Magaidi walituvamia, lakini tuna wajibu muhimu kuboresha maisha- Ban

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiwa mjini Abuja, Nigeria alikozuru na mkuu wa UNFPA Babatunde Osotimehin.(Picha:UM/X/NICA:640431)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema ingawa makundi ya kigaidi yanauvamia Umoja wa Mataifa na kuangamiza maisha, Umoja huo una majukumu muhimu ya kuboresha mustakhabali wa dunia. Taarifa kamili na Amina Hassan

(Taarifa ya Amina)

Ban amesema hayo kwenye hafla maalum mjini Abuja, palipofanyika shambulizi la bomu lililowaua wafanyakazi 23 wa Umoja wa Mataifa miaka mine iliyopita.

Katibu Mkuu ameongeza kwamba wanawaenzi wenzetu, wanawake kwa wanaume, ambao walipokonywa kutoka kwetu kwa njia katili. Tunakariri ahadi yetu ya kuendelea kushikamana na familia zao.

 Aidha, Ban amesema kuwa shambulizi kama hilo haliwezi kuvunja ari ya Umoja wa Mataifa

Kadhalika amesema kwamba magaidi waliuvamia Umoja wa Mataifa na kuyaangamiza maisha mengi. Lakini tuna jukumu la kujenga. Kuboresha maisha ya watu wenye uhitaji. Kutokomeza njaa, magonjwa na ujinga. Kuendeleza heshima ya haki za watu, haki za binadamu na uhuru.

Katibu Mkuu amesema huu ni wakati muhimu katika historia ya Nigeria, na anaunga mkono kazi ya Umoja wa Mataifa nchini humo.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031