Mwakilishi wa Katibu Mkuu Awasili Nchini CAR

Kusikiliza /

Abdoulaye Bathily @UN Photo/Marco Dormino

Mwakilishi  Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhusu Jamhuri Ya Afrika ya Kati (CAR), Abdoulaye Bathily, aliye pia mwanachama wa kamati ya mapatano ya kimataifa kuhusu mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,  amewasili nchini Bangui- mji mkuu wa nchi hiyo ambapo atashiriki kwa matayarisho ya Kongamano la Brazzaville.

Bwana Bathily ameeleza kuwa lengo la safari yake nchini humo ni kuzikumbusha pande zote husika na wadau wote kwamba Umoja wa mataifa unazingatia umuhimu wa kutafuta suluhu ya mgogoro nchini CAR, na kuongeza kuwa kongamano la Brazzaville ni njia bora ya kuleta pande zote kwenye meza ya mazungumzo ili kuafikiana na kufanya maamuzi ya pamoja ambayo yanalenga kuendeleza maridhiano na amani  ya nchi hiyo.

Vile vile amezishukuru nchi jirani kwa usaidizi na jitihada zao za kujaribu kuleta amani, na akasisitiza  kuwa Umoja wa Mataifa utendelea kusaidia CAR kupitia Ujumbe wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA.

 

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031