Tunahitaji mashujaa zaidi wa usaidizi wa kibinadamu: OCHA

Kusikiliza /

Toby Lanzer katika harakati za usambazaji wa misaada.Picha@UNHCR

Wakati wa kuadhimisha siku ya wafanyakazi wa usaidizi wa kibinadamu hii leo, Toby Lanzer, ambaye ni Kaimu Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, amesema ni muhimu kukumbuka waliofariki dunia wakati wa kutoa misaada ya kibinadamu katika vita na mizozo.

Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, Lanzer ameeleza kwamba maudhui ya mwaka huu yakiwa ni dunia inahitaji mashujaa zaidi wa usaidizi wa kibinadamu, yanamaanisha kwamba mahitaji yanazidi kuongezeka, kadri mizozo inaibuka kwenye sehemu mbali mbali, na vile vile mashujaa hao si wafanyakazi wa kimataifa tu, akisema:

" Hii siku ni njia ya kutambua kwamba kuna mashujaa wengi wa kibinadamu, na wengi wao ni raia tu wa kawaida waliopo kwenye nchi ambapo shida inaibuka, na wakati huu raia wanaowajibika ndiyo wa kwanza kusaidia majirani zao na jamii"

Aidha amezungumzia changamoto ambazo wasamaria wanakumbana nazo:

" Ukifanya kazi katika sehemu ya vita, si tu shida ya usalama, bali pia ugumu wa kutoa usaidizi kwenye hal ngumui, yaani changamoto za kuwasiliana na mamlaka za serikali, kujadiliana ili kupata njia, kuhakikisha kwamba vifaa vinafikia walengwa tu na vinatumia kwa njia bora…"

Hatimaye alikumbusha kwamba wasamaria wema hawawezi kila kitu. Jukumu lao ni kuboresha hali ya kibinadamu na kuondoa mateso ya vita, lakini suluhu endelevu ya mizozo ni ya kisiasa na si usaidizi wa kibinadamu.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930