Nyumbani » 12/08/2014 Entries posted on “Agosti 12th, 2014”

Siku ya Tembo Duniani yatukumbusha hatari zinazowakumba:UNEP

Kusikiliza / Tembo Picha@UNCEP

Takribani tembo 25,000 huuawa kila mwaka miongoni mwa idadi nzima ya tembo kati ya 420,000 na 650,000 waliopo duniani. Ni kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP, likiadhimisha siku ya tembo duniani Agosti 12 ikiwa ni mwaka wa tatu huku likikumbusha dunia kuwa iwapo ujangili utaendelea tembo watatoweka duniani. [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu 730,000 wapatiwa msaada wa chakula Gaza

Kusikiliza / Mgao wa chakula@UNRWA

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP pamoja na lile la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limeanza kampeni maalum ya kusambaza chakula kwa watu 730,000 ambao wameathirika na mzozo na ambao awali hawakupatiwa msaada wa chakula kwa njia nyingine. Pablo Recalde, Mkuu wa WFP Palestina amesema kufuatia sitisho la mapigano lililoanza [...]

12/08/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaonya Sri Lanka isiendelee kufukuza waomba hifadhi

Kusikiliza / Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards Picha@UNIFEED

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR limeeleza wasiwasi wake na hali ya watu wanaoomba hifadhi nchiniSri Lankawakati huu ambapo idadi ya wanaofukuzwa nchini inaendelea kuongezeka licha ya maombi ya jamii ya kimataifa kusitisha kitendo hicho. Tangu Agosti Mosi mwaka huu raia 88 waPakistanwamerudishwa nyumbani ambapo kwa mujibu wa UNHCR, maishayaoyako hatarini. UNHCR [...]

12/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watalaam wa haki waomba hatua zichukuliwe Iraq kuzuia mauaji ya kimbari

Kusikiliza / Rashida Manjoo,mtalaamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake

Kundi la watalaamu mbali mbali wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo limeeleza kutiwa wasiwasisanana hatari ya mauaji inayokumba jamii ya Wayazidi waliolazimishwa kukimbia makwao na wengine wanaoshambuliwa na wanamgambo wa IS. Mjumbe maalum kuhusu maswala ya walio wachache, Rita Izsak, amesema hatua zote zinapaswa kuchukuliwa ili kuzuia mauaji ya wingi na uwezekano [...]

12/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Burundi na harakati za ushirikishaji wanawake kwenye uongozi

Kusikiliza / Mkaazai wa Burundi.Picha ya UM/Martine Perret(maktaba)

Wakati dunia ikielekea kufikia ukomo wa malengo ya milenia mwakani, nchi mbali mbali zimepiga hatua katika kuhakikisha kwamba zinafikia malengo hayo. Lengo la tatu la maendeleao ya milenia ni kuimarisha usawa wa kijinsia na kustawisha wanawake. Ndani ya lengo hili kuna suala la kumshirikisha mwanamke katika nafasi za uongozi. Je nchini Burundi lengo hili limefikiwa?Basi [...]

12/08/2014 | Jamii: Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

UNSMIL yatoa wito kwa pande kinzani Libya ziunge mkono juhudi za kusitisha mapigano

Kusikiliza / Nembo ya UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL, umelaani vikali mapigano yanayoendelea mjini Tripoli, licha ya wito uliotolewa mara kwa mara wa kusitisha mapigano mara moja na kutotumia nguvu kutatua tofauti za kisiasa. Ujumbe huo umetoa wito kwa pande zinazozozana kuunga mkono juhudi za kusitisha mapigano mara moja. UNSMIL imelaani pia kuongezeka idadi ya raia [...]

12/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mjumbe mmoja wa Tume ya uchunguzi Gaza ajitoa

Kusikiliza / Baudelaire Ndong Ella, mwakilishi wa kudumu wa Gabon katika ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva na rais wa Baraza la Haki za Binadamu. @UN Photo / Jean-Marc Ferre

Siku moja baada ya Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa kutangaza wajumbe watatu walioteuliwa kuunda jopo la tume ya uchunguzi wa ukiukwaji huko Ukanda wa Gaza mmoja wa wajumbe hao Amal Alamuddin, amesema hayuko tayari kuridhia jukumu hilo. Rais wa Baraza la haki za binadamu aliyeunda jopo hilo Baudelaire Ndong Ella amesema [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Dkt. Nabarro kuwa mratibu wa UM wa Ebola, ataka hofu na woga viepukwe

Kusikiliza / Dkt. David Nabarro, Mratibu wa UM kuhusu ugonjwa wa Ebola. (Picha:UN Photo/Mark Garten)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani na kutangaza kumteua Dkt. David Nabarro kama mratibu mwandamizi wa Umoja wa Mataifa kuhusu ugonjwa wa Ebola. (Sauti ya Ban)  "Dkt. Nabarro atawajibika kuhakikisha mfumo wa umoja wa Mataifa unatoa mchango wa dhati katika kuratibu harakati za kimataifa [...]

12/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tatizo la wakimbizi lazidi kuwa sugu nchini Iraq

Kusikiliza / Picha@UNHCR/R. Nuri

  Takriban raia 400,000 wa Iraq kutoka makundi ya walio wachache wamelazimika kuhama makwao kaskazini magharibi  mwa nchi, wakikimbia ukatili unaotekelezwa na wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali, ISIL, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNCHR. Priscilla Lecomte na taarifa zaidi. (Taarifa ya Priscilla) Wengi wa watu waliolazimika kuhama wamepewa makazi katika kata ya [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana tumieni kura zenu kuleta maendeleo endelevu: Ban

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. (Picha:UN Photo/Evan Schneider)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumza kwenye tukio la siku ya vijana duniani hii leo na kuzungumzia umuhimu wa afya ya akili ya vijana na vijana kutumia vyema kura zao kufikia maendeleo endelevu. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Ban alitumia hadhara hiyo kumkaribisha mgeni wake Bi. Raquelina Langa kutoka [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama wawasili Sudan Kusini

Kusikiliza / Wawakilishi wa Baraza la Usalama walipoika katika uwanja wa ndege wa Juba. Hapa Balozi Eugene Gasana wa Rwanda na Balozi Samantha Powers wa Marekani wanaokaribishwa na mwakilishi wa Sudan Kusini. @UNMISS/JC McIlWaine

Wawakilishi 15 wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamewasili Juba mji mkuu wa Sudan Kusini wakitokea Ulaya, katika harakati za kusaidia kumaliza mzozo uliokumba nchi hiyo tangu mwezi Disemba mwaka jana. Kwenye Uwanja wa Juba walilakiwa na Waziri wa Mambo ya nje Ellia Emora kwa niaba ya Rais Salva Kiir [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Serikali ya Gambia yabatilisha ziara ya wataalam wa haki za binadamu dakika ya mwisho

Kusikiliza / Rais wa Gambia El Hadji Yahya Jammeh akihutubia baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. @UN Photos/Erin Siegal

Wataalam wawili wa haki za binadamu wameelezea kusikitishwa na uamuzi wa serikali ya Gambia kuahirisha hadi mwakani ziara yao nchini humo, ambayo ilikuwa imepangwa kuanza leo hadi Agosti 18, 2014. Katika barua ya tarehe 6 Agosti, serikali ya Gambia iliwajulisha mtaalam kuhusu utesaji, Juan E. Méndez, na Christof Heyns ambaye ni mtaalam kuhusu mauaji kinyume [...]

12/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vijana wasikilizwe si washinikizwe cha kufanya: Balozi wa vijana

Kusikiliza / Vijana hawa wanapaswa kusikilizwa maoni  yao. (Picha:UNFPA/Idriss Qarqouri (NICA ID:587729)

Lian Kariuki ni ambaye ni Balozi wa vijana duniani kupitia taasisi ya A World at School amezungumza na Idhaa hii katika mahojiano maalum na kueleza kile anachoona kuwa ni chanzo cha vijana kukumbwa na matatizo ya afya ya akili. (Sauti Lian-1) Lian akapendekeza cha kufanya kuondokana na tatizo hilo ikiwemo kuwasikiliza vijana kile wanachotaka. (Sauti [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dawa za majaribio zinaweza kutumiwa kutibu Ebola kwa sasa: Wataalamu

Kusikiliza / Mhudumu wa afya akivalia sare ya kujikinga wakati wa kuwahudumia waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola,Kailahun,Sierra Leone.Picha:IRIN/Tommy Trenchard

Shirika la afya duniani, WHO limeridhia dawa ya majaribio ya kutibu Ebola itumike kutibu wagonjwa kwa sasa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Jopo la wataalam wa maadili ya utabibu ambalo limekuwa likikutana mjini Geneva limefikia uamuzi kuwa, matibabu ya majaribio ambayo madhara yake bado hayajulikani, yanaweza kutumiwa ili kunusuru maisha ya watu [...]

12/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuvunje ukimya afya ya akili ya vijana: Ban, Ashe

Kusikiliza / IYD

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya vijana ikiangazia afya ya akili ya kundi hilo, chapisho jipya la Umoja wa Mataifa linaonyesha kuwa asilimia 20 ya vijana duniani kote wanakumbwa na tatizo hilo kila mwaka. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika ujumbe wake wa siku hii amesema hali inakuwa mbaya zaidi kijana [...]

12/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031