Nyumbani » 17/07/2014 Entries posted on “Julai 17th, 2014”

Ban awakutanisha wawakilishi wapya kuhusu Syria na wanahabari

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akutana na Staffan de Mistura(kushoto) na Ramzy Ezzeldin Ramzy katika makao makuu(Picha/UM/Eskinder Debebe/NICA)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amemtambulisha Mwakilishi wake mpya kuhusu Syria, Staffan de Mistura na makamu wake Ramzy Ezzeldin Ramzy kwa waandishi wa habari. Akiwatambulisha wawili hao mjini New York, Bwana Ban ameelezea kubahatika kuweza kuwa na imani na hekima ya wanadiplomasia hao, ambao amesema watasafiri kwenda Syria, nchi za ukanda [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kula wadudu kuepukana na njaa

Kusikiliza / Kuuza wadudu wanoitwa Mopane, Afrika ya Kati. Picha@ FAO

Lengo la kwanza katika malengo ya maendeleo ya milenia ni kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa. Wakati malengo hayo yanafika ukomo mwakani, bado mtu mmoja kati ya wanane ameathirika na njaa duniani. Mashirikia ya kimataifa yamejaribu kubaini suluhu mbadala ili kutimiza mahitaji ya chakula kwa wote. Njia moja isiyo ya kawaida ni kubadilisha milo yetu na [...]

17/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango wawekwa wa hatua za dharura kulinda urithi wa utamaduni wa Iraq

Kusikiliza / Erbill Citadel..yenye umri wa miaka 8000, Iraq. Picha:UNESCO

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limefanya leo mashauriano na wataalam wa utamaduni wa Iraq na wa kimataifa, na kuafikia mpango wa hatua za dharura za kulinda utajiri wa urithi wa kitamaduni wa Iraq. Mpango huo unanuia kupata uungwaji mkono wa wadau wote, yakiwemo mashirika ya kitaifa na kimataifa, wahudumu wa kibinadamu, wachuuzi wa [...]

17/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Djinit amrithi Mary Robinson kama Mjumbe wa Ban wa Maziwa Makuu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon na Said Djinit wa Algeria,  Mjumbe Mteule katika Ukanda wa Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake katika Ukanda wa Maziwa Makuu. Bwana Djinnit anaichukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye amekubali wadhifa mpya aliopewa na Katibu Mkuu kama Mjumbe wake kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa [...]

17/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMA yakaribisha ukaguzi wa matokeo ya uchaguzi wa urais Afghanistan

Kusikiliza / Afghanistan elections3

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umekaribisha kuanza kwa ukaguzi wa matokeo ya kura ya kuwania urais wa mwaka 2014 nchini humo. Ukaguzi huo unafuatia makubaliano yaliyokifikiwa na wagombea wawili wa urais nchini Afghanistan, Dkt. Abdullah Abdullah na Dkt. Ashraf Ghani. Makubaliano hayo yalifikiwa kwa juhudi za Waziri wa Mambo ya Nje Marekani, [...]

17/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNRWA yalaani kuwekwa kwa silaha katika shule Gaza

Kusikiliza / Watoto kutoka Yarmouk. UNRWA/Rami Al-Sayyed

Takriban roketi 20 zimepatikana katika shule iliyo wazi inayosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA. Silaha hizo zilipatikana na maafisa wa UNRWA mnamo Jumanne wakati wa shughuli za kawaida za upelelezi katika majengo yao. Hadi sasa haijabainika ni nani alitega silaha hizo. UNRWA imelaani kitendo hicho katika shule ikiongeza [...]

17/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha usitishaji mapigano kwa sababu za kibinadamu Gaza

Kusikiliza / Robert Serry, Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mashariki ya Kati ziarani Gaza/Picha@ UN Photo/Shareef Sarhan

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha hatua iliyochukuliwa mapema leo na Israel kusitisha mapigano kwa muda wa saa tano ili kuruhusu shughuli za kibinadamu kwa raia wa Gaza, zikiwemo usambazaji misaada na kufanyia ukarabati miundo mbinu muhimu kama umeme na maji. Usitishaji mapigano huo uliotokana na juhudi za upatanishi za Mratibu [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Libya ni ya kutia hofu, asema Mitri

Kusikiliza / Tarek Mitri, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya. UN Photo/Devra Berkowitz

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili kuhusu Lybia na kazi za Ujumbe wa Umoja wa Matiafa nchini humo, UNSMIL. Tarek Mitri, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNSMIL, amewaambia wanachama wa baraza hilo kwamba raia wa Lybia wanazidi kutiwa hofu kadri mzozo unavyoendelea kuongezeka Lybia. " Kasi ya mabadiliko [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo Afrika yamulikwa kwenye Baraza Kuu

Kusikiliza / Kikao cha Baraza Kuu Picha/UM

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya mdahalo kuhusu kuendeleza kwa uwekezaji barani Afrika na mchango wake katika kufikia malengo ya maendeleo ya bara la Afrika, yakiwemo kutokomeza umaskini na kufikia ukuaji na maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi. Akizungumza wakati wa mdhahalo huo, rais wa Baraza Kuu John W. Ashe, amesema kuwa katika [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zakumbushwa kuhusu wajibu wa kulinda sheria ya kimataifa

Kusikiliza / Sang-Hyun-Song, Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.
UN Photo/Paulo Filgueiras

Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Sang Hyun Song, ameziomba nchi zote duniani zishirikiane kupambana na ukwepaji wa sheria, ikiwa leo ni siku ya sheria ya kimataifa duniani. Taarifa kamili na Amina Hassan. Raisi Sang Hyun Song amekumbusha kwamba, tarehe 17, Julai, mwaka 1998, nchi 120 zilitia saini kwenye maktaba wa Roma uliounda [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufadhili zaidi unahitajika kuwahudumia wakimbizi waSudan Kusini walioko Uganda:WFP

Kusikiliza / Wakimbzi kutoka Sudan kusini wawasili Uganda Picha/WFP/Tine Frank

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limepaza sauti likiomba msaada zaidi ili liweze kushughulikia wakimbizi wanaoendelea kumiminika Kaskazini mwa Uganda kutoka Sudan Kusini. Taarifa kamili na John Kibego wa Redio washirika ya Spice FM, nchini  Uganda.  (Tarifa ya Johhn Kibego)  Shirika la WFP linaomba kupigwa jeki zaidi wakati ripoti ya Shirika la Umoja wa [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031