Nyumbani » 01/07/2014 Entries posted on “Julai 1st, 2014”

UNEP yaanzisha mpango wa uzalishaji na utumiaji endelevu

Kusikiliza / Upandaji miti sahihi kwenye eneo husika hulinda mazingira halisi ya eneo hilo.@UNEP

Mpango mpya wa kuwawezesha wanunuzi kufanya maamuzi wanayoelewa wakati wanaponunua bidhaa za matumizi umezinduliwa leo, ukilenga kuhakikisha matumizi bora ya rasilmali. Mpango huo ambao umezinduliwa na Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, utalenga kutoa maelezo kamili kwa wanunuzi kuhusu athari za kimazingira na kijamii za bidhaa wanazotumia, kama njia muhimu ya kuchochea mienendo endelevu zaidi [...]

01/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jenerali Sakyi wa Ghana kuongoza ujumbe wa UM India na Pakistan

Kusikiliza / Picha@UNMISS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Jenerali Delali Johnson Sakyi wa Ghana kuwa Mwangalizi Mkuu wa Kijeshi na Mkuu wa Kundi la Umoja wa Mataifa la Uangalizi India na Pakistan (UNMOGIP). Meja Jenerali Sakyi ataichukua nafasi ya Meja Jenerali Young-Bum Choi wa Jamhuri ya Korea, ambaye amehitimisha huduma yake ya miaka miwili [...]

01/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vifo kutokana na Ebola vyaongezeka hadi 467

Kusikiliza / Muuguzi akimuhudumia mgonjwa mwenye virusi vya Ebola. WHO/Chris Black

  Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kufikia Juni 30, idadi ya vifo vilivyotokana na mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola imepanda na kufikia watu 467, huku visa vya maambukizi ya virusi hivyo hatari katika nchi tatu zilizoathiriwa za Guinea, Liberia na Sierra Leone vikiwa sasa vimetimu 759. Idadi kubwa zaidi ya vifo hivyo imetokea [...]

01/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mauaji ya vijana wa Israel

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@UN Photo

Mauaji ya vijana watatu wa Israel waliotekwa katikati mwa mwezi Juni kwenye Ukingo wa Magharibi, yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. Kwa mujibu wa duru za habari, wanajeshi wa Israel waliipata miili mitatu ya vijana hao kaskazini mwa Hebron, mnamo Jumatatu. Israel inaripotiwa kuanza mashambulizi ya angani kwa maeneo ya [...]

01/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto watumikishwa katika mizozo 23 duniani: UM

Kusikiliza / watoto waliotumikishwa kijeshi wakichora katika kituo cha UNICEF, Jamhuri ya Afrika ya Kati @UNICEF/Brian Sokol

Mwaka 2013, watoto wametumikishwa, na kuuawa, kulemazwa ama kubakwa katika mizozo 23 tofauti duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu illiyotolewa leo kuhusu watoto na mizozo. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo mjini New York, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila  Zerrougui, amesema kumeripotiwa visa vya [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upandaji miti Bulengo..GOMA, DRC

Kusikiliza / Picha@MONUSCO

Paza sauti yako na si kiwango cha maji ya bahari, ni maudhui yaliyochaguliwa mwaka huu kwa ajili ya kulinda mazingira ya sayari ya dunia ili kuepusha nchi za visiwa vidogo kumezwa na maji ya bahari. Maudhui hayo yanatekelezwa kila kona ya dunia ikiwemo kwenye kambi za wakimbizi wa ndani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, [...]

01/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UN, mashirika ya hisani yaanza kuwapiga jeki wakimbizi Pakistan

Kusikiliza / Watoto wakiwa Kaskazini mwa Waziristan, huko Pakistan. Photo: IRIN/Fakhar Kakahel(UN News Centre)

  Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wameanza juhudi za haraka ili kuyakabili mahitaji muhimu kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 460,000 walioko maeneo ya kaskazini mwa Waziristani huko Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan. Imeelezwa kwamba zaidi ya asilimia 74 ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kwamba baadhi [...]

01/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi 800,000 Afrika wakabiliwa na uhaba wa chakula

Kusikiliza / sudan msaada wa chakula

Takriban wakimbizi milioni moja barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwa viwango vya kutia hofu, huku mashirika ya Umoja wa Mataifa yakihangaika kukidhi mahitaji ya chakula yanayozidi kuongezeka. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na lile la Chakula Duniani, WFP, yameanza kupunguza kiasi cha chakula kinachotolewa kwa wakimbizi, hali ambayo yamesema ni hatarishi, hususan kwa [...]

01/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wahimiza utulivu baada ya mauaji ya vijana Israel

Kusikiliza / Picha@Ravina Shamdasani/OCHR

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imepigwa na huzuni baada ya miili ya wavulana watatu wa Israel walioripotiwa kupotea hapo tarehe 12 Juni kupatikana wakiwa wameuawa katika Ukingo wa Magharibi. Ofisi hiyo imetoa rambirambi zake kwa jamii za wavulana hao na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahalifu wa mauaji hayo. [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Jarida | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa auawa Mali

Kusikiliza / Walinda Amani wa MINUSMA @MINUSMA/Blagoje Grujic

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon amelaani vikali tukio la kuuawa kwa mlinda amani mmoja wa Umoja wa Mataifa katika shambulio la bomu nchini Mali hapo jana. Mlinda amani huyo kutoka Burkina Faso aliuawa na wengine sita kujeruhiwa maeneo ya Timbuktu, katika mlipuko wa bomu. Bwana Ban amepeleka rambirambi zake kwa familia [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi nne zaridhia mkataba kuhusu kutokuwa na utaifa

Kusikiliza / @UNHCR/ S. Boness

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kwa pamoja na Ofisi ya sheria ya Umoja wa Mataifa, leo wanakutana kwa shughuli maalumu mjini Geneva ambako pia nchi za Ubelgiji, Gambia, Georgia na Paraguay zitajitokeza na kuridhia mkataba wa Umoja wa Maitaifa kuhusu watu wanaokosa utaifa. Taarifa kamili na Amina Hassan Taarifa ya Amina [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO, WHO yatoa orodha vyakula 10 vinavyoandamwa na wadudu

Kusikiliza / @FAO

Kumetolewa ripoti mpya inayoonyesha vyakula aina kumi duniani ambavyo ndani yake kunakutikana wadudu hatari wanaoweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu. Hata hivyo habari njema ni kwamba ripoti hiyo imebainisha mbinu za kukabiliana na wadudu hao wanaokaa ndani ya mimea.Taarifa zaidi na George Njogopa Taarifa ya George Imefahamika kuwa wadudu hao ambao wengi wao [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia wanaouawa Iraq yaendelea kupanda

Kusikiliza / wakimbizi wanaoendelea kukimbia mapigano Mosul @UNHCR Inje Colijn

Zaidi ya raia 2,400 wa Iraq waliuawa katika mwezi Juni pekee katika vitendo vya kigaidi na machafuko, kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya raia 1,500 na askari 800 wa vikosu vya usalama. Mji wa Baghdad ndio ulioathirika [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031