Nyumbani » 09/07/2014 Entries posted on “Julai 9th, 2014”

UNHCR yahamishia wakimbizi wa Syria kwa kambi mpya nchini Iraq.

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria wakiingia mkoa wa Kurdistan nchini Iraq. Picha@UNHCR/G.Gubaeva

Licha ya nchi ya Iraq kuwa na wakimbizi wa ndani kwa ajili ya mapigano katika nchi hiyo, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi , UNHCR, linaendelea kusaidia wakimbizi kutoka Syria waliohamia Iraq baada ya machafuko nchini mwao. UNHCR imefungua Kambi ya kudumu katika mkoa wa Kurdistan ulio kaskazini mwa Iraq, ili kuhudumia wakimbizi zaidi ya 225,000 kutoka [...]

09/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mapigano mengine yasababisha wakimbizi wa ndani kuongezeka Yemen

Kusikiliza / Karibu watu milioni 15 Yemeni, kama familia hii, wanahijati msaada wa kibinaadamu mwaka. OCHA/Eman al Awami.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Yemen, Johannes Van der Klaauw ameeleza wasiwasi wake juu ya usalama wa wananchi waliomo katikati ya mapigano kaskazini mwa nchi hiyo. Zaidi ya wananchi 200 wameripotiwa kuuawa, wakiwemo wanawake na watoto, na wengine maelfu wametegwa katikati ya eneo la mapigano, mjini Amran, wakishindwa kukimbia. Mapigano yalisimamishwa kwenye eneo hilo [...]

09/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia hali inayotia shaka Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema kuwa amesikitishwa na wimbi jipya la machafuko ambalo limeughubika Ukanda wa Gaza, kusini mwa Israel na Ukingo wa Magharibi.   Akikutana na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo mjini New York, Ban amesema kuwa huu ni wakati wa mtihani mgumu zaidi [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi ya wananchi ndani ya kanisa

Kusikiliza / Mashambulizi yaliyotokea leo @MINUSCA VIDEO

Ujumbe wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, umelaani mashambulizi ya kikatili dhidi ya wakimbizi wa ndani yaliyotokea tarehe saba Julai ndani ya kanisa kuu la dayosisi ya Saint Joseph na kwenye makao ya askofu, mjini Bambari. Kwa mujibu wa waandishi wa habari, zaidi ya watu elfu sita walikuwa wametafuta hifadhi ndani [...]

09/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laiomba Lebanon kuchagua rais mpya haraka

Kusikiliza / Dereck Plumbly, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon akizungunza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Usalama

Baraza la Usalama likikutana leo tarehe 9, Julai, kujadili hali ya nchi ya Lebanon, limeipongeza nchi hiyo kwa jitahada zake katika kulinda amani iliyopo sasa kwa kipindi cha miezi minne, na kuiomba pia lizibe pengo la kiti cha uraisi haraka iwezekanavyo. Dereck Plumby, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, ameripoti kuhusu hali ya usalama [...]

09/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO yaihimiza Uchina kuendelea kufanyia marekebisho mfumo wake wa afya

Kusikiliza / Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. Picha@PAHO/WHO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Dr. Margaret Chan, amesema ni jambo la umuhimu mkubwa kwa serikali ya Uchina kuendelea na hata kuongeza kasi ya kufanyia marekebisho mfumo wake wa huduma za afya, ili kujenga mfumo utakaokabiliana na changamoto za afya sasa na za siku zijazo. Dr. Chan amesema hayo wakati akikamilisha ziara [...]

09/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majeruhi wa kiraia nchini Afghanistan waongezeka kwa asilimia 24 Mwaka 2014

Kusikiliza / Georgette Gagnon, mkuu wa haki za binadamu atembelea mtoto aliyejeruhiwa na kilipuzi manamo Febrruaru 2013(Picha ya UM/Fardin Waezi)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umesema kuwa kumekuwa na ongezeko la vifo na majeruhi wa kiraia nchini humo kwa asilimia 24 kufikia Juni 2014. Mengi yamesababishwa na mapigano ya nchi kavu na pia kwa mabomu yaliyotekwa chini ya ardhi. Ujumbe huo ukishirikiana na Ofisi ya Haki za Binadamu, umezindua ripoti inayoangazia mapigano [...]

09/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpango mpya wazinduliwa kukabiliana na ukatili wa kingono

Kusikiliza / Picha@UNICEF

Nchini Tanzania, msichana mmoja kati ya watatu hukabiliana na ukatili wa kingono kabla hajafikisha miaka kumi na minane. Bado desturi ya siri inakuwepo na kusababisha watekelezaji wengi kukwepa sheria. Ili kudhibiti ukatili huo, serikali ya Tanzania imezindua mpango mpya wa miaka mitatu wa kuripoti ukatili wa kingono kwa kupitia madawati ya jinsia na watoto yanayofunguliwa [...]

09/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya Haki za Wapalestina yakutana kuhusu ukuta tatanishi

Kusikiliza / Wanawake wa kipalestina wakitembea karibu na ukuta wa kiisraeli katika Ukingo wa Magharibi. Picha: IRIN/Shabtai Gold(UN News Centre)

Kamati kuhusu haki za watu wa Palestina, leo imefanya kikao cha kuadhimisha miaka kumi tangu ulipotolewa ushauri wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu hatua ya Israel ya kujenga ukuta katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua Mahakama ya Kimataifa ya Haki ilisema kuwa ujenzi wa ukuta huo ulikuwa [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani shambulizi dhidi ya makao makuu ya serikali Somalia

Kusikiliza / Nicholas Kay, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Somalia. Picha@UN Photo/David Mutua

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nichola Kay, amelaani shambulizi lililofanywa jana usiku dhidi ya Villa Somalia, ambayo ni makao makuu ya serikali ya Somalia mjini Mogadishu. Shambulizi hilo ni miongoni mwa msururu wa mashambulizi yanayotekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab dhidi ya taasisi za kisiasa nchini [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii za wavuvi ziwa Tanganyika zabadilisha mbinu za kukausha samaki

Kusikiliza / Picha@FAO

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO, limetoa ripoti mpya kuhusu mafanikio ya mradi lililoutekeleza katika jamii za wavuvi wa samaki ndogondogo, ziwani Tanganyika, nchini Burundi.  Samaki hao wanaoitwa ndagala, kawaida hukaushwa chini.  Mchanga, mvua na matope huharibu bidhaa hizo mara kwa mara, jinsi anavyoeleza afisa wa FAO Yvette Diei Ouadi: " Ilikadiriwa, mwaka 2004, [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini kuadhimisha miaka mitatu ya uhuru kwenye hali ya utata

Kusikiliza / southSudanIndependence1

Siku ya leo, Sudan Kusini, ambayo ni nchi changa zaidi duniani, inaadhimisha siku yake ya uhuru ilioupata mnamo tarehe 9, Julai 2011. Taarifa zaidi na John Ronoh. Kwenye siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon ametuma ujumbe wake kwa viongozi wa taifa hilo, akisema wana wajibu wa kuumaliza mgogoro uliopo sasa. [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shughuli za Umoja wa Mataifa Iraq zapigwa jeki na Kuwait

Kusikiliza / Familia hii ilikimbia mapigano Mosul, Iraq na wako karibu na kituo cha Khazair.Wanamatumaini ya kukakaa mji wa Erbil hadi itakapokuwa salama kurudi nyumbani(Picha@UNHCR/R.Nuri

Kuwait imetoa mchango wa dola milioni 9.5 kwa ufadhili wa huduma za Umoja wa Mataifa za kibinadamu nchini Iraq. Mratibu wa masuala ya kinadamu na misaada ya dharura, Valerie Amos amekaribisha mchango huo, akisema kuwa utasaidia wahudumu wa kibinadamu nchini Iraq kuongeza juhudi za kutoa misaada kwa familia zilizolazimika kuhama na jamii za wenyeji wao. [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930