Nyumbani » 14/08/2014 Entries posted on “Agosti 14th, 2014”

Mashirika ya kibinadamu yakaribisha kuongezeka kwa sitisho la mapigano Gaza

Kusikiliza / Watoto 344 wamezaliwa kwenye kambi za UNRWA @UNRWA

Sitisho la mapigano Gaza limeongezeka kwa siku tano, mapema siku ya alhamis, kufuatia mazungumzo ya amani yanayoendelea Misri. Kwa mujibu wa msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric, Mashirika ya kibinadamu yamekaribisha hatua hiyo kwa kusema itawawezesha wafanyakazi wa kibinadamu kuendelea na shughuli za kutafuta majeruhi ambao bado wamenaswa kwenye vifusi vya numba zilizobomolewa. Vile [...]

14/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miji inayojaribu kuhimili majanga ya hali ya hewa yafika 2000

Kusikiliza / mafuriko nchini Pakistan @UN Photos/Evan Schneider

Idadi ya miji iliyojiunga na mtandao wa kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na hatari za tabianchi imefikia 2000. Kampeni iliyozinduliwa mwaka 2010 iitwayo Making Cities Resilient: My City is Getting Ready! inalenga kuelimisha viongozi kuhusu hatari zitokanazo na hali ya hewa kama vile mafuriko au maporomoko ya ardhi, na kubadilisha mifumo ya ujenzi [...]

14/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vifo vya watoto wachanga bado changamoto Tanzania

Kusikiliza / Baby Nyariek@Picha Unifeed

Lengo la nne ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia ni kuhakikisha kwamba huduma za afya zinapatikana kwa raia ili kutokomeza vifo vya watoto wachanga. Huko Mwanza Tanzania, changamoto nyingi zinawakumba wanawake wajawazito kwa sababu ya kutokuwepo kwa zahanati na hospitali karibu na makazi yao husususan vijijini. Je wanawake wajawazito wana maoni yapi kwa ajili ya [...]

14/08/2014 | Jamii: Jarida, Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yachukua hatua kupunguza athari za misako ya usalama kwa raia

Kusikiliza / Mlinda amani wa UNAMID katika moja ya doria kuhakikisha usalama wa raia huko Khor Abeche. (Picha: Albert Gonzalez Farran, UNAMID)

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID umesema unatiwa hofu na misako ya kuimarisha usalama inayofanywa na majeshi ya serikali ya Sudan kwenye kambi za wakimbizi wa ndani Darfur Kusini. Taarifa ya UNAMID imesema misako hiyo inaweza kuwa na madhara kwa raia na hivyo tayari imechukua hatua kupunguza [...]

14/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marekani yamulikwa kwenye Kamati kuhusu kutokomeza ubaguzi wa rangi

Kusikiliza / marafiki wa rangi mbalimbali2

Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusika na utokomezaji wa ubaguzi wa rangi, leo imekamilisha tathmini yake ya ripoti tatu kuhusu Marekani na jinsi inavyotekeleza vipengele vya mkataba kuhusu utokomezaji wa aina zote za ubaguzi wa rangi. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua Akiongoza ujumbe wa Marekani uliowasilisha ripoti hizo, Mwakilishi wake wa Kudumu [...]

14/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wakimbizi wa ndani Iraq imefika milioni 1.5

Kusikiliza / Jamii ya Yezidi wamelala kivulini baada ya kukimbia Sinjar.Picha© UNHCR/N.Colt

Siku Moja baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kwamba tatizo la kibinadamu Iraq limefikia ngazi ya juu kabisa ya dharura, Ujumbe wa Umoja huo nchini Iraq, UNAMI, umeeleza kwamba idadi ya wakimbizi inazidi kuongezeka kila siku. Taarifa zaidi na John Ronoh. Taarifa ya John Kwa mujibu wa msemaji wa UNAMI, Eliana Naaba, hali mbaya ya [...]

14/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Safari za ndege kutoka nchi zenye Ebola si lazima zisababishe maambukizi:WHO

Kusikiliza / Wahudumu wa afya katika moja ya harakati za kinga na tiba dhidi ya ugonjwa huo huko Afrika Magharibi. (Picha@WHO)

Shirika la afya duniani, WHO limesema ni uwezekano mdogo sana wa maambukizi ya kirusi cha Ebola pindi mtu anaposafiri kwa ndege au kupokea wasafiri wanaotoka nchi zenye maambukizi ya ugonjwa huo. Ripoti ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi. (Taarifa ya Assumpta) Dokta Isabelle Nuttal, Mkurugenzi wa masuala ya tahadhari kutoka WHO amewaambia waandishi wa habari mjini [...]

14/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amwelezea Rais Poroshenko hofu yake kuhusu mzozo wa Ukraine

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akizungumza na Rais wa Ukraine Petro Poroshenko @UN Photos/Sophia Paris

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea kutiwa wasiwasi na hali nchini Ukraine alipofanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Petro Poroshenko kuhusu mzozo unaoendelea mashariki mwa nchi hiyo. Taarifa kamili na George Njogopa Taarifa ya George Njogopa Taarifa iliyotolewa na msemaji wake imesema kuwa Katibu Mkuu amemwambia Rais Poroshenko kwamba amekuwa [...]

14/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM kuzuru Azerbaijan

Kusikiliza / Nembo ya UM

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuzuru nchini Azerbaijan kuanzia Agosti 18 mwaka huu kwa ajili ya kuendesha uchunguzi kuhusiana na uvunjifu wa haki za binadamu. Jopo hilo ambalo hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza kufanya  nchini humo litakuwa na jukumu la kuangalia namna shughuli za kibiashara zinavyokiuka haki za binadamu. [...]

14/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

MONUSCO yalaani mauaji ya watu sita wa familia moja huko Kivu Kusini

Kusikiliza / Martin Kobler@UN

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuleta utulivu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, MONUSCO, Martin Kobler amelaani vikali mauaji ya watu sita wa familia moja huko Mutarule, jimbo la Kivu Kusini akisema ni uhalifu. Mauaji hayo yalitokea Jumatano ambapo Kobler amesema kitendo hicho hakikubaliki na tayari vikosi vya MONUSCO kwa kushirikiana na [...]

14/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031