Nyumbani » 07/08/2014 Entries posted on “Agosti 7th, 2014”

Heko SLA/Minni Minawi kwa kuchukua hatua kuepusha watoto jeshini:UNAMID

Watoto hawa wacheza katika kituo cha jamii kilichojengwa na UNAMID katika kambi ya wakimbizi wa ndani , Khor Abeche, kusini Darfur (Picha/UM/Albert González Farran/NICA)

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID, umekaribisha hatua mpya ziliyochukuliwa na kikundi kilichojihami cha Sudan Liberation Army/Minni Minawi, SLA/Minni Minawi cha kupiga marufuku uandikishaji watoto kwenye vikosi vyake. Naibu Mkuu wa UNAMID Abidoun Bashua amesema hatua hiyo inatokana na agizo la mkuu wa kikundi hicho Minni Minawi [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa kitaifa Sudan ni fursa ya kumaliza mizozo inayoendelea: UNAMID

Kusikiliza / Mohamed Ibn Chambas,  Mwakilishi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika. Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepokea taarifa kuhusu hali ya usalama na kibinadamu huko Darfur nchini Sudan ambapo Katibu Mkuu amesema changamoto ya sasa ni vile ambavyo jamii ya kimataifa inaweza kushawishi pande zote kwenye mzozo huwa ili zitambue kuwa nguvu za kijeshi na mwendelezo wa hali ya sasa havikubaliki. Ripoti ya [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania na harakati za kutokomeza mila na desturi potovu

Kusikiliza / Mwanamke mjane Tanzania. Picha:UNICEF/Tanzania

Usawa wa kijinsia na kuwezesha wanawake ni lengo namba tatu la maendeleo ya Milenia ikimulika pia kutokomeza tabia za unyanyasaji wanawake hasa wakati waume zao wanapofariki dunia. Nchini Tanzania, harakati zinaendelea kuondokana na mila na desturi potofu zinazokandamiza wanawake. Je hali iko vipi? Basi ungana na Martin Nyoni wa Redio Washirika Redio SAUT kwa makala [...]

07/08/2014 | Jamii: Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa watiwa wasiwasi na hali ya usalama Iraq kaskazini

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Mosul waliotafuta hifadhi Kurdistan @UNHCR/ S. Baldwin

Umoja wa Mataifa umesema una wasiwasi sana kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama na ya kibinadamu kaskazini mwa Iraq. Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Gyorgy Busztin amesema hali hiyo inatokana na kwamba kundi la waislamu wenye msimamo mkali la ISIL na waasi wengine wamevamia maeneo ya Ninewa, [...]

07/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uchaguzi wa 2015 utakuwa mtihani wa demokrasia kwa Burundi

Kusikiliza / Mkuu wa BNUB,  Parfait Onanga Anyanga, @UNphotos

Ingawa serikali ya Burundi inajitahidi kujenga mazingira ya utulivu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015, mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Parfait Onanga-Anyanga amesema bado hali ya kisiasa ni ya sintofahamu baina chama tawala na vile vya upinzani. Aliwaeleza wajumbe wa Baraza la Usalama siku ya jumatano, kuwa bado hakuna mazungumzo [...]

07/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bei za vyakula zaendelea kupungua duniani: FAO

Kusikiliza / Kupungua kwa bei ya nafaka kumesaidia kushuka kwa bei ya vyakula.Picha@FAO

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limetangaza kipimo cha bei za vyakula kwa mwezi wa Julai kinachoonyesha kushuka  kwa bei za vyakula kwa mwezi wa nne mfululizo. Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Mtalaam wa Kiuchumi  Sherin Mustafa amesema, vyakula ambavyo vimeshuka kwa bei hasa ni nafaka, mafuta na bidhaa za [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani mauaji ya wafanyakazi wa kibinadamu Sudan Kusini

Kusikiliza / Kikao cha baraza la usalama.Picha/UM/NICA

Baraza la Usalama limelaani vikali mashambulizi yaliyotokea hivi karibuni dhidi ya wafanyakazi wa kibinadamu huko Sudan Kusini wakati wanamgambo wajiitao  Jeshi la Ulinzi  wa Maban walipokabiliana na askari wa jeshi la kitaifa SPLA  wenye asili ya Nuer. Rais wa Baraza la usalama Balozi Mark Lyall Grant amesema wajumbe wamesema mauaji hayo yanaweza kuwa uhalifu wa [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shawishini FDLR ijisalimishe: Kobler aiambia jamii ya kimataifa

Kusikiliza / Wakati wa hotuba yake Martin Kobler kwa kikao kilichoangazai DRC.Picha/UM/Paulo Filgueiras/NICA

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja huo Martin Kobler amesihi jamii ya kimataifa kushawishi kikundi cha FDLR kushiriki kwenye mpango wa upokonyaji silaha. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Kobler amesema miezi mitano tangu [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yasaka muongozo wa tiba dhidi ya Ebola

Kusikiliza / Harakati za kudhibiti Ebola nchini Guinea-Conakry. Picha @WHO

Wakati mkutano wa kamati ya dharura ya shirika la afya duniani WHO kuhusu mustakhbali wa Ebola ukiingia siku yake ya pili, Shirika hilo limesema mapema wiki ijayo litaitisha kikao cha jopo la wataalamu wa maadili ya kitabibu kuhusu majaribio ya tiba dhidi ya ugonjwa huo huko Afrika Magharibi. Amina Hassan na taarifa kamili. (Taarifa ya [...]

07/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yaomba usaidizi wa kibinadamu kwa watu wa Gaza ambapo hali inazorota

Kusikiliza / Picha ya UNAMA

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, leo imetoa ombi la dola milioni 367 za kuwasaidia watu wa Gaza, ambao limesema hali yao imezidi kuwa dhoofu. Fedha hizo zinatarajiwa kukidhi mahitaji ya watu milioni 1.8 ambao wameathiriwa na mapigano, wakiwemo 490,000 waliolazimika kuhama makwao na ambao wanahitaji misaada ya kunusuru maisha [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wahusika wa ukatili Cambodia wafungwa kifungo cha maisha

Kusikiliza / Wakati wa kusikilizwa kwa kesi mahakama, Cambodia.Picha ya UM/NICA/maktaba

Nchini Cambodia mahakama maalum inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewahukumu kifungo cha maisha wahusika wawili wa vitendo vya uhalifu dhidi ya binadamu vilivyofanyika miaka ya sabini nchini humo. John Ronoh na taarifa kamili.  (Taarifa ya John) Jopo la majaji wa mahakama hiyo maalum limeamua kuwa Nuon Chea na Khieu Samphan wana hatia ya kutekeleza [...]

07/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031