Nyumbani » 19/08/2014 Entries posted on “Agosti 19th, 2014”

Ebola: Jukumu la UM ni kusaidia jamii kwa ujumla, unyanyapaa haufai

Kusikiliza / Dkt. David Nabarro, Mratibu wa UM kuhusu ugonjwa wa Ebola. (Picha:UN Photo/Mark Garten)

Wiki moja baada ya kuteuliwa kuwa Mratibu Mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ugonjwa wa Ebola, Dkt. David Navarro amesema kesho anakwenda Afrika Magharibi ili abaini hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Umoja huo kusaidi raia, jamii na serikali zilizoathirika kwa ugonjwa huo.  Ataanzia Dakar, Senegal, halafu atakwenda Liberia, Sierra Leone, Guinea na hatimaye Nigeria. Akizungumza na [...]

19/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNMISS yalaani urushaji risasi karibu na kambi ya wakimbizi Bentiu

Kusikiliza / Kituo cha UNMISS.UN Photo/Martine Perret

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS umelaani tukio la Jumatatu usiku la ufyatuaji risasi angani uliofanyika karibu an kambi yake huko Bentiu, jimbo la Unity, tukio lililodumu kwa nusu saa. Taarifa ya UNMISS inasema chanzo cha ufyatulianaji huo wa risasi hewani ni wanajeshi wa kikosi cha serikali SPLA walioko karibu na uwanja [...]

19/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Usalama Bangui unatia moyo, lakini viungani bado: Gaye

Kusikiliza / Babacar Gaye, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UM huko CAR na Mkuu wa MINUSCA. (Picha:UN/JC McIlwaine)

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea ripoti kuhusu hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Katim, CAR wakati ambapo siku zinahesabika kabla kikosi cha kulinda amani cha umoja huo kuanza kazi yake nchini humo tarehe 15 mwezi ujao. Ripoti iliwasilishwa na mwakillishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini [...]

19/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sauti za mashujaa wa usaidizi wa kibinadamu kutoka DRC na Tanzania

Kusikiliza / Jack Kahorha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC @Picha ya OCHA

Tarehe 19, Agosti kila mwaka , ikiwa ni siku ya watoa huduma za kibinadamu duniani, Umoja wa Mataifa umekumbuka jitihada za wasamaria wema kote duniani kwa kuwapatia nafasi ya kuzungumzia uzoefu wao na maisha yao kama mashujaa wa usaidizi wa kibinadamu. Priscilla Lecomte amezungumza na  Gloria Kafuria kutoka shirika lisilo la kiserikali la Concern, Tanzania [...]

19/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ethiopia yaongoza barani Afrika kwa kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi

Kusikiliza / Wakimbizi waSudan Kusini wanoishi katika makazi ya muda wakisubiri mahema kutoka UNHCR.Ethipoia inawahifadhi zaidi ya wakimbizi 600,000.Picha© UNHCR/P.Wiggers

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema hivi sasa Ethiopia inaongoza barani Afrika kwa kuhifadhi idadi kubwa ya wakimbizi, nafasi ambayo awali ilikuwa inashikiliwa na Kenya. Kwa sasa Ethiopia inahifadhi wakimbizi karibu 630,000  ikiwa ni takwimu za hadi mwezi uliopita ilhali Kenya inahifadhi zaidi ya wakimbizi 575,000 waliosajiliwa na wasaka hifadhi. Mizozo [...]

19/08/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoa huduma za kibinadamu wakumbukwa; Ban aweka shada la maua

Kusikiliza / Maadhimisho ya siku ya wasaidizi wa kibinadamu @Fiona Blyth

Leo ni siku ya kimataifa ya watoa huduma za kibinadamu duniani ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa na matukio mbali mbali kukumbuka wale waliofariki dunia wakiwa kazini na wale wanaoendelea kutekeleza jukumu hilo bila kujali hatari zinazowakabili. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Saa Tatu na Nusu asubuhi kwenye makao makuu ya Umoja wa [...]

19/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ebola: Ishara ya matumaini Nigeria na Guinea

Kusikiliza / Muuguzi akimfariji mgonjwa aliyethibitika kuwa na kirusi cha Ebola.(Picha: WHO/Chris Black)

Shirika la afya duniani, WHO limetoa taarifa likisema kuwa kwa sasa hakuna taarifa mpya ya maambukizi ya kirusi cha ugonjwa wa Ebola huko magharibi mwa Afrika kulikoripotiwa mkurupuko wa ugonjwa huo. Ugonjwa huo uliibuka Guinea, Liberia, Sierra Leone na Nigeria ambako mjini Lagos hali ya Nafuu imeanza kupatikana kwani kupona kwa kwa mmoja wa walioambukizwa [...]

19/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhalifu dhidi ya wasamaria ni ukosefu wa ubinadamu: Eliasson

Kusikiliza / Jan Eliasson, Picha ya UN

Baraza la usalama limekutana kujadili jinsi ya kulinda maisha ya wasamaria wema katika mizozo, kulingana na maadhimisho ya siku hii ya wasaidizi wa kibinadamu, likijaribu kuelewa sababu za kuongezeka kwa idadi ya wasamaria wanaouawa kila mwaka.  Taarifa zaidi na Abdullahi Boru (Taarifa ya Abdullahi) Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson, amelielezea Baraza [...]

19/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yazindua operesheni kabambe ya kufikisha misaada kaskazini mwa Iraq

Kusikiliza / Watoa huduma wakati wa kuwasilisha misaada kwa watu waliolazimika kukimbia makwao.Picha© UNHCR/E.Colt

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, linazindua operesheni kabambe ya kuwafikishia misaada takriban watu nusu milioni ambao wamelazimika kuhama makwao kaskazini mwa Iraq. Operesheni hiyo ya kusafirisha misaada kwa njia ya angani, barabara na bahari, itaanza hapo kesho Jumatano kwa usafirishaji wa shehena za misaada kwa ndege kutoka Aqaba, Jordan kwenda Erbil [...]

19/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya usaidizi wa kibinadamu: Tuangazie pia udhibiti wa migogoro: Ashe

Kusikiliza / ocha-whd-

Katika kuadhimisha siku ya wasaidizi wa kibinadamu ulimwenguni leo Agosti 19, Umoja wa Mataifa umewakumbuka wafanyakazi wote waliopoteza maishayaowakitafuta amani duniani wakiwemo 22 waliofariki dunia katika shambulizi la bomu kwenye makuu ya Umoja huo mjiniBaghdad,Iraqmwaka jana. Rais wa Baraza Kuu la Umoja huo John Ashe katika ujumbe wake wa siku hii amesema kila siku maelfu [...]

19/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tunahitaji mashujaa zaidi wa usaidizi wa kibinadamu: OCHA

Kusikiliza / Toby Lanzer katika harakati za usambazaji wa misaada.Picha@UNHCR

Wakati wa kuadhimisha siku ya wafanyakazi wa usaidizi wa kibinadamu hii leo, Toby Lanzer, ambaye ni Kaimu Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, amesema ni muhimu kukumbuka waliofariki dunia wakati wa kutoa misaada ya kibinadamu katika vita na mizozo. Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, Lanzer ameeleza kwamba maudhui ya [...]

19/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930