FAO,WFP ,IFAD wazindua mkakati wa kilimo na chakula endelevu

Kusikiliza /

Vyakula tofauti sokoni

Mashirika ya chakula na kilimo lile la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD na mpango wa chakula duniani WFP, leo yamezindua matokeo ya ushirikiano wa mashirika hayo katika kuendeleza malengo na viashiria kwa ajili ya kielelezo cha maendeleo endelevu kimataifa katika kilimo, usalama wa chakula na virutubisho.

Taarifa ya pamoja ya mshirika hayo imeeleza kuwa hii ni hatua muhimu katika mchango wa mjadala wa kimataifa kuhusu ajenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ambayo yanatarajiwa kuchukua nafasi ya malengo yanayokamilika mwaka huo.

Malengo na viashiria hivyo yaliwasilishwa kwenye mkutano mkuu katika makao makuu ya WFP ambapo rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf alikuwa mgeni rasmi huku pia naibu waziri wa mamabo ya nje wa Italia Lapo Pistelli akihudhuria.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031