Nyumbani » 15/07/2014 Entries posted on “Julai 15th, 2014”

Idadi ya maambukizi ya kipindupindu yapungua Haiti

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkewe atembelea familia Los Palmas Picha ya UM/Paulo Filgueiras

Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti inaendelea kupungua lakini matatizo ya maji safi na usafi wa mazingira yanaathiri kasi ya maendeleo, na kusababisha ongezeko la magonjwa yatokanayo na maji , amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa. Bwana Ban aliwasili katika Kisiwa hicho cha Karibea hapo Jumatau katika ziara yake ya kuchagiza [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNFPA yasaidia kupaza sauti ya mkunga Tanzania

Kusikiliza / Elvina-Mkunga Tanzania. Picha@UNFPA

Uimarishaji wa afya ya uzazi ni lengo nambari tano katika malengo ya milenia ambayo yatafikia ukomo mwakani. Ili kutimiza lengo hili ni muhimu kuhakikisha kwamba watoa huduma wana vifaa vinavyohitajika na kwamba idadi ya watoa huduma, kama vile wakunga, inakwenda sambamba na walio na mahitaji. Katika nchi zinazoendelea, bado lengo hili haliijafikiwa kikamilifu kwa sababu [...]

15/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani mashambulizi mjini Kabul

Kusikiliza / Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA Ján Kubiš Picha ya Fardin Waezi / UNAMA

Umoja wa mataifa umelaani shambulizi la kujitoa mhanga lililosababisha vifo vya watu 43 wakiwemo watoto 8 Idadi ya vifo kutokana na shambulizi hilo ambalo lilifanyika katika soko la Urgun jimbo la Paktika kusini mashariki mwa Afghanistan, imelifanya kuwa baya zaidi mwaka huu wa 2014, ambapo raia 67 pia wamejeruhiwa. Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa [...]

15/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Madawa ya kulevya yanaathiri ukuaji wa uchumi na maendeleo

Kusikiliza / UNODC_DRUGS

Biashara haramu ya madawa na mashirika ya uhalifu yanaathiri maisha ya watu na jamii kwa ujumla, amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  katika ujumbe wake maalum alioutuma kwenye mkutano wa viongozi kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani.  Mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, [...]

15/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yafungua kituo cha ukanda kuratibu shughuli za kupambana na Ebola

Kusikiliza / Harakati za kudhibiti Ebola nchini Guinea-Conakry. Picha @WHO

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza leo tarehe 15 Julai kufunguliwa kwa kituo cha ukanda ambacho kitaratibu shughuli zote za kupambana na mlipuko wa Ebola. Takwimu zilizotolewa na shirika hilo leo zinaonyesha kwamba idadi ya watu walioathirika na Ebola inakaribia kufikia elfu moja, huku watu mia 600 kutoka nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone [...]

15/07/2014 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ziarani Nigeria, Malala ataka wasichana wa Chibok waachiliwe

Kusikiliza / Malala Yousafzai Picha ya UM/faili

Malala Yousafzai, mtoto wa Kipakistani aliyenusurika kifo aliposhambuliwa na wanamgambo wa Taliban wanaopinga elimu ya watoto wa kike, amelitaka kundi la kigaidi la Boko Haram kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara kutoka shule ya Chibok, kaskazini mwaNigeria. Malala ambaye yupo ziarani nchiniNigeria, alikutana hapo jana na wazazi wa wasichana hao, wawakilishi wa mashirika ya umma na [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ziarani Haiti

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa Los Palmas atembelea familia na kituo cha maji Picha ya/Paulo Filgueiras/NICA ID:594793

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ambaye yupo ziaraniHaiti, leo anatarajiwa kukutana na timu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSTAH. Hii leo pia Bwana Ban anatarajiwa kuzindua rasmi kituo cha michezo kiitwacho  "Michezo kwa Tumaini"nchini humo, akishirikiana na  rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bacth. Hapo jana [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unene uliokithiri utotoni linazidi kuwa tatizo la afya duniani

Kusikiliza / Nembo ya WHO

Uzito wa kupindukia miongoni mwa watoto linakuwa tatizo la afya ya umma katika nchi nyingi zinazoendelea, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. WHO imesema idadi ya watoto wenye unene wa kupindukia kote duniani imeongezeka kutoka milioni 31 mwaka 1990 hadi milioni 44 wakati huu, huku nchi zinazoendelea zikishuhudia kiwango cha ongezeko kilicho asilimia [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yaomba kusitishwa kwa mauaji ya raia Gaza

Kusikiliza / Kufuatia mzozo UNRWA imetangaza hali ya dahrura katika maeneo matano ya ukanda wa Gaza(Picha@UNRWA)

Kuna uwezekano wa maafa na uharibifu zaidi Gaza iwapo juhudi za kusitisha mzozo kati ya Israeli na Palestina hazitafaulu. Hiyo ni kauli ya Shirika la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA, ambalo limesema kwamba kufikia sasa Wapalestina 174 wameuwawa na zaidi ya 1,100 kujeruhiwa tangu Israeli ilipoanza mashambulizi Gaza. Akiwahutubia waandishi wa habari msemaji wa UNRWA, [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 10 Yemen waathirika na njaa

Kusikiliza / Yemen. Picha@OCHA/Eman Al-Awami(UN News Centre)

Utafiti uliofanyika nchini Yemen na Shirika la Mpango wa chakula Duniani WFP na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Watoto UNICEF, unaonyesha kwamba bado watu milioni 10, yaani asilimia 40 ya watu waliopo Yemen, wanakumbwa na ukosefu wa usalama wa chakula.  Taarifa Zaidi na Priscilla Lecomte Kwa mujibu wa WFP, katika watu hawa, ni [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031