Nyumbani » 14/07/2014 Entries posted on “Julai 14th, 2014”

Ban amteua Agostinho Zacarias wa Musumbiji kuwa Naibu Mratibu wa UM Burundi

Kusikiliza / Agostinho Zacarias, picha ya UNDP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo amemteua Bwana Agostinho Zacarias kuwa Naibu Mratibu Maalum kwa Muda, na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi. Bwana Zacarias pia atachukua wadhifa wa Mratibu Mkaazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini humo akichukua nafasi ya Bi. Rosine [...]

14/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Matumaini mapya kwenye vita dhidi ya ukatili wa kijinsia DRC

Kusikiliza / Wanawake wakikaa pamoja nje ya Heal Africa Transit Centre ya wahanga wa ukatili wa kingono. Picha@Aubrey Graham/IRIN

Jeannine Mabunda Lioko Mudiayi ameteuliwa leo na raisi Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kuwa Mshauri wa Raisi kuhusu Ukatili wa Kingono na utumikishwaji wa Watoto. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika vita, Zainab Hawa Bangura pamoja na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu [...]

14/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wavuvi waokolewa na maisha ya deni, India

Kusikiliza / wavuvi wadogo wadogo kwenye eneo la tamil Nadu - India

Wakati malengo ya maendelo ya milenia yanatarajia kufikia ukomo mwakani, Umoja wa Mataifa umezindua ripoti kuhusu mafanikio yaliyopatikana. Lengo la kwanza likiwa ni kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa, na kupunguza kwa nusu idadi ya watu maskini ifikapo mwaka 2015, takwimu zinaonyesha kwamba lengo hili limetimia. Nchini India, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD [...]

14/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa kuongeza vigezo vya biashara ya viungo vya pilipili

Kusikiliza / Viungo. Picha@FAO/Daniel Beaumont

Viungo kama pilipili manga, oregano ama majani ya chai vina hatari ya kuambukizwa na vidudu mbali mbali, kwa mujibu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusu vigezo vya vyakula, Codex Alimentarius.  Majukumu ya Kamati hiyo ambayo imeundwa na Shirika la Chakula na Kilimo FAO na Shirika la Afya Duniani WHO ni kulinda afya ya watumiaji [...]

14/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sitisha mapigano kwanza Gaza kuokoa maisha ya wananchi: UNOCHA

Kusikiliza / Mkaazi wa Palestina akipita mbele ya askari wa Israeli mashariki mwa Jerusalem. Picha: IRIN/Andreas Hackl(UN News Centre)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, James Rawley, amesema kwamba amesikitishwa na mapigano ya wiki hii ambayo yamewaathiri zaidi wananchi wa kawaida wa Ukanda wa Gaza. Rawley amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea shule iliyopigwa bomu kwenye ukanda huo, akiandamana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuwasaidia Wakimbizi [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha azimio la Baraza la Usalama kuhusu Syria

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq Picha@UM

Akizungumza baada ya kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama kuhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema katibu mkuu wa umoja wa mataifa amekaribisha azimio hilo ambalo litawezesha mashirika ya umoja wa mataifa kufikisha misaada kwa walengwa nchini humo kwa njia ya moja kwa moja zaidi. [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Mary Robinson kuwa Mjumbe Maluum wa mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Bi Mary Robinson Picha@UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametangaza kumteua Bi Mary Robinson wa Ireland kuwa Mjumbe wake Maalum kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Bi Robinson ataendelea kuhudumu kama rais wa wakfu wake wa Climate Justice. Kutokana na uzoefu katika kazi ya wakfu wake, Bi Robinson anatarajiwa kusisitiza mtazamo unaowajali watu katika mikakati inayojikita kwa [...]

14/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laazimia kuanzisha utaratibu wa ukaguzi wa misaada ya kibinadamu Syria

Kusikiliza / Kikao cha baraza la Usalma @NICA

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja wamepitisha azimio la kuanzishwa kwa utaratibu wa ukaguzi wa shughuli za upakiaji, usafirishaji na upekuzi wa shehena zote za misaada ya kibinadamu ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake kwa ajili ya raia wa Syria.   Akitangaza matokeo ya kura [...]

14/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ITU na UN Women watangaza tuzo mpya ya teknolojia na usawa wa jinsia

Kusikiliza / ITU

Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU na lile la masuala ya wanawake, UN Women, kwa pamoja yametangaza kuanzisha tuzo mpya ya kimataifa kwa ajili ya kutambua juhudi bora  zaidi katika kutumia teknolojia ya mawasiliano (ICT) kuendeleza usawa wa jinsia. Tuzo ya GEM-TECH, itawatambua viongozi na mashirika yanayotumia uwezo wa teknolojia kuleta mabadiliko. Tuzo hiyo itatolewa [...]

14/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMA yakaribisha kundi la marekebisho na Ubia wa Uchaguzi Afghanistan.

Kusikiliza / Picha: UNAMA News Centre

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umekaribisha makubaliano yaliyokifikiwa na wagombea waliwili wa urais nchini Afghanistan, Dkt. Abdullah Abdullah na Dkt. Ashraf Ghani kwa ajili ya kutafuta suluhu kwa mkwamo uliotokea baada ya uchaguzi na hivyo kuruhusu timu ya marekebisho na ubia kurejea na kushughulikia utaratibu wa uchaguzi nchini humo. Makubaliano hayo yalifikiwa [...]

14/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na mapigano ya Gaza

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@UN Photo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa bado anaingiwa na woga kuhusiana na hali ya mambo katika eneo la Gaza ambako amesema kuwa pamoja na mwongozo uliotolewa na Baraza la Usalama lililotaka usitishwaji mapigano, lakini hali imeendelea kuwa mbaya na siyo tu kwa raia wa Palestina lakini pia kwaWaisrael. Katika taarifa yake [...]

14/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Saudia Arabia yatoa taarifa kuhusu maambukizi ya kirusi corona

Kusikiliza / Hospitalini, Saudi Arabia @WHO

Saudia Arabia imetoa taarifa kuelezea mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona ambavyo tayari vimeua watu kadhaa na wengine wakiendelea kupata matibabu. Taarifa iliyotolewa na kitengo kilichowekwa maalumu kwa ajili ya kufuatilia hali ya ugonjwa huo imeonyesha kuwa kuanzia tarehe 3 Julai hadi tarehe 10 Julai, jumla ya wagonjwa 7 zaidi walithibitika kuambukizwa virusi vya [...]

14/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wabunge wa Israel na Palestina wana jukumu la kukomesha mashambulizi na kulinda raia: IPU

Kusikiliza / mnembo wa IPU @IPU

Shirika la Muungano wa Wabunge, IPU, limetoa wito kwa pande zote katika mzozo wa Israel na Palestina kukomesha mashambulizi yao ya angani na roketi mara moja na kuzuia mauaji zaidi ya raia. Taarifa kamili na John Ronoh. Taarifa ya John Ronoh IPU imetoa wito pia kwa wabunge wa Israel na Palestina kuchukua hatua zozote zinazohitajika [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu ziarani Haiti

Kusikiliza / Upatikanaji wa maji safi. Picha: MINUSTAH

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon leo ameanza ziara yake kwenye nchi za Haiti na Jamhuri ya Dominika, ambapo atakutana na viongozi wa nchi hizo mbili na kutathmini miradi iliyotekelezwa huko kutokomeza umaskini. Nchini Haiti, atazindua pia kampeni kubwa ya usafi vijijini pamoja na Waziri Mkuu Laurent Lamothe, akizungumza pia na jamii [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM yaomba ufadhili zaidi kuwasaidia wakimbizi wa Syria Lebanon

Kusikiliza / Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Lebanon inaongezeka kwa kasi zaidi ya uwezo wa jamii ya kimataifa kuchangia fedha za kukidhi mahitaji yao yanayoongezeka, amesema Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Ross Mountain. Bwana Mountain amesema wakimbizi wapya wa Syria wapatao 12,000 wanaingia Lebanon kila wiki, huku idadi nzima ikitarajiwa kufikia milioni 1.5 [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yawasikitikia watoto wanaoathirika na mapigano Gaza

Kusikiliza / Watoto wawili wakisimama mbele ya nyumba ambayo polisi imesema imepigwa bomu la anga na Israel kwenye kambi la wakimbizi la Maghazi katikati mwa Ukanda wa Gaza. UN Photo/Shareef Sarhan

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF Anthony Lake amesema mapigano yanayoendelea huko Gaza yamegeuza maisha ya watoto kua magumu huku kiasi cha 33 wakiwa wamepoteza maisha katika siku za hivi karibuni kutokana na mapigano hayo. Taarifa kamili na George Njogopa Taarifa ya George Mkurugenzi huyo ambaye amesisitiza kuwa hakuna [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na machafuko Libya

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-moon, ameelezea kusikitishwa mno na ongezeko la machafuko katika mji mkuu waLibya,Tripoli, na madhara ya mapigano ya hivi karibuni kwa raia.Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa Amina) Ban ametoa wito kwa pande zinazokinzana kuepukana na kutumia machafuko kama njia ya kufikia malengoyaoya kisiasa. Ban amesema anaamini kuwa vitendo [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031