Nyumbani » 08/07/2014 Entries posted on “Julai 8th, 2014”

Watoto wa Somalia kukumbwa na hali ya njaa

Kusikiliza / UN News Centre

Hali ya ukame inavyozidi kuongezeka nchini Somalia kutokana na ukosefu wa mvua, mashirika ya kimataifa yanatiwa wasiwasi na nchi hii kukumbwa na janga la njaa.  Katika hospitali ya Baidoa, kusini mwa Somalia, wakina mama wanazidi kuleta watoto wao waliougua utapiamlo, wengi wakiwa kwenye hatari ya kupoteza maisha. Ni matibabu gani wanapatiwa? Ungana na Amina Hassan [...]

08/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Australia yamulikwa kwa kuwarudisha wasaka hifadhi Sri Lanka kwa nguvu

Kusikiliza / @Ravina Shamdasani/OCHR

Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, leo imeelezea kusikitishwa na tukio la hapo Jumapili ambapo serikali ya Australia iliwarudisha watu 41 waliokimbilia nchi hiyo wakitafuta hifadhi salama wakitoka nchini Sri Lanka. Ofisi hiyo imesema hatua hiyo ilichukuliwa bila kuthibitisha kikamilifu madai ya watu hao ya kiusalama. Msemaji wa ofisi hiyo, Ravina Shamdasani [...]

08/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban atoa ujumbe wa amani kwa Siku ya Uhuru Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati taifa la Sudan Kusini likijiandaa kuadhimisha miaka mitatu tangu kujinyakulia uhuru mnamo Julai 9, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema viongozi wa taifa hilo changa zaidi wana wajibu wa kuumaliza mgogoro uliopo sasa, ambao amesema umebuniwa na mwanadamu. Katika taarifa iliyosomwa na msemaji wake, Bwana Ban amekumbusha kuhusu matumaini na matarajio [...]

08/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMA yatoa tamko kuhusu matokeo ya awali ya uchaguzi wa Urais- Afghanistan.

Kusikiliza / Afghanistan elections3

Ujumbe huo umeeleza kuwa matokeo yaliyotolewa siyo ya mwisho na kuna uwezekano wa kubadilika, na hivyo basi ni mapema kwa mgombea yeyote kudai ushindi wa uchaguzi huo. UNAMA imeendelea kuhimiza taasisi za uchaguzi hasa Kamisheni Huru ya Uchaguzi (IEC) na Kamisheni Huru ya Malalamishi ya Uchaguzi (IECC) wadhihirishe uajibikaji wao kwa kutilia maanani hali ya [...]

08/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake 145,000 wakimbizi wa Syria wanaubeba mzigo wa familia zao: UNHCR

Kusikiliza / Mstari wa wanawake wakikimbia Syria, wakibeba watoto, wakivuka ndani ya Jordan kutoka kusini mwa Syria. Picha: UNHCR/N. Daoud.

Ripoti mpya ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, imesema zaidi ya familia 145,000 za wakimbizi wa Syria zilizoko Misri, Lebanon, Iraq na Jordan, au kila moja katika familia zote za wakimbizi, zinaongozwa na wanawake ambao wanahangaika peke yao kujikimu kimaisha. Ripoti hiyo inaweka bayana mahangaiko ya kila siku ya kutafuta riziki, huku wanawake hao wakijitahidi [...]

08/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WFP yaongeza usambazaji misaada kwa maeneo magumu kufikiwa Sudan Kusini

Kusikiliza / SouthSudanRefugees1

Mashirika hayo yamesema kuwa kote nchini Sudan Kusini, kumewekwa mfumo wa pamoja wa huduma za dharura, ili wahudumu wa misaada ya dharura waweze kusafiri kwa ndege hadi maeneo yenye ugumu kufikiwa, na kuweza kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu ambao ama wamepokea usaidizi mdogo sana au hawajapata usaidizi wowote wa kibinadamu. Taarifa ya pamoja ya [...]

08/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yaeleza wasiwasi juu ya hali ya usalama CAR

Kusikiliza / Picha@WFP/George Forminyen

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP linatiwa wasiwasi kwa kushindwa kufikisha misaada ya kibinadamu kadri hali ya usalama inavyozidi kuzorota, anavyoeleza msemaji wake, Elisabeth Byrs: " Mnajua kwamba mashambulizi yameanza tena maeneo ya Bambari, na ghasia hizo zinaweka shughuli za kibinadamu hatarini. Hali ni ngumu sana kwa wafanyakazi [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tatizo la Ebola Afrika Magharibi lapatiwa sikio kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza / Said Djinnit, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa afrika Magharibi. Picha: UN Photo/Devra Berkowitz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa Afrika ya Magharibi, ikitaja hali tete eneo la Sahel na kuzorota usalama nchini Nigeria, huku suala la Ebola likitajwa kama linalopaswa kupewa kipaumbele na jamii ya kimataifa. Taarifa ya Joshua Baraza hilo ambalo limekutana kuhusu uimarishaji amani Magharibi mwa [...]

08/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubia mpya kuboresha sekta ya afya kupitia huduma za tabianchi.

Kusikiliza / madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Leo kimbunga kikipiga vikali kisiwa cha Japan, Shirika la Afya Duniani WHO na Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO yametangaza kufungua ofisi ya pamoja ya Afya na Tabianchi. Mashirika haya mawili yameamua kushirikiana ili kupambana na madhara ya kiafya yatokanayo na majanga ya tabianchi kama vile joto kali, mafuriko, ukame, ama [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wajiandaa kutoa misaada ya dharura Sinjar, Iraq

Kusikiliza / Picha: UNHCR_Iraq/ S. Baldwin

Timu ya wataalam wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, ilikwenda kwenye eneo la Sinjar, magharibi mwa Ninewa nchini Iraq, ambako familia zipatazo 8,000 zimekimbilia kutoka kwenye eneo jirani la Tal Afar. Timu hiyo imekwenda kufanya tathmini ya mahitaji ya kibinadamu ya dharura zaidi, ili kujiandaa kwa kutoa misaada. Mwakilishi wa UNICEF [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wahamiaji wanaokufa Mediterenia yaendelea kuongezeka

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria waokolewa katika bahari la Mediterenia. Picha@UNCHR/A. d'Amato(UN News Centre)

Idadi ya wahamiaji ambao wamekufa kwenye Bahari ya Mediterenia wakijaribu kukimbilia Ulaya imeongezeka na kufikia watu 500, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Mnamo Jumatatu, walinzi wa pwani ya Libya waliiambia UNHCR kuwa walikuwa wametoa miili 12 kutoka kwenye ajali ya boti ambayo inaaminika kutokea Jumapili.  Miongoni mwa wahanga [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930