari 24 na hadi sasa hauajafanyika. Wajumbe wa baraza wamesema kucheleweshwa kwa uchaguzi huo kunaweza kuathiri [...]

29/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkataba wa Paris kutoka COP21 umeanza kuzaa matunda:Pasztor

Kusikiliza / Bwana Janos Pasztor. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambaye amemaliza muda wake, Janos Pazstor, amesema mkataba wa mabadiliko ya tabianchi uliopitishwa mwaka jana Paris, Ufaransa umeanza kuzaa matunda. Akizungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani, Bwana Pasztor amesema dhihirisho hilo limetokana na ahadi zilizoanza kutekelezwa hata na [...]

29/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wakutana kutathmini mkakati wa amani na usalama wa DRC

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC washuka boti iliowaleta nyumbani baada ya kuvuka mto Oubangui.Picha © UNHCR/G.Diasivi

Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje na Wawakilishi wa nchi wanachama wa mkakati wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na ukanda wa Maziwa Makuu (PSC), umependekeza kuwa mikutano ya siku za usoni ya mfumo wa kikanda wa kufuatilia utekelezaji wa mkakati huo, itenganishwe na mikutano mikuu [...]

29/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya kusaka amani Syria yaanza Geneva

Kusikiliza / Watoto wa Syria wakiwa katika mazingira duni. Picha: OCHA/Josephine Guerrero (MAKTABA)

Mazungumzo ya kusaka suluhu ya mgogoro wa Syria yameanza leo mjini Geneva Uswisi,  licha ya kukosekana kwa uwakilishi wa upande wa upinzani. Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, ameanza kukutana na mwakilishiwa  kudumu wa serikali ya Syria katika Umoja wa Mataifa Bwana Bashar Jaafari. Kiongozi  huyo anatarajiwa kuendelea kukutana na washiriki [...]

29/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watu walazimika kuhama makwao Mashariki mwa DRC, MONUSCO yaongeza ushirikiano na FARDC

Kusikiliza / Mlinda amani wa MONUSCO akiwa kwenye lindo. (Picha:MONUSCO/Abel Kavanagh)

Mashambulizi yanayofanyika na waasi wa Mai-Mai, FDLR, na ADF mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC yamelazimisha maelfu ya watu kukimbia makwao, Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR ambalo limesihi mamlaka za serikali kukabiliana na hali ya kiusalama na kuwapatia makazi wakimbizi hao wa ndani. Leo [...]

29/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya Burundi kila pande inavutia kwake: Balozi Delattre

Kusikiliza / Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Francois Delattre.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Leo Baraza la Usalama limejadili kuhusu ziara yake nchini Burundi, huku  Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Francois Delattre akikariri maombi ya Baraza hilo kwa mamlaka za serikali ya Burundi. Taarifa zaidi ya Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Balozi Delattre amewasilisha ripoti ya ziara hiyo ambayo iliandaliwa na ujumbe wa Ufaransa [...]

29/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP, ZAYED kutenegeza kitabu kuhusu uchumi rafiki kwa mazingira

Kusikiliza / Achim Steiner, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP (Picha@UN-Radio)

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP na taasisi ya kimataifa ya mazingira iitwayo Zayed leo wametia saini makubaliano ya kuzalisha kitabu cha kiada cha kimataifa kuhusu ujumuishwaji wa uchumi unaozingatia maizingira. Makubaliano hayo yamesainiwa  na Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner na mwenyekiti wa kamati kuu ya Zayed Dk Mohammed Ahmed [...]

29/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa ina wajibu wa kusaidia nchi zinazowahifadhi wakimbizi wa Syria- ILO

Kusikiliza / Picha:UNHCR/G.Gubayeva

Wakati kongamano la wahisani wa Syria likiandaliwa kufanyika jijini London wiki ijayo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani, ILO, Guy Ryder, amesema ni wajibu wa msingi wa jamii ya kimataifa kuzisaidia nchi zinazowahifadhi wakimbizi wa Syria ili ziweze kukidhi changamoto za kiuchumi na kijamii zinazoletwa na mzozo wa wakimbizi hao. Bwana Ryder amesema hayo [...]

29/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Madai zaidi ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto CAR yajitokeza:Zeid

Kusikiliza / Wahanga wa unyanyasaji wa kingono.(Picha:UM/Marie Frechon)

Kamishina Mkuu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa mataifa  Zeid Ra'ad Al Hussein Ijumaa amesema  ana wasiwasi mkubwa kwa sababu ya kuendelea kwa madai ya unyanyasaji wa kingono nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) unoafanywa na vikosi vya kigeni. Tuhuma hizo zinasemekana kufanyika mwaka 2014, lakini zimebainika tu katika wiki za [...]

29/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 100 za CERF kusaidia wakimbizi na wenye dharura, Tanzania mojawapo

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Burundi wakijiandikisha katika kambi ya Nduta nchini Tanzania.(Picha:UNHCR/Video capture)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa Ethiopi, leo ametangaza kutoa dola Milioni 100 kutoka mfuko wa kushughulikia majanga, CERF kwa ajili ya operesheni za usaidizi wa kibinadamu zinazokabiliwa na ukata ikiwemo Afrika. Maeneo ya Afrika ni pamoja na Mashariki na Kati mwa bara hilo ambapo Ban amesema fedha zitasaidia mamilioni ya wahitaji [...]

29/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kunyonyesha kunapunguza vifo kwa watoto na saratani kwa kina mama: UNICEF

Kusikiliza / Nutrition-1-breastfeeding-fupi

Mfululizo wa nyaraka zilizochapishwa na jarida la kitabibu la The Lancet la Uingereza zinatoa ushahidi kwamba kuimarisha mazoea ya kunyonyesha kunaweza kuokoa maisha ya watoto zaidi ya 820,000 kwa mwaka, huku 9 kati 10 wakiwa ni watoto wachanga wa umri wa chini ya miezi sita. Hii ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM na wataalamu wa Afrika wamemtaka Rais wa Sierra Leone kusaini muswada wa utoaji mimba salama

Kusikiliza / Msichana nchini Sierra Leone. Picha ya UNICEF.

Kundi la tume za haki za binadamu za Umoja wa Mataifa na Afrika leo wamemtaka Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, kuokoa maisha ya mamilioni ya wanawake kwa kutia saini muswada wa utoaji mimba wa mwaka 2015 ili uanze kufanya kazi bila kuchelewa zaidi. Wataalamu hao wameonya kwamba kusita kuondoa sheria ya utoaji mimba [...]

28/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maadhimisho ya Holocaust duniani

Kusikiliza / Mmoja wa washirikii wa kumbukizi ya Holocaust katika tukio la mwaka 2016 makao makuu ya UM.(Picha:UM/Manuel Elías)

Maadhiimisho ya siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga na manusura wa mauaji ya halaiki ya Holocaust ambayo imefanyika kote duniani mnamo tarehe 27 Februari, imetoa somo kuhusu kuepukana na chuki zinazoweza kusababisha mauaji kama hayo. Ungana na Joseph Msami katika makala itakayokukutanisha na mmoja wa manusura na somo kwa vijana kupitia mauji hayo.  

28/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Inawezekana kuondoa mafuta ya kisukuku: Kyte

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nishati endelevu kwa wote Rachel Kyte.(Picha:UM)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu nishati endelevu kwa wote Rachel Kyte amesema inawezekana kutimiza  lengo la kuondoa mafuata yatokanayo na kisukuku na  kuongeza maradufu uwekezaji katika nishati safi ifikapo mwaka 2020. Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa, Bi Kyte amesema lengo hilo lililowekwa na Katibu Mkuu linawezekana akisisitiza [...]

28/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kongamano la Geneva kuhusu Syria liwe fursa isiyopotezwa- de Mistura

Kusikiliza / Staffan de Mistura, mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwenye mzozo wa Syria. (Picha:UN/Mark Garten)

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Stafan de Mistura, ametoa wito kwa watu wa Syria wapaze sauti ya pamoja kwa washiriki wa kongamano kuhusu Syria mwishoni mwa wiki hii, wakiwataka wasipoteze fursa inayotolewa na kongamano hilo. Katika ujumbe aliourekodi kabla ya kuanza kongamano la pande kinzani za Syria jijini Geneva [...]

28/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Naibu mkuu wa MONUSCO atembelea Ituri

Kusikiliza / Mkratibu wa Masuala ya Kibinadamu nchini DRC Mamadou Diallo akitembelea hospitali ya Gety, Ituri. Picha kutoka akaunti ya Twitter ya mkuu wa OCHA DRC, Rein Paulsen.

Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, Mamadou Diallo ametimiza ziara ya siku mbili Kaskazini Mashariki mwa nchi kwenye jimbo la Ituri. Taarifa iliyotolewa na OCHA inaeleza kwamba ametembelea maeneo ya Geti, Bukiringi na Komanda ambapo vitendo vingi vya ukiukaji wa haki za binadamu vimeripotiwa kwa [...]

28/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kiongozi wa OCHA aangazia hali ya kibinadamu Eritrea na Ethiopia

Kusikiliza / Bi Kyung Wha Kang ziarani Eritrea. Picha kutoka akaunti ya Twitter ya OCHA.

Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, Kyung-wha Kang, amehitimisha ziara ya siku tatu nchini Eritrea akisihi jumuiya ya kimataifa kuongeza usaidizi wake kwa watu wanaoishi kwenye mazingira magumu nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Bi Kang amekutana na viongozi wa serikali na kutembelea vituo vya [...]

28/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha muafaka Somalia kuhusu mfumo wa serikali baada ya uchaguzi

Kusikiliza / Bendera ya Somala ikipepea wakati wa kuapishwa kwa wabunge mara ya kwanza nchini humo mwaka 2012.(Picha:UM/Stuart Price)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha uamuzi uliofanywa leo na serikali kuu ya Somalia kuhusu mfumo wa serikali mpya itakayowekwa na mchakato wa uchaguzi baadaye mwaka huu, ambayo itakuwa jumuishi na shirikishi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Ban amewapa heko viongozi wa Somalia kufuatia uamuzi huo, ambao amesema unafungua [...]

28/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNECE, UNITAR zaanzisha ubia wa kutekeleza SDGs

Kusikiliza / SDGs

Katika kuwezesha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs, taasisi mbili za Umoja wa Mataifa mjini Geneva zimeanzisha ubia ili kukuza viwango na uwezo katika kufikia melengo hayo. Taasisi hizo ambazo ni kamisheni ya uchumi ya bara Ulaya  UNECE na taasisi ya mafunzo na utafiti UNITAR kwa pamoja katika taarifa zimeeleza kuwa maeneo yatakayopewa kipaumbele  [...]

28/01/2016 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kuhusu hali Somalia

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Manuel Elias)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limefanya kikao leo Alhamis kujadili hali nchini Somalia, ambapo Mwakilishi mpya wa Katibu Mkuu nchini humo, Michael Keating, amesema kuwa ingawa hali ya usalama bado inatoa changamoto kubwa, muafaka mpya wa kuleta nuru umefikiwa leo. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Akilihutubia Baraza la Usalama kwa [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kesi ya Gbagbo si kesi dhidi ya Cote d'Ivoire- ICC

Kusikiliza / Laurent Gbagbo akikana mashtaka huko The Hague, Uholanzi hii leo. (Picha:ICC video capture)

Mjini The Hague Uholanzi kesi dhidi ya Rais wa zamani wa Cote d’Ivoire na Laurent Gbagbo na mshirika wake Charles Ble Goude imeanza leo rasmi kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, Jaji Cuno Tarfusser wa Italia anayeongoza kesi hiyo akisema si kesi dhidi ya Cote d'Ivoire. (Sauti ya Jaji Tarfusser) « Hii ni kesi [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa chakula wazidi Yemen- FAO

Kusikiliza / Picha:WFP/Yemen

Zaidi ya watu milioni 14 wanakumbwa na ukosefu wa chakula nchini Yemen, limesema leo Shirika la Chakula na Kilimo duniani FAO, likisema ni ongezeko la asimilia 36 ikilinganishwa na mwaka 2014. FAO katika taarifa imesema uhaba wa chakula umesababishwa na mapigano na mfumuko wa bei za bidhaa zinazoingizwa kutoka nje,  ambazo zinachangia asilimia 90 ya [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNCHR , wadau kusaidia waathirika wa mafuriko Burundi

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Burundi wanaotafuta uhifadhi.(Picha:UNHCR/Federico Scoppa)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Burundi, kwa kushirikiana na wadau wanahaha kusaidia maelfu ya watu walioathirika kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha nchini humo. Takribani nyumba 7,000 zimeathiriwa na mafuriko nchini humo, wakati huu ambapo  serikali aimetoa ombi kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia waathiriwa hao. Katika mahojiano maalum na idhaa [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OECD na UNHCR watoa wito wa kuongeza sera za kuwajumuisha wakimbizi:

Kusikiliza / Picha:UNHCR

Mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD) Ulaya na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR),kwa pamoja wametoa wito kwa serikali kuongeza juhudi za kusaidia wakimbizi kujumuishwa katika jamii na kuchangia katika jamii na uchumi barani Ulaya. Wakizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa masuala ya ulinzi na ujumuishi wa [...]

28/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kobler alaani vikali utekaji wa mbunge Libya, ataka aachiliwe mara moja

Kusikiliza / Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Martin Kobler.(Picha:UM/Manuel Elías)

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL, Martin Kobler, amelaani vikali utekaji wa mbunge Mohamed al-Ra'id, na kutaka mbunge huyo aachiwe huru mara moja bila masharti yoyote. Bwana al-Ra'id alitekwa nyara hapo jana akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege, baada ya kushiriki kikao cha wawakilishi wa bunge [...]

28/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO yatia msukumo wa kudhibiti magonjwa kama Ebola na MERS

Kusikiliza / Wachungaji wakichunga ngamia huko Chad. Picha:FAO

Tishio la maradhi ya kuambukiza kwa wanyama kama Ebola na virusi vya corona vinavyosababisha matatizo ya kupumua MERS ni maradhi ambayo yataendelea kuwepo amesema Juan Lubroth, mkuu wa mifugo wa shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilomo FAO, akihoji endapo dunia iko tayari kuyachunguza na kuzuia kuenea kwake. Ameongeza kuwa cha kutia uchungu [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaitisha kikao cha dharura kuhusu kirusi Zika

Kusikiliza / Picha:PAHO/WHO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO Dkt. Margaret Chan ameamua kuitisha mkutano wa kamati ya kimataifa ya kanuni za afya ili kujadili iwapo mlipuko wa virusi vya Zika unasababisha dharura ya kimataifa ya afya. Akizungumza kwenye kikao cha bodi tendaji ya shirika hilo leo mjini Geneva, Uswisi, amesema kikao hicho kitafanyika tarehe Mosi [...]

28/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwelekeo wa matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania watia matumaini- UNFPA

Kusikiliza / Mwanamke akiwekewa kipandikizi, moja ya njia za uzazi wa mpango. (Picha:UNFPA/Tadej Znidarcic)

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya njia za uzazi wa mpango imeonyesha ongezeko katika baadhi ya nchi ikiwemo Tanzania. Takwimu zinasema kuwa matumizi sasa ni asilimia 27 ya watanzania wenye uwezo wa kutumia njia hizo ikiwemo sindano, vipandikizi na mipira ya kiume na ya kike. Lakini ni hatua gani ambazo zimechangia ongezeko hilo [...]

28/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Hali iliyoko Mashiriki ya Kati si endelevu – Ban akariri

Kusikiliza / Picha ya IRIN

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema kwamba Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameshikilia msimamo wake na kukariri kauli aliyoitoa kwenye Baraza la Usalama mnamo Jumanne Januari 26, kuhusu Mchakato wa amani Mashariki ya Kati. Amesema hayo leo akizungumza na waandishi wa habari baada ya maoni kadhaa kuibuka kuhusu hotuba ya Katibu [...]

27/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwelekeo wa uwekezaji wa kigeni Afrika watia shaka 2016- UNCTAD

Kusikiliza / Sekta ya  ujenzi ni miongoni mwa maeneo  yanayopaswa kuchangia katika viteugauchumi vya kigeni. (Picha:UN/Paulo Filguieras)

Ripoti mpya ya kamati ya maendeleo ya biashara ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD kuhusu mwelekeo wa uwekezaji wa vitegauchumi wa kigeni duniani imeonyesha bayana kuzidi kudidimia kwa uwekezaji huo katika nchi za Afrika hususan zile zinazoendelea. Hata hivyo mataifa mengine yamenufaika kwa kupata uwekezaji mkubwa ambapo kwa ujumla yaelezwa kuwa uwekezaji huo duniani umeongezeka kwa [...]

27/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mapigano Jebel Marra, Darfur yawalazimu maelfu kukimbia makwao

Kusikiliza / Kambi ya wakimbizi wa ndani ya Zamzam ilioko Darfur Kaskazini(Picha ya UM//Olivier Chassot)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Sudan, Marta Ruedas, ameeleza kutiwa wasiwasi na athari za mapigano katika eneo la Jebel Marra katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ambako takriban watu 19,000 wamekimbilia jimbo la Darfur Kaskazini, huku wengine 15,000 wakikimbilia jimbo la Darfur ya Kati katika kipindi cha wiki mbili zilizopita. Eneo la Jebel Marra [...]

27/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama halijajitahidi vya kutosha kuhusu Syria- OCHA

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA Stephen O'Brien.(Picha:UM/Manuel Elias)

Leo Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Syria, mzozo nchini humo ukikaribia kuingia mwaka wa sita na ripoti zikionyesha kwamba hali inazidi kuzorota. Akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la Usalama, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA Stephen O'Brien amesema OCHA inakadiria kuwa watu wapatao milioni [...]

27/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Licha ya Ebola, Sierra Leone yapiga hatua kukuza haki za binadamu

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Ari Gaitanis

Leo hali ya Sierra Leone ikifanyiwa tathmini ya haki za binadamu kwenye kikao cha Baraza la Haki za Binadamu huko Geneva Uswisi, Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Joseph Fitzerald Kamara amesema kwamba mlipuko wa Ebola ulisimamisha kwa muda jitihada za serikali katika kukuza maendeleo na haki za binadamu nchini humo. Ameeleza kwamba rais alilazimika [...]

27/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maisha ya upweke kwa wakimbizi wa Syria nchini Lebanon

Kusikiliza / Jawaher baada ya kupata mawasiliano na nduguze. (Picha:UNHCR-video capture)

Mwaka wa sita sasa mzozo wa Syria unaendelea bila ya nuru ya kupata suluhu la kisiasa. Raia wa Syria wamekimbia makazi yao na wamesalia wakimbizi wa ndani na wengi wao wamesaka hifadhi nchi jirani na wengine kuvuka bahari na majangwa  hadi Ulaya. Miongoni mwao ni Jawaher ambaye sasa anaishi Lebanon. Raha ya maisha aliyozoea nchini [...]

27/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila uwekezaji uwe jawabu kwa changamoto za mabadiliko ya tabianchi- Ban

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Ariane Rummery

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa viongozi wa uwekezaji katika sekta binafsi lengo likiwa ni kuangalia hatari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta ya biashara. Akizungumza kwenye mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesimama mbele ya wawekezaji hao akiwa na matumaini mapya kuwa ushirikiano kati ya [...]

27/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNMAS yalaani mashambulizi dhidi ya timu wategua mabomu

Kusikiliza / UNMAS/Lee Woodyear

Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia huduma za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini UNMAS limelaani vikali shambulio katika jimbo la Helmand nchini Afghanistan lililolenga timu ya kudhibiti mabomu ya kutegwa ardhini nchini humo DAFA. Taarifa ya UNMAS imesema kuwa shambulio hilo pia lilielekezwa kwa asasi isiyo ya kiserikali ya udhibiti wa mabomu ya kutegwa [...]

27/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa sanyansi na teknolojia wa UNISDR umeanza leo Geneva

Kusikiliza / Mkuu wa UNISDR, Robert Glasser.(Picha:UNISDR)

Mkutano wa sayansi na teknolojia wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNISDR umeanza leo mjini Geneva kwa kuwaenzi mamia ya wanasayansi ambao wamechangia muda wao kwa utafiti kuhusu mabadiliko ya tabianchi na athari zake. Mkuu wa UNISDR bw. Robert Glasser, amesema kazi ya mamia ya wanasayansi waliochangia kwenye jopo [...]

27/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uelewa wachochea matumizi ya njia za uzazi wa mpango Tanzania

Kusikiliza / Picha ya UNFPA Tanzania.

Wakati mkutano wa kimataifa kuhusu uzazi wa mpango ukiendelea huko Indonesia, Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) nchini Tanzania limesema uelewa wa faida za matumizi ya njia hizo ni moja ya sababu ya matumizi kuongezeka hadi asilimia 27 huku matarajio ikiwa ni kufikia asilimia 80 mwaka 2020. Akihojiwa na idhaa hii, afisa programu wa [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumbukizi ya Holocsoust: ubaguzi wakemewa, Tanzania yaadhimisha

Kusikiliza / Photo: UNIC

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga na manusura wa mauaji ya halaiki ya Holocaust, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kumbukizi hii inadhihirisha kile kinachoweza kutokea iwapo binadamu atasahau utu wao. Taarifa kamili na Flora Nducha.. (TAARIFA YA FLORA) Katika ujumbe wake Ban amesema mauaji ya Holocaust dhidi [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ahadi za serikali mpya ya Tanzania kubana matumizi zaridhisha IMF

Kusikiliza / Ujenzi na usafiri ni miongoni mwa sekta zilizobeba ukuaji wa uchumi nchini Tanzania. Hapa ni mjini Dar es Salaam.

Matarajio ya kiuchumi ya Tanzania yanatia matumaini sana, amesema leo mkuu wa Ujumbe wa Shirika la Fedha Duniani, IMF, Hervé Joly, huku serikali ya awamu ya tano ikiwa imeahidi kulipa malimbikizo kwa wanaotoa huduma. Bwana Joly amehojiwa na idhaa hii wakati IMF imekamilisha tathmini ya tatu ya uchumi wa Tanzania kupitia mfumo wa PSI,ambao mapendekezo [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kesi dhidi ya Gbagbo kuanza kesho kwenye mahakama ya ICC

Kusikiliza / Aliyekuwa rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo akiwa kwenye mahakama ya ICC mwaka 2011.(Picha:UM//ICC/AP Pool/Peter Dejong)

Kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa Côte d’Ivoire, Laurent Gbagbo itaanza hapo kesho Januari 28, 2016, kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Mkuu wa mahakama hiyo, Fatou Bensouda. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Laurent Gbagbo, ambaye ni rais wa zamani wa Côte d’Ivoire, aliwasilishwa kwenye ICC [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya yawafungisha virago maelfu Darfur: UNAMID

Kusikiliza / Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakishirikiana na askari wa Umoja wa Afrika (UNAMID) huko Darfur. Picha:UN Photo

Taarifa kutoka Darfur Sudan zinasema maelfu ya wakimbizi wa ndani wanakimbilia katika miji na vijiji vya maeneo ya Kati na Kaskazini mwa Dafur kutokana na mapigano kati ya majeshi ya serikali na kundi la upinzani la Sudan's Liberation Movement, SLM. Amina Hassan na taarifa kamili… (TAARIFA YA AMINA) Mpango wa Umoja wa Mataifa na Muungano [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mbinu za kisasa zahatarisha kutoweka kwa aina asilia za wanyama:FAO

Kusikiliza / Picha:Werner Lempert GmbH/Ramona Waldner

Ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo duniani, FAO imesema kitendo cha wafugaji na watunga sera duniani kote kuvutiwa na mbinu za kisasa ili kuwa na aina bora ya wanyama katika zama za sasa za ongezeko la joto duniani kunatishia uwepo wa mbegu asilia za wanyama. FAO imesema jamii zinatumia mbinu kama vile kuchanganya [...]

27/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 339 zahitajika kukidhi mahitaji yakibinadamu Afghanistan 2016:OCHA

Picha:WFP / Hukomat Khan

Jumuiya ya watoa misaada wa kimataifa kwa pamoja nchini Afghanistan wanatafuta dola milioni 393 ili kukidhi mahitaji ya kuokoa maisha kwa watu wasiojiweza na waliotengwa nchini humo kwa kipindi cha 2016. Msaada huo unaojumuisha chakula, fursa za afya, lishe, maji safi na kujisafi utawafikia watu takribani milioni 3.5 waliowekwa katika mpngo maalumu wa huduma za [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP imetaka hatua zichukuliwe kulinda mali asili ya Afrika:

Mnyama pori ziwa Naivasha nchini Kenya.(Picha:UM/Milton Grant)

Naibu Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa mataifa la mpango wa mazingira UNEP Ibrahim Thiaw, ametoa wito wa ulinzi mzuri dhidi ya wanyamapori na mali asili tele ya Afrika kama njia ya kufanikisha ajenda ya Muungano wa Afrika AU ya mwaka 2063. Akizungumza katika kikao cha faragha cha baraza la Muungano wa Afrika mjini [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumbukizi ya Holocaust, Ban atoa ujumbe jamii iache kubagua

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon alipotembelea kambi ya Auschwitz Birkenau mwaka 2013 kujionea hali ilivyokuwa. (Picha:rld War. UN /Evan Schneider)

Ikiwa leo  ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga na manusura wa mauaji ya halaiki ya Holocaust, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kumbukizi hii inadhihirisha kile kinachoweza kutokea iwapo binadamu atasahau utu wao. Katika ujumbe wake Ban amesema mauaji ya Holocaust dhidi ya wayahudi yalikuwa uhalifu mkubwa ambao hadi sasa [...]

27/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama wafika Gitega kukutana na Rais

Kusikiliza / Picha:VIDEO CAPTURE

Wakiwa ziarani Afrika, wajumbe wa Baraza la Usalama wametembelea Burundi ambako wamejadili na wawaklishi wa vyama vya upinzani, asasi za kijamii, na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza mustakhbali wa nchi hiyo ambayo sasa iko mzozoni. Mkutano wa faragha na Rais Nkurunziza ulifanyika nje ya mji mkuu Bujumbura kwenye eneo tulivu la Gitega. Safari hiyo ya [...]

26/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Vitendo vya ukiukaji wa haki vyaongezeka DRC

Kusikiliza / Wakati wa uchaguzi mwaka 2011. Picha ya MONUSCO.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeorodhesha visa 347 vya ukiukaji wa haki za binadamu mwezi Disemba mwaka 2015 nchini humo. Kwa ujumla, idadi ya visa hivyo imefika 3,877 mwaka uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 64 ikilinganishwa na mwaka 2014. Kwa mujibu wa ripoti [...]

26/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Somalia na Ethiopia watumikishwa Yemen

Kusikiliza / Wahamiaji wa Somalia wakisubiri usafiri pwani Yemen. Picha ya UNHCR/R. Nuri

Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Yemen, Johannes van der Klaauw, ameeleza kwamba baadhi ya watu waliokimbilia Yemen kutoka Somalia na Ethiopia wanaripotiwa kutumikishwa vitani na waasi nchini humo. Bwana Van der Klaauw amesema hayo akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa, huku akiongeza kwamba wengi wa wahamiaji hawana [...]

26/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM na mashirika ya misaada waomba dola milioni 298 kwa ajili ya wakimbizi Iraq:

Kusikiliza / Hapa ni Zahko nchini Iraq wanaume wabeba vifaa vya kukabiliana na baridi.(Picha:OCHA/Iason Athanasiadis)

Kukiwa hakuna mwangaza wa kuitisha vita nchini Syria Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu na mae ndeleo nchini Iraq wametoa ombi la dola milioni 298 kwa ajili ya kuendelea na msaada kwa takribani wakimbizi 250,000 wa Syria walioko nchini Iraq. Ombi hilo limetolewa katika uzinduzi wa mpango wa ukurasa mpya wa Iraq katika kusaidia [...]

26/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hofu ya kirusi Zika, WHO yaitisha mkutano.

Kusikiliza / Picha:WHO

Shirika la Afya Duniani, WHO tarehe 28 mwezi huu litaitisha mkutano maalum kuhusu kirusi aina ya Zika. Amesema leo msemaji wa WHO Christian Lindmeier, wakati huu ambapo kirusi hicho tayari kimeripotiwa kwenye nchi 20 huku Brazil ikiwa ni nchi iliyoathirika zaidi. Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Bwana Lindmeier ameeleza kwamba kirusi chenyewe [...]

26/01/2016 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kumbukizi ya Haiti – VIDEO

haiti kumbukizi fupi

26/01/2016 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

UM na wadau wa kibinadamu waomba pande kinzani Syria ziwezeshe kuwafikia wahitaji

Kusikiliza / Picha:IRIN/Jodi Hilton

Viongozi wa Mashirika ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, wametoa wito kwa pande kinzani nchini Syria zikomeshe mapigano na kuruhusu wahudumu wa kibinadamu kuwafikia watu wanaohitaji usaidizi wa kibinadamu. Miongoni mwa waliotoa wito huo ni Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu nchini Syria, Yacoub El Hillo, ambaye amesema mateso wanayopitia watu wa Syria ni makubwa mno, [...]

26/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wa Palestina wana haki ya kukata tamaa: Ban Ki-moon

Kusikiliza / Gaza ambapo bado huduma za maji, ajira na afya ni duni, vijana wanakata tamaa. UN Photo/Shareef Sarhan

Leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejadili hali ya Mashariki ya Kati likiwemo suala la Palestina, huku Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwasilisha ripoti yake na kusihi pande zote kwenye mzozo wa eneo hilo kuchukua hatua ili kutoharibu daima uwezekano wa kutekeleza suluhu ya mataifa mawili. Bwana Ban ameeleza kwamba hakuna dalili ya kupungua [...]

26/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

India na Ufaransa kuunda setilaiti ya kuchambua tabianchi

Kusikiliza / Mtazamo wa dunia kutoka anga za juu. (Picha:Climateaction-tovuti)

India na Ufaransa zitaingia makubaliano ya kuunda setilaiti inayochambua mabadiliko ya tabianchi. Hatua hiyo inafuatia mazungumzo kati ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na Rais Francois Hollande wa Ufaransa ambapo taasisi mbili za masuala ya anga za juu za nchi hizo zitahusika na utengenezaji. Mpango huu unaimarisha ushirikiano wa awali kati ya taasisi hizo [...]

26/01/2016 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukuaji wa uchumi pekee si hakikisho la uwepo wa ajira zenye utu: ILO

Kusikiliza / Picha:ILO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la kazi duniani, ILO Guy Ryder amesema misukosuko ya uchumi katika nchi za kundi la BRICS inaweza kufuta mafanikio yaliyokwishapatikana katika kuwezesha uwepo wa kundi la watu wa kipato cha kati. Amesema hayo mjini Ufa huko Urusi katika mkutano wa kwanza mawaziri wa kazi wa nchi zinazounda kundi hilo ambazo ni [...]

26/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Timu ya kuchunguza ukiukaji wa haki Burundi iko tayari, ruksa ndio shida:UM

Kusikiliza / Picha:UNHCR/T.W.Monboe

Baraza la Haki za Binadamu limeunda jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kwenda Burundi kuchunguza unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo. Jopo hilo linajumuisha wawakilishi maalumu wawili na mjumbe wa tume ya Afrika kwa ajili ya haki za binadamu. Amina Hassan na taarifa kamili.. (TAARIFA YA AMINA) Mbali ya kuchunguza [...]

26/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 550 zahitajika kusaidia wahamiaji na wakimbizi Ulaya:UNHCR&IOM

Kusikiliza / Picha:UNHCR/Hereward Holland

Wakati vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati na kwingineko vikizidi kuwafungisha virago watu na kuelekea Ulaya kuomba hifadhi , Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi(UNHCR) na lile la Kimataifa la Uhamiaji(IOM) na washirika wao 65 wametoa ombi la dola milioni 550 ili kusaidia mahitaji ya kibinadamu ya watu hao wanaoingia Ulaya. Kwa mujibu wa [...]

26/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF na ombi la dola Bilioni 2.8 kukwamua watoto maeneo mbali mbali

Kusikiliza / Mtoto Lara kutoka Syria akiwa safarini kuelekea Ulaya. (Picha:UNICEF/07714/Kljajo)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limezindua ombi la dola Bilioni 2.8 kwa ajili ya kufikia watoto Milioni 43 wanaokumbwa na dharura mbali mbali duniani. Flora Nducha na maelezo zaidi. (Taarifa ya Flora) Kwa mara ya kwanza asilimia 25 ya ombi hilo, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kitaelekezwa kwenye elimu kwa watoto [...]

26/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya kisiasa ya UM kuanzishwa Colombia

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Manuel Elias)

Baraza la usalama la Umoja Mataifa leo limepitisha azimio la kuanzisha ofisi yake ya kisiasa nchini Colombia. Azimio hilo pamoja na mambo mengine limezingatia ombi la serikali ya Colombia kwa Umoja wa Mataifa la kutaka uwepo wa ofisi hiyo ili kufanikisha utekelezaji wa makubaliano ya kumaliza mzozo yanayotarajiwa kutiwa saini baina yake na kukundi cha [...]

25/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Usalama wa chakula CAR shakani

Kusikiliza / Picha:UNIFEED VIDEO CAPTURE

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati machafuko yamesababisha hali tete ya usalama wa chakula na hivyo kuongeza kadhia kwa raia wa nchi hiyo mjini na vijijini. Watoto wanakumbwa na hatari ya utampiamlo huku afya ya jamii kwa ujumla ikizorota. Ungana na Grace Kaneiya katika makala inayofafanua madhila hayo na juhudi za Umoja wa Mataifa katika [...]

25/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Waathirika wa Boko Haramu wanahitaji kujua siyo kosa lao

Kusikiliza / Picha ya Lucian Read/WorldPictureNews (NICA ID: 546761)

Wanawake na wasichana ambao wamefanyiwa ukatili na kundi la kigaidi la Nigeria la Boko Haram wanahitaji kujua sio kosa lao. Ujumbe huo ni kutoka kwa mtaalamu wa Umoja wa mataifa ambaye amerejea kutoka ziara ya kutembelea makambi ya wakimbizi wa ndani zilizoko Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ya Afrika. Mtaalamu huyo ambaye ni mwakilishi maalumu [...]

25/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO , RFI kupigia chepuo historia ya bara Afrika

Kusikiliza / books22a

Shirika la Elimu ,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na redio ya kimataifa ya Ufaransa RFI, leo wametiliana saini makubaliano ya ushirikiano wa kihariri wa kupigia chepuo ukusanyaji wa kitabu cha historia ya Afrika. Taarifa ya UNESCO inasema kuwa katika makubaliano hayo RFI kupitia kipindi chake cha wiki kiitwacho kumbukumbu ya bara kitajikita katika historia [...]

25/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban atiwa hofu na mkwamo wa serikali ya mpito Sudan Kusini.

Kusikiliza / Mustakhbali wa watoto hawa wa Sudan Kusini uko mikononi mwa viongozi wa nchi hiyo. (Picha:UNMISS/Facebook)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon ameelezea hofu yake kuhusu mkwamo kwa pande zote Sudan Kusini dhidi ya kuanzisha majimbo 28 na kushindwa kwao kukamilisha miayadi ya tarehe 22 Januari ya kuanzisha serikali ya mpuito ya Umoja wa kitaifa nchini Sudan Kusini. Amesisitiza kwamba kuundwa kwa serikali ya mpito ni hatua muhimu katika [...]

25/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yafikisha misaada Yemen

Kusikiliza / Picha ya UNIFEED.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limefanikiwa kufikisha misaada ya chakula kwenye maeneo yaliyozingirwa mjini Taiz nchini Yemen ambapo watu wanakumbwa na njaa. Kwa mujibu wa taarifa ya WFP iliyotolewa leo, msafara wa WFP umepeleka vyakula vya mwezi mmoja kwa familia 3,000 baada ya kutimiza mazungumzo na pande kinzani za mzozo [...]

25/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO bado kuamua kuhusu usaidizi wake kwa uchaguzi DRC

Kusikiliza / Uchaguzi wa mwaka 2011 ulipata msaada wa MONUSCO. Picha ya Radio Okapi/ John Bompengo

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO umeeleza utayari wake wa kusaidia tume ya kitaifa ya uchaguzi CENI katika maandalizi ya uchaguzi nchini humo lakini bado kiwango cha usaidizi chapaswa kuamuliwa. Hii ni kwa mujibu wa video zilizotolewa na MONUSCO baada ya ziara ya rais wa CENI kwenye eneo [...]

25/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kasi ya kuenea kwa kirusi cha Zika inatutia hofu- WHO

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan. (Picha:WHO)

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO Dkt. Margaret Chan amesema taarifa za kuenea kwa kasi kwa kirusi cha Zika zinatia hofu kubwa . Akizungumza kwenye kikao cha bodi ya wakurugenzi ya WHO, Dkt, Chan amesema hofu hiyo inazingatia uwezekano wa uhusiano unaodaiwa kuwepo kati ya kirusi hicho na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo. [...]

25/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Lebanon Sigrid Kaag azuru Iran

Kusikiliza / Sigrid Kaag, Mratibu Maalum wa UM nchini Lebanon.  (Picha: MAKTABA/OPCW-UM)

Mratibu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Lebanon Bi. Sigrid Kaag, Jumapili amekutana na maafisa wa serikali ya Iran mjini Tehran. Mratibu huyo maalumu amejadili na maafisa wa serikali kuhusu hali ya kisiasa nchini Lebanon, maendeleo ya kikanda yanayoathiri Lebanon na juhudi za kuchagiza utulivu na usalama katika kanda nzima. Wakati za ziara [...]

25/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 500 zasakwa kusaidia wakimbizi CAR na Nigeria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Nigeria. Picha ya IRIN/Anna Jefferys

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake Jumatatu ya leo wametoa wito kwa nchi wahisani kuchangia zaidi ya dola nusu milioni mwaka huu ili kusaidia maelfu ya watu wanaolazimika kukimbia machafuko Nigeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, pamoja na jamii zinazowapokea na kuwapa malazi na huduma zingine muhimu. [...]

25/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA imezindua ombi kusaidia wakimbizi Cameroon mwaka 2016

Kusikiliza / Kambi ya wakimbizi ya Gado, Cameroon. Zaidi ya wakimbizi 120,000 wamewasili nchini Cameroon, waliokimbia mgogoro katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Picha: OCHA / John James.

Serikali ya Cameroon, Umoja wa Mataifa na wadau wake wamezindua mkakati wa kushughulikia mahitaji wa wakimbizi nchini Cameroon, na wakati huo huo kutangaza mipango ya kikanda kwa wakimbizi wa Nigeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), kwa mwaka 2016 kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA). John [...]

25/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano huko Darfur yashuhudiwa zaidi wakati huu: Ladsous

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID wakiwa kwenye doria. (Picha:Albert González Farran, UNAMID)

Leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kujadili hali ya usalama, kisiasa na kibinadamu kwenye eneo la Darfur nchini Sudan, huku mashambulizi dhidi ya raia na mapigano baina ya serikali na vikundi vilivyojihami yakiwa yameongezeka tena mwezi huu. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja [...]

25/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali lazima zishirikiane na WHO kutokomeza utipwatipwa kwa watoto:Ripoti

Kusikiliza / Watoto Laos wakila chakula shuleni. Picha: Benki ya Dunia / Bart Verweij

Tume ya kutokomeza utipwatipwa kwa watoto (ECHO) leo Jumatatu imewasilisha ripoti yake ya mwisho kwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO ikihitimisha mchakato wa miaka miwili wa juhudi za kukabiliana na kiwango cha juu cha utipwatipwa kwa watoto na uzito wa kupindikia kote duniani. Ripoti hiyo imetoa mapendekezo kadhaa kwa serikali yenye lengo [...]

25/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo kuhusu Syria yasogezwa hadi Ijumaa: de Mistura

Kusikiliza / staffan de Mistura. (Picha: UN Photo / Jean-Marc Ferré)

Mazungumzo kuhusu Syria yaliyokuwa yaanze leo, Geneva, Uswisi, yamesogezwa mbele hadi Ijumaa wiki hii ya tarehe 29. Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura ametangaza hayo leo akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva akisema yatafanyika kwa miezi Sita. Amesema mialiko kwa washiriki inatarajiwa kuanza kusambazwa Jumanne na [...]

25/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwekezaji wa kigeni Afrika wapungua 2015: Ripoti

Kusikiliza / Dr. Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD. (Picha@UNCTAD)

Uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja barani Afrika ulipungua mwaka jana kwa asilimia 31ambayo ni sawa na dola bilioni 38. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya awali ya makadirio ya uwekezaji mwaka 2015 kimataifa iliyotolewa na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, mwezi  huu wa Januari ambapo kwa mujibu [...]

25/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WMO yathibitisha mwaka 2015 umevunja rekodi ya joto duniani:

Kusikiliza / Picha: UNICEF/Olivier Asselin

Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limethibitisha kwamba wastani wa joto kimatifa kwa mwaka 2015 umevunja rekodi zote zilizopita kwa kiwango cha nyuzi joto 0.76C iki ni juu ya wastani wa mwaka 1961-1990 . Kwa mujibu wa WMO kwa mara ya kwanza kabisa mwaka 2015 kiwango cha joto kilikuwa nyuzi joto [...]

25/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa kuahirishwa kwa uchaguzi Haiti.

Kusikiliza / 639893Ban_Kimoon1

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-moon ameelezea kusikitishwa kwake na hatua ya kuahirishwa kwa uchaguzi mchini Haiti hivi karibuni uchaguzi ambao ulipangwa kufanyika Januari 24. Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa Bwana Ban amewataka wadau wote kufanya kazi kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unakamilika bila kuchelewa kupitia ridhaa yenye suluhisho litakalowapa fursa [...]

23/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu yazidi kuzorota Yemen: McGoldrick

Kusikiliza / Shahd, (11 ) Yemen, Picha na : UNICEF/UNI196752/Mahyoob

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Yemen, Jamie McGoldrick amesema juhudi za kuzifikia wilaya tatu zinazohitaji misaada ya kibinadamu nchini humo zinaendelea, ambapo mazungumzo na pande kinzani yanasongeshwa. Katika taarifa yake kuhusu ziara ya hivi karibuni nchini humo, kiongozi huyo amesema alijionea hali halisi ya kibinadamu na sasa wanasaka namna ya kuyafikia maeneo kusudiwa kwa [...]

23/01/2016 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mtazamo wa serikali ya Burundi kuhusu mzozo ni tofauti na wengine: Balozi Samantha

Kusikiliza / Mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Samantha Power akisalimiana na wenyeji wao kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura. (Picha:UNIC/Burundi)

Ujumbe wa Baraza la usalama uliokuwepo Burundi umehitimisha ziara yake na sasa unaelekea Ethiopia kwa ajili ya mazungumzo zaidi kuhusu Burundi na Somalia. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kiwanja cha ndege mji mkuu Bujumbura, mmoja wa wajumbe kwenye baraza hilo, Balozi Samantha Power wa Marekani amesema baada ya mazungumzo yao na pande zote ikiwemo [...]

22/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutoka Abu Dhabi hadi Afrika – matumizi ya nishati mbadala

Kusikiliza / Paneli ya nishati ya jua nchini Mali. Picha: World Bank/Curt Carnemark

Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya nishati mapema wiki hii wamekuwa na mkutano mjini Abu Dhabi, falme za kiarabu kuhusu nishati za baadaye. Huu ni mkutano wa siku tano uliowakutanisha viongozi na wataalamu wa nishati endelevu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu au ajenda 2030 wakati [...]

22/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kaskazini mwa Mali kwahitaji uwekezaji zaidi

Kusikiliza / Eneo la Bandiagara, kusini mwa Mali.(Picha:UM/John Isaac)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Sahel, Toby Lanzer amemaliza leo ziara yake nchini Mali ambapo ametembelea maeneo ya kaskazini mwa nchi yaliyokumbwa na mzozo wa kisiasa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA, Bwana Lanzer ametambua mafanikio [...]

22/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama Burundi tofauti na tunavyosikia- Balozi Martin

Kusikiliza / Mwakilishi wa kudumu wa Angola kwenye UM ambaye yuko kwenye msafara wa ujumbe wa baraza la usalama nchini Burundi. (Picha:UNIC/Burundi)

Wanachama wa Baraza la Usalama wamekutana leo na rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na wamejadili hali ya usalama nchini humo pamoja na mchakato wa mazungumzo ya amani yanayoratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuongozwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda. Hiyo ni kwa mujibu wa Balozi Ismael Martins mwakilishi wa kudumu wa Angola kwenye [...]

22/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wanapaswa kutekeleza kwa vitendo dhamira yao ili kufankisha maendeleo Afrika-Kituyi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi.(Picha:UM/Jean-Marc Ferre)

Kwa miongo minne sasa, mkutano wa jukwaa la uchumi limekuwa na lengo la kuimarisha hali kote ulimwenguni kitu ambacho kimesaidia katika programu ya mikutano ya kila mwaka. Mkutano huo wa kila mwaka wa Davos, Uswisi ni moja ya kiungo muhimu kinachowakutanisha viongozi mbali mbali kwa ajili ya juhudi za pamoja zinazolenga kuimarisha malengo na ajenda [...]

22/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Dansi ya Tchopa ni utamaduni muhimu miongoni mwa kabila la Lhomwe, Malawi

Kusikiliza / Wachezaji wa dansi ya Tchopa nchini Malawai.(Picha:UNESCO)

Dansi ya Tchopa ni utamduni unaopatikana miongoni mwa watu wa Lhomwe wanaoishi Kusini mwa Malawi na ni moja ya tamaduni ambazo zimeorodheshwa katika orodha ya tamaduni za dunia na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO. Lengo kuu ni kuhakikisha kwamba tamaduni hizi zinalindwa na umuhimu wake kutambulika na  kizazi hiki na kijacho. Katika makala [...]

22/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama Kivu Kaskazini yatia wasiwasi

Kusikiliza / Picha: UNHCR/B.Sokol

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa usaidizi wa kibinadamu OCHA huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC imesema hali ya usalama kwenye jimbola Kivu Kaskazini inazidi kudorora na kutia wasi wasi mkubwa. Rein Paulsen amesema kwa miezi kadhaa sasa hali inazidi kuwa mbaya huko Beni, Lubero, Masisi, Rutshuru na Walikale [...]

22/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Amani ya kudumu Nigeria ihusishe ujumuishaji wanawake na watoto kwenye jamii

Kusikiliza / Picha:UNICEF/NYHQ2007-0515/Nesbitt

Wataalamu watatu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa serikali ya Nigeria kuhakikisha mipango ya kuboresha jamii hasa zile zilizokumbwa na mashambulizi ya Boko Haram, zinahusisha kujumuisha wanawake na watoto. Katika taarifa yao ya pamoja baada ya kuhitimisha ziara yao nchini Nigeria, wataalamu hao wamesema hatua hiyo itahakikisha uboreshaji huo unawezesha [...]

22/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama wakutana na Rais Nkurunziza

Kusikiliza / Wanachama wa Baraza la Usalama wakiwasili kwenye uwanja wa ndege nchini Burundi. Picha ya UNIC Bujumbura.

Nchini Burundi, wajumbe wa Baraza la usalama walioanza ziara yao jana leo wameihitimisha baada ya kuwa na mazungumzo na pande mbali mbali akiwemo Rais Pierre Nkurunziza, vikundi vya kiraia, vyama vya siasa na spika wa bunge la nchi hiyo. Muda mfupi uliopita nimezungumza na mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga kufahamu yaliyojiri. (Kibuga package)

22/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Heko Zimbabwe kwa kuharamisha ndoa za utotoni

Kusikiliza / Mazingira ya shule kama haya ni fursa nzuri ya kuepusha watoto wa kike na ndoa katika umri mdogo. (Picha:UN/Marco Dormino)

Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe umekaribisha  uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini humo wa kuharamisha ndoa kwa watoto ambao ni watu wenye umri wa chini ya miaka 18. Taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF mjini Harare imesema uamuzi huo wa kihistoria utasaidia kusongesha haki za mtoto na hivyo kumaliza utamaduni [...]

22/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

El Niño yatishia wakazi Milioni 60 katika nchi zinazoendelea- WHO

Kusikiliza / Picha:UNICEF/ Martin Crespo

Shirika la afya duniani, WHO na wadau wake wametoa ripoti leo ikitabiri kuwa ongezeko kubwa la dharura za kiafya kutokana na mwelekeo wa El Niño ambayo kwingineko inasababisha mvua kubwa na mafuriko na kwingineko ukame. WHO imesema mvua kubwa zeney mafuriko zimeanza kushuhudiwa Tanzania, Kenya na Ecuador ilhali Ethiopia na Malawi hazipati mvua za kutosha [...]

22/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uimarishaji sekta ya teknolojia ni muhimu katika kufanikisha SDGs:UNCTAD

Kusikiliza / Maabara ya kompyuta nchini Sudan Kusini.(Picha:UM/JC McIlwaine)

Mataifa ya Afrika yawekeze katika sekta ya teknolojia ya digitali ili yaweze kufanikisha ajenda ya mwaka 2030, huo ni ujumbe wa Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi kwa mkutano wa jukwaa la uchumi huko Davos, Uswisi. Katika mahojiano maalum na Idhaa ya hii, Dkt. Kituyi amesema [...]

22/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ugaidi nchini Somalia ni kikwazo kwa kukuza haki za binadamu

Kusikiliza / Huyu ni kijana aliyekamatwa kwa madai kuwa mwanachama wa kundi la Al Shabaab nchini Somalia.(Picha:UM/Stuart Price)

Mwanasheria Mkuu wa Somalia, Ahmed Ali Dahir amesema tishio kubwa kwa haki za binadamu nchini Somalia ni mashambulizi ya kigadi dhidi ya viongozi wa serikali na raia. Priscilla Lecomte na taarifa kamili. (Taarifa ya Priscilla) Bwana Dahir amesema hayo leo wakati Somalia ikiangaziwa katika Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi, huku [...]

22/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tumesikitishwa na matamshi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja Malawi: OHCRC

Kusikiliza / Rupert Colville.(Picha:UM/Jean-Marc Ferre)

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imelaani matamashi ya msemaji wa moja ya vyama vikuu vya siasa nchini Malawi ya kwamba wapenziwa jinsia moja kuwa ni wabaya zaidi kuliko mbwa na hivyo wauawe. Tamko hilo limetolewa mapema mwezi huu na msemaji wa chama hicho Kenneth Msonda, katika ukurasa wake binafsi wa [...]

22/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rasimu ya sheria Denmark ya kunyang'anya vifaa wasaka hifadhi yatia wasiwasi

Kusikiliza / Wasaka hifadhi wakaguliwa na polisi nchini Macedonia. Picha ya UNICEF/Gjorgji Klincarov

Leo kwenye baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva Uswisi, nchi wanachama wamejadili hali iliyoko nchini Denmark ikiwemo sheria mpya inayotarajiwa kupitishwa na bunge la taifa hilo kuhusu wasaka hifadhi. Sheria hiyo ikipitishwa itaruhusu mamlaka za serikali kuchunguza vifaa binafsi vya wasaka hifadhi wanapoingia nchini humo, na kuwanyang'anya pesa au vifaa venye thamani ya zaidi [...]

21/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Yatosha sasa vita Syria: UM

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria.Picha ya UNHCR/O.Laban-Mattei

Zaidi ya mashirika 120 ya misaada ya kibinadamu  na Umoaj wa Mataifa yametoa tamko la pamoja la kuitaka dunia kuungana na kukomesha vita nchini Syria. Machafuko nchinibumo yameingia mwaka wa sita sasa zaidi yaw tau 200,000 wamefariki dunia, huku wengine zaidi milioni 13 ndani na nje ya nchi wakiwa wanahitaji misaada. Miongoni mwa mashirika yaliyotoa [...]

21/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Licha ya uharibifu, hazina za kitamaduni zinaweza kukarabatiwa tena: UNESCO

Kusikiliza / Maeneo ya urithi Syria.(Picha:©UNESCO/F. Bandarin)

Licha ya uharibifu wa thamani isiyokadirika wa urithi wa kitamaduni nchini Iraq, maeneo ya kitamaduni yanaweza kukarabatiwa na kurejeshwa katika hali ya awali baada ya migogoro. Huo ni mtazamo wa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na Utamaduni kitengo cha maandalizi ya kukabili dharura Bw. Giovanni Boccardi. Afisa waandamizi wa UNESCO [...]

21/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpango wa ujenzi kwenye Ukingo wa Magharibi walaaniwa na Katibu Mkuu

Kusikiliza / Ukuta unaogawanya Israel na maeneo ya Palestina yaliyotawaliwa, kwenye ukingo wa magharibi. Picha ya Photo: IRIN/Shabtai Gold

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu ripoti zinazoonyesha kwamba serikali ya Israel imeidhinisha kutangazwa kwa eka 370 kuwa ardhi ya taifa, kwenye ukingo wa Magharibi, kusini mwa Jericho. Amesema, uamuzi huo ukitekelezwa, utakuwa kitendo cha kujitwalia eneo la ardhi kubwa zaidi tangu Agosti mwaka 2014. Katibu Mkuu amekariri [...]

21/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM na Bank ya dunia kuzindua jopo maalumu kwa ajili ya maji

Kusikiliza / Mtoto akisubiri wakati mama yake akijaza kipipa cha maji. Picha ya UN/Tobin Jones

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Rais wa Bank ya dunia, Jim Yong Kim kwa pamoja wametangaza nia ya kuunda jopo jipya la kuchagiza hatua za haraka kuelekea lengo la maendeleo endelevu la maji na usafi (SDG 6) na mengine yanayoshabihiana. Lengo la maendeleo endelevu nambari 6 linahakikisha uwepo na uendelevu wa [...]

21/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban azipongeza Equatorial Guinea na Gabon kwa nia ya kuataka suluhu ya mzozo

Kusikiliza / Kijijini nchini Gabon, Picha ya UN/Gill Fickling

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha hatua ya kufanyika kwa mkutano wa pande tatu wa mawaziri kuhusu mzozo baina ya Jamhuri ya Equatorial Guinea na Gabon, uliofanyika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. Ban amezipongeza pande zote kwa kuonyesha ari ya kisiasa ya kasi mpya katika mchakato wa kukamilisha [...]

21/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kisa cha pili cha Ebola chagunduliwa Sierra Leone

Kusikiliza / Umakini unapaswa kuendelea ili kuhakikisha Ebola inatokomezwa. Picha ya UNICEF/NYHQ2014-3000/James

Nchini Sierra Leone, mtu wa pili amegunduliwa kuwa kirusi cha homa ya Ebola. Ametangaza leo msemaji wa Shirika la Afya duniani WHO, Tarik Jasarevic. Kisa hicho cha pili kinafuata kisa cha kwanza kilichogunduliwa nchini humo wiki iliyopita saa chache tu baada ya Sierra Leone kutangaza kuwa imetokomeza Ebola. Bwana Jasarevic amesema mgonjwa huyo ambaye sasa [...]

21/01/2016 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Grandi atembelea Za’atari azungumza na wakimbizi wa #Syria

Kusikiliza / Filipo Grandi, mkuu wa UNHCR akimsikiliza mkimbizi wa Syria aliyeko kambi ya Za'atari nchini Jordan. (Picha:UNifeed-Video capture)

Zaatari, kambi ya wakimbizi wa Syria nchini Jordan! Mzozo nchini Syria ukiingia mwaka wa Sita nuru bado haiko machoni mwa wakimbizi waliosaka hifadhi hapa. Maisha kambini hayana uhakika wakati huu ambapo usaidizi wa kimataifa nao umetindikiwa. Kamishna mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa Filipo Grandi akatumia fursa ya ziara yake nchini Jordan [...]

21/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

DiCaprio aibwatia sekta ya mafuta na gesi kwenye kongamano la uchumi Davos:

Kusikiliza / Leonardo di Caprio akihitubia Kongamano la Uchumi Duniani, Davos. Picha ya kutoka akaunti ya Twitter ya ClimateAction.

Leonardo DiCaprio ameyabwatia makampuni makubwa ya mafuta na gesi duniani kwa kuwa kwa kuwa na tamaa na kuchangia mabadiliko ya tabia nchi, katika hotuba yake kwenye kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos. Mtayarishaji na muigizaji huyo nyota wa Hollywood ameyasema hayo mbele ya wakuu wa nchi, mawaziri na wakuu wa makampuni akitoa wito wa kuchukua [...]

21/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban na hatua tano za kuchukua hatua kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Matumizi ya kuni kwa ajili ya nishati ya kupikia ni moja ya sababu za mmomonyoko wa ardhi na  uharibifu wa mazingira. (Picha:2006 © UNEP)

Mkutano wa jukwaa la uchumi duniani huko Davos, Uswisi ukiwa umeingia siku ya pili, mada kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na hatua za kuchukua imeangaziwa hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisema mwelekeo uko dhahiri. Ban akizungumza kwenye moja ya mijadala amesema athari ziko dhahiri shahiri na zimejidhihirisha kila kona ya [...]

21/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa jopo la UM kuhusu afya ya mama na mtoto

Kusikiliza / Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete. (Picha-MAKTABA/UN/Amanda Voisard)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza wajumbe wa kwanza wa jopo la ushauri la ngazi ya juu kuhusu afya ya mama na mtoto  #Everywomaneverychild. Jopo hilo la watu  12 litakuwa na wenyeviti wanne akiwemo Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete, na Waziri Mkuu wa Ethiopita Hailemariam Desalegn. Wengine ni Rais wa [...]

21/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM wasihi Ethiopia kutotumia ukatili dhidi ya waandamaji

Kusikiliza / Ethiopia.(Picha:Eskinder Debebe)

Wataalam wa haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameisihi serikali ya Ethiopia kusitisha hatua kali zinazochukuliwa na vikosi vya usalama dhidi ya waandamanaji nchini humo, huku tayari waandamanaji zaidi ya 140 wakiwa wameuawa na wengine kufungwa. Kwenye taarifa iliyotolewa leo, wataalam hao wameeleza kwamba maandamano hayo yameanza wiki tisa zilizopita baada ya serikali [...]

21/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati dhidi ya mabadiliko ya tabianchi ni fursa kwa wanawake: Dk Glemarec

Kusikiliza / Picha ya FAO/Georges Gobet

Mkuu wa sera na mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake, UN Women Dk Yannick Glemarec amesema kuna fursa ya kupunguza pengo la kijinsia kupitia harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchilicha ya chamgamoto kadhaa kama vile rasilimali fedha, teklnolojia na soko. Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa mjini Abu Dhabi [...]

21/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa Baraza la Usalama wawasili Burundi

Kusikiliza / Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakilakiwa uwanja wa ndege wa Bujumbura. (Picha:UNIC/Burundi)

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa umewasili hii leo jioni nchini Burundi katika juhudi za kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo. Wajumbe hao wanatarajia kukutana hapo kesho kwa mazungumzo na rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza kutoka Bujumbura, Muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anaarifu zaidi. (Taarifa ya Kibuga) Ujumbe wa Baraza la usalama [...]

21/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mchakato wa amani Sudan Kusini ukiendelea, ukiukwaji wa haki waripotiwa

Kusikiliza / Mkimbizi katika kituo cha kuhifadhi raia cha UNMISS (Picha/UM/Video capture)

Nchini Sudan Kusini kumeripotiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa na pande zote kwenye mzozo ulioanza nchini humo Disemba mwaka 2013. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo, vitendo kama mauaji kinyume cha sheria, ukatili wa kingono, utumikishaji na mashambulizi dhidi ya raia [...]

21/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watangaza jopo la ngazi ya juu la uwezeshaji wanawake kiuchumi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia kikao, Davos.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Mkutano wa jukwaa la uchumi ukiendelea huko Davos, Uswisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametumia fursa hiyo kushiriki katika matukio mbali mbali ikiwemo kutangaza jopo la uwezeshaji wanawake kiuchumi duniani na kuzindua jopo la kusongesha malengo ya maendeleo endelevu. Flora Nducha na taarifa kamili. (Taarifa ya Flora) Jopo hilo la uwezeshaji wanawake [...]

21/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

M-Pesa yabadilisha maisha ya watu Kenya

Kusikiliza / M-pesa.(Picha:Video capture/World Bank)

Nchini Kenya mfumo wa M-Pesa unaowezesha kufanya malipo kupitia simu za mkononi umeenea nchini kote, Benki ya Dunia ikikadiria kwamba hivi sasa umeanza kutumiwa na asilimia 80 ya watu nchini humo, kwa kipindi cha miaka minne tangu tu. Kuanzia mwuzaji mitumba hadi mashirika ya kimataifa, wote wanatumia mfumo huo ambao unachangia pakubwa katika ukuaji wa [...]

20/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amelaani vikali shambulio la kigaidi Pakistan

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia waandishi wa habari New York.(Picha:UM/

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali shambulio la kigaidi la wanamgambo wenye silaha lililofanyika leo kwenye chuo kikuu cha Bacha Khan mjini Charsadda, Pakistan, na kuuwa watu 19 huku wengine wengi wakijeruhiwa. Ban amesikitishwa na vitendo hivyo vya ghasia na kutoa wito wa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika na [...]

20/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa kimataifa unafanikiwa kukiwa na mipango kabambe:Ban

Kusikiliza / Ban Ki-moon akihutubia kikao cha mshikamano wa kimataifa Global Compact.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Umoja wa mataifa umedhihirisha kwamba palipo na mipango kabambe basi ushirikiano wa kimataifa unafanikiwa, hayo ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipozungumza leo kwenye kikao cha mshikamano wa kimataifa Global Compact kandoni mwa mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya uchumi mjini Davos Uswisi. Ban amesema ajenda ya mwaka 2030 [...]

20/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lengo la dola milioni 750 kusaidia shule kwa watoto wa Syria lazima lifikiwe:Brown

Kusikiliza / Mtoto akiwa na mifugo yake karibu ya mpaka wa Syria. Picha ya FAO.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu elimu Gordon Brown ameitolea wito dunia wakiwemo wafanyabiashara kufikia lengo la dola milioni 750 katika wiki mbili zijazo ili kufadhili maeneo ya shule kwa ajili ya watoto milioni moja wakimbizi wa Syria. Akizungumza katika kongamano la kimataifa la uchumi mjini Davos Uswisi, Bw Brown amesema [...]

20/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dunia ipaze sauti kukomesha machafuko Syria: WFP

Kusikiliza / Watoto hawa wanakula vitafunio vilivyosambazwa na WFP nchini Syria.(Picha:Dina El-Kassaby, WFP/Syria,)

Ikiwa ni takribani miezi 60 tangu kuzuka kwa mgogoro wa Syria , Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP kwa pamoja na mashirika 100 ya misaada ya kibinadamu yametoa tamko zito leo wakitaka dunia ipaze sauti kukomesha machafuko nchini Syria ili kutoa ahueni kwa mamilioni ya raia wanaoteseka nchini humo. Tamko hilo limetolewa mjini Roma [...]

20/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Slovenia na UNICEF washirikiana kusaidia watoto wahamiaji na wakimbizi:

Kusikiliza / Picha:UNICEF

Ikiwa wahamiaji na wakimbizi 3000 wanapitia Slovenia kila siku , shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na serikali ya Slovenia leo wametangaza ushirika wenye lengo la kuboresha huduma na ulinzi kwa watoto wanaokimbia. Wakati idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji wanakaa kwa muda mfupi Slovenia kabla ya kuendelea na safari yao, bado [...]

20/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ubia mpya kusaidia wakulima wadogo wadogo kupata masoko- WFP

Kusikiliza / Picha:FAO/Napolitano

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limetangaza kuingia makubaliano ya kuwezesha wakulima wadogo wadogo katika nchi zinazoendelea kupata masoko ya mazao yao. Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Etharin Cousin ametangaza mpango huo leo huko Davos, Uswisi wakati wa jukwaa la uchumi duniani akisema makubaliano yanahusisha mashirika makubwa ya umma na ya kibinafsi. Amesema kupitia mfumo [...]

20/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNEP na Benki ya maendeleo ya Kiislam watia saini makubaliano ya uhifadhi wa mazingira

Kusikiliza / Naibu mkurugenzi mtendaji wa UNEP Bw. Ibrahim Thiaw(kushoto) na Rais wa IDB, Dr. Ahmad Mohammad Ali al Madani(kulia). Picha:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira(UNEP) na Benki ya Maendeleo ya Kiislam IDB leo wameafikiana kushirikiana katika masuala mbalimbali yanayohusu uhifadhi wa mazingira katoka kupigia upatu maendeleo endelevu na vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Naibu mkurugenzi mtendaji wa UNEP Bw. Ibrahim Thiaw na Rais wa IDB, Dr. Ahmad Mohammad Ali al [...]

20/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake wanaokimbilia Ulaya hatarini kwa unyanyasaji wa kijinsia:UNHCR,UNFPA,WRC

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria(Picha ya UNHCR)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, shirika la idadi ya watu duniani UNFPA na tume ya wanawake wakimbizi WRC wanatiwa hofu na hatari zinazowakabili wanawake na wasichana wakimbizi na wahamiaji wanaohamia Ulaya. Mashirika hayo yamesema msimu mkali wa baridi inamaanisha sio watu wengi wanaochukua safari ya hatari kupitia bahari kuingia Ulaya hivi [...]

20/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika Cote d'Ivoire

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Manuel Elias)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu hali nchini Cote d'Ivoire ambapo limepatiwa ripoti kuhusu operesheni za Umoja huo kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Taarifa zaidi na  Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Nats… Kikaoni Baraza la usalama, Rais wa kikao Balozi.. akitangaza kupitishwa kwa kauli moja kwa azimio namba [...]

20/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bila ya ufadhili katika sekta ya kilimo Syria itaangamia zaidi:FAO

Kusikiliza / Picha:FAO

Wakati mapigano yanapamba moto Syria kwa mwaka wa sita sasa, sekta ya kilimo nayo inaangamia pole pole na kuwatumbukiza mamilioni ya watu katika njaa, na kusababisha kasi ya upungufu wa tija na kupanda kwa bei ya chakula, limesema Shirika la Chakula na Kilimo FAO.Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) FAO leo imetoa wito [...]

20/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nishati bunifu ni suluhu ya athari za mabadiliko ya tabianchi- Dkt. Han

Kusikiliza / Dkt. Han Seun-Soo (Picha:UN Radio/Basma Baghall)

Huko Abu Dhabi, Falme za kiarabu, wataalamu wamekuwa na mjadala kuhusu jinsi ubunifu kwenye nishati unaweza kusaidia kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi wakati huu ambapo tayari nchi wanachama wa UM zimepitisha mkataba mpya wa kudhibiti mabadiliko hayo. Akizungumza kwenye mjadala huo Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupunguza athari za [...]

20/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunafuatilia kirusi cha Zika- Tanzania

Kusikiliza / Hapa ni katika chumba cha kuhifadhi chanjo katika hospitali ya Mnazi moja, Zanzibar, Tanzania.(Picha:UN/Tanzania)

Serikali ya Tanzania imesema inafuatailia kwa karibu taarifa za za uwepo wa kirusi aina ya Zika ambacho kimeelezwa na shirika la afya ulimwenguni WHO kupatikana kwenye mataifa 18 duniani ikiwemo Uganda. Kirusi hicho kinachoenezwa na mbu aina  ya Aedes kinadaiwa kuwa na uhusiano na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo na mpaka sasa WHO inaendelea na [...]

20/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha uteuzi wa mawaziri wa mkataba wa kitaifa Libya

Kusikiliza / Mtoto akionyesha alama ya amani, nchini Libya. Picha ya Umoja wa Mataifa/Iason Foounten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha tangazo la baraza la Urais la uteuzi wa mawaziri kwa ajili ya serikali ya mkataba wa kitaifa ya Libya. Amesema hii ni hatua kubwa katika kuelekea utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa na suluhu ya mgogoro wa nchi hiyo. Katibu Mkuu amesema anatarajia kupitishwa kwa serikali mpya [...]

20/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wenye njaa CAR yaongezeka maradufu– WFP

Kusikiliza / Picha:WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na wadau wake limesema kuwa nusu ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wanakabiliwa na njaa ambapo, mtu mmoja kati ya sita ikiwemo, wanawake, watoto na wanaume hawana uhakika na mlo wa baadaye. John Kibego na taarifa zaidi.  (Taarifa ya Kibego) Katika taarifa yake ya leo, [...]

20/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa ajira watarajiwa kuongezeka 2016 na 2017- ILO

Kusikiliza / Picha:ILO

Licha ya kushuka viwango vya ukosefu wa ajira katika baadhi ya nchi zilizoendelea, ripoti mpya ya tathmini ya Shirika la Kazi Duniani, ILO imeonyesha kuwa mzozo wa ajira duniani huenda hautaisha, hususan katika nchi zinazoibuka. Ripoti hiyo imesema kuwa kuendelea kuwepo viwango vya juu vya ukosefu wa ajira kote duniani na ajira duni katika nchi [...]

19/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

M-Power yashinda tuzo ya nishati za baadaye Abu Dhabi

Kusikiliza / Picha ya UNEP

Shirika la Off Grid Electric lenye makao makuu yake nchini Tanzania ni miongoni mwa washindi tisa wa tuzo ya Zayed Future Energy iliyotangazwa leo mjini Abu Dhabi, falme za kiarabu. Tuzo hiyo ya dola milioni 4 inatuza watu, kampuni na shule bunifu katika nishati mbadala. Off Grid Electric ambayo inajulikana kwa jina la M-Power inauza [...]

19/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msimu wa baridi wakumba watoto wanaokimbilia Ulaya

Kusikiliza / Mtoto anayekumbwa na baridi kali kwenye eneo la kupokea wakimbizi nchini Macedonia. Picha ya  UNICEF/Ashley Gilbertson VII

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF limeonya kwamba watoto wanaokimbia barani Ulaya wanakumbwa na madhara ya msimu wa baridi, ikiwemo vichomi vikali yaani pneumonia na ugonjwa wa kuhara. Kwenye taarifa iliyotolewa leo UNICEF imeeleza kwamba watoto hawa hawana nguo za kuwakinga na baridi kali na theluji, na sehemu wanakolala hazina joto la [...]

19/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wananchi wa Sudan Kusini wamechoka kuwa tegemezi- Mogae

Kusikiliza / Bwana Festus Mogae akisalimiana na wakazi wa Bentiu. (Picha:UN/JC McIlwaine)

Hivi karibuni, Festus Mogae ambaye ni mwenyekiti wa kamisheni ya pamoja ya kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini, JMEC, alikuwa ziarani kwenye maeneo ya Malakal na Bentiu. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kumwezesha kukutana na pande mbali mbali ikiwemo serikali, pande kinzani na hata mashirika yanayotoa misaada ya kibinadamu. [...]

19/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Messi miongoni mwa wajumbe wa jopo la kuchagiza utekelezaji wa SDGs

Kusikiliza / Rais John Dramani Mahama wa Ghana. (Picha:UN/Cia Pak)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza jopo la watu 17 maarufu la kuchagiza utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa mwaka jana. Taarifa ya msemaji wake imesema jopo hilo litaongozwa na Rais John Draman Mahama wa Ghana kwa ushirikiano na Waziri Mkuu wa Norway Erna Solberg. Wajumbe wengine ni Bi. Graca [...]

19/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Denmark yaweka rekodi mpya ya matumizi ya upepo kwenye nishati

Kusikiliza / Tabo za upepo huko Denmark. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Denmark imeweka rekodi mpya duniani ya kutumia upepo kuzalisha nishati ya umeme. Kwa mujibu wa tovuti ya Climate action ambayo inafuatilia utekelezaji wa hatua za kukabili mabadiliko ya tabianchi, asilimia 40 ya umeme uliotumika nchini Denmark mwaka 2014  ulitokana na upepo na kufikia asilimia 60 mwezi Januari mwaka 2015. Waziri wa nishati wa Denmark Rasmus [...]

19/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dola bilioni 1.3 zahitajika kusaidia watu milioni 5.1 Sudan Kusini:OCHA

Kusikiliza / Usambazaji wa misaada kwa wakimbizi nchini Sudan Kusini.(Picha:UM/JC McIlwaine)

Mpango wa kusaidia masuala ya kibinadamu Sudan Kusini kwa mwaka 2016 uliozinduliwa leo rasmi mjini Juba umeomba dola bilioni 1.3 ili kukabiliana na mahitaji ya lazima ya kuokoa maisha kwa watu zaidi ya milioni tanonchini humo. Jumla ya mashirika 114 ya misaada ya kibinadamu yakiwemo ya kimataifa, yasio ya kiserikali yaani NGOs na mashirika ya [...]

19/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ufaransa yatakiwa kulinda uhuru wa watu inapokabiliana na ugaidi

Kusikiliza / Maua yaliyowekwa nje ya Bataclan  Paris kwa ajili ya wahanga wa mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Hali ya sasa ya dharura nchini Ufaransa na sheria ya ufuatiliaji wa mawasiliano ya elektroniki unaweka vikwazo vya kupita kiasi na visiyvo na uwiano dhidi ya uhuru wa kimsingi wa watu , limeonya leo kundi la Umoja wa Mataifa la wataalam wa haki za binadamu . Katika orodha ya vitu vinavyowatia hofu walivyoileza serikali ya [...]

19/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulinzi wa raia wapaswa kuimarishwa kwenye mizozo ya kisasa

Kusikiliza / Shule ya Jabalia kwenye eneo la GAza, Palestina, ambayo imeshambuliwa na makombora. UNRWA Archives/Shareef Sarhan

Leo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limejadili namna ya kuimarisha ulinzi wa raia wakati wa mizozo, na wajibu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa na pande kinzani za mzozo. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Akihutubia kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema raia wanazidi kuwa [...]

19/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi yakaribisha wajumbe wa Baraza la usalama

Kusikiliza / Picha:UNHCR/T.W.Monboe

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unatarajia kufanya ziara ya siku mbili nchini Burundi katika juhudi za kukwamua mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini humo. Serikali ya Burundi imekaribisha ziara hiyo kwa kusema ni fursa ya kushuhudia hali halisi inayojiri  Burundi. Kutoka Bujumbura, Mwandishi wetu Ramadhani Kibuga anaarifu zaidi. (TAARIFA YA KIBUGA)

19/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa haki za binadamu wakaribisha kuachiliwa kwa raia wa Marekani Iran

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu. Picha: Umoja wa Mataifa/ Jean-Marc Ferré

Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa leo wamekaribisha  hatua ya serikali ya Iran ya kuwaachilia huru raia wanne wa Marekani wenye asili ya Iran na kuitolea wito serikali ya Tehran kufungua mlango wa kuachiliwa mahabusu wote wanaoshikiliwa kinyume cha sheria  katika magereza ya nchi hiyo. Mwishoni mwa juma maafisa wa serikali ya [...]

19/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hadi sasa hakuna uhusiano kati ya Zika na watoto wenye vichwa vidogo- WHO

Kusikiliza / kirusi cha Zika hicho kinaenezwa na mbu aina ya Aedes

Shirika la afya duniani, WHO linafuatilia kwa karibu taarifa za uwepo wa kirusi aina ya Zika katika mataifa 18 duniani, kirusi ambacho kinadaiwa kuwa na uhusiano na watoto wanaozaliwa na vichwa vidogo. WHO imesema kirusi hicho kinachoenezwa na mbu aina ya Aedes, kimeripotiwa katika mataifa ya Amerika, Afrika na Pasifiki Magharibi na ndicho kinachosababisha ugonjwa [...]

19/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi ya Boko Haram, UNHCR yahaha kusaidia waliopoteza makazi

Kusikiliza / Makazi ya muda mashariki mwa Diffa nchini Niger(Picha© UNHCR/B.Bamba)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi,  UNHCR na wadau wake wanahaha kusaidia takribani watu Laki Moja waliopoteza makazi yao kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na Boko Haram hivi karibuni. Wakazi hao kutoka eneo la Diffa, kusini-mashariki mwa Niger wako katika mazingira magumu kutokana na kukosa makazi, vyakula na wanahusisha pia wenyeji ambao walikuwa wanawapatia [...]

19/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wanaopoteza maisha Iraq ni kubwa-ripoti ya UM

Kusikiliza / Wanawake wa Mosul. Picha: HCR/S. Baldwin (Maktaba)

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inaelezea kwa undani athari kubwa za vita vinavyoendelea kwa raia nchini Iraq, ikionyesha takriban raia 18,802 wameuawa na wengine 36,245 kujeruhiwa kati ya Januari Mosi 2014 na Oktoba 31 mwaka 2015. Ripoti pia inasema watu wengine zaidi ya milioni tatu wamekuwa wakimbizi wa ndani wakiwemo watoto zaidi ya [...]

19/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaonya juu ya hatari ya watu wa Pembe ya Afrika wanaovuka bahari kuingia Yemen

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wakimchukua kijana mmoja kutoka chombo cha waokozi wa pwani wa Italia, Gregoretti kilichowaokoa mapema wiki hii kutoka bahari ya Mediterranean. (Picha:UNHCR/F.Malavolta)

Takwimu za karibuni za shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kuhusu wanaowasili kwa njia ya bahari kuingia Yemen zinaonyesha licha ya mgogoro unaoendelea watu zaidi ya 92,000 waliwasili kwa boti 2015. UNHCR inasema hiyo ni idadi kubwa kabisa kwa mwaka kwa kipindi cha mungo mmoja uliopita.Hata hivyo safari hiyo pia ilighubikwa na [...]

19/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya dola milioni 800 zahitajika Somalia- OCHA

Kusikiliza / Msichana akitembea barabarani wakati jua likitua katika kambi ya wakimbizi wa ndani (IDPs) karibu na mji wa Jowhar, Somalia. Picha:UN Photo/Tobin Jones

Jumuiya ya masuala ya kibinadamu nchini Somalia leo imezindua mpango wa masuala ya kibinadamu ya kuyapa kipaumbele mwaka 2016 (HRP) mjini Mogadishu, ukitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuhakikisha ufadhili unaohitajika na kwa wakati. Amian Hassan na taarifa kamili. (Taarifa ya Amina) Mpango huo mpya unatafuta dola milioni 885 ili kuwafikia watu milioni 3.5 wanaohitaji [...]

19/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS yaweka kambi ya matibabu kwa wakazi wa Malakal na Upper Nile

Kusikiliza / Kituo cha afya nchini Sudan Kusini.(Picha:UNMISS)

Walinda amani wa mpango wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini UNMISS wameendesha huduma ya bure ya kambi ya matibabu waliyoiweka maalumu kwa ajili ya jamii za Malakal, Upper Nile. Walinda Amani hao kutoka jeshi la wanamaji la Bangladeshi wamejitolea kutoa huduma za msingi za matibabu kwa wakazi kwenye kituo kipya kwenye ukingo wa Magharibi wa [...]

19/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR: Kamishina mkuu akaribisha vibali vya kufanya kazi kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Wakimbizi katika kambi ya Nizip Kusini Mashariki mwa Uturuki.(Picha:UNHCR)

Katika hatua ya mabadiliko makubwa ya sera, serikali ya Uturuki, imechapisha sheria mpya ambazo zinawaruhusu maelfu kati ya wakimbizi milioni 2.5 wa Syria waliopo nchini humo kuomba vibali vya kufanya kazi. Wakimbizi walioorodheshwa na kuwemo Uturuki kwa takribani miezi sita wataruhusiwa kuomba vibali hivyo katika majimbo waliyowasili kwa mara ya kwanza . Wasyria watakaokuwa na [...]

18/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Matumizi ya dawa za kulevya na athari zake nchini Uganda

Kusikiliza / Polisi wakifanya upelelezi katika nyumba ya mtu anayedaiwa kulima na kuuza bangi mjini Hoima, Uganda.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/J.Kibego)

Matumiz ya madawa ya kulevya huwa ni kikwazo cha maendeleo ya jamii katika nchi nyingi duniani, na pia huhusishwa na utendaji wa makosa ya jinai. Nchini Uganda hasa kwenye Ziwa Albert, matumizi ya madawa hayo miongoni mwa vijana yanaarifiwa kuchochea uhalifu wa aina mbalimbali ukiwemo wizi, kama anavyosimulia John Kibego katika makala ifuatayo. (Makala ya [...]

18/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Syria: maisha ya wakazi 200,000 wa Deir-ez-Zor iliyozingirwa hatarini

Kusikiliza / Misaada inasambazwa kwenye mji wa Madaya ambao umezingirwa pia. Picha ya WFP/Hussam Alsaleh

Mashirika ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yameelezea wasiwasi wao kuhusu watu wapatao 200,000, hasa wanawake na watoto, wanaozingirwa mkwenye mji wa Deir-Ez-Zor, nchini Syria. Hayo yamesemwa na Stéphane Dujarric msemaji wa Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari leo mjini New York Marekani, akiongeza kwamba watu hawa wanahitaji misaada ya kibinadamu, hususan vyakula, [...]

18/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban na Rais Buhari wajadili Boko Haram, ufisadi na uchumi Nigeria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Rais Buhari wa Nigeria. Picha ya Mark Garten.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana leo na rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, mjini Abu Dhabi, kwenye Falme za Kiarabu, UAE, ambapo amepongeza juhudi za rais huyo katika kupambana na ufisadi, hali mbaya ya usalama na kuendeleza maendeleo ya uchumi Nigeria. Ban amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuziunga mkono juhudi hizo. [...]

18/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watalii duniani ilivunja rikodi mwaka 2015

Kusikiliza / Nambari zilizoonyesha ni idadi ya watu waliosafiri kwenye sehemu hizo kwa ajili ya utalii na asilimia ya utalii mzima. Picha ya UNWTO

Idadi ya watu wanaosafiri nje ya nchi yao kwa ajili ya utalii iliongezeka kwa asilimia 4.4 mwaka 2015 na hivyo kuvunja rikodi mpya kwa mwaka wa sita mfululizo. Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii UNWTO limesema kwenye taarifa yake kuwa idadi ya watalii ilifikia bilioni 1.2 mwaka 2015 na ongezeko hilo limechangia pakubwa katika [...]

18/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO imefungua kituo kipya cha dharura na polio Jordan

Kusikiliza / Chanjo dhidi ya Polio. (Picha:Maktaba:UN/JC McIlwaine)

Kama sehemu ya kuimarisha shughuli zake za dharura kanda ya Mashariki ya Kati na kupambana na polio Shirika la Afya Duniani (WHO) limefungua kituo cha kikanda kwa ajili ya dharura za kiafya na kutokomeza polio mjini Amman, Jordan. Kwa mujibi wa WHO idadi ya watu wanaohitaji huduma za kiafya za dharura ni kubwa sana kutokana [...]

18/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kitabu kipya cha FAO chapendekeza mbinu mpya za kilimo endelevu

Kusikiliza / Wakulima wakifanya kazi Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Picha: FAO / A. Masciarelli

Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, limetoa leo kitabu kipya kinachopendekeza kubadili mfumo wa kuhifadhi na kuongeza mazao ya kilimo, kikitoa mwongozo wa kuweka mustakhabali endelevu kwa kilimo na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu. Kitabu hicho kinamulika jinsi uzalishaji wa nafaka kuu duniani, mathalan mahindi, mchele na ngano unavyoweza kufanywa kwa njia zinazoheshimu na kulinda [...]

18/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA NA Iran kuimarisha ushirikiano

Kusikiliza / Yukiya Amano, IAEA na Dr Ali Akbar Salehi, Iran wakihutubia waandishi wa habari.(Picha: F. Dahl/IAEA)

Shirika la kimataifa la nguvu  za Atomiki IAEA, na serikali ya Iran zimekubaliana kuimarisha mahusiano baina ya pande mbili ikiwa ni matokeo ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukiya Amano nchini humo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (TAARIFA YA GRACE) Kwa mujibu wa taarifa ya IAEA  Bwana Amano amekuwa na mazungumzo na Mwenyekiti na [...]

18/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tisho la El nino laongezeka msimu wa kupanda ukikaribia Kusini mwa Afrika:

Kusikiliza / Kusini mwa Afrika, ukame watishia maisha ya watu. Picha ya FAO.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linazidi kuhofia usalama wa chakula Kusini mwa Afrika ambako watu takribani milioni 14 wanakabiliwa na njaa kufuatia ukame uliosababisha mavuno hafifu mwaka jana. Priscilla Lecomte na taarifa kamili (TAARIFA YA PRISCILLA) Kwa mujibu wa WFP majira ya El Nino ambayo yanachangia hali kuwa mbaya Zaidi ukanda mzima [...]

18/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjini Abu Dhabi Ban Ki-moon atoa wito kwa uchumi unaojali mazingira

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban ki-moon katika ziara yake . UN Photo.

Leo mijini Abu Dhabi, kwenye Falme za Kiarabu, UAE, kumezinduliwa kongomano kuhusu nishati za baadaye, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema nishati endelevu kwa bei nafuu zitachangia pakubwa katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, pamoja na kuokoa maisha ya watu milioni 4.3 wanaofariki kila mwaka kutokana na vyanzo duni vya nishati, [...]

18/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua za dharura zahitajika kupunguza mateso gerezani Benin- UM

Kusikiliza / Kwenye gereza nchini Mali. Picha MINUSMA/Marco Dormino

Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia utesaji, (SPT), imeitaka serikali ya Benin ichukue hatua mara moja ili kukabiliana na msongamano na mateso gerezani, na kuboresha hali ya ujumla ya walio vizuizini. Kamati hiyo imesema hayo mwishoni mwa ziara ya wataalam wake nchini Benin, ambao wamesema kuwa ingawa Benin imepiga hatua kwa kiasi fulani tangu [...]

18/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatua za kukabiliana na ugaidi kutishia fedha zinazotumwa nyumbani na Wasomali wa ughaibuni

Kusikiliza / Pesa za Somalia.(Picha:UM/Stuart Price)

Utumwaji wa fedha nyumbani kutoka kwa Wasomali waishio ughaibuni kunatishiwa na hatua za lazima za kukabiliana na ugaidi lakini ambazo hazikufikiriwa vyema. Amina Hassan na taarifa kamili (TAARIFA YA AMINA HASSAN) Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba hatari za hatua hizo zinaathiri pakubwa haki za binadamu za watu wa Somalia [...]

18/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yatiwa hofu na mapigano huko Darfur ya Kati

Kusikiliza / Doria ya UNAMID, Darfur. Picha ya Albert González Farran, UNAMID

Ujumbe wa pamoja wa Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, Sudan umesema una wasiwasi mkubwa kutokana na mapigano yanayoendelea huko Darfur Kati baina ya vikosi vya serikali na vikundi vilivyojihami. Mapigano hayo ni kwenye eneo la Jebel Marra karibu na kituo cha UNAMID kilichoko Nertiti. Katika taarifa yake UNAMID imeripoti kuangushwa kwa [...]

17/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tutapimwa kwa kuboresha maisha ya watu si kwa ahadi- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon wakati wa uzinduzi wa ripoti. (Picha:UN/Basma Banghal)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwenye uzinduzi wa ripoti ya uchangiaji kwa masuala ya kibinadamu huko Dubai Falme za kiarabu na kusema kuwa wakati wa kusaka suluhu za muda mfupi kwa ajili ya misaada hiyo umekwisha. Ban amesema hayo kwa kuzingatia kuwa majanga yanazidi duniani kila uchao na mahitaji yanaongezekwa kwani [...]

17/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti kuhusu usaidizi wa kibinadamu kuwasilishwa leo Dubai

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa Palestina wakati wa msimu wa baridi nchini Syria. Picha ya UNRWA/Taghrid Mohammad

Jopo la ngazi ya juu kuhusu uchangishaji fedha kwa usaidizi wa kibinadamu hii leo linawasilisha ripoti yake ya mapendekezo ya jinsi ya kufanikisha harakati hizo kwenye mkutano unaofanyika leo huko Dubai, Falme za kiarabu. Akizungumza na waandishi wa habari New York, Marekani, Kristalina Georgieva ambaye ni mwenyekiti mwenza wa jopo hilo amesema wameamua kuwasilisha ripoti [...]

17/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lapongeza chaguzi Afrika Magharibi, likihofia pia usalama

Kusikiliza / Guinea /Picha na UNDP

Baraza la usalama limekaribisha chaguzi za karibuni zilizofanyika nchini  Nigeria, Togo, Burkina Faso, Guinea na Côte-d’Ivoire, huku pia likisistiza haja ya chaguzi zijazo nchini Niger, Benin, Cabo Verde, Ghana na Gambia kuwa huru, za haki, amani, jumuishi na za kuaminika. Wajumbe wote 15 wa baraza pia wameelezea hofu yao kwamba mivutano ya kisiasa nchini Guinea-Bissau [...]

17/01/2016 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani vikali shambulio la Ouagadougou

Kusikiliza / Baraza la usalama:picha na UM

Wajumbe wa baraza la usalama wamelaani vikali mashambulio ya kigaidi mjini Ouagadougou, Burkina Faso, yaliyotokea Ijumaa ya tarehe 15 Januari 2016, ambapo watu 29 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Kundi la kigaidi la Al Mourabitoune, ambalo linauhusiano na kundi la Al-Qaida limekiri kuhusika na mashambulizi hayo. Wajumbe wametuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika, [...]

17/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran vyaondolewa:IAEA

Magavana wa IAEA / Picha na IAEA

  Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki, IAEA limetangaza kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran kufuatia nchi hiyo kuanza kukidhi matakwa ya makubaliano ya mwezi Julai kati yake na mataifa yenye nguvu zaidi duniani. Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukia Amano ametangaza hatua hiyo leo , hatua ambayo imeungwa mkono pia na Katibu [...]

16/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulio la kigaidi mjini Ouagadougou, Burkina Faso

Rais Roch Kabore

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi lililotokea jana Ijumaa mjini Ouagadougou, Burkina Faso, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 20 na kujeruhi wengine wengi. Ban ambaye ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu wa waarithika, watu wa Burkina Faso na serikali , pia amewatakia nafuu ya haraka majeruhi na [...]

16/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na waziri wa Bahrain wajadili changamoto za usalama katika kanda

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon. (Picha: MAKTABA: UN Photo/NICA)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amezungumza kwa njia ya simu na waziri wa mambo ya nje wa ufalme wa Bahrain, Sheikh Khalid bin Ahmed Al Khalifa. Miongoni mwa mambo waliyojadili ni hali katika eneo la Ghuba ya Uajemi ikiwa ni pamoja na changamoto za Amani na usalama katika kanda hiyo. Ban [...]

16/01/2016 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia wa Msumbiji wanaowasili Malawi inaongezeka :UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Mozambique.(Picha:UNHCR/Video Capture)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi ya watu wanaokimbia Msumbiji na kutafuta hifadhi nchini Malawi imeongezeka sana katika wiki chache zilizopita. Katika kijiji cha Kapise, wilaya ya Mwanza kilometa chache kutoka mji mkuu Lilongwe , timu ya UNHCR imeorodhesha watu  1,297 waliowasili huku theluthi mbili wakiwa wanawake na watoto na [...]

15/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Maadhimisho ya muongo wa watu wenye asili ya afrika

Kusikiliza / Dkt. Deloys Blakeley akiwa kwenye maonyesho ya muongo wa watu wenye asili ya Afrika.(Picha:UM/

Kwa zaidi ya miaka mia 400, biashara ya utumwa imekuwa janga lililoikumba Afrika, ikikadiriwa kwamba zaidi ya watu milioni 15, wanaume, watoto na wanawake wamekuwa wahanga wa biashara hii kupitia bahari ya Atlantiki. Hadi leo, Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba watu wapatao milioni 200 wenye asili ya Afrika wanaishi Marekani na kwenye bara la Amerika [...]

15/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjini Madaya, watu wanahitaji msaada wa kuokoa maisha

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa Palestina wakati wa msimu wa baridi nchini Syria. Picha ya UNRWA/Taghrid Mohammad

Timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF iliyowasili mjini Madaya nchini Syria wiki hii imeshuhudia kifo cha mtoto wenye umri wa miaka 16 aliyeathirika na unyafuzi. Msemaji wa UNICEF Syria Hanaa Singer amenukuliwa kwenye taarifa ya shiriki hilo akisema mtoto huyo alifariki dunia hospitalini,  huku watoto 22 wenye unyafuzi wakiwa wamebainiwa [...]

15/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulio dhidi ya AMISOM Somalia

Kusikiliza / Walinda amani walioko kwenye kikosi cha ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini Somalia, AMISOM wakiwa kwenye doria. (picha:AMISOM / Tobin Jones)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio la kigaidi lililotekelezwa asubuhi ya leo katika kituo cha ujumbe wa Afrika nchini Somalia AMISOM mjini El Adde, mkoani Geddo nchini humo. Idadi ya waathirwa katika shambulio hilo bado inahakikishwa. Taarifa ya Katibu Mkuu iliyotolewa na ofisi ya msemaji wake inasema kuwa Ban amepongeza juhudi [...]

15/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa na Zimbabwe kuanzisha mpango wa kukabiliana na El-nino

Kusikiliza / Ukame waathiri pia mifugo. Picha ya FAO Zimbabwe

Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Zimbabwe yamekutana leo mjini Harare kujadili athari zilizosababishwa na El-Nino nchini humo na kutayarisha mpango wa dharura ili kukabiliana na tatizo hilo. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini humo imesema kwamba huenda hali ya ukame inaweza kuwa mbaya zaidi mwaka 2016 ikilinganishwa na mwaka 2015, watu [...]

15/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hassen Ebrahim Mussa ndiye kamanda mpya wa UNISFA

Kusikiliza / Picha:Martine Perret

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon leo ametangaza uteuzi wa Meja Jenerali Hassen Ebrahim Mussa wa Ethiopia kama kamanda mpya wa vikosi vya usalama vya muda vya Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Abyei (UNISFA). Anachukua nafasi ya Luteni Jenerali  Birhanu Jula Gelalcha wa Ethiopia ambaye atahitimisha muda wake tarehe 20 ya mwezi [...]

15/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kongamano la WIPO lakutanisha wabunifu wa mitindo Afrika kuhusu hati miliki

Kusikiliza / Miongoni mwa wanamitindo walioshamirisha kongamano hilo kwa kuonyesha mitindo mbali mbali. (Picha:WIPO/Videocapture)

Sekta ya ubunifu wa mitindo barani Afrika ina uwezo mkubwa wa kukua, kwani kuna wingi wa talanta na ubunifu kote barani. Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hati Miliki Duniani, WIPO, matumizi yafaayo ya hati miliki yanaweza kuchangia maendeleo endelevu ya sekta hiyo. Kwa mantiki hiyo, hivi karibuni, WIPO iliandaa kongamano kuhusu hati [...]

15/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

AMISOM yashambuliwa na Al-Shabaab Somalia

Kusikiliza / Askari wa AMISOM. Picha ya UN/Stuart Price

Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika nchini Somalia, Balozi Francisco Madeira, amelaani vikali mashambulizi yaliyotokea leo alfajiri kwenye kituo cha ujumbe wa Muungano huo nchini Somalia, AMISOM huko El Adde, kwenye eneo la Gedo nchini humo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na AMISOM shambulio hilo la kigaidi limefanywa na kikundi cha [...]

15/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid aonya kuibuka kwa ukiukwaji mpya wa haki Burundi ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia:

Kusikiliza / Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein.(Picha:UM/Violaine Martin)

Tunaanzia Burundi, Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataida  Zeid Ra'ad Al Hussein ametoa taarifa akiionya Burundi juu ya kuibuka kwa mwenendo mpya unaotia wasiwasi ikiwa ni pamoja na kesi za unyanyasaji wa kijinsia unaofanywa na vikosi vya usalama na ongezeko kubwa la kupotea kwa watu na visa vya mateso. Flora Nducha [...]

15/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atangaza mpango dhidi ya misimamo mikali

Kusikiliza / Mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na Boko Haram kaskazini-mashariki mwa Nigeria yamekuwa na madhara makubwa. (Picha: Mohammad Ibrahim/Irin http://bit.ly/1NgnlDy)

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza mpango wake wa kukabiliana na ghasia zinazochagizwa na misimamo mikali akisema ni muhimu kwa kuwa vitendo hivyo ni shambulizi la moja kwa moja dhidi ya katiba inayounda chombo hicho. Akitangaza mbele ya Baraza Kuu, Ban amesema mpango wake wa utekelezaji wenye mapendekezo 70 yanayojikita kwenye misingi [...]

15/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO kukabiliana na ukame Ethiopia

Kusikiliza / fao ETHIOPIA FUPI

Nchini Ethiopia, Shrika la chakula na kilimo FAO linasema ukame uliokumba nchi hiyo kwa takribani miongo mitatu kutokana na ukame uliosababishwa na mvua za El-Nino umesababisha watu zaidi ya milioni 10 kukumbwa na njaa , huku mifugo ikiwa imekufa kwa wingi na mazao kuharibika. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) FAO ambayo imezindua [...]

15/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia wa Msumbiji wanaowasili Malawi inaongezeka :UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Mozambique baada ya kuwasili Kapise, Malawai. (Picha© UNHCR/M. Mapila)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema idadi ya watu wanaokimbia Msumbiji na kutafuta hifadhi nchini Malawi imeongezeka sana katika wiki chache zilizopita. Katika kijiji cha Kapise, wilaya ya Mwanza kilometa chache kutoka mji mkuu Lilongwe , timu ya UNHCR imeorodhesha watu  1,297 waliowasili huku theluthi mbili wakiwa wanawake na watoto na [...]

15/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kisa kipya cha Ebola Sierra Leone, serikali na wadau wachukua hatua:WHO

Kusikiliza / Chanjo ya ebola.(Pichaya UM/WHO/M. Missioneiro/maktaba)

Siku moja baada ya Shirika la afya duniani, WHO kutangaza kutokomezwa kwa Ebola huko Afrika Magharibi, mtu mmoja amefariki dunia kutokana na Ebola huko Sierra Leone na hivyo kutishia uwezekano wa kuibuka upya kwa kirusi hicho kwenye nchi hizo. Msemaji wa WHO Geneva, Uswisi, Tarik Jasarevic amesema mgonwja huyo mwanamke alifariki dunia tarehe 12 mweiz [...]

15/01/2016 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Apu ya #ShareThe Meal yatimiza lengo lake

Kusikiliza / Watoto hawa wanakula vitafunio vilivyosambazwa na WFP nchini Syria.(Picha:Dina El-Kassaby, WFP/Syria,)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP limetangaza leo kwamba limefikia lengo lake la kuwapatia watoto wakimbizi 20,000 wa Syria waliopo Jordan mlo wa shuleni kwa mwaka mzima, kupitia mradi wake mpya wa apu ya simu za mkononi iitwayo "Share the Meal". Kwenye taarifa  iliyotolewa leo, WFP imesema kwamba sasa Share the [...]

15/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNMISS yakutanisha upinzani na jamii ya wakimbizi wa ndani

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Sudan Kusini baada ya kuwasili katika jimbo la Upper Nile.(Picha:UNHCR/Jake Dinneen)

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, Ellen Margrethe Løj, amekariri dhamira ya ujumbe huo ya kuunga mkono utekelezaji wa makubaliano ya amani kuhusu kuutanzua mzozo nchini humo. Bi Margrethe Løj amesema hayo akifungua mkutano wa wajumbe wa SPLM Upinzani na wawakilishi wa watu waliolazimika kuhama makwao katika kituo cha ulinzi [...]

15/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO kuendesha tafiti kuhusu maambukizi ya Ebola kupitia mbegu za kiume

Kusikiliza / Picha:UNMEER/Martine Perret

Shirika la afya duniani, WHO kanda ya Afrika limesema tafiti zaidi zinahitajika kufahani ni jinsi gani wanaume waliopona Ebola wanasababisha maambukizi ya kirusi cha homa hiyo hatari kupitia mbegu zao za kiume. Mkurugenzi wa magonjwa ya kuambukiza wa WHO katika kanda hiyo Magda Robalo amesema hayo akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kwa kuzingatia [...]

15/01/2016 | Jamii: Ebola | Kusoma Zaidi »

#Burundi yazidi kumtia hofu Ban, kadhalika Madaya #Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia waandishi wa habari New York.(Picha:UM/

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejelea kauli yake kuhusu ukosefu mkubwa wa utulivu nchini Burundi, sanjari na hali isiyotabirika. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mipango yake ya utekelezaji kwa mwaka huu wa 2016, Ban amesema hofu zaidi ni kwamba ghasia zinaweza kuenea [...]

15/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa WFP yuko ziarani Zambia

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa WFP, Ertharin Cousin. Picha: WFP(UN News Centre)

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Ertharin Cousin, anafanya ziara ya kikazi nchini Zambia. Amewasili leo Alhamisi mjini Lusaka na atakuwepo nchini humo hadi Januari 17. Ziara yake imekuja wakati ambapo ukame na msimu wa eli Nino umeathiri pakubwa Kusini mwa Afrika hususani wakulima wadogowadogoambao ndio wazalishaji wakubwa katika eneo hilo. [...]

15/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mali amani iko karibu mbele yetu: MINUSMA

Kusikiliza / Walinda amani wa MINUSMA wakiwa na wakaazi nchini Mali.(Picha:MINUSMA)

Nchini Mali, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MINUSMA unashirikiana na jeshi la kitaifa liitwalo FAMA katika kurejesha hali ya usalama kaskazini mwa nchi na kupambana na waasi wa kigaidi, wakati ambapo serikali inaendelea kutekeleza mchakati wa amani. Kwenye makala hii Priscilla Lecomte anakupeleka kaskazini magharabi ambapo walinda amani wanaletea wananchi missada ikiwa ni moja ya [...]

15/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mawaziri wakutana Kenya kwa maandalizi ya baraza kuu la mazingira:UNEP

Kusikiliza / Mkutano wa mawaziri nchini Kenya.(Picha:UNEP)

Mawaziri wa mazingira kutoka kote duniani wanakutana Nairobi Kenya kwa ajili ya maandalizi ya baraza kuu la Umoja wa mataifa la mazingira UNEA kutathimini na kutoa taswira ya sera za kimataifa za mazingira. Wajumbe wamejadili uwezekano wa mada zitakazojadiliwa kwenye UNEA ,mkutano wa ngazi ya juu kabisa wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kufanya [...]

14/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WHO zataka kuzingirwa kwa raia Syria kusitishwe

Kusikiliza / Picha:WFP/Abeer Etefa

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, na Shirika la Afya Duniani, WHO, yametaka kuzingirwa kwa jamii na raia nchini Syria kusitishwe, wakati yakikaribisha kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu kwa jamii zilizozingirwa huko Madaya, Foua'a na Kafraya. Katika taarifa ya pamoja, UNICEF na WHO zimesema kuwa timu zao zilipozuru Madaya, zilikutana na watoto [...]

14/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazopokea wahamiaji ziwalinde dhidi ya ubaguzi:Ruteere

Kusikiliza / Wakimbizi na wahamiaji kutoka Syria wakisaka usafiri wa treni kwenye mpaka wa Serbia na Croatia. (Picha: © Francesco Malavolta/IOM 2015)

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina za kisasa za ubaguzi Mutuma Ruteere amesema nchi zinazopokea wahamiaji zihakikishe wanajumuishwa katika jamii wanakosaka hifadhi hususan wakati huu ambako kumeshuhudiwa wimbi kubwa la wahamiaji kuelekea barani Ulaya. Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa hii Bwana Ruteere amesema hatua hiyo ni muhmu kwani uwepo wao ugenini huenda [...]

14/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasiwasi waongezeka nchini DRC: MONUSCO

Kusikiliza / Mkuu wa MONUSCO, Maman Sidikou. Picha ya MONUSCO (flickr)

Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni changamoto kubwa ya mwaka 2016, amesema leo Maman Sidikou, Mwakalishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo, akihutubia Baraza la Usalama. Taarifa zaidi na Flora Nducha. (Taarifa ya Flora) Akiripoti kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa DRC, Kinshasa, Bwana [...]

14/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yaomba dola milioni 800 za usaidizi Syria na maeneo ya Palestina yaliyokaliwa

Kusikiliza / Picha:UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limetangaza ombi la changisho la dola milioni 817 ili kuwasaidia wakimbizi wa Syria walioko nchini Syria na maeneo ya Palestina yaliyokaliwa, wakati maeneo hayo yakiendelea kukumbwa athari za mzozo, kukaliwa na vizuizi. Wengi wa raia wa Palestina 450,000 walioko nchini Syria wamelazimika kuhama, na [...]

14/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwaka 2016 wapaswa kuwa mwaka wa utekelezaji: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban akihutubia Baraza Kuu. Picha:UN Photo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu New York, Marekani na kutangaza malengo yake kwa mwaka huu wa 2016. Katika hotuba yake ametaja mafanikio yaliyopatikana mwaka 2015, yakiwemo makubaliano kuhusu tabianchi, ajenda ya maendeleo ya 2030, makubaliano ya kisiasa kuhusu Iran, huku akitaka [...]

14/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maambukizi ya Ebola Liberia yameisha, nchi zote 3 sasa huru- WHO

Kusikiliza / Watoto nchini Liberia sasa ni matumaini. (Picha:Facebook UNMIL)

Shirika la Afya Duniani, WHO limetangaza kuwa Liberia sasa imeondolewa kwenye orodha ya nchi ambako maambukizi ya kirusi cha Ebola yanaendelea. Tangazo hili linakuja siku moja baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufanya kikao kuhusu Ebola, ambapo Katibu Mkuu Ban Ki-moon alipongeza juhudi za jamii ya kimataifa katika kupambana na homa hiyo. Kuhusu [...]

14/01/2016 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mfanyakazi wa UNEP ajeruhiwa katika mashambulio ya kigaidi Jakarta

Kusikiliza / Picha:UNEP

Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira (UNEP) amejeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika leo Alhamisi kwenye maeneo ya jirani na ofisi za Umoja wa Mataifa katikati ya mji wa Jakarta. Assumpta Massoi na Taarifa kamili. (Taarifa ya Assumpta) Mfanyakazi huyo raia wa Uholanzi ni mtaalamu wa masuala ya misitu na [...]

14/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za simu za kiganjani zimeenea kuliko maji na umeme: Ripoti

Kusikiliza / Picha:WorldBank

Huduma za simu za kiganjani au rununu zimesambaa zaidi duniani hivi sasa kuliko umeme au maji.Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu ya Benki ya duniani kuhusu Intaneti ikitanabaisha kuwa hali hiyo inatokana na kupanuka kwa wigo wa teknolojia ya digitali. Mchumi wa benki ya dunia Deepak Mishra amesema licha ya hali hiyo [...]

14/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watoto bado wanahitaji huduma na msaada baada ya Ebola:UNICEF

Kusikiliza / Mtoto aliepoteza familia yake kwa virusi vya Ebola. Picha:UN Photo / Martine Perret

Takribani watoto 23,000 children ambao walipoteza mzazi mmoja au wote, au walezi kutokana na Ebola nchini Guinea, Liberia na Sierra Leone wataendelea kuhitaji huduma na msaada limesema shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF , wakati likikaribisha tangazo la kutokuwepo visa vipya vya ugonjwa huo Afrika ya Magharibi. Kudhibiti Ebola ni mafanikio makubwa [...]

14/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ebola ilitoa mtihani mkubwa kwa nguvu na utashi wetu; tusilegee – Ban

Kusikiliza / Katika makazi yenye wakazi wengi huko Freetown, nchini Sierra Leone, Saidu Bah, mhamasishaji akielimisha jamii kuhusu Ebola. (Picha:UNMEER/Kingsley Ighobor)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema leo kuwa kuibuka kwa mlipuko wa homa ya Ebola katika nchi za Afrika Magharibi, ulikuwa mtihani mkubwa kwa nguvu na utashi wa pamoja, lakini jamii ya kimataifa iliongeza nguvu jitihada zake, na leo hii hali ni tofauti sana. Ban amesema hayo akilihutubia Baraza Kuu la Umoja [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matokeo ya uchaguzi wa wabunge yatangazwa CAR

Kusikiliza / Walinda amani wasaidia kusafirisha makaratasi ya kupiga kura nchini CAR. Picha ya MINUSCA/Nektarios Markogiannis

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, MINUSCA, umeripoti leo kuwa matokeo ya uchaguzi wa wabunge yametangazwa Jumanne hii na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi nchini humo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema kwamba tayari wagombea [...]

13/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kongamano lafanyika kuendeleza haki za binadamu katika nchi za Kiarabu

Kusikiliza / Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein.(Picha:UM/Violaine Martin)

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, ametoa wito kwa nchi za Kiarabu zijiunge hima kwa mikataba yote ya msingi kuhusu haki za binadamu, na kuhakikisha kuwa inafuatwa na kutekelezwa. Kamishna Zeid amesema hayo akishiriki katika kongamano la siku mbili kuhusu mchango wa Ofisi yake katika kuendeleza na [...]

13/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shambulio Pakistani laua watu 15, Ban alaani

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.(Picha:UM/Cia Pak)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio lililotokea leo kwenye kituo cha utoaji wa chanjo dhidi ya Polio nchini Pakistani. Shambulio hilo katika mji wa Quetta limesababisha vifo vya watu wapatao 15 huku wengine 25 wamejeruhiwa. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akituma salamu za rambirambi kwa familia za [...]

13/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Msaada wa wahisani waisaidia WFP kundelea na huduma za ndege Sudan

Mgao wa chakula kupitia usambazaji kwa anga

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha mchango mkubwa kutoka kwa wahisani uliosaidia operesheni zake za huduma za ndege za kibinadamu za Umoja wa Mataifa (UNHAS) nchini Sudan kwa mwaka 2015. Shirika hilo limesema michango hiyo iliyofika kwa wakati kutoka fuko la fedha la kibinadamu CHF, tume ya Ulaya ya [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya de Mistura na P5 Geneva kuhusu Syria yaweka nuru

Kusikiliza / Kikao kikiendelea cha de Mistura na P5. (Picha:UNTV/Video capture)

Mkutano kati ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria, Staffan de Mistura, na wawakilishi wa nchi tano zenye ujumbe wa  kudumu wa baraza la usalama P5, ni fursa ya kuwapatia taarifa za karibuni zaidi baada ya ziara  yake kwenye ukanda husika. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa Bwana de Mistura [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatimaye misaada ya chakula yawasili Madaya Syria

Kusikiliza / Shehena iliyobeba bidhaa muhimu yawasili Madaya nchini Syria.(Picha:UNIfeed/video capture)

Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu baina ya mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibinadamu dhidi ya pande kinzani nchini Syria kuhusu kuruhusu misaada ya kibinadamuk atika maneo yaliyozingirwa na vikosi vyenye sialaha, hatimaye eneo liitwalo Madaya limefikiwa. Hatua hii ya kutoa ahueni kwa raia ambao wamekuwa wakisubiri misaada ya chkual na bidhaa nyingine [...]

13/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP na kaunti ya Baringo Kenya kuimarisha uhakika wa chakula

Kusikiliza / Usambazaji wa chakula na WFP nchini Turkana,Kenya.(Picha:WFP/Andrew Macua & Geoffery Arasa)

Nchini Kenya shirika la mpango wa chakula duniani, WFP na serikali ya kaunti ya Baringo wamesaini makubaliano ya miaka miwili ya kuimarisha uwezo wa jamii kuhimili na kukabili njaa. Mwakilishi wa WFP nchini  humo Annalisa Conte amesema wamechukua hatua hiyo kwa kuzingatia kuwa chini ya mpango wa ugatuzi wa madaraka Kenya, serikali za mitaa zina [...]

13/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika kujadili fursa za mkataba wa COP21: Muyungi

Kusikiliza / Mkulima akimwagilia majani nchini Senegal. Picha ya UN/Carl Purcell

Mjumbe wa kamati ya wataalamu wa Afrika wanaowashauri marais kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, ambaye pia ni msimamizi wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania ,Richard Muyungi amesema nchi za Afrika zitakutana kuangalia fursa zilizopo baada ya mkataba wa COP21. Akihojiwa na Joseph Msami wa idhaa hii Bwana Muyungi amesema baada ya dunai kushuhudia makubaliano ya mkataba [...]

13/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa haki za binadamu wa UM kufanya ziara ya mwisho Japan

Kusikiliza / Marzuki Darusman.(Picha:UM/Devra Berkowitz)

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Jamuhuri ya watu wa Korea DPRK  Marzuki Darusman, atazuru Japan Januari 18 and 22 kutathimini maendeleo ya karibuni kuhusu DPRK na kujadili njia za kuhakikisha uwajibikaji wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini humo ukiwemo vitendo vya utekaji. Mtaalamu huyo huru ambaye muda wake [...]

13/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Afrika inatathimini matokeo ya mkataba wa COP21: Muyungi

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Ariane Rummery

Mjumbe wa kamati ya wataalamu wa Afrika wanaowashauri marais kuhusu mabadiliko ya tabianchi , Richard Muyungi amesema baada ya kupitishwa kwa makubaliano ya mabadiliko ya tabianchi bara la Afrika linafanya uchambuzi wa matokeo ya nini bara hilo limepata. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Bwana Muyungi amesema baada ya kukamlishwa kwa tahimini kamati hiyo itakutana [...]

13/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mindaoudou aliambia Baraza la Usalama Cote d'Ivoire bado inakabiliwa na changamoto nyingi

Kusikiliza / Aïchatou Mindaoudou akihutubia Baraza la Usalama. Picha:UN Photo/Manuel Elías

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limefanya kikao leo kuhusu hali nchini Cote d'Ivoire, ambapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini humo, Aïchatou Mindaoudou, ameliambia Baraza hilo kuwa nchi hiyo bado inakabiliwa na changamoto nyingi, licha ya ufanisi katika uchaguzi wa rais na kuboreka kwa hali ya usalama. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kushikamana na Kutegemeana ni kanuni za Ajenda ya 2030 : Eliasson

Kusikiliza / Jan Eliasson. Picha ya UN/Evan Schneider

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 ni ajenda ya karne ya 21 inayounganisha nchi zote kote duniani. Akihutubia kikao kilichofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekeni kuhusu maadili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu, amesema kanuni za malengo hayo [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Sekta ya ndege na meli zitozwe kodi za utoaji hewa ya ukaa:IMF

Kusikiliza / Picha:: UN Photo/PG

Shirika la fedha duniani, IMF limependekeza sekta ya usafiri wa anga na majini kuwekewa kodi ya utoaji wa hewa ya ukaa kama njia mojawapo ya kufikia malengo ya kimataifa ya kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Katika ripoti yake, IMF imekadiria kuwa iwapo dola 30 itatozwa kwa kila tani moja yah hewa ukaa kwenye sekta hizo itachangia [...]

13/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa wa elimu kama chachu ya SDG's wamalizika India:

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Mark Garten

Mkutano wa kimataifa wa siku tatu wa kutambua elimu kama mwezeshaji muhimu wa utambuzi mpana wa malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG's unamalizika leo mjini Ahmedabad nchini India. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ni muhimu kwa jamii kuangalia kila lengo la SGD na kubaini jinsi gani [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama latoa wito kuhusu mchakato wa amani Mali

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Loey Felipe

Wanachama wa Baraza la Usalama wamekaribisha hatua za awali zilizochukuliwa na serikali ya Mali katika utekelezaji wa makubaliano ya amani wakiisihi kuchukua harakati zinazotakiwa ili kuendeleza utaratibu wa amani pamoja na vyama vya upinzani na vikundi vilivyojihami. Miongoni mwa hatua zinazohitajika ni kuandaa doria za usalama za pamoja kaskazini mwa nchi, kutekeleza mpango wa kusalimisha [...]

13/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM kutathimini njia za kuwajumuisha katika jami walioachiliwa na Boko Haram:

Kusikiliza / Wanafunzi katika shule ya Maiduguri, Nigeria. Picha:IRIN/Obinna Anyadike(UN News Centre)

Watalaamu watatu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa watazuru Nigeria kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi huu ili kutathimini njia za kusaidia kuwajumuisha katika jamii wanawake na watoto waliotoroka au kuokolewa kutoka kwenye mikono ya kundi la Boko Haram. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA ) Kwa mujibu wa wataalamu hao [...]

13/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uenyekiti wa G-77 na China; Afrika ya Kusini yakabidhi kijiti kwa Thailand

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon.(Picha:UM/Cia Pak)

Matukio na maamuzi mengi ya kihistoria yaliyopitishwa mwaka 2015 hayangalikuwa na mafanikio bila ya ushirika thabiti wa kundi la nchi 77 na China. Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyotoa jijini New York, Marekani wakati wa makabidhiano ya uenyekiti wa kundi hilo kwa Thailand baada ya Afrika Kusini kuhitimisha muda [...]

12/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahitaji ya kibinadamu Syria yaongezeka kwa 2016, dola milioni 8 zahitajika

Kusikiliza / Filippo Grandi. Picha ya UN/Evan Schneider

Wakati vita nchini Syria vikielekea mwaka wa sita bila dalili ya ukomo wake, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu na maendeleo yametoa wito kwa nchi wanachama wa Umoja huo zichangie ombi la dola bilioni 7.73 zinazohitajika kufadhili utoaji misaada kwa watu milioni 22.5 nchini Syria, na katika ukanda mzima mwaka 2016. Ombi hilo la [...]

12/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kusomesha watoto wakimbizi wa Syria wapata milioni 250

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa Syria wakisoma shuleni nchini Lebanon. Picha kutoka UNIFEED / UNHCR Lebanon.

Mradi wa dharura wenye lengo la kusaidia watoto wakimbizi wa Syria milioni moja kurejea shuleni umepata ufadhili wa dola milioni 250, amesema leo Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu kwa Wote, Gordon Brown. Ameeleza kwamba ufadhili huo wa kwanza umeahidiwa na Muungano wa Ulaya na sekta ya kiserikali na binafsi kutoka nchi za [...]

12/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kusini Mashariki mwa Asia wahitimisha miaka mitano bila Polio: WHO

Kusikiliza / Usambazaji wa chanjo ya polio  nchini India.(Picha:WHO-SEARO/Anuradha Sarup)

Shirika la afya ulimwenguni WHO limetangaza kuwa ukanda wa kusini mashariki mwa Asia umehitimisha miaka mitano bila kisa chochote cha polio na kusema ni hatua muhimu wakati huu ambapo ugonjwa huo unasalai tishio katika nchi nyingine. Taarifa ya WHO inasema kuwa nchi katika ukanda huo zimepiga hatua kubwa za kishujaa katika kuwalinda watoto dhidi ya [...]

12/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM alaani mashambulizi ya bomu misikitini Iraq

Kusikiliza / Shambulio la bomu nchini Iraq. Picha kutoka maktaba ya IRIN.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Iraq Ján Kubiš, amelaani mashambulizi ya mabomu dhidi ya misikiti sita kwenye eneo la Muqdadiya jimbo la Diyala nchini Iraq. Amesema kwa mara nyingine maeneo ya ibada yanashambuliwa, na waliotekeleza wanataka kuchochea ghasia za kidini wakiwa na hamasa ya kutaka kuirejesha nchi katika siku za [...]

12/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mswada wa ufuatiliaji Uingereza watishia uhuru wa kijieleza: UM

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Haki za Binadamu. Picha: Umoja wa Mataifa/ Jean-Marc Ferré

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wameonya kuwa muswada wa ufuatiliaji nchini Uingereza, unatishia uhuru wa kujieleza na kujumuika ndani na nje ya nchi hiyo. Katika taarifa yao wataalamu hao David Kaye anayehusika na uhuru wa kujieleza, Maina Kiai wa uhuru wa kukusanyika na kujumuika na Michel Forst anayehusika na watetezi wa [...]

12/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya UNICEF yatoa mwanga kwa watoto walioacha shule Sudan Kusini

Kusikiliza / Mtoto Nyayow na kakake ambao wampeta fursa kurudi shule.(Picha/UNICEF/Video capture)

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, imebainisha kuwa takriban watoto milioni 24 katika maeneo ya mizozo hawaendi shule. Nchini Sudan Kusini, mzozo uliopo sasa umeifanya hali iliyo mbaya tayari kuwa janga kwa watoto. Watoto 413,000 zaidi wamelazimika kuacha shule. Lakini kuna matumaini. Kupitia kampeni ya kurejesha watoto shuleni [...]

12/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Papa Francis kukutana kwa faragha na mwakilishi wa UM wa usalama barabarani

Kusikiliza / Usalama barabarani(Picha:Benk ya dunia)

Papa Francis atampokea na kukutana naye kwa faragha alhamisi wiki hii mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu usalama barabarani, Jean Todt, atakayeambatana na Christian Friis Bach, katibu mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi kwa Ulaya. Viongozi hao watajadili haja ya kuongeza usalama barabarani duniani kote ili kuokoa maisha [...]

12/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa Kibinadamu Libya alaani shambulizi dhidi ya mtambo wa umeme Benghazi

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Iason Foounten

Naibu Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu ambaye pia ni Mratibu Mkaazi wa masuala ya kibinadamu na Umoja wa Mataifa nchini Libya, Ali Al-Za'tari, amelaani vikali shambulizi la hivi karibuni dhidi ya mtambo wa kuzalisha umeme mjini Benghazi. Al-Za'tari ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu inayoendelea kuzorota nchini Libya, akiongeza kuwa mashambulizi kama hayo yanaongeza [...]

12/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauaji ya wanahabari wa Al-Sharqiya, Iraq

Kusikiliza / Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNAMA, Ján Kubiš

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Iraq, Ján Kubiš, amelaani vikali mauaji ya wanahabari wawili wa televisheni ya Al-Sharqiya, katika mkoa wa Diyala nchini Iraq. Bwana Kubiš amesema mauaji ya Saif Talal na Hassan Al-Anbaki wakiwa wanafanya kazi yao ya kutoa habari kuhusu matukio ya Diyala ni kitendo cha uovu na uoga kilichotekelezwa na watu [...]

12/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia baada ya meli kuzama pwani ya Somaliland

Kusikiliza / Harakati za IOM kuokoa wahamiaji waliokuwa wanaelekea Italia.(Picha:IOM/Francesco Malavolta)

Wahamiaji 36 wamekufa maji wakati meli iliyokuwa imebeba wahamiaji 106 , wasomali na Waethiopia  kuzama pwani ya jimbo lililojitenga la Somaliland kaskazini mwa Somalia siku ya Ijumaa, limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. IOM, ikishirikiana na kitengo cha usaidizi kwa wahamiaji Somaliland (MRC) wanausaidia uongozi wa Somaliland kwa kugawa chakula, maji na madawa kwa [...]

12/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

DRC: watu milioni 7.5 wahitaji usaidizi wa kibinadamu

Kusikiliza / Usambazaji wa chakula nchini DRC. Picha ya OCHA DRC (akaunti ya Twitter)

Watu milioni 7.5 wanahitaji usaidizi wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wakiwa ni takriban asilimia 9 ya idadi ya watu wote nchini humo. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa hivi karibuni na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA nchini humo, kuhusu mpango wa misaada ya kibinadamu [...]

12/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani vikali shambulio la bomu Uturuki lililoua 10

Kusikiliza / Nassir Abdulaziz Al-Nasser.(Picha:UM/Devra Berkowitz)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amealaani shambulio la kigaidi alilooliita  la kupuuzwa huko Sultanahmet nchini Uturuki lililosababisha vifo vya watu 10 na kujerhi takribani 15. Taarifa ya Katibu Mkuu kupitia ofisi ya msemaji wake inasema kuwa Bwana Ban anatarajia kuwa  watakelezaji wa shambulio hilo watafikishwa katika vyombo vya sheria huku akituma rambirambi [...]

12/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mahitaji muhimu yafikia walionaswa kwenye mapigano Madaya, Syria

Kusikiliza / Msafara wa magari yaliyowasili Madaya Syria. Picha ya OCHA Syria (akaunti ya Twitter).

Nchini Syria, hatimaye msafara wa magari yaliyobeba bidhaa muhimu za kuokoa maisha ya watu wanaokumbwa na njaa umewasili kwenye mji wa Madaya nchini humo. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia. (Taarifa ya Grace) Shehena ni pamoja na vifaa vya tiba, vyakula na mablanketi kutoka Umoja wa Mataifa na washirika wake na lengo ni kufikia wakazi 42,000 [...]

12/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya wahamiaji kuongezeka kwa kasi, wana mchango mkubwa kiuchumi: DESA

Kusikiliza / Takwimu za wahamiaji wa Kimataifa 2015

Ripoti ya mwaka kuhusu wahamiaji iliyotolewa leo na idara ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA, inaonyesha kuwa kasi ya ongezeko la wahamiaji kimataifa ni kubwa kuliko kasi ya ongezeko la idadi ya watu duniani. Flora Nducha na maelezo  kamili. (Taarifa ya Flora) Akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa Mkuu [...]

12/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nepal: Ujumbe wa akiolojia wa UNESCO kuanzisha mbinu kukabili athari baada ya maafa

Kusikiliza / Tetemeko hilo limesababibisha athari nyingi(Picha:Laxmi Prasad Ngakhusi/ UNDP Nepal.)

Tetemeko la ardhi la 2015 nchini Nepal halikuwa tu zahma kubwa kwa binadamu bali pia lilisababisha athari kubwa kwa utamaduni nchini humo likiharibu urithi wa kipekee wa nchi hiyo. Urithi huo ambao una nafasi kubwa katika maisha ya watu na chanzo kikuu cha pato la utalii utajengwa upya mwa mujibu wa shirika la Umoja wa [...]

12/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya watoto Yemen si shwari:UNICEF

Kusikiliza / Picha ya UNICEF Yemen.

Wakati hamna dalili yoyote ya kukomesha vita nchini Yemen, takriban watoto milioni 10 ndani ya nchi hiyo wametangulia mwaka mpya katika machungu na mateso, limesema Shirika la Umoja wa Matifa la Kuhudumia watoto, UNICEF. John Kibego na taarifa zaidi. (Taarifa ya Kibego)  Mwakilishi wa UNICEF huko Yemen Julien Harneis, amesema, mashambulio ya mabomu yasiokoma na [...]

12/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji zaidi ya 18,000 wamevuka kusaka hifadhi Ulaya kwa siku 11:IOM

Boti bahari ya mediteranea ikiwa imebeba watu kutoka nchi mbali mbali wanaoelekea Ulaya (Picha ya UNHCR/A. D'Amato (2014)

Shirika la kimataifa la uhamaiaji IOM linasema zaidi ya wahamaiji 1,700 huvuka kila siku kwa kutumia bahari kusaka hifadhi barani Ulaya,  takwimu hizi zikiwa ni za siku 11 za mwanzo wa mwaka 2016. Idadi hii imefanya wahamiaji kufikia kiasi cha zaidi ya elfu kumi na nane hadi sasa. Mmoja wa wafanyakazi wa IOM mjini Roma [...]

12/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 31 kusaidia wahitaji huko ziwa Chad

Kusikiliza / Wakimbizi wa Chad. Picha ya OCHA

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa kibinadamu, OCHA Stephen O'Brien ameidhinisha dola Milioni 31 kwa ajili ya kusaidia mashirika ya kibinadamu yanayotoa misaada huko Nigeria na ukanda wa ziwa Chad. Fedha hizo zinatoka mfuko wa dharura ya majanga wa Umoja wa Mataifa, CERF na unalenga kukabiliana na hali ya kibinadamu [...]

12/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yaongoza kwa kuwa na watoto wasiokwenda shule:UNICEF

Kusikiliza / Mmoja wa watoto akijifunza licha ya mazingira magumu huko Sudan Kusini. (Picha:© UNICEF/UNI169063/Nesbitt)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema watoto takribani Milioni 24 walio katika nchi 22 zenye mizozo hawako shuleni. Katika taarifa yake ya leo, UNICEF imesema Sudan Kusini ndiyo yenye idadi kubwa zaidi ambako zaidi ya nusu ya watoto wenye umri wa kuwa shule za msingi na sekondari hawako shuleni. Nchi ya [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyumba 1,000 za wakimbizi zateketezwa kwa moto Sudan Kusini

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini.Picha ya UM/JC Mcllwaine

Kambi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS inayowapa hifadhi raia 48,000 tangu Disemba 2013 kwenye eneo la Malakal imeteketezwa kwa moto, amesema leo msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani. Bwana Dujarric amesema moto huo ambao ulianza jumapili umeshadhibitiwa baada ya kusababisha [...]

11/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mahitaji muhimu yafikia walionasa kwenye mapigano Madaya, Syria

Kusikiliza / Shehena ya vifaa vya misaada vilivyowasili Madaya, Syria. (Picha:UNifeed/Videocapture)

Hatimaye msafara wa magari yaliyobeba shehena za bidhaa muhimu za kuokoa uhai wa binadamu walio kwenye maeneo yaliyoshikiliwa huko Syria, umewasili kwenye mji wa Madaya nchini humo. Shehena ni pamoja na vifaa tiba, vyakula na mablanketi kutoka Umoja wa Mataifa na washirika wake na lengo ni kufikia wakazi 42,000 ambao wameripotiwa kukumbwa na njaa kutokana [...]

11/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mchakato wa amani Mali bado ni dhaifu: Baraza la Usalama

Kusikiliza / Herves Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa. Picha: UN Photo/Loey Felipe

Leo Baraza la Usalama limejadili hali ya usalama na kibinadamu nchini Mali pamoja na kufuatilia operesheni za ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSMA. Akihutubia kikao hicho, mkuu wa idara ya Umoja wa Mataifa ya operesheni za kulinda amani, Hervé Ladsous amesisitiza umuhimu wa kutekeleza maazimio ya makubaliano ya amani, akisema utekelezaji wake ukizidi [...]

11/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Miaka 6 baada ya tetemeko la ardhi Haiti, changamoto bado nyingi

Kusikiliza / Ukarabati baadaya tetemeko la ardhi Haiti mwaka 2010. Picha ya UN/Marco Dormino

Kuelekea miaka sita tangu kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi lililoua zaidi ya watu 200,000 nchini Haiti tarehe 12, Januari, 2010, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameeleza mshikamano wake na familia za wahanga. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amemnukuu Katibu Mkuu [...]

11/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

PASADA yaleta nuru kwa mtoto Halima anayeishi na VVU

Kusikiliza / Halima akimhudumia mteja wake wakati wa mafunzo ya kutengeneza nywele anayopata kupitia usaidizi wa PASADA. (Picha:UNICEF/Videocapture)

Harakati za kupambana na Ukimwi zinashika kasi duniani kila uchao. Miongoni mwa harakati hizo ni kuhakikisha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wanapatiwa dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo. Mathalani hadi Juni 2015 idadi ya wanaopatiwa dawa hizo walikuwa zaidi ya Milioni 15 na laki Nane ikiwa ni nyongeza kutoka Milioni 13 na Nusu [...]

11/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yahimiza utulivu kufuatia hali tete Darfur Magharibi

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani kwenye eneo la El-Geneina, Darfur Magharibi. Picha ya UNAMID/Albert Gonzalez Farran

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur, UNAMID, umeeleza kutiwa hofu na hali tete inayoendelea katika mji wa El Geneina na karibu na kijiji cha Mouli, yapata kilomita 15 kutoka El Geneina, Darfur Magharibi. Kwa mantiki hiyo, UNAMID imetoa kwa mamlaka za serikali kufanya juhudi zote kuidhibiti hali. Taarifa ya [...]

11/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkuu mpya wa UNAMID awasili Darfur kuanza kazi rasmi:

Kusikiliza / Jumbe Omari Jumbe, Radio UNAMID. Picha:UN Photo/Jean-Marc Ferré

Mkuu mpya wa vikosi vya pamoja vya Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika vya kulinda Amani Darfur UNAMID , Martin Uhomoibhi amewasili Darfur Sudan kuanza rasmi majukumu yake. Bwana Uhomoibhi amesema , Muungano wa Afrika na Umoja wa Mataifa wana nia njema kabisa ya kusaidia pande kinzani kawenye mgogoro wa Dafur kufikia suluhu kwa [...]

11/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Watoto wanaokimbia Yemen bila walezi watafuta usalama Somaliland

Kusikiliza / Mtoto mkimbizi kutoka Yemen akiwa katika chumba cha uhifadhi nchini Somaliland.(Picha:UNHCR/O.Khelifi)

Zaidi ya watoto 9,500 kutoka Yemen wamekimbia machafuko nchini humo na kutafuta usalama katika jimbo huru la Somaliland nchini Somalia, wakiwa peke yao bila wazazi au walezi, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR. UNHCR imesema watoto hao ni miongoni mwa zaidi ya watoto 168,000 ambao wamekimbia machafuko nchini Yemen [...]

11/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uchumi Afrika kuendelea kukua 2016 , lakini changamoto bado zipo:

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Eskinder Debebe

Ukuaji wa uchumi barani Afrika unatarajiwa kupanda na kufikia asilimia 4.2 mwaka 2016 baada ya mambo kutokuwa mazuri sa na mwaka uliopita. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya matazamo wa uchumi wa duniani iliyochapishwa na benki ya dunia mwezi huu ,ambayo pia inasema kwa ujumla uchumi unatarajiwa kukua kote duniani chini ya asilimia 3. [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vituo vya afya ni mwarobaini wa Fistula: UNFPA Tanzania

Kusikiliza / Agnes Maratho akisaidiwa na mamake baada ya kufanyiwa upasauji wa fistula katika hospitali ya rufaa ya Hoima, Uganda.(Picha ya Idhaa ya kiswahili/John Kibego)

Uwepo wa vituo vya afya ni  moja ya mikakati ya kukabiliana na ugonjwa wa Fistula unaowapata wanawakwe baada ya kujifungua amesema Naibu Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA nchini Tanzania Rutasha Fulgence. Katika mahojiano na idhaa hii kuhusu namna shirika hilo na wadau wanavyoendeleza mapambano dhidi ya Fistula Bwana [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu mpya wa UNAMID Martin Uhomoibhi awasili Dafur:

Kusikiliza / Hafla ya kumkaribisha Dr Martin Uhomoibhi, Mkuu mpya wa UNAMID. Picha:UNAMID

Mkuu mpya wa vikosi vya pamoja vya vya kulinda Amani Dafur vya Umoja wa mataifa na Muungano wa Afrika, UNAMID amewasili El Fashar, Kaskazini mwa Dafur Jumatatu kuanza rasmi majukumu yake. Amina Hassan na taarifa kamili. (TAARIFA TA AMINA) ACTUALITY: FANFARE, PARADE…. Hivyo ndivyo alivyopokelewa Dr. Martin Uhomoibhi (Pron:Umwobi) raia wa Nigeria anayechukua nafasi ya [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa kukodisha baiskeli New York wafikia Milioni 10 mwaka jana

Kusikiliza / Uendeshaji wa baiskeli jijini New York. (Picha:tovuti ya Climateaction)

Mpango wa utekelezaji wa hatua kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ClimateAction unaofanya kazi kwa ubia na shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP umezungumzia mafanikio ya mtandao wa kukodisha baiskeli kwenye jiji la New York, nchini Marekani. Mtandao huo umemnukuu Meya wa New York, Bill de Blasio akisema kuwa kwa mwaka jana pekee mtandao huo [...]

11/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ubelgiji imechangia Euro milioni 2.45 kusaidia wakimbizi wa Palestina:UNRWA

Kusikiliza / Picha:UNRWA/ Alaa Ghosheh

Serikali ya Ubeligiji imetoa mchango wa Euro milioni 2.45 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA ikiunga mkono shughuli za shirika hilo katika kutoa huduma kwa wakimbizi kwenye maeneo yanayokaliwa ya Wapalestina. Mchango huo utagawanywa baina ya mradi wa UNRWA wa kusaidia makazi kwenye Ukanda wa Gaza na mpango wa [...]

11/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa laadhimisha miaka 70

Kusikiliza / Mkutano wa kwanza wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjini London, Uingereza. Picha ya UN/Marcel Bolomey

Leo ikiwa ni miaka 70 tangu kufanyika kwa mara ya kwanza kwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Baraza hilo limekuwa jukwaa la watu wote. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia. (Taarifa ya Grace) Nats… Huu ulikuwa ni ufunguzi wa mkutano wa kwanza wa Baraza [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki, UN 70, UN@70, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

UM na Ulaya waitaka Marekani ifunge gereza la Guantánamo

Kusikiliza / Miongoni mwa wataalamu Ben Emmerson anayehusika na uhuru wa mahakama.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Kundi la wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na Ulaya wameitaka Marekani ikomeshe ukwepaji sheria katika usimamizi wa haki za binadamu na ifunge gereza la Guantanamo.Taarifa kamili na John Kibego. (Taarifa ya Kibego) Wataalamu hao kupitia barua yao ya wazi wamesema Marekani kwa kutumia gereza hilo lililoanza kushikiliwa wafungwa miaka 14 iliyopita, [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulio dhidi ya hospitali huko Yemen

Kusikiliza / Mashambulizi yanakwamisha huduma za jamii Yemen, mathalani pichani ni foleni kwa ajili ya  kununua mikate. Picha ya UNDP/Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio dhidi ya hospitali inayoendeshwa na madaktari wasio na mipaka, MSF huko jimbo la Sa'ada nchini Yemen ambalo limesababisha vifo vya watu wanne. Mpaka sasa bado haijafahamika ni nani aliyefanya shambulio hilo la Jumapili ambalo pia limesababisha majeruhi kadhaa. Ban kupitia taarifa ya msemaji wake ametuma [...]

11/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa dola milioni 7 kwa misaada ya kibinadamu eneo la Ziwa Chad

Kusikiliza / Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA Stephen O'Brien.(Picha:UM/UNifeed/video capture)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa,  Stephen O'Brien, ameidhinisha utoaji wa dola milioni saba za Kimarekani kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Dharura, CERF, kwa minajili ya kutoa usaidizi wa kibinadamu katika eneo la Ziwa Chad. Kuendelea kwa machafuko na athari za kiuchumi na kijamii kutokana na hali mbaya [...]

08/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya kwa wazee Afrika Mashariki

Kusikiliza / Wazee wakisaka huduma ya afya nchini Tanzania.(Picha/Idhaa ya kiswahili/Tumaini Anatory)

Uzee hutizamwa na jamii kama kipindi kigumu kilichojawa na kadhia nyingi. Moja ya kadhia inayokumba kundi hili ni  upatikanaji wa huduma za kijamii mathalani afya. Malengo mapya ya maendeleo endelevu SDGS yaliyoridhiwa na nchi wanachama hivi karibuni yanaanisha nafasi ya wazee katika kupatiwa huduma ya afya na kuangalia ustawi wao kwa ujumla. Lengo namba tatu [...]

08/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Dansi ya asili ya kiarabu yatambuliwa na UNESCO kama urithi wa dunia

Kusikiliza / Wasichana wadogo pia hucheza kwenye hafla za al-razfa. Picha ya Mamlaka za Utalii na Utamaduni za Abu Dhabi/2008

Urithi wa dunia ni maeneo, majengo au mila zenye thamani kubwa ya kitamaduni au kimazingira duniani. Ni hazina inayotunzwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ambalo huorodhesha sehemu na mila hizo na kuhakikisha zinatunzwa ipasavyo. Mwezi Disemba mwaka 2015, UNESCO imeingiza sehemu 20 mpya katika orodha ya Urithi wa [...]

08/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

CAR: kikosi cha walinda amani cha DRC charudishwa kwao

Kusikiliza / Kikosi cha walinda amani wa DRC nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Aprili 2015. Picha ya MINUSCA/Dany Balepe

Kikosi cha walinda amani kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC kilichokuwa kimetumwa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenye Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSCA kitarudishwa DRC. Hii ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric ambaye amezungumza leo na waandishi wa habari mjini New York Marekani, akieleza kwamba maamuzi [...]

08/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ahofia mashambulizi ya anga na mapigano Yemen

Kusikiliza / Picha ya UNICEF MENA

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amesema anatiwa hofu na ongezeko la mashambulizi ya pamoja ya anga , mapigano ya ardhini na uvurumishaji wa makombora nchini Yemen, licha ya wito uliotolewa mara kadhaa wa kusitisha mapigano. Ban amesema hofu yake kubwa ni hususan mashambuzi ya anga kwenye maeneo ya amakazi ya watu na [...]

08/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO alaani mauaji ya Ruqia Hassan mwandishi habari wa Syria

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa UNESCO, Irina Bokova. Picha:UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO bi Irina Bokova, ameelezea hasira yake kufuatia taarifa za kuthibitisha mauaji ya mwandishi habari wa Syria Ruqia Hassan. Amesema analaani vikali mauaji hayo na kupongeza ujasiri wa mwandishi huyo aliyesimamia haki za binadamu na uhuru mwingine katika mazingira magumu na kupuuzia [...]

08/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi ya kigaidi Libya

Kusikiliza / Watoto wakibembea katika eneo la Zawiya, Libya. Picha:UN Photo/Iason Foounten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  amelaani shambulio la kigaidi nchini Libya lilolenga kituo cha polisi mjini Zliten magaharibi mwa nchi. Taariaf iliyotolewa na msemaji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Ban ameelezea rambirambi zake kwa familia za waliopoteza maisha au kujeruhiwa na kwa watu wa Libya. Katibu Mkuu pia amelaani mashambulizi  yanayoendelea kutekelezwa [...]

08/01/2016 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aipongeza Sri Lanka kwa mwaka mmoja wa kipindi cha mpito

Kusikiliza / Msichana nchini Sri Lanka.(Picha:UM/Evan Schneider)

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon amempongeza Rais wa Sri Lanka, Maithripala Sirisena, serikali na watu wa nchi hiyo kwa kutimiza mwaka mmoja wa serikali ya mpito wa kisiasa. Ban ametiwa moyo na serikali kujidhatiti katika ajenda ya mabadiliko  ambayo yana lengo la kuhakikisha amani ya kudumu , utulivu na mafanikio kwa watu [...]

08/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO na FARDC kushirikiana Kivu Kaskazini: UM wasema ni hatua nzuri

Kusikiliza / Mjini Bunanga nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo< DRC(Picha ya Clara Padovan)

Jeshi la kitaifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC limetangaza leo kutuma askari zaidi Kivu Kaskazini ili kupambana na waasi wa FDLR kwa kushirikiana na vikosi vya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO. Tangazo hilo lililotolewa na redio ya Umoja wa Mataifa Radio OKAPI linafuatia mashambulizi yaliyotokea Alhamisi kwenye kijiji cha Miriki, [...]

08/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waliozama Mediteranea wiki moja ya mwaka huu yatisha:IOM

Kusikiliza / Wahamiaji waliookolewa katika pwani ya Italia wakisubiri kusafirishwa.(Picha ya UNHCR)

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limesema wiki moja tangu kuanza kwa mwaka mpya wa 2016, idadi ya wahamiaji au wakimbizi waliofariki dunia au kupotea kwenye bahari ya Mediteranea imefikia 46, wengi wao wakikumbwa na zahma hiyo kwenye meli pwani ya Uturuki siku ya Jumanne. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi na waandishi wa habari msemaji wa [...]

08/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chanjo dhidi ya Kipindupindu sasa maradufu

Kusikiliza / Chanjo. (Picha: MAKTABA:UN/JC McIlwaine)

Utolewaji wa chanjo ya kipindupindu kimataifa utaongezeka mara mbili baada ya shirika la afya ulimwenguni WHO kumtihibitisha mzalishaji wa tatu wa chanjo atakayesaidia katika upungufu na upatikanaji katika nchi nyingi . WHO imesema kampuni hiyo ya Korea Kusini OCV imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba  madawa na chanjo kutoka nchi mbalimbali na wakala wa kimataifa wa [...]

08/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yapongeza walioiwezesha kusaidia watu milioni moja Uganda 2015

Kusikiliza / Watoto wanaopokea mgao wa chakula nchini Uganda.(Picha ya WFP)

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), nchini Uganda limepongeza mataifa yaliyotoa msaada ulioliwezesha kusaidia takribani watu miolioni moja nchini humo kupata chakula mnamo mwaka wa 2015. Taarifa kamili na John Kibego. (Taarifa ya John Kibego) Katika taarifa yake WFP imesema, idadi ya waliofaidi kwa msaada wake iliongezeka kwa watu laki mbili ikilinganishwa na mwaka [...]

08/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani kutimuliwa afisa wa haki za binadamu Yemen, Zeid ataka uamuazi ubadilishwe:

Kusikiliza / Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein.(Picha:UM/Violaine Martin)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na Kasmishina Mkuu wa haki za Binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein wamesema kitendo cha serikali ya Yemen kumtimua mwakilishi wa haki za binadamu wa Umoja wa mataifa nchini Yemen hakistahili, ban akilaani vikali huku Zeid akitaka uamuzi huo ubadilishwe. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA [...]

08/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi CAR

Kusikiliza / Picha ya MINUSCA

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR Parfait Onanga-Anyanga amekaribisha tangazo la matokeo ya Uchaguzi wa rais na wabunge yaliyotangazwa leo nchini humo. Taarifa iliyotolewa leo na idara ya operesheni za kulinda amani ya Umoja wa Mataifa, imesema kwamba bwana Onanga-Anyanga amepongeza wagombea Anicet Georges Dologuélé na [...]

07/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

DR Congo yaorodhesha wakimbizi 6,000 toka Sudan Kusini:

Kusikiliza / Picha:UNHCR

Takribani wakimbizi 6000 wamewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakitokea majimbo ya Equatoria Sudan Kusini. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR watu hao ambao pia wanajumuisha raia wa Congo wanaongia kwenye eneo la Dungu na walianza kukimbia mwezi Desemba kama anavyothibitisha, Teresa Orango afisa habari wa Kanda [...]

07/01/2016 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Urusi na India wametangaza ushirika kufikia malengo ya nishati mbadala:UNEP

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Pasqual Gorriz

Kampuni ya uzalishaji wa nishati ya jua yaani sola ya India (SECI) na ile ya Urusi (REA) wametia saini makubaliano ya kuanzisha mradi mkubwa wa nishati ya jua nchini India kuanzia mwaka huu wa 2016 hadi mwaka 2022. Mradi wa majaribio wa megawati 500 utaanza kwanza kama sehemu ya makubaliano. Makampuni hayo mawili yameafikiana njia [...]

07/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakazi wa vijijini Kenya kunufaika na mitambo midogo ya nishati

Kusikiliza / Kenya2

Kampuni ya Powerhive nchini Kenya inayohusika na kuzalisha nishati salama imeingia makubaliano na kampuni ya Enel Green ya italia ili kuweka mitambo ya kusambaza nishati ya umeme kwenye maeneo ya vijijini nchini Kenya. Kwa mujibu tovuti ya Climate Action inayofanya kazi kwa ubia na shirika la  mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, mitambo hiyo ya [...]

07/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kobler alaani mashambulizi ya kigaidi Libya

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Iason Foounten

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Martin Kobler amelaani vikali mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea leo dhidi ya kituo cha mafunzo ya usalama mjini Zliten. Bwana Kobler ambaye pia ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNSMIL ameeleza kushtushwa sana na shambulio hilo. Ametuma salamu zake za rambirambi [...]

07/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

China kufunga machimbo ya makaa ya mawe kudhibiti uchafuzi wa hewa

Kusikiliza / Mandhari ya mji mkuu wa China, Beijing. (Picha:Climateactionprograme/bit.ly/22Nc1co)

Mamlaka ya taifa ya nishati nchini China, NEA haitoidhinisha machimbo mapya ya makaa ya mawe nchini humo ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo, ikiwa ni  hatua za kudhibiti utoaji wa gesi chafuzi. Katika taarifa iliyotolewa leo, mamlaka hiyo imesema pamoja na  hatua hizo,  machimbo mengine zaidi ya 1,000 yanayofanya kazi sasa yatafungwa ifikapo mwishoni [...]

07/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wa UNAMID waviziwa, wapokonywa silaha

Kusikiliza / Doria ya UNAMID, Darfur. Picha ya Albert González Farran, UNAMID

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID, umesema kuwa msafara wake wa walinda amani umeviziwa leo na kikundi chenye silaha kisichojulikana, ambapo mlinda amani mmoja amejeruhiwa na silaha kupokonywa. Tukio hilo limetokea karibu na eneo la Anka, Darfur Kaskazini, mwendo wa takriban kilomita 55 kaskazini mwa mji wa [...]

07/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula zimeshuka kwa mwezi Disemba:FAO

Kusikiliza / Picha:FAO

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema bei za bidhaa za chakula zimeshuka kwa mwaka wa nne mfululizo mwaka jana kwa wastani wa asilimia 19.1 kutokana na kuyumba kwa uchumi kimataifa hali ambayo imechangia pia kushuka kwa bei za chuma na soko la  nishati duniani. Kwa mujibu wa FAO miongoni mwa bidhaa zilizoathirika zaidi na [...]

07/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

CTBTO yakutana Vienna kufuatia jaribio la nyuklia DPRK

Kusikiliza / DPRK

Kamati ya kuchukua hatua ya nchi wanachama wa Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya Silaha za Nyuklia, CTBTO, imekutana leo mjini Vienna, siku moja baada ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK kufanya jaribio la silaha za nyuklia, ambalo ilidai kuwa jaribio la bomu la haidrojeni. Taarifa kamili na Grace Kaneiya [...]

07/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Filippo Grandi aeleza dira yake kwa UNHCR

Kusikiliza / Filippo Grandi, mkuu wa UNHCR. Picha ya UNHCR/S. Hopper

Kamishna Mkuu Mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi amezungumza leo kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi akieleza mipango anayotaka kutekeleza katika muda wake ili kukabiliana na swala la wakimbizi linalozidi kuongezeka huku idadi yao ikiwa imefika milioni 60. Mathalani amesisitiza umuhimu wa kutekeleza [...]

07/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukuaji uchumi duniani kudhoofika, lakini hali shwari: Ripoti

Kusikiliza / Mchumi mkuu  kwenye Benki ya Dunia, Kaushik Basu. Picha:WorldBank

Ukuaji dhaifu wa uchumi katika nchi zinazoibuka kiuchumi utakuwa na madhara katika ukuaji wa uchumi duniani kwa mwaka huu wa 2016. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwezi huu ya Benki ya dunia kuhusu matarajio ya uchumi duniani. Hata hivyo ripoti imesema licha ya hali hiyo, kasi ya ukuaji uchumi duniani itaongezeka na kuwa [...]

07/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

DR Congo yaorodhesha wakimbizi 6,000 toka Sudan Kusini:

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini, kwenye kambi ya Malakal, Picha ya Umoja wa Mataifa/Isaac Billy

Takribani wakimbizi 6,000 wamewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wakitokea majimbo ya Equatoria Sudan Kusini. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR watu hao ambao pia wanajumuisha raia wa Congo wanaongia kwenye eneo la Dungu na walianza kukimbia mwezi Disemba .Nini kilichowachagiza kufungasha virago vyao , Teresa Orango [...]

07/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misaada yapaswa kuwafikia walengwa Syria hima:UM

Kusikiliza / Familia hii ya wakimbizi wa Syria inaishi barabarani nchini Uturuki. Picha ya UNHCR/S. Baldwin

Umoja wa Mataifa umetaka umetoa wito wa kuondolewa vikwazo vya kufikisha misaada kwa takribani watu laki nne wanaozingirwa na makundi kinzani ya machafuko nchini Syria. Kwa mujibu wa mwakilishi mkazi wa ofisi ya UM ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA nchini humo Yacoub El Hillo, wito huo unafuatia mwitikio kidogo wa makundi kinzani ambapo mwaka [...]

07/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yataka iwezeshwe kufika haraka Taiz ili kutoa misaada ya dharura

Kusikiliza / Uwasilishaji wa misaada ya kiafya nchini Yemen.(Picha ya WHO/Yemen/facebook)

Shirika la afya duniani, WHO limeelezea wasiwasi juu ya kuzidi kuzorota kwa hali ya kiafya kwenye mji wa Taiz nchini Yemen ambako zaidi ya watu 250,000 wanaishi huku wamezingirwa na vikundi vinavyopigana  tangu mwezi Novemba mwaka jana. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Katika taarifa yake WHO imesema hali si shwari kwani hospitali [...]

07/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sigrid Kaag akutana na waziri mkuu wa Lebanon

Kusikiliza / Sigrid Kaag akikutana na wakimbizi wa Syria nchini Lebanon. Picha ya UN/maktaba

Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya Lebanon Bi Sigrid Kaag leo Alhamisi amekutana na waziri mkuu wa Lebanon Tammam Salam aliporejea kutoka Saudi Arabia kwenye  ziara ya kikazi. Bi Kaag amempa taarifa waziri mkuu huyo kuhusu mkutano wake na waziri wa mambo ya nje wa Saudia Adel Al-Jubeir na maafisa wengine wa [...]

07/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UM nchini CAR azungumza na wagombea urais

Kusikiliza / Parfait ONanga-Anyanga akizungumza na wagombea urais wa CAR. Picha ya MINUSCA.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR Parfait Onanga-Anyanga amekutana leo na wagombea urais 28 miongoni mwa 30 waliogombea katika uchaguzi uliofanyika tarehe 30, Disemba, mwaka 2015. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric aliyezungumza na waandishi wa habari leo [...]

06/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Naondoka Mali nikiwa na matumaini; Hamdi

Kusikiliza / Mongi Hamdi. Picha ya UN/Devra Berkowitz

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, Mongi Hamdi amesema anaondoka Mali na moyo wa amani na uaminifu kuhusu mchakato wa amani. Amesema hayo kwenye ujumbe wake wa mwisho akihitimisha muda wake kama mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali MINUSMA, akimshukuru Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, wawakilishi [...]

06/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laahidi hatua kali kufuatia madai ya jaribio la nyuklia DPRK

Kusikiliza / Baraza la usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali jaribio la nyuklia lililofanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK, leo Jumatano ya Januari 6, kufuatia kikao kikao cha dharura walichokuwa nacho leo kushughulikia suala hilo nyeti. Taarifa ya Baraza la Usalama ilotolewa na Msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa jaribio [...]

06/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

CTBTO yaendelea kuchambua taarifa za jaribio la mlipuko DRPK

Kusikiliza / DPRK

Wataalamu wa Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO, wanaendelea na kazi ya kutathmini ripoti za mitetemo iliyobainika kwenye eneo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK. Katibu Mtendaji wa CTBTO Lassina Zerbo amesema hayo akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu kutoka Ouagadougou akieleza [...]

06/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bora baridi kuliko mashambulizi huko Syria; wasema wakimbizi

Kusikiliza / Vibanda vya makazi ya wakimbizi, vyaimarishwa kwa kutumia matairi ya gari. (Picha: Video Capture/UNIFEED)

Mzozo wa Syria ukiwa umeingia mwaka wa tano, wakimbizi waliosaka hifadhi kwenye bonde la Bekaa nchini Lebanon wanahaha kujinusuru na baridi kali. Theluji ya kwanza imeanguka na maelfu ya wakimbizi ambao tayari wamekumbwa na machungu, wanazidi kuhaha, na miongoni mwao ni Abu Hamada. Yeye, mkewe na watoto wao 10 waliwasili Bekaa miaka miwili iliyopita na [...]

06/01/2016 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi yakataa mazungumzo ya kisiasa, UM waiomba ishiriki

Kusikiliza / Maandamano mjini Bujumbura. Picha ya MENUB.

Umoja wa Mataifa unaiomba serikali ya Burundi ishiriki mazungumzo ya kisiasa, ukielezea kuendelea kuwa na wasiwasi kuhusu mauaji yanayozidi nchini humo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amesema hayo akijibu swali wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari leo mjini New York Marekani alipoulizwa msimamo wa Umoja huo kuhusu tangazo la Burundi la [...]

06/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zeid aitaka Thailand kuchunguza kikamilifu kutoweka kwa watu

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye UM Zeid Ra'ad Al Hussein. (Picha: UN Photo / Jean-Marc Ferré)

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein Jumatano ameitaka serikali ya Thailand kuchukua hatua na kuchunguza kikamilifu wapi walipo watu takribani 82 walioorodheshwa kama wametoweka akiwemo mwanasheria anayeheshimika sana nchini humo Somchai Neelapaijit, aliyetoweka yapata miaka 12 iliyopita. Zeid pia ameitaka serikali ya Thai kujumuisha katika sharia zake kitendo cha kutowesha watu [...]

06/01/2016 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazoendelea zijitutumue kusambaza utamaduni: Dk. Kimizi

Kusikiliza / Picha:UNESCO

Nchi zinazoendelea zinapaswa kutumia mbinu mbadala ili kueneza tamaduni zao hususani katika medani ya kimataifa amesema Kaimu Katibu Mkuu wa Tume ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO), Dk. Moshi Kimizi. Katika mahojiano na idhaa hii kuhusu ripoti ya hivi karibuni ya UNESCO inayoonyesha kuwa nchi zilizoendelea kiviwanda bado zimetawala katika [...]

06/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani jaribio la nyuklia DPRK, asema latia hofu kubwa

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akizungumza na waandishi wa habari. (Picha:UN/Rick Bajornas/Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amelaani jaribio la nyuklia chini ya ardhi lililotangazwa kufanywa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, DPRK, leo Januari 6, akisema linatia hofu kubwa. Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina) Akiongea mbele ya waandishi wa habari jijini New York Jumatano asubuhi, Ban amesema jaribio [...]

06/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wa polisi kuwa karibu na jamii wazinduliwa CAR

Kusikiliza / Polisi ya CAR wakati wa uzinduzi wa mradi mpya na MINUSCA. Picha ya MINUSCA.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA umezindua mradi wa kupeleka polisi karibu zaidi na jamii kwa ushirikiano na mamlaka za usalama za nchi hiyo na zile za mji mkuu, Bangui. Priscilla Lecomte na taarifa zaidi. (Taarifa ya Priscilla) Kwenye taarifa iliyotolewa leo, MINUSCA imesema lengo ni kuimarisha uaminifu [...]

06/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jaribio la bomu la Haidrojeni DPRK ni ukiukwaji wa azimio la Baraza la Usalama:IAEA

Kusikiliza / Yukiya Amano, Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA. Picha:IAEA

Serikali ya Jamhuri ya watu wa Korea DPRK leo Jumatano imetangaza kwamba imefanya jaribio la bomu la Haidrojeni. Akizungumzia tamko hilo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki , IAEA Bwana Yukiya Amano amesema.. (SAUTI YA YUKIYA AMANO) “Endapo itathibitika ni kweli jaribio hilo limefanyika basi huo ni ukiukwaji mkubwa wa azimio [...]

06/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani mashambulio ya Taliban Kabul yaliouwa 5 na kujeruhi 56

Kusikiliza / Jiji la Kabul, Afghanistan. Picha ya Ari Gaitanis/UNAMA

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa msaada nchini Afghanistan UNAMA umelaani mashambulio ya mabomu katika maeneo ya raia mjini Kabul mapema mwezi huu. Kundi la Taliban limekiri kuhusika na mashambulio matatu tofauti ya kujitoa muhanga yaliyofanyika kati ya tarehe mosi na 4 Januari amvbayo yamekatili maisha ya watu watano na kujeruhi wengine 56. Waaathitika hao [...]

06/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tumenasa mitetemo isiyo ya kawaida huko DPRK: CTBTO

Kusikiliza / Lassina Zerbo, Katibu Mtendaji CTBTO. (Picha:UN/Maktaba)

Shirika la Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya silaha za Nyuklia, CTBTO, limesema kuwa vituo vyake vya ufuatiliaji vilinasa mitetemo isiyo ya kawaida kwenye eneo la nchi hiyo majira ya usiku. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Katibu Mtendaji wa CTBTO Lassina Zerbo amesema makadirio ya awali yanaonyesha kufanyika katika eneo la nyuklia la [...]

06/01/2016 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malawi ni kinara wa mapitio ya upunguzaji wa hatari za majanga Afrika:UNISDR

Kusikiliza / Waathirika wa mafuriko wakikimbilia mashua ya Jeshi huko Makalanga, Malawi. Picha:UNDP / Arjan de Merwe van

Afrika imefungua ukurasa mpya katika harakati zake za utekelezaji wa mkataba wa Sendai kwa ajili ya kupunguza hatari ya majanga. Kinara ni Malawi, ambayo imefanyia tathimini na kuzipitia sera na hatua zake takribani mwaka mmoja baada ya kukumbwa na mafuriko makubwa. Tathimini ya siku kumi nchini Malawi iliyofanywa na wataalamu watatu kutoka Msumbiji, Afrika Kusini [...]

06/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban aelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa inayoendelea Haiti:

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban akihutubia katika kituo cha MINUSTAH, Haiti. Picha:MINUSTAH

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kisiasa nchini Haiti inayoambatana na mchakato wa uchaguzi. Ameutaka uongozi wa Haiti na wadau wote wa kisiasa kutatua changamoto zilizopo na kuhakikisha kwamba mchakato wa uchaguzi unakamilika haraka iwezekanavyo katika njia ya uwazi, jumuishi nay a haki. Katibu Mkuu anatambua kwamba [...]

06/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Changamoto ya Mediterenea ni miongoni mwa maafa ya kibinadamu:Swing

Kusikiliza / Wakimbizi wakiwasili kwenye kisiwa cha Lampedusa. Picha ya UNHCR

Mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM Lacy Swing amesema wakati idadi kubwa ya wahamiaji na wakimbizi waliowasili barani Ulaya mwaka 2015 imeongeza shinikizo na hofu, hiyo sio changamoto iliyo nje ya uwezo wa bara Ulaya kama muungano kuishughulikia kwa pamoja. Amesema kunahitajika fikra thabiti, za pamoja na hatua ili kuweza kuwa na mtazamo [...]

06/01/2016 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Waliofurushwa makwao Iraq wahaha kwa mapigano zaidi na baridi

Kusikiliza / Hapa ni Zahko nchini Iraq wanaume wabeba vifaa vya kukabiliana na baridi.(Picha:OCHA/Iason Athanasiadis)

Watu wapatao 400,000 nchini Iraq hawana makazi ya kutosha huku wengine 780,000 wakiishi bila bidhaa muhimu za nyumbani na za kuendeleza ubora wa maisha yao wakati huu wa msimu wa baridi kali, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA. Kwa mujibu wa OCHA, serikali ya Iraq na wadau wa kitaifa [...]

05/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Karen AbuZayd ndiye mshauri wa mkutano wa masuala ya wakimbizi na wahamiaji

Kusikiliza / Karen AbuZayd (Picha:UN/ JC McLlwaine)

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ametangaza leo uteuzi wa Bi Karen AbuZayd wa Marekani kama mshauri maalumu wa mkutano wa kushughulikia wimbi kubwa la uhamaji wa wakimbizi na wahamiaji ambao utafanyika kwenye baraza kuu la umoja wa Mataifa mwezi septemba 2016. Mshauri huyo maalumu atafanya kazi kwa karibu na vyombo vya Umoja [...]

05/01/2016 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Safari kuelekea mlima Kilimanjaro kwa ajili ya amani

Kusikiliza / Walinda amani kutoka UNMISS baada ya kufika katika kilele cha mlima Kilimanjaro.(Picha:UNIFEED/Video capture)

Walinda amani kutoka kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS katika juhudi za kueneza ujumbe wa amani ulimwenguni na nchini Sudan Kusini walipanga safari kuelekea nchini Tanzania kwa lengo la kupanda mlima Kilimanjaro ili kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kilele cha mlima huo. Safari hii ambayo ni ya kwanza kuwahi [...]

05/01/2016 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930