Afghanistan sasa inaandika historia: UNAMA

Kusikiliza /


Wakati wananchi wa Afghanistan kesho wanapiga kura katika uchaguzi wa Rais na viongozi wa majimbo, mwakilishi wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jan Kubis amesema historia imeanza kuandikwa.

Amesema historia inaandikwa kwani kwa mara ya kwanza mamlaka za uchaguzi nchini humo zikiwemo zile za serikali kuu na majimbo zinawajibika kwa asilimia mia moja na uratibu wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria iliyokubalika.
Kubis ambaye ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Afghanistan, UNAMA amesema ari imedhihirisha leo kwani ameshuhudia maandalizi ya vifaa kama inavyopaswa kuwa kwa maandalizi hayo.

Kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi, kampeni zilimalizika tarehe Pili Aprili baada ya wagombea 11 wa Urais kuanza kampeni zao tarehe Pili Februari ilihali waliokuwa wanawania nafasi za majimbo walianza kampeni zao tarehe Nne Machi.

Sambaza

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2016
T N T K J M P
« jul    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031