Nyumbani » 20/08/2014 Entries posted on “Agosti 20th, 2014”

Ban alaani mauaji ya mwandishi wa habari Foley

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha/UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mauaji ya kikatili ya mwandishi wa habari James Foley. Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imemkariri Ban akisema kuwa kitendo hicho kibaya ni ishara ya kampeni ya ugaidi inayoendeshwa na kikundi cha waislamu wenye msimamo mkali ISIL dhidi ya wananchi wa Iraq na Syria. [...]

20/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Uharibifu wa misitu ni jinamizi linaloiandama Uganda

Kusikiliza / Msitu wa kijamii unaoangamia wilayani Buliisa

Uharibifu wa misitu unasalia kuwa changamoto kubwa katika juhudi za kulinda mazingira kwani watu hukata miti kiholela na hivyo kuhatarisha maisha sio tu ya wanyama bali pia ya binadamu kwa ujumla. Uganda ni mojawapo ya nchi ambayo inakabiliana na changamoto hii. Je ni kwa kiasi gani? Katika kuelewa kuhusu changamoto zinazotokana na uharibufu wa misitu [...]

20/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatujasahau wasichana wa Chibok, Nigeria: UNFPA

Kusikiliza / Mkuu wa UNFPA nchini Nigeria Bi. Ratidza Ndhlovu,UN Photo/Loey Felipe

Shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA limesema halijasahau mahitaji ya wanawake na wasichana huko Chibok, Kaskazini mwa Nigeria ambako kundi la Boko Haram limekuwa tishio na kuharibu harakati za maisha ya kila siku ya jamii. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Mkuu wa UNFPA nchini Nigeria Ms. Ratidza Ndhlovu amesema usaidizi huo [...]

20/08/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Oman yaridhia Mkataba wa kupiga marufuku matumizi ya mabomu ya ardhini

Kusikiliza / Bomu la ardhi likilipuliwa. UN Photo/Robel Mockonenn

Oman imeridhia mkataba wa kimataifa wa Ottawa unaopinga matumizi, uzalishaji na biashara ya mabomu ya kutegwa ardhini na hivyo kufanya idadi ya nchi zilizotia saini mkataba huo kufikia 162. Sherehe za utiaji saini mkataba huo zimefanyika leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, ambapo mwakilishi wa kudumu wa Oman, Balozi Lyutha [...]

20/08/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Amri ya kutodhihaki ufalme Thailand ni ukiukwaji wa haki ya kujieleza

Kusikiliza / Picha@Ravina Shamdasani/OCHR

Kamishna ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imesema kuwa kumeendelea kujitokeza kwa vitendo vya kikatili pamoja na hukumu kali zinawakabili baadhi ya wananchi wa Thailand ambao hushurutishwa kupitia sheria ya lèse majesté inayolaumiwa kwa kukandamiza uhuru wa kujieleza. Msemaji wa Kamishina hiyo Ravina Shamdasani,amesema kuwa kuwepo kwa hali hiyo kunaendelea kubinya uhuru [...]

20/08/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mladenov aonya juu ya kulengwa kwa Sunni katika jimbo la Basra

Kusikiliza / Nikolay Mladenov@Picha/UNAMI

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq  Nickolay Mladenov, amesema ameshtushwa na machafuko yaliyozuka hivi karibuni ambayo yaliwalenga wananchi wa jamii ya Sunni walioko katika jimbo la Basra na kuelezea wasiwasi wake baada ya kuwepo kwa ripoti iliyonyesha kufanyika utekaji na mauwaji katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo. Mwanadiplomasia huyo amesema kuwa [...]

20/08/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na kurejea kwa mapigano Gaza

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. UN Photo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali kuvunjwa kwa makubaliano ya upelekaji wa misaada ya dharura katika eneo la Gaza ambayo yalipaswa kumalizika usiku wa manane. Ban amesema kuwa kutozingatiwa kwa makubaliano hayo ambayo yalitoa fursa kwa wafanyakazi wa usamaria mwema kusambaza misaada ya dharura kwa mamia ya raia wa Gaza ni [...]

20/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yataka mifumo ya kufuatilia magonjwa ya wanyama iimarishwe

Kusikiliza / Ngamia watuhumiwa hasa katika kueneza virusi MERS. Photo: World Bank/Curt Carnemark

Wakati mkutano wa mawaziri wa afya na kilimo ukiendelea huko Indonesia, Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ya wanyama unahitaji usaidizi endelevu ili kuzuia vitisho kwa magonjwa ya binadamu. George Njogopa na taarifa kamili. Taarifa ya George Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa kimataifa wa [...]

20/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa MONUSCO atembelea "visiwa vya amani" magharibi mwa DRC

Kusikiliza / Martin Kobler mkuu wa MONUSCO akizungumza na wanafunzi kwenye kijiji cha Kivu Kaskazini, @MONUSCO/SylvainLiechti

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, MONUSCO, Martin Kobler, ameanza ziara maalum ya kutembelea visiwa vya amani mashariki mwa nchi hiyo. Kwa mujibu wa MONUSCO, visiwa vya amani ni sehemu maalum zilizopata amani baada ya miaka mengi ya mapigano, ambapo MONUSCO inajaribu kutengeneza hali [...]

20/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani rabsha wakati wa ukaguzi wa kura Afghanistan

Kusikiliza / Wapiga kura wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi, Afghanistan.Picha@UNAMA

Umoja wa mataifa umeelezea hofu yake kufuatia mapigano kati ya wafuasi wa mgombea urais nchini Afghanistan Dkt. Abdullah Abdullah na watendaji wa Tume huru ya uchaguzi ambapo watu kadhaa walijehuriwa katika kituo cha ukaguzi huo mjini Kabul. Hii si mara ya kwanza kwa wawakilishi wa timu ya kampeni kurushiana maneno ambayo yamesababisha mapigano. Mwakilishi Maalum [...]

20/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baada ya kuishi miaka 30 DRC, wakimbizi wa Angola warejeshwa makwao

Kusikiliza / Wakimbizi wa Angola.Picha ya UNHCR/Celine Schnitt

Wakimbizi 500 wa Angola waliokuwa wanaishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wamesafiri kutoka mji mkuu Kinshasa kurudi makwao, baada ya kuishi ukimbizini kwa zaidi ya miaka 30. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte (Taarifa ya Priscilla) Shughuli hiyo inaendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR pamoja na Shirika la Kimataifa la [...]

20/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa chakula wanyemelea wahanga wa Ebola Afrika Magharibi

Kusikiliza / Mhudumu wa afya akimhudumia mgonjwa ambaye anawezekana kuwa na ugonjwa wa Ebola. (UNIFEED video capture)

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP linasema karibu watu Milioni Moja nukta Tatu wanahitaji msaada wa chakula kwenye maeneo yaliyokumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi. Taarifa kamili na Abdullahi Boru. (Taarifa ya Abdullahi) WFP inasema jamii kwenye maeneo ambayo serikali zimeyaweka chini ya karantini kutokana na mlipuko wa Ebola ziko [...]

20/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031