Hafla ya kukaribisha michuano ya Kombe la Dunia yafanyika kwenye UM

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-Moon asaini mpira: Picha ya UM

Leo kwenye Umoja wa Mataifa, imefanyika hafla ya kukaribisha rasmi michuano ya Kombe la Dunia. Hafla hiyo iliyoandaliwa na ubalozi wa Brazil na ubalozi wa Uholanzi kwenye Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na Idara ya Habari ya Umoja wa Mataifa, imewaleta pamoja wawakilishi wa kudumu wa nchi 32 ambazo zinashiriki michuano ya Kombe la Dunia, wote wakiwa wamevalia sare za timu za nchi zao.

Katibu Mkuu Ban Ki-Moon ameongea wakati wa hafla hiyo, akiwachekesha waliokuwepo kwa kusimulia ustadi wake mwenyewe katika kucheza kandanda.

"Mie mwenyewe napanga kutizama michuano hiyo kadri niwezavyo. Baadhi yenu mnajua kwamba nimecheza kandanda mara kwa mara, na baadhi ya mabalozi walioko hapa leo. Hata niliuvunja mkono wangu wakati Fulani. Nadhani natakiwa kuacha kujaribu kucheza ule mtindo wa Pele wa 'bicycle kick'."

Bwana Ban pia ameelezea umuhimu wa michezo katika kuwaleta watu pamoja

"Mkusanyiko wetu hapa leo ni fursa ya kusherehekea maadili bora zaidi ya michezo: kuvuta pamoja, mchezo mwema na heshima kwa wote. Michezo ina uwezo wa kipekee wa kutuunganisha, na kutuonyesha ni nini tulicho nacho kinachofanana. Hakuna ushahidi dhahiri zaidi kuliko hafla ya leo. Ni nini kingine kinachoweza kuwafanya mabalozi kuvua suti na tai zao na kuvalia hivi?!"

Bwana Ban amezitakia timu zote zinazoshindana nchini Brazili kila la kheri.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031