UM yataja wigo wa walinda amani MINUSCA na siri ya mafanikio DRC

Kusikiliza /

Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed

Jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani huko Jamhuri ya Afrika ya Kati litakuwepo maeneo yote tofauti na sasa na hivyo kudhibiti vitendo vinavyofanywa na vikundi vilivyojihami ikiwemo Anti-Balaka na Seleka vya ukatili kwa raia.

Amesema Mnadhimu Mkuu wa ofisi ya Kijeshi ya Idara ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa Brigedia Jenerali Ahamed Mohammed alipozungumza na Idhaa hii baada ya baraza la usalama kuunda mamlaka mpya ya Umoja huo nchini humo, MINUSCA.

Amesema hayo wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaripoti kuwa Anti-Balaka wanazuia na kushambulia raia wanaokimbiliaCameroonili kuokoa maisha yao.

(Sauti ya Brigedia Jenerali Mohammed)

Katika hatua nyingine mnadhimu huyo amesema mafanikio ya ulinzi wa amani huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, yametokana na kikosi cha kujibu mashambulizi cha MONUSCO kinachoudwa na askari kutokaAfrika Kusini,MalawinaTanzania.

(Sauti ya Brigedia Jenerali Mohammed)

Mahojiano kamili na Brigedia Jenerali Mohammed yanapitikana kwenye tovuti yetu.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031