Changamoto mpya ni kikwazo kwa ulinzi wa amani lakini hatukati tamaa: UNAMID

Kusikiliza /

Mkuu wa kikosi cha UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella. (Picha:Sojoud Elgarrai UNAMID).

Wakati maudhui ya siku ya ulinzi wa amani duniani hii leo ni Vikosi vya amani, vikosi vya mabadiliko, vikosi vya mustakhbali mwema, Mkuu wa kikosi cha ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, UNAMID Luteni Jenerali Paul Mella amesema ongezeko la uhalifu eneo hilo unakwamisha harakati za mustakhbali mwema kwa raia.

Luteni Jenerali Mella amesema hayo alipozungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa.

(Sauti ya Lt. Jenerali Mella)

Hata hivyo licha ya changamoto hizo amesema wana matumaini kutokana na hatua ya hivi karibuni ya serikali ya kuitisha mjadala wa kitaifa wakati huu ambapo makundi makubwa yanataka wigo wa mpango wa amani wa nchi hiyo upanuliwe na uhusishe nchi nzima badala ya kujikita kwa Darfur pekee.

(Sauti ya Lt. Jenerali Mella)

Mahojiano kamili na mkuu huyo wa kikosi cha UNAMID yatapatikana kwenye tovuti yetu.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031