Nyumbani » 03/07/2014 Entries posted on “Julai 3rd, 2014”

Faida zinazopatikana kutokana na uwekezaji Afrika zaimarika

Kusikiliza / Dkt. Mukhisa Kituyi, Katibu Mtendaji wa UNCTAD. (Picha@UN/Jean-Marc Ferré)

Katika muongo uliopita, faida ya uwekezaji barani Afrika imeongezeka na kufikia kiwango kikubwa kuliko mabara mengine. Ripoti ya maendeleo ya Kiuchumi Afrika 2014 iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, inaonyesha kwamba kati ya miaka 1990 na 1994, dola 7.4 zilihitajika kuwekezwa ili kuzalisha kipimo kimoja cha ziada cha [...]

03/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama walaani mauaji ya mvulana wa Kipalestina

Kusikiliza / Baraza la Usalama. UN Photo

Wajumbe wa Baraza la Usalama wameelezea huzuni yao na kulaani vikali utekaji nyara na kuuawa kwa mvulana wa Kipalestina iliotekelezwa Julai 2 Mashariki mwa mji wa Jerusalem. Wametuma rambirambi zao kwa jamii iliopoteza mvulana huyo na watu wa Palestina kwa ujumla.Wamesema kwamba wote waliohusika na mauaji hayo ya kinyama wakamatwe na kuchukuliwa hatua, kulingana na [...]

03/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ziarani Kenya- Ban Ampanga Mwana simba-Tumaini

Kusikiliza / Katibu Mkuu apanga mtoto yatima wa Simba kutoka Nairobi National Park. Picha@ UN Photo/Eskender Debebe

Ulinzi wa wanyamapori ni jambo ambalo linaendelea kusisitizwa na jamii zote duniani, hasa kwa ajili ya urithi wa kizazi cha leo na vizazi vijavyo. Hivi majuzi Katibu mkuu akiwa mjini Nairobi, Kenya alimpanga mtoto yatima wa Simba na kumpa jina "Tumaini". Ujumbe alionuia kuwasilisha kwa upangaji huo ni nini? Basi ungana na John Ronoh kwa [...]

03/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kuwazuilia watafuta hifadhi na wakimbizi kukomeshwe: UNHCR

Kusikiliza / wakimbizi wanaoendelea kukimbia mapigano Mosul @UNHCR Inje Colijn

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, leo limetoa mkakati wa kimataifa unaolenga kuzisaidia nchi kukomesha desturi ya kuwakamata na kuwazuilia watafuta hifadhi, wakimbizi na watu wasio na utaifa kote duniani. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua UNHCR imesema kuwa desturi hiyo katika baadhi ya nchi ina madhara makubwa na [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO, Ulaya yaweka mkakati mpya kukabili kifua kikuu

Kusikiliza / Wagonjwa wa kifua kikuu kutoka Myanmar wakiishi kwenye vibanda wakati wa matibabu katika Klinik ya Wangpha kwenye mpaka wa Thailand. Picha: IRIN/Sean Kimmons(UN News Centre)

  Shirika la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na chama cha upumiaji barani Ulaya, leo kimetoa mwongozo mpya unaoainisha mikakati ya kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu katika nchi ambazo tatizohiloni la kiwango cha chini. Hadi sasa inaelezwa kuwa kuna nchi 33 duniani ambazo kiwango cha ugonjwa huo kipo chini na kwamba kila [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake na wasichana katika hatari ya ukatili na unyanyasaji Iraq: UNFPA

Kusikiliza / Wanawake na watoto Iraq. Picha:UNHCR/S.Baldwin

  Wakati watu wapatao milioni moja wakiwa wamelazimika kuhama kaskazini na magharibi mwa Iraq, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, limeonya kuwa takriban wanawake na wasichana 250,000, wakiwemo waja wazito wapatao 60,000 wanahitaji usaidizi wa dharura kuwaepusha na hatari ya ukatili wa kingono na unyanyasaji. Taarifa kamili na Amina Hassan Taarifa [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mbunge “Hayd”

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, amelaani vikali mauaji ya mbunge Mohamed Mohamud "Hayd" na mlinzi wake yaliyotokea leo asubuhi mjini Mogadishu, akieleza kutiwa wasiwasi na mashambulizi kadhaa yanayodaiwa na kundi la Al-Shabab tangu mwanzo mwa Ramadan. Nicholas Kay amesema, mwezi wa Ramadan ni mwezi wa amani na [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria hatarini wakati ufadhili ukididimia

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani wa Tartous, Magharibi ya Syria, ndio mamilioni ya waliopokea msaada wa UNHCR. Picha@UNHCR

   Hali ya kibinadamu ya wakimbizi wa Syria huenda ikazorota zaidi katika miezi michache ijayo wakati mashirika ya misaada yakikabiliwa na ugumu wa kupata fedha za kukidhi mahitaji yanayoongezeka, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.  UNHCR imesema kuwa idadi ya wakimbizi katika ukanda mzima inatazamiwa kuongezeka hadi milioni 3.6 [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031