Nyumbani » 01/08/2014 Entries posted on “Agosti 1st, 2014”

Ban amteua Omar Abdi wa Canada kuwa Naibu Mkuu wa UNICEF

Kusikiliza / Omar Abdi wakati akiwasilisha bajeti ya 2014-2017 kwa bodi kikao cha 2013. Picha© UNICEF/NYHQ2013-0531/Markisz

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametangaza leo kuteuliwa kwa Omar Abdi, raia wa Canada aliyezaliwa nchini Somalia, kuwa Naibu Katibu Mtendaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Bwana Abdi sasa hivi ni Msimamizi wa Ukaguzi wa Matumizi ya fedha, UNICEF. Amewahi kuhudumu kama Naibu Msimamizi na Mkurugenzi wa UNICEF ukanda wa Mashariki [...]

01/08/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban ashtushwa na kuvunjwa kwa sitisho la mapigano

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric.Picha ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  amelaani vikali kitendi cha kikundi cha Hamas kuvunja sitisho la mapigano huko Ukanda wa Gaza. Sitisho la mapigano hilo lilitakiwa kuanza asubuhi ya leo Ijumaa kwa kipindi cha saa 72, lakini mapigano yalirejea baada ya ripoti iliyotolewa na jeshi la Israel kudai kwamba askari wawili wa Israel [...]

01/08/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Upatikanaji wa elimu kwa kila mtoto bado ni safari inayokabiliwa na changamoto nchini Uganda

Kusikiliza / Watoto darasani nchini Uganda. Picha ya UM/UN Radio/Kiswahili/John Kibego

Lengo la pili la milenia ni kufikia upatikanaji wa elimu ya msingi kwa wote. Kwa mujibu wa lengohilo, kila mtoto, awe wa kike au wa kiume, anapaswa kuhitimisha elimu ya msingi. Katika miaka kumi ya kwanza tangu kuazimiwa malengo ya maendeleo ya milenia mwaka 2000, viwango vya watoto kusajiliwa shuleni Kusini mwa Jangwa laSaharabarani Afrika, [...]

01/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Kupitia elimu idadi ya akina mama wanaonyonyesha watoto imeimarika Kenya

Kusikiliza / Picha@UNICEF

Leo Agosti mosi ni siku ya kwanza ya wiki ya unyonyeshaji duniani. Wiki hii ni fursa ya kuchagiza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto katika kujenga kinga dhidi ya magonjwa na pia kuimarisha afya ya mama. Katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki hii nchini Kenya kumefanyika hafla ya uzinduzi wa kampeni katika hospitali ya [...]

01/08/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kutoa elimu kwa waliokosa ni hatua katika kufanikisha lengo la pili, Tanzania

Kusikiliza / Watoto wa shule Uganda. Picha: Idhaa ya Kiswahili/John Kibego

Katika jitihada za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia yatakayofikia ukomo mwakani, Umoja wa mataifa unasema kwamba ni dhahiri kuwa malengo ya maendelo ya milenia ya Umoja wa Mataifa yameleta mabadiliko katika maisha ya wananchi wa nchi husika. Mfano ni mpango wa Serikali ya Tanzania, MEMKWA wa kutoa elimu kwa wale waliokosa fursa hiyo kwa [...]

01/08/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani mauaji ya wabunge Somalia.

Kusikiliza / Mwakili maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay.Picha ya UM/Jean-Marc Ferré

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM Nicholas Kay, amelaani kuuawa kwa mbunge wa bunge la serikali ya shirikisho nchini humo Sheikh Aden Madeer.. Taarifa ya UNSOM imemkariri Bwana Kay akielezea kusikitishwa na vitendo vya mashambulizi dhidi ya wabunge akisema kuwa mauaji hayo ni njia ya kuhujumu wale wanaojitahidi kuendeleza [...]

01/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 369 zahitajika kusaidia Wapalestina.

Kusikiliza / Picha ya@UNICEF/Eyad El Baba

Waziri wa Mambo ya Kijamii na Kilimo wa Palestina, Shawqi Issa na Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, James Rawley, wametoa wito kwa pamoja kwa kufadhili mahitaji ya kibinadamu ya Gaza. Wamesema kwamba raia wote wa Gaza, idadi yao ikiwa ni milioni 1.8, wameathiriwa na mzozo kwa njia mbali mbali. Wito [...]

01/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asifu hatua ya Mahakama Uganda kufuta sheria dhidi ya ushoga

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. UN Photo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha uamuzi wa mahakama ya kikatiba nchini Uganda wa kufuta sheria iliyoharamisha mapenzi ya jinsia moja huku akisema huo ni ushindi wa utawala wa kisheria. Taarifa ya msemaji wa Umoja huo imemkariri Ban akipongeza wote wale waliochangia hatua hiyo muhimu hususan watetezi wa haki za binadamu nchini [...]

01/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha uamuzi wa Afghanistan kutosajili watoto katika Jeshi

Kusikiliza / Nembo ya UNAMA

Umoja wa Mataifa leo umekaribisha uamuzi wa serikali ya Afghanistan kuondoa na kuzuia uandikishaji au utumikishaji wa  watoto katika majeshi ya  nchi hiyo. Serikali ya Afghanistan ilitoa hakikisho lake hivi karibuni la kuunga mkono mpango maalum wenye vigezo 15 vya kutekeleza mkakati uliotiwa saini na serikali hiyo na Umoja wa Mataifa, mwaka 2011. Mpango huo [...]

01/08/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Haki za wazee zamulikwa kwenye mkutano wa New York

Kusikiliza / Wachezaji wawili wakifurahia mchezo wa chesi katika jiji la New York.  Picha: UN Photo / Grunzweig

Kikao cha tano cha kamati ya inayoshughulikia masuala ya wazee kinamalizika leo hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kikimulika masuala ya haki za binadamu za watu wazee. Taarifa kamili na John Ronoh Kamati hiyo inayoshughulikia haki za wazee iliundwa kufuatia azimio namba 65/182 la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa [...]

01/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sitisho la mapigano kwa siku tatu Gaza matatani

Kusikiliza / Kituo cha usambazaji wa umeme , Gaza baada ya mashambulizi ya anga na Israeli katika kambi ya wakimbizi ya Nusseirat, Ukanda wa Gaza.Picha ya UM/Shareef Sarhan

Huko Mashariki ya Kati, pande zote husika kwenye mzozo huko ukanda wa Gaza zilikubali kusitisha mapigano kwa muda wa siku tatu, lakini jeshi la Israel limedai kwamba kikundi cha Hamas hakijaheshimu makubaliano hayo. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon pamoja na waziri wa Mambo [...]

01/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na viongozi wa Afrika magharibi wajadili mpango wa kudhibiti Ebola

Kusikiliza / Photo: WHO/T. Jasarevic

Wakati ugonjwa wa Ebola ukiendelea kuenea na kusababisha vifo huko Afrika Magharibi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO wanafanya mkutano huko Guinea-Conakry kuzindua mpango wa haraka kudhibiti ugojwa huo uliosababisha vifo vya watu 729 hadi sasa kati ya zaidi ya visa 1300 vilivyoripotiwa. Assumpta Massoi na taarifa kamili. (Taarifa ya Assumpta) Mpango huo [...]

01/08/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wiki ya unyonyeshaji watoto maziwa ya mama yaanza leo, UNICEF yatoa tamko

Kusikiliza / Picha: WHO/SEARO/Anuradha Sarup(UN News Centre)

Leo Agosti Mosi ni mwanzo wa wiki ya unyonyeshaji watoto duniani ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema hiyo ni mojawapo ya njia bora zaidi na rahisi ya kukuza watoto wenye afya na familia thabiti. Maudhui ya mwaka huu yanaoanisha unyonyeshaji na mafanikio ya malengo ya maendeleo ya milenia ya Umoja [...]

01/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukaguzi wa matokeo ya uchaguzi Afghanistan, UNAMA yasifu uwepo wa wataalamu

Kusikiliza / Wapiga kura wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi, Afghanistan.Picha@UNAMA

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umekaribisha hatua ya kuwasili leo kwa waangalizi na wataalamu wa kimataifa nchini humo kabla ya kuanza hapo kesho kwa kazi ya ukaguzi wa matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa tarehe 14 Juni. Mkuu wa UNAMA ambaye ni mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa [...]

01/08/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031