Nyumbani » 11/07/2014 Entries posted on “Julai 11th, 2014”

Mtandao wa wanahabari watoto Tanzania wafika Afrika ya Kusini kwa ajili ya afya ya wakina mama

Kusikiliza / Picha@UNICEF

Nchini Afrika Kusini, mashirika ya kimataifa na wadau mbali mbali wa misaada ya kijamii na ya kibinadamu wamekutana kwa ajili ya kongamano la tatu kuhusu afya ya akina mama, watoto na watoto wachanga. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuimarisha afya ya walio kwenye mazingira magumu zaidi, yaani akina mama na watoto na kuhakikisha kwamba [...]

11/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Ulaya zaombwa kuwasaidia wasaka hifadhi wa Syria

Kusikiliza / Picha: UNHCR/L. Addario

Nchi za bara Ulaya zimehimizwa kufungua milango kwa wakimbizi wa Syria na kuwapa utaratibu sahihi wanaosaka hifadhi.  Wito huo umetolewa na Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani, UNHCR wakati wa uzinduzi wa ripoti kuhusu hali ya wakimbizi wa Syria walioko Ulaya. UNHCR imeyaomba mataifa hayo kuwapokea vilivyo na kuwalinda wakimbizi hao wanaokimbia mzozo nchini Syria. Shirika hilo [...]

11/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yaendelea kufuatilia mkurupuko wa Ebola Afrika Magharibi

Kusikiliza / Muuguzi akimuhudumia mgonjwa mwenye virusi vya Ebola. WHO/Chris Black

Shirika la afya duniani WHO, linajitahidi kufuatilia kwa makini hali ya mlipuko wa virusi vya Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone. Nchini Guinea, kuenea kwa virusi kumepungua kwa kiasi kikubwa, na kisa kimoja tu kimeripotiwa kwa siku 7 zilizopita. WHO inaendelea kufuatilia hali kwa makini hasa ikilenga jamii ambazo zilikuwa zimepuuza mapendekezo [...]

11/07/2014 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP inatumia simu za mkononi kuwasiliana na wakimbizi kambini

Kusikiliza / Agnes Niyanzira @WFP

Tatizo la njaa linasalia kuwa changamoto kubwa katika nchi nyingi, hususan katika nchi kunakoshuhudiwa ghasia. Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kunaendeshwa mradi wa utafiti wa usalama wa chakula kupitia simu za rununu miongoni mwa wakimbizi, ukiendeshwa na Shirika la chakula duniani WFP. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo inayoangazia mama mkimbizi katika [...]

11/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahitaji ya kibinadamu yazidi kufurika Gaza

Kusikiliza / Hali ya uhai kutokana na vizingiti yanazidi kufifia Gaza na Ukanda wa Magharibi. Picha@ Shareef Sarhan/UNRWA

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, imesema kuwa inasikitishwa na ongezeko la mahitaji ya dharura ya kibinadamu Gaza kufuatia kuanza kwa operesheni za kijeshi za Israel mnamo Julai 7, ambazo zimeelezwa kuwa na lengo la kukomesha mashambulizi ya roketi kutoka Gaza. OCHA imesema kuwa, mbali na mauaji na majeraha mengi [...]

11/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waasi wa Afrika ya Kati wanajihusisha na biashara za madini

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakati wa kikao Picha UM/Evan Schneider/NICA

Baraza la Usalama leo limejadili hali Jamhuri ya Afrika ya Kati na ripoti kutoka kamati ya vikwazo dhidi ya watekelezaji wa uhalifu nchini humo. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte Vikwazo vinatarajiwa kuwekwa ili kuzuia baadhi ya waasi kusafiri nje ya nchi, kama njia moja ya kutia shinikizo juu ya pande zote za mzozo, ndivyo alivyoeleza [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasaidia wakimbizi wa Nigeria nchini Cameroon

Kusikiliza / Wakimbizi wanaokimbia ukatili wa Boko Haram katika taifa la  Borno, Nigeria. Picha: IRIN/Anna Jefferys(UN News Centre)

Kufuatia machafuko yanayoendela kaskazini mwa Nigeria, raia wengi wamekimbia na kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Cameroon ambapo Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP linawapa usaidizi, licha ya mazingira yasiyo salama na matatizo ya usafiri. Elizabeth Brys ambaye ni Msemaji wa WFP ameeleza kwamba hii ni mara ya kwanza kwa WFP kutoa usaidizi karibu [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatolea wito ufadhili zaidi wakati tatizo la wakimbizi wa Sudan Kusini likiongezeka

Kusikiliza / Kundi la wakimbizi wa ndani wakiwemo wanawake na watoto wakipumzika katika eneo la Ethiopia baada ya kuvuka mto wa Baro kutoka Sudan ya Kusini. Picha: UNHCR/L.F.Godinho(UN News Center)

Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR na wadau wanaokabiliana na tatizo la wakimbizi kufuatia kuzorota usalama Sudan Kusini wametoa ombi jipya la dola milioni 658 ili kusaidia wakimbizi takriban 715,000 mwishoni mwa mwaka huu wa 2014. Taarifa kamili na John Ronoh.(Taarifa ya Ronoh) Mzozo huo unaoshuhudiwa na hali mbaya ya kibinadamu katika [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya idadi ya watu yamulika vijana milioni 1.8 waliopo duniani

Kusikiliza / UNFPA/Idriss Qarqouri (NICA ID:587729)

  Leo tarehe 11 Julai ikiwa ni siku ya idadi ya watu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewaomba viongozi wote duniani kuwekeza katika hatma ya vijana, akisema vijana milioni 1.8 waliopo duniani, hasa katika nchi zinazoendelea, wana nguvu za kupambana na changamoto zinazokumba ulimwengu, lakini bado wananyimwa fursa ya kupta [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za Binadamu yasikitishwa na mauaji ya raia Gaza na Israel

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu. Picha: UN Multimedia

  Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, leo imeelezea kusikitishwa na operesheni za kijeshi za Israel, ambazo zimesababisha mauaji ya raia Ukanda wa Gaza, na pia makombora yanayorushwa kiholela kutoka Gaza kwenda Israel. Kufikia Alhamis mchana, Wapalestina wapatao 88, wakiwemo watoto 21 na wanawake 11, walikuwa wameuawa Gaza kutokana na mashambulizi ya [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031