Watoa huduma za kibinadamu wakumbukwa; Ban aweka shada la maua

Kusikiliza /

Maadhimisho ya siku ya wasaidizi wa kibinadamu @Fiona Blyth

Leo ni siku ya kimataifa ya watoa huduma za kibinadamu duniani ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa na matukio mbali mbali kukumbuka wale waliofariki dunia wakiwa kazini na wale wanaoendelea kutekeleza jukumu hilo bila kujali hatari zinazowakabili. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Saa Tatu na Nusu asubuhi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon aliongoza kumbukizi hii kwa kuweka shada la maua kwenye eneo maalum.. kimya kilitawala na hatimaye akazungumza na ndugu na jamaa za wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakiwa kazini.

Chimbuko la siku ya leo ni tukio la mwaka 2003 huko Baghdad Iraq ambako ofisi za UM zilishambuliwa na wafanyakazi 22 wa kibinadamu waliuawa…

Umoja wa Mataifa unasema idadi ya wanaouawa wakati wanaokoa wengine iliongezeka kwa asilimia 66 mwaka jana ikilinganishwa na mwaka uliotangulia Afghanistan ikitajwa kuwa hatari zaidi.

Valerie Amos Mkuu wa ofisi ya huduma za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa..

Zaidi ya Theluthi moja walikuwa ni wahanga wa mashambulio ya kulengwa au mapigano wakati wanasambaza misaada."

 

Takwimu za Humanitarian Outcomes zinaonyesha mwaka huu pekee hadi Agosti 15 wafanyakazi 79 wameuawa na ongezeko kubwa ni Julai na Agosti maeneo husika zaid yakiwa ni Gaza na Sudan Kusini.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031