Vijana hawataki msaada wanataka uwekezaji: Alhendawi

Kusikiliza /

Ahmed Alhendawi, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Imeelezwa kuwa masuala ya vijana yanafanana kote duniani bila kujali mahali wanakotoka, na wanchotaka vijana sio msaada bali ni uwekezaji utakaowapatia fursa ya kujenga maisha. Hayo yamesemwa na Ahmad Alhendawi  Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya vijana, wakati wa mkutano wa kamisheni ya Idadi ya watu na maendeleo unaojadili utekelezaji wa makubaliano ya Cairo miaka 20 iliyopita,mkutano ambao unaendelea hapa makao makuu New York.Alhendawi amesema maswala yaliyowasilishwa kwake na vijana yanajikita katika upatikanaji wa elimu kwa vijana ili waweze kuchangia katika maisha yao kiuchumi na kijamii na pia katika kushiriki katika ujenzi wa nchi huku akitolea wito ujenzi wa miradi ambayo itayowezesha vijana kushiriki

Ameongeza kwamba ni muhimu kujumuisha vijana katika kupanga, kutekeleza na kutathmini sera zinazolenga kuwanufaisha.

Halikadhalika amesema ni muhimu kutambua uwezo wa vijana na historia ili  kuwatambua kama wananchi muhimu katika kutekeleza maendeleo endelevu kwa sababu vijana sio tu kikundi cha watu lakini ni mali kubwa na fursa.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031