Nyumbani » 02/07/2014 Entries posted on “Julai 2nd, 2014”

Mwakilishi wa UM Masahriki ya Kati alaani mauaji ya kijana wa Kipalestina

Kusikiliza / Robert Serry, Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu Mashariki ya Kati

  Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mashariki ya Kati Bwana Robert Serry amelaani vikali mauaji ya mvulana wa Kipalestina mnjini Jerusalem. Bwana Serry ameunga mkono ujumbe wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon unaosisitiza kuwa hakuna haki ya kumuua raia yeyote bila sababu. Amsema wote wanaohusika na mauaji hayo ya kinyama wanapaswa kuchukuliwa hatua, kulingana [...]

02/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zerrougui afanya ziara ya kutathmini utumikishwaji watoto vitani Sudan Kusini

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Alipozindua ripoti ya mwaka kuhusu watoto na mizozo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila Zerrougui, amesema kumeripotiwa visa vya utumikishwaji wa watoto katika majeshi 7 ya kitaifa, ikiwemo Sudan Kusini. Mwezi Juni, Leila Zerrougui alifunga safari ya kwenda Sudan Kusini ili atathmini hali ya utumikishwaji wa watoto [...]

02/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Somalia ipo kwenye njia panda : Ging

Kusikiliza / John Ging, Mkuu wa operesheni ndani ya OCHA alipozungumza na waandishi wa habari hii leo mjini New York, kuhusu ziara yake huko CAR. (Picha:UM/JC McIlwaine)

Taifa la Somalia lipo kwenye njia panda, huku hali ya kibinadamu nchini humo ikiendelea kuwa dhoofu. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni katika Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadam, OCHA, John Ging, wakati akikutana na waandishi wa habari mjini New York. Bwana Ging amesema ingawa kulikuwa na makubaliano ya ufadhili yaliyosainiwa mjini Brussels, Ubeljiji ya [...]

02/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yaanza kusambaza misaada kwa wakimbizi Pakistan

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Waziristan waliotafuta hifadhi maeneo ya Khost, Pakistan. @UNAMA/Fardin Waezi

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza usambazaji wa mahitaji ya dharura kwa zaidi ya familia 130 za Kiafghanistan ambazo zimeingia mtawanyikoni kutokana na machafuko huko Pakistani kaskazini mwa Waziristan. Operesheni ya kijeshi inayoendelea kaskazini mwa Waziristan imesababisha maelfu ya raia waliokuwa wakiishi mpakani mwa Pakistan na Afghanistan kukosa makazi . Ripoti ya hivi karibuni [...]

02/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rwanda kuongoza Baraza la Usalama Julai, ulinzi wa amani kuwekwa mbele

Kusikiliza / Balozi Eugène-Richard Gasana

Rwanda itaongoza Baraza la Usalama kwa kipindi cha mwezi mzima wa Julai. Mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo, Eugene Gasana, amesema kwamba urais huo utazingatia Ulinzi wa Amani, Rwanda ikiadhimisha mwaka huu miaka kumi tangu ilipoanza kuchangia katika jeshi la Ulinzi wa Amani la Umoja wa Mataifa. Katika muktadha huo, Rwanda imeamua kuandaa mjadala wa [...]

02/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sri Lanka isitishe ghasia kwa msingi wa kidini: UM waomba

Kusikiliza / Heiner Bielefeldt,  Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini. Picha@UN Photo/Paulo Filgueras

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kuwa na dini na kuhusu masuala ya walio wachache wameiomba leo serikali ya Sri Lanka kuchukua hatua ili wasitishe ghasia zinazotekelezwa na vikundi vya wafuasi wa Budha wenye msimamo mkali dhidi ya jamii za Wakristo na za Waislamu. Wameomba wapelekwe mbele ya sheria. Zaidi ya visa 350 [...]

02/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Yemen kuna tatizo kubwa duniani lililofichwa: UM

Kusikiliza / Yemen. Picha@OCHA/Eman Al-Awami(UN News Centre)

Nchi ya Yemen imo katika hali mbaya ya kibinadamu, inayozidi hali za matatizo mengi duniani, wamesema leo wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wakizungumza na waandishi wa habari. Wamesema nchi hiyo imedhoofika sana, na mwelekeo si mzuri kutokana na viashiria mbalimbali. Mkuu wa operesheni wa ofisi ya usaidizi wa kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA, [...]

02/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yatiwa moyo na ahadi za serikali kupunguza vifo vya uzazi

Kusikiliza / Mama na mtoto wake aliyedhaifu wakitoka katika kituo cha afya cha UNICEF katika mkoa wa Maradi. Picha@ UNICEF/Olivier Asselin(UN News Centre)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limeelezea matumaini yake ya kukabiliana na vifo vya kina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kutokana na msukumo uliotolewa na serikali katika kongamano moja la kimataifa lililomalizika huko Afrika Kusini. UNICEF imesema kuwa ahadi zilizotolewa na serikali ambazo zimesema kuwa zitaongeza [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Sudan Kusini watoa wito kwa amani

Kusikiliza / Kundi la wakimbizi wa ndani wakiwemo wanawake na watoto wakipumzika katika eneo la Ethiopia baada ya kuvuka mto wa Baro kutoka Sudan ya Kusini. Picha: UNHCR/L.F.Godinho(UN News Center)

Wakimbizi wa Sudan Kisuni walioko nchini Uganda wamezungumuzia vita vinavyotokota nyumbani mwao. Wanaziomba pande zinazozozana kurudi kwenye meza ya mazungumzo ndio amani ipatikane, watoke ukimbizini. Taarifa kamili na John Kibego wa Radio wahsirika ya Spice fm, aliyetembelea kambi moja nchini humo.  (Taarifa ya John Kibego)

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IPU yalaani mauwaji ya vijana wa Israel, Palestina

Kusikiliza / mnembo wa IPU @IPU

Jumuiya ya Umoja wa Mabunge (IPU) imelaani vikali matukio ya mauaji ya vijana wa Kiisrael na Palestina na imetaka pande zote kutojiingiza kwenye mzozo zaidi kutokana na matukio hayo. Taarifa iliyotolewa na IPU, imesema kuwa imesikitishwa na kupokea kwa huzuni kubwa  taarifa hizo na kwamba wakati huu inaendelea kuwa bega kwa bega na wale waliofika [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP yasema operesheni zake Ethiopia zakabiliwa na uhaba wa ufadhili.

Kusikiliza / Picha@WFP/George Forminyen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa shughuli za kuwahudumia wakimbizi nchini Ethiopia huenda zikakumbwa na hali ngumu katika kipindi cha kuanzia mwezi Septemba mwaka huu iwapo kutakosekana misaada ya dharura. WFP imesema kuna uwezekano mkubwa huduma zake nchini humo zikazorota iwapo hadi kufikia mwezi huo wa Septemba hakuna misaada yoyote itakayotolewa. Shirika [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Valerie Amos asikitikia taabu wanazopata raia wa Iraq

Kusikiliza / Picha ya UNHCR

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya misaada ya kibinadamu na uratibu wa mambo  ya dharura Valerie Amos ameelezea wasiwasi wake juu ya kuporomoka kwa ustawi wa kibinadamu nchini Iraq ambako hadi sasa watu zaidi ya milioni 1.2 wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea. Taarifa kamili na George Njogopa [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031