Nyumbani » 07/07/2014 Entries posted on “Julai 7th, 2014”

UM wahimiza wanasiasa nchini Iraq kuchagua Spika wa Bunge haraka

Kusikiliza / Nikolay Mladenov@Picha/UNAMI

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladinov, leo amekuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Iraq na kutoa himizo lake kwa wote kuzingatia mkakati wa harakati za kikatiba na kuhakikisha kwamba waakilishi wa baraza wanakutana haraka iwezekanvyo. Bwana Mladenov ameeleza kuwa amepata hakikisho kutoka [...]

07/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwaelimisha wasichana ndio ufunguo wa maendeleo endelevu

Kusikiliza / Wanafunzi wa kike Tanzania @UNICEF Tanzania / Holt 2014

Mkutano wa kutoa ahadi za kusaidia utoaji elimu kote duniani umechangisha dola bilioni 28.5 kutoka kwa wafadhili na nchi zinazoendelea. Mkutano huo wa Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya Elimu au GPE ulifanyika mjini Brussels, Ubeljiji kati ya tarehe 25 na 26 Juni, ukilenga kuchangisha fedha zaidi za kusaidia upatikanaji elimu. Fedha hizo za ziada [...]

07/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi Zanzibar wahamasishwa kuhusu ukatili wa kingono

Kusikiliza / wanafunzi zanzibar1

Katika kisiwa cha Zanzibar, shule za wilaya za Kaskazini A zimeunda vilabu shirikishi ili kujadiliana kuhusu ukatili wa kingono. Ameir Haji kutoka kituo cha vijana Zanzibar amehudhuiria uhamasishaji ulioandaliwa na mkuu wa idara ya Elimu wa wilaya hiyo. Ni nini kilichofanyika? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

07/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Pakistan walioko Afghanistan wahitaji chakula kwa dharura:UM

Kusikiliza / Watoto wakiwa Kaskazini mwa Waziristan, huko Pakistan. Photo: IRIN/Fakhar Kakahel(UN News Centre)

Familia nyingi za Wapakistan zilizolazimika kuhama katika mikoa ya Khost na Paktika nchini Afghanistan zinahitaji chakula kwa dharura, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Operesheni za kijeshi katika eneo la Waziristan, kaskazini mwa Pakistan zilikuwa zimewalazimu watu wapatao 95,000 kukimbilia Afghanistan. Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq [...]

07/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Australia kuwafukuza wahamiaji wa Sri Lanka waliokamatwa baharini

Kusikiliza / Picha@UNHCR/A. Di Loreto(UN News Centre)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeeleza wasiwasi wake kuhusu maamuzi ya Australia kufukuza waomba hifadhi salama 41 kutoka Sri Lanka.  Mahakama Kuu ya Australia imesitisha pia maombi mengine 153 ya waomba hifadhi salama kutoka Sri Lanka. UNHCR imesema, imepata taarifa kutoka mamlaka za Australia kwamba vigezo vya kuthibitisha maombi ya hifadhi [...]

07/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waatalam wa Usalama wakutana Vienna Kujadili Maendeleo kuhusu Ujasusi wa Nyuklia

Kusikiliza / Mlipuko wa nyuklia. (Picha-Maktaba)

Wataalamu 350 wa Ujasusi wa Kinyuklia watakuwa na mkutano ya siku tatu mjiniVienna, Autria tokea tarehe 7-10 Julai 2014 kujadili juu ya utumiaji wa nguvu za Kinyuklia pamoja na kujaribu kuthathmini vyanzo na historia ya miyale nyuklia, hasa ile inayopatikana kwenye sehemu kulikotendeka uhalifu. Watalamu hao watakuwa na mazungumzo yanayolenga matumizi ya chembe chembe hizo [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanaleta mabadiliko: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Wakati dunia ikiangazia awamu ya mwisho ya harakati za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, MDGs, ni dhahiri sasa kuwa malengo hayo yanaleta mabadiliko katika maisha ya watu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, wakati wa kikao cha Baraza la masuala ya Kiuchumi na Kijamii, ambapo pia imezinduliwa ripoti ya [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wataalamu waonya kuhusu hali mbaya ya chakula Somalia

Kusikiliza / Picha ya OCHA

Wataalamu wa masuala ya chakula duniani wameonya juu ya Somalia kukumbwa na hali mbaya zaidi ya ukosefu wa chakula katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba mwaka huu. Wataalamu hao kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya dharura wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wahisani wa maendeleo nchini humo wakahamisha mada na [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa alaani mashambulizi dhidi ya Bunge la Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay

Nchini Somalia, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Nicholas Kay, amelaani vikali mashambulizi yaliyotokea dhidi ya Bunge la Somalia na mashambulizi kadhaa yanayodaiwa na kundi la Al-shabab tangu mwanzo mwa Ramadan, akisikitishwa kuona vitendo hivi kutokezea mwezi huo ambao ni mwezi wa Amani na Imani. Kay amewasifu walinzi wa Bunge [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay akemea ubaguzi wa elimu dhidi ya watoto wa kike, wanawake

Kusikiliza / Wasichana wa shule. UNICEF Tanzania. Picha@ Pudlowksi

Pamoja na wito unaoendelea kutolewa na jumuiya za kimataifa unaotaka kuondolewa kwa aina yoyote ya ubaguzi dhidi ya wanawake ikiwemo haki ya kupata fursa, lakini hadi sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watoto wa kike milioni 35 wameshindwa kupata elimu wanayostahili. Taarifa kamili na John Ronoh Kulingana na Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031