Somalia imebadilika, tuisaidie isirudi nyuma: mtalaam wa UM Tom Nyanduga

Kusikiliza /

watoto 50,000 wameathirika na utapiamlo Somalia @UN Photos

Nchini Somalia, wakati kundi la kigaidi la Al-shabab likendelea kufanya mashambulizi na kukabiliwa na Ujumbe wa Muungano la Afrika unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa, AMISOM, raia wako hatarini kuathirika na baa la njaa jinsi waliovyoathirika mwaka 2011, ambapo zaidi ya watu 250,000 wamefariki dunia.

Mtalaam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini humo, Bahame Tom Nyanduga, ametoa wito kwa ufadhili wa dola milioni 663, ili kusaidia raia milioni 2.9 wanaokumbwa na ukosefu wa usalama wa chakula.

Amesema, Somalia imebadilika, serikali yake ikijitahidi kutengeneza katiba mpya na kuheshimika ndani na nje ya nchi, na kwa hiyo inafaa kusaidiwa.
Katika mahojiano aliyofanya na idhaa hii, ameanza kutoa maelezo zaidi kuhusu hali iliyopo sasa hivi kwa raia.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031