Wataalam wa afya wakutana kutathmini maadili ya matibabu ya Ebola

Kusikiliza /

Wafanyakazi wa wizara ya afya Monrovia, Liberia katika kituo cha afya kinachofadhiliwa na WHO,MSF.Picha ya UNMIL/Staton Winter

Jopo la wataalam wa maadili ya utabibu wamekutana mjini Geneva kutathmini mchango wa matibabu ya majaribio katika kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Akiwahutubia waandishi wa habari mjini New York, Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema kuwa kuwatibu hivi karibuni wahudumu wawili wa afya kwa kutumia dawa za majaribio, kumeibua mjadala kuhusu ikiwa dawa ambazo hazijajaribiwa na kuthibitishwa kuwa salama kwa matibabu ya binadamu zinapaswa kutumiwa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola.

"Jopo hilo lilijadili ikiwa ni jambo la uadilifu kutumia dawa ambazo hazijasajiliwa na ambazo madhara yake hayajulikani kwa matibabu ya watu, na ni vigezo gani vinapaswa kutumiwa kufanya uamuzi wa matumizi hayo. Chini ya uongozi wa Shirika la Afya Duniani, hatua zinazochukuliwa sasa katika nchi zote nne zilizoathiriwa ni kuzuia na kudhibiti maambukizi, uchagizaji wa jamii na kuwasaka watu ambao wamegusana na wagonjwa wa Ebola."

Tangu ulipolipuka magharibi mwa Afrika, ugonjwa wa Ebola umewaua takriban watu 1000 katika nchi za Guinea, Liberia, Sierra Leone na hivi karibuni, Nigeria.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031