Nyumbani » 31/03/2015 Entries posted on “Machi, 2015”

Mtalaam huru Tom Nyanduga asifu mchango wa hayati Balozi Bari Bari wa Somalia

Kusikiliza / Hayati Yusuf Mohamed Ismail "Bari Bari". Picha ya Umoja wa Mataifa/Jean Marc Ferré.

Kufuatia mashambulizi ya tarehe 27 mwezi huu kwenye hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu yaliyosababisha vifo vya raia kadhaa akiwemo mwakilishi wa kudumu wa Somalia kwenye Ofisi za Umoja wa Mataifa Geneva, Yusuf Mohamed Ismail Bari Bari, mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga, ametaka [...]

31/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNSMIL yakaribisha sitisho la mapigano kwenye eneo la Sidra, Libya

Kusikiliza / Picha: IRIN / Jorge Vitoria Rubio(UN News Centre)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL, umekaribisha sitisho la mapigano na kuondoka kwa majeshi kwenye eneo la lenye mafuta la Sidra nchini humo. Uamuzi huo unafuatia wiki kadhaa za mazungumzo kati ya kundi la Alshuruq na kikosi cha ulinzi wa mafuta ambayo yameratibiwa na UNSMIL. UNSMIL ikipongeza pande zote kwa utashi wao na [...]

31/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF yataka watoto walindwe Yemen

Kusikiliza / Watoto nchini Yemen, mustakhbali wao mashakani. (Picha:OCHA)

Takribani watoto 62 wameuawa na wengine 30 wamejeruhiwa katika wiki moja iliyopita ya mapigano nchini Yemen. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, likisema mapigano hayo pia yamesambaratisha huduma za msingi za afya, elimu huku watoto wakisalia na kiwewe. Mwakilishi wa UNICEF nchini Yemen Julien Harneis amesema [...]

31/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sauti za matumaini kutokana na huduma ya maji zaangaziwa UM

Kusikiliza / Cristina Gallach, msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano kwenye Umoja huo, akizindua rasmi maonyesho ya "Maji kwa Uhai". Picha ya Umoja wa Mataifa/Eskinder Debebe.

Mwaka 2015 ukiwa ni ukomo wa muongo maalum ulioadhimishwa na Umoja wa Mataifa kuhusu maji kwa uhai, uzinduzi wa maonyesho umefanyika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Maonyesho hayo yaitwayo Sauti za maji kwa uhai ni picha zinazoonyesha jinsi upatikanaji wa maji unavyobadilisha maisha ya watu. Aidha uzinduzi huo [...]

31/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Asilimia 50 ya nchi duniani hazijatimiza uandikishwaji wa watoto shuleni

Kusikiliza / Darasa kwa ajili ya wanawake kwenye kambi ya wakimbizi wa Darfour, nchini Sudan, Elimu kwa watu wazima ni miongoni mwa malengo ya Elimu kwa Wote. Picha ya UNAMID/Albert González Farran

Tangu kuzinduliwa kwa malengo ya Elimu kwa wote miaka 15 iliyopita huko Dakar, nchini Senegal, ni asilimia 50 ya nchi zote duniani ambazo zimetimiza malengo hayo ya kuandikisha watoto wote shule ya msingi. Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyomo kwenye ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni UNESCO itakayochapishwa tarehe [...]

31/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto wameuawa na mabomu ya kutegwa ardhini Ukraine

Kusikiliza / Mtoto aliyekimbia makwao na familia yake, kwenye hema ya UNHCR, nchini Ukraine. Picha ya UNHCR.

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limesema kuwa watoto wapatao 109 wameripotiwa kujeruhiwa huku wengine 42 wakiuawa na mabomu ya kutegwa ardhini na mabomu vilipuzi ambavyo havikulipuka katika maeneo ya Donetsk na Luhansk, mashariki mwa Ukraine tangu Machi mwaka 2014. Mwakilishi wa UNICEF ukanda wa Kati na Mashariki mwa Ulaya, Marie Pierre [...]

31/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM Lebanon azuru kambi ya Wapalestina Ein El-Hilweh

Kusikiliza / Sigrid Kaag akitembelea kambi ya wakimbizi ya wapalestina, kusini mwa Lebanon. Picha ya Ofisi wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa Lebanon, UNSCOL.

Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Sigrid Kaag amezuru leo kambi ya wakimbizi wa Palestina ya Ein El-Hilweh kusini mwa Lebanon. Akiwa ameandamana na Bi Heli Uusikyla, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakmibizi wa Palestina, UNRWA, Bi Kaag amekutana na wawakilishi wa kambi hiyo, ambao wamemweleza [...]

31/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban awa na mazungumzo Waziri Mkuu wa Lebanon nchini Kuwait

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon (Kuila) akiwa na Waziri Mkuu wa Lebanon Tammam Salam mjini Kuwait. (Picha: UN/Evan Schneider)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliyeko ziarani Mashariki ya Kati amekuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lebanon, Tammam Salam kando mwa mkutano wa wahisani wa Syria nchini Kuwait. Katika mazungumzo yao, Ban amemshukuru kwa nchi yake kujitoa kwa hali na mali kusaidia wakimbizi wa Syria huku akielezea azma ya Umoja wa [...]

31/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hayati Balozi wa Somalia akumbukwa na mtalaam huru kutoka Tanzania

Kusikiliza / Mwenda zake Balozi Yusuf Mohamed Ismail(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré/2014/maktaba)

Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Somalia, Bahame Tom Nyanduga, amelaani vikali mashambulizi yaliyotokea dhidi ya hoteli moja mjini Mogadishu yaliyosababisha vifo vya raia wengi akiwemo mwakilishi wa kudumu wa Somalia kwenye Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Balozi Yusuf Mohamed Ismail 'Bari Bari'.Ametambua mchango mkubwa wa Balozi Bari bari katika [...]

31/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yapambana na ugonjwa unaothiri kondoo na mbuzi

Kusikiliza / Mifugo@FAO

Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO limezindua leo kampeni ya kutokomeza tauni ya kondoo na mbuzi ifikapo mwaka 2030. Katika taarifa iliyotolewa wakati wa mkutano maalum wa siku tatu kuhusu ugonjwa huo ulioanza mjini Abidjan, nchini Côte d'Ivoire, FAO imesema ugonjwa huo umeongezeka sana katika kipindi cha miaka 15 iliyopita na hivyo kuathiri mifugo [...]

31/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi la kambi ya wakimbizi Yemen

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Zeid Ra'ad Al Hussein@UN Photos Paulo Filgueiras

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al-Hussein, amelaani vikali shumbulizi la angani lililofanywa Jumatatu dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya Al-Mazraq huko Harad, kaskazini mwa Yemen, na kuzitaka pande husika katika mzozo kuwalinda raia na kuheshimu sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na ya kibinadamu. Cecile [...]

31/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wasyria hawaombi kuhurumiwa, wanaomba msaada- Ban

Kusikiliza / Mama na mwanawe kutoka Syria katika kambi ya Zaátri nchini Jordan (Picha© UNHCR/S.Malkawi)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameuambia mkutano wa kutoa ahadi za ufadhili kwa ajili ya Syria mjini Kuwait kuwa, watu wa Syria ni waathiriwa wa tatizo baya zaidi la kibinadamu la nyakati zetu, huku akikumbusha kuwa raia hao wa Syria hawaombi kuhurumiwa, bali wanaomba kusaidiwa. Akielezea aliyojionea wakati alipozuru kambi za wakimbizi [...]

31/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNODC yazindua mwongozo wa kuimarisha utawala wa sheria Somaliland

Kusikiliza / Picha@UNODC

Mwongozo mpya wa kuimarisha mfumo wa sheria wa jimbo la Somaliland, Somalia umezinduliwa na Shirika la inayohusika na madawa na uhalifu katika Umoja wa Mataifa, UNODC. Chombo hicho ambacho kimeundwa ili kitumiwe na polisi, waendesha mashtaka, wanasheria na majaji katika jimbo hilo, kinatoa mwongozo wa kina kuhusu kuzuia uhalifu na sheria ya uhalifu. Dhamira kuu [...]

31/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mfumo wa upatikanaji wa chakula unahatarisha afya ya binadamu:WHO

Kusikiliza / Wafanayakazi katika kiwanda cha chakula(Picha ya FAO/Giuseppe Bizzarri)

Kuelekea siku ya afya duniani tarehe Saba mwezi ujao, Shirika la afya duniani, WHO linakadiria ongezeko la maambukizi ya magonjwa kupitia vyakula kutokana na mfumo wa upatikanaji wa bidhaa hiyo kutoka inakozalishwa hadi kwa mlaji.Assumpta Massoi na ripoti kamili. (Ripoti ya Assumpta) Taarifa ya WHO kanda ya Ulaya inasema kuna mlolongo mrefu na mgumu wa [...]

31/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa usaidizi Syria wafanyika leo Kuwait

Kusikiliza / Wakimbizi wengi wanomiminika Ugiri nipamoaj na hawa wa Syria Picha ya UNHCR/B. Szandelszky (Maktaba0

Nchini Kuwait hii leo kunafanyika mkutano wa Tatu wa kimataifa kuhusu usaidizi wa Syria ambapo Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu misaada ya kibinadamu Valerie Amos amesema mzozo huo unazidi kuzorotesha hali ya kibinadamu. Akihojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa, Bi. Amos amesema licha ya wahisani kujitoa kwa hali na [...]

31/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amezikwa na Boko Haram angali mzima: Ibrahim, miaka 10

Kusikiliza / Mtoto Ibrahim(Picha ya UM//UNHCR/Hélène Caux)

Kwa kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, kaskazini mwa Cameroon, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR limekuwa likipokea maelfu ya raia wa Nigeria wakikimbia mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram. Baada ya kuwapokea mpakani, wengi wakiwa wamejeruhiwa, kubakwa au kuathiriwa na njaa, UNHCR linawapa hifadhi wakimbizi hao kwenye kambi ya Minawao [...]

30/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu Syria inazorota kila siku- Valerie Amos

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA, Bi. Valerie Amos (Picha ya UM)

Suluhu la kisiasa linapaswa kupatikana haraka nchini Syria, kwani hali ya kibinadamu inazidi kuzorota kila uchao. Hayo yamesemwa na Mratibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu, Valerie Amos, wakati akihutubia mkutano wa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotoa ufadhili kwa watu wa Syria katika mji mkuu wa Kuwait, Kuwait. Bi Amos amesema watoto ndio walioathiriwa zaidi, watoto [...]

30/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kikwete aitaka jamii ya kimataifa isaidie Afrika kupambana na ukosefu wa ajira

Kusikiliza / Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete. Picha: UN Photo/Eskender Debebe

Wakati wa uzinduzi wa kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu ajira bora, linalofanyika kuanzia leo mjini New York, Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete amesema, ingawa amefurahi kuona kwamba ukosefu wa ajira umewekwa kipaumbele na jamii ya kimataifa hadi kuwa moja ya malengo ya maendeleo endelevu, bado nusu ya wafanyakazi duniani kote wanakumbwa na hali ngumu [...]

30/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vanuatu hatarini kukumbwa na njaa

Kusikiliza / Picha: UNICEF Pacific.

Wiki mbili baada ya kimbunga PAM kushambulia visiwa vya Vanuatu, Mratibu wa Misaada ya kidinadamu nchini humo, Osnat Lubrani, ametembelea jimbo la Tafea ambalo ni miongoni mwa visiwa vilivyoathirika zaidi. Bi Lubrani amesema, licha ya jitihada za serikali za kufikisha maji, vyakula na huduma za afya katika kila kisiwa, bado hali ya dharura haijaisha na [...]

30/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hakuna mahitaji mapya ya kibinadamu kutokana na uchaguzi Nigeria- OCHA

Kusikiliza / Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya Kibinadamu, Kyung-wha Kang, akihutubia Baraza la Usalama leo.(Picha ya UM/Loey Felipe)

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya Kibinadamu, Kyung-wha Kang, amelihutubia Baraza la Usalama leo kuhusu mahitaji ya kibinadamu kutokana na mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa Nigeria na nchi jirani, akisema kuwa licha ya ripoti za mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na Boko Haram katika majimbo ya  Yobe, Gombe na Borno, [...]

30/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Moustapha Soumaré awasili Sudan Kusini kama Naibu Mkuu wa UNMISS

Kusikiliza / Mjini Bentiu nchini Sudan kusini(Picha ya UM/JC McIlwaine)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umetangaza kuwasili kwa Bwana Moustapha Soumaré, akiwa ni Naibu Mwakilishi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa nchini humo. Taarifa ya UNMISS imesema Bwana Soumaré anauchukua wadhfa huo akiwa na uzoefu mkubwa katika operesheni za ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa, masuala ya kibinadamu na [...]

30/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukatili unaofanywa na Boko Haram umekithiri dunia isikae kimya:Chambas

Kusikiliza / Mohammed Ibn Chambas(Picha ya UM/Eskinder Debebe)

Ukatili unaotekelezwa na kundi la kigaidi la Boko Haram umekithiri na kuvuka mipaka na hivyo kuwa tishio la dunia amesema mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu waUmoja wa Mataifa,  Magharibi mwa Afrika Mohammed Ibn Chambas. Taarifa kamili na Amina Hassan (TAARIFA YA AMINA) Akihutubia  Baraza la Usalama kwa njia ya video katika kikao kilichojadili athari za [...]

30/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wamulika umuhimu wa maji kwa uhai

Kusikiliza / Ukosefu wa maji ni shida kwenye kambi hii ya wakimbizi wa ndani ya Darfur, nchini Sudan. Picha ya Umoja wa Mataifa/Albert González Farran

Mwaka huu wa 2015, Umoja wa Mataifa ukitimiza muongo maalum wa kuchukua hatua kwa ajili ya maji kwa uhai, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekuwa na mjadala maalum ili kutathmini mafanikio yaliyopatikana. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Akizungumza wakati wa mkutano wa ngazi ya juu uliofanyika leo mjini New York, Naibu [...]

30/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ajira zisizo rasmi na ukosefu wa ajira ni changamoto: rais Kikwete

Kusikiliza / Rais Kikwete akihutubia ECOSOC leo New York. Picha ya R. Ollivier-Mrejen.

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete leo amehutubia katika kongamano la siku tatu kuhusu mikakati mipya ili kutokomeza ukosefu wa ajira, linalofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York. Amesema nchi za kiafrika zimezalisha ajira milioni 37 kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, wakati kila mwaka ni vijana milioni 122 ambao wanaingia kwenye [...]

30/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki Hii-Machi 20- Video

t

30/03/2015 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Ban aelekea Kuwait kwa kongamano la ufadhili kwa Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria wakipiga foleni kwa ajili ya misaada katika kambi ya Za'atri nchini Jordan. Picha: UNHCR / S. Malkawi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, leo anaugana na viongozi wengine nchini Kuwait kwa ajili ya kongamano la kimataifa la kutoa ahadi za misaada ya kibinadamu kwa ajili ya Syria hapo kesho. Akiwahutubia waandishi wa habari mjini Baghdad kabla ya kuelekea Kuwait, Ban amesema.. "Kutoka hapa, naelekea Kuwait kushiriki kongamano la kutoa ahadi [...]

30/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bado nahofia tatizo la usalama na athari kwa raia wa Iraq- Ban

Kusikiliza / Familia iliyopata hifadhi katika hoteli nchini Iraq baada ya kukimbia mapigano. Picha: UNHCR/S.Baldwin

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki-moon, amesema kuwa bado anatiwa wasiwasi na tatizo la kiusalama nchini Iraq na athari zake kwa raia. Ban amesema hayo akikutana na wanahabari mjini Baghdad, mara tu baada ya kukutana na Waziri Mkuu, Haider al-Abadi, Rais Fuad Masum na Spika wa Bunge Saleem al-Jabouri. Ban amesema, wametathmini hatua [...]

30/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yakanusha kuwepo kwa Ebola Iraq

Kusikiliza / Wakaazi mjini Erbil nchini Iraq(Picha ya Rick Bajornas)

Shirika la Afya Ulimwenguni,WHO kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Iraq imekanusha taarifa za kuwepo kwa kisa cha Ebola mjini Abu Gharib kusini mwa Baghdad. Taarifa ya WHO inasema mnamo March 28 chombo kimojawapo cha habari nchini Iraq kiliripoti kuwepo kwa kisa cha Ebola nchini humo na hivyo shirika hilo likaendesha  uchunguzi ili kubaini [...]

30/03/2015 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yataka dunia kunusuru watu wa Syria

Kusikiliza / Usambazaji wa chakula Yarmouk, Syria(Picha ya WFP/Bashar Elias)

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeishukuru taifa la Kuwait kwa kusaidia katika operesheni za ugawaji vyakula nchini Syria na kutolea mwito jumuiya ya kimataifa kuendelea kusaidia jamii za watu wa nchi hiyo wanaoathiriwa na mgogoro unaondelea.Taarifa ya shirika hilo inasema kuongezeka kwa mahitaji ya dharura kunakwenda sambamba na ufinyu wa rasilimali za malighafi [...]

30/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon aipongeza Nigeria kwa uchaguzi

Kusikiliza / 150220-vote

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewapongeza watu wa Nigeria kwa kufanya uchaguzi ambao ameutaja kuwa wenye amani na utulivu kwa ujumla. Aidha amelaani mashambulizi yaliyoripotiwa kufanyika na Boko Haram na wengine ambao wamejaribu kuzorotesha utaratibu wa uchaguzi. Uchaguzi ukiendelea leo jumapili, Katibu mkuu amewaomba wanigeria wote waendelee kukuza hali hiyo ya utulivu [...]

29/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kampeni ya saa ya moja kwa ajili ya dunia yamulika mabadiliko ya hali ya hewa

Jengo la Umoja wa Mataifa wakati wa kampeni ya "Earth Hour", picha ya UN.

  Taa za majengo ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa zitazimwa leo usiku pamoja na zaidi ya majengo maarufu 1,200 duniani kote, viwanda, nyumba za watu binafsi, ofisi, ili kuonyesha mshikamano wa kimataifa katika kupambana na madabiliko ya tabianchi. Kampeni hiyo iitwayo ¨Earth Hour¨ yaani saa moja kwa ajili ya dunia, imeanzishwa mwaka 2007 [...]

28/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon atumainia uchaguzi wa Nigeria wenye amani

Kwa upande wa kulia Rais Jonathan Goodluck akisamiana na Jenerali Muhammadu Buhari ambaye naye anagombea urais. Picha ya UNDP Nigeria.

  Leo ikiwa unafanyika uchaguzi wa rais na wabunge nchini Nigeria, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewaomba raia wote waende kupiga kura kwa wengi. Amekaribisha azimio la pamoja lililotolewa na wagombea rais Goodluck Jonathan, na aliyekuwa rais zamani, Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari, la kuheshimu matokeo ya uchaguzi na kutaka uchaguzi uwe wenye [...]

28/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awaomba viongozi wa Kiarabu kupambana na misingi ya ugaidi

Katibu Mkuu akiongea na waandishi wa habari nchini Misri. Picha ya msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Nchi za Kiarabu zinahitaji kuimarisha utawala wa sheria, kuheshimu haki za wanawake na binadamu wote kwa ujumla ili kufikia utulivu endelevu wa kisiasa. Hii ni kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihudhuria mkutano wa muungano wa nchi za kiarabu, mjini Sharm el-sheik, Misri. Amewasihi viongozi wa Kiarabu waongeze ushirikiano wao [...]

28/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ulinzi wa amani uzingatie eneo husika: Jenerali Mwamunyange

Kusikiliza / Mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akiwa kwenye kikao hicho. (Picha: Tanzania mission to the UN)

Wakuu wa majeshi ya ulinzi na usalama kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanakutana jijini New York kwenye kikao cha siku moja. Lengo ni kujadili mustakhbali wa shughuli za ulinzi wa amani za Umoja huo wakati huu ambapo changamoto mpya zinaibuka. Umoja wa Mataifa unasema miongoni mwa changamoto hizo ni kutakiwa kulinda amani sehemu [...]

27/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Rais Kikwete kuhutubia kuhusu masuala ya ajira New York

Kusikiliza / Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania. (Picha:MAKTABA: UN /Eskinder Debebe)

Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete atashiriki kwenye mkutano maalum utakaofanyika mjini New York wiki ijayo kuhusu mikakati mipya ili kufikia maendeleo endelevu pamoja na kutokomeza ukosefu wa ajira. Rais Kikwete atahutubia mkutano huo utakaoanza tarehe 30 Machi hadi Mosi Aprili, mkutano ambao umeandaliwa na Baraza la Uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC na [...]

27/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa Maji na harakati za kusaka raslimali hii adhimu

Kusikiliza / Maji(Picha ya UM/Evan Schneider)

Maji ni uhai, huu ni usemi maarufu sana miongoni mwa wengi lakini usemi hauonekani kutimia kwa nchi nyingi zinazoendelea kutokana na ukosefu wa rasilimali hii adhimu.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo ya Maji iliyozinduliwa mwezi huu huko India, ifikapo mwaka 2030 uhaba wa maji duniani utakuwa pungufu kwa asilimia 40 iwapo [...]

27/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hafla ya kumbukizi ya utumwa yafana

Kusikiliza / Kumbikizi ya biashara ya utumwa.(Picha ya UM/Devra Berkowitz)

Kukumbuka utumwa na  biashara ya utumwa katika bahari ya Atlantiki huibua hisia za mateso na udhalilishaji hususani kwa bara la Afrika. Katika kuhakikisha matukio kama hayo yaliyo kinyme na haki za binadamu hayajirudiii, Umoja wa Mataifa umekuwa na matukio kadhaa ikiwamo hafla ya kumbukizi ya biashara hiyo haramu.Joseph Msami ni shuhuda katika hafla hiyo iliyofanyika [...]

27/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa inapaswa kuonyesha nguvu zake dhidi ya ugaidi

Kusikiliza / Waziri wa Mambo ya nje ya Ufaransa, Laurent Fabius.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Laurent Fabius amesema raia wa kawaida wanajiuliza kwa nini nchi zinazojiita "Umoja wa Mataifa" hazijaweza kupambana na hatari ya ugaidi na kuiondoa. Ameongeza kwamba kinachoendelea mashariki ya kati ni mpango wa kikatili wa kuwaangamiza watu kwa msingi wa kidini au kikabila. Amesema hayo akizungumza wakati wa mjadala wa [...]

27/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lizipeleke kesi za Iraq na Syria ICC- Kamishna Zeid

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein akihutubia Baraza la Usalama kwa njia ya video.

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra'ad Al Hussein, amelitaka Baraza la Usalama la Umoja huo lichukuwe hatua mathubuti ili kuikomesha mizozo ya Iraq na Syria kwa kuzipeleka kesi za mizozo hiyo kwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC. Kamishna Zeid amesema hayo akilihutubia Baraza hilo kwa njia [...]

27/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO yahitaji dola 124 kutoa misaada ya kiafya Syria

Kusikiliza / Utoaji wa chanjo dhidi ya polio nchini Syria(Picha ya WHO/Syria)

Mgogoro wa Syria ukiwa unaingia mwaka wa tano na ikiwa ni siku chache kabla ya kongamano la tatu la kimataifa la changizo la kibinadamu, shirika la afya ulimwenguni WHO linataka kiasi cha dola 124 ili kuendelea na usaidizi wa kiafaya katika Jamhuri ya Kiarabu ya Syria. Akiongea mjini Geneva mwakilishi wa WHO mjini Damascus Dk [...]

27/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msaada wa WFP wafikia watu 160,000 Vanuatu

Kusikiliza / Raia wa Vanuatu wanaopokea msaada wa WFP. Picha ya Victoria Cavanagh/WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema leo kwamba tayari vyakula vya msaada vimefika kwenye visiwa 22 ambavyo vimeathirika na kimbunga PAM, nchini Vanuatu. Taarifa ya WFP imesema kwa sasa wanasaidia harakati zianzoongozwa na serikali za kupanga masuala ya mgao wa misaada, huduma za vifaa na usafirishaji na kuwapatia vyakula vya ziada pale vile [...]

27/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uhalifu wa jinai Mashariki ya Kati ukabiliwe kwa dharura- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon. (Picha:UN/Evan Schneider)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kuwa makosa ya jinai yanayofanywa katika ukanda wa Mashariki ya Kati yanahitaji kukabiliwa kwa dharura. Ban amesema hayo wakati akilihutubia Baraza la Usalama, ambalo limekutana leo kufanya mjadala wa wazi kuhusu wahanga wa mashambulizi na ukiukwaji dhidi ya makundi ya walio wachache kikabila au kidini [...]

27/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Azimio la nafasi ya mtaalamu wa haki za albino lapitishwa Geneva

Kusikiliza / Mtoto kama huyu wa DRC aliye na ulemavu wa ngozi, albino wako hatarini ya ukatili katika baadhi ya nchi(Picha ya UM /Marie Frechon)

Katika kuhakikisha vitendo dhalimu dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino ikiwamo mauaji na ubaguzi vinatokomezwa Umoja wa Mataifa umepitisha azimio la kuanziswha kwa nafasi ya mtaalamu maalum kuhusu haki za kundi hilo atakayechunguza ukatili dhidi ya albino na kukuza usawa.Katika kikao cha 28 cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa [...]

27/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban afungua mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi duniani

Kusikiliza / Zaidi ya viongozi 300 wa jeshi wamehudhuria mkutano wa wakuu wa majeshi ya ulinzi. Picha ya DPKO.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefungua mkutano wa kwanza kabisa wa wakuu wa majeshi ya ulinzi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa akitaja mambo mawili ambayo ni muhimu kuimarisha operesheni za ulinzi wa amani za umoja huo. Mosi mchango wa askari na vifaa pindi ujumbe unapoanzishwa na pili utashi wa kisiasa [...]

27/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu kujadili ukiukwaji wa Boko Haram

Kusikiliza / Katika jimbo la Borno, kaskazini mwa Nigeria, baada ya mashambulizi ya Boko Haram. Picha ya UN.

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, limetangaza leo kuwa litafanya kikao maalum mnamo Aprili mosi kuhusu ukiukwaji unaotekelezwa na kundi la Boko Haram. Hatua hiyo inafuatia ombi la ujumbe wa Algeria kwa niaba ya wawakilishi wa Afrika kwenye Baraza hilo, ambalo liliwasilishwa kwenye sekritariati ya Baraza mnamo Alhamis jioni. Hapa, ni Rais [...]

27/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tume huru ya uchunguzi Syria yapewa mwaka mmoja zaidi

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria nchini Lebanon. Picha: WFP

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuongeza kwa mwaka mmoja zaidi muda wa tume huru ya kimataifa ya uchunguzi kuhusu Syria. Azimio hilo limepitishwa kwa kura 29 huku Sita zikipinga na nchi 12 hazikuonyesha upande wowote. Kwa mujibu wa azimio hilo, hatua hiyo inatokana na kuendelea kuzorota kwa hali [...]

27/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNHCR yashutumu LRA kwa kuteka wakimbizi wa DRC

Kusikiliza / Raia wa DRC wakikimbia mashambulizi ya LRA kwenye jimbo la Orientale. (Picha:Maktaba UNHCR/D.Nthengwe)

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeshutumu vikali kitendo cha waasi wa Lord's Resistance Army, LRA cha kuteka nyara wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wakimbizi hao 15 na raia mmoja wote walitekwa nyara Jumamosi wakati wakilima shamba lao lililo upande wa DRC karibu na mpaka na Jamhuri ya Afrika [...]

27/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mauaji ya Albino Malawi yachukua hatua, Tanzania nayo iimarishe:UM

Kusikiliza / Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino. (Picha:@UNICEF Tanzania/Giacomo Pirozzi)

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha mpango wa hatua tano uliotangazwa na serikali ya Malawi katika kukabiliana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino. Msemaji wa ofisi hiyo Rupert Colville akizungumza Geneva, Uswisi ametaja mpango huo kuwa ni Mosi elimu kwa umma, pili, kuimarisha ulinzi wa kijamii na kuongeza [...]

27/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu Syria imezorota, yataka suluhu la kisiasa

Kusikiliza / Valerie Amos akihutubia Baraza la Usalama leo. Picha ya UM

Mratibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos, ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa, jamii ya kimataifa inapswa kuonyesha ari zaidi ili kufikia suluhu la kisiasa kwa mzozo wa Syria. Bi Amos amesema, kama baraza hilo lilivyosema mara kwa mara, hakuna suluhu la kibinadamu [...]

26/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Singapore yaendelea na maombolezo

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akitia saini kwenye kitabu cha maombolezo katika ofisi za ujumbe wa kudumu wa Singapore katika Umoja wa Mataifa jijini New York. Aliyesimama ni mwakilishi wa kudumu wa Singapore Balozi Karen Tan. (Picha: UN/Evan Schneider)

Singapore inaendelea na maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Baba wa Taifa hilo Lee Kuan Yew. Lee ambaye anajulikana kama Baba wa Taifa la Singapore, alifariki dunia Jumatatu akiwa na umri wa miaka 91. Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametuma salamu za rambirambi kwa serikali na wananchi wa Singapore kufuatia kifo [...]

26/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Alikuwa mtoto vitani miaka 10, sasa awasaidia wahanga wengine

Kusikiliza / Picha ya Umoja wa Mataifa.

Wakati wa mjadala maalum wa Baraza la Usalama kuhusu watoto waliotumikishwa vitani, Junior Nzita Nsuami, kijana mmoja kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, amewaelezea Wanachama wa Baraza hilo mateso aliyoyapitia akiwa miongoni mwa watoto hao. Kijana huyo alitumikishwa vitani tangu alipokuwa na umri wa miaka 12, na akajisalimisha akiwa na umri wa miaka 22. [...]

26/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Heko India kwa usaidizi wa kudhibiti saratani: IAEA

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA, Yukia Amano alipokutna na  R. A Badwe nchini India(Picha ya Tata Memorial Centre )

  Mkurugenzi Mkuu wa shirika la nishati ya atomiki duniani, IAEA, Yukia Amano amesema kuanzishwa kwa mipango bora ya kudhibiti saratani kwenye nchi zinazoendelea kunadhihirisha jinsi teknolojia ya nyuklia inavyoweza kuchangia maendeleo duniani. Bwana Amano amesema hayo wakati wa ziara yake kwenye kituo cha saratani cha hospitali ya kumbukumbu ya Tata mjini Mumbai, nchini India. [...]

26/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sanaa ya kukumbuka utumwa yazinduliwa New York

Kusikiliza / Uzinduzi wa Safina ya Marejeo au "The Ark of Return". Picha ya Eskinder Debebe/Umoja wa Mataifa.

Safina ya marejeo au The Ark of Return kwa kiingereza ni sanaa iliyochongwa na msanifu wa Marekani Rodney Leon ili kukumbuka daima utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati ambapo muongo wa watu wenye asili ya kiafrika imeanza rasmi. Katibu Mkuu Ban [...]

26/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuyakalia maeneo ya Wapalestina na mizozo inaongeza mahitaji ya kibinadamu- OCHA

Kusikiliza / Makazi ya Gaza. Picha ya UNRWA.

Mahitaji ya kibinadamu katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa yanaongezekakutokana na kuendelea kwa Israel kuyakalia maeneo hayo na mizozo ya mara kwa mara, kulingana na tathmini ya mwaka 2014 ya Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA. Kulingana na ripoti hiyo iitwayo, "Maisha yaliyovurugika", raia wa Palestina wanaendelea kuwa wahanga wa vitisho kwa maisha yao, usalama [...]

26/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuelekea uchaguzi Nigeria, Chambas awasilisha ujumbe wa Ban

Kusikiliza / Mohammed Ibn Chambas, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Afrika Magharibi. (Picha:UNOWA)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Afrika Magharibi, Mohammed Ibn Chambas anaendelea kufuatilia kwa karibu hali nchini Nigeria wakati huu ambapo nchi hiyo inaelekea uchaguzi mkuu keshokutwa Jumamosi. Umoja wa Mataifa kupitia Naibu Msemaji waje Farhan Haq umetolea mfano ziara ya Alhamisi ya mwakilishi huyo huko jimbo la Gombe, [...]

26/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ana taarifa za kinachoendelea Yemen

Kusikiliza / Uharibifu wa mali na miundombinu unaosababishwa na mapigano baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo inakadiriwa kuwa asilimia 95 katika baadhi ya maeneo ya Yemen. Picha: OCHA / EmanAl-Awami

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ana taarifa ya kwamba Saudi Arabia imetangaza kuanza operesheni za kijeshi nchini Yemen kufuatia ombi la serikali hiyo. Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari akiseam kuwa Ban ana taarifa kuwa nchi nyingine hususan zile ambazo ni wanachama wa [...]

26/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ataja changamoto za mkataba wa kupinga matumizi ya silaha za kemikali:

Kusikiliza / Nchini Iraq mwaka 1991, mmoja wa wajumbe wa Tume maalum ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa wakati wa ukaguzi wa silaha za nyuklia, kemikali na baiolojia nchini humo. (Picha: UN /H Arvidsso)

Miaka 40 tangu kupitishwa kwa mkataba wa kimataifa wa kupiga marufuku matumizi ya silaha za kikemikali, kuna matumaini kwasababu katika kipindi hicho kumekuwepo na jitihada za pamoja za kutokomeza matumizi yake. Hiyo ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku ya leo ya mkataba huo wa kupinga [...]

26/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jumuiya ya kimataifa inawajibu wa kusaidia kumaliza mgogoro wa Israel na Palestine

Kusikiliza / Picha:2014/UNRWA/Taghrid Mohammad

Baraza la Usalama leo limekuwa na mashauriano kuhusu hali Mashariki ya Kati ambapo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Amani katika ukanda huo Robert Serry amelihutubia baraza hilo akisema bado mvutano kati ya Palestina na Israel unaendelea kuleta madhara makubwa kwa watu  wa Gaza na  kutaka suluhu la kisiasa [...]

26/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wapunguzwa DRC, waongezwa CAR

Kusikiliza / Walinda amani wa MONUSCO wakisimamia shughuli za kujisalimisha kwa waasi mashariki mwa DRC. Picha ya MONUSCO.

Baraza la Usalama leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza muda wa mamlaka za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa mwaka mmoja zaidi. Taarifa kamili na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Azimio la kuongeza muda huo pia limepunguza askari 2,000 kutoka kundi la walinda amani nchini DRC, [...]

26/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa UM kukutana NY

Kusikiliza / Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed, Mnadhimu Mkuu wa Ofisi ya Kijeshi ya Idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa. Picha:Grece Kaneiya

Mkutano wa kwanza kabisa wa wakuu wa majeshi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa utafanyika kesho kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York. Mnadhimu Mkuu wa Ofisi ya Kijeshi ya Idara ya Ulinzi wa Amani ya Umoja wa Mataifa Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed amesema lengo ni kuangalia jinsi ya kukabiliana na changamoto [...]

26/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mustakhbali wa afya CAR uko njiapanda:WHO

Kusikiliza / Hali ya afya nchini CAR inasuasua(Picha ya WHO/C.Black)

Shirika la afya duniani, WHO na wadau wake wanahitaji dola Milioni 63 kwa ajili ya huduma za tiba na afya ya uzazi huko Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR. WHO imesema kiasi hiyo kinalenga kuimarisha huduma za afya ambazo bado hazijakwamuka licha ya amani kuimarika kwa kiasi fulani. Kwa mujibu wa WHO, nchini CAR vituo [...]

26/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya waomba hifadhi ilivunja rekodi mwaka 2014 – UNHCR

Kusikiliza / Msichana huyu kutoka Syria amelala karibu na baba yake baada ya kuokolewa bahari ya mediterenia.(Picha ya UNHCR/A.D'Amato)

Vita nchini Syria na Iraq, pamoja na mizozo ya silaha katika nchi zingine, vilisababisha kuongezeka kwa idadi ya waomba hifadhi katika nchi zilizostawi kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miaka 22. Taarifa kamili na Joseph Msami. Taarifa ya Msami Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, [...]

26/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Lazima wanawake tukaze mwendo safari ndefu: Rais Ellen Jonhson Sirlief

Kusikiliza / Rais Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia. (Picha:UN/Paulo Filgueiras)

Bado nafasi ya mwanamke ni finyu duniani kwa mfano malipo ya mishahara kwa wanawake yanatofautiana na wanaume kwasababau tu za kijinsia. Ni sehemu ya kauli ya Rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf wakati akihojiwa na Joseph Msami wa Idhaa hii jijini New York, Marekani. Rais huyo wa kwanza mwanamke barani Afrika pia amesema ili kuepuka migogoro Afrika [...]

26/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kizazi hiki lazima kipate elimu juu ya utumwa: Ban

Kusikiliza / Kumbukizi ya utumwa iliyopo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Picha ya UN/Devra Berkowitz.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki- Moon amesema ni muhimu kizazi hiki kifahamu madhara ya biashara ya utumwa ili kuhakikisha vitendo hivyo havijirudii katika historia ya mwanadamu kote duniani. Akiongea katika kumbukizi ya siku hii baada ya kuzindua katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kumbukizi ya kudumu ya wahanga [...]

25/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nafasi ya mwanamke katika meza ya majadiliano ni muhimu:KEWOPA

Kusikiliza / Wanwake wa bunge la Kenya (Kewopa)Picha ya UM/radio/kiswahili

Ushirikishwaji wa  wanawake katika maswala mbali ya kijamii ni muhimu kwa ajili ya maendeleo kwa wote. Hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa inahakikisha  wanawakilishwa ipasavyo katika meza ya majadiliano hususan wakati huu ambapo dunia inafikia ukomo wa malengo ya maendeleo ya milenia na kuanza malengo ya maendeleo endelevu. Hilo limedhihirisha wakati wa mahojiano kati ya [...]

25/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Nimeibiwa utoto wangu, asema kijana aliyetumikishwa vitani DRC

Kusikiliza / Junior Nzita Nsuami, ambaye alitumikishwa na waasi nchini DRC akiwa na umri wa miaka 12 akihutubia Baraza la Usalama jijini New York. (Picha:UN/Devra Berkowit)

Huyu ni Junior Nzita Nsuami, kijana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC aliyeetumikishwa na waasi wakati wa vita dhidi ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Mobutu Sese Seko. Anasema amepitia mateso mengi mwilini mwake, yeye ni mhanga wa utumikishwaji watoto vitani na ametumikishwa na waasi wakati akiwa na umri wa miaka 12. Junior [...]

25/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Maendeleo endelevu na ujuimuishwaji ni ufunguo wa maendeleo: Mshiriki wa mkutano

Kusikiliza / Picha: Kiswahili Radio/UM

Wakati mkutano wa kupanga na kutekeleza malengo endelevu na majadiliano ya kimataifa ukiendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, ushirikishwaji wa makundi yote katika jamii na nammna ya kuyatekeleza kwa kuzingatia mahitaji ya nchi vimemulikwa. Mkutano huo unaoleta wawakilishi wa nchi na asasi za kiraia pamoja, umejadili nafasi na ushiriki wa [...]

25/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

WPF yapokea magari 67 kutoka Urusi

Kusikiliza / Magari ya WFP kutoka Urusi(Picha ya UM/Radio kswahili)

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Uganda limekaribisha mchango wa magari ya mzigo 67 kutoka serikali ya Urusi ambayo yatasaidia kuimarisha uwezo wake wa kusambaza chakula katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati. John Kibego na maelezo kamili. (Taarifa ya John Kibego) Magari hayo aina ya KAMAZ ni sehemu ya mchango wa kimataifa [...]

25/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji wa haki unaotisha umefanyika Iraq- Ripoti

Kusikiliza / Wanawake wa Mosul. Picha: HCR/S. Baldwin (Maktaba)

Ukiukwaji wa haki za binadamu ambao watu wa Iraq wamekuwa wakikumbana nao ni mkubwa na ulioenea kwa njia inayotisha. Hayo yamesemwa na Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Flavia Pansieri. Bi Pansieri amesema hayo mbele ya Baraza la Haki za Binadamu, akiwasilisha ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iraq katika muktadha wa [...]

25/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za msichana mkimbizi zaleta nuru Uganda

Kusikiliza / Sarah Mayi kwenye sherehe za siku ya wanawake aktika kambi  ya Kyangwali, Uganda(Picha ya UM/UN radio kiswahili)

Ukimbizini, watu hujishughulisha na kazi mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya kilasiku na kustawi kiuchumi kando na msaada kutoka kwa mashirika mbali mbali yakiwamo yale ya Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa harakati hizo ni klimo na biashara ambapo wakimbizi hushikana mikono. John Kibego anakuletea mahojiano na  msichana kutoka Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye amepata matumaini [...]

25/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto milioni 15 wahanga wa ukatili vitani mwaka 2014:

Kusikiliza / Picha: UNICEF/UNHQ-2015-0203/RICH

Baraza la Usalama leo limekuwa na mjadala maalum kuhusu watoto walio wahanga wa vikundi vilivyojihami, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akisema mwaka 2014 umekuwa mwaka mbaya zaidi kwa usalama wa watoto, milioni 15 wakiwa wahanga wa ukatili huo. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Akihutubia Baraza la Usalama, Ban [...]

25/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo endelevu yawe jumuishi na shirikishi

Kusikiliza / Jamii ya wafugaji ya wamaasai nchini Kenya(Picha ya UM/Andi Gitow)

Wawakilishi wa mataifa na asaasi za kiraia wanakutana mjini New York katika mjadala kuhusu uandaaji na utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015 huku mjadala ukijikita katika kuhakikisha mfumo shirikishi na jumuishi. Miongoni mwa wanaohudhuria ni mwakilishi wa jamii ya wafugaji nchini Tanzania kutoka taasisi ya wafugaji na maendeleo (PIDO) Martha Ntoipo [...]

25/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kinga na hadhi ya watendaji wa UM viheshimiwe: Ban

Kusikiliza / Gert Danielsen (anayetizama kamera),mfanyakazi wa UNDP akimkumbatia mfanyakazi mwenzake baada ya kuachiliwa huru huko Sana'a, Yemen. (Picha: UN Maktaba/UNDP/Noeman Al Sayyad )

Katika siku ya kuonyesha mshikamano na wafanyakazi wanaoshikiliwa au wasiojulikana waliko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kuimarishwa kwa juhudi za kulinda watendaji hao wanapokuwa kwenye majukumu yao. Ban amesema ghasia na mizozo iliyoenea mwaka uliopita imekuwa na gharama kwa Umoja wa Mataifa na watendaji wake kwani hadi tarehe 15 mwezi huu [...]

25/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watetezi wa haki za binadamu Libya wanashambuliwa- ripoti

Kusikiliza / Baraza la haki za binadamu kikao cha 18, mjini Geneva, Uswizi.(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré)

Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu imebainisha kuwepo mashambulizi mengi na vitisho dhidi ya watetezi wa haki za binadamu nchini Libya, na wakati mwingine hata baada ya kulazimika kuondoka nchini humo. Ripoti hiyo ya pamoja ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL na Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja [...]

25/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majaribio ya chanjo ya Ebola kuanza Guinea

Kusikiliza / Chanjo ya ebola yafanyiwa majaribio nchini Guinea(Pichaya UM/WHO/M. Missioneiro/maktaba)

Serikali ya Guinea na Shirika la Afya Duniani, WHO, zimezindua majaribio ya kwanza kabisa ya chanjo ya Ebola wiki hii katika jamii iliyoathiriwa ya Basse-Guinée, ambayo ni moja ya maeneo ambako visa vya Ebola ni vingi zaidi nchini humo. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Jaribio hilo la dawa ya chanjo aina ya [...]

25/03/2015 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki ya dunia yarejesha operesheni zake Guinea Bissau

Kusikiliza / Picha: World Bank

Benki ya dunia imetangaza kuanza tena kwa operesheni zake nchini Guinea Bissau baada ya kusitisha kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwezi Aprili mwaka 2012. Tangazo hilo limetolewa wakati wa mjadala wa bodi tendaji ya Benki hiyo kuhusu hatma ya uhusiano kati yake na nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya dunia nchini Guinea [...]

25/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanawake watumwa walikuwa jasiri licha ya madhila: Ban

Kusikiliza / Picha@UM

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya wahanga wa utumwa na biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki, Umoja wa Mataifa umeamua kutumia siku hiyo kukumbuka wanawake wengi watumwa waliosimama kidete kutetea utu wa jamii zao licha ya madhila yaliyokuwa yanawapata.Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon katika ujumbe wake wa siku hiyo [...]

25/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama yazorota nchini Mali : Mtalaam wa UM

Kusikiliza / Walinda amani wakiwa kwenye doria kwenye moja ya maeneo, nchini Mali. (Picha ya @MINUSMA)

Nchini Mali, hali inazidi kuwa tete kutokana na vitisho vya usalama kutoka kwa waasi wanaotaka kuweka dola la uislamu wenye msimamo mkali na wale wanaotaka uhuru wa maeneo ya kaskazini mwa Mali ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya Mali tangu 2012. Hii ni kwa mujibu wa mtalaam maalum kuhusu haki za binadamu nchini humo, Suliman [...]

24/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Cote d'Ivoire iendelee na jitahada zake inapoelekea uchaguzi

Kusikiliza / Kujisalimisha kwa waasi bado ni changamoto kubwa nchini Côte d'Ivoire. Picha ya UNOCI.

Jitihada za Côte d'Ivorie katika kurejesha usalama, kuimarisha sekta ya sheria na kusalimisha waasi zinapaswa kuendelea, wakati ambapo nchi hiyo inaelekea uchaguzi wa rais mwezi wa Oktoba mwaka huu amesema mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uwezeshaji wa uwezo wa Cote d'Ivoire, Mohammed Ayat. Amesema hayo katika mjadala uliofanyika leo mjini Geneva, Uswisi kwenye [...]

24/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lakariri nia yake ya kuiwekea Sudan Kusini vikwazo

Kusikiliza / Wakati wa kikao cha Baraza la Usalama.(Picha ya Devra Berkowitz)

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamesema kuwa hali nchini Sudan Kusini inahitaji kukabiliwa kwa dharura, wakiongeza kuwa pande zote zinazozozana zinapaswa kutoa amri dhahiri zinazopinga ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria ya haki za binadamu, na ukiukwaji mwingine bila kuchelewa. Baraza hilo limeelezea kusikitishwa na kushindwa kwa Rais [...]

24/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM hautabagua wanandoa wa jinsia moja

Kusikiliza / Umoja wa Mataifa hautabagua wanandoa wa jinsia moja. Picha ya IRIN.

Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya usimamizi katika Umoja wa Mataifa, Yukio Takasu, amesema leo kuwa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu ikielekeza kuhusu marupurupu ya wafanyakazi wa Umoja wa huo ikiwemo pale wanapofunga ndoa, ilitokana na kanuni za Umoja wa Mataifa za utangamano wa watu wenye asili tofauti na kutobagua. Bwana Takasu amesema hayo [...]

24/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kuchangia ubinadamu Syria kufanyika mwishoni mwa mwezi huu

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria(Picha ya UNHCR)

Mkutano wa Tatu wa kimataifa kuhusu usaidizi wa Syria  utafanyika huko nchini Kuwait tarehe 31 mwezi huu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ndiye atakuwa mwenyekiti wa mkutano huo utaokuwa chini ya uenyeji wa kiongozi mkuu wa Kuwait Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah. Viongozi wengine waandamizi watakaohutubia ni kutoka ofisi ya Umoja wa [...]

24/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Biashara mtandao ni fursa lakini umakini wahitajika: UNCTAD

Kusikiliza / Mwelekeo sasa ni biashara mtandao lakini kwa umakini. (Picha:UNCTAD)

Ripoti mpya ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema kuna fursa kwa nchi zinazoendelea kunufaika na biashara mtandao, E-Commerce. Pamoja na fursa, ripoti hiyo iliyotolewa Jumanne pia inataja hatari zitokanazo na ununuzi na uuzaji wa bidhaa kupitia mitandao. Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara ni mojawapo ya [...]

24/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto waendelea kuathirika zaidi na mzozo Yemen

Kusikiliza / Watoto nchini Yemen(Picha:Tovuti OCHA)

  Vurugu inayoendelea nchini Yemen inazidi kuathiri watoto, idadi ya watoto wanaouawa au kujeruhiwa mwaka 2014 ikiwa imeongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na mwaka 2013. Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, Christophe Boulierac, amesema hali hiyo imesababishwa na mapigano yanayozidi nchini humo, akitaja mfano wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea kwenye [...]

24/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNSMIL yatoa mapendekezo ya kuumaliza mzozo wa kisiasa Libya

Kusikiliza / Nembo ya UNSMIL

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Libya, Bernardino Leon, ametembelea miji ya Tobruk na Tripoli ili kuwasilisha mapendekezo yake kuhusu jinsi ya kuongeza kasi ya mazungumzo ya amani, ambayo yamekuwa yakiendelea kwa majuma kadhaa, wakati hali ya usalama inapozidi kuzorota na kuhatarisha mazungumzo hayo.Mapendekezo hayo ni pamoja na kuunda serikali ya mseto ikiongozwa na rais, [...]

24/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushairi na nafasi yake katika maridhiano nchini Somalia

Kusikiliza / Mshairi Halima Ma'alim Abukar akiwa studioni. (Picha: Video capture UNSOM)

Somalia, nchi inayojulikana duniani kwa utamaduni wa mashairi. Hivi sasa sanaa hiyo inatumika kuimarisha amani na maridhiano kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza zaidi ya miongo miwili iliyopita. Mabingwa wa utunzi na ughani wanachukua nafasi yao huku harakati zikiendelea ili kurithisha tasnia hiyo adhimu kwa vijana ambapo tayari jukwaa la wasani nchini humo [...]

24/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 29 zahitajika kunusuru watu wa Vanuatu.

Kusikiliza / Picha:Vanuatu/OCHA

Changisho la dharura limezinduliwa leo kwa ajili ya kusaidia zaidi ya nusu ya idadi ya watu nchini Vanuatu walioathiriwa na kimbunga PAM kilichoikumba nchi hiyo siku 11 zilizopita. Changisho hilo linataka jumuiya ya kimataifa kuchangia zaidi ya dola miloni 29 ili kusaidia serikali katika kukabilina na athari za kimbunga PAM ambapo zaidi ya watu elfu [...]

24/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Utafiti waonyesha ukatili dhidi ya watoto Malawi umeenea- UNICEF

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Tobin Jones

Watu wawili kati ya watatu nchini Malawi hukumbana na ukatili wakiwa watoto, huku msichana mmoja kati ya watano akikumbana na ukatili wa kingono kabla ya kutimu umri wa miaka 18, limesema Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Taarifa kamili na Joshua Mmali. (Taarifa ya Joshua) Hayo yamebainika katika ripoti mpya ya utafiti uliofanywa nchini Malawi kuhusu [...]

24/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kifua Kikuu bado ni tishio tuchukue hatua:WHO

Kusikiliza / Barakoa zazuia maambukizi ya kifua kikuu. Picha ya IRIN/David Gough

Leo ni siku ya Kifua Kikuu, TB, duniani ambapo Shirika la Afya Duniani, WHO linataka utekelezaji wa mkakati utakaotokomeza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu, wagonjwa sambamba na machungu yatokanayo na ugonjwa huo ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utambuzi mapema wa wagonjwa. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) Mkakati huo unataja misingi mikuu mitatu [...]

24/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu CAR bado zinatia wasiwasi

Kusikiliza / CAR waislamu UN Photo-Evan Schneider

Mtalaam huru kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Marie-Thérèse Keita Bocoum ameeleza wasiwasi wake juu ya watu kutoka makundi madogomadogo wanaokumbwa na ukiukaji wa haki za bainadamu. Akizungumza wakati wa mjadala maalum kuhusu CAR kwenye Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi, mtalaam huyo amekaribisha jitihada zilizofanywa [...]

24/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNHCR awatembelea wakimbizi wa Nigeria kaskazini mwa Cameroon

Kusikiliza / Wakimbizi wa kutoka Nigeria wakipanga foleni kuteka maji katika kambi ya Minawao nchini Cameroon(Picha ya UNHCR/D.Mbaiorem)

Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameanza ziara ya siku mbili Cameroon, ambayo inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Nigeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Kwa mujibu wa mamlaka za jimbo la Kaskazini mwa Cameroon, zaidi ya wakimbizi 74,000 wa Nigeria [...]

24/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya mafanikio Kifua Kikuu bado ni tishio tuchukue hatua:WHO

Kusikiliza / WHO yataka mshikamano kutokomeza Kifua Kikuu duniani. (Picha:Tovuti ya WHO)

Leo ni siku ya Kifua Kikuu, TB, duniani ambapo shirika la afya duniani, WHO linataka utekelezaji wa mkakati wenye lengo la kuwa na dunia isiyo na vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu, wagonjwa sambamba na machungu yatokanayo na ugonjwa huo ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana kupitia utambuzi mapema wa wagonjwa. Mkakati huo unataja misingi mikuu mitatu ya kuzingatiwa [...]

24/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN Women kwenye ziara ya mshikamano na Sierra Leone

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa UN-Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka. (Picha: UN/Eskinder Debebe)

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women,  Phumzile Mlambo-Ngcuka, yumo ziarani nchini Siera Leone, akidhamiria kuonyesha mshikamano wa shirika hilo na serikali na watu wa Sierra Leone, wakati huu ambapo taifa hilo linaendelea kukabiliana na athari za mlipuko wa Ebola nchini humo, ambao uliwaambukiza zaidi ya watu 10,000, kuwaua 3480 na [...]

23/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Misemo ya wahenga yadhihirika kambini Kyangwali nchini Uganda

Kusikiliza / Betty akiwa katika ya wanaotafsiri hotuba yake akiongea ka Mgeni wa Heshima. Picha: Kibego.

Wahenga walisema penye nia pana njia na kama haitoshi haba na haba hujaza kibaba! Misemo hiyo imedhihirika huko kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda ambako mwanamke mmoja mkimbizi kutoka Sudan Kusini licha ya kuishi mazingira magumu, ametumia fursa zilizokuwa zinamzingira kubadili siyo tu maisha yake bali na ya jamii inayomzunguka. Je amefanya nini? [...]

23/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yazindua chombo cha kurahisisha upatikanaji wa takwimu zake

Kusikiliza / Ukusanyaji wa takwimu(Picha ya UNICEF)

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF limebadilisha tovuti zake za takwimu ili kuwezesha upatikanaji rahisi wa takwimu zake kuhusu afya, lishe, elimu, maji na huduma za kujisafi, ulinzi wa watoto na HIV na Ukimwi. Takwimu hizo sasa zimewekwa katika muundo ambao unajumuisha maelezo kuhusu nchi na chombo cha kuonyesha picha za takwimu [...]

23/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kutokomeza ukeketaji Kenya ifikapo 2030 kunawezekana: wajumbe

Kusikiliza / Asmah Mohamed, mtoto wa miaka 6, akifarijiwa na mama yake baada ya kukeketwa, nchini Kenya. Picha ya UNICEF/NYHQ2005-2229/Getachew

Mwelekeo wa kupunguza ukeketaji nchini Kenya unaleta matumaini ya kutokomeza mila hiyo inayoathiri wanawake na wasichana nchini humo. Hii ni kwa mujibu wa Martha Tureti, mfanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la World Vision linalohamasisha jamii nchini Kenya ili kuondoa vitendo vya ukeketaji. Akizungumza na idhaa hii wakati wa  Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu [...]

23/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 6.2 zahitajika kusaidia wakulima CAR

Kusikiliza / Wakulima wakipalilia shamba huko CAR. Picha: FAO

Wakulima huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wana mahitaji ya dharura ya mbegu na pembejeo kwa ajili ya msimu wa upanzi unaonza mwezi ujao, limesema shirika la chakula na kilimo duniani, FAO. Katika taarifa yake, FAO imesema msaada huo wa dharura ni muhimu ili kuepusha kuzorota zaidi kwa usalama wa chakula na hali ya [...]

23/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujangili wa tembo umeendelea kwa hali ya juu mwaka 2014

Kusikiliza / Tembo Picha@UNCEP

Takwimu mpya zinaonyesha kuwa mauaji haram ya tembo kwa mwaka 2014 yameendelea kwa kiwango cha juu ambacho kinaathiri uwepo kwa tembo katika siku za usoni. Taarifa ya Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Ripoti hiyo iliyotolewa na Mktaba wa kimataifa kuhusu biashara ya vyumbe vilivyo hatarini, CITES, imesema kiwango cha ujangili hakijaongezeka mwaka 2014 ikilinganishwa na [...]

23/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Amani ni lazima ipatikane Gaza baada ya uharibifu mkubwa- ripoti

Kusikiliza / Jengo ambalo linadaiwa kushambuliwa na shambulio la angani la Israeli mwezi Agosti (Picha ya UM/Shareef Sarhan)

Waisraeli, Wapalestina pamoja na jamii ya kimataifa wana wajibu wa kumaliza uhasama ambao unatishia kulipua mzozo wa mara kwa mara, na kuepusha ukiukaji zaidi wa haki za binadamu, kwa mujibu wa ripoti mypa za Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na Joshua Mmali. Taarifa ya Joshua Ripoti kuhusu hali ya haki za binadamu katika maeneo ya [...]

23/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki Hii Machi 13-Video

pp

23/03/2015 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Tanzania, Kenya na Msumbiji zatajwa ripoti ya WMO 2014

Kusikiliza / Mafuriko nchini Malawi, mwezi Oktoba, 2014. Picha ya UN Malawi

Leo ikiwa ni siku ya utabiri wa hali ya hewa, Shirika la Kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limesema mwaka 2014 ulikuwa na joto kali zaidi kihistoria, maeneo mengi ya dunia yakiwa yamekumbwa pia na mafuriko. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Katika ripoti yake iliyotolewa leo, WMO imesema kiwango cha [...]

23/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

PAM yasambaratisha zaidi ya asilimia 80 ya shule huko Vanuatu

Kusikiliza / Picha:UNICEF

Kimbunga PAM kilichopiga hivi karibuni nchi ya Vanuatu kimeripotiwa kuathiri takribani watu 166,000 kwenye visiwa 22 vilivyopo nchini humo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema idadi hiyo ya waathiriak ni pamoja na watoto 82,000 ambao sasa hawawezi kwenda shule kutokana na shule zao kusambaratishwa au kugeuzwa makazi ya kimbilio kwa waathirika [...]

23/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki Hii Machi 6-Video

p

23/03/2015 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

FAO yalenga kuongeza fedha kwa ajili ya lishe na mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva akihutubia mkutano(Picha ya FAO/Giulio Napolitano)

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakula na kilimo duniani, FAO José Graziano da Silva amefungua mkutano wa wiki nzima wa baraza tendaji la shirika hilo akisihi wajumbe walegeze misimamo yao juu ya mpango wa kazi na bajeti ya chombo hicho. Da Silva amesema bajeti pendekezwa ya zaidi ya dola Bilioni Moja kwa kipindi cha mwaka [...]

23/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laonywa kuwa Yemen yaelekea kusambaratika

Kusikiliza / baraza-la-usalama: Picha ya UM

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, wamekutana Jumapili mchana kuhusu hali Mashariki ya Kati, wakimulika taifa la Yemen ambalo mustakhbali wake umekumbwa na hali ya sintofahamu hivi karibuni. Mshauri Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Jamal Benomar, ameliambia baraza hilo kwa njia ya video kutoka Qatar kuwa taiafa ya Yemen lipo [...]

22/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Historia itufunze kukabiliana na ubaguzi wa rangi sasa- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. (Picha:UN/Amanda Voisard)

Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ubaguzi wa Rangi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa kila siku, watu wa kila umri hukumbana na chuki, kunyimwa haki na kudhalilishwa kwa misingi ya rangi ya ngozi, asili yao, utaifa au kabila na aina nyingine za ubaguzi. Ban amesema kuwa ubaguzi kama [...]

21/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulizi ya bomu Al-Hasakah, Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon.Picha ya UM/NICA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amelaani mashamabulizi yaliyolenga sherehe ya maadhimisho ya Nowruz katika mji wa Al-Hasakah kaskazini mashariki mwa Syria. Ripoti za awali zimesema kuwa mashambulizi mawili tofauti ya bombu yaliua na kwajeruhi watu wapatao 100, wakiwemo wanawake na watoto.

21/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kutoka CSW59 tunaondoka na mengi: Tanzania

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Loey Felipe

Mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani umekunja jamvi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbili za majadiliano, vikao na tathmini ya maazimio ya Beijingi miaka 20 iliyopita. Halikadhalika washiriki kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliangalia jinsi ya kuimarisha utekelezaji wa maazimio hayo ya mkutano wa [...]

21/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 700 hawapati huduma ya maji safi duniani

Kusikiliza / Mradi wa UNICEF wa maji huko Bubango Tanzania(Picha ya UM/Evan Schneider)

Mwishoni mwa juma Tarehe 22 Machi,ni maadhimisho ya siku ya maji duniani. Siku hii ni fursa ya kumulika umuhimu wa maji kwa ustawi wa jamii. Maadhimisho ya mwaka huu pia yanaangazia matumizi ya vyoo na huduma za kujisafi. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema licha ya kwamba upatikanaji wa mjai ya [...]

20/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ashukuru Italia kwa mchango wake kwenye UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akibadilishana nyaraka za makubaliano na Waziri wa Mambo ya nje wa Italia Mr. Paolo Gentiloni mjini Turin. (Picha: UN/Eskinder Debebe)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa salamu za rambirambi kwa serikali ya Italia na wananchi kufuatia vifo na majeruhi vya raia wa nchi hiyo kwenye shambulio la Alhamisi huko Tunis Tunisia. Ban ametoa rambirambi hizo mjini Turin wakati wa hafla ya utiaji saini makubaliano kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya [...]

20/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wataka Pakistan isitishe adhabu ya kunyongwa kwa Shafqat Hussain

Kusikiliza / Picha:UN/Staton Winter

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza wito wao kwa mamlaka za Pakistan kutupilia mbali  adhabu ya kunyongwa inayomkabili Shafqat Hussain ambaye alikamtwa akiwa na umri wa miaka 14 akihusishwa na kutoweka kwa mvulana mmoja. Mtu huyo alipatikana na  hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kuteka nyara na kuuwa bila kukusudia . Katika taarifa yao [...]

20/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban aongea na Netanyahu baada ya Uchaguzi Israel

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon(kulia) na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu(kushoto). Picha:UN Photo/Evan Schneide

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameongea kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akimpongeza kwa kushinda uchaguzi wa hivi karibuni. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imesema Bwana Ban amemwambia Waziri mkuu huyo kwamba anatarajia kushirikiana na serikali mpya itakapoundwa. Aidha amemsihi Waziri mkuu kuirudishia serikali ya [...]

20/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Morocco yapokea viongozi wa Libya kwa ajili ya mazungumzo ya amani

Kusikiliza / Viongozi washiriki wa mazungumzo ya kisiasa(Picha ya UNSMIL)

Awamu nyingine ya mazungumzo ya kisiasa kati ya wadau wote wa Libya imeanza leo nchini Morocco.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya UNSMIL, ambao unaratibu mazungumzo hayo, umesema katika taarifa yake kwamba washiriki wa mazungumzo watajadili kuhusu uundwaji wa serikali jumuishi, utaratibu wa kurejesha usalama hasa mji mkuu Tripoli na kujisalimisha kwa vikundi vilivyojihami. UNSMIL [...]

20/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sauti ya furaha yasikika kote duniani

Kusikiliza / Picha ya Umoja wa Mataifa/ Albert Gonzalez Farran

Tarehe 20 Machi ikiwa ni siku ya furaha duniani, Umoja wa Mataifa umeandaa kampeni ya kukusanya maoni ya watu kutoka duniani kote ikitaka wakijibu swali , Je sauti ya furaha ni ipi? Na ni wimbo gani unaokupatia  furaha zaidi? Kampeni hiyo iliongozwa na wasanii  mbalimbali wakiwemo Cody Simpson na Pharell Williams. Katika maadhimisho hayo Priscilla [...]

20/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yatarajia kupeleka misaada kwa watu 162,000 Vanuatu

Kusikiliza / Nchini Vanuatu, idadi ya watu wanaohitaji msaada bado haijajulikana kikamilifu. Picha ya UNICEF.

Shirika la mpango Chakula Duniani WFP linasaidia serikali ya Vanuatu katika jitihada zake za kuwapelekea watu 162,000 vyakula vya dharura vikiwemo mchele, maharage na biskuti baada ya kimbunga PAM kupinga nchi hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Geneva, msemaji wa WFP Elisabeth Byrs amesema wataaalam wa WFP waliofika Vanuatu saa 48 tu baada [...]

20/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misitu hudhibiti mabadiliko ya tabianchi: FAO

Kusikiliza / Mtoto anayepanda miti nchini Haiti. Picha ya Umoja wa Mataifa/Logan Abassi.

Misitu ina jukumu la msingi katika kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa angani na hivyo kudhibiti mabadiliko ya tabianchi. Ni ujumbe wa José Graziano da Silva, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo FAO, aliotoa leo katika maadhimisho ya siku ya misitu duniani. Hata hivyo, amesisitiza kwamba misitu huathirika na mabadiliko ya tabianchi. " [...]

20/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulio ya Ijumaa huko Yemen

Kusikiliza / Farhan Haq, Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa. (Picha: video capture)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika siku ya Ijumaa na kusababisha vifo vya watu kadhaaa huku wengine wangi wakijeruhiwa. Mashambulio hiyo yamefanyika wakati wa swala ya Ijumaa kwenye misikiti miwili iliyoko mji mkuu, Sana'a, halikadhalika kwenye jengo la serikali na msikiti mwingine huko Sa'dah. Naibu msemaji wa [...]

20/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mapigano kusini mwa Ufilipino yakimbiza maelfu:UNHCR

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNHCR akikutana na wakaazi wa kisiwa cha Mindanao, Ufilipino. Picha:UNHCR/A.Jain

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema mapigano kusini mwa Ufilipino kati ya majeshi ya serikali na watu wanaotaka kujitenga yamesababisha watu wapatao 120,000 kukimbia makazi yao. UNHCR inasema mapigano hayo ya wiki nane sasa kwenye manispaa 13 za eneo la Maguindanao, yamesababisha watu kusaka hifadhi kwenye majengo ya umma pamoja na [...]

20/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mauaji kwa msingi wa ubaguzi wa rangi yakumbukwa na Baraza Kuu

Kusikiliza / Ukuta ulikuwa unatenga raia wenye asili ya kiafrika na ya Ulaya nchini Afrika ya Kusini, miaka ya 70. Picha ya mkataba wa Umoja wa Mataifa/Pendl

Mjini New York, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo kujadili kuhusu ubaguzi wa rangi, kesho tarehe 21 Machi ikiwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi. Taarifa zaidi na Grace Kaneyia. (Taarifa ya Grace) Katika hotuba yake kwa niaba ya rais wa Baraza la Usalama, Sam Kutesa, Makamu Rais wa baraza [...]

20/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua yatakiwa kudhibiti unywaji pombe holela: Maembe

Kusikiliza / Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania Anna Maembe (Picha ya UM/Radio kiswahili)

Suala la unywaji pombe nyakati za kazi ni miongoni mwa mambo  yaliyoibuliwa wakati wa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, jijini New York, Marekani na kuelezwa kusababisha kuporomoka siyo tu utendaji kazi bali kuathiri maendeleo . Idhaa hii ilizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania Anna [...]

20/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Utoaji chanjo uimarishwe kwenye nchi zilizodhibiti Ebola:WHO

Kusikiliza / Chanjo ya surua. ONU/Marie Frechon

Shirika la afya duniani, WHO limetaka kuimarishwa kwa harakati za utoaji wa chanjo dhidi ya magonjwa kama vile surua, donda koo na mengineyo yanayoweza kuzuilika kwa chanjo kwenye nchi ambazo tayari zimedhibiti mlipuko wa Ebola. Mkurugenzi wa chanjo WHO Dkt. Jean-Marie Okwo-Bele amesema hatua hiyo ni muhimu kutokana na kuripotiwa kwa visa vya surua kwenye [...]

20/03/2015 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uwepo wa wanawake bungeni ni muhimu katika kuendeleza maswala yao:KEWOPA

Kusikiliza / Wanachama wa KEWOPA wakati wa mjadala New York(Picha ya UM/radio kiswahili)

Tumeweza kupitisha sheria mbali mbali nchini Kenya  zinazoangazia maswala ya wanawake nchini Kenya. Hiyo ni kauli ya Cecily Mbarire, mwenyekiti wa Muungano wa wanawake wa bunge nchini Kenya, KEWOPA ambayo ametoa kwenye mkutano ulioandaliwa na chama hicho kando mwa mkutano wa 59 wa kamisheni ya  hali ya wanawake duniani, CSW59 unaofikia ukomo leo. Amesema sheria [...]

20/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Utumikishaji watoto jeshini Sudan Kusini waendelea:UNICEF

Kusikiliza / Watoto waliokuwa wakitumikishwa jeshini huko Gumuruk, jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini.(Picha ya UNICEF/Mariantonietta)

Mustakhbali wa watoto nchini Sudan Kusini umesalia mashakani hasa kwenye majimbo ya Upper Nile na Unity kutokana na watoto kuendelea kutumikishwa vitani. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) UNICEF inasema watendaji wake pamoja na wadau walioko eneo hilo wameripoti [...]

20/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma ya maji yasalia anasa kwa baadhi ya wakazi duniani

Kusikiliza / Harakati za kuwasilisha maji safi nchini Haiti.UN Photo/Logan Abassi

Wakati suala la kupata maji safi na salama limeripotiwa kuwa moja ya mafanikio ya malengo ya maendeleo ya milenia, bado watu Milioni 748 duniani kote wanakumbwa na mkwamo kwenye kupata huduma hiyo adhimu. Hiyo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF katika taarifa yake iliyotolewa Ijumaa kuelekea siku ya [...]

20/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Juhudi zaidi zahitajika katika usafi wa mazingira

Mazingira ya mijini ni kero kwa wakazi iwapo usafi wake hautazingitiwa. Picha hii ilipigwa Hanoi, Vietnam. (Picha: UN/Kibae Park)

Msimu wa mvua ukiwa umeshika kasi sehemu mbalimbali Tanzania, mazingira yako katika hatari kubwa ya kuharibika ikiwa hatua za makusudi hazitachukuliwa kukabiliana na uchafu katika sehemu mbalimbali. Jackson Sekiete wa redio washirika Morning Star ya jijini Dar es salaama amemulika hali ya usafi katika jiji hilo na kukutumia makala ifuatayo.

19/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ilibidi kufanya maamuzi magumu kutokomeza Ebola : Rais Sirleaf

Kusikiliza / Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf. Picha:UN Photo/Mark Garten

Rais wa Liberia Ellen Johson Sirleaf amesema nchi yake ililazimika kufanya maamuzi magumu kwa kusema yatosha hatua iliyofanikisha kutokomeza homa kali ya Ebola iliyoikumba nchi hiyo ya Afrika Magharibi mwaka jana. Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York, Rais Sirleaf amesema hali likuwa ya kutisha hasa kwa kuzingatia kuwa watu [...]

19/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Machafuko Nigeria yamesababisha tatizo kubwa la kibinadamu- OCHA

Kusikiliza / John Ging wa OCHA akiongea na wanahabari mjini New York. Picha ya UM. (MKATABA)

Mzozo kaskazini mashariki mwa Nigeria umekuwa na athari kubwa, zikiwemo kuchangia idadi kubwa ya kukimbia makwao, ukiukwaji mkubwa wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu, sheria ya haki za binadamu na kuongezeka kwa tatizo la kibinadamu. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni za Kibinadamu katika Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, John Ging, ambaye amehitimisha [...]

19/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ISIL huenda wametenda uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari- ripoti

Kusikiliza / Picha: UNHCR/B.Szandelszky

Kundi linalotaka kuweka dola la uislamu wenye msimamo mkali, yaani ISIL, huenda limetenda aina tatu za uhalifu mkubwa zaidi wa kimataifa, mathalani uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya kimbari. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ambayo imetolewa leo Alhamis na Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo [...]

19/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuko tayari kwa majadiliano na Umoja wa Mataifa: DRC

Kusikiliza / Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Raymond Tshibanda akihutubia Baraza la Usalama. (Picha:UN/Loey Felipe)

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, imesema imejizatiti kuhakikisha uchaguzi ujao unakuwa wa kidemokrasia. Hakikisho hilo limetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa DRC Raymond Tshibanda alipohutubia baraza la usalama siku ya alhamisi wakati wa kikao kuhusu hali inayoendelea nchini humo. (Sauti ya Tshibanda) "Na ndio maana baada ya mjadala wa wazi [...]

19/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hakuna demokrasia Maldives bila haki: Mtaalamu

Kusikiliza / Gabriela Knaul.(Picha: UN /Jean-Marc Ferré)

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na wanasheria Gabriela Knaul ameonya kuhusu kudorora kwa kasi kubwa kwa uhuru wa mfumo wa haki nchini Maldives tangu afanye ziara nchini humo mwaka 2013. Bi. Knaul amesema hayo wakati huu ambapo Rais wa zamani wa visiwa hivyo Mohammed Nasheed akiwa amehukumiwa kifungo cha miaka [...]

19/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM waitaka Pakistan isitishe adhabu ya kifo

Kusikiliza / Picha:UN/Staton Winter

Umoja wa Mataifa umeeleza kusikitishwa na kuongezeka kwa visa na kasi ya kutekelezwa kwa adhabu ya kifo nchini Pakistan tangu mwezi Disemba 2014. Jingine la lililousikitisha umoja huo ni tangazo la serikali ya Pakistan hivi karibuni kuwa itaanza tena kutekeleza adhabu ya kifo kwa kesi zote, na wala si tu kwa kesi zinazohusiana na ugaidi. [...]

19/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Je kuna uhusinao kati ya kipato na furaha: mjadala

Kusikiliza / Hafla ya siku ya 2013 (Picha ya UM/Devra Berkowitz/maktaba)

Tukielekea siku ya furaha duniani ambayo itaadhimishwa kesho ijumaa tarehe 20 Machi, Idara ya mawasiliano ya Umoja wa Mataifa leo imeongoza mjadala maalum kuhusu uhusiano kati ya furaha na kipato. Mjadala huo umekuwa ukiendelea katika jamii ya wanasayansi tangu mwaka 1974 ambapo utafiti mmoja ulionyesha kwamba nchi zinazoendelea zikizidi kuwa tajiri, kiwango cha furaha ya [...]

19/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yazindua mpango mpya wa vocha za vyakula CAR

Kusikiliza / WFP ikigawa msaada wa chakula CAR. Picha: WFP

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) limeanza mpango wake wa kwanza wa vocha za chakula nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ili kusaidia watu zaidi ya 100,000 wanoatahiriwa na machafuko. Mpango huu wa hutoa mwanya kwa wapokeaji kuchagua vyakula vya asili. Mustapha Darboe ni mwakilishi wa WFP nchini CAR. (Sauti ya Darboe) Kwa mujibu [...]

19/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa CSW59 umenifunza mengi: Bi Rukia

Kusikiliza / Bi. Rukia Mohamad(Picha ya UM/kiswahili)

Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hali ya wanawake unaelekea ukomo wake hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, baada ya kuwaleta pamoja watu mbali mbali kwa ajili ya kujadili maswala ya wanawake. Mmoja wa watu waliohudhuria ni Rukia Mohamad ambaye ni mke wa gavana wa kata ya wajir, Kaskazini Mahariki mwa Kenya. Yeye [...]

19/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Hatua za kuondoa MONUSCO DRC zizingatie taratibu maalum: Kobler

Kusikiliza / Martin Kobler, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa(MONUSCO).
Picha: UN Photo/Sylvain Liechti

Wakati baraza la usalama likielekea kuongeza muda wa ujumbe wake huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO kwa mwaka mmoja zaidi, imeelezwa kuwa mpango wowote wa kuhitimisha shughuli  za ujumbe huo ni lazima uzingatie taratibu maalum ili kuhakikisha nchi inabakia salama kwa mustakbali wa taifa zima. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya [...]

19/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza lalaani shambulio la kigaidi Tunisia

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Paulo Filgueiras

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamelaani vikali shambulio la kigaidi yaliyofanywa kwenye makumbusho ya kimataifa mjini Tunis, Tunisia siku ya Jumatano na kusababisha vifo vya watu wapatao 20. Katika taarifa yao wajumbe hao wametuma rambirambi zao kwa familia za wahanga na serikali ya Tunisia huku wakisisitiza umuhimu wa watuhumiwa wa shambulio [...]

19/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Grail International na harakati za kuwezesha maazimio ya Beijing

Kusikiliza / Hyasinta Mgona (kushoto) na Irene Mwansasu (Kulia) walipohojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha:UN/Kiswahili Unit)

Mkutano wa 59 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani ukikaribia kufikia ukingoni kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, sauti za watoto wa kike nazo zimepazwa. Watoto wa kike wanataka fursa zaidi ikiwemo kupatiwa muda wa kusoma ili waweze kuishi ndoto zao za kuwa na maisha bora yenye hadhi na utu. Miongoni mwa wawezeshaji [...]

19/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Viongozi Nigeria watoa hakikisho la uchaguzi huru na haki: Feltiman

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Rick Bajornas

Mkuu wa masuala ya siasa kwenye Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Nigeria ambapo amekuwa na mazungumzo na viongozi mbali mbali wakiwemo wa kisiasa kutoka chama tawala na upinzani. Halikadhalika amekutana na viongozi wa usalama, tume ya uchaguzi, wanadiplomasia na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Afrika [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Majanga ya asili huzorotesha maendeleo: Benki ya dunia

Kusikiliza / Majanga kama haya ya mafuriko Sudan Kusini huwa na madhara kiafya: Picha: UN-Photo-Isaac-Bill

Kuendelea kukuwa kwa majanga ya asili kote duniani kunarudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa mujibu wa benki ya dunia. Kwa mujibu wa benki ya dunia madhara ya majanga ya asili kwa pato la nchi (GDP) ni mara 20 zaidi kwa nchi zinazoendelea ikilinganishwa na zile zenye viwanda. Rachel Kyte, ni mjumbe maalum wa benki ya [...]

18/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lasikitishwa na kuvunjika kwa mazungumzo Sudan Kusini

Kusikiliza / Baraza la usalama/Picha na Leoy Felipe wa UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesikiliza leo tathmini ya kusambaratika kwa mazungumzo ya amani baina ya pande zinazozozana Sudan Kusini, ambayo imewasilishwa na Haile Menkerios, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Sudan na Sudan Kusini, na pia kuhusu Muungano wa Afrika, AU. Kufuatia kuwasilishwa kwa tathmini hiyo, wanachama wa Baraza la Usalama wameelezea [...]

18/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Gordon Brown aomba shule ziwe sehemu salama

Kusikiliza / Shuleni Nigeria. Picha ya UN.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Elimu, Gordon Brown ametoa wito leo kwa mabadiliko ya msingi ili kuimarisha dhamira ya kimataifa ya kutetea haki za wanafunzi wa kike na wa kiume, akisema ni lazima mwaka 2015 uwe mwaka wa kusitisha ukiukaji wa haki za watoto. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Brown [...]

18/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua iliyofikiwa Haiti inafungua njia kufanyika uchaguzi: Honoré

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Haiti Sandra Honoré. (Picha: UN/Loey Felipe)

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, Sandra Honoré amekaribisha hatua ya pande za kisiasa nchini humo za kuzingatia misingi ya mashauriano na kulegeza misimamo, mambo ambayo amesema yatafungua njia ya kufanyika kwa chaguzi zilizocheleweshwa kwa kipindi kirefu sasa. Bi. Honoré ambaye ni Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini [...]

18/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tathmini ya uharibifu wa kimbunga Pam yaonyesha mahitaji zaidi

Kusikiliza / Picha: UNICEF

Tathmini ya pamoja inayoongozwa na serikali ya Vanuatu ikishirikiana na mashirika ya kibinadamu, imefikia maeneo mapya, hususan yale yaliyoathiriwa zaidi na kimbunga Pam, yakiwemo Malampa, Penama, Shefa na Tafea. Inakadiriwa kuwa nyumba zipatazo 30,000 ziliharibiwa na kimbunga hicho katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi. Tathmini hiyo imeonyesha kuwa chakula, maji, vifaa tiba, makazi na vifaa vya kujisafi [...]

18/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujumuishaji wa walemavu hujenga uthabiti dhidi ya majanga

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Albert González Farran

Ujumuishaji ndiyo njia bora zaidi ya kujenga uthabiti. Huo ndio ujumbe walioupeleka watu wenye ulemavu kwenye kongamani la tatu la kimataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga, ambalo limehitimishwa mjini Sendai, Japan. Kongamano hilo limeelezwa kuwa hatua zimepigwa kwa kiasi kikubwa, lakini juhudi zaidi zinahitajika kuhusu ujumuishaji na kuweka mifumo inayowawezesha watu wenye ulemavu kupata chochote, [...]

18/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Demokrasia Myanmar, kuna dalili za kurudi nyuma: mtaalam wa UM

Kusikiliza / Mtoto mwenye kabila ya Rohingya, katika kambi ya wakimbizi, magharibi mwa wilaya ya Rakhine, Myanmar. Picha ya David Swanson/IRN

Mtalaam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Myanmar Yanghee Lee, ameziomba mamlaka za Myanmar kukubaliana na maswala yanayotatiza utaratibu wa demokrasia nchini humo. Akitoa leo ripoti yake ya kwanza kuhusu Myanmar mbele ya Baraza la Haki za Binadamu, Bi Lee amesema kwamba vitendo kadhaa vya serikali vinaweza kuharibu mafanikio yaliyopatikana hadi [...]

18/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uhuru wa imani au kuabudu kuangaziwa Lebanon

Kusikiliza / Heiner Bielefeldt, Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini. Picha@UN Photo/Paulo Filgueras

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kuabudu Heiner Bielefeldt kuanzia tarehe 23 mwezi huu atakuwa na ziara ya takribani wiki mbili nchini Lebanon. Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema lengo la ziara hiyo ni kutathmini hali ya uhuru wa kuabudu na imani nyinginezo nchini  humo. Bwana [...]

18/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Manusura wa Ebola Sierra Leone wapata pigo upya hata baada ya kupona..

Kusikiliza / Sherri Bangura, manusura wa Ebola huko Sierra Leone. (Picha:WHO Video capture)

Jamii ya kimataifa kila uchao inahaha siyo tu kusaidia matibabu kwa wagonjwa wa Ebola kwenye nchi zilizokubwa na ugonjwa huo Afrika Magharibi bali pia usaidizi kwa manusura. Hii ni kwa kuzingatia kuwa watu waliopona ugonjwa huo wanaporejea makwao wanakumbana na madhila makubwa ikiwemo kukataliwa na jamii zao. Hilo lilinakuwa ni pigo mara mbili kama ilivyo [...]

18/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kongamano la Sendai laafikia mfumo wa kupunguza hatari za majanga

Kusikiliza / Kongamano la Kimataifa Sendai, Japan. Picha:UN Photo/Eskinder Debebe

Kongamano la kimataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga limehitimishwa leo mjini Sendai, Japan kwa kuafikia mfumo wa udhibiti wa majanga, wa mwaka 2015 hadi 2030. Mfumo huo unafuatia ule wa Hyogo wa kuchukua hatua, ulioafikiwa miaka kumi iliyopita, na ambao uliweka kwa kifupi mambo ya kipaumbele katika kujenga uwezo wa taasisi, serikali na mashirika kupunguza [...]

18/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Nigeria yapiga hatua kuheshimu haki za makundi ya walio wachache: UM

Kusikiliza / Rita Izsak. (Picha:UN/Maktaba)

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu makundi ya walio wachache Bi Rita Izsak amesema kimsingi hakuna unyanyasaji wa makundi hayo nchini Nigeria. Akilihutubia baraza la haki za binadamu mjini Geneva, mtaalmu huyo maalum amesema nchi hiyo imechukua hatua za kuhakikisha kila kundi katika kila ukanda nchini humo linajumuishwa ili kuepuka kupuuzwa kwa makundi madogo [...]

18/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Matumizi ya tumbaku yanapungua, lakini vita bado- WHO

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Martine Perret

Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani WHO, zinaonyesha kupungua kwa matumizi ya tumbaku na kuongezeka idadi ya watu wasiovuta sigara. Joshua Mmali na ripoti kamili. (Taarifa ya Joshua) WHO imesema licha ya mwelekeo huo, serikali zinapaswa kuongeza juhudi za kupambana na sekta ya tumbaku na kupunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya bidhaa za [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini CAR, wasiwasi Burundi: Baraza

Kusikiliza / Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa François Delattre katika ziara ya Baraza la Usalama nchini CAR. UN Photo/Dany Balepe

Wanachama wa Baraza la Usalama leo wamejadili ziara yao waliyofanya barani Afrika, kuanzia tarehe 9 hadi 13 Machi katika nchi za Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Ethiopia na Burundi. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina Hassan) Kuhusu CAR, rais wa Baraza la Usalama na Mwakilishi wa Kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walinda amani wawili wafariki dunia katika ajali ya helikopta Mali

Kusikiliza / Walinda amani wa MINUSMA kwenye maeneo ya GAO, kaskazini mwa nchi. Picha ya MINUSMA

Nchini Mali walinda amani wawili kutoka Uholanzi wamefariki dunia siku ya jumanne katika ajali ya helikopta. Ajali hiyo imetokea kwenye maeneo ya Gao, kaskazini mwa Mali wakati helikopta ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSMA ilipolazimika kutua kwa haraka. Taarifa ya MINUSMA inasema kwamba madaktari waliofika eneo eneo la tukio walishindwa kuwaokoa walinda [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vikundi vya ugaidi na uhamiaji haramu vyamtia hofu Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon (kushoto) akizungumza na waziri mkuu wa Italia Matteo Renzi mjini Roma. (Picha:UN/Eskinder Debebe)

Akiwa ziarani nchini Italia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki- Moon ameelezea kusikitishwa kwake na kuongezeka kwa kundi la kigaidi  linalotaka uwepo wa  dola la kiisilamu ISIL au Daesh nchini Libya. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Roma, Ban ameitaka nchi hiyo kusaidia katika juhudi za kutafuta suluhu Libya. Kadhalika Katibu Mkuu akamulika [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mapigano yanatishia mustakhbali wa ukanda wa Sahel:UM

Kusikiliza / Robert Piper akizungumza na wakulima maeneo ya Timbuktu @OCHAROWCA

Mzozo unaoendelea kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika unatishia harakati za kukwamua maisha ya maelfu ya watu ambao hali zao tayari ziko taabani kwenye eneo hilo. Hayo ni kwa mujibu wa Robert Piper mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa ukanda wa Sahel alipohojiwa na Radio ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wazazi wahimizwa kutokwamisha uwezo wa mtoto wa kike

Kusikiliza / Irene Mwansasu wakati wa mahojiano(Picha ya UM/radio)

  Wazazi wametakiwa watoe fursa sawa kwa watoto wao wa kiume na wa kike, ili wote waweze kukuza uwezo na vipaji vyao. Ni kauli ambayo imetolewa na Irene Mwansasu, msichana mwenye umri wa miaka 17, kutoka Tanzania, akiwa mmoja wa washiriki wa mkutano unaoendelea hapa New York wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake. Katika mahojiano [...]

18/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wakaribisha kuondolewa kwa kizuizi cha nyumba viongozi Yemen

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen Jamal Benomar. Picha: UN Photo/Eskender Debebe

Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen Jamal Benomar, amekaribisha kuondolewa kwa kizuizi cha nyumbani kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na Mawaziri wengine na kusema kuwa hiyo ni dalili njema katika majadiliano ya kisiasa yanayoendelea. Katika taarifa yake Bwana Jamal amesema itasaidia katika kurejesha usalama na haki ya kisiasa nchini Yemen hususani pale [...]

17/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Lazima kuwe na fedha za kuwezesha wanawake: Halima Mdee

Kusikiliza / Joseph Msami katika mahojiano na Halima Mdee/Picha na ubalozi wa Tanzania

Uwekezaji kifedha, uwajibikaji mujarabu wa wanawake ni moja ya mambo ambayo yakitekelezwa kikamilifu wanawake na wasichana wanaweza kupiga hatua katika nyanja mbalimbali. Katika mahojiano maalum na Joseph Msami mjini New York, mwakilishi wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Halima Mdee katika mkutano wa 59 wa Kamisheni ya hali ya wanawake anasema uwezeshaji kwa [...]

17/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon aiomba DRC kushirikiana na MONUSCO

Kusikiliza / Picha ya MONUSCO

Katika ripoti yake iliyotolewa jumatatu kuhusu operesheni za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameishauri serikali ya DRC kushirikiana na MONUSCO ili kupata ufanisi katika operesheni zake dhidi ya waasi wa FDLR. Amesema kwamba ukosefu wa mafanikio katika vita dhidi ya FDLR unaweza kudhoofisha [...]

17/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mapigano mapya Sudan Kusini yalaaniwa na UNMISS

Kusikiliza / Zaidi ya raia 100,000 wametafuta hifadhi katika kambi za UNMISS Sudan Kusini. Hapa ni Juba. Picha ya UN/Isaac Billy

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, umelaani mapigano yaliyoibuka leo karibu ya kambi ya Umoja wa Mataifa ambapo bado wakimbizi wa ndani 53,000 wametafuta hifadhi, ukisema ni mapigano makubwa zaidi tangu kuvunjwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano mwanzo wa mwezi huu. UNMISS imesema mashambulio hayo yanaathiri usalama wa raia walio ndani ya kambi [...]

17/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya Katibu Mkuu haionyeshi hali halisi Darfur- Sudan

Kusikiliza / Balozi Hassan Hamid Hassan akihutubia waandishi wa habari.(Picha ya UM/Loey Felipe)

Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Sudan kwenye Umoja wa Mataifa, Hassan Hamid Hassan, amesema kuwa ripoti za Katibu Mkuu zilizowasilishwa leo kuhusu hali katika jimbo la Darfur hazioani na hali halisi ya mambo kwenye jimbo hilo. Mapema Jumanne, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani, Herve Ladsous, amewasilisha ripoti mbili kwenye Baraza la [...]

17/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ebola : mgonjwa mmoja kati ya watano ni mtoto

Kusikiliza / Takwimu zinazoonyesha idadi ya watoto walioathirika na Ebola. (Picha:UNICEF facebook)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limeonya kwamba ni muhimu kutopunguza jitihada katika kupambana na mlipuko wa Ebola, kwa sababu bado ugonjwa huo haujadhibitiwa. Katika ripoti iliyotolewa leo, UNICEF imeonyesha kwamba asilimia 20 ya visa vya Ebola ni watoto, na kwa ujumla, watoto 16,000 wamepoteza mzazi mmoja au wawili kutokana na Ebola. [...]

17/03/2015 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mtafiti aibuka kidedea Sasakawa mwaka 2015

Kusikiliza / Allan Lavell,ni mshindi wa tuzo ya Sasakawa (Picha ya UM)

  Tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa kuhusu upunguzaji athari za majanga ijulikanayo kama tuzo ya Sasakawa imekwenda kwa mtafiti Allan Lavell, muingereza mwenye makazi  yake nchini Marekani. Jopo la uteuzi likiongozwa na Profesa Murat Balamir limesema ushindi wa Lavell unatokana na mfumo aliopendekeza wa kupunguza athari za majanga unaoelezwa kuwa unafaa nyakati [...]

17/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usalama wa chakula Uganda

Kusikiliza / Kilimo nchini Tanzania.(Picha ya UM/ B Wollf)

Usalama wa chakula duniani hutegemea uwepo wa mazao bora yatokanayo na kilimo. Hata hivyo ili kilimo kiwe bora kinahitaji mbegu bora  ambazop wataalamu wanasema ni vyema zikatokana na eneo husika au mbegu asili.Je ni kwa kiasi gani nchi zinahifadhi mbegu asili? Basi tuelekee Uganda ambako mwandishi wetu John Kibeo amefuatilia harakati kama hizo zinazofanywa nchini [...]

17/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yasaidia usalama wa chakula kwenye nchi zilizoathirika na vita vya Syria.

Kusikiliza / Mgogoro wa Syria umepelekea wengi kukimbia makwao na kusabibisha mgogoro wa chakula(Picha ya FAO)

Shirika la chakula na kilimo FAO linaongeza msaada wake kwa Jordan na nchi nyingine katika ukanda huo zilizoathirika na mgogoro wa kibinadamu  unaoendelea nchini Syria na sasa unaingia mwaka wa tano.Kwa sasa waziri wa kilimo wa Jordan , Akef Alzoubi, na mkurugenzi mkuu wa FAO José Graziano da Silva ameanzisha miradi mitatu  ili kuimarisha usalama [...]

17/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Japan na Uholanzi zajiunga na mradi wa UNISDR wa miji inayostahimili majanga:

Kusikiliza / Picha:UNISDR

Nchi mbili zilizo katika msitari wa mbele kwenye juhudi za kimataifa za kupunguza hatari ya majanga leo zimeungana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari za majanga (UNISDR) katika mradi wa ushirikiano wa kuimarisha uwezo wa miji kustahimili majanga. Wizara ya miundombinu na mazingira ya Uholanzi, jumuiya ya biashara ya Japan inayowakilisha makampuni [...]

17/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali Darfur na UNAMID

Kusikiliza / Herves Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa. Picha: UN Photo/Loey Felipe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali katika jimbo la Darfur, Magharibi mwa Sudan, ambapo limesikiliza ripoti mbili za Katibu Mkuu kuhusu Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Darfur, UNAMID. Amina Hassan na maelezo zaidi.. (Taarifa ya Amina) Ripoti hizo mbili zimewasilishwa na Herves Ladsous, Mkuu [...]

17/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya yatumia mbinu ya upendeleo maalum kuhakikisha usawa kwa wote

Kusikiliza / Waziri Waiguru. Picha ya Idhaa ya kiswahili.

Kenya iko katika njia sahihi kisheria na inatambua umuhimu wa usawa kati ya wanaume na wanawake na inahimiza taifa lizingatie hatua za upendeleo maalum ili kuhakikisha kwamba usawa wa kijinsia unaafikiwa. Hiyo ni kauli ya waziri wa Ugatuzi na mipango nchini Kenya Anne Waiguru katika mahojiano maalum na Idhaa hii. Bi. Waiguru ambaye anahudhuria mkutano [...]

17/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

WFP inapeleka msaada wa kiufundi na chakula Vanuatu:

Kusikiliza / Picha: UNICEF Pacific.

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeombwa kutoa msaada wa kiufundi, kusimamia misaada na mipango ya ugawaji wa chakula kwa watu walioathirika na kimbunga PAM kisiwani Vanuatu. Grace Kaneiya na taarifa kamili (TAARIFA YA GRACE KANEIYA) WFP imesema ina akiba kubwa ya biskuti zenye kutia nguvu na ziko tayari kusafirishwa kwa ndege hadi Vanuatu [...]

17/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaanza kuwahamisha wakimbizi 50,000 kufuatia mafuriko Ethiopia

Kusikiliza / Wakimbizi wa Sudan Kusini wahamishwa na UNHCR baada ya kambi yao kufurikwa nchini Ethiopia. Picha ya UNHCR.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeanza kuwahamisha wiki hii zaidi ya wakimbizi 50,000 wa Sudan Kusini kutoka kwenye maeneo yanayoathirika na mafuriko mchini Ethiopia kabla ya msimu wa mvua kuanza mwezi April. Wakimbizi hao wanahamishwa kutoka kwenye makambi ya Leitchuor na Nip Nip kwenye jimbo la Gambella Magharibi mwa Ethiopia. Mwaka [...]

17/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu leo limezungumza na tume ya uchunguzi kuhusu Syria:

Kusikiliza / Mji wa Homs nchini Syria ulioharibika na makombora. Picha ya OCHA.

Baraza la haki za binadamu mjini Geneva , leo limekuwa na mazungumzo na tume ya uchunguzi kuhusu hali ya Syria. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi bwana Paulo Sérgio Pinheiro, amesema  raia daima wamekuwa wahanga wakubwa wa machafuko nchini Syria, wakilengwa na pande zote, majeshi ya serikali na makundi ya wapinzani yenye [...]

17/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kilimo hubeba mzigo mkubwa wa athari za majanga:Ripoti ya FAO

Kusikiliza / Mafuriko haya katika jimbo la Sindh nchini Pakistan mwaka 2010 yaliharibu karibu hekari Milioni Mbili za mazao. (Picha: FAO)

Wakati mkutano wa kupungua hatari ya majanga ukielekea ukingoni kesho Jumatano , ripoti ya kimataifa ya tathimini ya majanga kwa mwaka 2015 inasema , kwa wastani hasara ya kila mwaka kutokana na majanga inakadiriwa kuwa dola bilioni 314. Shirika la chakula na kilimo FAO linawasilisha ujumbe muhimu kwenye mkutano huo , kwamba matokeo ya awali [...]

17/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wasaidia maridhiano Côte d'Ivoire

Kusikiliza / Vijana wa Angovia wajifunza kuishi pamoja kwa amani. Picha ya UNOCI.

Nchini Côte d'Ivoire, jukumu la Ujumbe wa Umoja wa Mataifa UNOCI ni kurejesha maridhiano na kujenga uwezo wa mamlaka za serikali, baada ya vurugu iliyoibuka kati ya mshindi wa uchaguzi Alassane Ouattara na aliyekuwa rais Laurent Gbagbo, mwaka 2010. Wakati ambapo nchi inaelekea uchaguzi mwingine wa rais, mwezi Oktoba mwaka huu, Ujumbe wa Mataifa unaendelea [...]

16/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wataka muziki uwape watu furaha

Kusikiliza / Picha ya UNICEF.

Je furaha inaweza kuwa na sauti gani ? Ni swali linaloulizwa na Umoja wa Mataifa ukielekea kwenye maadhimisho ya siku ya furaha duniani, tarehe 20 Machi. Kwa maana hiyo Umoja wa Mataifa umezindua kampeni kwenye mitandao ya kijamii inayoitwa #HappySoundsLike yaani “Sauti ya Furaha” ukiiomba jamii ya kimataifa kuchagua wimbo bora unaomfanya mtu kufurahi zaidi. [...]

16/03/2015 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Watu wenye ulemavu wasiachwe nyuma katika katika kupunguza majanga.

Kusikiliza / Seneta Paul Njoroge Ben(Picha ya UM/Radio)

Mwakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Kenya anayedhuria kongamano kuhusu kupunguza majanga mjini sendai Japan Seneta Paul Njoroge Ben , amesema ni lazima watu wenye ulemavu wahusishwe kikamilifu ili wajisalimishe majanga yanapotokea.Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa nchini Japan Bwana Ben anafafanua (SAUTI BEN) Kadhalika amesema serikali ya Kenya imepiga hatua katika kujali [...]

16/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mashambulio ya Jumapili katika makanisa Pakistan

Kusikiliza / Wananchi nchini Pakistan. (Picha:Ofisi ya UM Pakistan)

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulio mawili ya kigaidi yaliyotokea jana Jumapili katika makanisa mjini Lahore Pakistan wakati wa ibada za asubuhi. Ban amesema amesikia kwa masikitiko makubwa kwamba kundi la Taliban nchini humo limetaja kuhusika na mashambulio hayo, huku likitishia kufanya mashambulio Zaidi kama hayo katika siku za usoni. [...]

16/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kutesa ziarani Misri

Kusikiliza / Sam Kutesa, rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Picha ya Umoja wa Mataifa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Sam Kutesa, leo ameondoka New York kuelekea Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, kwenye ziara rasmi ambayo itaanza Machi 17 hadi 19. Akiwa Misri, Rais Kutesa anatarajiwa kukutana na Rais Abdel Fattah Al-Sisi wa Misri, na baadaye Waziri wa Mambo ya Nje, Sameh Shoukry. Mbali na mikutano hiyo, [...]

16/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WMO yaunda mifumo ya tahadhari kwa watu wanoishi kwenye mazingira magumu

Kusikiliza / Mifumo ya tahadhari inayofaa kwa jamii nzima ni muhimu kupunguza hatari za majanga. UNISDR/Amir Jina

Wakati wa majanga, watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, wanawake, watoto au wazee huathirika zaidi kwa sababu hawafikiwi na wito wa tahadhari, au kwa sababu hawajui jinsi ya kujiokoa. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Hali ya hewa duniani, WMO, Michel Jarraud amesema hayo akihojiwa na redio ya Umoja wa Mataifa wakati wa kongamano la tatu la [...]

16/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kimbunga PAM chawalazimisha watu 3,300 kuhama

Kusikiliza / Picha:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu OCHA limehitimisha tathmini ya awali kuhusu hali ya kibinadamu katika visiwa vya Vanuatu baada ya kimbunga PAM kukumba eneo hilo. Kwa mujibu wa OCHA, vifo 24 vimethibitishwa na watu 3,300 wametafuta hifadhi katika vituo 37 vya dharura. Tathmini hiyo iliyofanywa na ndege imeonyesha uharibifu mkubwa [...]

16/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Michezo inasaidia kuonyesha uwezo wa wanawake- UN Women

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Logan Abassi

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN Women, Phumzile Mlambo-Ngcuka, amesema kuwa michezo ina umuhimu mkubwa kwa wanawake na wasichana, kwani mara nyingi inasaidia kudhihirisha uwezo wao. Bi Mlambo-Ngcuka ameyasema hayo wakati wa mkutano ulioandaliwa na shirika la UN Women likishirikiana na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, wakati wa [...]

16/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban ampongeza mfalme Mswati III kwa kukabiliana na umasikini na ukimwi

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban(kulia) na Mfalme Mswati III. Picha: UN Photo/Eskinder Debebe

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana na mfalme Mswati III kandoni mwa mkutano wa kupunguza hatari ya majanga unaonedelea Sendai Japan. Katika mkutano wao Ban amempongeza mfalme na utawala wa Swaziland kwa juhudi kubwa za kushughulikia matatizo ya kutokuwepo usawa wa kipato, kupunguza umasikini na vita dhidi ya HIV/ ukimwi nchini humo. Viongozi hao [...]

16/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kila mtu ajitahidi katika kupunguza hatari za majanga:Ban

Kusikiliza / Kibanda kimezungukwa na maji kutokana na mafuriko makubwa Sudan Kusini, ambako watu wengi wamepoteza makazi yao na mazao kuharibiwa.
Picha: UN Picha / Tim McKulka

Ushiriki wa kila mtu unahitajika ili kupata mafanikio katika maswala ya majanga, amesema Katibu Mkuu Ban Ki-moon, akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa kando mwa kongamano la tatu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga, mjini Sendai, Japan. Kuhusu matokeo ya kongamano la Sendai, Katibu mkuu amesema matumaini yake ni kusikiliza kutoka [...]

16/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake timizeni wajibu wenu: Mdee

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Marco Dormino

Ustawi wa wanawake unategemea zaidi utekelezaji mzuri wa majukumu ya wanawake katika nafasi walizonazo amesema mwakilishi wa bunge la Tanzania Halima Mdee katika vikao vya mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake unaoendelea jijini New York. Katika mahojiano maalum na idhaa hii Bi Mdee aliye moja ya wabunge chipukizi amesema changamoto zianazowakabili wanawake ni [...]

16/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na viongozi wa Japan kando ya mkutano wa kupunguza majanga

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alipokutana na Bwana Natsuo Yamaguchi (Picha ya UM/Eskinder Debebe)

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon leo amekutana na viongozi wa serikali ya Japan kandoni mwa mkutano wa kupunguza majanga unaoendelea mjini Sendai. Miongoni mwa viongozi hao ni Bwana Natsuo Yamaguchi, mbunge na mwakilishi mkuu wa chama cha  Komeito , na pia bwana Nobutaka Machimura, spika wa bunge la Japan.Katika mkutano wao Ban [...]

16/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa kubaki Afghanistan mwaka mmoja mwingine

Kusikiliza / Mkuu wa UNAMA bado ana wasiwasi juu ya hali ya haki za binadamu nchini Afghanistan. Picha ya Umoja wa Mataifa.

Leo Baraza la usalama kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza muda wa mamlaka ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan(UNAMA) kwa mwaka mmoja wa ziada. Akihutubia Baraza hilo kuhusu mwelekeo wa kisiasa nchini humo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNAMA, Nicholas Haysom amesema matumaini ya maridhiano na amani yapo nchini humo. [...]

16/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya mpito kuhusu Eritrea yabaini wazi mwelekeo wa ukiukaji wa haki:

Kusikiliza / Picha:UN Photo/WF

Ripoti ya mpito ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Eritrea imebaini bayana mwelekeo wa ukiukaji wa haki za binadamu. Ripoti hiyo iliyowasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu inafuatia uchunguzi wa miezi minne uliofanywa na tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Eritrea. Wakati tume [...]

16/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua za kimataifa zahitajika kukabiliana na wadudu wa mimea:FAO

Kusikiliza / Miongoni mwa wadudu wanao sababisha madhara mengi katika kilimo.(Picha ya FAO)

Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) linasema kushindwa kufuatilia na usambaaji wa magonjwa na wadudu wanaoathiri mimea kunaweza kusababisha janga kubwa katika kilimo na usalama wa chakula. Grace Kaneiya na taarifa kamili. (Taarifa ya Grace)  Kauli hiyo imetolewa mjini Roma ambako FAO inafanya mkutano wa kila mwaka wa tume ya hatua za usafi na kukabili wadudu CPM. [...]

16/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tumepiga hatua lakini migogoro inatutisha:Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akihutubia chuo kikuu cha Umoja wa Mataifa wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kwa upande wa kushoto ni waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe. Picha ya Umoja wa Mataifa/Eskinder Debebe

Akiwa nchini Japan kuhudhuria kongamano la kupunguza majanga Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea chuo cha Umoja wa Mataifa na kuzungumzia maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo akisema mengi yamefikiwa ikiwamo maendeleo, kupinga ukoloni, na hata kulinda haki za binadamu. Taarifa zaidi na Joshua Mmali.. (TAARIFA YA JOSHUA MMALI) Licha ya hayo Bwana [...]

16/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, UN 70 | Kusoma Zaidi »

WHO yahudumia mahitaji ya afya kwa waathirika wa kimbunga Pam

Kusikiliza / Kimbunga Pam ikipiga kisiwa cha Vanuatu. Picha:UNICEF Pacific / Alice Clements

Shirika la Afya Duniani(WHO) kwenye kanda ya Magharibi mwa Pacific kwa ushirikiano na wizara ya afya ya Vanuatu linaratibu juhudi za misaada ya afya wakiwahusisha wadau wengine ili kufikisha misaada inayohitajika ya afya kwa wanaohitaji kufuatia kimbunga kikubwa Pam kilichoikumba Vanuatu. Kimbunga ilikikumba kisiwa cha Vanuatu Machi 13 na 14 kikiambatana na upepo mkali. Wakati [...]

16/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNISDR azungumzia mkutano wa Sendai- Video

Margareta-W

15/03/2015 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Mifumo bora ya afya yahitajika kupunguza hatari za majanga

Mafuriko yaliyotokea Malawi mapema mwezi Januari mwaka huu yamesababisha mlipuko wa kipindupindu. Picha ya UNDP.

Mlipuko wa Ebola, mzozo wa Syria au majanga yanayotokea katika maeneo ya Asia-Pasifiki ni mifano inayoonyesha kwamba mifumo bora ya afya ni msingi wa mpango mpya wa kupugunza hatari za majanga unaojadiliwa mjini Sendai, Japan, wamesema leo wataalam wa afya. Bruce aylward , ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa shirika la Afya duniani, WHO, amesema ili kuvumilia [...]

15/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa mafunzo kutoka Japan

Ban Ki-moon akitembelea kiwanda cha kusafisha maji machafu cha Minami Gamo. Picha ya UN/Eskinder Debebe.

Katika kongamano la tatu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza hatari za majanga linaloendelea mjini Sendai, Japan, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema hatuwezi kuzuia majanga kwani ni kuamua kwa mungu lakini tunaweza kupunguza hatari zao kwa kujitayarisha vizuri zaidi. Ameongeza kwamba bora kuwekeza pesa katika mifumo ya tahadhari kuliko kugharimu ukarabati baada ya uharibifu. Akizungumza [...]

15/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yajiapanga kukabiliana na madhara ya kimbunga PAM

Kusikiliza / Rais wa Vanuatu Baldwin Lonsdale akiongea katika kongamano la kupunguza majanga mjini Sendai Japan/ Picha na UM

Timu ya misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Pacific kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kibinadamu OCHA inahaha kuepusha athari mbaya za kimbunga huko Vanuatu. Katika siku mbili kimbunga hicho PAM kimeathiri mataifa mengi ya visiwani yaliyoko kusini mwa bahari ya Pacific ambapo OCHA inasema kuwa kimbunga hicho kibaya na kilichoko katika [...]

14/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupunguza maafa ni muhimu kwa ajenda ya maendeleo: Wahlström

Kusikiliza / Margareta Wahlström. Picha na Devra Berkowitz wa UM

Mwakilishi maalum  wa Katibu Mkuu katika kupunguza majanga Margareta Wahlström amesema mkutano wa kupunguza majanga unaoendelea mjini Sendai Japan una lengo la kuandaa mkakati wa pamoja kwa ajili ya kupunguza maafa hatari  baada ya mwaka 2015. Katika mahojiano  na redio ya Umoja wa Mataifa kiongozi huyo amesema mkutano huo pia unakusudia kupitia mkataba uliosainiwa  miaka [...]

14/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni jukumu la kila mtu kupunguza majanga-Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban ki-Moona akiwa na waiziri Abe wa Japan mjini Sendai / picha na Debeb

Kupunguza majanga ni jukumu la kila mtu amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati wa ufunguzi wa kongamano la la tatu la Umoja wa Mataifa kuhusu kupunguza majanga linaloendelea mjini Sendai, Japan. Moja ya matokeo yanayotarajiwa kupitiakongamano hilo ni kupitishwa kwa mkakati mpya utakaookoa maisha ya watu na kupunguza gharama za uharibifu [...]

14/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuthamini wanawake ni desturi Rwanda: Waziri Gasinzigwa

Kusikiliza / Waziri Oda Gasinzigwa pamoja na Waziri wa Jinsia wa Liberia na Mjumbe Maalum wa Muungano wa Afrika Bineta Diop wakizungumza na waandishi wa habari. Picha ya UN/Evan Schneider

Rwanda inaongoza duniani kote kwa idadi ya wanawake wabunge. Tangu uchaguzi wa bunge la mwaka 2013, wanawake ni asilimia 63 ya wabunge. Kwa mujibu wa Waziri wa Masuala ya Jinsia na Familia wa Rwanda, Oda Gasinzigwa, mafanikio hayo yamesababishwa na utashi wa kisiasa pamoja na utamaduni wa Rwanda ambao tangu muda mrefu unathamini mchango wa [...]

13/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Harakati za kumkomboa mwanamke

Kusikiliza / Picha: NICA

Mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW59 unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kukiwa na matukio mbali mbali yanayotathimini nafasi ya mwanamke duniani katika nyanja mbalimbali ikiwamo kiuchumi, kisiasa na kijamii. Mkutano huu hufanyika kila mwaka, lakini wa mwaka huu ni wa muhimu zaidi kwa kuwa unatathmini miaka 20 [...]

13/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Wanawake wasikwamishe harakati zao za kusonga mbele:

Kusikiliza / Wanawke wakijifunza kutengeneza Shea Butter nchini Nigeria. (picha: UNDP)

Wakati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunaendelea vikao vya mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, maeneo mbali mbali duniani harakati za kumkwamua mwanamke nazo zinasonga mbele. Mashirika yasiyo ya kiserikali mathalani yanachagiza harakati hizo ili kuweka bayana vikwazo ni vipi wakati  huu ni miongo miwili tangu mkutano wa kimataifa [...]

13/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Hospitali ziendelee kufanya kazi wakati wa majanga ili kuokoa maisha:WHO

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Michel Szulc-Kryzanowski

Shirika la afya duniani WHO limesema kuziacha hospitali ziendelee kufanya kazi wakati wa majanga ya asili na mlipuko wa magonjwa ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya watu. WHO inasema mkakati huo ambao inauita "mpango salama wa hospitali" tayari umesharidhiwa nan chi 70, na shirika hilo litauwasilisha kwenye mkutano wa tatu wa kimataifa wa kupunguza [...]

13/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lawaomba wanasiasa wa Burundi kuthamini utulivu wa nchi

Kusikiliza / Wanachama wa Baraza la Usalama wakikutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza. Picha ya MENUB/V. Monteiro

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekutana na Rais wa Burundi mawaziri wa mambo ya nje na ya ndani, wawakilishi wa vyama vya kisiasa, jamii, tume ya Uchaguzi na Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Burundi kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari jijini Bujumbura. Katika hotuba yake rais wa [...]

13/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa WFP na UNDP ziarani Myanmar

Kusikiliza / Ertharin Cousin wa WFP (kushoto) na Helen Clark wa UNDP (mwenye kofia, kulia), katika kambi ya wakimbizi, Myanmar. Picha ya UNDP.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula( WFP), Ertharin Cousin, na Mkuu wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP), Helen Clark wamekutana na viongozi wa Myanmar na kutembelea maeneo ya Rakhine ambapo vurugu inaendelea tangu mwaka 2012 na watu kunyanyapaliwa kwa misingi ya kikabila na kidini. Viongozi [...]

13/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM wahofia hali ya waliokamatwa Myanmar

Kusikiliza / Picha ya Umoja wa Mataifa

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasiwasi wake juu ya hali ya zaidi ya wanafunzi na waandamanaji 100 waliokamatwa baada ya kushiriki maandamano nchini Myanmar jumanne ya wiki hii. Msemaji wa ofisi hiyo Ravina Shamdasani amesema ingawa baadhi ya waandamanaji waliachiliwa, bado idadi hiyo wanashikiliwa kwenye gereza la Tharawaddy huku 60 [...]

13/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la usalama ziarani Burundi

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Martine Perret

Wajumbe wa Baraza la usalama wako ziarani nchini Burundi wakitokea Addis Ababa Ethiopia. Mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga ana ripoti kamili kuhusu yaliyojiri kwenye ziara hiyo. (Taarifa ya Kibuga)  

13/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viwango vya ubora wa miji kukabili majanga vyatangazwa:UNISDR

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Yutaka Nagata

Ofisi ya Umoja wa mataifa ya kupunguza hatari ya majanga UNISDR leo imekubali kusaidia kuchagiza viwango vipya vya kimataifa (ISO) katika miji 45 ambayo tayari inatambuliwa kwa nia yao ya kuhakikisha raia wao wanakuwa salama dhidi ya majanga ya asili ikiwemo mafuriko, vimbunga na matetemeko ya ardhi. Viwango vipya vya ISO kwa ajili ya ubora [...]

13/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto nchini Syria wanashuhudia wafungwa wakinyongwa hadharani:UM

Kusikiliza / Picha: UNICEF

Tabia ya watoto na vijana nchini Syria kukutanika pamoja na kuangalia video za watu wakinyongwa ni moja ya mambo ambayo yanatia hofu shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) wakati mgogoro huo ukiendelea na kuingia mwaka wa tano. Hayo yamesemwa na mfanyakazi wa UNICEF Hanaa Singer ambaye mwaka jana mzima amekuwa akiratibu misaada ya [...]

13/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Côte d'Ivoire na Suriname wafuta adhabu ya kifo

Kusikiliza / Picha ya Umoja wa Mataifa.

Ofisi ya Haki za Binadamu leo imekaribisha maamuzi ya bunge la Suriname na Côte d'Ivoire kufuta adhabu ya kifo kwenye sheria za nchi zao, mapema mwezi huu. Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu Ravina Shamdasani akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva amesema, wanatumai sheria hizo zitatiwa saini na kutangazwa rasmi na marais wa [...]

13/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wito mpya kwa Haiti watolewa na OCHA

Kusikiliza / Suluhu endelevu zahitajika kwa Haiti. Picha ya OCHA.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, limetoa wito mpya wa ufadhili kwa ajili ya Haiti, miaka mitano baada ya tetemeko la ardhi lililokumba kisiwa hiki na kusababisha vifo zaidi ya 200,000. Msaidizi wa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo Peter de Clercq amesema ni wito wa aina mpya kwani [...]

13/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nini kifanyike kumaliza vita na mateso Syria?:UM

Kusikiliza / Mji wa Homs nchini Syria ulioharibika na makombora. Picha ya OCHA.

Viongozi wanane wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa wanasema mgogoro wa Syria ambao unaingia mwaka wa tano sasa unaendelea kukatili maisha ya watu na kuleta hasara kubwa, ukiwa ni mgogoro ambao jumuiya ya kimataifa imeshindwa kuusitisha. Taarifa kamili na John Kibego.. (TAARIFA YA JOHN KIBEGO) Viongozi hao ambao ni Mkurugenzi wa Shirika la [...]

13/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dunia imekutana Japan afiki jinsi ya kukabiliana na hatari ya majanga:

Kusikiliza / Mtazamo wa anga wa uharibifu mkubwa iliyosababishwa na Tsunami katika pwani ya Indonesia baina ya miji ya Banda Aceh na Meulaboh. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Wadau mbalimbali kutoka kila penmbe ya dunia wanakutana Japan mwisho wa wiki kwa ajili ya mkutano wa tatu wa kimataifa katika miaka 21 , kuafikiana mtazamo mpya kwa kukabili hatari ya majanga utakaopunguza idadi ya vifo na hasara za kiuchumi. Flora Nducha na taarifa kamili.. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) Tangu mkutano wa mwisho wa aina [...]

13/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunahakikisha watoto wa kike wanajitambua: Bi. Maembe

Kusikiliza / Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Anna Maembe (Picha ya Idhaa ya kiswahili)

Tanzania imesema imechukua hatua ili kuhakikisha watoto wa kike wanaoanza darasa la kwanza wanaendelea na masomo hadi wanapohitimu ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana ya uwiano sawa wa uandikishaji watoto wa kike na wa kiume shuleni. Akihojiwa na Idhaa hii kando mwa vikao vya mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake jijini New York, Katibu [...]

13/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa nchi za Afrika ya Magharibi waonja shubiri ya Ebola:UN

Kusikiliza / Picha: UN NEWS CENTRE

Mataifa ya Afrika ya Magharibi ambayo yana visa kidogo vya Ebola au hayana kabisa tayari yameathirika na zahma ya ebola kwa sababu ya uhusiano wa karibu zilionao na mataifa matatu yaliyokumbwa zaidi na ugonjwa huo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo. Adoulaye Mar Dieye , mkurugenzi wa shirika la [...]

12/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ustawi wa wanawake Tanzania

Kusikiliza / Mwanamke kazini.(Picha ya UN Women)

Wakati mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW59 ukiendelea mjini New York, wanawake sehemu mbalimbali duniani wanahimizwa kujikwamua katika nyanja mbalimbali zikiwamo za kiuchumi. Nchini Tanzania licha ya changamoto kadhaa wanawake wanajitahidi kujikwamua kiuchumi kama anavyoeleza Alex Kipondamali wa redio washirika Uhuru Fm ya jijini Dar- es- salaam nchini Tanzania.

12/03/2015 | Jamii: Makala za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UNSOM alaani shambulio la Baidoa

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia bwana,  Nicholas Kay, amelaani vikali shambulio la leo mjini Baidoa Somalia ambalo limesababisha vifo na majeruhi kwa wafanyakazi wa ulinzi na usalama, pamoja na raia. Bwana Kay amesema amezungumza na Rais Sharif Hassan Sheikh Adan leo na kumpa salamu za rambirambi kufuatia mkasa huo. [...]

12/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wanawake na usalama: viongozi wataka utekelezaji

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Kay Muldoon

Viongozi wa nchi za kiafrika na Muungano wa Afrika wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikishwaji wa wanawake katika masuala ya usalama na amani. Wamesema hayo wakizungumza na waandishi wa habari mjini New York kando mwa Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake, CSW. Mazungumzo hayo yamefuatia mkutano maalum uliofanyika tarehe 10, Machi kuhusu majukumu [...]

12/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Shime dunia ikomeshe machafuko Syria: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashiriki katika kampeni ya ushikamano na watu wa Syria(Picha ya OCHA)

Watu wa Syria wanajihisi kuendelea kutelekezwa na dunia unapoelekea mwaka wa tano wa mgogoro wa nchi hiyo ambao umeigawanya nchi yao. Ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki- Moon. Katika tamko lake la kutaka juhudi za pamoja za kuinusuru nchi hiyo na machafuko, Katibu Mkuu amesema watu wa Syria na majirani [...]

12/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Benki ya dunia yasitisha huduma zake Yemen.

Kusikiliza / Mtoto kwenye moja ya majengo ya mji mkuu wa Yemen, Sana'a. (Picha: Benki ya dunia)

Benki ya dunia imetangaza kusitisha operesheni zake nchini Yemen kutokana na kuzorota kwa usalama nchini humo. Taarifa ya benki hiyo imesema hatua hiyo inazingatia tathmini ya kina iliyofanywa juu ya athari ya mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini humo kwenye miradi wa inayotekelezwa na Benki ya dunia. Sitisho hilo linahusu miradi yote inayofadhiliwa na chombo cha [...]

12/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake wa Rwanda na nafasi katika maridhiano

Kusikiliza / Wanawake nchini Rwanda wamechangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya nchi. Picha ya UNDP Rwanda.

Mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW59  unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kukiwa na matukio mbali mbali ikiwemo nafasi ya wanawake na wasichana wa Afrika kwenye amani, ulinzi na maendeleo ya bara hilo. Miongoni mwa washiriki ni Waziri wa Jinsia na maendeleo ya familia nchini Rwanda, Oda Gasinzigwa [...]

12/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Kobler ataka kuaminiana kurejee kati ya MONUSCO na serikali-DRC

Kusikiliza / Mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler. Picha: Radio OKAPI

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO), umeeleza uko tayari kurejesha ushirikiano baina ya serikali ya DRC na Umoja wa Mataifa katika vita dhidi ya waasi wa FDLR, vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo. Mkuu wa MONUSCO, Martin Kobler amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari mjini Kinshasa, akiongeza kwamba ni [...]

12/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zahma Mediterranean, UNHCR yawasilisha mapendekezo

Kusikiliza / Manusura wa ajali ya mediterenia © UNHCR/F.Fossi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limewasilisha kwa Muungano wa Ulaya, EU, mapendekezo thabiti ya kushughulikia changamoto zitokanazo na maelfu ya wakimbizi na wahamiaji kuweka rehani maisha yao kila mwaka wakisaka maisha bora Ulaya. Mapendekezo hayo yamo kwenye barua iliyoandikwa na Kamishna Mkuu wa UNHCR António Guterres kwa EU ikiwa ni sehemu [...]

12/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali yazorota kwa wakimbizi mzozo wa Syria unapoingia mwaka wa 5

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria(Picha ya UNHCR)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR, limesema kwamba, wakati mzozo wa Syria unapoingia mwaka wa tano, mamilioni ya wakimbizi walioko katika nchi jirani na wale wa ndani wamejikuta katika mazingira yanayozidi kuzorota. Priscilla Lecomte na taarifa kamili. (Taarifa ya Priscilla) UNHCR imeonya kuwa bila usaidizi zaidi kutoka jamii ya kimataifa, mustakhbali wa [...]

12/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hepatitis B yapatiwa mwongozo mpya:WHO

Kusikiliza / Mama mzee akipata matibabu kambini huko Sudan Kusini. UNHCR/B. Sokol

Shirika la Afya Duniani, WHO, leo kwa mara ya kwanza limetoa mwongozo wake wenye mapendekezo sita kuhusu matibabu ya homa ya ini aina ya Hepatitis B. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Homa ya Hepatitis B hutokana na kirusi kinachoambukizwa kupitia kwenye damu na majimaji mengine ya mwili, na ambacho huvamia ini na [...]

12/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tusipowekeza katika watoto tunawadhulumu- wataalam wa UM

Kusikiliza / Watoto hawa wanaoishi kwenye vituo vya hifadhi huko Sudan Kusini. (Picha:UNMISS/Ilya Medvedev)

Kuwapa kipaumbele watoto katika utungaji wa sera na matumizi ya sera ndiyo njia pekee ya kulinda haki zao, wamesema wataalam wa Umoja wa Mataifa, katika mjadala kuhusu haki ya mtoto. Katika mjadala huo unaaofanyika kwenye Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi, rais wa Baraza hilo, Joachim Ruecker amesema kuwa kubadili sera kunahitajika kwa [...]

12/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto milioni 14 wameathiriwa na mzozo Syria na Iraq- UNICEF

Kusikiliza / Watoto wakimbizi kutoka Syria wakijizuia baridi(Picha© UNHCR/B.Sokol)

Watoto wapatao milioni 14 kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati wameathiriwa na mzozo unaoendelea nchini Syria na Iraq, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto, UNICEF. UNICEF imesema, wakati mzozo wa Syria unapoingia mwaka wa tano, hali ya zaidi ya watoto milioni 5.6 nchini humo imesalia kuwa tete zaidi. Idadi hiyo inajumuisha watoto [...]

12/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usaidizi wahitajika mifuko ya kuendeleza wanawake: Balozi Manongi

Kusikiliza / Balozi Tuvako Manongi, mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye UM. (Picha:UN/Maktaba)

Tanzania imesema mifuko ya uwezeshaji wanawake iliyoanzishwa nchini humo ni mojawapo ya mbinu za kukwamua kutoka katika lindi la umaskini wanawake hususan wale walioko pembezoni. Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi amesema hayo alipohojiwa na idhaa hii baada ya kutoa mada kwenye tukio lililokuwa linajadili mbinu za kufungua fursa [...]

12/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Hatma ya wanawake uongozini Afrika yamulikwa New York

Kusikiliza / Wanawake wakihudhuria maadhimisho ya siku ya wanawake, nchini Côte d'Ivoire. Picha ya Umoja wa Mataifa/Ky Chung

Ajenda ya Afrika ya mwaka 2063 imesisitiza umuhimu wa kuwezesha vijana ili kuleta maendeleo kupitia huduma za afya, elimu, teknolojia, na ajira. Hata hivyo, kuwapa wasichana fursa sawa katika mkakati huo bado ni changamoto. Ni mada ambayo imeangaziwa leo kwenye mkutano maalum kuhusu uongozi wa wasichana na wanawake katika ajenda ya Afrika ya 2063, uliofanyika [...]

11/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Elimu bora ni changamoto kwa wakimbizi Uganda

Kusikiliza / wakimbizi UNHCR Uganda

Nchini Uganda, katika wilaya ya Kiryandongo iliyoko katikati mwa nchi, idadi ya wakimbizi wanaoishi kambini imeongezeka sana tangu kuibuka kwa mzozo wa Sudan Kusini, Disemba, mwaka 2013, uliosababisha watu wengi kukimbia mapigano. Kwa ujumla, ni zaidi ya wakimbizi 500,000 waliotafuta hifadhi nchini humo kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR, [...]

11/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wako katika mazingira magumu Zaidi kwa sababu ya mlolongo wa migogoro:Zerrougui

Kusikiliza / Watoto hawa ni miongoni mwa wathirika wa mizozo nchini CAR(Picha ya Catianne Tijerina)

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwa ajili ya watoto na vita vya silaha Bi. Leila Zerrougui amesema mwaka 2014 umekuwa na migogoro mingi na imewaweka watoto katika mazingira magumu zaidi ya athari za vita.Bi. Zerrougui  ameyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti yake ya mwaka  kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva [...]

11/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Tukimwezesha mwanamke wa kijijini tutaiwezesha jamii: Bi. Ruto

Picha@JoyWo

  Wakati mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake ukiendelea mjini New York, mke wa makamu wa rais wa Kenya Bi.Rachel Ruto, ambaye ni miongoni mwa washiriki, amesema kwamba alianzisha shirika lisilo la kiserikali la Joyful women kwa ajili ya kumwezesha mwanamke wa kijijini.Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa hii, Bi. Ruto ambaye ni [...]

11/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

WHO na WFP walenga kutokomeza Ebola

Kusikiliza / Msaada wa chakula kwa maeneo yaliyoathirika na ebola.(Picha ya UM/UNIFEED/video capture)

Shirika la Afya Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP wamezinua leo ubia mpya katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone ili kutokomeza kabisa ugonjwa wa Ebola. Ushirikiano huo utasaidia mashirika hayo mawili kuimarisha usaidizi wao kwa watu walioathirika na ugonjwa wa Ebola, WFP ikiwapatia wataalam wa afya [...]

11/03/2015 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkenya ashika hatamu ICC

Kusikiliza / Jengo la ICC. (Picha@ICC)

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai, ICC, leo wamemchagua Jaji Fernández de Gurmendi kuwa rais wa mahakama hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu, 2015-2018. Jaji Joyce Aluoch kutoka Kenya amechaguliwa kuwa makamu wake wa kwanza, huku Jaji Kuniko Ozaki wa Japan akichaguliwa kuwa makamu wa pili wa rais wa ICC. Taarifa ya [...]

11/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zeid ataka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya washukiwa wa uhalifu Côte d'Ivoire

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra'ad Al-Hussein. (Picha:UN/Jean-Marc Ferré)

Kamishna wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein ameitaka serikali ya Cote d'Ivoire kuhakikisha wahusika wa vitendo vya ukatili dhidi ya binadamu wakati wa mgogoro baada ya uchaguzi mwaka 2011 wanafikishwa katika vyombo vya sheria na haki kutendeka.Kauli ya Kamishna Zeid inakuja siku chache baada ya wafuasi wa aliyekuwa rais [...]

11/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kesi ya Gbagbo na Blé Goudé kusikilizwa pamoja- ICC

Kusikiliza / Charles Blé Goudé(Picha@ICC)

Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya jinai, ICC, leo imempa Mwendesha Mashtaka Mkuu idhini ya kuziunganisha kesi za aliyekuwa rais wa Cote d'Ivoire, Laurent Gbagbo na Charles Blé Goudé, ili kuwezesha kuharakisha kuendeshwa kwa mashtaka dhidi yao. Mahakama hiyo pia imehamisha tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi ya Gbagbo kutoka Julai 5, 2015 na kuirudisha nyuma [...]

11/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa baraza la usalama wakutana na Rais wa mpito wa CAR.

Kusikiliza / Baraza la Usalama likitembelea kabi ya wakimbizi wa ndani nchini CAR. Picha ya MINUSCA.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanaendelea na ziara yao huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR ambapo leo wanakuwa na mazungumzo na viongozi wa mamlaka ya mpito akiwemo Rais Catherine Samba-Panza kwenye mji  mkuu Bangui. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa ziara [...]

11/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Upatu wamwezesha mwanamke wa kijijini:Bi Ruto

Kusikiliza / Bi Rachel Ruto(Picha ya Idhaa ya kiswahili)

Uwezeshaji wa mwanamke kiuchumi ni muhimu kwani unachangia kuimarisha familia na jamii kwa ujumla, amesema mke wa makamu Rais wa Kenya, Rachel Ruto alipohojiwa na Idhaa hii kando mwa vikao vya mkutano wa 59 wa kamisheni ya hali ya wanawake jijini New York.Bi. Ruto ambaye ni mlezi wa shirika lisilo la kiserikali la Joyful Women [...]

11/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

FAO yaja na mkakati wa kuinua maendeelo vijijini

Kusikiliza / Wakulima wakianika mpunga barabarani nchini Vietnam. Picha ya FAO.

Shirika la chakula na kilimo FAO limetoa ripoti mpya inayoonyesha namna mipango mikubwa ya maendeleo inavyoweza kuleta mabadiliko na maendeleo jumuishi na endelevu vijijini. Ripoti hiyo mpya inayoitwa ya uchumi wa kilimo au Agrocorridors inaelezwa na FAO kuwa yaweza kuwa nyenzo mkakati wa mitaji binafsi na uwekezaji mkubwa katika miradi inayonufaisha wakulima wadogo wadogo na [...]

11/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalam wa UM aonya kuhusu teknolojia mpya na unyanyasaji wa watoto

Kusikiliza / Picha ya UN/Jean Pierre Laffont

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uuzaji wa watoto, utumikishaji wa watoto katika biashara ya ngono na picha za ngono, Maud de Boer-Buquicchio, amesema leo kuwa bado uuzaji na unyanyasaji wa watoto umeenea katika maeneo yote duniani. Taarifa kamili na Joshua Mmali (Taarifa ya Joshua) Bi Buquicchio amesema mamilioni ya watoto wanasumbuliwa na kunyanyaswa [...]

11/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mabunge yazingatie usawa wa jinsia: UN-Women/IPU

Kusikiliza / Picha ya UNDP

Haki za mwanamke si jambo la mjadala bali ni suala la kufikia ustawi wa dunia, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge duniani, IPU, Martin Chungong katika kikao kuhusu mabunge na usawa wa kijinsia, kikao ambacho ni sehemu ya mkutano wa 59 wa kamisheni kuhusu hali ya wanawake unaoendelea mjini kwenye makao makuu ya Umoja [...]

11/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Kamisheni ya UM kukutana na raia wa Eritrea ughaibuni Sweden na Ujerumani

Kusikiliza / Wakimbizi wa Eritrea: Picha ya UNCHR

Kamisheni hiyo tayari imezuru nchi 5 nyingine Ulaya na Afrika kuzungumza na zaidi ya wakimbizi na wahamiaji 400 wa Eritrea kuhusu hali ya haki za binadamu Eritrea. Wanakamisheni hiyo wanatarajia kuwa ziara hiyo ya Sweden na Ujerumani itawawezesha kukusanya ushuhuda wa ziada ili kuhakiki taarifa walizokusanya tayari, kwani nchi hizo mbili zina idadi kubwa ya [...]

11/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ushiriki wa wanawake kwenye vyama vya ushirika umeongezeka:Utafiri

Picha ya World Bank/Victor Neagu

Ushiriki wa wanawake kwenye vyama vya ushirika umeongezeka miongo miwili iliyopita na hivyo kuleta mabadiliko katika maisha yao. Hiyo ni kwa mujibu wa utafiti wa pamoja uliofanywa kwa njia ya mtandao na shirika la kazi duniani, ILO na shirikisho la vyama vya ushirika duniani, ICA. Rais wa ICA Dame Pauline Green wa ICA amesema utafiti [...]

11/03/2015 | Jamii: Hapa na pale, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Tsunami ya Japan yakumbukwa katika mkesha wa mkutano wa kupunguza majanga

Kusikiliza / Baada ya kimbunga Haiyan, Ufilipino. Picha ya OCHA/Jose Reyna

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari ya majanga (UNISDR), Margareta Wahlström, leo Jumatano ameshiriki mjini Tokyo katika hafla ya kuwakumbuka wale wote waliopoteza maisha kwenye tetemeko la ardhi na tsunami nchini Japan iliyotokea Machi 11 mwaka 2011. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Amesema wakati dunia ikiwakumbuka wote waliopoteza [...]

11/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania yataka kuwaonyesha ukali wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi

Kusikiliza / 03-05-albinos-tanzania

Utashi wa kisiasa upo ili kukemea ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, albino, amesema Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Pindi Chana, baada ya Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kuziomba serikali za Tanzania, Malawi na Burundi kuchukua hatua za kusitisha mauaji hayo. Akizungumza na idhaa [...]

11/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Utashi wa kisiasa umeleta mabadiliko kwa wanawake:AAWORD

Kusikiliza / Juliette Gathoni-Kimemiyah, Afisa wa Shirika la AAWORD, Kenya. 
Picha: Assumpta Massoi

Utafiti uliofanywa na shirika moja nchini Kenya linalohusika na tafiti za maendeleo, AAWORD umebaini mafanikio makubwa pindi serikali inapojizatiti kuwezesha na kuwapatia fursa wanawake. Afisa kutoka shirika hilo la wanawake, Juliette Gathoni-Kimemiyah ambaye yuko New York kuhudhuria mkutano wa 59 wa kamisheni kuhusu hali ya wanawake ametolea mfano sera ya kuhakikisha asilimia 30 ya zabuni [...]

11/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Ukatili wa kijinsia shuleni wakwamisha mafanikio ya elimu- ripoti

Kusikiliza / Picha ya UNICEF/ Andy Brown

Vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanyika shuleni vina matokeo mabaya katika elimu ya mamilioni ya watoto duniani kote, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na mashirika ya kimataifa mbele ya Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake, CSW. Nora Fyles, Mkurugenzi wa Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa Elimu kwa Wasichana, UNGEI, amesema licha ya mafanikio yaliyopatikana [...]

10/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Siku ya wanawake duniani yaibua matumaini Somalia

Kusikiliza / Wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake nchini Somalia. (Picha ya UM/UNifeed)

Siku ya wanawake duniani imeadhimishwa kote dunaini ambapo imewaleta pamoja wanawake na wadau mbalimbali wa harakati za wanawake. Hata katika nchi mbazo zimeshuhudia migogoro mbalimbali ikiwamo Somalia imeadhimisha siku hii.Ungana na Joseph Msami katika makala ifuatayo.

10/03/2015 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubia ni muhimu kati ya wanawake na sekta ya biashara: Robinson

Kusikiliza / Mary Robinson, Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za maziwa makuu

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Mary Robinson ametaka ushirikiano zaidi kati ya wanawake na sekta binafsi kama njia mojawapo ya kukabiliana na mabadiliko hayo ili ajenda ya maendeleo endelevu iweze kutekelezeka. Bi. Robinson amesema hayo alipohutubia kikao kuhusu kuokoa uhai na kulinda mustakhbali kilichofanyika ikiwa sehemu ya [...]

10/03/2015 | Jamii: Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Rais wa zamani wa Finland kinara mpya wa kupunguza hatari ya majanga:Ban

Kusikiliza / Tarja Halonen (Picha ya UM/JC McIlwaine)

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon atamkaribisha rasmi Rais wa zamani wa Finland Bi Tarja Halonen, kama kinara wa tatu wa kimataifa kwa ajili ya kupunguza hatari ya majanga (DRR), wakati atakaposhiriki naye kifungua kinywa siku ya Jumapili pamoja na wawakilishi wengine kutoka kote duniani wanakutana mjini Sendai Japan kwa ajili ya mkutano [...]

10/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu laanza mashauriano na mtaalam wa uhuru wa kuabudu

Kusikiliza / Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Maifa.(picha ya UM/maktaba)

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo limeanza kufanya mashauriano na Mtaalam Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kuabudu au kuwa na dini Heiner Bielfeldt, ambaye amemulika suala la ukatili unaotekelezwa kwa jina la dini, akisema kuwa ukatili kama huo unaweza kuchukua sura tofauti tofauti. Amesema katika baadhi ya nchi, [...]

10/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ubia wa kimataifa umeokoa mamilioni ya maisha ya wanawake na watoto- Ban

Kusikiliza / Mama na mwanae(Picha@UNICEF/Ghana 2014 Logan)

Tangu mwaka 2010, uhai wa wanawake na watoto 2.4 umeokolewa katika nchi 49 ambazo zililengwa na mkakati wa Kila Mama, Kila Mtoto, kwa mujibu wa ripoti mpya ambayo imetolewa leo ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. Vuguvugu la Kila Mama, Kila Mtoto lilizinduliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon mnamo mwaka 2010, ili [...]

10/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yasaidia wakulima wadogo wadogo barani Afrika

Kusikiliza / Picha: FAO/Gisselle Paulino

Shirika la Chakula na Kilimo FAO limeridhika na mradi ulioanzishwa miaka mitatu iliyopita barani Afrika, kwa lengo la kuimarisha usalama wa chakula pamoja na kuwezesha wakulima wadogo wadogo. Mradi huo umeiiga mfano wa Brazil ambayo ni nchi iliyofanikiwa katika vita dhidi ya njaa na umaskini, na mradi huo umetekelezwa katika nchi tano ikiwemo Msumbiji, Malawi [...]

10/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usawa wa jinsia bado safari ni ndefu: Rais Sirleaf

Kusikiliza / Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf(kulia) akihojiwa na Joseph Msami wa Redio ya Umoja wa Mataifa(kushoto). Picha: Joseph Msami

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf amesema miaka 20 baada ya mkutano wa Beijing uliotaka uwepo usawa wa kijinsia kote duniani, yako mabadiliko dhahiri husuani barani Afrika. Taarifa kamili na Flora Nducha. (TAARIFA YA FLORA) Katika mahojiano maalum na Joseph Msami wa idhaa hii mjini New York Rais huyo wa kwanza mwanamke kuchaguliwa barani Afrika, [...]

10/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa baraza la usalama la UM wawasili CAR

Kusikiliza / Rais wa Baraza la Usalama François Delattre na Mkuu wa MINUSCA Babacar Gaye. Picha ya MINUSCA.

Ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa unaozuru mataifa matatu ya Afrika, leo umewasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Ujumbe huo ambao pia utakwenda Burundi na Addis Ababa Ethiopia, umewasili mjini Bangui saa kumi za jioni za Afrika ya Kati. Rais wa Baraza la usalama ambaye ni Mwakilishi wa Kudumu wa [...]

10/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maisha yazidi kuwa mafupi huku uchumi ukisambaratika Syria – ripoti

Kusikiliza / Syrian-refugees

Ripoti mpya kuhusu athari za mzozo nchini Syria imeonyesha ukubwa wa kuvurugwa maendeleo ya kibinadamu na kiuchumi kutokana na vita nchini humo, ambavyo vimedumu sasa miaka minne. Taarifa kamili na Joshua Mmali. (Taarifa ya Joshua) Ripoti hiyo inaonyesha kuwa baada ya miaka minne ya vita vya silaha, kuvurugwa kwa uchumi na ustawi wa kijamii, hali [...]

10/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kizuizini kunahusishwa na vitendo vya usumbufu, watoto ni lazima walindwe:Mtaalam

Kusikiliza / Picha:UN Photo/Nektarios Markogianni

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya utesaji , Juan E. Mendez leo amezitaka serikali kupitisha sheria mbadala za zile za kuwaweka watoto kizuizini ambazo zitazingatia maslahi ya watoto na wajibu wa serikali wa kuwalinda watoto hao dhidi ya utesaji na usumbufu mwingine. Amesema uwekaji watoto kizuizini kunahusiana na usumbufu kwa watoto na [...]

10/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania, Malawi na Burundi chukueni hatua za ulinzi wa Albino: UM

Kusikiliza / Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, albino. (Picha:@UNICEF Tanzania/Giacomo Pirozzi)

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein ameelezea wasiwasi wake juu ya ongezeko la mashambulizi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino. Amesema katika kipindi cha miezi sita watu 15 nchini Tanzania, Malawi na Burundi wametekwa na kujeruhiwa na wengine kuuawa akisema watu watatu kati yao wamekumbwa na visa hivyo wiki [...]

10/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wenye umri wa miaka 10 wanaozwa Niger:FEVVF

Kusikiliza / Mariama Moussa, Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za wahanga wa ukatili kwenye familia nchini Niger.(Picha:UN/G.Kaneiya)

Ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini Niger bado unaendelea kukwamisha maendeleo ya kundi hilo licha ya nchi hiyo kuridhia mikataba mbali mbali ya kimataifa ikiwemo ile ya haki za mtoto. Hayo ni kwa mujibu wa Mariama Moussa, Rais wa shirika lisilo la kiserikali la kutetea wanawake na watoto waliokumbwa na ukatili wa kijinsia nchini [...]

10/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Stephen O'Brien ndiye anamrithi Valerie Amos OCHA

Kusikiliza / Picha: OCHA

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Moon leo ametangaza uteuzi wa Stephen O'Brien wa Uingereza kama msaidizi wa Katibu Mkuu kwa masuala ya kibinadamu katika ofisi ya kuratibu masauala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. O'Brien anachukua nafasi ya Valerie Amos ambaye pia anatoka Uingereza na ambaye Katibu Mkuu anamshukuru sana kwa huduma [...]

09/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tatizo la dawa za kulevya ni tishio linalovuka mipaka- Kutesa

Kusikiliza / Rais wa Baraza Kuu Sam Kutesa(Picha ya UM/Kim Haughton)

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Sam Kutesa, ameitaka jamii ya kimataifa kujadili kwa njia ya uwazi jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazoletwa na matumizi, uzalishaji na usafirishaji haramu ya dawa za kulevya, huku ikizingatia mitazamo ya wadau tofauti. Bwana Kutesa amesema hayo wakati akihutubia kikao cha 58 cha Kamisheni kuhusu Dawa za [...]

09/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban atoa heko kwa mradi wa Solar Impulse

Kusikiliza / watu wa asili nchini Mongolia wakitumia mabamba ya nishati ya jua katika ger, hema lao la kiasili @UN Photo/Eskinder Debebe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameupongeza mradi wa Solar Impulse na kuutakia kila la kheri katika jaribio la kihistoria la kufanya safari ya kuizunguka dunia kwa ndege isiyotumia hata tone moja la mafuta. Ndege hiyo iitwayo Solar Impulse 2 inatumia nishati ya jua, na tayari imeshahitimisha mkondo wa kwanza wa safari yake, [...]

09/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu, Taathira za Mabadiliko ya Hali ya Hewa | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano kati ya UM na EU wamulikwa barazani:

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akihutubia Baraza la Usalama. Picha:UN/Evan Schneider)

Ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda ni moja ya ajenda ya kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika kwenye makao makuu mjini New York ambapo taasisi iliyoangaziwa ni Muungano wa Ulaya, EU. Akihutubia kikao hicho, Katibu Mkuu Ban Ki-moon amesema ushirikiano kati ya vyombo  hivyo viwili hususan ulinzi [...]

09/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Maelfu wafurushwa mjini Mogadishu:

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric, (Picha:UN/Jean-Marc Ferré)

Wadau wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamenukuu mashirika ya misaada nchini Somalia yakisema kuwa maelfu ya watu wamefurushwa kutoka makazi ya muda kwenye mji mkuu Mogadishu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kitendo hicho kimefanyika wiki ya kwanza ya mwezi huu wa Machi ambapo hata notisi ya kuondoka makazi hayo ya muda [...]

09/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake watengewa fedha kuwezeshwa kiuchumi Tanzania

Kusikiliza / Picha hii ni ya wanawake wakibeba mizigo katika kijiji cha Bubango, Tanzania. Picha: UN Photo/Evan Schneider

Wakati mkutano wa 59 kuhusu hadhi ya wanawake duniani ukiwa umetia nanga mjini New York, kundi hilo linapigiwa upatu wa maendeleo kupitia wadau mbalimbali ambapo nchini Tanzania inaelezwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Korogwe inahakikisha wanawake wanatengewa fedha kwa ajii ya kuwezeshwa kiuchumi. Ungana na Martin Mhina wa redio washirika Voice of Africa ya Tanga [...]

09/03/2015 | Jamii: Makala za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Ukwepaji kodi na rushwa huyeyusha dola Trilioni Moja duniani: Mchunguzi

Kusikiliza / Picha@UM/Stuart Price

Mchunguzi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa, Juan Pablo Boholavsky ameliambia Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva, kuwa zaidi ya dola Trilioni Moja ambazo ni fedha za umma hutoweka kutokana na ukwepaji kodi, rushwa na uhalifu na hivyo kukwamisha ufikishaji wa huduma za msingi kwa wananchi. Bwana Boholavsky [...]

09/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uharibifu wa urithi wa utamaduni ni uhalifu wa vita:Ban

Kusikiliza / Mji wa kale wa Hatra(Picha@UNESCO)

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekasirishwa na uharibifu wa maeneo ya urithi na utamaduni wa asili nchini Iraq unaofanywa na kundi la ISIL, kukiwa na ripoti za uvamizi na uharibifu wa mji wa kale wa  Hatra, ambao ni eneo la urithi wa UNESCO kaskazini mwa nchi hiyo. Katibu Mkuu ametoa wito wa [...]

09/03/2015 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu awafuata raia wa Eritrea nchini Ubelgiji

Kusikiliza / Bi Sheila B. Keetharuth, Mtaalamu Maalum juu ya hali ya haki za binadamu nchini Eritrea. Picha:UN Photo/Amanda Voisard

Mtaalamu maalum wa haki za binadamu nchini Eritrea Sheila B. Keetharuth, ameanza ziara rasmi ya siku tatu nchini Ubelgiji kuanzia leo kwa lengo la kukusanya taarifa sahihi kuhusu hali ya raia wa Eritrea wanaoishi nchini humo kama wakimbizi au wahamiaji. Taarifa ya Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imemkariri Bi. Keetaruthu akisema [...]

09/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yawaomba wanawake wa DRC washiriki kwa wingi katika uchaguzi ujao

Kusikiliza / Martin Kobler, Mkuu wa MONUSCO.(Picha ya UN/Rick Bajornas)

  Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Martin Kobler, amewaomba wanawake nchini humo wajiandae kushiriki kwa wingi katika uchaguzi ujao. Mkuu huyo wa MONUSCO amesema hayo wakati wa sherehe ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika mjini Kinshasa, ambako amesema pia kuwa wanawake ni matumaini ya amani [...]

09/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59 | Kusoma Zaidi »

Kupinga ubaguzi dhidi ya wanawake ni wajibu wa kila mtu: Pansieri

Kusikiliza / Simamia usawa wa kijinsia (Picha kampeni ya Benki Kuu/Dominic Chavez)

Wakati vikao vya kamati kuhusu hali ya wanawake vikiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kikao cha 28 cha Kamati ya Kutokomeza Ubaguzi dhidi ya Wanawake kinafanyika mjini Geneva, Uswisi. Taarifa kamili na Joshua Mmali. (Taarifa ya Joshua) Akizungumza kwenye kikao hicho, Naibu Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Flavia Pansieri, [...]

09/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mkutano wa CSW59, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Ban alaani vikali shambulio la Kidal nchini Mali

Kusikiliza / Picha:MINUSMA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani vikali shambulio la Jumapili nchini Mali lililokatili maisha ya watoto wawili wa Mali na askari mmoja wa kulinda amani kutoka nchini Chad, huku walinda amani wengine 11 wakijeruhiwa na raia watatu. Shambulio hilo la roketi kwenye kambi ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA) mjini Kidal [...]

09/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kamisheni ya 59 kuhusu wanawake yaanza vikao vyake New York

Kusikiliza / Mkutano wa kimataifa wa wanawake wang'oa nanga mjini New York kwa ajili ya kujadili maswala ya mwanamke kama huyu.Hapa ni Darfur Kaskazini (Picha ya UM/Albert Gonzalez Farran)

Mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake duniani, CSW59 umeanza jijini New York leo ukileta pamoja wanawake na wadau wa masuala ya wanawake kutoka nchi mbali mbali wanachama wa Umoja wa huo. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace)  Wanawake wakifanikiwa, sote nasi tunasonga mbele! Wasichana wakikwamisha, dunia yote inapata machungu! Ndivyo alivyoanza [...]

09/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu Zaidi wajiunga na kampeni ya "Mimi ni"( #I belong) kukomesha hali ya kutokuwa na utaifa:UNHCR

Kusikiliza / Abou ameshika kitambulisho chake cha Senegal baada ya kuteseka kwa muda mrefu maishani(Picha ya UNHCR/ H. Caux)

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema watu mbalimbali mashuhuri na maarufu duniani wamejiunga na kampeni ya " Mimi ni" au I belong yenye lengo la kukomesha hali ya kutokuwa na utaifa. Flora Nducha na taarifa kamili. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA) UNHCR imesema hali ya kutokuwa na utaifa bado ni changamoto kubwa [...]

09/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zama za kila mtu kukusanya takwimu zimekwisha: Profesa Ngalinda

Kusikiliza / Picha inayoonyeshaTakwimu (Picha ya UM/Mark Garten)

Zama za kila mtu kukusanya takwimu zimefikia ukingoni na sasa hatua zinachukuliwa ili takwimu ishike nafasi yake katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Amesema Mkuu wa Chuo cha Takwimu mashariki mwa Afrika, Profesa Innocent Ngalinda alipohojiwa na Idhaa hii jijini New York, kando ya mkutano wa kamisheni ya Takwimu, ambapo amesema kitendo cha kila mtu [...]

09/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 3.78 kutoka Japan kuimarisha usaidizi wa kibinadamu:UNIDO

Kusikiliza / Fumito Miyake(kushoto) waziri wa kudumu wa Japan na Taizo Nishikawa, naibu mkurugenzi wa UNIDO

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO limepokea mchango wa dola Milioni 3.78 kutoka serikali ya Japan kwa ajili ya miradi ya kuimarisha usaidizi wake wa kibinadamu barani Afrika na wakimbizi wa Syria walioko Uturuki. Makubaliano hayo yameridhiwa kati ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa  UNIDO na afisa wa ubalozi wa Japani kwenye [...]

09/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maandamano ya New york yapigia chepuo usawa wa kijinsia

Kusikiliza / Ban march

Wito huo ulikuwa maudhui ya maandamano yaliyofanyika mjini New York ; Marekani, kwa ajili ya kupambana na ukatili wa kijinsia, unyanyapaa na kupigania elimu kwa wote. Zaidi ya watu 1,000 kutoka nchi mbalimbali wametembea jumapili hii katika mitaa ya mji huu wakiomba usawa wa kijinsia utimizwe kote duniani.  Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la masuala ya wanawake [...]

08/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Shambulio jingine Mali: UM walaani

Picha ya MINUSMA

Wanachama wa Bara za la Usalama wamelaani vikali shambulio jingine la kigaidi lililotokea leo nchini Mali, kwenye maeneo ya Kidal dhidi ya kambi ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSMA. Watoto wawili na mlinda amani mmoja kutoka Chad wamefariki dunia kwenye shambulio hilo, na wengine kujeruhiwa. Wanachama wa baraza la Usalama wamepeleka salamu [...]

08/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maelfu ya watu waandamana siku ya wanawake duniani

Kusikiliza / Maandamano yaliyofanyika mjini New York. Picha ya UN Women.

  Maelfu ya watu wameandamana mjini New York, Marekani, leo jumapili ikiwa ni siku ya wanawake duniani kwa ajili ya kupigania usawa wa kijinsia. Shirika la masuala ya wanawake katika Umoja wa Mataifa , UN Women lilitarajia kukusanya zaidi ya watu 8,000 katika maandamano hayo ambayo yataanza mbele ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa [...]

08/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Somalia yapiga hatua ya kuimarisha mamlaka za serikali

Msafara wa Naibu Katibu mkuu kwa ajili ya kuweka amani.(Picha ya UM/Tobin Jones/maktaba)

  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, akiwa ziarani kwenye mji wa Kismayo nchini humo leo, amekaribisha mafinikio ya ofisi ya mpito ya mkoa wa Juba, ambayo imeunda baraza la mkoa. Hata hivyo, Bwana Kay amesisitiza umuhimu wa kufuatilia utaratibu wazi na jumuishi, ambapo wanawake na makundi ya [...]

08/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake bado wanakumbwa na madhila kwenye amani na vita:Ban

Ujumbe wa Katibu Mkuu wa UM siku ya leo.

Leo ni siku ya wanawake duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema madhila yanayokumba wanawake na wasichana na watoto wa kike bado yanatikisa maeneo mbali mbali duniani. Katika ujumbe wake wa siku hii ametolea mfano maeneo ambayo watoto wadogo wa kike wenye umri wa miaka saba wanatumiwa kama silaha ya vita [...]

08/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Ninafarijika kuwasaidia wanawake:Mfanyakazi kutoka Jane Godall

Kusikiliza / Wanawake wakiwezeshwa wanabadili maisha ya watoto wao na jamii nzima. (Picha:Anne Kennedy | UNDP)

Wakati  siku ya wanawake ikiadhimishwa kote duniani leo machi 8, siku hii imetengwa ili kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii. Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinazoadhimisha siku hii ambako Stella Vuzo, Afisa wa kituo cha habari za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania amezungumza na msichana Happyness Steven George mwenye umri wa miaka 21 ambaye [...]

08/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Mahojiano, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalaani shambulio la kigaidi, Mali

Walinda amani wakiwa kwenye doria kwenye moja ya maeneo, nchini Mali. (Picha ya @MINUSMA)

Wanachama wa baraza la Usalama wamelaani vikali shambulio la kidaidi lililotokea leo kwenye mji mkuu Bamako, nchini Mali, ambapo watu 5 wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa. Miongoni mwa majeraha ni wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa. Wanachama wa Baraza la Usalama wamepeleka salamu zao za rambirambi kwa familia za wahanga na serikali za Mali, [...]

07/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yasaidia serikali ya Tanzania kukabiliana na tatizo la uhamiaji haramu

Kusikiliza / Wahamiaji kutoka Ethiopia wakirudi kwao. Picha ya IOM.

Nchini Tanzania, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM, limesaidia wahamiaji 54 wa Ethiopia kurudi makwao, kwa ushirikiano no idara ya uhamiaji ya serikali ya Tanzania. Wakimbizi hao walikuwa wamefungwa na serikali ya Tanzania kwa zaidi ya miezi minne kwa sababu ya kuingia nchini humo kinyume cha sheria na hivyo kukosa nyaraka halali za kusafiri. Miongoni [...]

06/03/2015 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za binadamu yasikitishwa na hukumu ya kifo Indonesia

Kusikiliza / Rupert Colville akiongea mbele ya waandishi wa habari 
@UN/Jean-Marc Ferre

Ofisi ya haki za binadamu imeisihi serikali ya Indonesia kujizuia kuwakatia hukumu ya kifo watu wamepatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Msemaji wa Ofisi hiyo Rupert Colville, amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva akisema wanasikitishwa na taarifa ya kunyongwa kwa washtakiwa sita mwezi Januari. Kwa mujibu wa [...]

06/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na kutokamilishwa kwa mazungumzo kuhusu Sudan Kusini

Kusikiliza / Watoto ndio waathirika wakubwa Sudan Kusini:UNICEF (Picha ya UNICEF/NYHQ2014-042/Holt)

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea masikitiko yake kutokana na kutohitimishwa kwa mafanikio mchakato wa amani wa Sudan Kusini unaoratibiwa na jumuiya ya IGAD. Halikadhalika Ban amesitikishwa na kitendo cha Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini na na makamu wake wa zamani Riek Machar kushindwa kuonyesha uongozi wao na kufikia makubaliano [...]

06/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WFP yasitisha usaidizi kwa wakimbizi 70,000 wa Syria kwa kukosa ufadhili

Kusikiliza / Mkimbizi kutoka Syria akionyesha vocha yake ya kielektroniki ya WFP. Picha ya WFP.

Wakimbizi 70,000 kutoka Syria waliotafuta hifadhi nchini Uturuki wamekosa usaidizi wa chakula kwa sababu Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP limepungukiwa fedha. Mradi ambao ulisitishwa kwenye baadhi ya kambi za wakimbizi zilizoko nchini Uturuki ni vocha za kielektroniki ambazo zinawasaidia wakimbizi kununua vyakula wanavyotaka sokoni. Mwezi Januari WFP ilikuwa inasaidia wakimbizi 220,000 wa Syria, [...]

06/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Harakati za kuwakomboa wanawake dhidi ya madhila ya ubakaji:DRC

Kusikiliza / Mwanamke ambaye alinufaika na huduma za Dr. Mukwega nchini DRC(Picha ya UM/video capture)

Tarehe Nane mwezi machi kila mwaka ni siku ya wanawake duniani. Siku hii imekuwa inaadhimishwa tangu mwaka 1908 na mwaka huu ujumbe ni wezesha mwanamke, wezesha ubinadamu na Pata Picha! Ujumbe huu unalenga kuangalia ni kwa jinsi gani mwanamke aliyewezeshwa kiuchumi, kijamii au kisiasa anaweza kukomboa jamii yake. Mathalani kijamii kuna madhila wanayokumbana nayo ikiwemo [...]

06/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Jukwaa la kimataifa la elimu lichochee elimu ya kustahimiliana: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban(kulia) na Irina Bokova(kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamduni UNESCO. Picha:UN Photo/Eskinder Debebe

Jukwaa la tatu la kimataifa kuhusu elimu litakalofanyika mwezi Mei mwaka huu huko Jamhuri ya Korea litakuwa na mchango mkubwa kwenye ajenda mpya ya maendeleo endelevu inayotarajiwa kupitishwa mwezi Septemba mwaka huu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema hayo kwenye kikao kilichofanyika New York, kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya jukwaa hilo. Amesema [...]

06/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Muziki watumainisha mustakhabali bora baada ya Ebola

Kusikiliza / Picha: Mark Garten

Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, mjini New York, wadau walioshirikiana katika juhudi za kimataifa dhidi ya mlipuko wa Ebola huko Afrika Magharibi wamekutana hivi karibuni katika tumbuizo maalum. Tumbuizo hilo lilileta pamoja wasanii kutoka maeneo mbalimbali hususan Afrika Magharibi, ambao pamoja na kuburudisha na kuelezea hali halisi ya Ebola, walipata fursa ya kusikiliza [...]

06/03/2015 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Somalia na ASWJ yapongezwa

Kusikiliza / Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay(UN Photo/Rick Bajornas)

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amekaribisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya serikali ya Somalia na kikundi cha Ahlu Sunna Wal Jamaa, ASWJ katikati mwa nchi hiyo. Taarifa ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM imesema kama makubaliano hayo yana vipengele vitano ambapo Kay amesema [...]

06/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

DRC bado inahitaji kuwezesha zaidi wanawake kisiasa

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na waziri wa familia wa DRC(Picha ya UM/Mark Garten)

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, idadi ya wanawake wabunge ni chini ya asilimia kumi. Hii ni kwa mujibu wa Aurelie Bitondo, mbunge wa zamani wa DRC ambaye sasa ni katibu wa mtandao wa wanawake wabunge na mawaziri wa kiafrika nchini humo. Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, ameeleza sababu zinazozuia wanawake kushirikishwa [...]

06/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lajadili hali Ukraine

Kusikiliza / Mkuu wa masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman akihutubia Baraza la Usalama(Picha ya UM/Devra Berkowitz)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limekutana leo kujadili hali nchini Ukraine, katika kikao ambacho kimehutubiwa na maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Wa kwanza kuhutubia Baraza hilo amekuwa Jeffrey Feltman, Msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya kisiasa, akisema kwamba hali Mashariki [...]

06/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake wakulima kutokomeza njaa

Kusikiliza / Wanawake wakiwa shambani. (Picha:Tovuti FAO)

Wakati wa kuelekea siku ya wanawake duniani, viongozi wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani(FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Kilimo na Maendeleo( IFAD) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani(WFP) wamekutana mjini Roma, Italia ili kusisitiza jukumu la wanawake wakulima katika kufanikisha usalama na uhakika wa chakula. Taarifa zaidi na Amina Hassan. (Taarifa ya Amina) [...]

06/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Tusikubali uharibifu huu wa ISIL kwenye mali za kale: UNESCO

Kusikiliza / Moja ya malikale katika jumba hilo kwenye mji wa Nimrud ambazo zimeharibiwa na kundi la kigaidi la ISIL. (Picha: UNESCO-tovuti)

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limelaani vikali uharibifu uliofanywa kwenye maeneo ya kumbukumbu ya vitu vya kale huko Nimrud nchini Iraq. Uharibifu huo umefanywa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la ISIL ambapo Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova amesema uharibifu huo unakumbusha jamii ya kimataifa kuwa hakuna kilicho [...]

06/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Walio hatarini kuathirika na mabadiliko ya tabianchi wasaidiwe wajitambue: Robinson

Kusikiliza / Kimbunga Haiyan kilipopiga Ufilipino,madhara yalikuwa dhahiri kwa wakazi wa visiwani humo. (Picha: UN/Maktaba)

Mjini Geneva, Uswisi kumefanyika mkutano unaoangalia jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyokwamisha jamii kufurahia haki za binadamu. Akizungumza kwenye mkutano  huo mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko  ya tabianchi Mary Robinson amesema jambo muhimu ni kuhakikisha kuna mfumo wa kuwawezesha watu walio hatarini kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi pindi majanga ya [...]

06/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tulenge 50-50 ifikapo 2030: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-moon akiwa na rais wa Liberia Ellen Sirleaf wakati wa maadhmisho ya siku ya wanawake kwenye UM(Picha ya UM/wa /Mark Garten)

Umoja wa Mataifa leo umeadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo wito umetolewa kuhakikisha vikwazo vinavyozidi kuwaengua wanawake kwenye harakati za kuendeleza jamii zao vinaondolewa ikiwa ni miaka 20 tangu mkutano wa Beijing kuhusu wanawake. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Tukio hilo lilianza kwa video ya uzinduzi wa mkutano wa nne wa kimataifa [...]

06/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Uzazi wakwamisha usawa wa wanawake makazini: ILO

Kusikiliza / Kazi wanayofanya ni moja na muda ni mmoja lakini malipo ni tofauti. (Picha: ILO)

Shirika la kazi duniani, ILO limesema miongo miwili tangu kufanyika kwa mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake huko Beijing, China, bado mustakhbali wa wanawake hususan sehemu ya kazi uko mashakani. Katika taarifa yake kuhusu pengo la ujira wakati uzazi iliyotolewa kuelekea siku ya wanawake duniani, tarehe Nane Machi, ILO imesema masuala kama ajira na [...]

05/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa Ujumbe wa UM Libya

Kusikiliza / Baraza la usalama(Picha ya UM/Mark Garten)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongeza muda wa mamlaka ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL hadi Machi 31 2015. Nakala ya azimio hilo imesema kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kwa kufuatia kutambua haja ya kuongeza muda wa UNSMIL kwa muda mfupi, na kwa kutambua [...]

05/03/2015 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yaunga mkono ushirikiano na jeshi la DRC dhidi ya FDLR

Kusikiliza / Picha: UN Photo/Sylvain Liechti

Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, MONUSCO, inaunga mkono kazi ya pamoja kati yake, majeshi ya FARDC na wakazi katika operesheni ya kuwasaka wapiganaji wa FDLR. Msemaji wa kijeshi wa ujumbe huo, Kanali Felix Bass, ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kila juma, baina ya mashirika ya umoja wa [...]

05/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwezeshaji wa wanawake Mwanza, Tanzania

Kusikiliza / @FAO/Tanzania

Uwezeshaji wa wanawake ni muhimu katika jamii kwani unatoa fursa kwa maendeleo katika jamii na hatimaye katika nchi. Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinachukua hatua katika kumuwezesha mwanamke ambako Paulina Mpiwa wa radio washirika Sengerema ya Mwanza nchini humo amezungumza na baadhi wa wanawake ili kutupatia hali halisi ya mwelekeo na kwanza anaanza na [...]

05/03/2015 | Jamii: Makala za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Majaribio ya uthabiti wa chanjo dhidi ya Ebola kuanza Guinea

Kusikiliza / Ufuatiliaji na upimaji ili kubaini iwapo mtu ana Ebola au la nchini Guinea. (Picha:WHO/A. Pallangyo)

Shirika la afya duniani WHO pamoja na wadau wake, mwishoni mwa wiki hii wanatarajia kuanza majaribio ya ufanisi wa chanjo dhidi ya Ebola nchini Guinea. Chanjo hiyo aina ya VSV-EBOV imetengenezwa na wakala wa afya ya umma nchini Canada ambapo imeelezwa chanjo nyingine ya pili itaanzishiwa majaribio kadri shehena ya kutosha itakapopatikana. Mkurugenzi Mkuu wa [...]

05/03/2015 | Jamii: Ebola | Kusoma Zaidi »

Congo yatoa wito wa ushirikiano ili kukomesha zahma ya Boko Haram

Kusikiliza / Wakimbizi wakiwa Diffa, Niger, baada ya kukimbia mashabulio ya Boko Haram nchini Nigeria. (Picha:OCHA/Franck Kuwonu)

Kikao cha ngazi ya juu cha haki za binadamu kimeendelea leo mjini Geneva, kwa wito kwa mataifa ya Afrika Magharibi kuungana ili kukomesha tishio la Boko Haram.Wito huo umetolewa na balozi Basile Ikoube wa Congo wakati akilielezea kwamba kundi hilo la wanamgambo wa Nigeria ni janga ambalo linaweza kumalizwa kwa muungano wa nguvu za kijeshi [...]

05/03/2015 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua zinahitajika kwa ajili ya usawa wa kijinsia bungeni licha ya miaka 20 ya maendeleo:IPU

Kusikiliza / Wanawake nchini Somalia wakishirikishwa kwenye utaratibu wa kisiasa na amani. Picha ya Unifeed.

Ingawa idadi ya wanawake Bungeni inakaribia mara mbili katika miaka 20 iliyopita, bado hatua na utashi wa kisiasa unahitajika kote duniani ili kukabili kujikokota kwa mchakato wa kuleta usawa, umesema muungano wa mabunge IPU. Taarifa kamili na Joshua Mmali. (Taarifa ya Joshua) Tangu mwaka 1995 wakati uliporidhiwa mpango wa kuwawezesha wanawake wastani wa wanawake bungeni [...]

05/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Viashiria viende sambamba na malengo endelevu: Tanzania

Kusikiliza / Dkt. Albina Chuwa, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Tanzania. Picha: Assumpta Massoi

Mkutano wa 46 wa kamisheni ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa unaendelea kwenye makao makuu ya Umoja huo ambapo moja ya masuala yanayojadiliwa ni jinsi ya kuweka viashiria vitakavyojumuishwe kwenye malengo ya maendeleo endelevu yanayotarajiwa kupitishwa na wakuu wa nchi mwezi Septemba mwaka huu. Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo, Dkt. Albina Chuwa [...]

05/03/2015 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwezesha wanawake kunaleta mabadiliko ya kijamii

Kusikiliza / Picha ya UN Women.

Kuwawezesha wanawake katika sekta ya uchumi kunasababisha mafanikio ya maendeleo katika jamii. Ni swala ambalo limejadiliwa katika kongamano maalum la siku ya wanawake duniani kuhusu fursa za kuwezesha wanawake na wasichana. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Kongamano hilo lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Ubia pamoja na Chama cha wafanyabiashara [...]

05/03/2015 | Jamii: Habari za wiki, Siku ya Wanawake Duniani 2015 | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031