Nyumbani » 16/07/2014 Entries posted on “Julai 16th, 2014”

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Awasili Nchini CAR

Kusikiliza / Abdoulaye Bathily @UN Photo/Marco Dormino

Mwakilishi  Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhusu Jamhuri Ya Afrika ya Kati (CAR), Abdoulaye Bathily, aliye pia mwanachama wa kamati ya mapatano ya kimataifa kuhusu mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,  amewasili nchini Bangui- mji mkuu wa nchi hiyo ambapo atashiriki kwa matayarisho ya Kongamano la Brazzaville. Bwana Bathily ameeleza kuwa [...]

16/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini ya amani CAR: Ladsous

Kusikiliza / Hervé Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani
Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatano ya Julai 16 jioni limejadili kuhusu hali ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati likiangazia maandalizi ya kuunda ujumbe wa umoja wa mataifa nchini humo, MINUSCA. Herve Ladsous, mkuu wa idara ya operesheni za kulinda amani kwenye Umoja wa Mataifa, DPKO, amesema kwamba kuna matumaini ya [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki Moon akutana na rais wa Haiti na Jamhuri ya Dominika

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akihutubia Seneti ya Jamhuri ya Dominika. UN Photo/Paulo Filgueiras

Akihitimisha ziara yake nchini Haiti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekutana na rais wa nchi hiyo, Bwana Logan Martelly akiwapongeza raia wa Haiti kwa bidii yao katika kujenga upya nchi baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoathiri nchi yao mwaka 2010, na licha ya hali mbaya ya kiuchumi. Amesifu serikali ya [...]

16/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu dhoofu kwa maelfu Sudan na Sudan Kusini: Amos

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA Valerie Amos.(Picha@UN Photo/Eskinder Debebe)

Mkuu wa Ofisi ya kuratibu masuala ya kibidamu na misaada ya dharura, Valerie Amos, amesema kuwa hali ya kibinadamu katika nchi za Sudan na Sudan Kusini, inaendelea kuzorota kwa mamia ya maelfu ya watu. Bi Amos, ambaye awali amelihutubia Baraza la Usalama, amewambia waandishi wa habari mjini New York kuwa mamia ya maelfu ya watu [...]

16/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lahofia hali Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza / Mtoto akiwa kambini Tomping Juba, Sudan Kusini. Picha ya UM/Eskinder Debebe

Wanachama wa Baraza la Usalama, ambao leo wamekutana kujadili hali Sudan na Sudan Kusini, wameelezea kusikitishwa na hali ya usalama na kibinadamu katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan, na kuzitaka pande zinazozozana kusitisha uhasama na kuanza mazungumzo ya moja kwa moja bila masharti yoyote. Baraza hilo pia limezitaka pande zinazozozana kuruhusu [...]

16/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Afghanistan

Kusikiliza / Kikao cha baraza la usalama wakati mkutano kujadili hali nchini Afghanistan. Picha/UM/Amanda Voisard

Baraza la Usalama limelaani vikali leo shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea tarehe 15 Julai, maeneo ya Paktika, nchini Afghanistan pamoja na mashambulizi yaliyotokea mjini Kabul, ambayo yalidaiwa na kundi la Wataliban. Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wananchi wengi wakiwemo watoto. Baraza la Usalama limepeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga, raia na serikali ya Afghanistan. [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNIDO yatoa ripoti ya takwimu kuhusu uchimbaji migodi

Kusikiliza / Mashine ya uchimbaji (Picha@UNIDO)

Uzalishaji wa kimataifa kutokana na shughuli za uchimbaji migodi na sekta ya utoaji huduma ulipanda kwa kiwango kidogo cha asilimia 1.7, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO. Ripoti hiyo ya takwimu za kimataifa kuhusu uchimbaji migodi na huduma huchapishwa kila miaka miwili, na hutoa takwimu [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ya binadamu ya faragha ni lazima ilindwe popote

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay(Picha ya UM)

Ufuatiliaji unaofanywa dhidi ya watu na serikali na kampuni kubwa za biashara bila idhini ya watu binafsi, ni ukiukwaji wa haki zao, ikiwemo haki ya kuwa na faragha, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na Amina Hassan Ripoti hiyo yenye kichwa, "haki ya [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 19 kati ya milioni 35 hawajui kama wana virusi vya HIV:UNAIDS

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé,@UNAIDS

Ripoti mpya ya Shirika linalohusika na HIV na Ukimwi, UNAIDS, imeonyesha kuwa takriban watu milioni 19 kati ya watu wapatao milioni 35 wanaoishi na virusi vya HIV kote duniani, hawajui kama wana virusi hivyo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé, juhudi zinapaswa kuongezwa kwa njia bora zaidi ili kuondoa tofauti baina ya [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 982 zahitajika kutimiza mahitaji ya kibinadamu Sudan

Kusikiliza / Watoto hawa wacheza katika kituo cha jamii kilichojengwa na UNAMID katika kambi ya wakimbizi wa ndani , Khor Abeche, kusini Darfur (Picha/UM/Albert González Farran/NICA)

Kuwepo kwa ongezeko kubwa la mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan katika kipindi cha miezi sita ya mwaka huu kumelazimu kupitiwa upya mpango wa misaada ya dharura iliyowekwa hapo awali. Taarifa kamili na John Ronoh. (Taarifa ya John Ronoh) Mashirika ya misaada kwa ajili ya Sudan yanasema kuwa kiasi cha dola za Marekani milioni 982 kinahitajika [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930