Nyumbani » 15/08/2014 Entries posted on “Agosti 15th, 2014”

Baraza la Usalama laidhinisha vizuizi dhidi ya wanamgambo wa Iraq na Syria

Kusikiliza / Wakati wa kikao cha Baraza la Usalama Agosti 15.Picha ya UM/Devra Berkowitz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuweka vizuizi dhidi ya watu sita wanaojihusisha na makundi ya waislamu wenye msimamo mkali ya ISIL na Al-Nusra. Katika azimio hilo wanachama wa baraza hilo wameelezea kutiwa wasiwasi sana na matokeo ya vitendo vya watu hao na msimamo wao mkali juu ya utulivu wa ukanda [...]

15/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

DRC: Mfanyakazi wa kibinadamu auawa na watoto wake watekwa nyara na LRA

Kusikiliza / Moustapha Soumare,UN Photo/Devra Berkowitz

Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. DRC Moustapha Soumare, amelaani vikali mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na wanamgambo wa Lords Resistance Army, LRA, tarehe 12 mwezi huu, maeneo ya Mayangu, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Soumare ambaye pia ni Naibu Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, amekaririwa akisema kuwa [...]

15/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tatizo la afya ya akili lilikuwa ni mada kuu, Siku ya vijana duniani

Kusikiliza / Vijana wakiwa makao makuu ya UM,waakti wa kongamano la vijana.Picha ya UM/Mark Garten.(maktaba)

Matatizo ya akili kwa vijana husababisha unyanyapaa na ubaguzi, ambavyo aghalabu vinatokana na kutokuwepo uelewa mwema wa matatizo ya afya ya akili. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ban Ki-moon, unyanyapaa unaohusiana na matatizo ya afya ya akili unaweza kuchangia kuwatenga waathiriwa au kuwafanya wakate tamaa katika kutafuta usaidizi, wakiogopa kuhusishwa na sifa mbaya. Katika kuadhimisha [...]

15/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Rwanda yapunguza vifo vya utotoni kwa 70%

Kusikiliza / Mtoto na mama yake Rwanda Picha ya UNICEF Rwanda

Lengo la maendelo ya milenia nambari nne ni kupunguza kwa theluthi mbili idadi ya vifo vya utotoni, kati ya mwaka 1990 na 2015. Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, Rwanda imevuka lengo hilo kwa kukupunguza vifo vya utotoni kwa asilimia 70. Je walitumia mbinu gani? Ungana na Priscilla [...]

15/08/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNMISS yalaani mapigano huko Bentiu

Kusikiliza / Picha@UNMISS

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS imesema kuwa alfajiri ya leo kumekuwepo na mapigano makali yaliyofanyika kwa kutumia silaha ndogo na vifaru eneo la kusini mashariki mwa makao ya ujumbe huo mjini Bentiu jimbo la Unity. Kaimu Mkuu wa UNMISS Toby Lanzer amesema wakati wa mapigano hayo, zaidi ya raia 340 walikimbia [...]

15/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viwanja vya ndege Tanzania kuwa na mashine maalum kudhibiti Ebola Tanzania.

Kusikiliza / Idara ya Magonjwa ya Kuambukiwa – Guinea Conakry -
@WHO – T. Jasarevic

Nchini Tanzania siku ya Alhamisi kulikuwepo na hofu ya Ebola baada ya wagonjwa wawili kulazwa katika hospitali moja jijini Dar es salaam wakihofiwa kuwa na ugonjwa huo. Kufahamu ukweli wa tukio hillo mwenzetu George Njogopa wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa jijini humo amezungumza na Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi Dkt. [...]

15/08/2014 | Jamii: Ebola, Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Safari ya kwanza ya mkuu wa usalama wa Umoja wa Mataifa ni Kenya

Kusikiliza / Peter Thomas Drennan Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya Usalama. @UN Photos/Eskinder Debebe

Peter Drennan aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya Usalama, amechagua Kenya na Somalia kwa ziara yake ya kwanza kama mkuu wa idara hiyo. Alipozungumza na Irene Mwakesi, wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa mjini Nairobi, Drennan amesema ilikuwa muhimu kutembelea Kenya kwa sababu ya [...]

15/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtaalamu wa haki za binadamu aitaka Sudan kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa

Kusikiliza / Mtaalam huru wa UM kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan, Mashood Adebayo Baderin.Picha/UM/Jean-Marc Ferré

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan, Mashood Adebayo Baderin, amtoa wito kwa serikali ya Sudan kumwachia huru mara moja Naibu Mwenyekiti wa chama cha Umma, Merial Al-Mahdi na kiongozi wa chama cha Congress, Ibrahim Al-Sheikh na wafungwa wote wa kisiasa. Grace Kaneiya na taarifa kamili (Taarifa ya [...]

15/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asema uamuzi wa Al Malik ni wa kuungwa mkono

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon. UN Photo/Paulo Filgueiras/NICA

Katibu mkuu wa Umoja w a Mataifa Ban Ki-moon amepongeza uamuzi wa Waziri Mkuu wa Iraq Bwana Nouri Al Maliki wa kukubali kujitoa katika kinyang'anyiro cha kiti cha Uwaziri Mkuu na badala yake kumuunga mkono Waziri mkuu mteule Bwana Heiner Al Abbadi kama mrithi wake. John Ronoh na ripoti kamili. (Taarifa ya John) Ban amesema [...]

15/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tanzania hakuna mgonjwa wa Ebola, mashine zaagizwa kuimarisha udhibiti

Kusikiliza / Udhibiti wa Ebola. picha@WHO(Video capture)

Serikali ya Tanzania imesema imeagiza vifaa vitakavyowezesha uchunguzi wa wagonjwa kwenye viwanja vyake vya ndege. Katibu Mkuu wizara ya Uchukuzi Dk.  Shaaban Mwijaka amesema hayo katika mahojiano na George Njogopa wa Idhaa hii jijini Dar es salaam. (Sauti ya Dkt. Mwijaka) Kuhusu safari za ndege amesema.. (Sauti ya Dkt Mwijaka.) Bwana akazungumzia uvumi wa kuwepo [...]

15/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi ni zaidi ya unavyoripotiwa

Kusikiliza / Udhibiti wa Ebola Kailahun, Sierraleone.Picha ya WHO(Video capture)

Shirika la afya duniani WHO limesema mlipuko wa ugonjwa wa Ebola utaendelea kwa kipindi kadhaa huku likitanabaisha kuwa mlipuko huo wa sasa ni mkubwa kuliko ilivyodhaniwa hapo awali. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Taarifa hiyo ya WHO inazingatia ripoti kutoka kwa wahudumu wa afya ambao wakienda kwenye maeneo yenye mlipuko hususan wanashuhudia [...]

15/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »