Nyumbani » 10/07/2014 Entries posted on “Julai 10th, 2014”

Ban amteua De Mistura kuwa mjumbe maalum kwa Syria

Kusikiliza / Katibu mkuu Ban Ki-moon na Staffan de Mistura. UN Photo/Rick Bajornas

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua leo Bwana Staffan de Mistura kuwa mjumbe wake maalum kwa ajili ya kutafuta makubaliano ya amani kwenye mzozo waSyria. Bwana de Mistura, ambaye aliwahi kuongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchiniIraqnaAfghanistan, anachukua nafasi ya Lakhdar Brahimi, ambaye alijiuzulu mwezi Mei. De Mistura aliwahi kuwa Naibu [...]

10/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM Lebanon atembelea wakimbizi wa Syria na wenyeji wao

Kusikiliza / Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Mratibu wa Huduma za kibinadamu nchini Lebanon Bwana Ross Mountain ametembelea maeneo ya Hermel na Arsal jijini Beirut ili kutathmini hali ya wakimbizi wa Syria na jamii za Lebanon zinazowapa hifadhi. Kuna raia wa Syria zaidi ya 376,000 ambao wamejiandikisha na Shirika la Kuhudimia Wakimbizi- UNHCR katika maeneo hayo. Bwana Mountain alikutana na viongozi wa [...]

10/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ziarani, Mia Farrow asisitiza haja ya kusaidia watoto wa CAR

Kusikiliza / Picha@UNICEF/Central African Republic/2013/Menezes

Mia Farrow, mcheza filamu maashuhuri, mwanaharakati na balozi mwema wa UNICEF amekamilisha ziara yake ya nne nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambko amejionea madhara ya ukatili uliokithiri, na pia kukutana na watu na kuwasikiliza wasimulia hadithi za ujasiri wa kutia moyo. Akiwa mji wa Boda, yapata mwendo wa saa nne barabarani kutoka mji mkuu [...]

10/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Chapisho la biashara la kimataifa laidhinishwa: UNCITRAL

Kusikiliza / Nembo ya UM

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya sheria zinazohusika na biashara za kimataifa imeidhinisha chapisho linalohusu mkataba unaozingatia uwazi baina ya wawekezaji na serikali. Mkataba huo ambao unatoa hali ya uwazi kwa pande zote iliratibiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 unatoa mwongozo pindi panapohusika mashauri yanayohusu migogoro ya uwekezaji baina ya mwekezaji na dola. [...]

10/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua za kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza hazitoshi: WHO

Kusikiliza / Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Margaret Chan(kwenye jukwaa) akihutubia 67th World Health Assembly. Picha:WHO/Martin

Hatua za kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza zimetajwa kuwa zisizotosha na pia hazionyeshi usawa, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Afya Duniani, WHO.  Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama vile magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na ugonjwa wa mapafu. Ripoti hiyo mpya ya WHO inamulika hali ilivyo sasa katika nchi 194. Daniel [...]

10/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Miradi endelevu yazuia taka na uchafu kwenye Kombe la Dunia Brazil: UNEP

Kusikiliza / UNEP

Miji nchini Brazil imekuwa ikitekeleza miradi kadhaa ya mazingira endelevu wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu 2014,kamavile kutoa vibali vya kutimiza viwango vya kulinda mazingira kwa nyanja za kuchezewa mpira na kulipa fidia kwa uvushaji wa gesi chafuzi kutokana na shughuli za Kombe la Dunia.  Miradi mingine iliyoidhinishwa na Mpango wa Brazil [...]

10/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto hatarini kuathiriwa vibaya na ghasia Ukanda wa Gaza na Israel: UNICEF

Kusikiliza / Msichana huyu kutoka Palestina analia baada ya nyumba yao kuharibiwa eneo la Khan Yunis, Gaza  Picha ya © UNICEF / Eyad El Baba

Kuongezeka machafuko Gaza na Israel kunatishia kuwadhuru watoto kwa kiwango kikubwa kwenye pande zote za mzozo, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, ambalo limerejelea ujumbe wa Katibu Mkuu wa kuziomba pande zote kujizuia na kuwalinda watoto. Tayari, katika siku tatu zilizopita watoto wapatao 19 wa Kipalestina wameripotiwa kuuawa katika [...]

10/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nusu ya watu duniani sasa wanaishi mijini: UM

Kusikiliza / Mji wa Dhaka, Bangladesh Picha ya UM/Kibae Park

Asilimia 54 ya watu kote duniani sasa wanaishi mijini, na kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 66 ifikapo mwaka 2050. Hayo yamedhihirika katika ripoti mya ya makadirio ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukuaji wa miji duniani, ambayo imezinduliwa leo mjini New York na idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa. Makadirio [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

OCHA: watu 300 wameshajeruhiwa Gaza

Kusikiliza / mtoto Palestina UNICEFPalestine

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, leo imetoa ripoti kuhusu hali ya usalama na ya kibinadamu katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi. Shirika hilo, limesema, tangu mwanzo wa operesheni za Israel kupiga mabomu dhidi ya maeneo hayo, zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na 300 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto, watu 900  wakilazimika kuhama [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya yatolewa kuhusu kuzuia malaria na afya ya mama na watoto

Kusikiliza / Roll back Malaria(RBM)Picha ya Benjamin Schilling/PSI

Ripoti mpya inayoonyesha faida za kupambana na malaria kwa afya ya akina mama na watoto imezinduliwa leo kwenye hafla maalum kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, daktari Erik Mouzin kutoka Ushirikiano wa Kutokomeza Malaria, ameeleza faida hizo akisema: " nadhani kwamba watu wamepata habari [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mafunzo Liberia kama njia ya kukabiliana na Ebola

Kusikiliza / WHO/Christina Banluta

Viongozi wa jamii katika wilaya tatu nchini Liberia Montserrado, Margibi, na Lofab wanapokea mafunzo kuhusu virusi vya Ebola, kama sehemu ya juhudi za Shirika la afya duniani WHO na wizara ya afya ya jamii katika kuhamasisha kuhusu ugonjwa huo, jinsi gani unaambukizwa na mchango wa umma katika kukabiliana na ugonjwa huo. Taarifa kamili na Grace [...]

10/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Saudi Arabia yashutumiwa kwa kuwafunga watetezi wa haki za binadamu

Kusikiliza / Navi Pillay, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Binadamu. Picha: UN Photo/Paulo Filguerias

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imeishutumu vikali serikali ya Saudia, ambayo inadaiwa kuendesha vitendo vya ukiukwaji wa haki binadamu, vikiwemo kuwakamata na kuwatesa baadhi ya watu wanaotetea haki za binadamu. George Njogopa ana taarifa kamili Taarifa ya George Shutuma hizo zinakuja katika wakati ambapo kukitolewa hukumu kwa mwanaharakati mmoja aliyehukumiwa [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika hali tete ya Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali Mashariki ya Kati na suala la Palestina, likimulika zaidi hali ya machafuko ambayo sasa yametanda eneo la Gaza. Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina) Wakati wa kikao cha leo, Baraza la Usalama limemsikiliza kwanza Katibu Mkuu Ban Ki-moon, ambaye amesema kwamba hivi [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031