Nyumbani » 30/09/2015 Entries posted on “Septemba, 2015”

Umoja wa Mataifa wasisitiza umuhimu wa kuheshimu utu wa wakimbizi na wahamiaji

Kusikiliza / Wakimbizi katika kambi ya Daadab, Kenya. Picha:UNHCR/ S. Ostermann

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mzozo wa uhamiaji na ukimbizi unaokumba dunia sasa ni mkubwa zaidi katika historia yake tangu vita vikuu vya pili. Akizungumza kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu uhamiaji na ukimbizi uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Bwana Ban amesema kwamba jamii ya kimataifa [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria za uwekezaji zinapaswa kuwezesha mataifa yanayoendelea kushindana kibiashara:UNCTAD

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Mukhisa Kituyi.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/Joseph Msami)

Miundo msingi iliyoboreshwa ni muhimu katika kupunguza gharama  za uzalishaji ili kukuza kipato cha jamii na taifa kwa ujumla. Amesema Katibu Mkuu wa kamati ya bishara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD,  Mukhisa Kituyi. Katika mahojiano maalum na Grace Kaneiya wa idhaa ya Kiswahili ya redio ya Umoja wa Mataifa, kuhusu mchango wa UNCTAD [...]

30/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa watarajia kurekebisha mfumo wake wa usaidizi wa kibinadamu

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban akihutubia katika kongamano la kimataifa kuhusu usaidizi wa kibinadamu. Picha:UN Photo/Mark Garten

Mwaka ujao mwezi Mei kutafanyika kongamano la kimataifa kuhusu usaidizi wa kibinadamu huko mjini Istanbul Uturuki ili kuunda upya mifumo ya usaidizi wa kibinadamu wa kimataifa. Katika kikao cha maandalizi ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kwamba licha ya jitihada za wahudumu wa kibinadamu, idadi ya wanaohitaji msaada huo inazidi kuongezeka, [...]

30/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wahanga wa silaha za kulipuka Yemen ndiyo kubwa zaidi duniani- OCHA

Kusikiliza / Uharibifu nchini Yemen

Idadi ya vifo na majereha kutokana na silaha za kulipuka nchini Yemen, ndiyo kubwa zaidi duniani, limesema Shirika la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA. Kwa mujibu wa taarifa ya OCHA, raia wapatao 4,500 waliuawa au kujeruhiwa kwa vilipuzi nchini Yemen katika miezi ya kwanza ya saba ya mwaka 2015. Idadi hiyo [...]

30/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Bendera ya Palestina yapeperushwa UM

Kusikiliza / Wakati wa hafla ya kupandisha bendera ya Palestina.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Leo ni siku ya kujivunia kwa wapalestina popote pale walipo duniani na ni siku ya matumaini. Ndivyo alivyoanza hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati wa sherehe ya kupandisha bendera ya mamlaka ya Palestina kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, kufuatia azimio la Baraza Kuu mapema mwezi huu. [...]

30/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maisha na elimu ya watu Sahel vinadhulumiwa: Lanzer

Kusikiliza / Hapa ni mjini Dan Kada nchini Niger eneo la Sahel, ambako upatikanaji wa chakula ni changamoto.(Picha:UM/WFP/Phil Behan)

Mratibu maalum wa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Sahel Toby Lanzer amesema hali ya kibaindamu katiak ukanda huo inazorota kila uchao kufuatia vuguvugu la ugaidi linalotekelezwa na kundi la Boko Haram . Akiongea na waandishi wa habari mjini New York Lanzer amesema janga hilo ndio linalokuwa kuliko yote Afrika akitolea mfano kuwa watu takribani [...]

30/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msanii wa Nigeria, Nneka, atumia muziki kupigania usawa wa jinsia

Kusikiliza / Mwanamuziki Nneka. Picha: WorldBank Video Capture

Katika mfululizo wa Makala za Benki ya Dunia kuhusu muziki kwa ajili ya maendeleo, tunakutana na nyota wa Nigeria, Nneka, ambaye ana uraia wa Nigeria na Ujerumani. Nneka, kama wanamuziki wenzake kutoka barani Afrika, wamejiunga katika mchakato wa Benki ya Dunia wa kutumia muziki kuchagiza mabadiliko na kuleta maendeleo. Katika Makala hii, Joshua Mmali anatumegea [...]

30/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Israeli ikikiuka makubaliano, nasi hatutatekeleza peke yetu: Rais Abbas

Kusikiliza / Rais Mahmoud Abbas wa Palestina akihutubia Baraza Kuu la UM. (Picha:UN/Cia Pak)

Rais Mahmoud Abbas wa mamlaka ya Palestina, ametoa wito kwa nchi zinazosema kuwa zinaunga mkono suluhu ya mataifa mawili kwa mzozo baina ya Palestina na Israel, zitambue pia Palestina kama taifa, sio Israel pekee. Rais Abbas amesema hayo akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika mjadala wa wazi wa kikao cha 70 cha baraza [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Elimu ndio ufunguo wa mabadiliko katika usawa wa jinsia- Rais Mahama

Kusikiliza / Rais wa Ghana, John Mahama. Picha:UN Photo/Cia Pak

Rais John Mahama wa Ghana, amesema leo kuwa tatizo la kutokuwa na usawa wa kijinsia linaweza kupatiwa mwarobaini iwapo mizizi yake itashughulikiwa, akiongeza kuwa elimu ndio ufungua wa kutimiza lengo la kufikia usawa wa jinsia. Rais Mahama amesema hayo wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, katika mjadala wa wazi wa [...]

30/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Upatikanaji wa ARV's kwa wenye VVU kutaepusha vifo Milioni 21:WHO

Kusikiliza / Mgonjwa wa ukimwi akipumzika katika kliniki ya Bairo Pite, Timor Leste. Picha:UN Photo/Martine Perret

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema mtu yeyote aliyeambukizwa virusi vya Ukimwi anapaswa kuanza tiba ya kupunguza makali ya ugonjwa huo, yaani Anti-Retroviral Therapy, ART haraka iwezekanavyo baada ya uchunguzi. Kwa mujibu wa WHO pendekezo hilo la "Tibu Kila Mtu" limeondoa uzuizi wa awali wa matumizi ya ART miongoni mwa watu wanaoishi na ugonjwa huo, [...]

30/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kwa umoja ule ule kwenye SDGs, tushirikiane pia kuondoa silaha za nyuklia:Ban

Kusikiliza / Mabaki baada ya mlipuko wa bomu, Hiroshima.(Picha ya maktaba UM/Mitsugu Kishida.

IKwa umoja ule ule kwenye SDGs, tushirikiane pia kuondoa silaha za nyuklia:Ban Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza matumizi ya silaha za nyuklia, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limeitisha mkutano usio rasmi kuhusu suala hilo ikiwa ni miaka 70 tangu silaha ya nyuklia kutumika dhidi ya binadamu huko Nagasaki na Hiroshima. Akizungumza [...]

30/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na mawaziri wa Nje wa P5, kuhusu Syria, Yemen na Sudan Kusini

Kusikiliza / Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama, P5.(Picha:UM/Mark Garten)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi tano wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama, yaani P5, ambapo wamemulika masuala ya Syria, Yemen na Sudan Kusini. Katika mkutano huo na mawaziri John F. Kerry wa Marekani, Wang Yi wa Uchina, Laurent Fabius [...]

30/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu lajadili CAR

Kusikiliza / Therese Keita-Boucoum. (Picha:UN/Jean-Marc Ferré)

Hii leo huko Geneva, Uswisi, Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limekuwa na mashauriano shirikishi kuhusu hali ilivyo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambapo wajumbe wameelezwa kuwa miezi ijayo itakuwa muhimu sana katika kuamua mustakhbali wa nchi hiyo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Wajumbe walipata taarifa kutoka kwa [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutokomeza umaskini ni lazima kuwe na uwanja sawa wa kufanya biashara:UNCTAD

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Mukhisa Kituyi.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/Joseph Msami)

Wakati nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimepitisha ajenda ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, Katibu Mkuu wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema biashara na uwekezaji katika miundo msingi ni muhimu katika kufanikisha malengo hayo . Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili jijini New York Bwana Kituyi amesema [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Machafuko Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika yanazima ndoto za vijana: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon.(Picha:UM/Mark Garten)

Baraza la usalama leo limekutana katika mjadala kuhusu utatuzi wa machafuko  Mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika pamoja na kupambana na vitisho  vya ugauidi katika kanda hizo. Taarifa ya Amina Hassan imesheheni (TAARIFA YA AMINA) Mkutano huo umehudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali hususani zinazoguswa kwa namna moja au nyingine [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Adhabu ya kifo si faraja kwa familia za wahanga: Zeid

Kusikiliza / Gereza nchini Haiti. Picha ya MINUSTAH/Logan Abassi

Asilimia 82 ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wametangua au hawatumii tena adhabu ya kifo, ikiwa ni ongezeko kubwa tangu kuanzishwa kwa Umoja huo ambapo nchi 14 tu zilikuwa hazitumii adhabu hii. Hii ni kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra'ad al Hussein, akihutubia kikao kuhusu adhabu ya kifo kwa [...]

30/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wajadili amani kwenye ukanda wa maziwa makuu

Kusikiliza / Polisi wa DRC kwenye doria katika kambi ya wakimbizi wa ndani karibu ya Goma. Picha ya MONUSCO/Sylvain Liechti.

Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, kumefanyika mkutano wa sita wa kikanda kuhusu mchakato wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na ukanda wa maziwa makuu, ukiangazia makubaliano ya amani, ulinzi na usalama yaliyopitishwa mwezi Februari mwaka 2013 huko Addis Ababa, Ethiopia. Akizungumza kwenye mkutano huo Katibu Mkuu wa [...]

30/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Sera za uhamiaji zimepitwa na wakati, tubadilike: IOM

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria waokolewa katika bahari ya Mediterenia. Picha@UNCHR/A. d'Amato(UN News Centre)

Leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kando ya mjadala wa wazi kutafanyika kikao cha ngazi ya juu kuhusu uhamiaji,  kikao kilichoitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Lengo la kikao hicho ni kuhamasisha ushirikiano na hatua za pamoja za kushughulikia matatizo na changamoto za uhamiaji wakati huu ambapo kuna mkanganyiko [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kwaherini, Tanzania itasalia mwanachahama mwaminifu wa UM: Kikwete

Kusikiliza / Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha:UN /Kim Haughton)

Nawaaga lakini Tanzania itasalia mwanachama mwaminifu wa Umoja wa Mataifa. Ni sehemu ya hotuba ya mwisho kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliyotoa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete anayemaliza muda wake wa uongozi wake baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwake mwezi ujao wa Oktoba. Katika hotuba yake Rais Kikwete amegusia masuala mbali mbali [...]

30/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zeid ataka pande zote katika mgogoro Afghanistan kulinda rai

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein. (Picha:UN /Jean-Marc Ferré)

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali ya haki za kibinadamu katika mji wa Kaskazini Mashariki wa Kunduz nchini Afghanistan, kufuatia shambulizi kubwa la jana lilitokelezwa na kundi la Taliban. Katika taarifa, Kamishna Zeid ametoa wito kwa pande zote katika mgogoro  huo [...]

29/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Rais Sirleaf ashukuru waliochangia katika kukabiliana na Ebola Afrika Magharibi

Kusikiliza / Rais was Liberia, Ellen Sirleaf Johnson.(Picha:UM/Cia Pak)

Rais was Liberia, Ellen Sirleaf Johnson amesema katika  kutafakari kuhusu nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathiriwa kwa kiasi kikubwa na homa ya Ebola ambazo ni Liberia, Guinea na Sierra Leone, imani ya kimsingi ya Umoja wa Mataifa imedhihirika, kwamba dunia inaweza daima kwa kupitia ubinadamu kukabiliana na hata maadui wasiotambuliwa na wanaotishia maendeleo ya pamoja. [...]

29/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama liwe shirikishi: Rais Mutharika

Kusikiliza / mutharika

Rais wa Malawi Peter Mutharika amelihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa 70 ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza umuhimu wa muundo shirikishi wa baraza la usalama . Amesema mundo huo mpya wa baraza hilo uwe na ufanisi, wa uwazi na wenye kuwajibika. Rais Mutharika akazungumzia masuala ya amani na usalama. [...]

29/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Balozi mwema wa UNICEF asihi wakimbizi na wahamiaji Ulaya wapewe ulinzi

Kusikiliza / Balozi Mwema wa UNICEF, Orlando Bloom akicheza na watoto wakimbizi kutoka Syria kwenye kambi ya Z'aatari, Jordan. Picha: UNIFEED VIDEO CAPTURE

Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, Orlando Bloom ametoa wito wa ulinzi zaidi kwa maelfu ya watoto wakimbizi na wahamiaji kadri wanavyoendelea na safari zao Ulaya. Katika taarifa, Bloom amesema wakati wa ziara yake kwa kituo cha kuwapokea wakimbizi cha Gevgelija, nchini Macedonia, kinachopakana na Ugiriki. Bloom alisikiliza hadithi [...]

29/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

CITES yataka usafiri wa anga ujiunge na mapambano dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori

Kusikiliza / Picha:UN Photo/John Isaac

Katibu Mkuu wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa kuhusu viumbe walio katika hatari ya kuangamia (CITES) John E. Scanlon amesema makundi ya uhalifu ya kimataifa yanatumia njia halali za usafiri kusafirisha bidhaa zao za magendo, mathalan pembe za vifaru vinasafirishwa kupitia kwa ndege, huku pembe mbichi za ndovu zikisafirishwa kupitia kwa bahari. Akihutubia mkutano wa [...]

29/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ebola tumeshinda tunashukuru marafiki zetu: Rais Koroma

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Martine Perret

Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amehutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akigusia masuala ya mabadiliko ya tabianchi, amani, usalama, usawa wa kijinsia na ugonjwa wa Ebola ambao ulitikisa nchi yake. Mathalani kuhusu mabadiliko ya tabianchi amesema hakuna nchi ambayo inaweza kukwepa athari za kijamii, kiusalama na kiuchumi zinazosababishwa [...]

29/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuishinda ISIL katika mbuga za vita haitoshi- Obama

Kusikiliza / Rais Barack Obama wa Marekani. Picha: UN Photo/Rick Bajornas

Rais Barack Obama wa Marekani, amesema haiotoshi kulishinda kundi linalotaka kuweka Uislamu wenye itikadi kali, ISIL, katika mbuga za mapigano tu. Rais Obama amesema hayo wakati wa mkutano wa viongozi kuhusu kukabiliana na ISIL na itikadi kali katili, ambao umefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kama sehemu ya mikutano ya [...]

29/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Raia wauawa wakisherehekea harusi Yemen, Ban alaani

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon. (Picha MAKTABA-UM/Eskinder Debebe)

Nchini Yemen, watu wapatao 135 wameuawa baada ya kushambuliwa kwa maroketi ya angani wakati wakiwa kwenye sherehe ya harusi katika kijiji kimoja cha mjini Mokha. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani shambulio hilo, akinukuliwa akituma rambirambi kwa familia za wafiwa huku akiwatakia ahueni majeruhi. Ban amerejelea wito wake wa mara kwa mara [...]

29/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanawake wanaajirika, wanaweza: Sophia Simba

Kusikiliza / Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto wa Tanzania Sophia Simba.(Picha ya Idhaa ya kiswahili)

Wanawake wanaajirika, wamesoma na wamepewa nafasi za uongozi, ni kauli ya matumaini ya waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia na watoto wa Tanzania Sophia Simba wakati wa mahojiano na Joseph Msami muda mfupi baada y akuhudhuria mkutano kuhusu usawa wa kijinsia mjini New York. Kwanza anaanza kwa kueleza mkutano huo ambao ni sehamu ya vikao [...]

29/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Kwenye #UNGA, Rais wa Rwanda azingatia usawa katika uongozi wa kimataifa

Kusikiliza / Rais wa Rwanda Paul Kagame akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Picha ya Umoja wa Mataifa/Cia Pak

Jukumu la Umoja wa Mataifa ni la msingi katika kukabiliana na changamoto za kisasa zikiwemo uhamiaji, mabadiliko ya tabianchi na utawala bora, amesema leo Rais wa Rwanda Paul Kagame akihutubia kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Hata hivyo, mabadiliko ya uongozi yanahitajika katika ushirikiano wa kimataifa ili kufanikiwa katika hayo na [...]

29/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa fedha si kitu, muhimu kuendeleza rasiliamli watu na kuaminiana: Rais Nyusi

Kusikiliza / Rais Felipe Nyusi wa Msumbiji.(Picha:UM/Idhaa ya kiswahili/video capture)

Msumbiji ilipata uhuru wake mwaka 1975 kutoka Ureno na sasa iko katika harakati za kujikwamua kiuchumi na kijamii lakini vurugu za hapa na pale zinakwamisha mipango  hiyo wakati huu ambapo nchi hiyo imeungana na mataifa mengine kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza na Rais Felipe Nyusi [...]

29/09/2015 | Jamii: Makala za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Dhamira yetu ni kuzuia ukatili wa itikadi kali, zaidi ya kukabiliana nao- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.(Picha:UM/Amanda Voisard/Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema vikundi katili vya itikadi kali, vikiwemo Da'esh na Boko Haram, ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa kimataifa, vikilenga wanawake na wasichana kinyama na kudunisha maadili ya ujumla ya amani, haki na utu wa mwanadamu, na kwamba tishio hilo linazidi kukua. Ban amesema hayo [...]

29/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Harakati za ukombozi zimetuibulia maadui wengi: Rais Nyusi

Kusikiliza / Rais Felipe Jacinto Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji. Picha:UN Photo/Cia Pak

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amesema harakati za nchi katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ziliibua maadui wengi ambao sasa wanasababisha vurugu zinazoendelea hata nchini mwake. Akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa hii baada ya kuhutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Nyusi amesema . (Sauti ya Nyusi) Na kwa hiyo ujumbe [...]

29/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Mashirika 12 ya UM yapaazia sauti haki za mashoga na wenye jinsia tofauti

Kusikiliza / Bendera.(Picha:UM/Mark Garten)

Katika hatua ya kwanza ya aina yake, mashirika kumi na mawili ya Umoja wa Mataifa yametoa leo taarifa ya pamoja ikitoa wito wa kuchukua hatua kutokomeza ukatili na ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na watu wanaojitambulisha kwa jinsia tofauti na muonekano wao, pamoja na barubaru na watoto. Taarifa kamili na Joshua Mmali (Taarifa [...]

29/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Mashirika ya Kimataifa walaani vurugu CAR

Kusikiliza / Wakimbizi mjini Bangui nchini CAR.(Picha:OCHA/Gemma Cortes)

Vurugu zimeripotiwa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambapo watu zaidi ya 30 wameuawa na wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa kwenye mji mkuu Bangui. Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani mlipuko huo wa ghafla wa vurugu kama anavyoelezea Amina Hassan katika ripoti hii. (Taarifa Kamili na Amina Hassan) Katika taarifa, [...]

29/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yamulikwa kando ya #UNGA

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini, kwenye kambi ya Malakal, Picha ya Umoja wa Mataifa/Isaac Billy

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Sudan Kusini umefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa Ban Ki-moon amewasihi viongozi wa nchi hii kurekebisha makosa yao na badala yake kujali raia waliowachagua. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Akihutubia kikao hicho, Bwana [...]

29/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Utekelezwaji wa mkataba wa amani Sudan Kusini ni jukumu letu sote: Kenyatta

Kusikiliza / Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.UN Photo/Amanda Voisard

Katika kuhakikisha usalama ukanda wa Afrika Mashariki  nchi wanachama zinapaswa kusaidia katika mchakato wa utekelezaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini na viongozi wa Sudan Kusini hivi karibuni amesema Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Katika mahojiano na Joseph Msami baada ya kuhutubia mkutano wa 70 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Rais Kenyatta anasema [...]

29/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Rais Museveni ataka mabadiliko ya mifumo ya uchumi barani Afrika

Kusikiliza / Rais wa Uganda Yoweri Museveni akihutubia Baraza Kuu. Picha ya Umoja wa Mataifa/Amanda Voisard.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amezingatia umuhimu wa ukuaji wa uchumi, viwanda, uwekezaji na biashara katika kuleta maendeleo kuliko misaada ya kibinadamu. Akihutubia kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Museveni amesema mabadiliko ya uchumi barani Afrika ni jambo la msingi. « Maendeleo endelevu bila mabadiliko ni kama kuzungumzia kiasi cha [...]

29/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa yatoa ahadi kwa ajili ya hatma ya Somalia

Kusikiliza / Bwana Ban amezingatia michango ya wanawake katika maendeleo Somalia. Picha ya Umoja wa Mataifa/Tobin Jones.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Somalia imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa taifa na demokrasia akisihi viongozi wa nchi hiyo kuendelea kuonyesha bidii ili kuboresha utawala wa sheria kupitia uchaguzi jumuishi ifikapo mwaka 2016. Bwana Ban amesema hayo kwenye mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Somalia uliofanyika leo sanjari na kikao [...]

29/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Hatufahamu tumeikosea nini Marekani: Mugabe

Kusikiliza / Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe akihutubia Baraza Kuu la UM. (Picha:UN/Amanda Voisard)

Leo ni siku ya pili ya mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo viongozi mbali mbali wanatarajiwa kuhutubia akiwemo Rais Paul Kagame wa Rwanda na Jakaya Kikwete wa Tanzania. Hapo jana nyakati za jioni, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alihutubia akirejelea tena wito wa vikwazo dhidi ya nchi yake vilivyowekwa na [...]

29/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Janga la wakimbizi Ulaya limesababishwa na binadamu: Zuma

Kusikiliza / Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini akihutubia Baraza Kuu. (Picha:UN Photo/Cia Pak)

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linaposhughulikia mizozo barani Afrika lihakikishe linasikiliza sauti za bara hilo na vyombo vyake vya kikanda badala ya kufanya vinginevyo. Ni kauli ya Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini alipohutubia mjadala wa wazi wa Baraza kuu akisema kuwa … (Sauti ya Zuma) "Hali ya sasa nchini Libya na ukanda [...]

28/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Viongozi waahidi kuimarisha mfumo wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Ukaguzi wa gwaride la UNFIL.(Picha:Pasqual Gorriz)

Katika kikao maalum kuhusu operesheni za ulinzi wa amani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni wakati sasa wa kuleta mabadiliko katika mfumo huo, akitaja ni lazima kuongeza uwezo wa kijeshi, polisi na kuwa na vikosi vya akiba. Halikadhalika amemulika umuhimu wa kupambana na ukatili wa kingono unaofanywa na walinda amani. Kwa [...]

28/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Obama ataja mambo ya kuzingatia kuimarisha ulinzi wa amani

Kusikiliza / Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Mongolia Sudan Kusini. Picha: UN Photo / Martine Perret

Marekani leo imeongoza mkutano wa viongozi kuhusu ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa ambapo Rais Barack Obama ametaja mambo manne ya kuzingatia katika kuimarisha mpango huo. Mosi ametaka nchi kuchangia zaidi askari na pili kuimarisha ulinzi wa raia akisema tofauti na miaka 20 iliyopita, walinda amani sasa wana mamlaka za kuchukua hatua zaidi kulinda [...]

28/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Kwenye meza ya chakula cha mchana, Ban awasihi viongozi wazingatie SDGs

Kusikiliza / Ban na viongozi wa dunia kwenye meza ya chakula. Picha: UN Photo/Amanda Voisard

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, leo amekuwa na hafla ya chakula cha mchana na viongozi wa dunia, akiwaambia kwamba wanasherehekwa miaka 70 ya Umoja huo, ingawa pia wanafahamu kuwa ni wakati wa misukosuko. Ban amesema kuafikia na kupitishwa kwa malengo 17 ya maendeleo endelevu ni hatua ya kwanza ya kazi kubwa ya [...]

28/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila mtu anasema lakini utekelezaji bado changamoto: Rais Nyusi

Kusikiliza / Rais Felipe Nyusi wa Msumbiji akihutubia Baraza Kuu la UM. (Picha:UN/Cia Pak)

Rais Felipe Nyusi wa Msumbiji amesema maendeleo chanya yatokanayo na kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa yanakabiliwa na ukungu kutokana na mizozo inayoendelea kukumba ulimwengu kwa sasa. Akihutubia katika mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New  York, Marekani,  Rais Nyusi amesema mizozo hiyo inazidi kuathiri  binadamu na kwamba ni kiashiria kuwa [...]

28/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Tusipochukua hatua Paris mwezi Disemba, sayari ya dunia iko mashakani: François Hollande

Kusikiliza / Rais wa Ufaransa Francois Hollande. Picha ya Umoja wa Mataifa/Cia Pak.

Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Ufaransa François Hollande amesisitiza umuhimu wa mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Paris mwezi Disemba mwaka huu akisema viongozi watapaswa kuchukua hatua, pengine hatma ya sayari ya dunia itakuwa mashakani. Amekaribisha michango iliyotangzwa na nchi 90, zikiwemo Marekani na China, kuhusu jitihada zao za kupunguza athari [...]

28/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Asilimia 90 ya wazee Afrika wanakosa huduma: ILO

Kusikiliza / Wachezaji wawili wakifurahia mchezo wa chesi katika jiji la New York. Picha: UN Photo / Grunzweig

Kuelekea siku ya wazee duniani tarehe Mosi mwezi ujao, shirika la kazi duniani, ILO limesema kuna uhaba wa watoa huduma Milioni 13 nukta sita ulimwenguni kote na hivyo kudumaza huduma za uangalizi kwa zaidi ya nusu ya wazee duniani. ILO katika utafiti wake mpya imebaini kuwa uhaba huo unakosesha huduma za muda mrefu za malezi [...]

28/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rais Putin asema mapinduzi Mashariki ya Kati hayakuleta chochote ila majanga, vita na umaskini

Kusikiliza / Picha ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na waziri wa mambo ya nje Lavrov. Picha kutoka akaunti ya Twitter na UN Photo.

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameeleza kusikitishwa na kuona kwamba baadhi ya nchi ambazo zinalaani vitendo vya kigaidi kutoka vikundi kama vile ISIS, wakati huo huo zinaendelea kufadhili vikundi hivyo na kuvipatia risasi. Katika hotuba yake leo mbele ya kikao cha 70 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais Putin amesema mapinduzi yaliyotokea Mashariki [...]

28/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Makubaliano kuhusu nyuklia Iran ni ushindi dhidi ya vita- Rais Rouhani

Kusikiliza / Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rouhani.(Picha:UM/Loey Felipe)

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rouhani, amesema leo kuwa makubaliano yaliyosainiwa baina ya Iran na Marekani, Uchina, Ufaransa, Urusi, Uingerereza, EU, na Ujerumani kuhusu mpango wa nyuklia nchini mwake (JCPOA), ni mfano bora wa ushindi dhidi ya vita. Rais Rouhani amesema hayo akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika mjadala wa [...]

28/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Shakira, Anjelique Kidjo wapigia upatu SDGS

Kusikiliza / Mwimbaji Angelique Kidjo wakati akiimba katika Umoja wa Mataifa, New York.(Picha:UM/Kim Haughton)

Kazi na dawa! Ndivyo inavyosikika katika tukio la kupaza sauti kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGS lililowaleta pamoja nyota mbalimbali wakiwemo wanamuziki na wanaharakati wakati wa uzinduzi wa malengo hayo. Ungana na Joseph Msami katika makala itakayosafirisha hisia zako katika eneo la tukio. (SAUTI MAKALA)

28/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Tupo tayari kushirikiana na dunia katika amani na maendeleo: China

Kusikiliza / Rais wa China Xi Jinping.(Picha:UM/Cia Pak)

China itaendelea kushirikiana na jumuiya ya kimataifa katika ujenzi wa amani na maendeleo amesema rais wa China Xi Jinping wakati akilihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa katika mkutano  wake wa 70 unaondelea mjini New York. Kiongozi huyo amesema kuwa katika kusongesha mbele maendeleo nchi yake iko tayari hushirikiana na nchi nyingine katika masuala ya [...]

28/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Marekani kuungana na nchi zaidi ya 50 kuimarisha ulinzi wa amani- Obama

Kusikiliza / Rais Barack Obama wa Marekani. Picha:UN Photo/Loey Felipe

Baada ya ufunguzi,  hotuba za mjadala wa wazi zilianza kutolewa ambapo katika hotuba yake, Rais Barrack Obama wa Marekani, ametangaza kuwa Marekani itaungana baadaye leo na nchi zaidi ya 50 katika kuzindua mkakati wa kuimarisha ulinzi wa amani. Rais Obama amesema anatambua kuwa ni lazima jamii ya kimataifa ijitahidi zaidi katika kuimarisha uwezo wa kulinda [...]

28/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

TEKNOHAMA yachangia maendeleo endelevu Tanzania: Rais Kikwete

Kusikiliza / Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania. Picha: UN Photo/Eskender Debebe

Uwekezaji katika Teknolojia za Habari na Mawasiliano, TEKNOHAMA umeleta mafanikio makubwa nchini Tanzania na inachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo endelevu amesema Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa Idhaa hii. Akihojiwa aye kabla ya kikao cha Shirika la Kimataifa la mawasiliano ITU ambapo tuzo mpya ya kumulika uongozi katika TEKNOHAMA [...]

28/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufadhili na Utashi wa kisiasa wahitajika kutimiza maendeleo Afrika: ripoti mpya

Kusikiliza / Kutokomeza umaskini kunawezekana, kwa mujibu wa ripoti hii. Picha ya UNICEF/ NIGB2010-0199/Pirozzi

Uongozi, ubunifu na uwekezaji katika huduma za kijamii ndio zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia barani Africa, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo mjini New York. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla ) Kwa mujibu wa ripoti hii iliyotolewa pamoja na Muungano wa Afrika, Shirika la Umoja wa [...]

28/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ahoji iweje bajeti za kijeshi ni rahisi kupatikana kuliko za maendeleo

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban akihutubia Baraza Kuu. Picha: UN Photo/Cia Pak

Mjadala wa wazi wa Baraza kuu la Umoja wa Mataifa umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa huo jijini New York, Marekani ukileta viongozi mbali mbali wan chi 193 wanachama wa chombo hicho ambacho mwaka huu kimetimiza miaka 70 tangu kuanzishwa kwake. Amina Hassan na maelezo zaidi. (Taarifa ya Amina) Nats Hii ni video [...]

28/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani wa UNAMID auawa, Ban alaani

Kusikiliza / Walinda amani wa UNAMID wakiwa doriani. (Picha:Albert González Farran, UNAMID)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya mlinda amani mmoja wa ujumbe wa pamoja wa Umoja huo na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID. Mlinda amani huyo kutoka Afrika Kusini aliuawa huku wenzake wengine wanne wakijeruhiwa wakati walipokuwa wakisindikiza msafara wa UNAMID uliokuwa umebeba vifaa huko Mellit, Darfur Kaskazini nchini [...]

28/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mateso na mauaji vyashamiri Burundi, watu 134 wameuawa tangu Aprili: Kamishna Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye UM Zeid Ra'ad Al Hussein. (Picha: UN Photo / Jean-Marc Ferré)

Kumekuwepo na ongezeko la matukio ya watu kukamatwa, kushikiliwa na hata kuuawa nchini Burundi, jambo ambalo limemtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Katika taarifa yake ya leo, amenukuliwa akisema kuwa tangu mwezi Aprili watu 134 wameuawa [...]

28/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa wazi wa Baraza Kuu waanza leo

Kusikiliza / Ratiba ya mjadala wa wazi unaoanza leo Jumatatu. (Picha:UN)

  Mjadala wa wazi wa mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza leo kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani ambapo wakuu wa nchi na serikali wanaanza kuhutubia katika kikao hicho cha siku tatu. Mjadala huu unafanyika baada ya siku tatu ya hotuba za viongozi zilizoanza Ijumaa baada [...]

28/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Tuwekeze katika elimu dhidi ya unyanyapaa kuutokomeza Ukimwi : Rais Mutharika

Kusikiliza / mutharika-malawi

 Mapambano dhidi ya unyanyapaa kwa waathirika wa ugonjwa wa Ukimwi na dhana potofu ni maeneo yakutilia mkazo ili kutokomeza ugonjwa huo amesema  Rais wa Malawi Peter Mutharika. Rais  Mutharika ambaye alikuwa miongoni mwa watoa mada katika majadala uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la makabiliano dhidi ya Ukimwi UNAIDS, amemwambia Joseph Msami kandoni mwa [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Hakuna taifa lililo salama kutokana na mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Rais Mohamed Buhari wa Nigeria.(Picha:UM/Amanda Voisard)

Rais Mohamed Buhari wa Nigeria amesema ijapokuwa mataifa ya Bara la Afrika hayajachangia pakubwa kwa viwango vya joto duniani, hakuna taifa lililo salama kutokana na mabadiliko ya tabianchi huku akiongeza mataifa yaliyoendelea pia hayataepukana na mzigo wa mabadiliko hayo. Kiongozi huyo amesema nchini Nigeria wameshudia mabadiliko ya hali ya hewa, kupanda kwa viwango vya usawa [...]

27/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi dhidi ya raia Bangui yakomeshwe:OCHA

Kusikiliza / Mlinda amani akiwa Bangui nchini CAR(Picha ya MINUSCA.)

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR Marc Vandenberghe, amelaani mashambulizi mapya dhidi ya raia mjini Bangui mnamo Septemba 26 na kutaka pande kinzani kuheshimu sheria za kimataifa na kulinda raia. Taarifa ya ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadmau OCHA nchini CAR inasema kuwa mapigano hayo yalizuka baada ya kifo [...]

27/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dunia ni lazima ichukue hatua sasa, bila kumwacha yeyote nyuma- Obama

Kusikiliza / Rais Barrack Obama wa Marekani.(Picha:UM/Amanda Voisard)

Rais Barrack Obama wa Marekani, amesema leo kuwa ufanisi uliopatikana katika kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia yanaleta fahari, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya. Rais Obama amesema hayo akihutubia viongozi wa dunia kwenye Umoja wa Mataifa, katika mkutano wa Maendeleo Endelevu, SDGs. Obama amesema kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia kama vile kupunguza [...]

27/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Viongozi waelezea azma yao kukamilisha mkataba wa tabianchi unaofaa nchi zote

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon.(Picha:UM/Evan Schneider)

Viongozi wa dunia wameelezea azma yao leo kukamilisha mkataba wa kudumu na wenye maana kuhusu tabianchi mjini Paris, Ufaransa, na ambao utazifaa nchi zote. Hayo yametangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, akikutana na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini New York, ambako mkutano kuhusu malengo ya maendeleo [...]

27/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Taasisi jumuishi na zinazowajibika zitawezesha maendeleo endelevu – Mkuu wa Safaricom

Kusikiliza / Bob Collymore, mkurugenzi wa Safaricom akishiriki kwenye mkutano wa sekta binafsi pamoja na mkuu wa UNDP Helen Clark. Picha ya Nicolo Gnecchi/UNDP.

Mkuu wa kampuni ya Simu ya Mkononi nchini Kenya, Safaricom, Bob Collymore amesema kuna haja ya kuwepo kwa mikakati dhabiti ya kupambana na ufisadi ili kuhakikisha usawa katika jamii hususan katika upatikanaji wa haki katika muktadha ya mataifa yanayoendelea. Collymore amesema haya wakaki wa mjadala kuhusu nafasi ya taasisi katika kufikia Ajenda ya Maendeleo Endelevu, [...]

27/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Teknolojia ni muhimu katika kufikia maendeleo endelevu: Benki ya Dunia

Kusikiliza / Hapa ni mjini Mogadishu nchini Somalia ambako huduma ya pesa kupitia teknolojia za zama hizi inatumika.(Picha:UM/Stuart Price)

Uunganishwaji wa kidijitali ni muhimu katika uchumi wa dunia na unaweza kutumika katika kuimarisha ushirikishwaji, kurahisisha kazi, na kuimarisha ubunifu, lakini ili kuhakikisha hili ni lazima sera sahihi ziwekwe. Hiyo ni kauli ya rais wa Benki ya Dunia, Jim Yong Kim. Dkt. Kim amesema hayo wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu maendeleo katika zama za [...]

27/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Kemeeni machafuko kulinda urithi wa tamaduni: UNESCO

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irian Bokova.(Picha:UM/Kim Haughton)

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova ametaka nchi wanachama wa UM kusimama kinyume na wale wenye nia ya kuleta migawanyiko, utengano na machafuko akisema mambo hayo huchangia kurudisha nyuma harakati za kuhifadhi urithi wa kitamaduni. Akizungumza katika mjadala kuhusu ulinzi wa kitamaduni kwa mnaufaa ya historia [...]

27/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Taasisi ya Bunge ni muhimu katika kufikia malengo ya SDG’s: IPU

Kusikiliza / Rais wa IPU Saber Chowdhury (Picha:UM/Eskinder Debebe)

Ili kufanikiwa kwa Ajenda Endelevu iliyopitishwa na viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani Ijumaa ya Septemba 25, ni lazima kuwepo kwa taasisi dhabiti, hususan bunge la kitaifa. Ni kauli ya Rais wa Umoja wa mabunge duniani, IPU Saber Hossain Chowdhury wakati wa mjadala kuhusu kujenga taasisi mahsusi zinazoyowajibika katika [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Liberia itatekeleza sheria itakayowanyima rufaa wanaowabaka wanawake- Rais Sirleaf

Kusikiliza / Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf. Picha:UN Photo/Mark Garten

Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, amesema leo kuwa serikali yake imepiga hatua katika kuongeza usawa wa jinsia, lakini akakiri kuwa bado kuna mapengo mengi, yakihitaji juhudi zaidi. Kwa mantiki hiyo, Rais Sirleaf ameahidi kuwa serikali yake itahakikisha kuwa mswada ulioko bungeni sasa kuhusu ukatili wa majumbani unapitishwa ili kuulinda usalama wa wanawake. "Serikali yangu [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali yangu inaahidi kuhakikisha usawa wa jinsia- Rais Kenyatta

Kusikiliza / Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakati wa mkutano wa leo, New York.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, amesema leo kuwa serikali yake itaendelea kuwa imara katika kuhakikisha usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake. Rais Kenyatta amesema hayo wakati wa mkutano uliowaleta pamoja viongozi wa dunia kutoa ahadi za kuchukua hatua kuhakikisha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake. Bwana Kenyatta amesema serikali yake itaendeleza ufanisi uliopatikana kwa wanawake [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miji iwajibike kulinda mazingira na uendelevu: Girardin

Kusikiliza / Mji wa New York nchini Marekani.(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Miji ina wajibu katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi hususani katika kupunguza matumizi ya hewa ukaa kutokana na shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwamo viwanda amesema Bi  Annick Girardin ambaye ni  waziri wa Ufaransa anayeshughulikia  maendeleo na nchi zinazongumza Kifaransa Francophone. Katika majadiliano mjini New York kuhusu namna miji inavyoweza kuwa endelevu kwa kulinda mazingira  [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

“Watalii bilioni moja, fursa bilioni moja,” ndio ujumbe wa Siku ya Utalii

Kusikiliza / Hapa ni mtazamo wa Sveti-Stefin, karibu na Budva pwani ya Adriatic ambayo ni eneo la utalii.(Picha:UM//Bijur)

Leo Septemba 27 ikiwa ni Siku ya Utalii Duniani, Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon, amesema kwamba siku hii inamulika uwezo wa utalii katika ulimwengu kwa ajili ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Huku watalii bilioni moja wa kimataifa wakisafiri duniani kila mwaka, utalii ni sekta iliyo na uwezo wa kubadili maisha ya [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi waahidi kuhakikisha usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati akihutubia kikao cha leo kushoto ni rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.(Picha:/Eskinder Debebe)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema ni vigumu kutimiza ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu bila kuwa na haki sawa na kamili kwa nusu ya idadi ya watu duniani, kisheria na katika vitendo, akipigia chepuo usawa wa jinsia na kuwawezesha wanawake. Ban amesema hayo akihutubia viongozi wa dunia, ambao wamekutana leo [...]

27/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

OECD na UNCTAD washirikiana kufanikisha Ajenda ya Maendeleo Endelevu

Kusikiliza / sdgsmall

Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OECD na Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD yameahidi kufanya kazi kwa pamoja katika maeneo ya umuhimu kwa Ajenda ya Maendeleo Endelevu yaliyopitishwa Ijumaa na vongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Katibu Mkuu wa OECD, Jose Ángel Gurría [...]

26/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya zaimarika Tanzania: Kikwete ashiriki uzinduzi wa mradi wa kimataifa

Kusikiliza / Rais wa tanzania Jakaya Kikwete wakati wa mkutano wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Picha ya Umoja wa Mataifa/amanda Voisard.

Shirika la Afya Duniani WHO, Benki ya Dunia pamoja na Mfuko wa Bill na Melinda Gates wamezindua mradi mpya wa ubia kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa huduma za msingi za afya kwenye nchi zenye kipato cha chini na cha kati. Mradi wa ufanisi wa huduma za msingi za afya, PHCPI umezinduliwa leo kwenye makao [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Malipo ya kidigitali yainua maisha ya raia Tanzania: Kikwete

Kusikiliza / Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Helen Clark wa UNDP kwenye mkutano wa malipo ya kidigitali #cash2digital. Picha kutoka akaunti ya Twitter ya @BetterThan_cash

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameeleza kwamba idadi ya watu wanaopata huduma za fedha na benki imeongezeka mara nne tangu mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 58 nchini Tanzania, benki nane nchini humo zikitoa huduma za akiba na mikopo sasa kupitia simu za kiganjani. Amesema hayo akihutubia mkutano kuhushu malipo ya kidigitali uliofanyika leo kwenye makao [...]

26/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa Safaricom aonyesha uhusiano wa sekta binafsi na #SDGs

Kusikiliza / Bob Collymore, mkurugenzi wa Safaricom akishiriki kwenye mkutano wa sekta binafsi pamoja na mkuu wa UNDP Helen Clark. Picha ya Nicolo Gnecchi/UNDP.

Mkuu wa kampuni ya Safaricom nchini Kenya Bob Collymore amesema wananchi na wanahisa wanapaswa kuwajibisha mashirika binafsi ili yajitahidi kuimarisha utendaji kazi wa uwe endelevu zaidi. Bwana Collymore amesema hayo alipohojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kando ya mkutano wa sekta binafsi uliofanyika leo mjini New york Marekani sanjari na mkutano wa Malengo ya [...]

26/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Tuondolewe vikwazo ili tufanikishe ajenda 2030: Mugabe

Kusikiliza / Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe. (Picha:UN/Cia Pak)

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amesema nchi  yake imejipanga sawa ili kuhakikisha inafanikisha utekeleza wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Akihutubia mkutano mahsusi baada ya kupitishwa kwa malengo hayo yajulikanayo pia kama ajenda 2030, Rais Mugabe amesema baada ya mashauriano ya wadau mbali mbali wamepitisha mpango mpya wa kitaifa unaoendana ajenda hiyo mpya. Mpango huo [...]

26/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya nyuklia yameweka mazingira bora ya ushirikiano. Dkt. Rouhani

Kusikiliza / Rais Hassan Rouhani wa Iran akihutubia Baraza Kuu la UM. (Picha:Video capture)

Mchakato wa miaka miwili sasa kati ya Iran na nchi sita zikiwemo tano wanachama watano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuhakikisha kuna makubaliano kuhusu masuala ya nyuklia, uweka mazingira bora ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa. Hayo yamesemwa na Rais Hassan Rouhani wa Iran alipohotubia mkutano wa baraza kuu la Umoja [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Bajeti za nchi zizingatie ustawi wa wanawake: Kikwete

Kusikiliza / Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Joseph Msami wa Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha:UN-Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema wanawake hawajengewi mazingira ya kutosha ya ustawi wa kijamii na  kiuchumi kama ilivyo wanaume hususani katika nchi zinazoendelea akitolea mfano wa bajeti za serikali ambazo hazizingatii ukuaji nwa kundi hilo. Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii muda mfupi baada ya kuhutubia mjadala kuhusu kupambana na ukosefu wa [...]

26/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Ban awa na mazungumzo na Rais Zuma jijini New York

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon (kushoto) na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini (Kulia) baada ya mazungumzo yao jijini New York. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Kando mwa vikao vya malengo ya maendeleo endelevu, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ambapo amemshukuru kwa ushirikiano ambao nchi yake inapatia Umoja wa Mataifa hususan masuala ya usalama na amani. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Ban na Zuma katika [...]

26/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Polio yatokomezwa Nigeria: WHO

Kusikiliza / Waathirika wa polio katika Jimbo la Kano, Nigeria, wakiwa juu ya baiskeli maalum iliyoundwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu. Picha: UNICEF / Sebastian Tajiri

Ugonjwa wa Polio si tatizo tena nchini Nigeria, limesema Shirika la Afya Duniani(WHO) huku likitoa hadhari kuwa nchi hiyo isibweteke bali iendelee kuwa makini. WHO imesema tangu mwezi Julai mwaka jana Nigeria haijaripoti kisa chochote cha Polio licha ya kwamba katika miaka ya karibuni nchi hiyo iliongoza kuwa na nusu ya visa vya polio ulimwenguni. [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kufanikisha SDGs, China kuongeza msaada hadi dola Bilioni 12 ifikapo 2030

Kusikiliza / Rais wa China, Xi Jinping akihutubia kikao cha SDGs jijini New York, Marekani. (Picha:UN/Cia Pak)

Maendeleo  ambayo China imeshuhudia katika miongo kadhaa yameleta ustawi siyo tu kwa wananchi wake bali pia kwa wakazi wa maeneo mbali mbali dunia. Amesema Rais Xi Jinping wa China wakati akihutubia katika siku ya pili ya mkutano wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, yaliyopitishwa Ijumaa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa. Mathalani amesema kwa [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Dola Bilioni 25 kuepusha wanawake, watoto na vijana dhidi ya magonjwa:Ban

Kusikiliza / Wagonjwa katika hospitali ya Cama ya wanawake na watoto, Mumbai, India. Picha:UN Photo/Mark Garten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametangaza ahadi ya dola Bilioni 25 zitakazotumika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo kuboresha afya ya wanawake, watoto na vijana barubaru. Tangazo hilo limetolewa kufuatia uzinduzi wa mkakati wa kimataifa kwa afya ya wanawake, watoto na vijana barubaru jijini New York, Marekani kando mwa mkutano wa kupitishwa [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajenda 2030 yahitaji ushirikiano zaidi ili kufanikisha: Ethiopia

Kusikiliza / Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, akihutubia Baraza Kuu. (Picha:UN /Cia Pak)

Tunapoanza zama za maendeleo mapya endelevu, tunahitaji jitihada za pamoja zaidi siyo kwa sababu malengo ni mengi kuliko yale ya milenia bali ni kwa sababu yanagusa dunia nzima. Ni kauli ya Wazir Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn aliyotoa wakati akihutubia mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani baada [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

SDG na Mapinduzi ya viwanda Afrika kuangaziwa leo UM

Uendelezaji wa viwanda vidogo vidogo kama hivi vya kuchomea chuma nchini Msumbiji vinaweza kubadili maisha ya jamii. (Picha:UNIDO)

Ikiwa leo ni siku ya pili ya mjadala kuhusu ajenda ya maendeleo endelevu, SDG iliyopitishwa Ijumaa na wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mikutano mbali mbali ya kando inaendelea na miongoni mwao ni ule unaohusu mkakati wa kuleta mapinduzi ya viwanda barani Afrika. Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu mkutano huo, [...]

26/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tumepiga hatua muhimu katika kuinua wanawake Tanzania: Kikwete

Kusikiliza / Rais Kikwete akihutubia mkutano wa #Planet5050. Picha ya Idhaa.

Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amezungumza katika mjadala kuhusu kupambana na ukosefu wa usawa na kuwezesha wanawake na wasichana ikiwa ni sehemu ya malengo ya maendeleo enedelevu SDGs uliofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani na ukiongozwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta. Katika mjadala huo Rais Kikwete amesema [...]

25/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Utu na ujumuishwaji muhimu katika kufanikisha SDGS: Rais Sirleaf

Kusikiliza / Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf. Picha ya Umoja wa Mataifa/ Amanda Voisard

Ajenda ya maendeleo endelevu SDGS itafanikiwa ikiwa ujumuishwaji, utu kwa wote na autolewaji wa fursa utazingatiwa amesema Rais wa Liberia Ellen Johson Sirleaf wakati akihutubia mkutano wa 70 wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaoendelea mjini New York. Hata hivyo Rais huyo wa kwanza mwanamke barani Afrika amesema ubia wa kimaendeleo unahitajika pamoja na [...]

25/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Rais Kenyatta asifu ajenda 2030, ataka maono ya pamoja kuifanikisha

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Cia Pak

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, amesema tangu kupitshwa kwa malengo ya milenia mwongo mmoja na nusu, kumekuwepo na mafaniko mengi, japo changamoto sio haba. Rais Kenyatta amesema hayo wakati wa hotuba yake kwa Baraza Kuu la Sabini la Umoja wa Mataifa. Akitolea mfano maendeleo yaliyopatikana baada ya kupitishwa kwa malengo ya milenia, Rais Kenyatta amesema [...]

25/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Ajenda 2030 ni ya kila mtu: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon(Picha:UM/Eskinder Debebe)

Zaidi ya watu milioni 8 wameshiriki katika uundaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs wakipata fursa za kusikilizisha sauti zao, amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwenye mjadala maalum uliofanyika leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, baada ya kupitishwa rasmi kwa ajenda hiyo ya 2030. Bwana Ban amesema [...]

25/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Gharama ya kupuuza mahitaji makubwa ya kibinadamu eneo la Ziwa Chad, itakuwa kubwa- O'Brien

Kusikiliza / Mratibu Mkuu wa masauala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Stephen O'Brien.(Picha:UM/Loey Felipe)

Mratibu Mkuu wa masauala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Stephen O'Brien, ameonya leo kuwa jamii ya kimataifa ikipuuza mahitaji makubwa ya kibinadamu katika eneo la Ziwa Chad, gharama yake itakuwa kubwa zaidi. Bwana O'Brien amesema hayo katika mkutano wa ngazi ya juu kujadili mzozo wa kibinadamu unaoibuka katika eneo hilo, na kuona njia bora [...]

25/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kutimiza SDGs kutahitaji kubadilisha njia za uzalishaji na matumizi ya chakula- FAO

Kusikiliza / UN Photo: UN Photo/Mark Garten

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, Jose Graziano da Silva, amesema leo kuwa kilimo na maendeleo ya vijijini vinapaswa kupewa msukumo mkubwa ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya kutokomeza umaskini na kutokomeza njaa, ambayo yamepitishwa leo. Akiongeza kuwa mabadiliko ya tabianchi yanafanya changamoto za kutimiza malengo hayo kuwa kanganyifu zaidi, Bwana [...]

25/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tuko pamoja na Burundi, wakiukwaji wa haki sheria ichukue mkondo wake:Ban

Kusikiliza / Bendera ya Burundi. (Picha:MAKTABA)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekuwa na mazungumzo na Makamu wa pili wa Rais wa Burundi Joseph Butore ambapo wamejadili usaidizi ambao umoja huo unaweza kupatia nchi hiyo wakati huu ambapo jitihada za kikanda zinaendelea kumaliza hali iliyopo nchini humo. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akitoa hakikisho la [...]

25/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maadhimisho ya siku ya amani duniani

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Evan Schneider

Ndoto ya amani i miongoni mwa kila mtu duniani lakini zaidi kwa vijana ambao wanaelezwa kuwa na nafasi kubwa katika kusongesha amani. Hii ni sehemu ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika siku ya amani duniani iliyoadhimishwa kote duniani Septemba 21. Katika muktadha huo ujumbe wa video wa Ban unasisistiza [...]

25/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Internet.org yabadili maisha kwenye maeneo kadhaa ikiwemo Afrika

Kusikiliza / Tovuti ya internet.org.(Picha ya Idhaa ya Kiswahili/Assumpta Massoi)

Wakati malengo ya maendeleo endelevu, SDG yakipitishwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, shughuli mbali mbali zimekuwa zikifanyika katika kuchagiza hatua hiyo. Mathalani kumekuwepo na uzinduzi wa malengo hayo kupitia filamu halikadhaliaka maonyesho ya jinsi ambayo teknolojia ambayo ni moja ya masuala yaliyotajwa kwenye malengo  hayo inaweza kubadili maisha ya watu. Ili kufahamu kwa [...]

25/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Sasa ni lazima tutumie SDGs kuubadilisha ulimwengu- Ban

Kusikiliza / Katibu mkuu katika mkutano wa SDG's. Picha:UN Photo/Mark Garten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kuwa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) ni mwongozo katika safari ya kuelekea mustakhbali bora zaidi. Ban amesema hayo akikutana na waandishi wa habari mjini New York, muda mfupi baada ya kupitishwa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na nchi wanachama. Akiitaja siku hii kama yenye kupewa [...]

25/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ajenda ya maendeleo endelevu ama SDGs yapitishwa

Kusikiliza / Picha ya Umoja wa Mataifa/ Cia Pak

Ajenda ya maendeleo endelevu au SDGs imepitishwa rasmi leo na nchi wanachama 193 ya Umoja wa Mataifa, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisema hatua kutoka kwa kila mtu duniani inahitajika. Amesema utashi wa kisiasa unahitajika, na pia ubia wa kimataifa ili kuhakikisha utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2030, ambayo inataka kuhakikisha [...]

25/09/2015 | Jamii: COP21, Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Rais Yoweri Museveni wa Uganda afungua rasmi mkutano wa SDGs

Kusikiliza / Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni akiongoza mkutano kuhusu idadi ya watu, tarehe 22 Septemba 2014, New York, Picha ya UN Photo/Kim Haughton

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema wakati mpya unaanza sasa katika jitihada za kutokomeza umaskini na kulinda sayari ya dunia. Museveni ambaye ni mwenyekiti mwenza wa mkutano wa ngazi ya juu kuhusu malengo ya maendeleo endelevu amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa cha kupitisha malengo hayo ambapo [...]

25/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yajipanga kwa janga la uhaba wa chakula Malawi

Kusikiliza / Watoto wakipanga foleni kusubiri mgao wa chakula shuleni nchini Malawi,huu ni mmoja wa mpango unaotumika kukabiliana na njaa(Picha ya WFP:Marielle Van Spronsen)

Shirika la mpango wa chakula duniani,  WFP linajipanga ili kuweza kutoa usaidizi wa kutosha kufuatia uhaba mkubwa wa chakula kuwahi kukumba Malawi katika kipindi cha muongo mmoja. Taarifa ya WFP imesema hatua hiyo inatokana la Rais Peter Mutharika wa Malawi kwa jamii ya kimataifa wakati akizindua mpango wa kitaifa wa kushughulikia uhaba wa chakula nchini [...]

25/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Papa Francis ahutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Papa Francis akihutubia baraza kuu la umoja wa mataifa. Picha: UN Photo/Eskender Debebe

Mara baada ya kuzungumza na wafanyakazi, Kiongozi wa Kanisa katoliki duniani Papa Francis amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likiwa na viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja huo kabla ya kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu. Priscilla Lecomte na taarifa zaidi. (Taarifa ya Priscilla) Nats.. Muongozaji akitambulisha viongozi wa dunia kwenye ukumbi wa [...]

25/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sababu saba zabainiwa kueleza wimbi la wakimbizi Ulaya

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria(Picha ya UNHCR)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limebaini sababu saba zinazoeleza ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaotafuta hifadhi barani Ulaya baada ya kukimbia machafuko nchini  Syria. Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Mkurugenzi wa UNCHR kwa ukanda wa Mashariki ya Kati Amin Awad amesema watu milioni minne wamekimbia Syria na [...]

25/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Papa Francis ahutubia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, New York

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Eskender Debebe

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amewasili katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo katika tukio la kwanza, amezungumza na wafanyakazi wa umoja huo. Akimkaribisha Papa Francis kuwahutubia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema ingawa ni yeye ndiye anayeonekana zaidi, ni [...]

25/09/2015 | Jamii: UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Wananchi wana imani na SDGs

Kusikiliza / Picha:Albert González Farranlbert González Farran

Kufuatia kupitishwa kwa ajenda ya maendeleo endelevu SDGs katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, baadhi ya wananchi kutoka ukanda wa Afrika Mashariki wanasema wana matumaini kuwa ajenda 2030 itainua ustawi wa jamii. Wakiongea katika mahojiano na Humprey Mgonja wa redio washirika SAUT ya Mwanza Tanzania wananchi hao wanasema.. (SAUTI WANANCHI)

25/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya Maendeleo Endelevu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

UNICEF yakaribisha kupitishwa kwa SDGs

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu UNICEF, Anthony Lake.(Picha:UM/JC McIlwaine)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika linalohusika na maslahi ya watoto, UNICEF, Anthony Lake, amekaribisha uamuzi wa kupitishwa kwa malengo ya maendeleo endelevu, SGDs, akiutaja kama mwisho wa mchakato na mwanzo wa jitihada za kugeuza ahadi kuwa vitendo. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Katika taarifa, Bwana Lake amesema ingawa hatua za maendeleo zitapimwa kwa [...]

25/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Papa Francis awasili makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Pope Francis akipokea maua kutoka kwa watoto baada ya kuwasili kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Mark Garten)

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis amewasili katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo kwa mujibu wa ratiba atakuwa na shughuli kadhaa ikiwemo kuzungumza na wafanyakazi wa umoja huo. Mara alipowasili amelakiwa na mwenyeji wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Papa Francis baada ya kukutana na [...]

25/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ethiopia na Senegal ni mfano wa mapinduzi ya viwanda Afrika:UNIDO

Kusikiliza / Mitaani katika soko la Sandaga, Senegal. Picha:UN Photo/Yutaka Nagata

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda duniani, UNIDO Li Yong amesema Ethiopia na Senegal zimeonyesha mfano wa jinsi mipango ya uendelezaji viwanda inayobuniwa na nchi husika inaweza kuleta mapinduzi ya viwanda barani Afrika na hivyo kufanikisha ajenda mpya 2030. Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa kuelekea kupitishwa kwa [...]

25/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Papa Francis kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo

Kusikiliza / Papa Francis akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. Picha kutoka Maktaba ya Umoja wa Mataifa.

Leo ikiwa ni siku ya kwanza ya mkutano wa kuridhia malengo ya maendeleo endelevu au SDGs ambao unajumuisha viongozi wa dunia mjini New York Marekani kwa siku tatu, Mkuu wa kanisa la katoliki Papa Francis anatarajiwa kutembelea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za kimataifa katika kutokomeza umaskini na [...]

25/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ushiriki wa jamii kwenye maendeleo ni siri ya mafanikio nchini Rwanda: Kagame

Kusikiliza / Raisi wa Rwanda Paul Kagame, @UN Photo/Paulo Filgueiras

Uhusiano baina ya raia na viongozi wao ni msingi katika kutimiza malengo ya maendeleo, amesema leo Rais wa Rwanda Paul Kagame akihudhuria kongamano la kimataifa kuhusu maendeleo endelevu lililofanyika jumatano na alhamis hii kwenye chuo kikuu cha Columbia mjini New York, Marekani. Kwenye hotuba yake aliyotoa mwisho wa mkutano huo uliohusisha Naibu Katibu Mkuu wa [...]

24/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, Malengo ya maendeleo ya milenia, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Harakati za mpito zaanza upya Burkina: Mjumbe wa Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Mohammed Ibn Chambas, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Afrika Magharibi. (Picha:UNOWA)

Mchakato wa mpito umeanza upya nchini Burkina Faso, amesema Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika Magharibi, Mohammed Ibn Chambas, akieleza kufuraishwa na kurejeshwa madarakani kwa Rais wa mpito Michel Kafando jumatano hii. Akiongea leo na Redio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Chambas amesema kwamba baraza la mawaziri litakutana ijumaa hii [...]

24/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

SDGS ni muhimu kwa ustawi wa nchi ninazoendelea: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.(Picha:UM/Amanda Voisard/Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema ajenda ya maendeleo endelevu SGDS inayozinduliwa  ijumaa hii jijini New York sio tu kwamba ni jumuishi lakini pia itatoa fursa kwa nchi zinazoendelea kupiga hatua  kupitia mipango ya ndani na sera. Akihutubia mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la nchi 77 na [...]

24/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuna uhusiano baina ya mizozo, umaskini na uhamiaji- Graziano da Silva

Kusikiliza / Mkulima kutoka Somalia. Picha: FAO/Frank Nyakairu

Mamilioni ya watu wanaolazimika kuhama makwao wakikimbia vita, umaskini na taabu nyinginezo, ni ukumbusho wa haja ya dharura ya kupata ufumbuzi wa amani kwa misingi ya haki ya kijamii na fursa bora za kiuchumi kwa wote. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo, FAO, José Graziano da Silva, ambaye pia amesema [...]

24/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Afrika inapaswa kuwa tayari kukabili ukuaji wa miji: Ban Ki-moon

Kusikiliza / Msongamano wa magari barabarani mjini Cairo, Misri.
Picha:UN Photo/B. Wolf

Bara la Afrika ndio sehemu ya dunia ambapo miji inakuwa kwa kasi zaidi, ameeleza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika mjadala maalum uliofanyika leo mjini New York Marekani, kuhusu Ajenda ya ukuaji wa miji barani Afrika. Katika hotuba yake, Bwana Ban amesema ukidhibitiwa na kuongozwa vizuri, ukuaji wa miji unaweza kuwa nyenzo [...]

24/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umuhimu wa Kaya miongoni mwa jamii ya Mijikenda ni dhahiri

Kusikiliza / Picha:UNESCO

Jamii ya Mijikenda ni kabila linalopatikana katika pwani ya kenya, na moja ya utambulisho wao ni Kaya- ikiwa misitu ambako wanaishi, na ambayo inatazamwa kama takatifu. Utamaduni huu unajumuisha pia maadili na usimamizi wa jamii. Licha ya umuhimu wake, kudidimia kwa raslimali ya ardhi na ukuaji wa miji ni tishio kwa tamaduni ambazo zinaendana na [...]

24/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani shambulizi la bombu msikitini, Yemen

Mkimbizi kutoka Syria(Picha UM/UNifeed/video capture)

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamelaani vikali mashambulizi ya bomu ya Septemba 24 kwenye msikiti mjini Sana'a, Yemen, ambalo lilisababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi. Katika taarifa, wajumbe hao wamepeleka ujumbe wa kuomboleza na rambirambi kwa familia na marafiki wa waliouawa na mejeruhi katika vitendo hivyo viovu, pamoja na kwa [...]

24/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sekta ya benki yaombwa kuchangia zaidi katika mabadiliko ya uchumi rafiki kwa mazingira

Kusikiliza / Gari linalotumia nishati ya umeme. Picha ya Umoja wa Mataifa/JC McIlwaine

Wakati ambapo watalaam wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi wanakutana wiki hii mjini New York, Marekani, Kamishna Mkuu wa France Strategie, idara ya mikakati na yanayotazamiwa ya Ufaransa, Jean Pisani, amesema ufadhili katika kubadilisha uchumi ili utumie gesi yenye uchafuzi mdogo unapaswa kuwa mkubwa na kuwa na mtazamo wa mbali. Amesema hayo akiongoza mjadala maalum [...]

24/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na Waziri Mkuu wa Australia

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Julie Bishop.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mashauriano leo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Julie Bishop, kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York. Katibu Mkuu na waziri huyo wa Australia wamejadili kuhusu ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu, na haja ya msingi ya kumulika utekelezaji wa [...]

24/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNAIDS yatoa wito kwa serikali na sekta ya dawa ziendeleze ahadi ya dawa nafuu

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé.(Picha:UM/Pierre Albouy)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Ukimwi, UNAIDS, limetoa wito kwa serikali na sekta ya kuunda dawa zihakikishe kuwa dawa zinaendelea kupatikana kwa watu wote, wakati viongozi wakikutana jijini New York kuridhia malengo ya maendeleo endelevu, yakiwemo malengo madogo kabambe yanayohusu afya ya umma. Kuongezeka kasi kwa gharama ya baadhi ya dawa [...]

24/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kila mtu ni mdau katika SDGs, hususan vijana- Ban

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Marco Dormino

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesisitiza leo umuhimu wa kuwaweka watoto na vijana katikati ya ajenda mpya ya maendeleo endelevu ya 2030. Ban amesema hayo katika hafla ya kuzindua chombo cha dijitali kitakachowawezesha watoto na vijana kutuma ujumbe wao moja kwa moja kwa viongozi wa dunia, wakikutana mjini New York kwa mkutano [...]

24/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yakaribisha tangazo la Ulaya kuongeza ufadhili kwa wakimbizi

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR António Guterres (Picha:UM/Jean-Marc FerrÃ)

Shirika la Umoja wa Mataifa  la kuhudumia wakimbizi UNHCR limekaribisha tangazo la baraza la Umoja wa Ulaya la kuongeza rasilimali kwa ajili ya misaada ya kibinadamu nchini Syria pamoja na kutoa hifadhi kwa watu 120,000. Taarifa ya UNHCR inasema uamuzi wa baraza la haki na mambo ya ndani la Ulaya kuhifadhi watu 120,000 halitatua tatizo [...]

24/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vifo huko Makka, Ban atuma rambirambi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon. (Picha MAKTABA-UM/Eskinder Debebe)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ametuma salamu za rambi rambi kwa familia, jamaa na serikali za mamia ya mahujaji waliofariki dunia huko, Makka Saudi Arabia wakiwa hija. Ban ametoa rambirambi hizo wakati wa mkutano wa mawaziri wa kundi la nchi 77 na China kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo. Amewatakia [...]

24/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sera madhubuti zahitajika kukabiliana na uhalifu kwa wanawake kupitia intaneti: Phumzile

Kusikiliza / Mwanamke kama huyo akiwa nchini DR Congo kunakoshuhudiwa mizozo ya mara kwa mara yuko hatarini ya unyanyasaji.(Picha:UM/Marie Frechon)

Licha ya Teknlojia ya Habari na Mawasiliano kuchangia pakubwa katika maendeleo duniani, wanawake bado wanakumbwa na changamoto chungu nzima zinatokana na mlipuko wa mtandao wa Intaneti. Hii ni kwe mujibu wa repoti iitwayo vita  dhidi ya wanawake na wasichana, wito kwa dunia kuchua hatua iliyoandaliwa na kikundi kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo ya [...]

24/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Balozi mwema wa UNICEF David Beckham aleta sauti za watoto kwa UM

Kusikiliza / David Beckham akiwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu Ban ki-moon. Picha kutoka kwa akaunti ya Twitter ya UNICEF.

Leo kwenye Umoja wa Mataifa, kimezinduliwa chombo cha aina yake kinacholeta sauti za watoto na vijana kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika hafla iliyoongozwa na Balozi Mwema wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, David Bekcham, Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake. Chombo hicho cha dijitali kilichoundwa na kamopuni [...]

24/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha makubaliano baina ya serikali ya Colombia na waasi wa FARC kuhusu wahanga

Kusikiliza / Watoto wakimbizi wa ndani nchini Colombia. Picha ya Umoja wa Mataifa/Mark Garten.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali ya Colombia na waasi wa FARC kuhusu masuala ya wahanga, hapo jana Septemba 23 mjini Havana, Cuba. Ban amepongeza pande zote kwa kutoa kipaumbele kwa maslahi ya waathiriwa katika mchakato wa amani. Taarifa ya msemaji wake imesema makubaliano hayo ni hatua [...]

24/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajenda 2030 na nuru kwa maisha ya watoto na vijana: Eliasson

Kusikiliza / Mtoto na mama yake baada ya kupewa matibabu hospitalini nchini Niger. Picha ya UNICEF/NYHQ2012-0156/Quarmyne.

Siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa kupitisha malengo ya maendeleo endelevu, Umoja wa Mataifa umekuwa na mkutano wa kuangazia malengo hayo na fursa zake kwa mtoto ambapo Naibu Katibu Mkuu Jan Eliasson amesema ajenda mpya inatoa nurukwa watoto. Assumpta Massoi na taarifa zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Watoto na malengo ya maendeleo endelevu, kumpatia [...]

24/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kilimo hai na utalii vyaweza kupunguza umaskini Tanzania:UNCTAD

Kusikiliza / Huyu ni nyati katika mbuga la wanayama la kitaifa la Mikumi nchini Tanzania.(Picha:UM/B Wolff)

Ripoti mpya ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema kilimo hai na utalii vikifanyika kwa pamoja vinaweza kukwamua Tanzania kutoka lindi la umaskini. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Ikiitwa kuimarisha uhusiano kati ya sekta ya utalii na kilimo nchini Tanzania, ripoti hiyo iliyotolewa leo imetokana na ufinyu [...]

24/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Heko Burkina Faso kwa kurejesha utawala wa mpito:Ban

Kusikiliza / Rais wa mpito Michel Kafando.(Picha:UM/Jenny Rockett)

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya kurejeshwa madarakani kwa rais wa serikali ya mpito nchini Burkina Faso, Michel Kafando sambamba na taasisi zake. Ban katika taarifa yake amesifu jitihada zilizofanikisha hatua  hiyo ikiwemo zile za jumuiya ya uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, jitihada ambazo amesema zimewezesha mzozo huo [...]

24/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malengo ya Maendeleo Endelevu yaangaziwa

Kusikiliza / SDG Goals Swahili-15

Leo ikiwa ni mapumiziko kwenye Umoja wa Mataifa kusherehekea sikukuu ya Eid Al Haji tunamulika malengo ya maendeleo endelevu SDG au ajenda 2030,  ambayo itaridhiwa rasmi mwisho wa wiki hii hapa New York Marekani. Katika mkutano huo wa ngazi ya juu ambapo viongozi wa dunia wanatarajiwa kushiriki wakiwemo Kiongozi wa kanisa katoliki duniani , Papa [...]

23/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ashish Thakkar aeleza matumaini yake kuhusu biashara barani Afrika

Kusikiliza / Ashish Thakkar akizindua kitabu chake kwenye duka la vitabu la Umoja wa Mataifa. Picha ya UN Photo/Kim Haughton

Wakati wa Afrika ni sasa! Hii ni kauli ya Ashish Thakkar, mfanya biashara mwenye uraia wa Uganda na Rwanda na mwenye asili ya India, ambaye ni miongoni mwa wawekezaji tajiri zaidi barani Afrika, leo akizindua kitabu chake kiitwacho “The Lion Awakes” yaani simba aamka. Bwana Thakkar ambaye pia ni mwenyekiti wa Kikao cha wafanyabiashara kwenye [...]

22/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shakira ashiriki na UNICEF kupigia debe maendeleo ya watoto wadogo

Kusikiliza / Balozi mwema wa UNICEF, Shakira. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Elimu ya awali, upendo na lishe bora ni misingi muhimu katika kuhakikisha akili za watoto wadogo zinakuwa vizuri. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF ambalo limekuwa na tukio maalum leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani, kwa ajili ya kumulika umuhimu wa [...]

22/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yaadhimisha siku ya amani

Kusikiliza / Maadhimisho ya siku ya amani nchini Sudan Kusini.(Picha:UNifeed/video capture)

Amani, amani, amani! Haya ni maneno yaliyosikika wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani ambayo kimataifa huadhimishwa kila Septemba 21. Maadhimisho yasiku hiyo yamefanyika pia nchini Sudan Kusini,  nchi ambayo imeshuhudia machafuko kwa takribani miaka mitatu. Ungana na Joseph Msami katika makala inayoelezea umuhimu tukio hili lilloshuhudia upazwaji wa sauti za kudai utulivu [...]

22/09/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuboresha mchakato wa uchaguzi wa Katibu Mkuu UM zaendelea

Kusikiliza / Nathalie Samarasinghe, Mkurugenzi mtandaji wa taasisi ya Umoja wa Mataifa nchini Uingereza, (UNA-UK). (Picha: UN/Amanda Voisard)

Tutahakikisha mchakato wa kumpata Katibu Mkuu ajaye wa Umoja wa Mataifa unakuwa wa wazi na shirikishi tofauti kabisa na ilivyokuwa tangu mwaka 1945. Ni kauli ya William Pace, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Global Policy aliyotoa wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani kuhusu mchakato wa kupatikana kwa kiongozi huyo wakati huu [...]

22/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM kutathmini hali ya wahamiaji Australia

Kusikiliza / François Crépeau.(Picha:UMJean-Marc Ferré)

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, François Crépeau, atafanya ziara nchini Australia kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 9, 2015, kufanyia tathmini8 programu za uhamiaji, sera na sheria zilizoundwa na Australia katika miaka ya hivi karibuni. Akitangaza ziara hiyo kwanza ya kukusanya taarifa nchini Australia, Bwana Crépeau amesema kuelewa jinsi [...]

22/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ajenda ya Maendeleo Endelevu 2030 itaendeleza gurudumu la MDGs- Bi Mohammed

Kusikiliza / Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo ya Milenia, SDGs, Amina Mohamed,. Picha: UN Photo/Mark Garten

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, Amina Mohammed, amesema kuwa wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha miaka 70 tangu kuanzishwa kwake, ni vyema kuwa umoja huo umeweka nguzo muhimu ya maendeleo, kwa kuunda ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030, ambayo malengo yake 17 yatapitishwa mwishoni mwa wiki [...]

22/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na mapigano na uharibifu Yemen

Kusikiliza / Mji wa kihistoria wa Sana'a nchini Yemen.(Picha:UNESCO/Maria Gropa)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameeleza kusikitishwa na mapigano na mashambulizi ya angani ambayo yamesababisha uharibifu zaidi katika miji ya Yemen, na kuongezeka hata zaidi kwa idadi ya wahanga wa kiraia katika siku chache zilizopita. Akikumbusha kuwa pande zote katika mzozo huo zina wajibu wa kuchukua tahadhari zote stahiki kuzuia vifo vya [...]

22/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Bangura akaribisha kufunguliwa mashtaka dhidi ya rais wa zamani wa Guinea

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono vitani. (Picha:UM/Mark Garten)

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika vita, Zainab Hawa Bangura amekaribisha kutangazwa leo kufunguliwa kwa mashtaka dhidi ya  aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Guinea, Moussa Dadis Camara katika muktadha wa uchunguzi wa matukio ya Septemba 28, 2009 . Katika taarifa, Bi Bangura amepongeza mamlaka ya kitaifa kwa [...]

22/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMID yaelekea kutimiza vigezo vyake, licha ya changamoto- Abdul Kamara

Kusikiliza / Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan, UNAMID, Abdul Kamara, kwenye ofisi yake. Picha ya Mohamad Almahady, UNAMID

Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan, UNAMID, amesema kuwa ujumbe huo umejitahidi kuboresha utendaji kazi wake katika kuwalinda watu wa Darfur, licha ya changamoto kubwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Katika mahojiano na Radio UNAMID, Bwana Abdul Kamara, ambaye anaondoka baada [...]

22/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Libya: Tumekamilisha kazi asema mwakilishi wa Ban Ki-moon

Kusikiliza / Bernadino Leon akiongea na waandishi wa habari mjini Skhirat, Morrocco. Picha ya UNSMIL.

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wka Libya, Bernadino Leon, amesema utaratibu wa mazungumzo ya amani umekamilishwa kazi imebakia kwa pande husika kwenye mzozo huo. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Bwana Leon amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Skhirat, nchini Morrocco, baada ya awamu nyingine ya mazungumzo [...]

22/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu lajadili haki za watu wa asili

Kusikiliza / Mkutano wa watu wa asili. Picha: UN Photo/Eskinder Debebe

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, limehitimisha leo mjadala wake wa siku mbili kuhusu hali za haki za binadamu zinazohitaji kumakinikiwa. Katika mjadala wake leo, Baraza hilo limesikiliza ripoti kuhusu haki za watu wa asili, zikiwasilishwa na mtaalam maalum kuhusu haki za kundi hilo, Victoria Tauli Corpuz, miongoni mwa wengine. Katika hotuba [...]

22/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Ulaya waipe umuhimu ajenda ya wakimbizi na wahamiaji: UNHCR

Kusikiliza / Picha: Alessandro Pesso

Wakati viongozi wa bara Ulaya wakikutana mjini Brussels Ubelgiji leo na kesho, Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, limewataka viongozi hao kuungana dhidi ya dharura ya janga la wakimbizi na wahamiaji ambalo linaongeza machafuko na lisilotabirika.Taarifa kamili na Abdullahi Boru. (Taarifa ya Abdullahi) Kwa mujibu wa UNHCR, hii ni fursa ya mwisho kwa [...]

22/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake na watoto kutoka Iraq wapatiwa makazi Ujerumani:IOM

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka eneo la Kurdistan, Iraq wakisubiri kusafirishwa na IOM. Picha: IOM 2014

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limewezesha wanawake na watoto 65 kutoka Dohuk na Erbil Iraq kupatiwa makazi huko Ujerumani. Hatua hiyo ni sehemu ya mpango unaofadhiliwa kwa pamoja na serikali ya Ujerumani na IOM ukiwa na lengo la kuona wahanga wa mzozo wa Iraq walio hatarini zaidi wanapatiwa hifadhi Ujerumani. Msemaji wa IOM Itayi [...]

22/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kay akaribisha uzinduzi wa baraza la Kitaifa la uchaguzi wa 2016 Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay(UN Photo/Rick Bajornas)

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia,  Nicholas Kay amekaribisha uzinduzi rasmi wa mchakato wa mashauriano kuhusu uchaguzi wa 2016 . Katika taarifa, Kay amesema anakaribisha makubaliano ya leo ya kuanzishwa kwa baraza la kitaifa kuhusu mchakato wa 2016, na kuongeza kuwa baraza hilo ni muhimu sana kwa juhudi za ujenzi [...]

21/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanachama wa Baraza la Usalama la UM Wapongeza washikadau wa kisiasa nchini Guinea Bissau

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama.(Picha:UM/Rick Bajornas)

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepata taarifa ya uteuzi wa tarehe 17 Septemba 2015, wa Carlos Correia, wa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Chama cha African Party for the Independence of Guinea and Cape Verde, PAIGC chama kikubwa cha kisiasa katika Bunge, kuwa Waziri Mkuu wa Guinea Bissau. Katika taarifa, [...]

21/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Majira ya baridi kali kuongeza machungu kwa wakimbizi Ulaya: Lykketoft

Kusikiliza / Picha:UNHCR/A.McConnell

Rais wa Baraza Kuu Umoja wa Mataifa Mogens Lykketoft amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani na kusema kuwa zahma inayokumba wakimbizi wanaosaka hifadhi barani Ulaya itakuwa kubwa zaidi wakati huu ambapo msimu wa baridi kali unakaribia. Amesema hali hiyo ya sasa ni janga kubwa dunia kuwahi kushuhudia tangu kumalizika kwa vita vikuu [...]

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon aiomba Ulaya ihurumie wakimbizi

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon.(Picha:UM/Maktaba/Devra Berkowitz)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameziomba nchi za Ulaya kuwajibika na kuwapokea wakimbizi wanaotafuta hifadhi barani Ulaya bila kuwarudisha mpakani au kuwatesa. Bwana Ban amesema hayo leo kwenye taarifa iliyotolewa na msemaji wake akieleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali ya mateso na ukiukaji wa haki unaokumba wakimbizi na wahamiaji wanaowasili Ulaya, akisisitiza [...]

21/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto 34 wamefariki dunia kwa utapiamlo Bentiu- OCHA

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Albert González Farran

Shirika la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, limesema leo kuwa watoto 34 walifariki dunia kutokana na utapiamlo katika kituo cha ulinzi wa raia, mjini Bentiu, jimbo la Unity, Sudan Kusini, katika wiki ya kwanza ya mwezi Septemba. Katika taarifa yake, OCHA imesema idadi hiyo inazidi kiwango wastani cha dharura, ambacho ni [...]

21/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Benki ya dunia yakomboa wavuvi na wakulima wa mwani Zanzibar

Kusikiliza / Mkulima wa mwani Zanzibar. (Picha:Video capture-Benki ya dunia)

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanaridhiwa baadaye mwezi huu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa na viongozi 193 wa nchi wanachama wa Umoja huo. Malengo hayo yako 17 na miongoni mwao ni lile namba moja linalohusika zaidi na kumaliza umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030. Huko Zanzibar nchini Tanzania, tayari Benki ya dunia imeona changamoto [...]

21/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa Intaneti wa kasi ya juu bado haupatikani kwa watu bilioni 4 duniani

Kusikiliza / Nchini Uganda, wasichana wanatumia mtandao Intaneti shuleni kupitia nishati ya jua. Picha ya SEED intiative.

Bado asilimia 57 ya watu duniani kote hawawezi kutumia Intaneti kupitia mtandao wenye kasi ya juu zaidi yaani broadband. Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Kamisheni ya Broadband kwa ajili ya maendeleo endelevu iliyotolewa leo, ikisema kwamba waliokosa mtandao huu ni watu wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea na ambao wangenufaika zaidi na mtandao huo katika [...]

21/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulaya sasa inalipa gharama mzozo wa Syria: Pinheiro

Kusikiliza / Familia ya wakimbizi wa Syria wakilala barabarani nchini Uturuki. Picha ya UNHCR/S. Baldwin

Mwenyekiti wa Kamisheni ya uchunguzi kuhusu Syria, Paulo Pinheiro, amelieleza Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kwamba taifa la Syria limefilisika kutokana na zaidi ya miaka minne ya vita huku jamii ya kimataifa ikishuhudia. Akiwasilisha ripoti yake mbele ya Baraza hilo mjini Geneva, Uswisi, Bwana Pinheiro amesema vita hivyo vikali vimeharibu umoja [...]

21/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ikiadhimisha siku ya amani, Burundi yatakiwa kurejesha utulivu

Kusikiliza / Bendera ya Burundi. (Picha:MAKTABA)

Barani Afrika nchini Burundi maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani yamefanyika huku sauti ya uwepo na amani ya kudumu ikipazwa kufuatia machafuko ya kisiasa katika  siku za hivi karibuni. Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga anatupasha kutoka Bujumbura (TAARIFA YA KIBUGA)  

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila mtu ana jukumu la kulinda amani: Balozi Mulamula

Kusikiliza / Wakati wa maadhimisho ya siku ya amani duniani nchini Tanzania.(Picha:Idhaa a Kiswahili/Stella Vuzo)

Nchini Tanzania nako kumefanyika maadhimisho ya siku ya amani duniani yakishirikisha taasisi mbali mbali ikiwemo Umoja wa Mataifa na wadau wake huku vijana wakichagiza nafasi ya kila mmoja kwenye ujenzi wa amani.. Nats.. Mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Liberata Mulamula ambaye amesema amani inapaswa [...]

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

McDonald’s na Mashirika mengine yashiriki kwenye kampeni ya kuunga mkono WFP

Kusikiliza / Picha:WFP

Leo ikiwa ni siku ya Amani Duniani, mashirika ya sekta binafsi yameshirikiana kwa ajili ya kusaidia jitihada za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula(WFP). Taarifa kamili na Abdullahi Boru.. (Taarifa ya Abdullahi) Lengo la ushirika huo wa sekta binafsi ni kusisitiza umuhimu wa usaidizi wa chakula katika kukuza amani duniani, mkuu wa [...]

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna maendeleo, lakini bado kuna kazi kuhusu Mpango wa Nyuklia Wa Iran, IAEA

Kusikiliza / Yukiya Amano.(Picha:IAEA)

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA, Yukiya Amano ameelezea bodi ya shirika hilo kuhusu ziara yake ya mwishoni mwa wiki nchini Iran, ambapo alifanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Hassan Rouhani na wakuu wengine wa serikali sambamba na wabunge. Kwa maelezo zaidi, huyu hapa Grace Kaneiya. (Taarifa [...]

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mizozo yazidi kusambaratisha dunia: Ban

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Paulo Filgueras

Leo ni siku ya amani duniani ambapo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameongoza katika tukio hilo la kila mwaka akisema mizozo inazidi kuigawa dunia na hali ya binadamu inakuwa mashakani. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Nats.. Tumbuizo katika bustani za Umoja wa Mataifa jijini New York, [...]

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

IAEA na mkakati wa kuongeza wanawake katika sayansi ya nyukilia

Kusikiliza / Picha@IAEA

Licha ya kuongezeka kwa idadi ya wanawake katika fani ya nyuklia  Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, linasema idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na wanaume, hasa kwa kulinganisha pengo kati ya wahitimu wa vyuo vikuu katika fani hiyo. Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Janice [...]

21/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serikali watumieni vijana kujenga amani na ustawi duniani:Ban

Kusikiliza / Nembo ya siku ya amani duniani. (Picha:UM)

Ingawa matarajio ya amani yanaonekana kuwa mbali katika dunia ya sasa iliyokumbwa na mizozo na mapigano, bado ndoto ya amani inadunda katika maisha ya watu kila pahali duniani. Ni sehemu ya ujumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliotoa kuelekea siku ya amani duniani tarehe 21 mwezi huu wa Septemba. Ban amesema [...]

21/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtalaam wa UM atoa wito kwa ajili ya watoto wa Yemen

Kusikiliza / Watoto nchini Yemen. Picha: UNICEF

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto kwenye mizozo, Leila Zerrougui amesema ni muhimu sana Baraza la Usalama na jamii ya kimataifa wakuze mazugumzo ya kisiasa ili kumaliza mzozo unoathiri watoto nchini Yemen. Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Bi Zerrougui amesema idadi ya vifo na mateso dhidi ya watoto imeongezeka sana mwaka [...]

20/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon alaani mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.(Picha: Maktaba UN/Evan Schneider)

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya roketi dhidi ya Israel yaliyofanywa hivi karibuni na wapalestina wenye itikadi kali kutoka Gaza. Kwenye taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake, Bwana Ban amenukuliwa akieleza wasi wasi wake kuhusu mashambulizi hayo dhidi yya makazi ya raia akisema mwelekeo wao ni hatari na [...]

20/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto wathiriwa pakubwa na vita nchini Yemen, UNICEF

Hapa ni Taiz Yemen wasichana wakienda kuteka maji.(Picha:OCHA/Abdulelah Taqi)

Vifaa muhimu vya maji  vilivyonuiwa kuwasaidia watu 11,000 katika maeneo yaliyoathiriwa pakubwa na vita nchini Yemen vimeharibiwa jana baada ya ghala linalotumiwa na shirika la kibinadamu katika mji wa Dhamar kusini mwa mji mkuu wa Yemen, Sana’a kuharibiwa katika shambulizi la bomu. Katika taarifa, Kaimu Mwakilishi wa UNICEF nchini Yemen, Jeremy Hopkins amesema, UNICEF imesikitishwa [...]

18/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wasanii wa Afrika watunga wimbo wa kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya maendeleo

Kusikiliza / Diamond akiwa anaimba wimbo wa "Tell Everybody". Picha ya Tarryn Hatchett

Katika kuelekea kuridhia malengo ya maendeleo endelevu mwisho wa mwezi Septemba, wimbo mpya uitwao "Tell Everybody" umezinduliwa hivi karibuni na kampeni ya Global Goals Afrika. Wimbo huo ulitengenezwa na watayarishaji kutoka Kenya, David King Muthami, Msumbiji, Ellputo na Nigeria, Cobhams Asuquo, ukihusisha wasanii wa Afrika wakiwemo Diamond kutoka Tanzania, Mafikizolo kutoka Afrika Kusini na Sauti [...]

18/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuwawezesha wanawake katika nafasi za maamuzi

Kusikiliza / Spika wa Uganda Rebecca Kadaga.(Picha:UM/Kim Haughton)

Malengo ya maendeleo ya milenia MDGs, yanafikia ukomo wake mwezi huu mjini New York kwa kuwaleta pamoja wawakilishi wa nchi mbalimbali kutahimini utekelezaji wa malengo hayo na kisha kupitisha ajenda mpya ya maendeleo endelevu yaani SDGS au ajenda 2030. Moja ya MDGs ni lengo namba  tatu ambalo ni usawa wa  kijinsia. Lengo hili  linalenga mbali [...]

18/09/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hungary zingatia haki za watoto wakimbizi: UNICEF

Kusikiliza / Picha: UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, linawasiliana na mwakilishi wa kudumu wa Hungary kwenye Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kujadili jinsi ya kulinda watoto wakimbizi na wahamiaji wanaoingia nchini humo. Taarifa ya UNICEF inasema mazungumzo hayo yanaangalia jinsi watoto wakimbizi na wahamiaji wanaweza kulindwa kwa mujibu wa ahadi za nchi [...]

18/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kamishna Mkuu wa UNRWA Pierre Krähenbühl azuru Syria

Kusikiliza / Pierre Krahenbul, Kamishna Mkuu wa UNRWA. Picha: UNRWA

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA, Pierre Krähenbühl, hapo jana amehitimisha ziara yake ya siku tatu nchini Syria, ambako alikutana na wakimbizi wa Kipalestina, wafanyakazi wa UNRWA na maafisa wa serikali. Akiwa mijini Homs na Damascus, Bw. Krähenbühl alielezea shukrani na mshikamano wake kwa kazi ya ujasiri na [...]

18/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tumepiga hatua za ubia kwa maendeleo, lakini bado kuna mianya- Ban

Kusikiliza / Picha: UNDP Philippines | #GlobalGoals

Ripoti mpya iliyozinduliwa leo kuhusu lengo namba nane la maendeleo ya milenia, imeonyesha kuwa, licha ya ufanisi uliopatikana katika kufikia malengo kadhaa, bado kuna mianya mikubwa katika kupunguza hatari zinazozikumba nchi maskini, nchi zisizo na pwani na nchi za visiwa vidogo zinazoendelea. Ripoti hiyo iitwayo, "Tathmini ya Ubia wa Kimataifa kwa Maendeleo," imeandaliwa na kikosi [...]

18/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa ionyeshe ukarimu kama Niger: Lanzer

Kusikiliza / Picha:UN Photo/WFP/Phil Behan

Mkuu wa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Sahel, Toby Lanzer ametaka jumuiya ya kimataifa kuonyesha ukarimu kama unaoonyeshwa na nchi mathalani Niger zinazopokea wakimbizi wanaofurushwa kutoakana na machafuko ya kigaidi nchini Nigeria. Akiongea mjini Geneva msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadmau OCHA Jens Larke amesema Bwana Lanzer amekaribisha [...]

18/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi Nigeria yasambaratisha watoto zaidi ya Milioni 1.4

Kusikiliza / Wakimbizi wa Nigeria waliokimbia mapigano ya jimbo la Borno; PIcha ya IRIN/Anna Jefferys

Nchini Nigeria kasi ya ongezeko la mashambulizi kutoka wka kikundi cha Boko Haram kimesababisha watoto zaidi ya Milioni Moja na Laki Nne kukimbia makwao nusu yao wakiwa na umri wa chini ya miaka mitano. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kiwango hicho ni [...]

18/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa wamulika madhara ya dawa za kulevya kwa jamii

Kusikiliza / Madawa ya kulevya(Picha ya UM/Victoria Hazou)

Wawakilishi wa serikali na wataalam kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, pamoja na mashirika ya kikanda na asasi za kiraia, wanakutana mjini Mexico kubadilishana mawazo kuhusu uzoefu wao katika kukabiliana na madhara ya masoko haramu ya dawa kijamii, kama vile ukatili, misongamano ya watu jela, utelekezaji na kudhoofika kwa mifumo ya kijamii. Mkutano huo wa [...]

18/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Muda unayoyoma kwa Ulaya kutatua mzozo wa wakimbizi: UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wasubiri kuchukua basi kuelekea Hungary baada ya kuvuka mpaka kutoka Serbia.(Picha© UNHCR/O.Laban-Mattei)

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema muda unayoyoma kwa bara la Ulaya kushughulikia sakata la wakimbizi na wahamiaji na kwamba hali iliyopo sasa inaweza kutumbukiza wasaka hifadhi hao kwenye mikono ya wasafirishaji haramu. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, msemaji wa UNHCR Adrian Edwards [...]

18/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Feltman ahutubia Baraza la usalama kuhusu Burkina Faso

Kusikiliza / Mkuu wa masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman akihutubia Baraza la Usalama(Picha MAKTABA: UN/Devra Berkowitz)

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi huko Burkina Faso, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao ambapo wajumbe wamepokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa masuala ya siasa kwenye umoja huo Jeffrey Feltman. Abdullahi Boru na maelezo kamili. (Taarifa ya Abdullahi) Kikao hicho kilikuwa cha dharura ambapo baada ya kukamilika wajumbe walitoa taarifa inayolaani kitendo [...]

18/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hungary inavunja sheria ya kimataifa kwa kufurusha wakimbizi: Zeid

Kusikiliza / Wakimbizi wakisimama mbele ya polisi nchini Hungary. Picha ya UNHCR/ Mark Henley

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein amesema amesikitishwa sana na vitendo vilivyofanywa na serikali ya Hungary na mamlaka zake za kuwakataza wakimbizi kuingia nchini humo, kuwafunga na kutumia nguvu dhidi yao, akisema baadhi ya vitendo vyao vinaweza kuwa ni ukiukaji wa sheria ya kimataifa. Kamishna Zeid amesema hayo kwenye taarifa iliyotolewa [...]

17/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ubia wa serikali na sekta binafsi waweza fanikisha ufadhili wa SDG

Kusikiliza / Lengo la tisa linalohimiza uundaji wa miundomsingi thabiti na kusisitiza ubunifu.(Picha@UM)

Wakati malengo ya maendeleo endelevu, SDG au ajenda 2030 ikitarajiwa kuridhiwa na wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wiki ijayo mjini New York, Marekani bado inelezwa kuwa kisichoeleweka ni  jinsi ya kupata mabilioni ya pesa ya kugharamia malengo hayo. Njia mojawapo inayoangaziwa ni kuhamasisha uwekezaji wa sekta ya kibinafsi katika kujenga miundombinu, barabara, [...]

17/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza mamlaka ya UNMIL hadi Septemba 30, 2016

Kusikiliza / Walinda amani nchini Liberia. Picha ya UNMIL/Staton Winter

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja wamepitisha azimio la kuongeza muda wa mamlaka ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia, UNMIL, hadi Septemba 30, mwaka 2016. Miongoni mwa mamlaka ya ujumbe huo, itakuwa ni ulinzi wa raia, kufanyia marekebisho taasisi za sheria na usalama, kuendeleza haki za [...]

17/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kuna dalili njema kuelekea COP 21 : Jonas

Kusikiliza / Mabadiliko ya tabianchi yanaathiri kilimo na maisha ya wakulima duniani kote. Picha ya FAO/L. Dematteis

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha uwasilishwaji wa mikakati kutoka nchi wanachama katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, mikakati ianayoelezwa kujenga msingi kuelekea katika mkutano wa makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP 21, utakaofanyika mjini Paris mwezi Disemba. Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu mabadiliko [...]

17/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Bangura ahimiza kuwatafuta na kuwarejesha wasichana Wayazidi waliotekwa na ISIL

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM kuhusu ukatili wa kingono vitani. (Picha:UM/Loey Felipe)

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika vita, Zainab Hawa Bangura, ametoa wito wa usaidizi katika kuwasaka na kuwarejesha nyumbani wasichana wa jamii ya Yazidi waliotekwa na kundi linalotaka kuweka dola la Uislamu wenye itikadi kali, ISIL. Bi Bangura ametoa wito huo wakati akikutana leo nchini Ujerumani na [...]

17/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Licha ya mazingira magumu, Aqeela ajitoa kwa hali na mali kumkomboa mtoto wa kike.

Kusikiliza / Bi. Aqeela Asifi akiwa katika moja ya madarasa akifundisha watoto wa kike. (Picha: Unifeed Video capture)

Suala la mtu kuwa ukimbizini ni tatizo kubwa na upatikanaji wa mahitaji muhimu kama vile chakula na malazi unakuwa ni adimu. Hali inakuwa mbaya zaidi kwenye suala la elimu tena ikiwa ni mtoto wa kike hasa kwenye maeneo ambayo mila, imani na tamaduni potofu zimeshika kasi kukwamisha watoto hao kupata haki yao hiyo ya msingi. [...]

17/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria ifuate mkondo kudhibiti unyanyasaji wa kingono mizozoni: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.(Picha:UM/Mark Garten)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ni lazima kuwa thabiti katika kuchukua hatua stahiki dhidi ya tuhuma za unyanyasaji wa kingono zinazofanywa na walinzi wa amani au wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika maeneo mbalimbali. Akizungumza katika mkutano wa nchi zinazochangia vikosi vya ulinzi wa amani vya umoja huo, Ban amesema ni [...]

17/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS na Kenya wazindua ushirikianao wa habari na teknolojia ili kuangamiza ukimwi 2030

Kusikiliza / Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Mkuu wa UNAIDS Michel Sidibe kwenye uzinduzi wa ushirikiano wao nchini Kenya. Picha ya UNAIDS.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibé wameanzisha chombo kipya bunifu cha kufuatilia na kubaini upungufu katika programu ya kupambana na Ukimwi nchini Kenya. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte (Taarifa ya Priscilla) Chumba hicho cha kufuatilia hali ya Ukimwi Kenya, [...]

17/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nyuklia yatumiwa kuimarisha uzalishaji wa kilimo nchini Kenya

Kusikiliza / Picha©FAO/Ami Vitale

Teknolojia za nyuklia zinaweza kuchangia katika kukuza sekta ya kilimo rafiki kwa mazingira, kwa kuzuia momonyoko wa ardhi, kuimarisha uzalishaji na matumizi ya maji. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Umoja wa Mataifa IAEA, linalokutana mjini Vienna, Austria  wiki hii kwa ajili ya kongamano lake la kila mwaka. Mwaka huu [...]

17/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jeshi Burkina Faso lisiyumbishe mchakato wa kisiasa: IPU

Kusikiliza / Nembo ya IPU

Umoja wa mabunge duniani, IPU umelaani mapinduzi ya serikali ya mpito nchini Burkina Faso sanjari na kupelekwa mrama kwa mchakato wa kurejesha utawala wa kidemokrasia nchini humo. Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa IPU Martin Chungong ametaka kurejeshwa haraka na kwa amani mchakato wa kidemokrasia utakaohitimishwa na uchaguzi huru na haki wa rais na wabunge [...]

17/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burkina Faso: Zeid alaani mapinduzi ya kijeshi

Kusikiliza / Rais wa mpito Michel Kafando.(Picha:UM/Jenny Rockett)

Kufuatia jeshi huko Burkina Faso kutangaza mapinduzi, Kamishna Mkuu wa haki za binadamu ndani ya Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na kitendo hicho. Katika taarifa yake, Kamishna Zeid pamoja na kulaani amesema kitendo cha kushikiliwa kwa Rais wa mpito Michel Kafando na Waziri Mkuu Isaac Zida hakikubaliki. Viongozi [...]

17/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Malaria yatia matumaini, lakini Afrika bado kuna kazi: Ripoti

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon alipotembelea kijiji kimoja huko Malawi mwaka 2010 kujionea harakati za matumizi ya vyandarua kudhibiti Malaria. (Picha:UN/Evan Schneider)

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema lengo la kubadili mwelekeo wa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria ifikapo mwaka 2015 limefanikiwa katika hali inayotia ushawishi mkubwa, ingawa bado mabilioni wako hatarini. Ripoti hiyo ya shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la afya WHO inazinduliwa Alhamisi ikiwa ni siku chache kabla [...]

17/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani kuzuiliwa kwa Rais wa Burkina Faso, Waziri Mkuu na mawaziri wengine

Kusikiliza / Baraza la Usalama (Picha ya UM/Maktaba)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatano jioni limelaani vikali kukamatwa na kuzuiliwa kwa Rais Michel Kafando na Waziri Mkuu, Isaac Zida wa Burkina Faso, pamoja na mawaziri kadhaa, likitaka waachiliwe wakiwa salama mara moja. Katika taarifa, wajumbe wa Baraza la Usalama wamesisitiza kuwa kuzuiliwa kwa viongozi hao na mawakala wa Régiment de sécurité [...]

16/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ataka rais wa Burkina Faso na Waziri Mkuu waachiliwe mara moja

Kusikiliza / Secretary-General Ban Ki-moon (right) meets with Michel Kafando, President of Burkina Faso, in Addis Ababa, Ethiopia, 30 January 2015. UN Photo/Eskinder Debebe (file)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ameeleza kusikitishwa na kutekwa na kuzuiliwa kwa Rais Michel Kafando na Waziri Mkuu, Yacouba Isaac Zida wa Burkina Faso, pamoja na mawaziri kadhaa wa kitaifa, ambako kumefanywa na Régiment de Sécurité Présidentielle leo mjini Ouagadougou. Taarifa ya msemaji wake imesema, Katibu Mkuu ametoa wito waachiliwe mara moja [...]

16/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yalaani vikali mashambulizi dhidi ya watoto Mjini Allepo, Syria

Kusikiliza / Mwanamke mkimbizi wa Syria na mtoto wake katika kambi ya Zaátari. Picha:UNHCR/S. Malkawi

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF limelaani vikali mashambulizi ya makombora yaliyofanyika jana katika maeno ya raia mjini Aleppo ambapo angalau watoto 19 waliuawa ikiwa ni pamoja watoto sita waliokuwa katika eneo salama linalofadhiliwa na shirika la UNICEF. Katika taarifa, UNICEF imesema shambulizi hili la kukemewa linaonyesha kwamba hata kitendo rahisi cha [...]

16/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Juhudi zaidi zahitajika kushughulikia mizizi ya kinachowafurusha watu makwao- O'Brien

Kusikiliza / Wakimbizi wengi wanomiminika Ugiriki nipamoaj na hawa wa Syria Picha ya UNHCR/B. Szandelszky (Maktaba)

Mratibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Stephen O'Brien, amesema leo kuwa Hatma ya Wasyria wanaojaribu kuingia Ulaya imeonyesha kuwa madhara ya mzozo wa Syria siyo tu kwa taifa au ukanda, bali ni ya kimataifa. Akisema kuwa mgogoro wa Syria umeibua moja ya mmiminiko mkubwa zaidi wa wakimbizi tangu vita vikuu vya [...]

16/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya sasa ya UNCTAD ni tofauti na za awali : Kituyi

Kusikiliza / Dr. Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD. (Picha@UN/Jean-Marc Ferré)

Katibu Mkuu wa shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema ripoti mpya ya kila baada ya miaka minne  iliyozinduliwa  mapema wiki hii inakwenda sambamba na  mipango ya maendeleo endelevu SDGs inayotarajiwa kupitishwa hivi karibuni na nchi wanachama. Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa idhaa hii Bwana Kituyi amesema pia [...]

16/09/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Harakati za kujikwamua kutokana na utegemezi wa mshahara nchini Uganda

Kusikiliza / DK. Kalinaki amefika hospitalini kutoka shambani majira ya asubuhi.(Picha;Idhaa ya Kiswahili/John Kibego)

Malengo 17 ya Maendeleo endelevu yakisubiriwa kuridhiwa mwezi huu wa Septemba, Daktari mmoja nchini Uganda amejihusisha moja kwa moja katika kilimo kwa nia ya kuhakikisha usalama wa chakula, na kuepuka utegemezi wa mshahara ambao anasema ni duni kulingana na mahitaji ya familia yake.Kupata zaidi, unngana na John Kibego katika makala ifuatayo.

16/09/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya mwanahabari wa Colombia, Flor Alba Núñez Vargas

Kusikiliza / Mkurugenzi mkuu wa UNESCO, Irina Bokova. Picha:UNESCO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Irina Bokova, amelaani leo mauaji ya mwanahabari wa Colombia, Flor Alba Núñez Vargas katika mji wa Pitalito, kusini mwa Colombia, mnamo Septemba 10. Akilaani mauaji hayo, Bi Bokova amesema vyombo huru vya habari na jamii huru huenda bega kwa bega, na kwamba mashambulizi dhidi ya moja [...]

16/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

#UNGA inafanyika kukiwa na mkanganyiko na matumaini: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.(Picha: Maktaba UN/Evan Schneider)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema mkutano wa 70 wa Baraza kuu la Umoja huo unafanyika wakati dunia iko katika kipindi mkanganyiko na matumaini. Akizungumza na waandishi wa habari hii leo kabla ya kuanza kwa mikutano ya ngazi ya juu ya baraza hilo hapo wiki ijayo, Ban amesema ni mkanganyiko kwa kuwa [...]

16/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu, UN 70, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Nishati inaunganisha ukuaji wa uchumi, usawa wa kijamii na ubora wa mazingira- Ban

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Derek Lovejoy

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema leo kuwa nishati ndio uzi muhimu unaounganisha ukuaji wa uchumi, usawa katika jamii na ubora wa mazingira. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Katibu Mkuu amesema hayo wakati wa mkutano kuhusu Nishati Endelevu kwa Wote, akisifu kujumuishwa kwa lengo nambari saba kuhusu nishati katika [...]

16/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Dakika 150 za mazoezi kila wiki zaweza kukuepusha na ugonjwa wa moyo : WHO

Kusikiliza / Mazoezi ya yoga.(Picha:UM/Pasqual Gorriz)

Shirika la Afya Duniani WHO ukanda wa Ulaya limezindua leo mkakati wa kukuza mazoezi ya viungo kwa kipindi cha miaka kumi, hadi mwaka 2025. Mkakati huo mpya unalenga kuhamasisha wakazi wa  nchi 53 ikiwemo ukanda wa Ulaya kuongeza muda wao wa kufanya mazoezi na hivyo kuishi maisha bora na marefu zaidi. Kwenye taarifa iliyotolewa leo, [...]

16/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji mkubwa wa haki ulifanyika Sri Lanka: Ripoti

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein. (Picha:UN /Jean-Marc Ferré)

Ripoti iliochapishwa leo na Umoja wa Mataifa imebainisha mfumo wa ukiukaji wa haki za kibinadamu uliokithiri nchini Sri Lanka kati ya 2002-2011, huku ikidhiirisha uwezekano wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutekelezwa na pande zote mbili katika mgogoro. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye [...]

16/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utunzaji wa tabaka la ozoni ni mfano wa kuigwa: Ban

Kusikiliza / Hapa ni mjini Ny-Ålesund nchini Norway.(Picha:UM/Mark Garten)

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya utunzaji wa tabaka la ozoni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon amesema jinsi dunia ilivyoweza kudhibiti tundu lililokuwepo kwenye tabaka hilo kwa kupunguza matumizi ya gesi aina ya CFCs ni mafanikio makubwa yanayopaswa kuigwa wakati wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi. Taarifa zaidi na Joshua Mmali. [...]

16/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UNCTAD imekuja wakati muafaka kuelekea SDGs:Kituyi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, Mukhisa Kituyi.(Picha:UM/Jean-Marc Ferre)

Katibu Mkuu wa Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amesema ripoti ya shirika hilo imekuja wakati muafaka ambapo nchi zinatarajiwa kuridhia maendeleo endelevu SDGs, baadaye mwezi huu. Akihojiwa na Idhaa hii baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo iitwayo "Kutoka maamuzi hadi hatua"amesema ni mujarabu kwani inataja mambo manne [...]

16/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Inasikitisha kambi za wakimbizi wa ndani zinaposhambuliwa: Beyani

Kusikiliza / Wakimbizi wa Nigeria wahofia kushambuliwa. Picha ya UNHCR/D.Mbaiorem

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Chaloka Beyani, amelaani vikali shambulio la kikatili kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani huko Yola, Kaskazini mwa Nigeria. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia. (Taarifa ya Grace) Kambi hiyo ni makazi ya wakimbizi 32,000 ambapo Beyani amesema shambulio hilo la kwanza tangu kuanza kwa mzozo kaskazini mwa [...]

16/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuzo za nchi za kusini mwa dunia kuwaleta pamoja nyota wa muziki na filamu

Kusikiliza / Mshindi wa tuzo ya Oscar, Forest Whitaker.(Picha:UM/Mark Garten)

  Tuzo za mwaka 2015 za nchi za kusini mwa dunia zinatazamiwa kuwaleta pamoja wana Sanaa maarufu, wakiwemo wacheza filamu wa Hollywood, Robert De Niro na Michael Douglas, ambao watasaidia kupaazia sauti ufanisi wa ushirikiano wa nchi za kusini mwa dunia, kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, pamoja na kupitishwa kwa ajenda mpya ya [...]

15/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Rais wa UNGA70 aangazia vipaumbele na mtazamo kuhusu Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban(kushoto) na Rais wa Baraza Kuu Mogens Lykketoft (kati). Picha:UN Photo/Eskinder Debebe

Ni Rais wa mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mogens Lykketoft kutoka Denmark akitangaza kufunguliwa rasmi wa kikao cha kwanza cha mkutano huo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani siku ya Jumanne. Tangazo hilo lilifuatiliwa na dakika moja ya wajumbe kusimama na kuwa kimya ikiwa ni [...]

15/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

Misitu yatajwa kama sehemu muhimu ya kuwezesha maisha

Kusikiliza / Misitu(Picha@FAO)

Inakadiriwa kwamba takriban watu Bilioni 2.4 kote ulimwenguni wanategemea misitu kwa ajili ya huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula , kuni, mbao, dawa na ajira bila kusahau kuwa ni chanzo  cha kipato. halikadhalika, muhimu kwa maisha ya theluthi moja ya watu ambao wanaishi vijijini na mijini vilevile, wanawake kwa waume, vijana kwa wazee. Ni kwa [...]

15/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Bi. Gamba kutoka Argentina kuongoza chombo cha uchunguzi kuhusu silaha

Kusikiliza / Virginia Gamba.(Picha:UM/Paulo Filgueiras)

Katibu mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Virginia Gamba kutoka Argentina kuongoza chombo cha uchunguzi cha pamoja cha umoja huo na shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali OPSCW. Chombo hicho, JIM kiliundwa hivi karibuni kufuatia azimio namba 2235 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu matumizi ya silaha za [...]

15/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watoto nchini Syria wakosa elimu: UNICEF

Kusikiliza / Mtoto nchini Syria. Picha ya WFP/Abeer Etefa

Zaidi ya watoto milioni mbili nchini Syria hawataingia shuleni mwaka huu, wakati ambapo shule zinafunguliwa upya, limesema leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudhumia Watoto UNICEF. Kwenye taarifa iliyotolewa leo, UNICEF imesema watoto wengine 400,000 wako hatarini kuacha shule mwaka huu kutokana na ghasia na vita. Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi [...]

15/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu lajadili kujumuishwa suala la jinsia katika kazi yake

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Kay Muldoon

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo Jumanne limefanya mkutano wake wa kila mwaka kuhusu kujumuisha suala la jinsia katika kazi yake yote na katika mikakati yake, kwa kumulika usawa wa jinsia. Rais wa Baraza hilo, Joachim Rücker, amesema wanawake wanawakilisha watu bilioni 3.5 duniani, au zaidi ya asilimia 50 ya idadi [...]

15/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtalaam wa UN akariri tahadhari yake kuhusu Burundi

Kusikiliza / Mtaalam maalum  wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya mpito Pablo de Greiff(Picha ya UM/Violaine Martin)

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya mpito Pablo de Greiff amesema mwelekeo wa Burundi sasa ni kinyume na mafanikio yaliyopatikana tangu makubaliano ya amani ya Arusha ya mwaka 2000. Akiwasilisha ripoti yake kuhusu ziara yake nchini humo katika Baraza la Haki za Binadamu linaloendelea mjini Geneva Uswisi, Bwana De Greiff amesema desturi [...]

15/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Balozi Mwema wa UNICEF, David Beckham ataka viongozi watokomeze ukatili dhidi ya watoto

Kusikiliza / Mwanasoka David Backham akitembelea watoto nchini Cambodia. Picha ya UNICEF/UKLA2015-00053/Irby

Balozi Mwema wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, David Bekham, anapigia chepuo barua iliyoandikwa na manusura kumi na wanane wa ukatili dhidi ya watoto, ikitoa wito kwa viongozi duniani kutokomeza unyanyasaji wa watoto ulioenea, na ambao unaathiri mamilioni ya watoto kote duniani. Taarifa kamili na Joshua Mmali (Taarifa ya Joshua) Mmoja wa watoto waliosaini barua [...]

15/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali zinazojiamini hutoa fursa ya demokrasia kwa raia: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon. (Picha MAKTABA-UM/Eskinder Debebe)

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya demokrasia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemulika maudhui ya mwaka huu yakiwa ni nafasi ya jamii, akilinganisha jamii na oksijeni kwenye demokrasia bila hiyo itakufa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Katika ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video, Bwana Ban amesema kwenye [...]

15/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yasikitishwa na ufurushaji wa wakimbizi wa ndani Bangui

Kusikiliza / Wakimbizi mjini Bangui nchini CAR.(Picha:OCHA/Gemma Cortes)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Aurélien A. Agbénonci na wadau wa kibinadamu nchini humo, wameeleza kusikitishwa na kufurushwa kwa wakimbizi wa ndani 114 kutoka kituo cha Saint Jean Gabaladja mjini Bangui, mnamo Septemba 12. Bwana Agbénonci amesema kuhamishwa kwa watu waliolazimika kuhama makwao ni lazima kufanyike kwa misingi [...]

15/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuzo ya NANSEN yaenda kwa mkimbizi wa Afghanistan

Kusikiliza / Mwalimu mkimbizi kutoka Afghanistan, Aqeela Asifi.(Picha:UNHCR/Sebastian Rich)

Mwalimu mkimbizi kutoka Afghanistan, Aqeela Asifi ameshinda tuzo yam waka huu ya wakimbizi ya NANSEN. Tuzo hiyo inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR imezingatia jinsi Bi. Asifi alivyojitolea maisha yake kuwapatia elimu watoto wakimbizi wa kike wa Afghanistan walioko nchini Pakistani. Taarifa ya UNHCR imesema imetambua ujasiri wake anapofanya kazi [...]

15/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

EU fanyeni uamuzi wa kijasiri kumaliza janga la wakimbizi:UNHCR

Kusikiliza / Wakimbizi wasubiri kuchukua basi kuelekea Hungary baada ya kuvuka mpaka kutoka Serbia.(Picha© UNHCR/O.Laban-Mattei)

Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR limeeleza masikitiko yake kufuatia Umoja wa Ulaya, EU kushindwa kuafikiana kuhusu pendekezo la kuwapatia makazi wakimbizi 120,000. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Baraza la mawaziri wa Muungano wa Ulaya lilikuwa na kikao chake mjini Brussels, Ubelgiji ambako waliridhia pendekezo la awali la kuwapatia hifadhi wakimbizi ElfuArobaini [...]

15/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa 70 wa Baraza kuu la UM waanza leo.

Kusikiliza / Ukumbi wa mikutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Sophia Paris)

Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaanza leo Jumanne kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa chini  ya Rais wake Mogens Lykketoft  kutoka Denmark. Kikao kitaanza kwa ajenda ya kuchagua Makamu wa Rais wa Baraza hilo na kufuatia na kikao cha kilele cha kuridhia ajenda ya maendeleo endelevu, SDG kitakachoanza tarehe 25 [...]

15/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu, UNGA70 | Kusoma Zaidi »

UM kuridhia malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs

SDGs

Mwisho wa mwezi huu wa Septemba viongozi 193 wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa watakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kwa ajili ya kuamua rasmi kuhusu ajenda 2030. Ajenda hiyo yenye malengo 17 ya maendeleo endelevu yanalenga pamoja na mambo mengine kutokomeza umaskini uliokithiri, kupambana na tofauti na [...]

14/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

“Lulu ya Afrika” yajitangaza ndani ya Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Hafla ya maonyesho kuhusu maajabu yapatikanayo Uganda. Picha: UN Photo/Rick Barjonas

Mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa yalifanyika maonyesho kuhusu maajabu yapatikanayo kwenye nchi moja ya Afrika Mashariki, ijulikanayo kama lulu ya Afrika, au Pearl of Afrika, yaani Uganda. Rais wa mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Sam Kutesa ambaye ni raia wa Uganga aliongoza dhifa hiyo [...]

14/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa waamua siku ya kimataifa ya kuzuia mauaji ya kimbari, mtalaam wa UM akaribisha azimio

Kusikiliza / Silaha na mapanga, mjini Gisenyi, Rwanda, mwaka 1994. Picha ya UN/John Isaac

Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adama Dieng amekaribisha azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la kuifanya tarehe 9 Disemba siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa mauaji ya kimbari na kuzuia mauaji hayo. Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Bwana Dieng amesema ni muhimu kukumbuka yaliyotokea zamani na waliofariki dunia ili [...]

14/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 69 cha Baraza Kuu chahitimishwa kwa sifa kemkem

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa akiashiria kufungwa rasmi kwa mkutano wa 69 wa baraza hilo. Kushoto ni Katibu Mkuu Ban Ki-moon. (Picha:UN/Rick Bajornas)

Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kimehitmishwa leo, huku Baraza hilo likipongezwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon kwa mafanikio yake katika kikao hicho. Akizungumza wakati wa mkutano wa kufunga kikao hicho, Katibu Mkuu amesema wakati muhimu zaidi katika kikao hicho cha 69 ulikuwa bila shaka kupitishwa kwa ajenda ya 2030 ya [...]

14/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, MKUTANO WA BARAZA KUU WA 69 | Kusoma Zaidi »

Muarobaini wa ndoa utotoni Tanzania na Ethiopia wapatikana

Kusikiliza / Amhara nchini Ethiopia.(Picha:Ashenafi Tibebe/Girls not Brides)

Tanzania na Ethiopia zimefanikiwa katika kuepusha wasichana kuozwa na badala  yake wanaendelea na masomo kutokana na mikakati kadhaa iliyotumika ikiwemo kushirikisha jamii katika mijadala kuhusu umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike. Princess Mabel Van Oranje muasisi na mwenyekiti wa ubia wa kimataifa wa kumaliza ndoa za utotoni amesema hayo wakati wa mkutano uliofanyika kwenye [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ireland kupiga jeki shughuli za WFP Uganda

Kusikiliza / Mgao wa msaada kutoka serikali ya Ireland.(Picha:WFP//Olandason Wanyama)

Serikali ya Ireland imeahidi kupiga jeki ya dola $800,000 kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa ajili ya kusaidia watoto wa shule katika eneo linalokabiliwa na njaa kali la Karomoja Kaskazini Mashariki mwa Uganda na wakimbizi walioko nchini humo. John Kibego na maelezo zaidi. (Taarifa ya Kibego) Katika mkataba wa makubaliano uliyotiiwa saini [...]

14/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tulitimiza mengi, asema Kutesa akihitimisha Urais wa Baraza Kuu

Kusikiliza / Sam Kutesa akiongea na waandishi wa habari leo akimaliza muhula wake. Picha ya UN/Rick Bajornas.

Kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kilitimiza mengi, yakiwemo kuafikia ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu na Ajenda ya Addis Ababa ya kuchukua hatua kuhusu kufadhili maendeleo. Hayo yamesemwa na Rais wa Baraza Kuu anayeondoka Sam Kutesa, akihutubia waandishi wa habari kwa mara ya mwisho katika wadhfa huo, kwenye makao makuu [...]

14/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Hoja ya kutaka kumshtaki Rais Somalia imalizwe kwa mashauriano:Kay

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay(UN Photo/Rick Bajornas)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay amekaribisha mwenendo ambao kwao pande husika nchini humo zinajikita katika kupatia suluhu mzozo juu ya hoja ya kumfungulia mashtaka Rais wa nchi hiyo na kupongeza ari yao ya kuhakikisha kuna amani na utulivu. Taarifa ya ofisi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa [...]

14/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

We Care Solar yashinda tuzo ya dola milioni moja kwa ajili ya kukuza nishati endelevu

Kusikiliza / Shirika la We Care Solar lapewa cheki ya dola milioni moja. Picha kutoka akaunti ya Twitter ya Idara ya Maendeleo Endelevu @SustDev

Kwenye maadhimisho yaliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York Marekani, Shirika lisilo la kiserikali la We Care Solar lenye makao makuu huko Carlifornia, limeshinda tuzo ya dola milioni moja kutokana na mradi wao wa kuimarisha afya ya watoto na wakina mama kupitia huduma za umeme utokakanao na nishati ya jua. [...]

14/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mfumo tuliobuni utasaidia kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu: GBC

Kusikiliza / Catherine Njau wa kampuni ya Kenya Greenbell Communications, Picha: ITC/Fredy Uehara

Programu iliyobuniwa na kampuni moja nchini Kenya kuunganisha mtandao wa wanawake Milioni Moja wajasiriamali duniani, ni moja ya fursa ya kutekeleza lengo namba nane la maendeleo endelevu la kuhakikisha ukuaji uchumi ambao ni jumuishi, shirikishi na endelevu. Meneja mradi wa shirika la Greenbell Communications, GBC, kutoka Kenya Catherine Njau ameiambia Idhaa kuwa kupitia programu hiyo [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu laazimia kuongeza uwakilishi kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa. Picha:UN Photo/Loey Felipe

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kufanyia mabadiliko Baraza la Usalama, na kuongeza usawa katika uwakilishi kwenye baraza hilo. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Sauti ya Amina) Sauti Kutesa…. Ni rais wa kikao cha 69 cha Baraza Kuu, Sam Kutesa, akitangaza matokeo ya kura ya kupitisha azimio la [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNCTAD yatoa mapendekezo ya kutokomeza umaskini

Kusikiliza / Bado umaskini uliokithiri unaendelea kwenye baadhi ya maeneo duniani kote, kama hapa Darfur, nchini Sudan. Picha ya UN/Albert González Farran

Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD, limetoa leo ripoti yake ya mwaka kuhusu jitihada za kupambana na umaskini, likisema hadi dola trilioni 4.5 zinapaswa kuwekezwa kila mwaka katika miundombinu, uhakika wa chakula, mazingira, afya na elimu. Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Uswisi, Katibu Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa WHO waangazia matangazo ya bidhaa zisizo na afya kwa watoto

Kusikiliza / Laos: lishe bora inaleta watoto zaidi shuleni. Picha: Benki ya Dunia / Bart Verweij

Huko Amman nchini Jordan kunafanyika mkutano wa siku mbili unaongazia athari za kutokuwepo kwa udhibiti wa utangazaji wa vyakula na vinywaji visivyo na afya kwa watoto vinavyoweza kusababisha utipwatipwa. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Mkutano huo ulioandaliwa na shirika la afya duniani, WHO ukanda wa Mediterania ya Mashariki unafanyika wakati huu ambapo [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tubadilike tunavyoshughulikia ukiukwaji haki la sivyo hatuna umuhimu: Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye UM Zeid Ra'ad Al Hussein. (Picha: UN Photo / Jean-Marc Ferré)

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeanza kikao chake cha 30 mjini Geneva Uswisi ambapo Kamishna Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja huo Zeid Ra'ad Al Hussein amesema mwaka mmoja tangu ashike wadhifa huo, kiwango cha machungu duniani kinazidi kuongezeka kila uchao na uwezo wa dunia kushughulikia inatia hasira. Taarifa zaidi [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wawakilishi wa mazungumzo Libya waafikia vipengele muhimu vya makubaliano

Kusikiliza / Bernardino Leon.(Picha:UM/Jean-Marc FerrÃ)

Wawakilishi wa baraza la kitaifa nchini Libya wameondoka mjini Skhirat, Morocco kwa kipindi cha saa 48, ili wafanyie tathmini vipengele muhimu vya rasimu ya makubaliano ya amani,  na baadaye kurejea na orodha ya majina ya wagombea wa serikali ya muungano. Tayari, washiriki wengine katika mazungumzo hayo wamewasilisha majina ya wagombea wao, wakiwemo wawakilishi wa bunge. [...]

14/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Changamoto yetu ya pamoja ni kutimiza uwezo mkubwa zaidi wa utalii- Ban

Kusikiliza / Sherehe ya rika nchini Nigeria kama sehemu ya Utalii(Picha ya UNWTO/Otuo, Nigeria)

Utalii huchangia pakubwa katika kufungua nafasi za ajira, kupunguza umaskini, kuwezesha wanawake, kutunza mazingira na kujenga amani, na changamoto ya pamoja ni kutimiza hata uwezo mkubwa zaidi wa sekta hiyo ambayo ni moja ya sekta kubwa zaidi na zinazokuwa kwa kasi zaidi.  Huo ni ujumbe alioutoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon kwa [...]

13/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Tunahitaji vijana ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha ya UM/Eskinder Debebe (Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kuwa wakati serikali zikijiandaa kupitisha ajenda mpya ya maendeleo endelevu ili kuleta mabadiliko kwa maisha ya watu wote ifikapo mwaka 2030, mchango wa vijana unahitajika ili kutimiza malengo hayo. Ban amesema hayo katika ujumbe wake kwa kongamano la vijana, ambao amesema walisaidia katika kubuni ajenda [...]

13/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale, Malengo ya Maendeleo Endelevu, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa nchi za kusini mwa dunia unaweza kuchangia kutimiza Ajenda 2030- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban ki-moon. Picha:UN Photo/Mark Garten

Katika kuadhimisha Siku ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikiano wa nchi za Kusini mwa Dunia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema siku hiyo inamulika hatua za maendeleo zinazopigwa na nchi hizo. Katika ujumbe wake, Ban amesema licha ya changamoto kadhaa zilizopo, nchi zinazoendelea zimeibuka kuwa muhimu kwenye nyanja za kiuchumi na kijamii. [...]

13/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Kenya iweke mustakhbali bora zaidi kwa wazee wote. Bi. Wamera

Kusikiliza / Bi. Esther Wamera akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa.(Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili/Grace Kaneiya)

Malengo 17 ya maendeleo endelevu yanatarajiwa kupitishwa na wakuu na viongozi wa nchi wanachama wa  Umoja wa Mataifa baadaye mwezi huu kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani. Malengo hayo yanalenga kusongesha pale ambapo malengo ya maendeleo ya milenia, MDG yamekwamia. Miongoni mwao ni lengo namba tatu ambalo linalenga afya na ustawi [...]

11/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Ban atoa taarifa kuhusu mustakhabali wa operesheni za ulinzi wa amani

Kusikiliza / Walinda amani wa UNMISS.(Picha:UNMISS)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa leo ajenda yake kuhusu mambo ya kipaumbele katika operesheni za ulinzi wa amani na hatua zinazopaswa kuchukuliwa ili kuyatimiza. Hii ni kufuatia kutolewa kwa ripoti kuhusu mustakhbali wa operesheni za ulinzi wa amani, kufuatia kazi ya jopo la ngazi ya juu lililoteuliwa mnamo Oktoba 2014, likiongozwa [...]

11/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuondoa ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika

Kusikiliza / Ma-Turmah mwenye umri wa maka 68 kwa mara ya kwanza akijifunza kusoma na kuandika jina lake katika shule ya watu wazima katika kijiji cha Maturmah,Liberia. Picha:UN Photo/Emmanuel Tobey

Septemba nane kila mwaka ni siku ya kuondoa ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni kujua kusoma na kuandika na jamii endelevu. Ujuzi wa kusoma na kuandika umetajwa kama ufunguo wa maendeleo endelevu au SDGs yanayopitishwa baadaye mwezi huu yakiitwa pia ajenda 2030,  kwani ndio msingi wa stadi, mitazamo [...]

11/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Diamond, SautiSol waungana na wenzao #SDGs: VIDEO

Diamond

Malengo ya maendeleo endelevu, SDGs au #Globalgoals yanapitishwa baadaye mwezi huu. Kupitia kampeni ya Global Gloals Africa campaign, wanamuziki wa Afrika wakiwemo SautiSol, Diamond, Yemi Alade na wengineo wakajumuishwa katika  uimbaji wa kibao hiki kikiwa na lugha ya kiswahili, kiingereza, kitoofan, kizulu na kifaransa. Ungana nao wakielezea umuhimu wa malengo  hayo 17. Kampuni ya Unilever [...]

11/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu, Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Vita na Amani: michoro ya mita 14 yazinduliwa New York

Kusikiliza / Wakati wa hafla ya uzinduzi wa "War and Peace". Picha ya UN/Evan Schneider

Michoro iitwayo "War and Peace", yaani Vita na amani, iliyotengenezwa na mchoraji wa Brazil marehemu Claudio Portinari imerejeshwa wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya kutembezwa kwa miaka michache nchini Brazil na Ufaransa. Michoro hiyo miwili mikubwa kabisa yenye urefu wa mita 14 iliwekwa awali mwaka 1957 kwenye makao makuu ya [...]

11/09/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na kanuni mpya za marekebisho ya madeni ya serikali, Mtalaam akaribisha hatua

Kusikiliza / Baraza Kuu.(Picha:UM/Marco Castro)

Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu athari za madeni ya nje na haki za binadamu, Juan Pablo Bohoslavsky, amekaribisha azimio lililopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa marekebisho ya madeni ya serikali. Kwenye taarifa iliyotolewa leo, mtalaam huyo amesema ni hatua ya kuridisha itakayosaidia kuzuia mizozo itokanayo na madeni yasiyokuwa [...]

11/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF yataka viongozi wa Ulaya watimize ahadi zao kuhusu wakimbizi

Kusikiliza / Mtoto alie katika hali ya uchovu kwenye bega la mtu katika mji wa Gevgelija, Ugiriki ambapo wanawake na watoto ni karibu theluthi moja ya wanaofika.
Picha:UNICEF / NYHQ2015-2065 / Georgiev

Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limekaribisha kuongezeka kwa ahadi kutoka kwa viongozi wa Ulaya za kuwasaidia wakimbizi na wahamiaji, likisema kwamba ahadi hizo zinapaswa kugeuzwa kuwa hatua za nchi zote wanachama wa EU kuwalinda watoto kikamilifu. Kufikia sasa, watoto tayari ni robo ya waomba hifadhi barani Ulaya mwaka huu. Katika miezi sita ya kwanza ya [...]

11/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uzuri wa Uganda waonyeshwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiongea wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya "Uganda the Pearl". Katikati ni Waziri wa Utalii Bi Mutagamba na kulia Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa. Picha ya Umoja wa Mataifa/Rick Bajornas

Maonyesho kuhusu Uganda yamezinduliwa jana usiku kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kwa ajili ya kuvutia watalii na wafanyabiashara kwenye nchi hiyo iliyopewa jina la lulu ya Afrika. Akiongea kwenye uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza kazi zilizotekelezwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja [...]

11/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yaijulisha WHO kuhusu mlipuko wa kipindupindu, DSM yaongoza

Kusikiliza / Picha:UNICEF Tanzania/Fred Lyimo

Wizara ya Afya na Jamii nchini Tanzania, imelijulisha Shirika la Afya Duniani, WHO kuhusu mlipuko wa kpindupindu nchini humo ambapo idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 14 huku wagonjwa waliothibitika wakiwa ni 1268. Amina Hassan na maelezo zaidi. (Taarifa ya Amina) WHO imepatiwa taarifa hizo leo huku Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa [...]

11/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila mtu ni mzee mtarajiwa, wekeni sera za kuboresha ustawi wa wazee:

Kusikiliza / Mwanaharakati wa haki za wazee kutoka Kenya, Esther Wamera. Picha: Assumpta Massoi

Wakati lengo namba tatu la maendeleo endelevu, SDGs linataka kuhakikisha afya bora na ustawi kwa watu wenye umri wote, nchini Kenya serikali na jamii imeombwa kuangazia ustawi wa wazee ambao baadhi yao wanakumbwa na madhila ikiwemo kukosa pensheni, malezi na hata matibabu. Akihojiwa na idhaa hii baada ya kuhutubia mkutano ulioangazia athari za SDG kwa [...]

11/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yakaribisha mapendekezo ya Kamisheni ya Ulaya kuhusu wakimbizi na wahamiaji

Kusikiliza / Wakimbizi wanaowasili bara Ulaya.(Picha:UNHCR/Video capture)

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limekaribisha mapendekezo ya Kamisheni ya Muungano wa Ulaya yaliyotangazwa Jumatano wiki hii kushughulikia mzozo wa wakimbizi uliopo sasa Ulaya. Shirika hilo limesema, kutokana na udharura wa hali iliyopo sasa hivi, mapendekezo hayo yanapaswa kutekelezwa kikamilifu na haraka. UNHCR imesema mkakati uliopendekezwa wa kuwahamisha wakimbizi 160,000 kutoka Ugiriki, Italia na Hungary, [...]

11/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama laridhia kuundwa kwa JIM, Ban azungumza

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Loey Felipe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua ya Baraza la usalama kupitisha siku ya Alhamisi, azimio la kuridhia pendekezo lake la kuunda na kuendesha chombo cha pamoja cha uchunguzi na shirika la kimataifa la kupinga silaha za kemikali, OPCW. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemnukuu Ban akisema kuwa hatua hiyo [...]

11/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Azimio lapitishwa kupeperusha bendera za Palestina na Holy See Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Bendera ya Palestina. (Picha:Facebook: Ubalozi wa Palestina)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio la kuruhusu kupeperushwa kwa bendera za Palestina na Holy See kwenye makao makuu jijini New York, Marekani na katika ofisi zake kwingineko. Kabla ya kupiga kura, mwakilishi wa Iraq ambayo ni kiongozi wa nchi za kiarabu kwa mwezi huu wa Septemba alitoa maelezo ya azimio hilo [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake wamesimama kidete kunasua watoto wao kutoka ugaidi:

Kusikiliza / Kikao cha kamati ya baraza la usalama kuhusu kukabili ugaidi na misimamo mikali kilipofanyika New York tarehe 09/09/2015. (Picha:UN /Devra Berkowitz)

Siku ya Jumatano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kamati ya baraza la usalama kuhusu udhibiti wa ugaidi na misimamo mikali ilikuwa na kikao cha kupatiana taarifa juu ya  harakati hizo. Wanawake watatu kutoka Iraq, Nigeria na Kenya walikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu wakieleza kile ambacho mashirika yao yanafanya kusaidia kukwamua nchi zao kutokana [...]

10/09/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Asilimia 30 ya shule nchini CAR zimeshabuliwa: ripoti

Kusikiliza / Watoto wa shule Bangui, CAR. Picha:UN Photo/Serge Nya-Nana

Mtandao wa kijamii wa Watchlist umezindua leo ripoti kuhusu mashambulizi dhidi ya shule nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ukisema karibu asilimia 30 ya shule 335 zilizochunguzwa zimeshambuliwa kati ya mwaka 2012 na mwezi Aprili 2015. Aidha asilimia 8 ya shule hizo zimetumiwa na vikundi vya waasi au walinda amani. Watchlist imesikitishwa pia na kuona [...]

10/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Janga la wahamiaji Ulaya-video

janga

10/09/2015 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mchango wa dola milioni 250 utawezesha watoto milioni 1 wa Syria kwenda shule- Brown

Kusikiliza / Mtoto nchini Syria. Picha ya WFP/Abeer Etefa

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu Duniani, Gordon Brown, amesema ingawa ulimwengu sasa unamulika wakimbizi wanaoingia barani Ulaya, kuna wakimbizi wa Syria milioni nne  walioko katika nchi za Jordan, Uturuki na Lebanon, milioni mbili miongoni mwao wakiwa watoto. Akiongea na wanahabari mjini New York kwa njia ya simu, Bwana Brown [...]

10/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Shindano la tuzo ya uvumbuzi wa kitamaduni lazinduliwa

Kusikiliza / Picha:UNAOC

Tuzo ya uvumbuzi unaoendeleza uiano baina ya tamaduni imezinduliwa leo na Jumuiya ya Ustaarabu katika Umoja wa Mataifa, UNAOC kwa ushirikiano na kampuni ya BMW. Tuzo hiyo inatunukiwa kwa miradi bunifu na endelevu duniani, ambayo huendeleza mazungumzo na uelewano baina ya tamaduni mbali mbali, na hivyo kuchangia amani na maendeleo. Mashirika kumi yenye uwezo wa [...]

10/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maonyesho ya Milan Expo yalenga kutokomeza njaa

Kusikiliza / Mwimbaji Bono wa kundi la U2(Picha:UM/UNifeed)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mpango wa Chakula, WFP, Ertharin Cousin, alimshukuru nyota wa bendi ya muziki ya U2 na mwanzilishi wa ONE, Bono, na Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi kwa juhudi zao za kupaazia sauti watu maskini na wenye njaa duniani. Bono na Bi Cousin walikutana Jumapili Agosti 6 kwenye hafla maalum iitwayo, [...]

10/09/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kulikuwa na watalii milioni 21 zaidi wa kimataifa miezi 6 ya kwanza 2015

Kusikiliza / Watalii katika Mlima wa Taishan, katika Mkoa wa Shandong, nchini China, ambayo imesajiliwa na UNESCO kama eneo la urithi wa dunia. 
Picha:UN Photo/ Eskinder Debebe

Idadi ya watalii wa kimataifa iliongezeka kwa asilimia 4 katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2015, kulingana na kipimo cha Shirika la Utalii Duniani, UNWTO. Maeneo mbalimbali ya utalii duniani yalipokea watalii wa kimataifa wapatao milioni 538 kati ya Januari na Juni 2015, ikiwa ni nyongeza ya watu milioni 21, ikilinganishwa na wakati kama [...]

10/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mtu mmoja kati ya wanne Afghanistan hana chakula: Ripoti

Kusikiliza / Mkulima akivuna mazao ya ngano Bamyan, Afghanistan. Picha: FAO / Giulio Napolitano

Ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa na wadau wake imeeleza kuwa hali ya upatikanaji wa chakula nchini Afghanistan inazidi kuzorota. Miongoni mwa viashiria vya kwamba hali ni mbaya, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ni ongezeko la idadi ya watu wanaouza ardhi au kurejea kwa ndugu, jamaa na marafiki kusaka msaada kutokana na ukosefu [...]

10/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shambulio dhidi ya watoa misaada huko Darfur lalaaniwa

Kusikiliza / Gari hili la UNAMID llilishambuliwa wakati likipeleka maji katika shule ya Labado, Darfur Kusini. Picha: UN Photo/Albert González Farran

Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio lililofanywa na watu wasiojulikana wakiwa na silaha dhidi ya gari lililokuwa limebeba watoa huduma za kibinadamu huko Darfur magharibi nchini Sudan. Mratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa nchini humo Marta Ruedas, amesema katika shambulio hilo dereva na afisa usalama waliuawa ilhali maafisa wawili wa wizara ya [...]

10/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

India yaongoza kwa binadamu kutumia viuadudu kujiua:WHO

Kusikiliza / viuadudu ni njia ya kwanza ya kujiua nchini India kwani vinapatikana kwenye kila nyumba vijijini ambapo vinatumiwa kwa mahitaji ya kilimo. Picha ya WHO/A. Balayannis

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya kujiua Shirika la Afya Duniani WHO limeeleza kuwa idadi ya watu wanaojiua inazidi idadi ya watu wanaokufa kutokana na vita na mauaji. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Kwa mujibu wa WHO, ni watu zaidi ya 800,000 wanaojiua kila mwaka, asilimia 75 ya [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuwaenzi wahanga kwa kuzuia daima majaribio ya nyuklia- Ban

Kusikiliza / Baraza la usalama. (Picha:UN/Loey Felipe.)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuadhimisha Siku ya Kupinga Silaha za Nyuklia, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon, ametoa wito kwa nchi wanachama ziwaenzi wahanga wa majaribio ya zamani ya zana hizo kwa kuzuia majaribio kama hayo siku zijazo. Bwana Ban ambaye amesema lengo la kutokomeza majaribio ya silaha [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Naondoka DR Congo nikiwa na matumaini makubwa: Kobler

Kusikiliza / Martin Kobler, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu DRC. Picha:MONUSCO / Myriam Asmani

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Martin Kobler, amesema amehitimisha jukumu lake kwa mafanikio makubwa ikiwemo kutokomeza kikundi cha M23, na yote ni kutokana na ushirikiano kutoka kwa wafanyakazi wote. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Kobler ambaye aliteuliwa mwezi Juni mwaka 2013 [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kutokidhi mahitaji ya kibinadamu Syria kunaongeza mzozo wa watoto wakimbizi- UNICEF

Kusikiliza / Mwanamke mkimbizi wa Syria na mtoto wake katika kambi ya Zaátari. Picha:UNHCR/S. Malkawi

Mzozo wa wakimbizi na wahamiaji Ulaya utazidi kuzorota iwapo juhudi zaidi hazitafanywa kuumaliza mgogoro wa Syria na kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya mamilioni ya watu walioathiriwa na machafuko, limesema Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF. UNICEF imesema kuwa mgogoro wa Syria umewaacha watu wapatao milioni 16 wakihitaji usaidizi wa kuokoa maisha na ulinzi, huduma za afya, [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mawasiliano mbalimbali, MKUTANO WA BARAZA KUU WA 69, Mkutano wa Tabianchi 2014, Rio+20, SIDS 2014, Siku ya Radio 2015, Siku ya Radio Duniani, Siku ya Walinda Amani 2014, Siku ya Wanawake Duniani 2015, Taarifa za dharura, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Ukoma wazidi kutesa nchi sita za Asia ikiwemo India na Bangladesh: WHO

Kusikiliza / Mgonjwa wa ukoma. (Picha:UN /Tim McKulka)

Shirika la afya duniani, WHO limetaka kuimarishwa kwa jitihada za kutokomeza magonjwa ya kitropiki yasiyopatiwa kipaumbele kama vile ukoma, mabusha, matende na kichocho ambayo yanaendelea kulemaza, kutesa na kuua watu huko Kusini Mashariki mwa Asia. Mkurugenzi wa WHO kwenye ukanda huo Dokta Poonam Khetrapal Singh amesema magonjwa hayo yanayotibika, yanakumba pia watu wasiopatiwa kipaumbele ambao [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana wanaorejea baada ya kulaghaiwa na ugaidi wahitaji msaada

Kusikiliza / Sureya Roble-Hersi, Makamu wa pili wa mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo ya Wanawake nchini Kenya. Picha:Assumpta Massoi

Ushiriki wa wanawake katika kupatia suluhu ugaidi na misimamo mikali ni jambo lisiloepukika wakati  huu ambapo siyo tu wavulana wanajitumbukiza kwa hiari kwenye ugaidi bali pia wasichana na hata wanawake. Hayo yamesemwa na Sureya Roble-Hersi, Makamu wa pili wa mwenyekiti wa shirika la Maendeleo ya wanawake nchini Kenya alipohojiwa na Idhaa hii kando mwa kikao [...]

10/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mateso ya walio wachache Mashariki ya Kati sasa ni mateso ya walio wengi: Eliasson

Kusikiliza / Mtoto nchini Syria. Picha ya WFP/Abeer Etefa

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson ameeleza wasiwasi wake kuhusu hatma ya makundi ya walio wachache kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati, huku wakiendelea kuteswa na vikundi vya waasi wenye itikadi kali ya kidini. Bwana Eliasson amesema hayo akiongea na Redio ya Umoja wa Mataifa baada ya kuhudhuria mkutano kuhusu mateso dhidi [...]

09/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Matumaini yapo kwa maridhiano kati ya Korea Kusini na Kaskazini: mtalaam wa UM

Kusikiliza / Marzuki Darusman, Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK. Picha:UN Photo/Devra Berkowitz

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK Marzuki Darusman amesema mawasiliano kati ya DPRK na Jamhuri ya Korea yameanza kubadilika. Kwenye taarifa iliyotolewa leo baada ya ziara yake ya siku tano nchini Jamhuri ya Korea, Bwana Darusman amesema wawakilishi wa nchi [...]

09/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Polisi na wanafunzi wahatarisha msitu wa Budongo nchini Uganda

Kusikiliza / Misitu(Picha ya UM/Pernaca Sudhakaran)

Wakati ambapo umuhimu wa misitu kwa mazingira na maendeleo endelevu unamulikwa kwenye kongamano la 14 la kimataifa la misitu linalofanyika mjini Durban, Afrika Kusini, hali ya misitu iliyopo Afrika Mashariki inaendelea kutia wasiwasi. Mathalani nchini Uganda, msitu wa Budongo, karibu na ziwa Albert, maghabiri mwa nchi, unahatarishwa na mafunzo ya polisi yanayofanyika humo. Kulikoni ? [...]

09/09/2015 | Jamii: COP21, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya visa vya Ebola yapungua, WHO yaendelea kuwa makini

Kusikiliza / Wafanyakazi wa kujitolea wakihamasisha jamii, nchini Liberia. Picha ya UNDP/Morgana Wingard (MAKTABA)

Mwakilishi maalum wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO kwa ajili ya Ebola, Bruce Aylward, amesema ametiwa moyo na taarifa za kupungua kwa idadi ya visa vya Ebola. Hata hivyo jitihada za kupambana na Ebola zinaendelea, ameeleza Bwana Aylward akiongea na waandishi wa habari leo mjini Geneva Uswisi baada ya kumaliza ziara ya [...]

09/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Azimio la kuendeleza usawa wa jinsia lahitaji msukumo

Kusikiliza / Picha:UN Women/Piyavit Thongsa-Ard

Haki za wanawake zinakabiliwa na hatari ya kurudi nyuma, licha ya azimio kuu la Umoja wa Mataifa lililolenga kuendeleza usawa. Onyo hilo limetolewa kwenye kongamano la kufanyia tathmini hatua zilizopigwa kimataifa kuendeleza usawa wa jinsia, kutokana na azimio la Baraza la Usalama nambari 1325 lililopitishwa miaka 15 iliyopita, kuhusu wanawake, amani na usalama. Wajumbe katika [...]

09/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Matumizi holela ya viua vijasumu yaathiri afya ya umma:WHO

Kusikiliza / Picha kutoka video ya UNIFEED/WHO

Shirika la Afya Duniani WHO limesema kwamba matumizi holela ya viua vijasumu au Antibiotics, na madawa mengine yanasababisha usugu kwa madawa hayo na watu kushindwa kupona. Mkurugenzi wa WHO kwa Ukanda wa Asia Kusini Mashariki, Daktari Poonam Khetrapal Singh amesema hayo akihutubia mkutano wa kikanda unaofanyika nchini Timor-Leste, akieleza kwamba hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kupambana [...]

09/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Visa 4 vipya vya homa ya matumbo vyapatikana Yarmouk

Kusikiliza / Wahudumu wa afya wa UNRWA, mjini Yalda, wakisambaza vifaa vya matibabu. Picha ya UNRWA.

Wahudumu wa afya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA wameweka kituo cha afya kwenye mtaa wa Yalda nchini Syria, ambako wamewatibu wagonjwa 280 kwa siku moja. Miongoni mwa wagonjwa hao walikuwamo wanne walioambukizwa homa ya matumbo. UNRWA pia imetowa tembe 200,000 za kutakatisha maji zilizotolewa na UNICEF kwa jamii [...]

09/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uvumbuzi unaojali mazingira watunukiwa kwenye tuzo za SEED

Kusikiliza / 2015 SEED Mshindi , Loja de Energias, kutoka Msumbiji.(Picha: SEED)

Wakati ulimwengu ukijiandaa kuridhia malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) mwishoni mwa mwezi huu, kampuni 27 zinazoongoza katika uvumbuzi unaojali mazingira na kufaidi jamii zimetunukiwa kwenye kongamano la Afrika la SEED, mwaka 2015, ambalo linafanyika jijini Nairobi. Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, tuzo za SEED hutambua ujasiriamali bunifu wa kijamii na mazingira, [...]

09/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Mzigo wa kiuchumi kwa ajili ya tabianchi ni mzito kwa bara la Afrika:Prof. Kowero

Kusikiliza / Daktari Godwin Kowero. Picha ya FAO/Giuseppe Carotenuto

Athari za kiuchumi kutokana na mabadiliko ya tabianchi kwa bara la Afrika ni nyingi na iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa haraka iwezekanavyo, huenda rasilimali ya misitu ikapotea. Hiyo ni kauli ya Profesa Godwin Kowero Katibu Mkuu wa African Forest Forum aliyotoa kandoni mwa mkutano wa 14 kuhusu misitu unaoendelea mjini Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo wenye kauli [...]

09/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kasi ya migawanyiko duniani inaongezeka kila uchao: Ban

Kusikiliza / Mtoto akionyesha alama ya amani, nchini Libya. Picha ya Umoja wa Mataifa/Iason Foounten

Dunia inasonga mbele kwa kasi kubwa sana, halikadhalika migawanyiko miongoni mwa watu pamoja na chuki, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati akihutubia kikao cha hali ya juu kuhusu utamaduni wa amani kilichofanyika leo jijini New York Marekani. Kikao hicho kilichoitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimefanyika wakati ambapo Ban [...]

09/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WFP waongeza jitihada za kumaliza utapiamlo Sudan Kusini

Kusikiliza / Mtoa huduma wa afya achukua vipimo vya mtoto(Picha© UNICEF/NYHQ2015-1399/Rich)

Shirika la Mpango wa Chakula, WFP na Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo yamezindua mpango uloimarishwa wa kupambana na hali mbaya ya utapiamlo nchini Sudan Kusini, ambako mgogoro umelazimu mamilioni ya watu kuhama makwao, huku ukiharibu huduma za msingi na kuongeza magonjwa na njaa. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Mpango huo wa [...]

09/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupunguza vifo vya watoto wachanga, Ethiopia kidedea, Angola bado: Ripoti

Kusikiliza / Picha ya UNICEF Tanzania/Kate Holt

Idadi ya vifo vya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano imepungua kutoka Milioni 12.7 mwaka 1990 hadi chini  ya Milioni Sita mwaka huu. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la watoto UNICEF, afya WHO, benki ya dunia na kitengo cha idadi ya watu, [...]

09/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua endelevu zahitajika kushughulkia wimbi la wakimbizi Ulaya:Sutherland

Kusikiliza / Picha:Photo: UNHCR / A.Penso

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhamiaji wa kimataifa Peter Sutherland amesema hatua endelevu zinapaswa kuzingatiwa katika kupokea wakimbizi wanaozidi kumiminika barani Ulaya kutokana na mapigano yanayoendelea huko Syria. Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Uswisi kando mwa maandalizi ya kongamano la kimataifa kuhusu wahamiaji litakayofanyika huko Istanbul, Uturuki mwezi ujao. [...]

08/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mwongozo wa kinga na tiba ya Ebola dhidi ya wajawazito

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Ari Gaitanis

Shirika la afya duniani, WHO limetoa mwongozo kuhusu uchunguzi na kinga kwa mwanamke mjamzito na anapojifungua endapo kuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola. Mwongozo huo wa mpito unatolewa kwa wajawazito ambao wanaweza kuwa hatarini kuambukiza wengine, au wale ambao wamepona Ebola na wanaweza kuambukiza au wale walio karibu na wagonjwa wa Ebola. Mathalani mwongozo huo [...]

08/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Majengo 13,000 ya wapalestina yamepangwa kubomolewa

Kusikiliza / Picha:UNRWA/ Alaa Ghosheh

Ripoti mpya kutoka kwa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA inaonyesha kwamba majengo 13,000 kwenye ukingo wa magharibi wa mto Jordani huko Mashariki ya Kati, yatabomolewa kwa mujibu wa takwimu za serikali ya Israel. Ripoti ya OCHA imesema pia kwamba idadi ya nyumba za wapalestina zinazobomolewa na Israel inaendelea kuongezeka, [...]

08/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Harakati za ulinzi wa kulinda misitu ya asili Tanzania

Kusikiliza / Mti katika msitu wa Nkula nchini DRC.(Picha:FAO/Giulio Napolitano)

Mkutano wa 14 kuhusu misitu unaendelea mjini Durban nchini Afrika Kusini, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika barani Afrika ukiwaleta pamoja watu kutoka nchi na maeneo mbalimbali ikwemo serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kuchangia katika maswala ya misitu na kujadili maendeleo endelevu. Moja ya ajenda ni kuhusu kuangalia mustakhabali wa misitu [...]

08/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ladsous azindua eneo bila silaha huko Bambari, CAR

Kusikiliza / Kifaru cha Umoja wa Mataifa wakati wa doria Bambari, angalau kilometa 400 kutoka mji mkuu wa Bangui.Picha: UN Photo / Catianne TIJERINA

Mkuu wa Idara ya Operesheni za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous ametangaza kuzindua eneo maalum mjini Bambari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambalo halitaruhusiwa kuwa na silaha kuanzia leo. Bwana Ladsous amesema hayo akiongea na waandishi wa habari akiwa ziarani nchini humo, akisema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, [...]

08/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Cheikh Ahmed asikitishwa na kufunuliwa kwa nyaraka za UM Yemen

Kusikiliza / Bwana Ismail Ould Cheikh Ahmed. Picha ya UN/ Simon Ruf.

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, ameeleza kusikitishwa na ripoti za vyombo vya habari kuhusu ufunuzi wa mawasiliano ya ndani ya Umoja wa Mataifa. Taarifa ye msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa yaliyomo katika ripoti hizo, hususan katika vyombo vya habari vya Yemen na mitandao ya [...]

08/09/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa isaidie ulinzi wa urithi wa kitamaduni: Eliasson

Kusikiliza / Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson na Mkurugenzi mkuu, UNESCO.(Picha:© UNESCO/ P. Chiang-Joo)

Mkutano wa kimataifa kuhusu harakati za ulinzi wa mali za urithi wa kitamaduni na mateso dhidi ya jamii za kidini unaendelea huko Paris, Ufaransa, ambapo awali Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema juhudi za kimataifa zinahitajika ili kuepusha vitendo hivyo. Akizungumza mjini humo kabla ya kuanza kwa mkutano huo unaohudhuriwa pia [...]

08/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu 8,000 wameuawa mashariki mwa Ukraine- ripoti ya UM

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein. (Picha:UN /Jean-Marc Ferré)

Takriban watu 8,000 wameuawa mashariki mwa Ukraine tangu kati kati mwa mwezi Aprili mwaka 2014. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya kumi na moja ya Umoja wa Mataifa ya ujumbe wa uangalizi wa haki za binadamu nchini Ukraine, ambayo imetolewa leo na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein. Kamishna Zeid [...]

08/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lafanya mkutano kuhusu wajibu wa kulinda raia

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Tobin Jones

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ametoa wito kwa nchi wanachama, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwenda hatua zaidi ya kuelewa wajibu wa kulinda na kuchukua hatua za kulinda raia. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Bwana Ban amesema hayo akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambalo [...]

08/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwezo wa kusoma na kuandika ni ufunguo kwa maendeleo endelevu: UNESCO

Kusikiliza / Mwanafunzi darasani nchini Mynmar(Picha:UM/Kibae Park)

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Irina Bokova amesema uwezo wa kusoma na kuandika ni ufunguo kwa maendeleo endelevu na jamii jumuishi.  Grace Kaneiya anafafanua zaidi. (Taarifa ya Grace) Kwenye ujumbe wake kwa siku hiyo Bi Bokova [...]

08/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa kidini watazamia kuzindua mwongozo wa maendeleo endelevu

Kusikiliza / Lengo la tano la malengo endelevu(Picha@UM)

Dini nane kubwa duniani zinatazamiwa kuzindua mipango kabambe ya kusaidia kunyanyua mamilioni ya watu kutoka kwa umaskini, sambamba na malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu (SDGs). Mipango hiyo ambayo Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu, UNFPA limetaja kuwa baadhi ya ahadi halisi zaidi kufikia sasa, itazinduliwa katika mkutano wa viongozi wa imani [...]

08/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Saudi Arabia, Iran, Marekani na Urusi ni suluhu kwa mzozo wa Syria: de Mistura

Kusikiliza / Wakati wa ziara ya Stephan De Mistura alipokutana na viongozi wa ngazi ya juu nchini Syria.(Picha ya UM)

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Syria Staffan de Mistura amesema iwapo kungalikuwepo na majadiliano ya dhati baina ya pande zenye ushawishi na kile kinachoendelea nchini Syria, mzozo huo ungalikuwa tayari umebakia historia, lakini kinachofanyika sasa si mambo ya dhat na ndio kinachochoea wananchi kukimbia nchi yao kwenda Ulaya. Akizungumza na [...]

08/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali Syria inawakatisha wengi tamaa na maelfu kukimbilia Ulaya- UNHCR

Kusikiliza / Picha:UNHCR/ Z.MacKaoui

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limesema kuwa hali inayozidi kuzorota ndani mwa Syria na nchi jirani inawashinikiza malefu ya Wasyria kuhatarisha kukata tamaa na kufanya safari hatarishi kukimbilia Ulaya. Priscilla Lecomte na taarifa zaidi. (Taarifa ya Priscilla) UNHCR imesema wakati mzozo wa Syria ukiwa katika mwaka wa tano bila dalili za [...]

08/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA yapitia upya mpango wa nyuklia wa Iran, huko DPRK ujenzi unaendelea

Mkuu wa IAEA Yukiya Amano akihutubia kikao cha bodi ya magavana wa shirika hilo. (Picha: Dean Calma/IAEA)

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki la Umoja wa Mataifa, IAEA Yukiya Amano amesema ofisi yake inapitia upya taarifa iliyotolewa na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia. Amesema hayo wakati akituhutubia kikao cha bodi ya magavana wa shirika hilo mjini Vienna, Austria akiongeza kuwa mapitio hayo yatahusisha pia kuthibitisha na kufuatilia mpango wa [...]

07/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Juhudi za WFP kusaidia katika mgao wa chakula kwa wanafunzi Kenya

Kusikiliza / Mgao wa chakula kwa watoto.(Picha:WFP/Amanda Lawrence-Brown)

Leo ikiwa ni mapumizko hapa nchini Marekani kuadhimisha sikukuu ya wafanyakazi, tunakuletea jarida maalum linalomulika juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kusaidia katika mgao wa chakula kwa wanafunzi nchini Kenya. Tuungane na Joseph Msami (MSAMI PACKAGE) SFX Ngonjera maalum ikiimbwa na wanafunzi wa shule ya msingi Nazareth katika [...]

07/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Janga la uhamiaji Ulaya, Ban azungumza na viongozi kwa simu

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon. (Picha: MAKTABA: UN Photo/NICA)

Wakati janga la wahamiaji wanaosaka hifadhi Ulaya likichukua sura mpya kila uchao, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameendelea na jitihada za mashauriano na viongozi wa bara hilo ili kuweza kupata suluhu. Miongoni mwa harakati hizo ni mazungumoz yake kwa njia ya simu na viongozi hao ambapo amewasihi wawe sauti ya wale wanaohitahi [...]

07/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kasi ya ukataji misitu duniani imepungua kwa asilimia 50:FAO

Kusikiliza / Ufunguzi wa mkutano wa 14 wa misitu duniani huko Durban Afrika Kusini. (Picha: ©FAO/Giuseppe Carotenuto)

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema kasi ya ukataji misitu duniani kwa ajili ya matumizi ya binadamu na kilimo inapungua ikilinganishwa na miaka 25 iliyopita. Taarifa hizo zimo kwenye chapisho la FAO lililotolewa leo huko Afrika Kusini siku ambayo kongamano la Kumi na Nne kuhusu misitu limeanza mjini Durban, ikiwa ni mara ya [...]

07/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa Afrika Mashariki

Kusikiliza / Usafi katika soko la Temeke jijini Dar Es Salaam.(Picha:UN/Tanzania/facebook)

Maadhimisho ya miaka sabini ya Umoja wa Mataifa ni fursa ya kutafakari, na kuangalia historia na hatua ambazo Umoja wa Mataifa umepiga. Kadhalika ni fursa ya kuangazia ambapo Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa kwa ujumla inapaswa kuimarisha juhudi zake ili kukabiliana na changamoto mbali mbali kupitia kazi zake za amani, maendeleo na haki [...]

04/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, UN 70 | Kusoma Zaidi »

Uwasilishwaji wa misaada kwa anga Darfur huenda ukakatizwa:WFP

Kusikiliza / Wakimbizi @UNAMID

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema kwamba huenda likalazimika kusitisha uwasilishaji wa msaada kwa njia ya anga jimboni Darfur, nchini Sudan kwa sababu ya ukosefu wa ufadhili. Hiyo ni kwa mujibu wa Bettina Luescher kutoka WFP alipohojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa Ijumaa. Kauli hiyo imekuja wakati ambapo Shirika hilo limetoa ombi [...]

04/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Serena, Neymar na Kolo Toure wachagiza SDGs

Kusikiliza / Kampeni ya darasa la ulimwengu kuhusu SDGs. (Picha:Video capture)

Mabalozi wema watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF leo wameungana na kampeni ya kuzindua kampeni ya kuelimisha watoto katika nchi zaidi ya 100 duniani kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Mabalozi hao ni bingwa nambari moja wa tenisi duniani kwa wanawake Serena Williams, na wasakata kabumbu mashuhuri Kolo Toure na [...]

04/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Msanii wa Nigeria, D'Banj apigania usawa wa jinsia kupitia muziki

Kusikiliza / Msanii nyota wa Nigeria, D'Banj.(Picha:World bank/video capture)

Benki ya Dunia ilizindua mapema mwaka huu mfululizo wa makala uitwao "Muziki kwa maendeleo". Kupitia mfululizo huo wa makala zinazowekwa kwenye tovuti yake, Benki ya dunia inawapa fursa wasanii kutoka kote duniani wanaohusika katika masuala ya maendeleo kushirikisha muziki wao na kuzunumzia masuala yanayowagusa zaidi. Mmoja wa wasanii hao ni nyota wa Nigeria, D'Banj. Ungana [...]

04/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa Polio Ukraine, UNICEF, WHO yachukua hatua

Kusikiliza / Chanjo dhidi ya Polio. (Picha:Maktaba:UN/JC McIlwaine)

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia watoto, UNICEF na lile la afya, WHO yametoa wito kwa wazazi nchini Ukraine kuwapeleka watoto wao kupata chanjo dhidi ya ugonjwa wa Polio baada ya mlipuko wa ugonjwa huo kuripotiwa nchini humo. Wito huo umetolewa wakati huu ambapo harakati za kusambaza chanjo zinaendelea baada ya [...]

04/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani shambulizi la kigaidi kwenye msikiti Yemen

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha ya UM/Eskinder Debebe (Maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi ya kujilipua kwenye msikiti mmoja huko Sana'a Yemen. Shambulizi hilo la tarehe Pili mwezi huu kwenye wilaya ya Jarraf, lilisababisha vifo vya watu zaidi ya 30 ilhali watu wapatao 100 walijeruhiwa. Ban amenukuliwa na msemaji wake akieleza kuwa mashambulizi ya aina hiyo na ya [...]

04/09/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi ya waasi yaongeza idadi ya wakimbizi wa ndani kaskazini mwa Nigeria

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Nigeria wanaowasili nchini Chad wakisubiri kujiandikisha Ngouboua, Magharibi mwa Chad(Picha © Chadian Red Cross/H.Abdoulaye)

Zaidi ya watu Milioni Mbili wamekimbia makazi yao kaskazini mwa Nigeria na hiyo ni kwa mujibu wa kitengo cha ufuatiliaji makazi cha shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM. Msemaji wa IOM Joe Millman amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa idadi hiyo ambayo ni sawa na kaya Laki Tatu imeongezeka kutoka Milioni Moja na [...]

04/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

GBC ya Kenya yaibuka kidedea shindano la teknolojia

Kusikiliza / Catherine Njau, mwakilishi wa Greenbell Communications ya Kenya baada ya kutangazwa washindi wa shindano hilo. (Picha:ITCNews)

Kampuni moja nchini Kenya imeibuka kidedea katika shindano la kampeni ya kuanzisha mfumo wa digitali wa kuunganisha mtandao wa wajasiriamali wanawake Milioni Moja na masoko. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Greenbell Communications, GBC ilikuwa miongoni mwa kampuni 300 zilizoingia kwenye shindano hilo lililoandaliwa na kituo cha biashara duniani, ITC, Google na CI&T [...]

04/09/2015 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali CAR imetengamaa, lakini bado inatia wasiwasi- Kamishna Zeid

Kusikiliza / Picha:UN Photo/ Catianne Tijerina

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, ambaye yupo ziarani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, amewaambia waandishi wa habari mjini Bangui kuwa ingawa hali nchini humo imeboreka ikilinganishwa na kilele cha mgogoro mwishoni mwa mwaka 2013 na mapema 2014, bado inatia wasiwasi kwa raia wa CAR [...]

04/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tatizo la wakimbizi Ulaya lahitaji juhudi za pamoja- Guterres

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNHCR akigawa blanketi kwa watu wanaosubiri kuvuka mpaka wa Ugiriki kwenye jamhuri ya zamani ya Yugoslavia, Macedonia. (Picha:UNHCR/A.Kitidi)

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema leo kuwa hali ya wakimbizi Ulaya inahitaji juhudi kubwa za pamoja, ambazo haziwezekani kupatikana kwa kufuata mtazamo wa sasa uliogawanyika. Taarifa zaidi na John Kibego. (Taarifa ya Kibego) Bwana Guterres amesema hayo wakati Muungano wa Ulaya ukiandaa mikutano ya dharura katika [...]

04/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu Libya yaingia siku ya pili

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Iason Foounten

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu Libya yameingia siku yake ya pili hii leo mjini Geneva, yakilenga kukamilisha mashauriano kuhusu makubaliano ya kisiasa na masuala mengineyo, ikiwemo kuunda serikali ya mkataba wa kitaifa. Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva Ahmad Fawzi, amesema kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya, Bernardino Leon, amekuwa na mikutano [...]

04/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ruzuku ya serikali kwa wakulima huenda ikaongeza uharibifu wa misitu- UNEP

Kusikiliza / Mipango ya kupunguza joto ni pamoja na upandaji miti ambao husaidia kufyonza hewa ya ukaa inayosababisha ongezeko la joto duniani. (Picha@ UN/Joshua Mmali)

Ripoti mpya ya Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, imesema kuwa ruzuku ya serikali kwa wakulima, ambayo inakadiriwa kuwa dola bilioni 200 kila mwaka, huchangia pakubwa katika uharibifu wa misitu kote duniani, huku watunga sera wakiwa hawatambui athari zake. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, takriban asilimia 80 ya uharibifu wa misitu [...]

04/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kituo cha ukeketaji mbadala cha UNFPA chaleta nuru mkoani Mara, Tanzania

Kusikiliza / Picha:UNFPA Video Capture

Ili kuimarisha juhudi za kutokomeza ukeketaji, kuna haja ya kuweka juhudi mahususi na kushirikisha jamii kwa ujumla. Juhudi hizi zinapaswa kuhimiza elimu na mazungumzo katika jamii ili kumaliza ukeketaji. Ni kwa mantiki hiyo ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA linaendesha kituo cha kutoa mafunzo mbadala ya ukeketaji. Basi ungana na [...]

03/09/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushrikishswaji wa mabunge katika kutekeleza SDGs ni kiungo muhimu:Spika Muturi

Kusikiliza / Mahojiano baina ya Spika wa bunge la Kenya Justin Muturi na Grace Kaneiya. Picha:Assumpta Massoi

Wakati mkutano wa maspika wa mabunge ukiwa umehitimishwa jijini New York, Marekani, kumetolewa wito wa kuwasaidia watu kutimiza ndoto zao wakati huu ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeafikiana malengo mapya ya maendeleo endelevu yatakayoridhiwa baadaye mwezi huu. Kwa upande wake mwakilishi wa Kenya katika mkutano huo wa maspika, spika wa bunge la taifa [...]

03/09/2015 | Jamii: Mahojiano, Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Harakati za wananchi, Rais wa Guatemala ajiuzulu, Ban atoa tamko

Kusikiliza / Ramani ya Guatemala.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anafahamu uamuzi wa kujiuzulu wa Rais wa Guatemala Otto Pérez Molina akisema anaamini kuwa mamlaka husika zitazingatia katiba na kuhakikisha demokrasia katika kipindi cha mpito. Taarifa ya msemaji wake imemnukuu akitoa wito kwa wananchi wa Guatemala kuhakikisha chaguzi za Jumapili hii ikiwemo wa Rais zinafanyika katika [...]

03/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Project Everyone kwa siku Saba kufikia watu Bilioni Saba kuhusu SDGs

Kusikiliza / Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa UM kuhusu SDGs Bi. Amina Mohamed (Kulia) akiwa mtunzi mashuhuri wa filamu Richard Curtis (kushoto) kwenye mkutano na waandishi wa habari. (Picha:UN/Mark Garten)

Mtunzi wa filamu mashuhuri duniani, Richard Curtis leo kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa wametangaza mkakati wa kampeni ya siku saba ya kufikisha kwa wakazi Bilioni Saba wa dunia hii malengo 17 ya maendeleo ya endelevu, SDGs yatakayozinduliwa baadaye mwaka huu. Shughuli hiyo imefanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani [...]

03/09/2015 | Jamii: Malengo ya Maendeleo Endelevu | Kusoma Zaidi »

Haitoshi kushtushwa na picha za maiti za watoto wakimbizi- UNICEF

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu UNICEF, Anthony Lake.(Picha:UM/JC McIlwaine)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia watoto, UNICEF, Anthony Lake, amesema haitoshi kwa ulimwengu kushtushwa na picha za kuvunja moyo za miili ya watoto iliyosukumwa na mawimbi hadi kwenye mwambao wa Ulaya, au zile za wakimbizi waliofariki dunia kwenye malori na zile za watoto kuvushwa mipaka ya nyaya na wazazi wao waliokata tamaa. Mkuu huyo [...]

03/09/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

DRC isaidiwe uchaguzi uwe huru na wa haki

Kusikiliza / Mkutano wa wajumbe na wawakilishi wa kimataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu, wakijadili uchaguzi DRC. Picha:MONUSCO

Wakati uchaguzi mkuu ukibisha hodi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DCR), timu ya wajumbe na wawakilishi wa kimataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu, imetoa wito kwa wadau wa kisiasa kukubaliana kuhusu masharti katika mchakato wa uchaguzi. Baada ya mkutano wao mjini Geneva, Uswisi, wajumbe hao ambao ni pamoja na Mjumbe maalum wa Katibu Mkuuwa [...]

03/09/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dira ya Kenya ya 2030 yalandana na ile ya maendeleo endelevu: Spika Muturi

Kusikiliza / Spika la bunge wa taifa la Kenya akiwasilisha ripoti.(Picha:IPU/Flickr)

Mkutano wa Nne wa maspika wa mabunge ukiwa umehitimishwa kwa kuazimia kuweka mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuweka demokrasia kwa faida ya watu wote, Spika wa Kenya amesema hilo ni jukumu adhimu na ambalo wameanza kuzingatia. Akihojiwa na idhaa hii baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, Spika wa bunge la [...]

03/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yataka huduma bora kwa watoto wakati Liberia ikitangaza kumalizika Ebola

Kusikiliza / Muhamasishaji akiwafundisha watoto kuhusu mbinu sahihi za unawaji mikono, ili kuzuia kuenea kwa magonjwa, ikiwa ni pamoja na Ebola. Picha: UNICEF / Timothy La Rose

Kwingineko, Shirika hilo la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, limekaribisha leo tangazo kuwa Liberia imekomesha maambukizi ya Ebola, na kuelezea matumaini yake kwamba nchi hiyo sasa itaweza kujikita katika kujikwamua kutokana na mlipuko wa homa hiyo, ambao umeathiri vibaya maisha ya maelfu ya watoto na jamii zao. Taarifa kamili na Joseph Msami. (Taarifa ya [...]

03/09/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930