Nyumbani » 06/08/2014 Entries posted on “Agosti 6th, 2014”

GAZA: Baada ya mapigano kusitishwa, UNDP yawekea kipaumbele ukarabati na ajira

Kusikiliza / Helen Clark. Mkuu wa UNDP. Picha: UNDP

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limekaribisha sitisho la mapigano huko Ukanda wa Gaza likisema kwamba sasa litajikita kusaidia wapalestina wapate mahitaji yao. Mkuu wa UNDP, Helen Clark, amesema hatua hiyo ni muhimu kwani nyumba za watu takriban 65,000 zimebomolewa ama kuharibika kwa kiasi fulani, akiongeza kwamba hiyo itawarudisha nyuma maendeleo [...]

06/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Idadi ya vifo vya Ebola yaongezeka

Kusikiliza / Mhudumu wa afya akivalia sare ya kujikinga wakati wa kuwahudumia waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola,Kailahun,Sierra Leone.Picha:IRIN/Tommy Trenchard

Wakati mkutano wa dharura ulioandaliwa na Shirika la Afya Duniani, WHO unaendelea ili kutathmini iwapo mlipuko huo unaibua hofu ya kimataifa katika afya ya umma, idadi ya vifo vya Ebola imezidi kuongezeka, kwa mujibu wa WHO. Tayari watu 932 wameshafariki dunia kutoka nchi za Sierra Leone, Liberia, Guinea na hivi karibuni, Nigeria. Fadela Chaib, msemaji [...]

06/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ukraine mateso yataendelea hadi ghasia zitakapositishwa: UM

Kusikiliza / Baraza la Usalama Picha@UN Photo/Loey Felipe/NICA

Baraza la Usalama limekutana Jumanne kuhusu Ukraine, likielezwa na John Ging, Mkurugenzi wa operesheni za Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, juu ya hali ya kibinadamu nchini humo. Ging amesema watu watazidi kuteseka iwapo ghasia hazitasitishwa nchini humo, na hatua zinahitajika kuchukuliwa ili kuzuia mzozo unaoendelea kuzorotesha hali ya usalama. Amesema Watu milioni 3.9 wanaishi [...]

06/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mradi wa Benki ya dunia waleta nuru kwa wahanga wa ukatili wa kingono DRC

Kusikiliza / Wanawake katika hospitali inayofadhiliwa na benki ya dunia.Picha@WORLD BANK

Vitendo vya kubaka wanawake na kunajisi watoto vimekuwa ni silaha ya vita kwenye maeneo ya mzozo ikiwemo huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wahanga wa vitendo hivyo huona kwamba ni mwisho wa maisha yao kutokana na unyanyapaa unaowakumba. Hata hivyo Benki ya dunia imepeleka nuru kwenye ukanda huo kupitia mradi wake na sasa kuna [...]

06/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Heshimu kinga ya bunge; IPU yaieleza serikali ya DRC

Kusikiliza / Nembo ya IPU @IPU

Umoja wa mabunge duniani, IPU umeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya kukamatwa na kutia korokoroni kwa mbunge wa upinzani huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, Jean-Bertrand Ewanga. Ewanga ambaye ni Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha Union for the Congolese Nation, UNC anadaia kuchochea chuki na kumtusi Mkuu wan chi, madai ambayo amekanusha [...]

06/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Sudan Kusini bado waamini silaha ni suluhu ya mzozo wao

Kusikiliza / mulet1

Baraza la Usalama leo limekutana kutathmini  hali iliyopo Sudan Kusini na mahitaji ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS. Naibu Mkuu wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa Edmond Mulet  amelieleza baraza hilo kwamba mashambulizi yanaendelea, waasi wengine wakilenga raia kwa misingi ya kikabila. Amesema, mapigano yanakwamisha shughuli [...]

06/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lakutana mahsusi kuhusu hali ya Gaza

Kusikiliza / Baraza Kuu juu ya hali ya Ukanda wa Gaza. Picha: UN Photo/Mark Garten

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao maalum kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza, huku sauti zikipaziwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua zote ziwezekanalo kuutatua mzozo huo uliodumu miaka mingi, ili kuwaepusha raia na madhila zaidi. Taarifa kamili na Joshua Mmali (Taarifa ya Joshua Mmali) Kikao cha leo cha Baraza Kuu kimehutubiwa na [...]

06/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Miaka 69 baada ya Hiroshima, harakati zaidi zahitajika: Ban

Kusikiliza / Hiroshima. Picha@UN Photo/DB

Miaka 69 tangu kuangushwa kwa bomu la atomiki huko Hiroshima, Japan, ni lazima tuhakikishe tunafikia lengo la wahanga wa tukio hilo la kuwa na dunia isiyo na silaha za nyuklia. Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika ujumbe wake uliosomwa kwa niaba yake na mwakilishi wake wa masuala ya kutokomeza silaha angamizi [...]

06/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vijana wawili washinda tuzo ya UPU

Kusikiliza / Nataša Miloševic mshindi kutoka Bosnia na Herzegovina.Picha@UPU

Vijana wawili ikiwamo mmoja kutoka Bosnia na Herzegovania wameibuka washindi wa shindano la kimatafa la uandishiwa wa barua lililoratibiwa na Umoja wa Posta Duniani kwa mwaka 2014. Hii ni mara ya kwanza kwa kijana wa Bosnia kuibuka mshindi kwenye shindano hilo tangu taifa hilo lilipojiunga rasmi na umoja huo UPU mwaka 1993. Kijana Natasa Milosevic [...]

06/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uchumi wa Pacific bado unajikongoja-UN

Kusikiliza / Nakala ya ripoti@ESCAP

Hali ya ukuaji uchumi katika eneo la Pacific imetajwa kuwa ni ya kusua sua huku Umoja wa Mataifa ukitoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo vyote vya ndani ili kufungua uwanja utaotoa nafasi ya kukuza maendeleo ya kijamii. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya kijamii na uchumi( [...]

06/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lalaani mapigano ya Iraq

Kusikiliza / Baraza la Usalama.Picha@UM/NICA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali tukio la kushambuliwa kwa miji ya Sinjar na Tal Afar iliyowashambuliwa na waasi wanaotaka kusimamisha Dola ya Kiislamu nchini Iraq ambao wamekuwa wakiendelea na mashambulizi katika maeneo kadhaa. Baraza hilo limelaani matukio hayo huku likielezea wasiwasi wake kuhusiana usala wa mamia ya raia walioko kwenye eneo [...]

06/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Pillay aishutumu Japan kwa kushindwa kuwakirimu waathirika wa vita

Kusikiliza / Navi Pillay. Picha@UNIFEED

Mkuu wa Kamishna ya Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kwa Serikali ya Japan ambayo inadaiwa kushindwa kutoa suluhisho la kudumu kwa watumwa wa kingono waliokumbwa na masahibu hayo wakati wa vita, akionya kuwa haki za waathirika hao zinazojulikana kama 'faraja kwa wanawake' zinaendelea kuvunjwa kwa miongo kadhaa tangu [...]

06/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa DRC waliopo Afrika ya Mashariki wanataka kurudi makwao

Kusikiliza / Wakimbizi wa DRC washuka boti iliowaleta nyumbani baada ya kuvuka mto Oubangui.Picha © UNHCR/G.Diasivi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema idadi kubwa ya wakimbizi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC waliosaka hifadhi kwenye nchi za Afrika ya Mashariki sasa wanataka kurejea makwao. Kwa sasa kuna wakimbizi 430,000 waliosaka hifadhi eneo hilo na naibu msemaji wa UNHCR huko DR Congo Simon Lubuku anaelezea hali yao [...]

06/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Benki ya dunia yatoa dola Bilioni Tano kukuza umeme Afrika, Tanzania na Kenya zimo

Kusikiliza / Watoto darasani.Picha@world bank

Benki ya dunia itatoa dola Bilioni Tano kwa ajili ya kuimarisha uzalishaji umeme kwenye nchi sita za Afrika, tangazo lililotolewa na Rais wa benki hiyo Jim Yong Kim wakati wa mkutano wa viongozi wa Afrika na Marekani mjini Washington. Taarifa zaidi na John Ronoh. (Taarifa ya John Ronoh ) Nchi hizo ni Kenya, Tanzania, Ethiopia, [...]

06/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930