Baraza la Usalama lahofia hali Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza /

Mtoto akiwa kambini Tomping Juba, Sudan Kusini. Picha ya UM/Eskinder Debebe

Wanachama wa Baraza la Usalama, ambao leo wamekutana kujadili hali Sudan na Sudan Kusini, wameelezea kusikitishwa na hali ya usalama na kibinadamu katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan, na kuzitaka pande zinazozozana kusitisha uhasama na kuanza mazungumzo ya moja kwa moja bila masharti yoyote.

Baraza hilo pia limezitaka pande zinazozozana kuruhusu ufikishaji wa misaada ya kibinadamu kwa walengwa, kulingana na azimio namba 2046.

Katika taarifa iliyosomwa mbele ya waandishi wa habari na Mwakilishi wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa, wanachama wa Baraza la Usalama pia wameelezea kusikitishwa na kuzorota hali Sudan Kusini, ikiwemo ile ya kibinadamu, ambayo sasa imewaweka watu milioni moja katika hatari ya kukumbwa na janga la njaa

"Wametiwa hofu na habari kuwa pande zote zinasajili wapiganaji na kuagiza silaha, kinyume na makubaliano ya tarehe 10 Juni, na wa tayari kuchukua hatua zifaazo, kwa kushauriana na nchi za ukanda huo, dhidi ya wale ambao hawatatekeleza ahadi zao za amani Sudan Kusini."

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031