Nyumbani » 05/08/2014 Entries posted on “Agosti 5th, 2014”

Palestina yasaka ushauri wa kujiunga na ICC

Kusikiliza / Fatou Bensouda,ICC amekutana leo na Riad Al-Malki,waziri wa mambo ya nje wa Palestina

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Jinai, ICC, Fatou Bensouda, amekutana leo na Riad Al-Malki, ambaye ni waziri wa mambo ya nje wa Palestina, huko The Hague, Uholanzi. Katika mkutano huo, Waziri Al-Malki ameeleza wasiwasi wake juu ya mapigano yaGazana amemwomba Bi Bensouda maelezo kuhusu jinsi ya kujiunga na Mahakama hiyo. [...]

05/08/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

LRA bado tishio kwa usalama wa CAR na DRC

Kusikiliza / Magofu ya nyumba iliyochomwa moto na wapiganaji wa LRA katika kijiji cha Nguili-Nguili, karibu na Mji wa Obo, Jamhuri ya Afrika ya Kati. Picha: UNHCR / D. Mbaiorem

Ripoti iliyotolewa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA inaonyesha kwamba bado mashambulizi yanayofanywa na kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army, LRA yanatishia usalama wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. OCHA imesema tangu mwezi wa Januari, mashambulizi 119 yalitokea na kusababisha [...]

05/08/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

EAC imepiga hatua utekelezaji malengo ya milenia:Eriyo

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Joyce Iriyo wakati wa mahojiano na Rashid Chilumba.Picha ya UM/Kiswahili/Richard Chilumba

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Jessica Eriyo amesema kanda ya Afrika Mashariki inayojumuisha nchi 5 wanachama imepiga hatua muhimu kwenye utekelezaji wa malengo ya millennia. Katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika kando mwa kongamano la vijana wa Afrika Mashariki juu ya mabadiliko ya tabia nchi jijini Mwanza, Tanzania, [...]

05/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

UNAMA yaomboleza mauaji ya wanajeshi wa kimataifa na wa Afghanistan

Kusikiliza / Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNAMA, Ján Kubiš

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA, umetuma rambirambi zake kwa familia na wafanyakazi wenza wa wanajeshi wa vikosi vya kimataifa na vya jeshi la Afghanistan, ambao waliuawa katika shambulizi lililotokea leo karibu na mji wa Kabul. Kwa mujibu wa ripoti za awali, wanajeshi kadhaa ama waliuawa au kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na mtu [...]

05/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNMISS yalaani mauaji ya wahudumu zaidi wa kibinadamu Maban

Kusikiliza / UNMISS

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, umelaani vikali mauaji ya wafanyakazi watano wa mashirika ya kibinadamu yasiyo ya kiserikali nchini humo, ambayo yalitekelezwa na kundi linalojiita Kikosi cha Ulinzi cha Maban. Mauaji hayo yalifanyika mapema leo asubuhi karibu na mji wa Bunj, kata ya Maban, jimbo la Upper Nile. Wawili kati ya [...]

05/08/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Twasikitishwa na ukamataji na utesaji wa watu Thailand: UM

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu. Picha: UN Multimedia

Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imesema inatiwa hofu na vile ambavyo wanaharakati, wasomi, waandishi wa habari na wanasiasa wanakamatwa na kutiwa mbaroni huko Thailand tangu kufanyika mapinduzi ya kijeshi mwezi mwaka huu. Ofisi hiyo inasema tangu tarehe 22 Mei Baraza la Kitaifa la amani na Utulivu nchini humo limeitisha zaidi ya [...]

05/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa DRC warejea nyumbani kutoka Congo-Brazaville

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka DRC kwenye kituo cha Nyakabande, Uganda. Picha@UNHCR/L.Beck(UN News Centre)

Wakimbizi 81 wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wamerejea makwao kutoka nchi jirani ya Congo-Brazaville, ikiwa ni kundi la mwisho miongoni mwa wakimbizi zaidi ya Laki Moja waliorejeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR.   Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Wakimbizi hao walikuwa wamekimbia DRC baada ya [...]

05/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO kuamua kuhusu Ebola

Kusikiliza / @WHO(Video capture)

Shirika la afya duniani WHO litaitisha kikao cha kamati yake ya dharura kutathmini iwapo mlipuko wa ugonjwa wa Ebola huko Afrika Magharibi unaibua hofu ya kimataifa katika afya ya umma. Mkutano huo huo utafanyika Jumatano na Alhamisi hii na ni mara ya kwanza kwa kamati hiyo kuitishwa kufanya uamuzi kuhusu Ebola, ugonjwa ambao tangu mwezi [...]

05/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaonya kuhusu kuongezeka mahitaji ya kibinadamu mashariki mwa Ukraine

Kusikiliza / Mfanyakazi wa UNHCR azungumza na mwanamume aliyefurushwa kutoka makazi yake katika eneo la Donetsk ambako kumeathiriwa na mzozo.Picha© UNHCR/I.Zimova

Raia wa Ukraine wapatao 730,000 wamekimbilia Urusi tangu mapigano yalipoanza mashariki mwa Ukraine, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. UNHCR imesema kuwa wengi wa wakimbizi hao wanakaa kwenye maeneo ya karibu na mpaka, ingawa mamlaka za Urusi zimeweka vituo 600 vya makazi ya muda, ambavyo vinawapa hifadhi raia 42,000 wa Ukraine. UNHCR imesema [...]

05/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto Gaza wabeba mzigo wa mzozo unaoendelea

Kusikiliza / Mtoto akiangalia nyumba ya jirani akiwa katika vifusi vya nyumba iliyoharibiwa © UNICEF/NYHQ2014-0984/El Baba

Mwezi mmoja wa mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa Gaza umesababisha vifo vya watoto takribani 400 wa kipalestina ilhali wengine zaidi ya 2,500 wamejeruhiwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kama anavyoripoti Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Katika ripoti yake ya hivi karibuni zaidi, UNICEF imesema asilimia 70 ya watoto hao [...]

05/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Raia wa Nigeria wafurika Chad kukimbia Boko Haram

Kusikiliza / UNHCR Logo

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema maelfu ya raia wa Nigeria kutoka jimbo la Borno wamekimbilia Chad kutokana na mashambulizi yanayofanywa na kikundi cha Boko Haram. Wakimbizi hao wameingia kisiwa cha Choua kisichokaliwa na watu ambacho ni makutano ya mipaka ya Chad, Nigeria na Niger na wengi wao ni wanawake na [...]

05/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asifu kusitishwa mapigano huko Gaza

Kusikiliza / Shule ya msingi ya wasichana ya Jabalia iliyokuwa inahifadhi wakimbizi wa kipalestina huko Gaza, baada ya kushambuliwa tarehe 30 mwezi Julai 2014. (Picha:UNRWA Archives/Shareef Sarhan)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha jitihada mpya zilizowezesha makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 72 huko Ukanda wa Gaza kuanzisha saa mbili ya asubuhi ya leo kwa saa za Mashariki ya Kati. Grace Kaneiya na ripoti kamili. (Taarifa ya Grace) Ban amekaririwa na msemaji wake akizitaka pande zote kuheshimu makubaliano hayo [...]

05/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031