Saudia Arabia yatoa dola milioni 35 kwa Wapalestina

Kusikiliza /

Mama na mtot wake mchanga kwenye hospitali ya Al-Shifa iliyoko Gaza, UNRWA ikisema idadi ya watoto wanaokufa kabla ya kufikisha umri wa mwaka mmoja imeongezeka kutokana na matatizo yanayokumba sekta ya afya. Picha ya UNICEF/Loulou d'Aki.

Ufalme wa Saudia umetangaza kutoa msaada wa dola milioni 35 kwa ajili ya kusaidia wakimbizi wa Palestina.

Kwenye taarifa yake, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina UNRWA imesema kwamba pesa hizo zitasaidia kukarabati shule na vituo vya afya nchini Jordan, kujenga vituo vya afya vitatu kwenye Ukingo wa Magharibi na kusaidia huduma za afya na elimu kwenye Ukanda wa Gaza.

Aidha, dola milioni 19 kati ya pesa hizo zitachangia katika kupunguza ukata wa fedha unaolikumba shirika hilo.

Tangazo hilo linafuata ripoti iliyotolewa awali wiki hii na UNRWA ikisema kwamba iwapo dola milioni 101 hazitapatikana maramoja, wanafunzi 500,000 hawataweza kurudi shuleni mwezi huu.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930