Nyumbani » 31/07/2014 Entries posted on “Julai, 2014”

Umoja wa Mataifa waomba kuwafikia raia wanaohitaji misaada Iraq.

Kusikiliza / Picha@UNAMI

Mtalaam wa Umoja wa Mataifa ameeleza kutiwa wasiwasi na hali ya ghasia na ukosefu wa usalama nchiniIraq, ambayo inaweza kuathiri maisha ya raia. Tunahitaji kuwafikia raia sasa hivi kwa njia salama, amesema Jacqueline Badcock, ambaye ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo, akiongeza kwamba wanahitaji kuwapatia msaada wa kibinadamu na huduma za msingi [...]

31/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Akiwa Costa Rica, Ban atoa mhadhara kuhusu sheria, haki na maendeleo endelevu

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon wakati alipokutana na Rais Luis Guillermo Solís, Costa Rica.Picha ya UM/Mark Garten/NICA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ambaye yuko ziarani nchini Costa Rica, leo ametoa mhadhara kwenye Mahakama ya Kikanda ya Haki za Binadamu, akiangazia ushirikiano wa taifa la Costa Rica na Umoja wa Mataifa, pamoja na fursa na changamoto zilizopo katika karne ya 21. Hotuba ya Katibu Mkuu imejikita kwa masuala ya sheria [...]

31/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhuru wa makundi ya kidini ni mtihani katika kuendeleza uhuru wa kuabudu Viet Nam- wataalam

Kusikiliza / Heiner Bielefeldt-Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini. Picha:UN Photo/Paulo Filgueiras

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini, Heiner Bielefeldt, leo akiwa ziarani Viet Nam, amesema kwamba jamii za kidini nchini humo zinahitaji kuwa na uhuru wa kuendeleza imani zao nje ya mipango inayoratibiwa na serikali ya nchi hiyo. Amesema kuwa kuruhusu uhuru huo utakuwa mtihani mkubwa kwa nchi [...]

31/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watu wa Roma (“Gypsies”) wanapaswa kulindwa- wataalam wa UM

Kusikiliza / Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari, Adama Dieng

Wakati wa kumbukizi ya miaka 70 ya mauaji ya kimbari ya watu wa Roma, wataalam wa Umoja wa Mataifa wameziomba nchi zote duniani ziwakumbuke watu hao. Watu wengi hawajui kwamba watu wa Roma, ambao pia wanajulikana kwa jina la "Gypsies" walilengwa na serikali ya Nazi, iliyotawala Ujerumani na sehemu mbalimbali za Ulaya wakati va vita [...]

31/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mimba za utotoni ni changamoto inayokabili lengo la pili la upatikanaji wa elimu kwa wote

Kusikiliza / Picha@Mark Tuschman/UNFPA

  Kuzidi kushadidi kwa mimba za utotoni katika maeneo mbali mbali Tanzania ni moja kati ya sababu ambazo zinakwamisha  katika kufikia lengo namba mbili la malengo la milenia ambalo ni upatikanaji wa elimu kwa wote. (Makala ya Martin Nyoni wa radio washirika Radio Sauti,Mwanza Tanzania)

31/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasikitishwa na hali ya kibinadamu Gaza

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu hali kwenye Ukanda wa Gaza. 
Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekutana kwa dharura leo tarehe 31 Julai, kufuatia kuzorota zaidi kwa hali ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza, na kuuawa kwa watu 19 kwenye shule moja ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina, UNRWA. Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu, OCHA, Valerie [...]

31/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Kenya Uganda wataka warudishwe nyumbani

Kusikiliza / Wakimbizi waKenya katika ofisi ya UNHCR nchini Uganda.Picha ya UN Radio/kiswahili/John Kibego

Wakimbizi wa Kenya walioko kwenye kambi ya Kiryandongo Magharibi mwa Uganda wameandamana hadi kwenye ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi la (UNHCR) kambini humo wakitaka serikali yao iwarudishe nyumani. Zaidi ya wakimbizi 1400 wa Kenya ambao wako katika kambi hiyo kwa sasa ni sehemu ya waliotoroka mchafuko ya baada ya uchaguzi [...]

31/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama wa chakula yaendelea kudorora Sudan Kusini

Kusikiliza / Lori likisafirisha mbegu za FAO. Picha:FAO/CAR

Juhudi za kutoa misaada kwa wakulima, wavuvi na wafugaji nchini Sudan Kusini zinakumbwa na matatizo kwa sababu ya upungufu wa ufadhili huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa janga la njaa katika baadhi ya maeneo, limeonya Shirika la chakula duniani, FAO. Taarifa kamili na Grace Kaneiya (Taarifa ya Grace) Kufikia sasa, FAO imepokea dola milioni 42 [...]

31/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto washirikishwe katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi- UNICEF

Kusikiliza / Picha@UNICEF(UN News Centre)

Watoto wanaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la gesi chafuzi hewani, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake, amesema, asilimia 99 ya vifo vitokanavyo na mabadiliko ya tabianchi vimetokea katika nchi zinazoendelea, na wengi wa waathirika ni watoto. [...]

31/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna vikwazo vya usafiri Afrika Magharibi licha ya kuenea kwa kirusi cha Ebola- WHO

Kusikiliza / Photo: WHO/T. Jasarevic

Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa hatari ya wasafiri wa ndege kueneza maambukizi ya kirusi cha Ebola kutoka nchi zilizoathiriwa bado  ni ndogo, lakini haiwezi kupuuzwa. Taarifa kamili na Amina Hassan. Taarifa ya Amina WHO haijapendekeza vikwazo vyovyote vya usafiri hadi sasa au kufungwa kwa mipaka kwa sababu ya mlipuko wa Ebola, ingawa imetoa [...]

31/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuhitimisha elimu ya msingi Uganda ni changamoto

Kusikiliza / Shule ya Msingi ya Hoima mjini Hoima. Picha: John Kibego/Radio Spice FM

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ingawa asilimia 90 ya watoto wameandikishwa shuleni, bado watoto milioni 85 duniani wamebaki nje ya shule. Hiki ni kikwazo cha kwanza katika kufikisha lengo nambari mbili la maendeleo ya milenia, likiwa kuhakikisha watoto    wote wa kike na wa kiume wanahitimu elimu ya shule ya msingi. Nchini Uganda, je ni [...]

30/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hakuna mahali salama kwa watoto wa Gaza- Zerrougui

Kusikiliza / Leila Zerrougui@UN Photo

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na mizozo ya silaha, Leila Zerrougui, amesema kuwa baada ya wiki tatu za vita katika Ukanda wa Gaza, hakuna mahali salama kwa watoto wa Gaza. Bi Zerrougui amesema hayo leo baada ya shule nyingine ya Umoja wa Mataifa inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 3,300 kupigwa [...]

30/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ukraine yaishutumu Urusi kwa kusaidia waasi nchini humo

Kusikiliza / Yuriy Sergeyev, Balozi wa Ukraine katika Umoja wa Mataifa. Picha@UN Photo/Mark Garten

Ukraine imeikabidhi Uholanzi jukumu la kufanya uchugunzi kuhusu ndege ya MH17, kwa sababu wahanga wengi walikuwa na uraia wa Uholanzi, kwa mujibu wa Yuriy Sergeyev, Balozi wake wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa. Akizungumza na waandishi wa habari, amesema Ukraine ina uhakika kwamba waasi wanaotawala eneo hilo ndio walioitungua ndege hiyo na wanaendelea kupiga makombora [...]

30/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hakuna mahali salama kwa watoto wa Gaza- Zerrougui

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na mizozo ya silaha, Leila Zerrougui, amesema kuwa baada ya wiki tatu za vita katika Ukanda wa Gaza, hakuna mahali salama kwa watoto wa Gaza. Bi Zerrougui amesema hayo leo baada ya shule nyingine ya Umoja wa Mataifa inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 3,300 kupigwa [...]

30/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Machafuko ya Gaza yamekithiri viwango, yakomeshwe- UM

Kusikiliza / Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson.Picha ya/UM/Loey Felipe/NICA

Pande zote katika mzozo wa Gaza zinapaswa kuelewa kwamba mzozo huo umekithiri viwango! Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson akizungumza mbele ya waandishi wa habari mjiniNew York, kufuatia shule ya UNRWA kupigwa kwa makombora kwenye Ukanda waGaza. Amesema kwamba watu 16 wameuawa na zaidi ya mia wamejeruhiwa kwenye [...]

30/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM akaribisha nia ya kuundwa utawala mpya kati mwa Somalia

Kusikiliza / Nicholas Kay, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia. Picha@UNSOM

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay, amekaribisha makubaliano na nia ya kuunda utawala katika eno la Kati nchini Somalia. Viongozi wa eno hilo walitia saini makubaliano yanayolenga kutekeleza mpango wa kuunda utawala kati mwa Somalia, wakiongozwa na serikali kuu ya Somalia. Makubaliano hayo yalishuhudiwa na mabalozi wa nchi kadhaa na wawakilishi [...]

30/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban ataka uchunguzi wa kudunguliwa ndege ya MH17 usitatizwe

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha@UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezea kusikitika kwamba wapelelezi wa kimataifa waliopewa jukumu la kuchunguza kudunguliwa kwa ndege ya Malaysia, MH17 wanaendelea kukabiliwa na vikwazo vya kufikia eneo la tukio hilo na kufanya kazi yao kwa sababu ya mapigano makubwa yanayoendelea katika eneo hilo. Taarifa ya msemaji wake imesema kuwa bado kuna [...]

30/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Misaada yafikia raia wa Syria kwa taabu- OCHA

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria Picha@UNHCR

Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Operesheni katika Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura, OCHA, John Ging, amezungumza mbele ya baraza la usalama kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria na usambazaji wa misaada ya kibinadamu. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte. (Taarifa ya Priscilla) Ripoti yake inafuatia azimio lililochukuliwa na barazahilowiki mbili zilizopita [...]

30/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asifu mradi wa nishati endelevu Nicaragua

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa azuru mradi wa nishati mbadala.Picha ya UM/Mark Garten/NICA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ambaye yuko ziarani Amerika ya Kusini, ameusifu mradi wa taifa la Nicaragua wa nishati mbadala itokanayo na nguvu za upepo, ambao ukimalizika utakuwa na uwezo wa kukidhi robo ya mahitaji yote ya nishati nchini humo. Mradi huo unalenga kupunguza uvushaji wa gesi chafuzi kwa tani laki moja [...]

30/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya usafirishaji haramu wa watu- Ban

Kusikiliza / Picha: ILO/A. Khemka(UN news Centre)

Ikiwa leo Siku ya Kupinga Usafirishaji Haramu wa Binadu inaadhimishwa kwa mara ya kwanza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ametoa wito hatua zichukuliwe kuutokomeza uhalifu huo na kuwapa tena matumaini waathiriwa wake, huku akitaka njia za ufadhili wa uhalifu huo zikatizwe na mali za wanaoutenda kunyakuliwa. Taarifa kamili na George Njogopa Taarifa [...]

30/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kenya yatakiwa kuwapatia wananchi wake huduma ya maji safi

Kusikiliza / Picha: World Bank/Allison Kwesell

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa juu ya haki ya maji safi ya kunywa Catarina de Albuquerque ameitaka Serikali ya Kenya kutekeleza kwa vitendo katiba inayotoa haki kwa kila mwananchi wa Kenya kuwa na fursa ya kupata maji safi na salama. Mtaalamu huyo ametoa wito huo mwishoni mwa ziara yake ya siku saba na kuongeza [...]

30/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa OCHA atiwa hofu na hali ya kibinadamu Gaza

Kusikiliza / Valerie Amos (Picha ya UM)

Mkuu wa Ofisi ya Kuratibu wa Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura, OCHA, Valerie Amos, ameelezea kutiwa hofu na kuchacha kwa machafuko Gaza baada ya muda mfupi wa usitishwaji mapigano wa kibinadamu. Bi Amos amesema kuwa shule moja inayotumiwa kama makazi ya raia waliokimbia makwao imelengwa katika kile alichokitaja kuwa ukiukwaji wa sheria ya [...]

30/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kwenye siku ya urafiki Ban atoa wito watu watafute urafiki wa kweli

Kusikiliza / Urafiki

Julai 30 ni Siku ya Urafiki Duniani- na kulingana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, siku hiyo inakuja wakati vita, machafuko na kutoaminiana vimetanda kote duniani. Katika ujumbe wake huo wa siku hiyo, Ban amesema watu ambao zamani wakiishi kwa amani, sasa wanajikuta wakizozana na majirani zao, huku watu wanaopaswa kuishi pamoja wakiwa wametenganishwa. [...]

30/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ziarani Nicaragua, Ban atoa wito kwa nchi zilinde haki za wahamiaji

Ban ahutubia wanahabari wiki karibuni Qatar. Picha ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa nchi zote zisaidie katika kulinda utu na haki za wahamiaji, hususan watoto, huku akiyalaani vikali makundi ya wahalifu wanaowasafirisha watoto hao kwa njia haramu yakiwaweka hatarini pamoja na kuwanyanyasa. Bwana Ban ambaye yuko ziarani nchini Nicaragua, amesema kuwa taifa la Nicaragua limeonyesha uongozi mzuri [...]

29/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Lengo la milenia kuhusu elimu DRC limevurugwa na migogoro

Kusikiliza / Melissa Kasoko

Wakati safari ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ikielekea ukomo wake mwakani, nchi husika zimo mbioni kufikia malengo manane ya maendeleo ya milenia. Upatikanaji wa elimu kwa watoto wote ni lengo namba 2, lakini sekta hii inakabiliana na changamoto ya kuhakikisha kwamba watoto wanapata elimu. Je vipi upatikanaji elimu unakabiliwa na uwepo wa migogoro [...]

28/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka magaidi wazuiwe kunufaika na biashara haramu ya mafuta Syria na Iraq

Kusikiliza / Balozi Eugene-Richard Gasana Picha ya UM/Paulo Filgueiras/NICA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limesisitiza wajibu wa nchi wanachama kuhakikisha kuwa zinazuia ufadhili wa vitendo vya kigaidi, huku likielezea wasiwasi wake kuhusu ripoti zinazosema kuwa makundi ya kigaidi kama ISIL na Jabhat Al-nusra yamefikia na kuteka viwanja na mabomba ya mafuta nchini Syria na Iraq. Katika taarifa iliyosomwa na rais wake kabla [...]

28/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakaribisha kuanza mazungumzo Mali

Kusikiliza / Balozi Eugène-Richard Gasana (kulia)na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Picha/UM/Devra Berkowitz/NICA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha kuanza kwa mazungumzo baina ya watu wa Mali mnamo Julai 16 mjini Algiers, kufuatia maazimio yake 2100 (2013) na 2164 (2014), pamoja na makubaliano ya awali ya Ouagadougou, kwa lengo la kufikia makubaliano ya kina ya amani yatakayoumaliza mzozo nchini humo. Katika taarifa iliyosomwa na rais wake, [...]

28/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wagombea Urais Afghanistan wakubali pendekezo la UM kuhusu ukaguzi wa kura

Kusikiliza / Wapiga kura wakati wa duru ya kwanza ya uchaguzi, Afghanistan.Picha@UNAMA

Wagombea wawili wa kiti cha urais nchini Afghanistan Dkt. Abdullah Abdullah na Dkt. Ashraf Gahani, wameelezea Umoja wa Mataifa kuwa wanaunga mkono pendekezo la Umoja huo, ambalo limekubaliwa na tume huru ya uchaguzi, IEC kuhusu vigezo vya kuhesabu tena na kuhakiki kura, kama sehemu ya kukaguliwa kwa duru ya pili ya uchaguzi nchini humo. Umoja [...]

28/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani mauji ya raia jimboni Ghor, Aghanistan

Kusikiliza / Nembo ya UNAMA(Picha@UNAMA)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umelaani vikali mauaji ya  Julai 25 yaliotokea katika Jimbo la Ghor ambapo watu 15 waliuawa wakiwemo wanawake watatu. Ripoti zinasema kwamba asubuhi ya Julai 24, mabasi mawili tofauti yaliyokuwa yakisafirisha raia yalisimamishwa na watu waliokuwa wamejihami, huku abiria wa basi la kwanza wakiamrishwa kushuka basi hilo na [...]

28/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pande zote katika mzozo wa Gaza ni lazima ziwajibike kwa uhalifu- Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwahutubia waaandishi wa habari kuhusu Gaza.Picha/UM/Mark Garten/NICA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ambaye amerejea mwishoni mwa wiki kutoka ziarani Mashariki ya Kati, ameunga mkono wito wa Baraza la Usalama wa kusitishwa mapigano mara moja na bila masharti kwa sababu za kibinadamu, huku akiongeza kuwa ni lazima kuwepo uwajibikaji na haki, kufuatia uhalifu uliotendwa na pande zote. Bwana Ban ambaye [...]

28/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yaomba dunia "kufikiria tena"ili kukabiliana na virusi vya homa ya ini

Kusikiliza / @WHO

Leo Julai 28  ni siku ya Homa ya Ini (Hepatitis) Duniani ambako Shirika la afya duniani WHO na wadau wanachagiza watunga sera, wahudumu wa afya na umma, "kufikiria tena" kuhusu ugonjwa huu unaouwa kimya kimya.Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii WHO imekaribisha hatua mpya zilizopigwa katika [...]

28/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay aonya juu ya kudunguliwa ndege ya Malaysia nchini Ukraine

Kusikiliza / Navi Pillay.Picha ya UM/UNIFEED

Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay amesema kuwa kitendo cha kudunguliwa kwa ndege ya Shirika la Malaysia kilichofanywa huko Mashariki mwa Ukraine kinaweza kuchukua sura uhalifu wa kivita. Taarifa kamili na George Njogopa Taarifa ya George Akielezea zaidi kuhusiana na tukio hilo lililotokea Julai 17 mwaka huu, Pillay [...]

28/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kay atuma salamu za Idd kwa wananchi wa Somalia

Kusikiliza / Mwakili maalum wa Katibu Mkuu, Somalia Nicholas Kay.Picha ya UM/Jean-Marc Ferré

Mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Nicholas Kay amewatumia salamu za Idd wananchi wa taifa hiloakisema kuwa kipindi hiki kinapaswa kutumiwa vyema na hasa kuwajali wale wenye mahitaji. Katika salamu za kuadhimisha kukamilika kwa kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani, Kay amesema kuwa anaungana na wananchi wa Somalia kusherehekea [...]

28/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka kusitishwa mapigano Gaza

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakati wa kikao.Picha ya UM/Paulo Filgueiras/NICA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yaliyoibuka upya katika eneo la Gaza ambayo yameshabisha watu kuendelea kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa. Taarifa kamili na John Ronoh Taarifa ya John Ronoh Baraza hilo la Usalama limesema lina wasiwasi mkubwa juu ya vifo na majeruhi yaliyosababishwa na hali mbaya ya [...]

28/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha usitishwaji mapigano wa kibinadamu kwa saa 12 Gaza

Kusikiliza / Picha ya @UNRWA

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha usitishwaji mapigano uliotekelezwa kwa sababu za kibinadamu huko Gaza, kwa kipindi cha saa 12. Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Ban amesema kuwa, wakati kipindi hicho cha utulivu kinapokaribia kumalizika, kuna picha nyingi za raia wa Gaza wanaojaribu kurejelea maisha yao ya kila siku, huku wakiwahudumia [...]

26/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laomba ufadhili haraka kuepusha baa la njaa Sudan Kusini

Kusikiliza / Mapigano yanayoendelea Sudan Kusini yameleta madhila makubwa ikiwemo njaa kwa wakazi hususan wanawake na watoto. (Picha-WFP)

Wanachama wa Baraza la Usalama wameelezea kusikitishwa na tatizo kubwa la kutokuwepo usalama wa chakula Sudan Kusini, ambalo sasa ndilo baya zaidi kote duniani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na rais wa Barazahilo, Eugène-Richard Gasana, wanachama wa Baraza la Usalama wameelezea hofu kubwa kuwa tatizohiloSudan Kusini huenda karibuni likafikia kiwango cha baa la njaa, kwa [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi wanachama wa UN ziache kuipelekea Syria silaha

Kusikiliza / Paulo Pinheiro(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré/NICA)

Urushiaji raia makombora , kuwatesa na kukiuka haki zao za binadamu kunaendelea nchini Syria bila ufuatiliaji wa kisheria. Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi kuhusu Jamhuri ya Kiarabu ya Lybia, Paulo Pinheiro amesema hivyo alipozungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa akitarajia kuripoti mbele ya Baraza la Usalama. "Tunaendelea kushuhudia ukwepaji mkubwa wa sheria Syria. Pande [...]

25/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto Sudan Kusini hawawezi kusibiri njaa itangazwe ndipo dunia ichukue hatua: UNICEF na WFP

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa WFP, Ertharin Cousin. Picha: WFP(UN News Centre)

Wakuu wa Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa wameonya leo kuwa watoto Sudan Kusini hawawezi kusubiri hadi baa la njaa litangazwe nchini humo, ndipo jamii ya kimataifa ichukue hatua. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF na yule wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, Ertharin Cousin, wamesema kuwa walikutana na watoto wenye [...]

25/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Harakati za kufikia lengo nambari moja:Tanzania

Kusikiliza / Picha@UNDP

Lengo namba moja katika malengo manane yaliyowekwa na viongozi wa dunia mnamo mwaka 2000, ni kumaliza njaa na umaskini uliokithiri. Watu bilioni 2.2 ni maskini au wamo hatarini kutumbukia katika umaskini, kulingana na ripoti ya maendeleo ya mwanadamu ya mwaka 2014, ambayo imezinduliwa wiki hii na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, [...]

25/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Uelewa wa malengo ya milenia waangaziwa Mwanza,nchini Tanzania

Kusikiliza / MDGs(Picha@UM)

Kiasi miaka 14 iliyopita Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Mataifa wanacham ilipitisha maazimio 8 ya maendeleo ambayo yatafikia ukomo mwaka 2015.  

25/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Iraq alaani uharibufu wa Urithi wa kihistoria mjini Mosul

Kusikiliza / wakimbizi wanaoendelea kukimbia mapigano Mosul @UNHCR Inje Colijn

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladenov, leo amelaani vikali vitendo vya kuharibu urithi wa kihistoria, likiwemo kaburi la Nabii Yona na Msikiti wa Mosul pamoja na majengo mengine muhimu ambayo yameorodheshwa na kuhifadhiwa kama urithi unaoonyesha utamaduni wa nchi hiyo. Amesema kuwa utesaji wa kupangwa wa [...]

25/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watalaam wa UM wasema mgogoro Iraq unawadhuru vibaya walio wachache

Kusikiliza / Familia hii ilikimbia mapigano Mosul, Iraq na wako karibu na kituo cha Khazair.Wanamatumaini ya kukakaa mji wa Erbil hadi itakapokuwa salama kurudi nyumbani(Picha@UNHCR/R.Nuri

Wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu, wamesema kuwa makundi ya kabila na dini za walio wachache yanataabika zaidi kutokana na mgogoro ambao tena umelighubika taifa la Iraq. Wataalam hao wameonya kuwa ikiwa hatua za kuwalinda watu hao wa makundi ya walio wachache hazitachukuliwa haraka, madhara ya mgogoro kwa makundi hayo yatakuwa [...]

25/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNICEF yawataka wanaozozana Gaza kutoshambulia shule na watoto

Kusikiliza / Picha@UNRWA

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limetoa wito kwa pande hasimu katika mzozo wa Gaza kutowashambulia watoto na shule, likisema kuwa mashambulizi dhidi ya shule ambako watoto wametafuta usalama hayawezi kukubaliwa kwa vyovyote vile. Taarifa iliyotolewa na Bi Maria Calivis, Mkurugenzi wa UNICEF ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, imesema [...]

25/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ujumbe wa UNRWA washambuliwa ukiizuru shule ya Beit Hanoun iliyoshambuliwa

Kusikiliza / Picha@UNRWA

Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwasaidia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, umeshambuliwa leo wakati ukiizuru shule ya Beit Hanoun, ambayo ilishambuliwa hapo jana na kusababisha vifo kadhaa na majeruhi. Lengo la ziara ya ujumbe huo wa UNRWA, ambao pia ulijumuisha mtaalam wa kimataifa wa silaha, lilikuwa ni kutathmini eneo la tukio la jana. [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Fao yahitaji msaada wa dharura kukabili baa la njaa SAHEL.

Kusikiliza / Msaada wa chakula, WFP

Umoja wa mataifa leo kupitia Shirika la chakula duniani FAO, umetoa wito kwa nchi wanachama kuangazia upya makubaliano ya hapo awali ya kupambana na  baa la njaa na uhaba wa chakula ili kulinda na kuongeza juhudi za kuboresha maisha ya  jamii maskini katika ukanda wa  SAHEL. Taarifa kamili na John Ronoh Kumekuwa na matatizo kadhaa [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sheria zinazolinda watu zinaweza kusaidia kutokomeza Ukimwi

Kusikiliza / Picha@UNAIDS

Kongamano la kimataifa kuhusu Ukimwi ambalo limekuwa likiendea mjini Melbourne, Australia, limehitimishwa kwa wito kwa serikali zipitishe sheria zinazowalinda watu badala ya zile zinazowakandamiza na kuwafanya wasijitokeze kupima na kutafuta huduma za matibabu dhidi ya virusi vya HIV. Washiriki kwenye  kongamano hilo wamehitimisha kuwa inawezekana kutokomeza Ukimwi, lakini mapambano hayo yanapaswa kuzingatia suala la sheria [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Magereza yafunguliwa kwenye kambi za UNMISS

Kusikiliza / Wanawake wakiteka maji kwenye kambi ya Bor, UNMISS. Picha@UNMISS

Visa vya uhalifu kwenye kambi za wakimbizi wa ndani Sudan Kusini vimepelekea kufunguliwa kwa magereza kwenye kambi hizo kwa ajili ya kuwafunga waliotekeleza uhalifu. Taarifa zaidi na Amina Hassan Kwa ujumla, magereza manne yamejengwa katika kambi za Bor, Bentiu, Juba na Malakal, na tayari yamepokea zaidi ya watu 300, chini ya ulinzi wa polisi wa [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usafirishaji haramu wa binadamu unahatarisha maisha ya wahamiaji- IOM

Kusikiliza / Picha:UNHCR/A. Rodriguez

Wahamiaji wa asili ya kiafrika  na waomba hifadhi wananyanyapaliwa mikononi mwa wasafirishaji haramu katika safari ya kuvuka bahari ya mediterenia wakielekea Ulaya, limesema Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM. Wahamijai hao kutoka Afrika waliookolewa na wanajeshi wanamaji wa Italia, mnamo Jumamosi iliyopita, wamesema kwamba walikumbana na ubaguzi wa rangi, kudungwa visu na walikuwa wamerundikana kwenye [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa ukanda wa Maziwa Makuu wakutana kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana

Kusikiliza / Picha@ILO

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa Maziwa Makuu, Mary Robinson, ambaye karibu atahitimisha hatamu yake, amesema kuwa ajira kwa vijana ni moja ya mambo yanayohitajika ili kupunguza mizozo na kuleta maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huo. Taarifa kamili na Joshua Mmali Bi Robinson amesema hayo wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi za [...]

25/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MINUSMA kutafuta ndege ya Air Algeria iliyopotea

Kusikiliza / Picha@UM/Marco Dormino

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, MINUSMA, umeanza kushughulikia kutafuta ndege ya Air Algeria (nambari AH 5017) iliyopotea angani leo, tarehe 24, Julai, baada ya kupokea maombi ya msaada kutoka kwa serikali za Mali na Algeria. Helikopta mbili za kikundi cha walinda amani cha Uholanzi zimeanza hapo hapo mizunguko kwa masaa kadhaa ili kupata [...]

24/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya amani CAR yasainiwa Brazzaville

Kusikiliza / Picha@WFP/George Forminyen

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya Kati, Abdoulaye Bathily, na yule kwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Babacar Gaye, wamekaribisha makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande zote za mzozo unaoendelea Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Makubaliano hayo ya kusitisha mapigano yalisainiwa jana tarehe 23 Julai, katika mkutano ulioandaliwa Brazzaville, [...]

24/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kamati ya UM yajadili uenezaji ugaidi katika taasisi za elimu

Kusikiliza / Mkutano wa Halmashauri ya Kamati ya Baraza la Usalama ya Kukabiliana na Ugaidi, CTED. Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Halmashauri ya Kamati ya Baraza la Usalama ya Kukabiliana na Ugaidi, CTED, ikishirikiana na Wakfu wa Imani wa Tony Blair, imekuwa na mdahalo leo kuhusu mchango wa elimu katika kukabiliana na misimamo mikali inayoeneza ukatili wa kigaidi. Miongoni mwa yaliyokuwa kwenye ajenda ya mdahalo huo ni pamoja na jinsi ya kutekeleza azimio namba 1624 (2005) [...]

24/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza uchaguzi wa rais Iraq akiwa Najaf

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon alipokutana na kiongozi wa dhehebu la kishia, Ayatollah Al-Sistani.(Picha ya UM/Eskinder Debebe)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amepongeza kuchaguliwa kwa rais mpya Iraq, Dkt. Fouad Massoum, na bunge la nchi hiyo, akisema kwamba anataraji kuwa serikali mpya jumuishi itaundwa haraka chini ya uongozi wake. Katibu Mkuu amesema kuwa serikali mpya ambayo ni jumuishi itaimarisha umoja wan chi, kukabiliana ipasavyo na ugaidi na ISIS, na [...]

24/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya ukaguzi ya 2013 yazinduliwa hapa makao makuu:UM

Kusikiliza / Picha kutoka Ofisi ya Ukaguzi ya Serikali ya Tanzania

Bwana Ludovic Utouh ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Tanzania. Aidha, ameteuliwa mwaka 2012 na baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa, kwa kipindi cha miaka sita. Bodi hii ina viti vitatu ambavyo vimechukuliwa kwa sasa na China, Uingereza na Tanzania. Taasisi [...]

24/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkaguzi wa Serikali ya Tanzania akagua Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / Ludovic Utouh, mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa

Wakati ripoti ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2013, ikitolewa rasmi leo tarehe 24, Julai, idhaa ya kiswahili imepata fursa ya kuongea na Bwana Ludovic Utouh, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ameteuliwa rasmi na Baraza Kuu kuwa mwanachama wa Bodi ya Ukaguzi [...]

24/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanawake na wasichana nchini Iraq hatarini kukeketwa kwa nguvu

Kusikiliza / Picha@UNHCR/S.Baldwin

Zaidi ya wanawake milioni 4 kazkazini mwa Iraq wanakabiliwa na hatari ya kuketwa, kwa mujibu wa viongozi wa Umoja wa Mataifa nchini humo. Kundi la Waislamu wenye msimamo mkali, ISIS, ambalo linatawala eneo hilo la Iraq limeripotiwa kutoa amri wanawake wote wafanyiwe ukeketaji. Mratibu wa Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Jacqueline Badcock, amesema [...]

24/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN Women, FAO, na IFAD zazindua tuzo ya ubunifu wa sayansi kwa vijana

Kusikiliza / share-fair-logo1

Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, yakiwemo la masuala ya wanawake, UN Women, lile la Chakula na Kilimo, FAO na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD, yametangaza tuzo mpya ya ubunifu wa kisayansi kwa vijana, ambayo itatolewa kwa wanafunzi binafsi au makundi ya wanafunzi. Vijana wanaombwa kuwasilisha michanganuo ya ubunifu au teknolojia, ikiangazia ubunifu au [...]

24/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa uboreshe mfumo wake wa ajira – Bodi ya Ukaguzi

Kusikiliza / Ludovic Utouh, mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa

Leo ripoti ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa ya mwaka 2013 imetolewa rasmi, Mkaguzi Mkuu wa Tanzania, Bwana Ludovic Utouh, akiwa mmoja wa wajumbe watatu wa bodi hiyo ya Ukaguzi wa Umoja wa Mataifa. Taasisi ishirini na nne za Umoja wa Mataifa ambazo zimekaguliwa, ukaguzi huo ukilenga kuimarisha uwazi, uwajibikaji na utawala bora wa taasisi [...]

24/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Djinnit alaani kuibuka tena mashambulizi ya kikatili Nigeria

Kusikiliza / Uharibifu baada ya shambulizi na Boko Haram katika kituo cha polisi Kano, Nigeria.PIcha:IRIN/Aminu Abubakar(UM/News Centre/maktaba)

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa Afrika ya Magharibi, Said Djinit, amelaani vikali mauaji ya raia yaliyoripotiwa kutekelezwa mwishoni mwa wiki na hapo jana na kundi ya kigaidi la Boko Haram kwenye mji wa Damboa, Jimbo la Borno naKaduna, jimbo laKaduna. Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina) Bwana Djinnit ameelezea kusikitishwa [...]

24/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu bilioni 2.2 ni maskini au waelekea kuwa maskini- ripoti ya UNDP

Kusikiliza / Picha: UNDP/DRC

Ripoti mpya kuhusu maendeleo ya mwanadamu imeonya kuwa, umaskini na utaka wa mara kwa mara ni tishio kwa maendeleo ya mwanadamu, na usipokabiliwa ipasavyo kwa sera na kanuni za kijamii, hakutakuwa na maendeleo kwa njia ya usawa na endelevu. Taarifa ya John Ronoh Ripoti ya maendeleo ya mwanadamu ya mwaka 2014, imezinduliwa leo mjini Tokyo, [...]

24/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya wahamiaji 800 walipoteza maisha mwaka huu-UNHCR

Kusikiliza / Picha@UNHCR/A. Di Loreto(UN News Centre)

Zaidi ya wahamiaji 800 walipoteza maisha katika kipindi cha mwaka huu wakati walipojaribu kuvuka bahari ya Mediterranian kuingia katika nchi za Ulaya. Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR ambalo limeongeza kuwa katika kipindi cha siku kumi zilizopita, wahamiaji 260 inasadikika wamefariki dunia au wamepotea na hawajulikani [...]

24/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shule nyingine ya UNRWA yashambuliwa tena Gaza

Kusikiliza / Picha ya @UNRWA

Kumekuwa na ripoti kwamba shule nyingine inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Maifa la Kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA imeshambuliwa na makombora yaliyovurumishwa na vikosi vya Israel,  likiwa ni tukio la pili la namna hiyo. Kwa mujibu wa Msemaji wa UNRWA, watu 15, wakiwemo walimu watatu wa UNRWA, wamefariki dunia kwenye tukio hilo, na wengine [...]

24/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM alaani mauaji ya mbunge mwingine Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu Somalia, Nicholas Kay, amelaani mauaji ya Saado Ali Warsame, mbunge wa kike katika Bunge la Somalia, na kuelezea kusikitishwa mno na mashambulizi yanayoendelea kuwalenga wabunge katika mji wa Mogadishu. Bi Warsame na dreva wake walifyatuliwa risasi na kuuawa wakisafiri kwenye gari leo Mogadishu. Pamoja na kuwa mbunge, Bi Warsame [...]

23/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatma ya Watoto wa Gaza iko hatarini

Kusikiliza / Mtoto aliyejeruhiwa, hospitalini, Gaza. Picha ya @UNICEF

Wakati Baraza la Haki za Binadamu likipitisha leo tarehe 23 Julai azimio la kuunda tume ya uchugunzi juu ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea Gaza, watoto wanaendelea kuwa wahanga wa kwanza wa mashambulizi yanayoendelea katika ukingo wa Gaza. Watu mia 600 wameshafariki dunia tangu mwanzo wa mashambulizi, watoto wakiwa ni asilimia 30 miongoni mwao. [...]

23/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku 15 tangu mzozo wa Gaza kuanza, hakuna muda wa kupoteza: Ban

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ambaye yupo ziarani Mashariki ya Kati, amewahutubia waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry. Alipoulizwa kuhusu ni kwa nini akakubali kutumia ndege iliyofadhiliwa na Qatar kwa usafiri wake, Ban amesema: "Hii ni siku ya 15 tangu [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Haki za Binadamu kuchunguza ukiukwaji wa haki za bindamu Palestina

Kusikiliza / Baraza la Haki za Binadamu(Picha ya UM/ Jean-Marc Ferré)

Baraza la Haki za Binadamu lililokutana leo mjini Geneva kwa kikao maalum kuhusu Palestina, limepitisha azimio la kuunda tume ya uchunguzi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kufanyika katika maeneo ya Palestina yaliokaliwa, hasa katika Ukanda wa Gaza. Jukumu la tume hiyo litakuwa ni kuendesha uchunguzi juu ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa za [...]

23/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wataalam wa UM wataka baa la wakimbizi wa ndani Nigeria lishughulikiwe

Kusikiliza / Chakola Bayani (Picha@UN/NICA)

Watalamu wawili wa haki za kibinadamu wametoa wito kwa serikali ya Nigeria na jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya hatma ya wakimbizi zaidi ya Milioni 3.3 wa ndani nchini humo kwa sababu ya machafuko tangu mwaka 2010. Idadi hiyo ni mojawapo ya idadi ya juu zaidi ya wakimbizi wa ndani duniani. [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Bi Loj kuwa Mkuu wa Ujumbe wake Sudan Kusini

Kusikiliza / Ellen Margrethe Loej, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Sudan ya Kusini, UNMISS
Picha: UN Photo/Eskinder Debebe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amemteua Ellen Margareth Loj, kutoka Denmark, kuwa mwakilishi wake maalum Sudan Kusini na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS. Bi Loj anachukua nafasi ya Hilde Johnson kutoka Norway, ambaye alimaliza mkataba wake Julai, 7. Katibu Mkuu amemshukuru Bi Johnson kwa uongozi na msimamo [...]

23/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jamii ya kimataifa yapaswa kusaidia Ethiopia kupokea wakimbizi wa Sudan Kusini- OCHA

Kusikiliza / Kundi la wakimbizi wa ndani wakiwemo wanawake na watoto wakipumzika katika eneo la Ethiopia baada ya kuvuka mto wa Baro kutoka Sudan ya Kusini. Picha: UNHCR/L.F.Godinho(UN News Center)

Tayari wakimbizi 180,000 wa Sudan Kusini wamepata hifadhi nchini Ethiopia baada ya kukimbia vita vinavyoendelea nchini mwao, asilimia 90 wakiwa ni wanawake na watoto wanaohitaji msaada wa dharura. Hayo yameripotiwa na John Ging, Mkuu wa Operesheni katika Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, akizungumza na waandishi wa habari mjini New York baada ya ziara [...]

23/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAIDS na wadau wazindua mkakati wa kuimarisha vipimo vya HIV

Kusikiliza / Picha@UNAIDS

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya ukimwi UNAIDS, kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani, WHO na lile la kuhudumia watoto UNICEF, na wadau wengine, limezindua mkakati wa vipimo ambao unahimiza kuboresha uwezo wa maabara kuhakikisha kwamba watu wanaoishi na virusi vya HIV wanaweza kupata huduma stahiki kwa matibabu ya HIV. Mkurugenzi [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yalaani mashambulizi kwenye shule yake

Kusikiliza / Watoto kutoka Yarmouk. UNRWA/Rami Al-Sayyed

Wakati huo huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Palestina, UNRWA, limelaani vikali kurushwa kwa makombora kwenye shule yake, Gaza katikati. Taarifa zaidi na John Ronoh. Zaidi ya watu 300 waliolazimika kuhama makwao kutokana na mashambulizi ya hivi karibuni walikuwa wametafuta hifadhi katika shule hiyo ya UNRWA. Makombora yaliyopiga shule hiyo mapema [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yakaribisha kasi mpya ya kukabiliana na virusi vya homa ya ini

Kusikiliza / hepatitis testing

Huku siku ya Homa ya Ini (Hepatitis) Duniani ikiwa inakaribia kuadhimishwa mnamo Julai 28, Shirika la Afya Duniani, WHO, limekaribisha hatua mpya zilizopigwa katika kukabiliana na ugonjwa huo. Homa ya ini, au hepatitis, hupatikana katika aina tano tofauti, A, B, C, D na E, na huathiri mamilioni ya watu kote duniani, yakisababisha ugonjwa ini na [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unafanyika Gaza: Pillay

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay(Picha ya UM)

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay, ameilaani Israel kwa kutofanya kila iwezalo kulinda maisha ya raia wa Gaza, akisema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa sheria ya kimataifa ya kibinadamu imekiukwa katika njia inayoweza kuchukuliwa kuwa uhalifu wa kivita. Akilihutubia Baraza la Haki za Binadamu mwanzoni mwa kikao maalum cha kujadili hali huko Gaza, [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ajiunga kwa mkesha wa siku 100 tangu wasichana wa Chibok kutekwa

Kusikiliza / Picha: UNESCO

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amerejelea wito wake wa kutaka wasichana wa shule waliotekwa Chibok waachiliwe mara moja, siku 100 baada ya kutekwa kwao. Bwana Ban ameelezwa kuunga mkono kikamilifu msururu wa mkesha kote duniani kuadhimisha siku 100 tangu watekwe nyara, na kuonyesha mshikamano na wasichana hao. Wasichana hao walikamatwa mnamo Aprili [...]

23/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Picha za wanawake na watoto wanaouawa na kuteseka Gaza zinavunja moyo: Ban

Kusikiliza / Zaidi ya wakimbizi 50,00 wantafuta hifadhi katika shule za UNRWA.Picha ya Shareef Sarhan/UNRWA/maktaba

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ambaye yuko ziarani Mashariki ya Kati, amesema picha za wanawake na watoto wanaouawa na kuteseka Gaza zinatia uchungu moyoni, akiongeza kwamba ni vigumu kustahmili kuziona. Ban amesema hayo akikutana na waandishi wa habari akiambatana na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina. Awali, Bwana Ban alikuwa Israel, ambako alikutana [...]

22/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya haki ya maji na usafi yaangaziwa Kenya

Kusikiliza / Picha ya World Bank/Arne Hoel(UN News Centre)

Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya binadamu ya kupata maji na usafi, Catarina de Albuquerque, ameanza leo ziara yake nchini Kenya kwa ajili ya kutathmini mafanikio na changamoto za nchi hii katika kutimiza haki ya raia wake ya kupata maji na usafi. Mtaalam huyo amesema ataangalia tofauti zilizopo baina ya maeneo ya [...]

22/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tanzania yachukua hatua kupambana na usafirishaji haramu wa watoto

Kusikiliza / @UN Photo/Evan Schneider

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM linaendesha mkutano pamoja na Sekritariati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu ili kusanifisha utaratibu wa kutunza na kusaidia waathirika wa biashara hiyo haramu. Tanzania ni moja ya nchi zilizokumbwa na shida ya usafirishaji haramu wa watoto, wakiwa ni wasichana wanaotumikishwa manyumbani kama watumwa, wanawake wanaolazimika kufanya biashara ya ngono, [...]

22/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laomba mapigano yasitishwe Gaza

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Mashariki ya Kati. UN Photo/Paulo Filgueiras

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili kuhusu mzozo unaoendelea baina ya Israel na Palestina, Katibu Mkuu Ban Ki Moon akilihutubia Baraza hilo kutoka Ramallah, Palestina, baada ya kutembelea nchi ya Israel. Katibu Mkuu amekaribisha jitihada za viongozi wote wanaojituma katika utaratibu wa kufikisha makubaliano ya kusitisha mapigano. Aidha, amelaani mashambulizi yaliyofanyika na jeshi la Israel [...]

22/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WanawakeTanzania wajiendeleza na kunufaisha mazingira kupitia matumizi ya biogesi

Kusikiliza / Judith Muketa akitengeza nishati mbadala kwa kutumia samadi ya ng'ombe (Picha ya World Bank)

Nchini Tanzania, mama mmoja amechukua mstari wa mbele na kubadilisha maisha ya jamii yake kwa kutumia nishati mbadala ya gesi itokanayo na samadi ya ngombe kwa kupikia chakula na pia kuweka umeme kwa nyumba ya Jamii yake. Je Huyu mama kutoka Tanzania lengo lake hasa ni nini? Basi ungana na John Ronoh kwa makala hii.

22/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasikitishwa na utesaji wa walio wachache nchini Iraq

Kusikiliza / Mkutano wa Baraza la Usalama: Hali katika Mashariki ya Kati, na suala la Palestina. UN Photo/Paulo Filgueiras

  Wanachama wa Baraza la Usalama wameelezea masikitiko yao kufuatia ripoti ya  utesaji wa kupangwa wa makundi ya walio wachache katika mji wa  mosul, nchini Iraq, unaotekelezwa na wafuasi wa waasi wa Jamhuri ya Kiislamu Iraq (ISIL) na makundi husika yaliyojihami. Baraza hilo limesikitishwa hasa na ripoti za vitisho kwa Wakristo mjini Mosul na maeneo [...]

22/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Takwimu mpya za UNICEF zaonyesha haja ya kuchukua hatua dhidi ya ukeketaji na ndoa za utotoni

Kusikiliza / Akiwa na mwaka mmoja, Fatima alikeketwa akiwa kijijini kwake katika mkoa wa Afar, Ethiopia ambayo ina idadi kubwa zaidi ya ukeketaji. Picha: UNICEF/Kate Holt.(UN News Centre)

Kongamano la kwanza kabisa la watoto wa kike linafanyika leo mjini London, Uingereza, kuzivalia njuga mila mbili potofu zinazoathiri mamilioni ya watoto wa kike kote duniani: ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni. Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina) Dhamira ya kongamano hilo ni kuchagiza uongezaji kasi kwa hatua za kutokomeza ukeketaji na [...]

22/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WHO kupambana na Polio kaskazini mwa Somalia

Kusikiliza / © UNICEF Somalia/2013/Holt

Visa vinne vipya vya polio vimethibitishwa nchini Somalia licha ya kampeni kubwa ya chanjo inayoendelea nchini humo. Kwa ujumla, ni watu 198, hasa watoto, ambao wameathirika na ugonjwa huo tangu mwanzo wa mlipuko wake Mei, 2013. Visa vyote vipya vimeripotiwa katika maeneo ya Puntland, kaskazini mashariki mwa nchi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia [...]

22/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatua zahitajika kukabiliana na Polio Syria na nchi jirani

Kusikiliza / WHO Syria (Picha ya WHO)

Katika ukanda wa Mashariki ya Kati, watoto milioni 25 wamepewa chanjo ya polio kwenye kampeni iliyotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na lile la Afya Duniani WHO. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte (Taarifa ya Priscilla) Ripoti iliyotolewa leo na WHO pamoja na UNICEF imeonyesha kwamba kampeni hiyo ilifanikiwa kufikia watoto [...]

22/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa CAR wanahitaji kwa dharura usaidizi wa kibinadamu: UNHCR

Kusikiliza / Mtoto aliona utapia mlo uliokithiri kutoka CAR hosptiatli ya Batouri nchini Cameroon© UNHCR/F.Noy

Hali ya kibinadamu ya watu wanaokimbia kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati kwenda nchi jirani imeendelea kuwa mbaya wakati mashirika ya kibinadamu yakihangaika kupata ufadhili wa kutosha ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao yanayoongezeka. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limesema kuwa idadi ya wakimbizi waliokimbilia nchi za Cameroon, Chad, Jamhuri ya [...]

22/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WHO yatiwa hofu na mashambulizi dhidi ya vituo vya afya Gaza

Kusikiliza / Mtoto huyu wa kipalestina asimama nje ya nyumba iliokuwa nyumba yao iliyoharibiwa baada ya mashambulizi ya angani kambini mji wa Rafhakusini mwa Ukanda wa Gaza (Julai 12)© UNICEF/NYHQ2014-0911/El Baba

Vituo vya afya vipatavyo 18 vimeharibiwa Gaza, huku wahudumu 20 wa afya wakijeruhiwa wakati mashambulizi ya Israel dhidi ya wanamgambo wa Hamas yakiendelea. Taarifa kamili na Grace Kaneiya. (Taarifa ya Grace) Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa limesikitishwa mno na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, likitoa wito kwa pande zote katika [...]

22/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Jarida | Kusoma Zaidi »

Kila kisa cha utumikishwaji wa watoto vitani ni janga kwa jamii: MONUSCO

Kusikiliza / Martin Kobler@UN

Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ikitolewa leo kuhusu hali ya watoto walioathirika na mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Mkuu wa Ujumbe wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, Martin Kobler, amesema kwamba mbali na takwimu, kila kisa cha uhalifu huo ni janga kwa mtoto, kwa familia na kwa jamii nzima. Amesema [...]

21/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Utumikishaji watoto katika vita nchini DRC umeendelea kua tatizo sugu- Ripoti

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Ripoti ya 5 Ya Katibu Mkuu wa Umoja Wa Mataifa kuhusu hali ya watoto walioathirika na mzozo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, imeonyesha kuwa tatizo tatizo sugu nchini humo kati ya mwaka 2010 na 2013. Ripoti hiyo imesema kuwa watoto waliathiriwa na mawimbi kadhaa ya mapigano, hususan katika mikoa ya mashariki mwa nchi [...]

21/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mashambulizi yanayoendelea Gaza hayakubaliki: Ban Ki Moon

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@UN Photo

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara yake nchini Misri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, amesema hali inayoendelea nchini Gaza haiwezi kukubaliwa tena. Ameipongeza nchi ya Misri kwa jitihada zake katika utaratibu wa amani, akisema kwamba mchango wa Misri umekuwa wa kuonekana tangu zamani katika kujenga amani ya Mashariki ya [...]

21/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ujerumani yapiga jeki UNICEF kuendeleza haki za watoto Libya

Kusikiliza / Watoto wakiingia shule iliyomo ndani ya tenti la UNICEF katika kambi la Shousha mpakani mwa Libya na Tunisia. UNICEF/Heifel Ben Youssef.(UN News Centre)

Serikali ya Ujerumani imetoa kiasi cha euro 100,000 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Watoto, UNICEF, ili kuliwezesha shirika hilo kutekeleza miradi yake nchini Libya. Kiasi hicho cha fedha kitasaidia kufanikisha kampeni ya kitaifa inayotekelezwa sasa nchini Libya ya lengo la kuwezesha watoto kutambua haki zao. Makabidhiano ya fedha hizo yamefanyika mjini Tripoli [...]

21/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la haki za binadamu kujadilia hali ya Gaza

Kusikiliza / Human Rights

Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linatazamia kukutana jumatano wiki hii kwa ajili ya kujadiili hali ya mambo katika ukanda wa Gaza. Kikao hicho kimeitishwa kwa pamoja kati ya Misri na Pakistan na kuungwa mkono na nchi wanachama 15 za baraza hilo. Miongoni mwa nchi hizo zilizounga mkono ni pamoja na China, [...]

21/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakichukuwa dakika ya ukimya kwa walio athirika na ndege MH17. UN Photo/Loey Felipe

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja, limepitisha azimio la kulaani vikali tukio la kutunguliwa kwa ndege ya Malaysia, MH17, mnamo Julai 17 kwenye jimbo la Donetsk Oblast, nchini Ukraine, ambalo lilisababisha vifo vya watu 298. Baraza la Usalama limepeleka tena risala za rambi rambi kwa familia za wahanga wa tukio [...]

21/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban Ki-moon ahimiza Misri kuwezesha utaratibu wa amani Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alipokuta na Sheikh Sabah Khaled Al-Hamad Al-Sabah.Picha ya UM//Eskinder Debebe

Akiendelea na ziara yake Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa MAtaifa Ban Ki-moon amewasili Misri kwa ajili ya kukutana na viongozi mbalimbali, na kuchagiza juhudi za kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Palestina. Utaratibu huo unaongozwa na Misri. Kwa mujibu wa msemaji wake, Katibu Mkuu anatarajia kukutana na Rais na [...]

21/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vikundi vya Saccos ni mbinu mojawapo ya kukabiliana na umaskini Tanzania

Kusikiliza / MDGS

Nchini Tanzania vikundi vya kuweka na kukopa maarufu saccos vimemea miaka ya hivi karibuni, vikundi hivi ni sehehmu ya mipango ya serikali chini ya mkakati wa taifa wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini mkukuta ulobuniwa mwaka 2005 kutimiza lengo la kwanza la millennia la kupambana na umaskini ulokithiri na baa la njaa. (Makala ya Rashid [...]

21/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yaonya kuhusu maambukizi ya virusi vya Ebola magharibi mwa Afrika

Kusikiliza / Mhudumu wa afya akimhudumia mgonjwa ambaye anawezekana kuwa na ugonjwa wa Ebola. (UNIFEED video capture)

Shirika la mpango wa chakula na kilimo, FAO, limesema kuwa idadi kubwa ya wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini huko Magharibi mwa Afrika huenda wakaambukizwa virusi vya Ebola kutokana na tabia yao ya kula  nyama mwitu. FAO imewataja popo walao matunda kama wanyama wanaoshukiwa kubeba virusi vya Ebola bila kuonyesha dalili zozote za ugonjwa huo. FAO [...]

21/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Gaza: UNRWA yasambaza misaada kutoka Dubai kwa wakimbizi 100,000 wa Palestina

Kusikiliza / Mtoto huyu wa kipalestina asimama nje ya nyumba iliokuwa nyumba yao iliyoharibiwa baada ya mashambulizi ya angani kambini mji wa Rafhakusini mwa Ukanda wa Gaza (Julai 12)© UNICEF/NYHQ2014-0911/El Baba

Wakati raia wanaotafuta hifadhi katika kambi za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA, wanatarajiwa kufika 100,000, mashirika ya kibinadamu yameshirikiana ili kusambaza misaada kutoka Dubai kwa njia ya ndege. Taarifa zaidi na John Ronoh. (Taarifa ya Ronoh) Kituo cha Kibinadamu cha Kimataifa (IHC), kilichopo Dubai, ni Shirika lisilo la kiserikali [...]

21/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ziarani Mashariki ya Kati, Baraza la Usalama lakutana usiku kuhusu Gaza

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama. Picha/UM

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, anendelea na ziara yake ya kuendeleza juhudi za kutafuta amani ya kudumu kwa mzozo wa Gaza, ambao umejadiliwa hadi usiku wa manane na Baraza la Usalama. Taarifa kamili na Grace Kaneiya Taarifa ya Grace Bwana Ban ambaye leo amekuwaKuwait, anatarajiwa pia kuelekea Cairo, Ramallah naAmman. Wakati [...]

21/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashirika 10 yatuzwa kwa juhudi za kupambana na Ukimwi

Kusikiliza / Picha@UNAIDS

Mashirika kumi ya kijamii yameshinda tuzo ya Red Ribbon ya mwaka 2014, kutokana na juhudi za kutoa msukumo katika kupunguza athari za maradhi ya Ukimwi. Tuzo hiyo imetolewa kwenye kikao maalum cha kongamano la kimataifa la 20 kuhusu Ukimwi mjini Melbourne, Australia. Mashirika yaliyoshinda tuzo hiyo mwaka huu yametoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC, [...]

21/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu wa asili hawawezi kupuuzwa katika malengo ya maendeleo endelevu

Kusikiliza / Mshiriki wa mkutano wa watu wa asili wa Umoja wa Mataifa.Picha/Devra Berkowitz

Malengo mapya ya maendeleo endelevu yasiwe hatua ya kurudi nyuma kwa watu wa asili, wameonya wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili. Wito huo umetolewa baada ya mkutano uliofanywa wiki iliyopita mjini New York na Kamati ya kuandaa malengo ya maendeleo endelevu, ambayo yatawasilishwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu mwezi Septemba. [...]

21/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana usiku kuhusu machafuko Gaza

Kusikiliza / Baraza la Usalama. Picha:UN Photo/Paulo Filgueiras

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumapili usiku wamekutana kuhusu hali Mashariki ya Kati, na kuelezea masikitiko yao kuhusu kuongezeka machafuko. Katika taarifa iliyosomwa na rais wa Baraza hilo, Richard Gasana, wanachama wa Baraza la Usalama wametoa wito sheria ya kimataifa ya kibinadamu iheshimiwe, ikiwemo ulinzi wa raia. "Wanachama wa Baraza la [...]

20/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ataka machafuko mapya Sudan Kusini yakomeshwe

Kusikiliza / Dr. Reik Machar, kiongozi wa waasi Sudan Kusini alipokutana na Adama Dieng na Navi Pillay kabla ya makubaliano ya Juni 10 . Picha ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa sana na shambulizi lililofanywa leo na vikosi vya waasi wa SPLA Upinzani vilivyo chini ya Makamu wazamani wa rais, Riek Machar kwenye mji wa Nassir, jimbo la Upper Nile, Sudan Kusini. Shambulizi hilo ni la kwanza tangu serikali na Bwana Machar waliporejelea makubaliano ya kusitisha [...]

20/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ziarani, Ban akutana na viongozi wa Mashariki ya Kati Rais Abbas

Kusikiliza / Ban na Rais Abbas wakiwa Qatar: Picha ya UM/Eskinder Debebe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa ukanda wa Mashariki ya Kati, akiwemo Rais Mahmoud Abbas wa Palestina na Amiri wa Qatar. Baadaye, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Khalid Bin Mohamed Al-Attiyah, amekutana na waandishi wa habari na kuelezea kusikitishwa kwake [...]

20/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban alaani utesaji wa makundi ya walio wachache Mosul, Iraq

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon. @UN-Maktaba

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali utesaji wa kupangwa wa makundi ya walio wachache nchini Iraq, unaotekelezwa na wafuasi wa waasi wa Jamhuri ya Kiislamu Iraq (IS) na makundi husika yaliyojihami. Bwana Ban amesikitishwa hasa na ripoti za vitisho kwa Wakristo Mosul na maeneo mengine yanayodhibitiwa na ISIL nchini Iraq, vikiwemo [...]

20/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wafugaji wakimbizi wasaidiwa na Fao Waziristan Kazkazini nchini Pakistan

Kusikiliza / Picha ya FAO

Mapigano yanayoendelea kwenye maeneo ya milima ya Waziristan Kazkazini, nchini Pakistan, yamesababisha takriban watu 800,000 kukimbia makwao. Shirika la Chakula na Kilimo FAO linakadiria kwamba asilimia 70 ya watu wamekimbia na mifugo wao, na kwa hivyo hawakuweza kupanda magari au basi, na wakalazimika kutembea kwa mwendo mrefu. Mifugo wengi, hususan ng’ombe, wamefariki wakati wa safari [...]

18/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNSMIL yalaani mauaji ya mbunge nchini Libya, ikihimiza ulinzi wa raia

Kusikiliza / Nembo ya UNSMIL

Ujumbe wa Umoja wa Matiafa nchini Libya, UNSMIL umelaani vikali kuuawa kwa mbunge Fariha Barkawi huko Derna mashariki mwa Libya, mnamo Alhamisi ya Julai 17. UNSMIL imelaani ukatili unaoendelea Benghazi na Tripoli, ambao unasbabisha majeruhi miongoni mwa raia na kupelekea watu kuhama makaazi yao, huku ikisisitiza wito wa kumaliza ukatili. Aidha, UNSMIL imesikitishwa na mauaji [...]

18/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali inaendelea kusambaratika Ukanda wa Gaza- Ripoti ya UNRWA

Kusikiliza / Picha@UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA kupitia msemaji wake Chris Gunness, limetoa ripoti mpya kuhusu  hali kwenye ukanda wa Gaza kufikia sasa. UNRWA imesema kuwa, kwa saa 24 zilizopita, idadi ya watu waliokimbia na kutafuta hifadhi ndani ya kituo cha UNRWA mjini Gaza imeongezeka maradufu toka 22,000 na kufikia zaidi [...]

18/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Msemaji wa WHO afariki kwenye ajali ya ndege ya Malaysia

Kusikiliza / Glenn Thomas, Picha ya WHO

Watu 298 wamefariki dunia kwenye ajali ya ndege ya Malaysia iliyotokea tarehe 17, Julai, akiwemo Glenn Thomas, mfanyakazi wa Shirika la Afya Duniani, WHO. Glenn Thomas ambaye alikuwa msemaji wa WHO alipanda ndege hiyo kwa ajili ya kuhudhuria kongamano la kimataifa kuhusu ukimwi litakaloanza wiki ijayo, nchini Australia. Gregory Hartl, msemaji wa WHO, amesema Glenn [...]

18/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Leo Julai 18 ni siku ya Mandela duniani:aenziwa

Kusikiliza / Hafla ya upanzi wa mti wa Mandela (Picha/um/Eskinder Debebe/NICA)

Kila mwaka, tarehe 18 Julai imekuwa ikiadhimishwa kama Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, tangu siku hiyo ilipoanzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Novemba 2009, ili kuenzi mchango wa Hayati Nelson Mandela kwa kukuza demokrasia, haki kwa watu wa rangi zote na maridhiano. Mwaka huu, siku hiyo imeadhimiswa kwa mara ya kwanza [...]

18/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Urithi wa Mandela unaendelezwa

Kusikiliza / Nelson Mandela akiwa Umoja wa Mataifa (Picha ya UM/faili)

Leo Julai 18 ni siku ya kimataifa ya Mandela duniani. Mandela atakumbukwa kwa sifa nyingi na mchango wake kwa dunia. Mandela amesifika katika sio tu nchi yake lakini duniani kote kwani aliyagusa maisha ya wengi. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo inayomulika urithi wa Mandela.

18/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kuhusu Ukraine kufuatia ajali ya ndege

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakati wa dakika ya ukimywa kuwakumbuka waliopoteza maisha yao.Picha/Loey Felipe/NICA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kuhusu hali nchini Ukraine, kufuatia ajali ya ndege ya Malaysia hapo jana mashariki mwa Ukraine, kwenye eneo linalodhibitiwa na waasi. Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina) Mwanzoni mwa mkutano wa leo, Rais wa Baraza la Usalama, Richard Gasana, amewasilisha ujumbe wa rambirambi za wanachama [...]

18/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC haifuatilii viongozi wa Afrika tu, bali wa dunia nzima: Msemaji wa ICC

Kusikiliza / Fadi El-Abdallah, Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC. Picha@UNIFEED

Wakati Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imeaadhimisha hapo jana miaka 16 tangu kusainiwa kwa mkataba wa Roma ulioiunda mahakama hiyo, msemaji wake, Fadi El-Abdallah, ameiambia Redio ya Umoja wa Mataifa kwamba ICC imeshaaminika na nchi nyingi duniani, kwani tangu kuwepo kwa ICC mwaka 2002, idadi ya nchi wanachama imeongezeka kutoka 60 hadi 122. "Tumeona [...]

18/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Tuzo ya Mandela yazinduliwa rasmi, Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela

Kusikiliza / Mti wenye kuadhimisha Siku ya Mandela. Picha@UN Photo.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limekutana mahsusi kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela, kuenzi mchango wa Hayati Nelson Mandela kwa kukuza demokrasia, haki kwa watu wa rangi zote na maridhiano. Katika mkutano huo, tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Nelson Rolihlahla Mandela pia imezinduliwa rasmi. Leo Julai 18 ni miaka 96 tangu [...]

18/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya raia 1,500 wameuawa Iraq mwezi Juni

Kusikiliza / Familia hii ilikimbia mapigano Mosul, Iraq na wako karibu na kituo cha Khazair.Wanamatumaini ya kukakaa mji wa Erbil hadi itakapokuwa salama kurudi nyumbani(Picha@UNHCR/R.Nuri

Umoja wa Mataifa umeyashutumu makundi yenye silaha nchini Iraq kwa kutekeleza vitendo vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, mwingine ambao huenda ukawa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Ripoti iliyoandaliwa na Ofisi ya Haki za Binadamu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI, imesema kuwa raia wapatao zaidi ya 1,500 waliuawa na wengine zaidi [...]

18/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto 10,000 wa Syria wamezuiwa kupata matibabu: UNICEF

Kusikiliza / syrianchildren

Serikali ya Syria imezuia usambazaji wa dawa na vifaa vingine vya kujisafi kwa takriban watoto 10,000 wanaoishi katika mji uliozingirwa wa Mouadamiya al-Sham, katika eneo la Damascus, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Mji huo ulioko mwendo wa kilomita 8 kutoka Damscus, umezingirwa tangu mwezi Agosti mwaka jana, na kulingana na UNICEF, hali [...]

18/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban awakutanisha wawakilishi wapya kuhusu Syria na wanahabari

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akutana na Staffan de Mistura(kushoto) na Ramzy Ezzeldin Ramzy katika makao makuu(Picha/UM/Eskinder Debebe/NICA)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amemtambulisha Mwakilishi wake mpya kuhusu Syria, Staffan de Mistura na makamu wake Ramzy Ezzeldin Ramzy kwa waandishi wa habari. Akiwatambulisha wawili hao mjini New York, Bwana Ban ameelezea kubahatika kuweza kuwa na imani na hekima ya wanadiplomasia hao, ambao amesema watasafiri kwenda Syria, nchi za ukanda [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kula wadudu kuepukana na njaa

Kusikiliza / Kuuza wadudu wanoitwa Mopane, Afrika ya Kati. Picha@ FAO

Lengo la kwanza katika malengo ya maendeleo ya milenia ni kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa. Wakati malengo hayo yanafika ukomo mwakani, bado mtu mmoja kati ya wanane ameathirika na njaa duniani. Mashirikia ya kimataifa yamejaribu kubaini suluhu mbadala ili kutimiza mahitaji ya chakula kwa wote. Njia moja isiyo ya kawaida ni kubadilisha milo yetu na [...]

17/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mpango wawekwa wa hatua za dharura kulinda urithi wa utamaduni wa Iraq

Kusikiliza / Erbill Citadel..yenye umri wa miaka 8000, Iraq. Picha:UNESCO

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limefanya leo mashauriano na wataalam wa utamaduni wa Iraq na wa kimataifa, na kuafikia mpango wa hatua za dharura za kulinda utajiri wa urithi wa kitamaduni wa Iraq. Mpango huo unanuia kupata uungwaji mkono wa wadau wote, yakiwemo mashirika ya kitaifa na kimataifa, wahudumu wa kibinadamu, wachuuzi wa [...]

17/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Djinit amrithi Mary Robinson kama Mjumbe wa Ban wa Maziwa Makuu

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon na Said Djinit wa Algeria,  Mjumbe Mteule katika Ukanda wa Maziwa Makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake katika Ukanda wa Maziwa Makuu. Bwana Djinnit anaichukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye amekubali wadhifa mpya aliopewa na Katibu Mkuu kama Mjumbe wake kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa [...]

17/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMA yakaribisha ukaguzi wa matokeo ya uchaguzi wa urais Afghanistan

Kusikiliza / Afghanistan elections3

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umekaribisha kuanza kwa ukaguzi wa matokeo ya kura ya kuwania urais wa mwaka 2014 nchini humo. Ukaguzi huo unafuatia makubaliano yaliyokifikiwa na wagombea wawili wa urais nchini Afghanistan, Dkt. Abdullah Abdullah na Dkt. Ashraf Ghani. Makubaliano hayo yalifikiwa kwa juhudi za Waziri wa Mambo ya Nje Marekani, [...]

17/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNRWA yalaani kuwekwa kwa silaha katika shule Gaza

Kusikiliza / Watoto kutoka Yarmouk. UNRWA/Rami Al-Sayyed

Takriban roketi 20 zimepatikana katika shule iliyo wazi inayosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina, UNRWA. Silaha hizo zilipatikana na maafisa wa UNRWA mnamo Jumanne wakati wa shughuli za kawaida za upelelezi katika majengo yao. Hadi sasa haijabainika ni nani alitega silaha hizo. UNRWA imelaani kitendo hicho katika shule ikiongeza [...]

17/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha usitishaji mapigano kwa sababu za kibinadamu Gaza

Kusikiliza / Robert Serry, Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mashariki ya Kati ziarani Gaza/Picha@ UN Photo/Shareef Sarhan

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekaribisha hatua iliyochukuliwa mapema leo na Israel kusitisha mapigano kwa muda wa saa tano ili kuruhusu shughuli za kibinadamu kwa raia wa Gaza, zikiwemo usambazaji misaada na kufanyia ukarabati miundo mbinu muhimu kama umeme na maji. Usitishaji mapigano huo uliotokana na juhudi za upatanishi za Mratibu [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali nchini Libya ni ya kutia hofu, asema Mitri

Kusikiliza / Tarek Mitri, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya. UN Photo/Devra Berkowitz

Baraza la Usalama leo limekutana kujadili kuhusu Lybia na kazi za Ujumbe wa Umoja wa Matiafa nchini humo, UNSMIL. Tarek Mitri, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNSMIL, amewaambia wanachama wa baraza hilo kwamba raia wa Lybia wanazidi kutiwa hofu kadri mzozo unavyoendelea kuongezeka Lybia. " Kasi ya mabadiliko [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo Afrika yamulikwa kwenye Baraza Kuu

Kusikiliza / Kikao cha Baraza Kuu Picha/UM

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya mdahalo kuhusu kuendeleza kwa uwekezaji barani Afrika na mchango wake katika kufikia malengo ya maendeleo ya bara la Afrika, yakiwemo kutokomeza umaskini na kufikia ukuaji na maendeleo endelevu na jumuishi ya kiuchumi. Akizungumza wakati wa mdhahalo huo, rais wa Baraza Kuu John W. Ashe, amesema kuwa katika [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zakumbushwa kuhusu wajibu wa kulinda sheria ya kimataifa

Kusikiliza / Sang-Hyun-Song, Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.
UN Photo/Paulo Filgueiras

Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Sang Hyun Song, ameziomba nchi zote duniani zishirikiane kupambana na ukwepaji wa sheria, ikiwa leo ni siku ya sheria ya kimataifa duniani. Taarifa kamili na Amina Hassan. Raisi Sang Hyun Song amekumbusha kwamba, tarehe 17, Julai, mwaka 1998, nchi 120 zilitia saini kwenye maktaba wa Roma uliounda [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ufadhili zaidi unahitajika kuwahudumia wakimbizi waSudan Kusini walioko Uganda:WFP

Kusikiliza / Wakimbzi kutoka Sudan kusini wawasili Uganda Picha/WFP/Tine Frank

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limepaza sauti likiomba msaada zaidi ili liweze kushughulikia wakimbizi wanaoendelea kumiminika Kaskazini mwa Uganda kutoka Sudan Kusini. Taarifa kamili na John Kibego wa Redio washirika ya Spice FM, nchini  Uganda.  (Tarifa ya Johhn Kibego)  Shirika la WFP linaomba kupigwa jeki zaidi wakati ripoti ya Shirika la Umoja wa [...]

17/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Awasili Nchini CAR

Kusikiliza / Abdoulaye Bathily @UN Photo/Marco Dormino

Mwakilishi  Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  kuhusu Jamhuri Ya Afrika ya Kati (CAR), Abdoulaye Bathily, aliye pia mwanachama wa kamati ya mapatano ya kimataifa kuhusu mgogoro wa Jamhuri ya Afrika ya Kati,  amewasili nchini Bangui- mji mkuu wa nchi hiyo ambapo atashiriki kwa matayarisho ya Kongamano la Brazzaville. Bwana Bathily ameeleza kuwa [...]

16/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuna matumaini ya amani CAR: Ladsous

Kusikiliza / Hervé Ladsous, Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani
Picha: UN Photo/Paulo Filgueiras

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Jumatano ya Julai 16 jioni limejadili kuhusu hali ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati likiangazia maandalizi ya kuunda ujumbe wa umoja wa mataifa nchini humo, MINUSCA. Herve Ladsous, mkuu wa idara ya operesheni za kulinda amani kwenye Umoja wa Mataifa, DPKO, amesema kwamba kuna matumaini ya [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ki Moon akutana na rais wa Haiti na Jamhuri ya Dominika

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akihutubia Seneti ya Jamhuri ya Dominika. UN Photo/Paulo Filgueiras

Akihitimisha ziara yake nchini Haiti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amekutana na rais wa nchi hiyo, Bwana Logan Martelly akiwapongeza raia wa Haiti kwa bidii yao katika kujenga upya nchi baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililoathiri nchi yao mwaka 2010, na licha ya hali mbaya ya kiuchumi. Amesifu serikali ya [...]

16/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu dhoofu kwa maelfu Sudan na Sudan Kusini: Amos

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA Valerie Amos.(Picha@UN Photo/Eskinder Debebe)

Mkuu wa Ofisi ya kuratibu masuala ya kibidamu na misaada ya dharura, Valerie Amos, amesema kuwa hali ya kibinadamu katika nchi za Sudan na Sudan Kusini, inaendelea kuzorota kwa mamia ya maelfu ya watu. Bi Amos, ambaye awali amelihutubia Baraza la Usalama, amewambia waandishi wa habari mjini New York kuwa mamia ya maelfu ya watu [...]

16/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lahofia hali Sudan na Sudan Kusini

Kusikiliza / Mtoto akiwa kambini Tomping Juba, Sudan Kusini. Picha ya UM/Eskinder Debebe

Wanachama wa Baraza la Usalama, ambao leo wamekutana kujadili hali Sudan na Sudan Kusini, wameelezea kusikitishwa na hali ya usalama na kibinadamu katika majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile nchini Sudan, na kuzitaka pande zinazozozana kusitisha uhasama na kuanza mazungumzo ya moja kwa moja bila masharti yoyote. Baraza hilo pia limezitaka pande zinazozozana kuruhusu [...]

16/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya kigaidi Afghanistan

Kusikiliza / Kikao cha baraza la usalama wakati mkutano kujadili hali nchini Afghanistan. Picha/UM/Amanda Voisard

Baraza la Usalama limelaani vikali leo shambulizi la kujitoa mhanga lililotokea tarehe 15 Julai, maeneo ya Paktika, nchini Afghanistan pamoja na mashambulizi yaliyotokea mjini Kabul, ambayo yalidaiwa na kundi la Wataliban. Mashambulizi hayo yamesababisha vifo vya wananchi wengi wakiwemo watoto. Baraza la Usalama limepeleka rambirambi zake kwa familia za wahanga, raia na serikali ya Afghanistan. [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNIDO yatoa ripoti ya takwimu kuhusu uchimbaji migodi

Kusikiliza / Mashine ya uchimbaji (Picha@UNIDO)

Uzalishaji wa kimataifa kutokana na shughuli za uchimbaji migodi na sekta ya utoaji huduma ulipanda kwa kiwango kidogo cha asilimia 1.7, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO. Ripoti hiyo ya takwimu za kimataifa kuhusu uchimbaji migodi na huduma huchapishwa kila miaka miwili, na hutoa takwimu [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki ya binadamu ya faragha ni lazima ilindwe popote

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay(Picha ya UM)

Ufuatiliaji unaofanywa dhidi ya watu na serikali na kampuni kubwa za biashara bila idhini ya watu binafsi, ni ukiukwaji wa haki zao, ikiwemo haki ya kuwa na faragha, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyochapishwa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa. Taarifa kamili na Amina Hassan Ripoti hiyo yenye kichwa, "haki ya [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 19 kati ya milioni 35 hawajui kama wana virusi vya HIV:UNAIDS

Kusikiliza / Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé,@UNAIDS

Ripoti mpya ya Shirika linalohusika na HIV na Ukimwi, UNAIDS, imeonyesha kuwa takriban watu milioni 19 kati ya watu wapatao milioni 35 wanaoishi na virusi vya HIV kote duniani, hawajui kama wana virusi hivyo. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Michel Sidibé, juhudi zinapaswa kuongezwa kwa njia bora zaidi ili kuondoa tofauti baina ya [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola milioni 982 zahitajika kutimiza mahitaji ya kibinadamu Sudan

Kusikiliza / Watoto hawa wacheza katika kituo cha jamii kilichojengwa na UNAMID katika kambi ya wakimbizi wa ndani , Khor Abeche, kusini Darfur (Picha/UM/Albert González Farran/NICA)

Kuwepo kwa ongezeko kubwa la mahitaji ya kibinadamu nchini Sudan katika kipindi cha miezi sita ya mwaka huu kumelazimu kupitiwa upya mpango wa misaada ya dharura iliyowekwa hapo awali. Taarifa kamili na John Ronoh. (Taarifa ya John Ronoh) Mashirika ya misaada kwa ajili ya Sudan yanasema kuwa kiasi cha dola za Marekani milioni 982 kinahitajika [...]

16/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Idadi ya maambukizi ya kipindupindu yapungua Haiti

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon na mkewe atembelea familia Los Palmas Picha ya UM/Paulo Filgueiras

Idadi ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti inaendelea kupungua lakini matatizo ya maji safi na usafi wa mazingira yanaathiri kasi ya maendeleo, na kusababisha ongezeko la magonjwa yatokanayo na maji , amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa. Bwana Ban aliwasili katika Kisiwa hicho cha Karibea hapo Jumatau katika ziara yake ya kuchagiza [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNFPA yasaidia kupaza sauti ya mkunga Tanzania

Kusikiliza / Elvina-Mkunga Tanzania. Picha@UNFPA

Uimarishaji wa afya ya uzazi ni lengo nambari tano katika malengo ya milenia ambayo yatafikia ukomo mwakani. Ili kutimiza lengo hili ni muhimu kuhakikisha kwamba watoa huduma wana vifaa vinavyohitajika na kwamba idadi ya watoa huduma, kama vile wakunga, inakwenda sambamba na walio na mahitaji. Katika nchi zinazoendelea, bado lengo hili haliijafikiwa kikamilifu kwa sababu [...]

15/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMA yalaani mashambulizi mjini Kabul

Kusikiliza / Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA Ján Kubiš Picha ya Fardin Waezi / UNAMA

Umoja wa mataifa umelaani shambulizi la kujitoa mhanga lililosababisha vifo vya watu 43 wakiwemo watoto 8 Idadi ya vifo kutokana na shambulizi hilo ambalo lilifanyika katika soko la Urgun jimbo la Paktika kusini mashariki mwa Afghanistan, imelifanya kuwa baya zaidi mwaka huu wa 2014, ambapo raia 67 pia wamejeruhiwa. Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa [...]

15/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Madawa ya kulevya yanaathiri ukuaji wa uchumi na maendeleo

Kusikiliza / UNODC_DRUGS

Biashara haramu ya madawa na mashirika ya uhalifu yanaathiri maisha ya watu na jamii kwa ujumla, amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon  katika ujumbe wake maalum alioutuma kwenye mkutano wa viongozi kuhusu tatizo la madawa ya kulevya duniani.  Mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Uchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa, ECOSOC, [...]

15/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yafungua kituo cha ukanda kuratibu shughuli za kupambana na Ebola

Kusikiliza / Harakati za kudhibiti Ebola nchini Guinea-Conakry. Picha @WHO

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza leo tarehe 15 Julai kufunguliwa kwa kituo cha ukanda ambacho kitaratibu shughuli zote za kupambana na mlipuko wa Ebola. Takwimu zilizotolewa na shirika hilo leo zinaonyesha kwamba idadi ya watu walioathirika na Ebola inakaribia kufikia elfu moja, huku watu mia 600 kutoka nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone [...]

15/07/2014 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ziarani Nigeria, Malala ataka wasichana wa Chibok waachiliwe

Kusikiliza / Malala Yousafzai Picha ya UM/faili

Malala Yousafzai, mtoto wa Kipakistani aliyenusurika kifo aliposhambuliwa na wanamgambo wa Taliban wanaopinga elimu ya watoto wa kike, amelitaka kundi la kigaidi la Boko Haram kuwaachilia huru wasichana waliotekwa nyara kutoka shule ya Chibok, kaskazini mwaNigeria. Malala ambaye yupo ziarani nchiniNigeria, alikutana hapo jana na wazazi wa wasichana hao, wawakilishi wa mashirika ya umma na [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban Ziarani Haiti

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa Los Palmas atembelea familia na kituo cha maji Picha ya/Paulo Filgueiras/NICA ID:594793

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, ambaye yupo ziaraniHaiti, leo anatarajiwa kukutana na timu ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MINUSTAH. Hii leo pia Bwana Ban anatarajiwa kuzindua rasmi kituo cha michezo kiitwacho  "Michezo kwa Tumaini"nchini humo, akishirikiana na  rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bacth. Hapo jana [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unene uliokithiri utotoni linazidi kuwa tatizo la afya duniani

Kusikiliza / Nembo ya WHO

Uzito wa kupindukia miongoni mwa watoto linakuwa tatizo la afya ya umma katika nchi nyingi zinazoendelea, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. WHO imesema idadi ya watoto wenye unene wa kupindukia kote duniani imeongezeka kutoka milioni 31 mwaka 1990 hadi milioni 44 wakati huu, huku nchi zinazoendelea zikishuhudia kiwango cha ongezeko kilicho asilimia [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNRWA yaomba kusitishwa kwa mauaji ya raia Gaza

Kusikiliza / Kufuatia mzozo UNRWA imetangaza hali ya dahrura katika maeneo matano ya ukanda wa Gaza(Picha@UNRWA)

Kuna uwezekano wa maafa na uharibifu zaidi Gaza iwapo juhudi za kusitisha mzozo kati ya Israeli na Palestina hazitafaulu. Hiyo ni kauli ya Shirika la kuwasaidia wakimbizi wa Palestina UNRWA, ambalo limesema kwamba kufikia sasa Wapalestina 174 wameuwawa na zaidi ya 1,100 kujeruhiwa tangu Israeli ilipoanza mashambulizi Gaza. Akiwahutubia waandishi wa habari msemaji wa UNRWA, [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu milioni 10 Yemen waathirika na njaa

Kusikiliza / Yemen. Picha@OCHA/Eman Al-Awami(UN News Centre)

Utafiti uliofanyika nchini Yemen na Shirika la Mpango wa chakula Duniani WFP na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Watoto UNICEF, unaonyesha kwamba bado watu milioni 10, yaani asilimia 40 ya watu waliopo Yemen, wanakumbwa na ukosefu wa usalama wa chakula.  Taarifa Zaidi na Priscilla Lecomte Kwa mujibu wa WFP, katika watu hawa, ni [...]

15/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Agostinho Zacarias wa Musumbiji kuwa Naibu Mratibu wa UM Burundi

Kusikiliza / Agostinho Zacarias, picha ya UNDP

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon leo amemteua Bwana Agostinho Zacarias kuwa Naibu Mratibu Maalum kwa Muda, na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi. Bwana Zacarias pia atachukua wadhifa wa Mratibu Mkaazi na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP nchini humo akichukua nafasi ya Bi. Rosine [...]

14/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Matumaini mapya kwenye vita dhidi ya ukatili wa kijinsia DRC

Kusikiliza / Wanawake wakikaa pamoja nje ya Heal Africa Transit Centre ya wahanga wa ukatili wa kingono. Picha@Aubrey Graham/IRIN

Jeannine Mabunda Lioko Mudiayi ameteuliwa leo na raisi Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kuwa Mshauri wa Raisi kuhusu Ukatili wa Kingono na utumikishwaji wa Watoto. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu kuhusu ukatili wa kingono katika vita, Zainab Hawa Bangura pamoja na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu [...]

14/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wavuvi waokolewa na maisha ya deni, India

Kusikiliza / wavuvi wadogo wadogo kwenye eneo la tamil Nadu - India

Wakati malengo ya maendelo ya milenia yanatarajia kufikia ukomo mwakani, Umoja wa Mataifa umezindua ripoti kuhusu mafanikio yaliyopatikana. Lengo la kwanza likiwa ni kutokomeza umaskini uliokithiri na njaa, na kupunguza kwa nusu idadi ya watu maskini ifikapo mwaka 2015, takwimu zinaonyesha kwamba lengo hili limetimia. Nchini India, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD [...]

14/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa kuongeza vigezo vya biashara ya viungo vya pilipili

Kusikiliza / Viungo. Picha@FAO/Daniel Beaumont

Viungo kama pilipili manga, oregano ama majani ya chai vina hatari ya kuambukizwa na vidudu mbali mbali, kwa mujibu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa inayohusu vigezo vya vyakula, Codex Alimentarius.  Majukumu ya Kamati hiyo ambayo imeundwa na Shirika la Chakula na Kilimo FAO na Shirika la Afya Duniani WHO ni kulinda afya ya watumiaji [...]

14/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sitisha mapigano kwanza Gaza kuokoa maisha ya wananchi: UNOCHA

Kusikiliza / Mkaazi wa Palestina akipita mbele ya askari wa Israeli mashariki mwa Jerusalem. Picha: IRIN/Andreas Hackl(UN News Centre)

Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, James Rawley, amesema kwamba amesikitishwa na mapigano ya wiki hii ambayo yamewaathiri zaidi wananchi wa kawaida wa Ukanda wa Gaza. Rawley amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea shule iliyopigwa bomu kwenye ukanda huo, akiandamana na Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuwasaidia Wakimbizi [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha azimio la Baraza la Usalama kuhusu Syria

Kusikiliza / Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq Picha@UM

Akizungumza baada ya kupitishwa kwa azimio la Baraza la Usalama kuhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu nchini Syria, msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema katibu mkuu wa umoja wa mataifa amekaribisha azimio hilo ambalo litawezesha mashirika ya umoja wa mataifa kufikisha misaada kwa walengwa nchini humo kwa njia ya moja kwa moja zaidi. [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Mary Robinson kuwa Mjumbe Maluum wa mabadiliko ya tabianchi

Kusikiliza / Bi Mary Robinson Picha@UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametangaza kumteua Bi Mary Robinson wa Ireland kuwa Mjumbe wake Maalum kuhusu mabadiliko ya tabianchi. Bi Robinson ataendelea kuhudumu kama rais wa wakfu wake wa Climate Justice. Kutokana na uzoefu katika kazi ya wakfu wake, Bi Robinson anatarajiwa kusisitiza mtazamo unaowajali watu katika mikakati inayojikita kwa [...]

14/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laazimia kuanzisha utaratibu wa ukaguzi wa misaada ya kibinadamu Syria

Kusikiliza / Kikao cha baraza la Usalma @NICA

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja wamepitisha azimio la kuanzishwa kwa utaratibu wa ukaguzi wa shughuli za upakiaji, usafirishaji na upekuzi wa shehena zote za misaada ya kibinadamu ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake kwa ajili ya raia wa Syria.   Akitangaza matokeo ya kura [...]

14/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ITU na UN Women watangaza tuzo mpya ya teknolojia na usawa wa jinsia

Kusikiliza / ITU

Shirika la Kimataifa la Mawasiliano, ITU na lile la masuala ya wanawake, UN Women, kwa pamoja yametangaza kuanzisha tuzo mpya ya kimataifa kwa ajili ya kutambua juhudi bora  zaidi katika kutumia teknolojia ya mawasiliano (ICT) kuendeleza usawa wa jinsia. Tuzo ya GEM-TECH, itawatambua viongozi na mashirika yanayotumia uwezo wa teknolojia kuleta mabadiliko. Tuzo hiyo itatolewa [...]

14/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNAMA yakaribisha kundi la marekebisho na Ubia wa Uchaguzi Afghanistan.

Kusikiliza / Picha: UNAMA News Centre

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umekaribisha makubaliano yaliyokifikiwa na wagombea waliwili wa urais nchini Afghanistan, Dkt. Abdullah Abdullah na Dkt. Ashraf Ghani kwa ajili ya kutafuta suluhu kwa mkwamo uliotokea baada ya uchaguzi na hivyo kuruhusu timu ya marekebisho na ubia kurejea na kushughulikia utaratibu wa uchaguzi nchini humo. Makubaliano hayo yalifikiwa [...]

14/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na mapigano ya Gaza

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@UN Photo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa bado anaingiwa na woga kuhusiana na hali ya mambo katika eneo la Gaza ambako amesema kuwa pamoja na mwongozo uliotolewa na Baraza la Usalama lililotaka usitishwaji mapigano, lakini hali imeendelea kuwa mbaya na siyo tu kwa raia wa Palestina lakini pia kwaWaisrael. Katika taarifa yake [...]

14/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Saudia Arabia yatoa taarifa kuhusu maambukizi ya kirusi corona

Kusikiliza / Hospitalini, Saudi Arabia @WHO

Saudia Arabia imetoa taarifa kuelezea mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona ambavyo tayari vimeua watu kadhaa na wengine wakiendelea kupata matibabu. Taarifa iliyotolewa na kitengo kilichowekwa maalumu kwa ajili ya kufuatilia hali ya ugonjwa huo imeonyesha kuwa kuanzia tarehe 3 Julai hadi tarehe 10 Julai, jumla ya wagonjwa 7 zaidi walithibitika kuambukizwa virusi vya [...]

14/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wabunge wa Israel na Palestina wana jukumu la kukomesha mashambulizi na kulinda raia: IPU

Kusikiliza / mnembo wa IPU @IPU

Shirika la Muungano wa Wabunge, IPU, limetoa wito kwa pande zote katika mzozo wa Israel na Palestina kukomesha mashambulizi yao ya angani na roketi mara moja na kuzuia mauaji zaidi ya raia. Taarifa kamili na John Ronoh. Taarifa ya John Ronoh IPU imetoa wito pia kwa wabunge wa Israel na Palestina kuchukua hatua zozote zinazohitajika [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu ziarani Haiti

Kusikiliza / Upatikanaji wa maji safi. Picha: MINUSTAH

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon leo ameanza ziara yake kwenye nchi za Haiti na Jamhuri ya Dominika, ambapo atakutana na viongozi wa nchi hizo mbili na kutathmini miradi iliyotekelezwa huko kutokomeza umaskini. Nchini Haiti, atazindua pia kampeni kubwa ya usafi vijijini pamoja na Waziri Mkuu Laurent Lamothe, akizungumza pia na jamii [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM yaomba ufadhili zaidi kuwasaidia wakimbizi wa Syria Lebanon

Kusikiliza / Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Idadi ya wakimbizi wa Syria nchini Lebanon inaongezeka kwa kasi zaidi ya uwezo wa jamii ya kimataifa kuchangia fedha za kukidhi mahitaji yao yanayoongezeka, amesema Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, Ross Mountain. Bwana Mountain amesema wakimbizi wapya wa Syria wapatao 12,000 wanaingia Lebanon kila wiki, huku idadi nzima ikitarajiwa kufikia milioni 1.5 [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yawasikitikia watoto wanaoathirika na mapigano Gaza

Kusikiliza / Watoto wawili wakisimama mbele ya nyumba ambayo polisi imesema imepigwa bomu la anga na Israel kwenye kambi la wakimbizi la Maghazi katikati mwa Ukanda wa Gaza. UN Photo/Shareef Sarhan

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF Anthony Lake amesema mapigano yanayoendelea huko Gaza yamegeuza maisha ya watoto kua magumu huku kiasi cha 33 wakiwa wamepoteza maisha katika siku za hivi karibuni kutokana na mapigano hayo. Taarifa kamili na George Njogopa Taarifa ya George Mkurugenzi huyo ambaye amesisitiza kuwa hakuna [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na machafuko Libya

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-moon, ameelezea kusikitishwa mno na ongezeko la machafuko katika mji mkuu waLibya,Tripoli, na madhara ya mapigano ya hivi karibuni kwa raia.Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa Amina) Ban ametoa wito kwa pande zinazokinzana kuepukana na kutumia machafuko kama njia ya kufikia malengoyaoya kisiasa. Ban amesema anaamini kuwa vitendo [...]

14/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lasikitishwa na mzozo wa Gaza

Hali ya uhai kutokana na vizingiti yanazidi kufifia Gaza na Ukanda wa Magharibi. Picha@ Shareef Sarhan/UNRWA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limeelezea kutiwa wasiwasi na tatizo la mzozo wa Gaza na ulinzi wa maisha na maslahi ya raia wa pande zote. Wanachama wa Baraza hilo wametoa wito wa kutaka hali hiyo itulizwe na kuhshimu tena makubaliano ya kusitisha mapigano ya Novemba 2012. Wametoa wito pia sheria ya kimataifa [...]

12/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani mashambulizi ya Al Shabaab ya karibun Mogadishu

Baraza la Usalama @UN Photo/Evan Schneider

Wanachama wa Baraza la Usalama, wamelaani vikali mashambulizi ya wiki iliyopita ambayo yamekuwa yakitekelezwa na kundi la kigaidi la Al Shabaab mjini Mogadishu, dhidi ya Villa Somalia, jengo la bunge na dhidi ya wabunge. Kauli hiyo imetolewa kufuatia taarifa aliyotoa Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Somalia, Nicholas Kay [...]

12/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa wanahabari watoto Tanzania wafika Afrika ya Kusini kwa ajili ya afya ya wakina mama

Kusikiliza / Picha@UNICEF

Nchini Afrika Kusini, mashirika ya kimataifa na wadau mbali mbali wa misaada ya kijamii na ya kibinadamu wamekutana kwa ajili ya kongamano la tatu kuhusu afya ya akina mama, watoto na watoto wachanga. Lengo la mkutano huo lilikuwa ni kuimarisha afya ya walio kwenye mazingira magumu zaidi, yaani akina mama na watoto na kuhakikisha kwamba [...]

11/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Ulaya zaombwa kuwasaidia wasaka hifadhi wa Syria

Kusikiliza / Picha: UNHCR/L. Addario

Nchi za bara Ulaya zimehimizwa kufungua milango kwa wakimbizi wa Syria na kuwapa utaratibu sahihi wanaosaka hifadhi.  Wito huo umetolewa na Shirika la kuhudumia Wakimbizi Duniani, UNHCR wakati wa uzinduzi wa ripoti kuhusu hali ya wakimbizi wa Syria walioko Ulaya. UNHCR imeyaomba mataifa hayo kuwapokea vilivyo na kuwalinda wakimbizi hao wanaokimbia mzozo nchini Syria. Shirika hilo [...]

11/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WHO yaendelea kufuatilia mkurupuko wa Ebola Afrika Magharibi

Kusikiliza / Muuguzi akimuhudumia mgonjwa mwenye virusi vya Ebola. WHO/Chris Black

Shirika la afya duniani WHO, linajitahidi kufuatilia kwa makini hali ya mlipuko wa virusi vya Ebola katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone. Nchini Guinea, kuenea kwa virusi kumepungua kwa kiasi kikubwa, na kisa kimoja tu kimeripotiwa kwa siku 7 zilizopita. WHO inaendelea kufuatilia hali kwa makini hasa ikilenga jamii ambazo zilikuwa zimepuuza mapendekezo [...]

11/07/2014 | Jamii: Ebola, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP inatumia simu za mkononi kuwasiliana na wakimbizi kambini

Kusikiliza / Agnes Niyanzira @WFP

Tatizo la njaa linasalia kuwa changamoto kubwa katika nchi nyingi, hususan katika nchi kunakoshuhudiwa ghasia. Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kunaendeshwa mradi wa utafiti wa usalama wa chakula kupitia simu za rununu miongoni mwa wakimbizi, ukiendeshwa na Shirika la chakula duniani WFP. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala ifuatayo inayoangazia mama mkimbizi katika [...]

11/07/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mahitaji ya kibinadamu yazidi kufurika Gaza

Kusikiliza / Hali ya uhai kutokana na vizingiti yanazidi kufifia Gaza na Ukanda wa Magharibi. Picha@ Shareef Sarhan/UNRWA

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura, OCHA, imesema kuwa inasikitishwa na ongezeko la mahitaji ya dharura ya kibinadamu Gaza kufuatia kuanza kwa operesheni za kijeshi za Israel mnamo Julai 7, ambazo zimeelezwa kuwa na lengo la kukomesha mashambulizi ya roketi kutoka Gaza. OCHA imesema kuwa, mbali na mauaji na majeraha mengi [...]

11/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waasi wa Afrika ya Kati wanajihusisha na biashara za madini

Kusikiliza / Baraza la Usalama wakati wa kikao Picha UM/Evan Schneider/NICA

Baraza la Usalama leo limejadili hali Jamhuri ya Afrika ya Kati na ripoti kutoka kamati ya vikwazo dhidi ya watekelezaji wa uhalifu nchini humo. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte Vikwazo vinatarajiwa kuwekwa ili kuzuia baadhi ya waasi kusafiri nje ya nchi, kama njia moja ya kutia shinikizo juu ya pande zote za mzozo, ndivyo alivyoeleza [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yasaidia wakimbizi wa Nigeria nchini Cameroon

Kusikiliza / Wakimbizi wanaokimbia ukatili wa Boko Haram katika taifa la  Borno, Nigeria. Picha: IRIN/Anna Jefferys(UN News Centre)

Kufuatia machafuko yanayoendela kaskazini mwa Nigeria, raia wengi wamekimbia na kutafuta hifadhi katika nchi jirani ya Cameroon ambapo Shirika la Mpango wa Chakula duniani WFP linawapa usaidizi, licha ya mazingira yasiyo salama na matatizo ya usafiri. Elizabeth Brys ambaye ni Msemaji wa WFP ameeleza kwamba hii ni mara ya kwanza kwa WFP kutoa usaidizi karibu [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yatolea wito ufadhili zaidi wakati tatizo la wakimbizi wa Sudan Kusini likiongezeka

Kusikiliza / Kundi la wakimbizi wa ndani wakiwemo wanawake na watoto wakipumzika katika eneo la Ethiopia baada ya kuvuka mto wa Baro kutoka Sudan ya Kusini. Picha: UNHCR/L.F.Godinho(UN News Center)

Shirika la kuhudumia wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR na wadau wanaokabiliana na tatizo la wakimbizi kufuatia kuzorota usalama Sudan Kusini wametoa ombi jipya la dola milioni 658 ili kusaidia wakimbizi takriban 715,000 mwishoni mwa mwaka huu wa 2014. Taarifa kamili na John Ronoh.(Taarifa ya Ronoh) Mzozo huo unaoshuhudiwa na hali mbaya ya kibinadamu katika [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Siku ya idadi ya watu yamulika vijana milioni 1.8 waliopo duniani

Kusikiliza / UNFPA/Idriss Qarqouri (NICA ID:587729)

  Leo tarehe 11 Julai ikiwa ni siku ya idadi ya watu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amewaomba viongozi wote duniani kuwekeza katika hatma ya vijana, akisema vijana milioni 1.8 waliopo duniani, hasa katika nchi zinazoendelea, wana nguvu za kupambana na changamoto zinazokumba ulimwengu, lakini bado wananyimwa fursa ya kupta [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya Haki za Binadamu yasikitishwa na mauaji ya raia Gaza na Israel

Kusikiliza / Ravina Shamdasani, Msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu. Picha: UN Multimedia

  Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, leo imeelezea kusikitishwa na operesheni za kijeshi za Israel, ambazo zimesababisha mauaji ya raia Ukanda wa Gaza, na pia makombora yanayorushwa kiholela kutoka Gaza kwenda Israel. Kufikia Alhamis mchana, Wapalestina wapatao 88, wakiwemo watoto 21 na wanawake 11, walikuwa wameuawa Gaza kutokana na mashambulizi ya [...]

11/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban amteua De Mistura kuwa mjumbe maalum kwa Syria

Kusikiliza / Katibu mkuu Ban Ki-moon na Staffan de Mistura. UN Photo/Rick Bajornas

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua leo Bwana Staffan de Mistura kuwa mjumbe wake maalum kwa ajili ya kutafuta makubaliano ya amani kwenye mzozo waSyria. Bwana de Mistura, ambaye aliwahi kuongoza ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchiniIraqnaAfghanistan, anachukua nafasi ya Lakhdar Brahimi, ambaye alijiuzulu mwezi Mei. De Mistura aliwahi kuwa Naibu [...]

10/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mratibu wa UM Lebanon atembelea wakimbizi wa Syria na wenyeji wao

Kusikiliza / Ross Mountain, Mratibu wa Hahaki za Binadamu. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Mratibu wa Huduma za kibinadamu nchini Lebanon Bwana Ross Mountain ametembelea maeneo ya Hermel na Arsal jijini Beirut ili kutathmini hali ya wakimbizi wa Syria na jamii za Lebanon zinazowapa hifadhi. Kuna raia wa Syria zaidi ya 376,000 ambao wamejiandikisha na Shirika la Kuhudimia Wakimbizi- UNHCR katika maeneo hayo. Bwana Mountain alikutana na viongozi wa [...]

10/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ziarani, Mia Farrow asisitiza haja ya kusaidia watoto wa CAR

Kusikiliza / Picha@UNICEF/Central African Republic/2013/Menezes

Mia Farrow, mcheza filamu maashuhuri, mwanaharakati na balozi mwema wa UNICEF amekamilisha ziara yake ya nne nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambko amejionea madhara ya ukatili uliokithiri, na pia kukutana na watu na kuwasikiliza wasimulia hadithi za ujasiri wa kutia moyo. Akiwa mji wa Boda, yapata mwendo wa saa nne barabarani kutoka mji mkuu [...]

10/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Chapisho la biashara la kimataifa laidhinishwa: UNCITRAL

Kusikiliza / Nembo ya UM

Kamisheni ya Umoja wa Mataifa juu ya sheria zinazohusika na biashara za kimataifa imeidhinisha chapisho linalohusu mkataba unaozingatia uwazi baina ya wawekezaji na serikali. Mkataba huo ambao unatoa hali ya uwazi kwa pande zote iliratibiwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 unatoa mwongozo pindi panapohusika mashauri yanayohusu migogoro ya uwekezaji baina ya mwekezaji na dola. [...]

10/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua za kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza hazitoshi: WHO

Kusikiliza / Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Margaret Chan(kwenye jukwaa) akihutubia 67th World Health Assembly. Picha:WHO/Martin

Hatua za kuzuia magonjwa yasiyo ya kuambukiza zimetajwa kuwa zisizotosha na pia hazionyeshi usawa, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Afya Duniani, WHO.  Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni kama vile magonjwa ya moyo, saratani, kisukari na ugonjwa wa mapafu. Ripoti hiyo mpya ya WHO inamulika hali ilivyo sasa katika nchi 194. Daniel [...]

10/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Miradi endelevu yazuia taka na uchafu kwenye Kombe la Dunia Brazil: UNEP

Kusikiliza / UNEP

Miji nchini Brazil imekuwa ikitekeleza miradi kadhaa ya mazingira endelevu wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu 2014,kamavile kutoa vibali vya kutimiza viwango vya kulinda mazingira kwa nyanja za kuchezewa mpira na kulipa fidia kwa uvushaji wa gesi chafuzi kutokana na shughuli za Kombe la Dunia.  Miradi mingine iliyoidhinishwa na Mpango wa Brazil [...]

10/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto hatarini kuathiriwa vibaya na ghasia Ukanda wa Gaza na Israel: UNICEF

Kusikiliza / Msichana huyu kutoka Palestina analia baada ya nyumba yao kuharibiwa eneo la Khan Yunis, Gaza  Picha ya © UNICEF / Eyad El Baba

Kuongezeka machafuko Gaza na Israel kunatishia kuwadhuru watoto kwa kiwango kikubwa kwenye pande zote za mzozo, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, ambalo limerejelea ujumbe wa Katibu Mkuu wa kuziomba pande zote kujizuia na kuwalinda watoto. Tayari, katika siku tatu zilizopita watoto wapatao 19 wa Kipalestina wameripotiwa kuuawa katika [...]

10/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya nusu ya watu duniani sasa wanaishi mijini: UM

Kusikiliza / Mji wa Dhaka, Bangladesh Picha ya UM/Kibae Park

Asilimia 54 ya watu kote duniani sasa wanaishi mijini, na kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 66 ifikapo mwaka 2050. Hayo yamedhihirika katika ripoti mya ya makadirio ya Umoja wa Mataifa kuhusu ukuaji wa miji duniani, ambayo imezinduliwa leo mjini New York na idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa. Makadirio [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

OCHA: watu 300 wameshajeruhiwa Gaza

Kusikiliza / mtoto Palestina UNICEFPalestine

Ofisi ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu, OCHA, leo imetoa ripoti kuhusu hali ya usalama na ya kibinadamu katika maeneo ya Gaza na Ukingo wa Magharibi. Shirika hilo, limesema, tangu mwanzo wa operesheni za Israel kupiga mabomu dhidi ya maeneo hayo, zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na 300 wamejeruhiwa, wakiwemo watoto, watu 900  wakilazimika kuhama [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ripoti mpya yatolewa kuhusu kuzuia malaria na afya ya mama na watoto

Kusikiliza / Roll back Malaria(RBM)Picha ya Benjamin Schilling/PSI

Ripoti mpya inayoonyesha faida za kupambana na malaria kwa afya ya akina mama na watoto imezinduliwa leo kwenye hafla maalum kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York. Akizungumza na Redio ya Umoja wa Mataifa, daktari Erik Mouzin kutoka Ushirikiano wa Kutokomeza Malaria, ameeleza faida hizo akisema: " nadhani kwamba watu wamepata habari [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO yatoa mafunzo Liberia kama njia ya kukabiliana na Ebola

Kusikiliza / WHO/Christina Banluta

Viongozi wa jamii katika wilaya tatu nchini Liberia Montserrado, Margibi, na Lofab wanapokea mafunzo kuhusu virusi vya Ebola, kama sehemu ya juhudi za Shirika la afya duniani WHO na wizara ya afya ya jamii katika kuhamasisha kuhusu ugonjwa huo, jinsi gani unaambukizwa na mchango wa umma katika kukabiliana na ugonjwa huo. Taarifa kamili na Grace [...]

10/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Saudi Arabia yashutumiwa kwa kuwafunga watetezi wa haki za binadamu

Kusikiliza / Navi Pillay, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Juu ya Haki za Binadamu. Picha: UN Photo/Paulo Filguerias

Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imeishutumu vikali serikali ya Saudia, ambayo inadaiwa kuendesha vitendo vya ukiukwaji wa haki binadamu, vikiwemo kuwakamata na kuwatesa baadhi ya watu wanaotetea haki za binadamu. George Njogopa ana taarifa kamili Taarifa ya George Shutuma hizo zinakuja katika wakati ambapo kukitolewa hukumu kwa mwanaharakati mmoja aliyehukumiwa [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lamulika hali tete ya Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali Mashariki ya Kati na suala la Palestina, likimulika zaidi hali ya machafuko ambayo sasa yametanda eneo la Gaza. Taarifa kamili na Amina Hassan (Taarifa ya Amina) Wakati wa kikao cha leo, Baraza la Usalama limemsikiliza kwanza Katibu Mkuu Ban Ki-moon, ambaye amesema kwamba hivi [...]

10/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yahamishia wakimbizi wa Syria kwa kambi mpya nchini Iraq.

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria wakiingia mkoa wa Kurdistan nchini Iraq. Picha@UNHCR/G.Gubaeva

Licha ya nchi ya Iraq kuwa na wakimbizi wa ndani kwa ajili ya mapigano katika nchi hiyo, Shirika la Kuhudumia Wakimbizi , UNHCR, linaendelea kusaidia wakimbizi kutoka Syria waliohamia Iraq baada ya machafuko nchini mwao. UNHCR imefungua Kambi ya kudumu katika mkoa wa Kurdistan ulio kaskazini mwa Iraq, ili kuhudumia wakimbizi zaidi ya 225,000 kutoka [...]

09/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mapigano mengine yasababisha wakimbizi wa ndani kuongezeka Yemen

Kusikiliza / Karibu watu milioni 15 Yemeni, kama familia hii, wanahijati msaada wa kibinaadamu mwaka. OCHA/Eman al Awami.

Mratibu wa misaada ya kibinadamu nchini Yemen, Johannes Van der Klaauw ameeleza wasiwasi wake juu ya usalama wa wananchi waliomo katikati ya mapigano kaskazini mwa nchi hiyo. Zaidi ya wananchi 200 wameripotiwa kuuawa, wakiwemo wanawake na watoto, na wengine maelfu wametegwa katikati ya eneo la mapigano, mjini Amran, wakishindwa kukimbia. Mapigano yalisimamishwa kwenye eneo hilo [...]

09/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia hali inayotia shaka Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, amesema kuwa amesikitishwa na wimbi jipya la machafuko ambalo limeughubika Ukanda wa Gaza, kusini mwa Israel na Ukingo wa Magharibi.   Akikutana na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo mjini New York, Ban amesema kuwa huu ni wakati wa mtihani mgumu zaidi [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa walaani mashambulizi ya wananchi ndani ya kanisa

Kusikiliza / Mashambulizi yaliyotokea leo @MINUSCA VIDEO

Ujumbe wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA, umelaani mashambulizi ya kikatili dhidi ya wakimbizi wa ndani yaliyotokea tarehe saba Julai ndani ya kanisa kuu la dayosisi ya Saint Joseph na kwenye makao ya askofu, mjini Bambari. Kwa mujibu wa waandishi wa habari, zaidi ya watu elfu sita walikuwa wametafuta hifadhi ndani [...]

09/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laiomba Lebanon kuchagua rais mpya haraka

Kusikiliza / Dereck Plumbly, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon akizungunza na waandishi wa habari baada ya kikao cha Baraza la Usalama

Baraza la Usalama likikutana leo tarehe 9, Julai, kujadili hali ya nchi ya Lebanon, limeipongeza nchi hiyo kwa jitahada zake katika kulinda amani iliyopo sasa kwa kipindi cha miezi minne, na kuiomba pia lizibe pengo la kiti cha uraisi haraka iwezekanavyo. Dereck Plumby, Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, ameripoti kuhusu hali ya usalama [...]

09/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

WHO yaihimiza Uchina kuendelea kufanyia marekebisho mfumo wake wa afya

Kusikiliza / Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO. Picha@PAHO/WHO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, Dr. Margaret Chan, amesema ni jambo la umuhimu mkubwa kwa serikali ya Uchina kuendelea na hata kuongeza kasi ya kufanyia marekebisho mfumo wake wa huduma za afya, ili kujenga mfumo utakaokabiliana na changamoto za afya sasa na za siku zijazo. Dr. Chan amesema hayo wakati akikamilisha ziara [...]

09/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majeruhi wa kiraia nchini Afghanistan waongezeka kwa asilimia 24 Mwaka 2014

Kusikiliza / Georgette Gagnon, mkuu wa haki za binadamu atembelea mtoto aliyejeruhiwa na kilipuzi manamo Febrruaru 2013(Picha ya UM/Fardin Waezi)

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, UNAMA umesema kuwa kumekuwa na ongezeko la vifo na majeruhi wa kiraia nchini humo kwa asilimia 24 kufikia Juni 2014. Mengi yamesababishwa na mapigano ya nchi kavu na pia kwa mabomu yaliyotekwa chini ya ardhi. Ujumbe huo ukishirikiana na Ofisi ya Haki za Binadamu, umezindua ripoti inayoangazia mapigano [...]

09/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpango mpya wazinduliwa kukabiliana na ukatili wa kingono

Kusikiliza / Picha@UNICEF

Nchini Tanzania, msichana mmoja kati ya watatu hukabiliana na ukatili wa kingono kabla hajafikisha miaka kumi na minane. Bado desturi ya siri inakuwepo na kusababisha watekelezaji wengi kukwepa sheria. Ili kudhibiti ukatili huo, serikali ya Tanzania imezindua mpango mpya wa miaka mitatu wa kuripoti ukatili wa kingono kwa kupitia madawati ya jinsia na watoto yanayofunguliwa [...]

09/07/2014 | Jamii: Mahojiano, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya Haki za Wapalestina yakutana kuhusu ukuta tatanishi

Kusikiliza / Wanawake wa kipalestina wakitembea karibu na ukuta wa kiisraeli katika Ukingo wa Magharibi. Picha: IRIN/Shabtai Gold(UN News Centre)

Kamati kuhusu haki za watu wa Palestina, leo imefanya kikao cha kuadhimisha miaka kumi tangu ulipotolewa ushauri wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu hatua ya Israel ya kujenga ukuta katika maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua Mahakama ya Kimataifa ya Haki ilisema kuwa ujenzi wa ukuta huo ulikuwa [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani shambulizi dhidi ya makao makuu ya serikali Somalia

Kusikiliza / Nicholas Kay, Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa, Somalia. Picha@UN Photo/David Mutua

Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nichola Kay, amelaani shambulizi lililofanywa jana usiku dhidi ya Villa Somalia, ambayo ni makao makuu ya serikali ya Somalia mjini Mogadishu. Shambulizi hilo ni miongoni mwa msururu wa mashambulizi yanayotekelezwa na wanamgambo wa Al Shabaab dhidi ya taasisi za kisiasa nchini [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jamii za wavuvi ziwa Tanganyika zabadilisha mbinu za kukausha samaki

Kusikiliza / Picha@FAO

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani, FAO, limetoa ripoti mpya kuhusu mafanikio ya mradi lililoutekeleza katika jamii za wavuvi wa samaki ndogondogo, ziwani Tanganyika, nchini Burundi.  Samaki hao wanaoitwa ndagala, kawaida hukaushwa chini.  Mchanga, mvua na matope huharibu bidhaa hizo mara kwa mara, jinsi anavyoeleza afisa wa FAO Yvette Diei Ouadi: " Ilikadiriwa, mwaka 2004, [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini kuadhimisha miaka mitatu ya uhuru kwenye hali ya utata

Kusikiliza / southSudanIndependence1

Siku ya leo, Sudan Kusini, ambayo ni nchi changa zaidi duniani, inaadhimisha siku yake ya uhuru ilioupata mnamo tarehe 9, Julai 2011. Taarifa zaidi na John Ronoh. Kwenye siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon ametuma ujumbe wake kwa viongozi wa taifa hilo, akisema wana wajibu wa kuumaliza mgogoro uliopo sasa. [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Shughuli za Umoja wa Mataifa Iraq zapigwa jeki na Kuwait

Kusikiliza / Familia hii ilikimbia mapigano Mosul, Iraq na wako karibu na kituo cha Khazair.Wanamatumaini ya kukakaa mji wa Erbil hadi itakapokuwa salama kurudi nyumbani(Picha@UNHCR/R.Nuri

Kuwait imetoa mchango wa dola milioni 9.5 kwa ufadhili wa huduma za Umoja wa Mataifa za kibinadamu nchini Iraq. Mratibu wa masuala ya kinadamu na misaada ya dharura, Valerie Amos amekaribisha mchango huo, akisema kuwa utasaidia wahudumu wa kibinadamu nchini Iraq kuongeza juhudi za kutoa misaada kwa familia zilizolazimika kuhama na jamii za wenyeji wao. [...]

09/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto wa Somalia kukumbwa na hali ya njaa

Kusikiliza / UN News Centre

Hali ya ukame inavyozidi kuongezeka nchini Somalia kutokana na ukosefu wa mvua, mashirika ya kimataifa yanatiwa wasiwasi na nchi hii kukumbwa na janga la njaa.  Katika hospitali ya Baidoa, kusini mwa Somalia, wakina mama wanazidi kuleta watoto wao waliougua utapiamlo, wengi wakiwa kwenye hatari ya kupoteza maisha. Ni matibabu gani wanapatiwa? Ungana na Amina Hassan [...]

08/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Australia yamulikwa kwa kuwarudisha wasaka hifadhi Sri Lanka kwa nguvu

Kusikiliza / @Ravina Shamdasani/OCHR

Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, leo imeelezea kusikitishwa na tukio la hapo Jumapili ambapo serikali ya Australia iliwarudisha watu 41 waliokimbilia nchi hiyo wakitafuta hifadhi salama wakitoka nchini Sri Lanka. Ofisi hiyo imesema hatua hiyo ilichukuliwa bila kuthibitisha kikamilifu madai ya watu hao ya kiusalama. Msemaji wa ofisi hiyo, Ravina Shamdasani [...]

08/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban atoa ujumbe wa amani kwa Siku ya Uhuru Sudan Kusini

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon

Wakati taifa la Sudan Kusini likijiandaa kuadhimisha miaka mitatu tangu kujinyakulia uhuru mnamo Julai 9, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema viongozi wa taifa hilo changa zaidi wana wajibu wa kuumaliza mgogoro uliopo sasa, ambao amesema umebuniwa na mwanadamu. Katika taarifa iliyosomwa na msemaji wake, Bwana Ban amekumbusha kuhusu matumaini na matarajio [...]

08/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMA yatoa tamko kuhusu matokeo ya awali ya uchaguzi wa Urais- Afghanistan.

Kusikiliza / Afghanistan elections3

Ujumbe huo umeeleza kuwa matokeo yaliyotolewa siyo ya mwisho na kuna uwezekano wa kubadilika, na hivyo basi ni mapema kwa mgombea yeyote kudai ushindi wa uchaguzi huo. UNAMA imeendelea kuhimiza taasisi za uchaguzi hasa Kamisheni Huru ya Uchaguzi (IEC) na Kamisheni Huru ya Malalamishi ya Uchaguzi (IECC) wadhihirishe uajibikaji wao kwa kutilia maanani hali ya [...]

08/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Wanawake 145,000 wakimbizi wa Syria wanaubeba mzigo wa familia zao: UNHCR

Kusikiliza / Mstari wa wanawake wakikimbia Syria, wakibeba watoto, wakivuka ndani ya Jordan kutoka kusini mwa Syria. Picha: UNHCR/N. Daoud.

Ripoti mpya ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, imesema zaidi ya familia 145,000 za wakimbizi wa Syria zilizoko Misri, Lebanon, Iraq na Jordan, au kila moja katika familia zote za wakimbizi, zinaongozwa na wanawake ambao wanahangaika peke yao kujikimu kimaisha. Ripoti hiyo inaweka bayana mahangaiko ya kila siku ya kutafuta riziki, huku wanawake hao wakijitahidi [...]

08/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF na WFP yaongeza usambazaji misaada kwa maeneo magumu kufikiwa Sudan Kusini

Kusikiliza / SouthSudanRefugees1

Mashirika hayo yamesema kuwa kote nchini Sudan Kusini, kumewekwa mfumo wa pamoja wa huduma za dharura, ili wahudumu wa misaada ya dharura waweze kusafiri kwa ndege hadi maeneo yenye ugumu kufikiwa, na kuweza kutoa misaada ya kibinadamu kwa watu ambao ama wamepokea usaidizi mdogo sana au hawajapata usaidizi wowote wa kibinadamu. Taarifa ya pamoja ya [...]

08/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yaeleza wasiwasi juu ya hali ya usalama CAR

Kusikiliza / Picha@WFP/George Forminyen

Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP linatiwa wasiwasi kwa kushindwa kufikisha misaada ya kibinadamu kadri hali ya usalama inavyozidi kuzorota, anavyoeleza msemaji wake, Elisabeth Byrs: " Mnajua kwamba mashambulizi yameanza tena maeneo ya Bambari, na ghasia hizo zinaweka shughuli za kibinadamu hatarini. Hali ni ngumu sana kwa wafanyakazi [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Tatizo la Ebola Afrika Magharibi lapatiwa sikio kwenye Baraza la Usalama

Kusikiliza / Said Djinnit, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa afrika Magharibi. Picha: UN Photo/Devra Berkowitz

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limesikiliza ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu ukanda wa Afrika ya Magharibi, ikitaja hali tete eneo la Sahel na kuzorota usalama nchini Nigeria, huku suala la Ebola likitajwa kama linalopaswa kupewa kipaumbele na jamii ya kimataifa. Taarifa ya Joshua Baraza hilo ambalo limekutana kuhusu uimarishaji amani Magharibi mwa [...]

08/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ubia mpya kuboresha sekta ya afya kupitia huduma za tabianchi.

Kusikiliza / madhara ya mabadiliko ya tabianchi

Leo kimbunga kikipiga vikali kisiwa cha Japan, Shirika la Afya Duniani WHO na Shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO yametangaza kufungua ofisi ya pamoja ya Afya na Tabianchi. Mashirika haya mawili yameamua kushirikiana ili kupambana na madhara ya kiafya yatokanayo na majanga ya tabianchi kama vile joto kali, mafuriko, ukame, ama [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wajiandaa kutoa misaada ya dharura Sinjar, Iraq

Kusikiliza / Picha: UNHCR_Iraq/ S. Baldwin

Timu ya wataalam wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, ilikwenda kwenye eneo la Sinjar, magharibi mwa Ninewa nchini Iraq, ambako familia zipatazo 8,000 zimekimbilia kutoka kwenye eneo jirani la Tal Afar. Timu hiyo imekwenda kufanya tathmini ya mahitaji ya kibinadamu ya dharura zaidi, ili kujiandaa kwa kutoa misaada. Mwakilishi wa UNICEF [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya wahamiaji wanaokufa Mediterenia yaendelea kuongezeka

Kusikiliza / Wakimbizi kutoka Syria waokolewa katika bahari la Mediterenia. Picha@UNCHR/A. d'Amato(UN News Centre)

Idadi ya wahamiaji ambao wamekufa kwenye Bahari ya Mediterenia wakijaribu kukimbilia Ulaya imeongezeka na kufikia watu 500, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Mnamo Jumatatu, walinzi wa pwani ya Libya waliiambia UNHCR kuwa walikuwa wametoa miili 12 kutoka kwenye ajali ya boti ambayo inaaminika kutokea Jumapili.  Miongoni mwa wahanga [...]

08/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wahimiza wanasiasa nchini Iraq kuchagua Spika wa Bunge haraka

Kusikiliza / Nikolay Mladenov@Picha/UNAMI

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Nickolay Mladinov, leo amekuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wa kisiasa nchini Iraq na kutoa himizo lake kwa wote kuzingatia mkakati wa harakati za kikatiba na kuhakikisha kwamba waakilishi wa baraza wanakutana haraka iwezekanvyo. Bwana Mladenov ameeleza kuwa amepata hakikisho kutoka [...]

07/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kuwaelimisha wasichana ndio ufunguo wa maendeleo endelevu

Kusikiliza / Wanafunzi wa kike Tanzania @UNICEF Tanzania / Holt 2014

Mkutano wa kutoa ahadi za kusaidia utoaji elimu kote duniani umechangisha dola bilioni 28.5 kutoka kwa wafadhili na nchi zinazoendelea. Mkutano huo wa Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya Elimu au GPE ulifanyika mjini Brussels, Ubeljiji kati ya tarehe 25 na 26 Juni, ukilenga kuchangisha fedha zaidi za kusaidia upatikanaji elimu. Fedha hizo za ziada [...]

07/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanafunzi Zanzibar wahamasishwa kuhusu ukatili wa kingono

Kusikiliza / wanafunzi zanzibar1

Katika kisiwa cha Zanzibar, shule za wilaya za Kaskazini A zimeunda vilabu shirikishi ili kujadiliana kuhusu ukatili wa kingono. Ameir Haji kutoka kituo cha vijana Zanzibar amehudhuiria uhamasishaji ulioandaliwa na mkuu wa idara ya Elimu wa wilaya hiyo. Ni nini kilichofanyika? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.

07/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Pakistan walioko Afghanistan wahitaji chakula kwa dharura:UM

Kusikiliza / Watoto wakiwa Kaskazini mwa Waziristan, huko Pakistan. Photo: IRIN/Fakhar Kakahel(UN News Centre)

Familia nyingi za Wapakistan zilizolazimika kuhama katika mikoa ya Khost na Paktika nchini Afghanistan zinahitaji chakula kwa dharura, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Operesheni za kijeshi katika eneo la Waziristan, kaskazini mwa Pakistan zilikuwa zimewalazimu watu wapatao 95,000 kukimbilia Afghanistan. Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Farhan Haq [...]

07/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Australia kuwafukuza wahamiaji wa Sri Lanka waliokamatwa baharini

Kusikiliza / Picha@UNHCR/A. Di Loreto(UN News Centre)

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeeleza wasiwasi wake kuhusu maamuzi ya Australia kufukuza waomba hifadhi salama 41 kutoka Sri Lanka.  Mahakama Kuu ya Australia imesitisha pia maombi mengine 153 ya waomba hifadhi salama kutoka Sri Lanka. UNHCR imesema, imepata taarifa kutoka mamlaka za Australia kwamba vigezo vya kuthibitisha maombi ya hifadhi [...]

07/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Waatalam wa Usalama wakutana Vienna Kujadili Maendeleo kuhusu Ujasusi wa Nyuklia

Kusikiliza / Mlipuko wa nyuklia. (Picha-Maktaba)

Wataalamu 350 wa Ujasusi wa Kinyuklia watakuwa na mkutano ya siku tatu mjiniVienna, Autria tokea tarehe 7-10 Julai 2014 kujadili juu ya utumiaji wa nguvu za Kinyuklia pamoja na kujaribu kuthathmini vyanzo na historia ya miyale nyuklia, hasa ile inayopatikana kwenye sehemu kulikotendeka uhalifu. Watalamu hao watakuwa na mazungumzo yanayolenga matumizi ya chembe chembe hizo [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanaleta mabadiliko: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon. Picha@UN Photo/Paulo Filgueiras

Wakati dunia ikiangazia awamu ya mwisho ya harakati za kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, MDGs, ni dhahiri sasa kuwa malengo hayo yanaleta mabadiliko katika maisha ya watu. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, wakati wa kikao cha Baraza la masuala ya Kiuchumi na Kijamii, ambapo pia imezinduliwa ripoti ya [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wataalamu waonya kuhusu hali mbaya ya chakula Somalia

Kusikiliza / Picha ya OCHA

Wataalamu wa masuala ya chakula duniani wameonya juu ya Somalia kukumbwa na hali mbaya zaidi ya ukosefu wa chakula katika kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba mwaka huu. Wataalamu hao kutoka shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya dharura wamesema kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa wahisani wa maendeleo nchini humo wakahamisha mada na [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa alaani mashambulizi dhidi ya Bunge la Somalia

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay

Nchini Somalia, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Nicholas Kay, amelaani vikali mashambulizi yaliyotokea dhidi ya Bunge la Somalia na mashambulizi kadhaa yanayodaiwa na kundi la Al-shabab tangu mwanzo mwa Ramadan, akisikitishwa kuona vitendo hivi kutokezea mwezi huo ambao ni mwezi wa Amani na Imani. Kay amewasifu walinzi wa Bunge [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay akemea ubaguzi wa elimu dhidi ya watoto wa kike, wanawake

Kusikiliza / Wasichana wa shule. UNICEF Tanzania. Picha@ Pudlowksi

Pamoja na wito unaoendelea kutolewa na jumuiya za kimataifa unaotaka kuondolewa kwa aina yoyote ya ubaguzi dhidi ya wanawake ikiwemo haki ya kupata fursa, lakini hadi sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watoto wa kike milioni 35 wameshindwa kupata elimu wanayostahili. Taarifa kamili na John Ronoh Kulingana na Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa [...]

07/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

92% ya watu waliolazimika kuhama makwao waondoka kambini Haiti

Nembo ya IOM

Asilimia 92 ya watu ambao walikuwa wanaishi katika kambi nchini Haiti kufuatia tetemeko la ardhi la Januari 2010, sasa wamepata makazi mbadala na kuondoka kambini, kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM. Takriban watu milioni 1.5 walikuwa wakiishi katika kambi za muda mara tu baada ya tetemeko hilo la ardhi lililoathiri taifa hilo [...]

06/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sudan yashutumiwa kuwarejesha wakimbizi na waomba hifadhi kwa lazima

Wkimbizi wa Eritrea: Picha ya UNCHR

Raia wa Eritrea wapatao 74 waliokwenda Sudan kuomba hifadhi wameondolewa kwa lazima na kurejeshwa nyumbani, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. Watu hao walirejeshwa Eritrea mnamo Jumatatu ya tarehe 30 Juni. UNHCR imesema kuwa waomba hifadhi hao walikuwa wameshtakiwa na kuhukumiwa kuingia Sudan kinyume na sheria, lakini hawakupewa fursa ya kufikia [...]

04/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini hatarini kutumbukia janga la njaa: WFP

Mapigano yanayoendelea Sudan Kusini yameleta madhila makubwa ikiwemo njaa kwa wakazi hususan wanawake na watoto. (Picha-WFP)

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, limeeleza leo wasiwasi wake kwamba nchi ya Sudan Kusini inaelekea kukabaliana na janga la njaa. WFP imesema mapigano yamesababisha ukosefu wa usalama wa chakula kwenye baadhi ya maeneo yaliyotengwa. Msemaji wa WFP Elisabeth Byrs ameelezea waandishi wa habari kuwa shirika hilo linakumbwa na changamoto nyingi wakati wa kufikisha [...]

04/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Vyama vya Ushirika vyasifiwa kuchagiza maendeleo

Kusikiliza / Picha@FAO/G. Napolitano

Tarehe tano mwezi Julai ni Siku ya Vyama vya Ushirika Duniani. Katika ujumbe wake wa kuiadhimisha siku hiyo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amesema kuwa imekuja wakati muhimu sana, ambapo Umoja wa Mataifa unafanya juhudi kufikia malengo ya maendeleo ya milenia, kufikia mkataba muhimu wa mabadiliko ya tabianchi na kuridhia ajenda ya [...]

04/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Faida zinazopatikana kutokana na uwekezaji Afrika zaimarika

Kusikiliza / Dkt. Mukhisa Kituyi, Katibu Mtendaji wa UNCTAD. (Picha@UN/Jean-Marc Ferré)

Katika muongo uliopita, faida ya uwekezaji barani Afrika imeongezeka na kufikia kiwango kikubwa kuliko mabara mengine. Ripoti ya maendeleo ya Kiuchumi Afrika 2014 iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD, inaonyesha kwamba kati ya miaka 1990 na 1994, dola 7.4 zilihitajika kuwekezwa ili kuzalisha kipimo kimoja cha ziada cha [...]

03/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wajumbe wa Baraza la Usalama walaani mauaji ya mvulana wa Kipalestina

Kusikiliza / Baraza la Usalama. UN Photo

Wajumbe wa Baraza la Usalama wameelezea huzuni yao na kulaani vikali utekaji nyara na kuuawa kwa mvulana wa Kipalestina iliotekelezwa Julai 2 Mashariki mwa mji wa Jerusalem. Wametuma rambirambi zao kwa jamii iliopoteza mvulana huyo na watu wa Palestina kwa ujumla.Wamesema kwamba wote waliohusika na mauaji hayo ya kinyama wakamatwe na kuchukuliwa hatua, kulingana na [...]

03/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ziarani Kenya- Ban Ampanga Mwana simba-Tumaini

Kusikiliza / Katibu Mkuu apanga mtoto yatima wa Simba kutoka Nairobi National Park. Picha@ UN Photo/Eskender Debebe

Ulinzi wa wanyamapori ni jambo ambalo linaendelea kusisitizwa na jamii zote duniani, hasa kwa ajili ya urithi wa kizazi cha leo na vizazi vijavyo. Hivi majuzi Katibu mkuu akiwa mjini Nairobi, Kenya alimpanga mtoto yatima wa Simba na kumpa jina "Tumaini". Ujumbe alionuia kuwasilisha kwa upangaji huo ni nini? Basi ungana na John Ronoh kwa [...]

03/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Kuwazuilia watafuta hifadhi na wakimbizi kukomeshwe: UNHCR

Kusikiliza / wakimbizi wanaoendelea kukimbia mapigano Mosul @UNHCR Inje Colijn

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, leo limetoa mkakati wa kimataifa unaolenga kuzisaidia nchi kukomesha desturi ya kuwakamata na kuwazuilia watafuta hifadhi, wakimbizi na watu wasio na utaifa kote duniani. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua UNHCR imesema kuwa desturi hiyo katika baadhi ya nchi ina madhara makubwa na [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO, Ulaya yaweka mkakati mpya kukabili kifua kikuu

Kusikiliza / Wagonjwa wa kifua kikuu kutoka Myanmar wakiishi kwenye vibanda wakati wa matibabu katika Klinik ya Wangpha kwenye mpaka wa Thailand. Picha: IRIN/Sean Kimmons(UN News Centre)

  Shirika la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na chama cha upumiaji barani Ulaya, leo kimetoa mwongozo mpya unaoainisha mikakati ya kukabiliana na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu katika nchi ambazo tatizohiloni la kiwango cha chini. Hadi sasa inaelezwa kuwa kuna nchi 33 duniani ambazo kiwango cha ugonjwa huo kipo chini na kwamba kila [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake na wasichana katika hatari ya ukatili na unyanyasaji Iraq: UNFPA

Kusikiliza / Wanawake na watoto Iraq. Picha:UNHCR/S.Baldwin

  Wakati watu wapatao milioni moja wakiwa wamelazimika kuhama kaskazini na magharibi mwa Iraq, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, limeonya kuwa takriban wanawake na wasichana 250,000, wakiwemo waja wazito wapatao 60,000 wanahitaji usaidizi wa dharura kuwaepusha na hatari ya ukatili wa kingono na unyanyasaji. Taarifa kamili na Amina Hassan Taarifa [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mbunge “Hayd”

Kusikiliza / Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM, Nicholas Kay

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Nicholas Kay, amelaani vikali mauaji ya mbunge Mohamed Mohamud "Hayd" na mlinzi wake yaliyotokea leo asubuhi mjini Mogadishu, akieleza kutiwa wasiwasi na mashambulizi kadhaa yanayodaiwa na kundi la Al-Shabab tangu mwanzo mwa Ramadan. Nicholas Kay amesema, mwezi wa Ramadan ni mwezi wa amani na [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Syria hatarini wakati ufadhili ukididimia

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani wa Tartous, Magharibi ya Syria, ndio mamilioni ya waliopokea msaada wa UNHCR. Picha@UNHCR

   Hali ya kibinadamu ya wakimbizi wa Syria huenda ikazorota zaidi katika miezi michache ijayo wakati mashirika ya misaada yakikabiliwa na ugumu wa kupata fedha za kukidhi mahitaji yanayoongezeka, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR.  UNHCR imesema kuwa idadi ya wakimbizi katika ukanda mzima inatazamiwa kuongezeka hadi milioni 3.6 [...]

03/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM Masahriki ya Kati alaani mauaji ya kijana wa Kipalestina

Kusikiliza / Robert Serry, Mratibu maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu Mashariki ya Kati

  Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mashariki ya Kati Bwana Robert Serry amelaani vikali mauaji ya mvulana wa Kipalestina mnjini Jerusalem. Bwana Serry ameunga mkono ujumbe wa Katibu Mkuu Ban Ki-Moon unaosisitiza kuwa hakuna haki ya kumuua raia yeyote bila sababu. Amsema wote wanaohusika na mauaji hayo ya kinyama wanapaswa kuchukuliwa hatua, kulingana [...]

02/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Zerrougui afanya ziara ya kutathmini utumikishwaji watoto vitani Sudan Kusini

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Alipozindua ripoti ya mwaka kuhusu watoto na mizozo, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila Zerrougui, amesema kumeripotiwa visa vya utumikishwaji wa watoto katika majeshi 7 ya kitaifa, ikiwemo Sudan Kusini. Mwezi Juni, Leila Zerrougui alifunga safari ya kwenda Sudan Kusini ili atathmini hali ya utumikishwaji wa watoto [...]

02/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Somalia ipo kwenye njia panda : Ging

Kusikiliza / John Ging, Mkuu wa operesheni ndani ya OCHA alipozungumza na waandishi wa habari hii leo mjini New York, kuhusu ziara yake huko CAR. (Picha:UM/JC McIlwaine)

Taifa la Somalia lipo kwenye njia panda, huku hali ya kibinadamu nchini humo ikiendelea kuwa dhoofu. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni katika Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadam, OCHA, John Ging, wakati akikutana na waandishi wa habari mjini New York. Bwana Ging amesema ingawa kulikuwa na makubaliano ya ufadhili yaliyosainiwa mjini Brussels, Ubeljiji ya [...]

02/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

IOM yaanza kusambaza misaada kwa wakimbizi Pakistan

Kusikiliza / wakimbizi kutoka Waziristan waliotafuta hifadhi maeneo ya Khost, Pakistan. @UNAMA/Fardin Waezi

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeanza usambazaji wa mahitaji ya dharura kwa zaidi ya familia 130 za Kiafghanistan ambazo zimeingia mtawanyikoni kutokana na machafuko huko Pakistani kaskazini mwa Waziristan. Operesheni ya kijeshi inayoendelea kaskazini mwa Waziristan imesababisha maelfu ya raia waliokuwa wakiishi mpakani mwa Pakistan na Afghanistan kukosa makazi . Ripoti ya hivi karibuni [...]

02/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Rwanda kuongoza Baraza la Usalama Julai, ulinzi wa amani kuwekwa mbele

Kusikiliza / Balozi Eugène-Richard Gasana

Rwanda itaongoza Baraza la Usalama kwa kipindi cha mwezi mzima wa Julai. Mwakilishi wa kudumu wa nchi hiyo, Eugene Gasana, amesema kwamba urais huo utazingatia Ulinzi wa Amani, Rwanda ikiadhimisha mwaka huu miaka kumi tangu ilipoanza kuchangia katika jeshi la Ulinzi wa Amani la Umoja wa Mataifa. Katika muktadha huo, Rwanda imeamua kuandaa mjadala wa [...]

02/07/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Sri Lanka isitishe ghasia kwa msingi wa kidini: UM waomba

Kusikiliza / Heiner Bielefeldt,  Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na imani au dini. Picha@UN Photo/Paulo Filgueras

Wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa kuwa na dini na kuhusu masuala ya walio wachache wameiomba leo serikali ya Sri Lanka kuchukua hatua ili wasitishe ghasia zinazotekelezwa na vikundi vya wafuasi wa Budha wenye msimamo mkali dhidi ya jamii za Wakristo na za Waislamu. Wameomba wapelekwe mbele ya sheria. Zaidi ya visa 350 [...]

02/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Yemen kuna tatizo kubwa duniani lililofichwa: UM

Kusikiliza / Yemen. Picha@OCHA/Eman Al-Awami(UN News Centre)

Nchi ya Yemen imo katika hali mbaya ya kibinadamu, inayozidi hali za matatizo mengi duniani, wamesema leo wataalam wawili wa Umoja wa Mataifa wakizungumza na waandishi wa habari. Wamesema nchi hiyo imedhoofika sana, na mwelekeo si mzuri kutokana na viashiria mbalimbali. Mkuu wa operesheni wa ofisi ya usaidizi wa kibinadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OCHA, [...]

02/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yatiwa moyo na ahadi za serikali kupunguza vifo vya uzazi

Kusikiliza / Mama na mtoto wake aliyedhaifu wakitoka katika kituo cha afya cha UNICEF katika mkoa wa Maradi. Picha@ UNICEF/Olivier Asselin(UN News Centre)

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limeelezea matumaini yake ya kukabiliana na vifo vya kina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kutokana na msukumo uliotolewa na serikali katika kongamano moja la kimataifa lililomalizika huko Afrika Kusini. UNICEF imesema kuwa ahadi zilizotolewa na serikali ambazo zimesema kuwa zitaongeza [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa Sudan Kusini watoa wito kwa amani

Kusikiliza / Kundi la wakimbizi wa ndani wakiwemo wanawake na watoto wakipumzika katika eneo la Ethiopia baada ya kuvuka mto wa Baro kutoka Sudan ya Kusini. Picha: UNHCR/L.F.Godinho(UN News Center)

Wakimbizi wa Sudan Kisuni walioko nchini Uganda wamezungumuzia vita vinavyotokota nyumbani mwao. Wanaziomba pande zinazozozana kurudi kwenye meza ya mazungumzo ndio amani ipatikane, watoke ukimbizini. Taarifa kamili na John Kibego wa Radio wahsirika ya Spice fm, aliyetembelea kambi moja nchini humo.  (Taarifa ya John Kibego)

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IPU yalaani mauwaji ya vijana wa Israel, Palestina

Kusikiliza / mnembo wa IPU @IPU

Jumuiya ya Umoja wa Mabunge (IPU) imelaani vikali matukio ya mauaji ya vijana wa Kiisrael na Palestina na imetaka pande zote kutojiingiza kwenye mzozo zaidi kutokana na matukio hayo. Taarifa iliyotolewa na IPU, imesema kuwa imesikitishwa na kupokea kwa huzuni kubwa  taarifa hizo na kwamba wakati huu inaendelea kuwa bega kwa bega na wale waliofika [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP yasema operesheni zake Ethiopia zakabiliwa na uhaba wa ufadhili.

Kusikiliza / Picha@WFP/George Forminyen

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya kuwa shughuli za kuwahudumia wakimbizi nchini Ethiopia huenda zikakumbwa na hali ngumu katika kipindi cha kuanzia mwezi Septemba mwaka huu iwapo kutakosekana misaada ya dharura. WFP imesema kuna uwezekano mkubwa huduma zake nchini humo zikazorota iwapo hadi kufikia mwezi huo wa Septemba hakuna misaada yoyote itakayotolewa. Shirika [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Valerie Amos asikitikia taabu wanazopata raia wa Iraq

Kusikiliza / Picha ya UNHCR

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya misaada ya kibinadamu na uratibu wa mambo  ya dharura Valerie Amos ameelezea wasiwasi wake juu ya kuporomoka kwa ustawi wa kibinadamu nchini Iraq ambako hadi sasa watu zaidi ya milioni 1.2 wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano yanayoendelea. Taarifa kamili na George Njogopa [...]

02/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNEP yaanzisha mpango wa uzalishaji na utumiaji endelevu

Kusikiliza / Upandaji miti sahihi kwenye eneo husika hulinda mazingira halisi ya eneo hilo.@UNEP

Mpango mpya wa kuwawezesha wanunuzi kufanya maamuzi wanayoelewa wakati wanaponunua bidhaa za matumizi umezinduliwa leo, ukilenga kuhakikisha matumizi bora ya rasilmali. Mpango huo ambao umezinduliwa na Shirika la Mpango wa Mazingira, UNEP, utalenga kutoa maelezo kamili kwa wanunuzi kuhusu athari za kimazingira na kijamii za bidhaa wanazotumia, kama njia muhimu ya kuchochea mienendo endelevu zaidi [...]

01/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Jenerali Sakyi wa Ghana kuongoza ujumbe wa UM India na Pakistan

Kusikiliza / Picha@UNMISS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Jenerali Delali Johnson Sakyi wa Ghana kuwa Mwangalizi Mkuu wa Kijeshi na Mkuu wa Kundi la Umoja wa Mataifa la Uangalizi India na Pakistan (UNMOGIP). Meja Jenerali Sakyi ataichukua nafasi ya Meja Jenerali Young-Bum Choi wa Jamhuri ya Korea, ambaye amehitimisha huduma yake ya miaka miwili [...]

01/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Vifo kutokana na Ebola vyaongezeka hadi 467

Kusikiliza / Muuguzi akimuhudumia mgonjwa mwenye virusi vya Ebola. WHO/Chris Black

  Shirika la Afya Duniani, WHO, limesema kuwa kufikia Juni 30, idadi ya vifo vilivyotokana na mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola imepanda na kufikia watu 467, huku visa vya maambukizi ya virusi hivyo hatari katika nchi tatu zilizoathiriwa za Guinea, Liberia na Sierra Leone vikiwa sasa vimetimu 759. Idadi kubwa zaidi ya vifo hivyo imetokea [...]

01/07/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban alaani mauaji ya vijana wa Israel

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon. Picha@UN Photo

Mauaji ya vijana watatu wa Israel waliotekwa katikati mwa mwezi Juni kwenye Ukingo wa Magharibi, yamelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. Kwa mujibu wa duru za habari, wanajeshi wa Israel waliipata miili mitatu ya vijana hao kaskazini mwa Hebron, mnamo Jumatatu. Israel inaripotiwa kuanza mashambulizi ya angani kwa maeneo ya [...]

01/07/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watoto watumikishwa katika mizozo 23 duniani: UM

Kusikiliza / watoto waliotumikishwa kijeshi wakichora katika kituo cha UNICEF, Jamhuri ya Afrika ya Kati @UNICEF/Brian Sokol

Mwaka 2013, watoto wametumikishwa, na kuuawa, kulemazwa ama kubakwa katika mizozo 23 tofauti duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu illiyotolewa leo kuhusu watoto na mizozo. Akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo mjini New York, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Mizozo, Leila  Zerrougui, amesema kumeripotiwa visa vya [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Upandaji miti Bulengo..GOMA, DRC

Kusikiliza / Picha@MONUSCO

Paza sauti yako na si kiwango cha maji ya bahari, ni maudhui yaliyochaguliwa mwaka huu kwa ajili ya kulinda mazingira ya sayari ya dunia ili kuepusha nchi za visiwa vidogo kumezwa na maji ya bahari. Maudhui hayo yanatekelezwa kila kona ya dunia ikiwemo kwenye kambi za wakimbizi wa ndani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, [...]

01/07/2014 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UN, mashirika ya hisani yaanza kuwapiga jeki wakimbizi Pakistan

Kusikiliza / Watoto wakiwa Kaskazini mwa Waziristan, huko Pakistan. Photo: IRIN/Fakhar Kakahel(UN News Centre)

  Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo wameanza juhudi za haraka ili kuyakabili mahitaji muhimu kwa zaidi ya wakimbizi wa ndani 460,000 walioko maeneo ya kaskazini mwa Waziristani huko Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan. Imeelezwa kwamba zaidi ya asilimia 74 ya wakimbizi hao ni wanawake na watoto na kwamba baadhi [...]

01/07/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi 800,000 Afrika wakabiliwa na uhaba wa chakula

Kusikiliza / sudan msaada wa chakula

Takriban wakimbizi milioni moja barani Afrika wanakabiliwa na uhaba wa chakula kwa viwango vya kutia hofu, huku mashirika ya Umoja wa Mataifa yakihangaika kukidhi mahitaji ya chakula yanayozidi kuongezeka. Shirika la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na lile la Chakula Duniani, WFP, yameanza kupunguza kiasi cha chakula kinachotolewa kwa wakimbizi, hali ambayo yamesema ni hatarishi, hususan kwa [...]

01/07/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM wahimiza utulivu baada ya mauaji ya vijana Israel

Kusikiliza / Picha@Ravina Shamdasani/OCHR

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imepigwa na huzuni baada ya miili ya wavulana watatu wa Israel walioripotiwa kupotea hapo tarehe 12 Juni kupatikana wakiwa wameuawa katika Ukingo wa Magharibi. Ofisi hiyo imetoa rambirambi zake kwa jamii za wavulana hao na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahalifu wa mauaji hayo. [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki, Jarida | Kusoma Zaidi »

Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa auawa Mali

Kusikiliza / Walinda Amani wa MINUSMA @MINUSMA/Blagoje Grujic

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon amelaani vikali tukio la kuuawa kwa mlinda amani mmoja wa Umoja wa Mataifa katika shambulio la bomu nchini Mali hapo jana. Mlinda amani huyo kutoka Burkina Faso aliuawa na wengine sita kujeruhiwa maeneo ya Timbuktu, katika mlipuko wa bomu. Bwana Ban amepeleka rambirambi zake kwa familia [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi nne zaridhia mkataba kuhusu kutokuwa na utaifa

Kusikiliza / @UNHCR/ S. Boness

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR kwa pamoja na Ofisi ya sheria ya Umoja wa Mataifa, leo wanakutana kwa shughuli maalumu mjini Geneva ambako pia nchi za Ubelgiji, Gambia, Georgia na Paraguay zitajitokeza na kuridhia mkataba wa Umoja wa Maitaifa kuhusu watu wanaokosa utaifa. Taarifa kamili na Amina Hassan Taarifa ya Amina [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO, WHO yatoa orodha vyakula 10 vinavyoandamwa na wadudu

Kusikiliza / @FAO

Kumetolewa ripoti mpya inayoonyesha vyakula aina kumi duniani ambavyo ndani yake kunakutikana wadudu hatari wanaoweza kusababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu. Hata hivyo habari njema ni kwamba ripoti hiyo imebainisha mbinu za kukabiliana na wadudu hao wanaokaa ndani ya mimea.Taarifa zaidi na George Njogopa Taarifa ya George Imefahamika kuwa wadudu hao ambao wengi wao [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia wanaouawa Iraq yaendelea kupanda

Kusikiliza / wakimbizi wanaoendelea kukimbia mapigano Mosul @UNHCR Inje Colijn

Zaidi ya raia 2,400 wa Iraq waliuawa katika mwezi Juni pekee katika vitendo vya kigaidi na machafuko, kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, UNAMI. Taarifa kamili na Joshua Mmali Taarifa ya Joshua Idadi hiyo inajumuisha zaidi ya raia 1,500 na askari 800 wa vikosu vya usalama. Mji wa Baghdad ndio ulioathirika [...]

01/07/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031