Nyumbani » 04/08/2014 Entries posted on “Agosti 4th, 2014”

MONUSCO kujadiliwa ndani ya Baraza la usalama wiki hii

Kusikiliza / Balozi Mark Lyall Grant, Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi wa Agosti. (Picha@UN-Paolo Filgueiras

Masuala ya amani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Burundi na Sudan ni miongoni mwa ajenda zitakazomulikwa ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu wa Agosti, amesema Mwakilishi wa kudumu wa Uingereza kwenye Umoja huo Mark Lyall Grant. Akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa programu ya mwezi huu, [...]

04/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yatiwa wasiwasi na ghasia zinazoendela Lebanon

Kusikiliza / Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Kaimu Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Ross Mountain, amelaani vikali mashambulizi dhidi ya jeshi la Lebanon na mapigano yanayoendelea kwenye maeneo ya Arsal. Mashambulizi hayo yamesababisha askari 16 na raia zaidi ya sita kufariki dunia, pamoja na watu wengine kujeruhiwa. Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa amepeleka rambirambi zake kwa familia za [...]

04/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Unyonyeshaji watoto na Ukimwi Afrika Kusini

Kusikiliza / Picha@UNICEF

Dunia ikiendelea kuadhimisha wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama, Afrika Kusini imefanikiwa kubadilisha jinsi ya kuhudumia akina mama walioathiriwa na virusi vya ukimwi kwa kuwashauri kunyonyesha watoto wao, kama njia bora ya kutunza afya zao. Je sera hiyo mpya imeleta mafanikio? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

04/08/2014 | Jamii: Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

UM wasikitishwa na tetemeko la ardhi China

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha: UN Photo/Mark Garten

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vya watu na kuharibika kwa majengo na miundombinu katika maeneo ya China kusini, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea jimbo la Yunnan, siku ya jumapili. Taarifa ya msemaji wake imemkariri Ban akituma rambirambi kwa serikali ya China na familia za wahanga huku [...]

04/08/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNMISS yalaani mauaji ya mtoa huduma za kibinadamu

Kusikiliza / Watoa huduma wa afya UNMISS. Picha ya UM

Huko Sudan Kusini kwenye jimbo la Upper Nile mtoa huduma za kibinadamu ameuawa huko Bunj, eneo la Maban wakati wa mapigano kati ya jeshi la serikali, SPLA na kikundi kinachojiita jeshi la ulinzi la Maban. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS umelaani vikali mauaji ya mfanyakazi huyo huku ukionyesha wasiwasi mkubwa kutokana [...]

04/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Bunge jipya Libya ni ishara ya amani: UNSMIL

Kusikiliza / Picha@UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, UNSMIL umepongeza kitendo cha kufanyika kwa mkutano wa wawakilishi wapya wa Bunge nchini humo licha ya wakati huu mgumu na hali dhoofu ya usalama ikisema kuwa ni njia ya kuendeleza mazungumzo ya kisiasa licha ya chagamoto zilizopo. Taarifa ya UNSMIL imesema hatua hiyo inadhihirisha kuwa raia wa nchi [...]

04/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban aingiwa na hofu kuhusu ghasia za Iraq

Kusikiliza / Kambi ya Baharka, ilioko kilometa 5 kaskazni mwa Erbili Iraq kaskazini, amabako maelfu ya wakimbizi wamekimbia mwakao kufuatia kutawanywa na ISIL.Picha/Emma Beals/IRIN

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ameshtushwa na ripoti kuwa  kundi la waasi linalojiita Dola ya Kiislamu nchini Iraq limetwaa mji mkubwa wa Sinjar pamoja na miji mingine miwili katika eneo hilo na kusababisha mamia ya raia kukosa makazi huku wengine wakiwa katika mahangaiko makubwa. Amesema kuwa kitendo hicho kimeongeza hali ya wasiwasi  kuhusu usalama wa [...]

04/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Bado nyuklia, maji na makaa ya mawe ni muhimu kwa nishati Afrika:

Kusikiliza / Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim. Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim amesema vyanzo vya nishati vya maji, nyuklia na makaa ya mawe ni muhimu kwa bara la Afrika linaoibukia hivi sasa. Amesema hayo katika mjadala unaoendelea huko Washington D.C kuhusu Afrika inayoibuka. (Sauti ya Kim) “Iwapo tutajikuta katika mazingira ambapo tunakataa makaa ya mawe, nyulia na hata [...]

04/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaomba dola milioni 100 kukabiliana na Ebola Afrika Magharibi

Kusikiliza / Harakati za kudhibiti Ebola nchini Guinea-Conakry. Picha @WHO

Shirika la Afya Duniani WHO, na marais wa nchi tatu za Afrika Magharibi zilizoathiriwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, wametoa ombi la dola milioni 100 kuwezesha kufadhili shughuli za kupambana na ugonjwa huo hatari. Ombi hilo limetolewa kufuatia ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Margaret Chan katika ukanda huo, ambapo alikutana na marais [...]

04/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtoto anyonye maziwa ya mama pekee miezi sita ya mwanzo: UNICEF

Kusikiliza / Mama akinyonyesha mwanawe katika hospitali, Belgrade,Serbia.Picha/UNICEF/NYHQ2011-1166/Holt

Wakati wiki ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama duniani ikiwa inaendelea Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF limekumbusha umuhimu wa kunyonyesha watoto ili kuepusha vifo vya utotoni. Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, Mtalaam wa UNICEF kwa ukanda wa Afrika ya Kati, Noel Marie Zagre, amezingatia mambo muhimu matatu.  Mosi kumpatia [...]

04/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani maandamano yaliyowelenga Wayahudi barani Ulaya

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha/UM/Paulo Filgueiras(picha ya maktaba)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa hivi karibuni dhidi ya watu wenye asili ya Kiyahudi ambao waliandamwa na ghasia na mashambulizi wakati kulipofanyika maandamano ya kupinga mashambulizi yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza. Taarifa zaidi na George Njogopa (Taarifa ya George) Maandamano hayo ambayo sehemu kubwa yamefanyika barani Ulaya yalihitimika kwa kuzusha ghasia dhidi [...]

04/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yalaani mauaji ya wanahabari Gaza

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova.Picha/UM/Amanda Voisard

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, amelaani vikali mauaji ya wanahabari na uharibifu wa vifaa vyao katika mzozo unaoendelea Gaza. Ameelezea kusikitishwa na mauaji ya mpiga picha Rami Rayan, watangazaji wa televisheni Sameh Al-Aryan na Ahed Zaqout pamoja na ripota wa gazeti Mohamed Daher, katika mashambulizi ya makombora Gaza. [...]

04/08/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hofu yatanda miongoni mwa wakimbizi wa wapalestina Gaza:UNRWA

Kusikiliza / Uharibifu uliotokana na mashambulizi huko GAza: Picha ya @UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema hofu imetanda miongoni mwa wakimbizi wa kipalestina huko Gaza wakati huu ambapo idadi ya waliokimbia makazi yao imefikia 270,000.  Taarifa zaidi na John Ronoh (Taarifa ya John Ronoh) UNRWA inasema idadi hiyo ni katika maeneo yake 90 ya kuhifadhi wakimbizi wa kipalestina kwenye [...]

04/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031