Nyumbani » 10/04/2014 Entries posted on “Aprili 10th, 2014”

Kuna mengi ya kujifunza, viongozi nchi zinazoendelea hukwamisha mipango miji: Mshiriki WUF7

Kusikiliza / Suzan Araka

Mmoja wa washiriki katika kongamano la saba la Kimataifa kuhusu Makazi ya Mijini, mshiriki kutoka Kenya Suzan Araka amesema kuna mengi ya kujifunza katika mji unakofanyika mkutano huo Medellin husuani suala la miundo mbinu ya barabara. Katika mahojino kwenye mabanda ya maonesho Bi Akara amesema kikwazo kikubwa katika upangaji bora wa miji katika nchi zinazoendelea ni [...]

10/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kila mtoto anastahili elimu bila kujali alipo: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akihutubia kwenye uzinduzi huo. (Picha-UM)

Asilimia 40 ya waliolazimika kukimbia makazi yao ni vijana na watoto barurabu na pindi wanapokumbwa na hali hiyo kiwango cha elimu yao hakiwezi kuzidi elimu ya msingi, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon huko Washington D.C wakati akizindua mpango wa dharura wa ushirika wa kuchukua hatua kwa ajili ya elimu. Ushirika huo [...]

10/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Viwango bora vya upangaji vinapaswa kuwanufaisha wote mijini, wasema washiriki kwenye WUF7

Kusikiliza / Mkutano wa miji nchini Colombia

Mipango ya kuendeleza miji inafaa kuwa ya mtazamo wa miongo mingi, huku ikizingatia viwango vya juu na uenezaji mzuri wa viwango hivyo kwa maeneo yote ya miji. Hayo yameibuka katika kuhitimisha mdahalo kuhusu upangaji na utungaji wa miundo ya miji kwa ajili ya utangamano wa kijamii, ambao umefanyika mnamo siku ya Jumatano, wakati wa kongamano [...]

10/04/2014 | Jamii: Hapa na pale, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Sekta ya kibinafsi inaweza kuchangia usawa mijini, wasema washiriki kwenye jukwa la Medellin

Kusikiliza / Patrick Magebhula

  Kikao cha saba cha Kongamano la Kimataifa kuhusu makazi ya mijini, kimeingia siku yake ya nne leo Alhamis, huku washiriki wakijadili mchango wa kampuni na biashara zinazomilikiwa na watu binafsi katika kufikia miji yenye usawa na endelevu kupitia utoaji wa huduma za kimsingi za mijini.. Wakati wa mijadala ya leo, washiriki wameelezea kutambua changamoto [...]

10/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu lapitisha azimio la kuimarisha usalama barabarani

Kusikiliza / Alama za barabarani kama zilivyo hizi nchini Hispania zinasaidia kupunguza ajail za barabarani. (Picha-Maktaba)

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio lenye lengo la kuimarisha usalama barabarani wakati huu ambapo takwimu za shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa watu 3,000 hufariki dunia kila siku duniani kutokana na ajali za barabarani. Shirika la afya duniani WHO linasema asimilia 80 ya vifo hivyo ni katika nchi za vipato vya kati [...]

10/04/2014 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mradi wa kunufaisha wananchi kupitia utalii wazinduliwa Tanzania

Kusikiliza / Dk Mukhisa Kituyi

Utalii ni sekta muhimu na kubwa  katika uchumi wa taifa la  Tanzania. Katika kuhakikisha kwamba sekta hii na sekta kama ya kilimo zinawanufaisha wananchi mradi mpya kwa ajili ya kuimarisha maisha ya watanzania kupitia utalii umezinduliwa. Mradi huu umafadhiliwa na Uswisi na uzinduzi umefanyika katika hoteli ya Kibo, Arusha nchini humo. Miongoni mwa waliohudhuria ni Mkurugenzi [...]

10/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu ya kinachoendelea Burundi: Ban azungumza na Marais wa Tanzania na Afrika Kusini

Kusikiliza / Stephen Dujarric

Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uzuiaji wa mauaji ya kimbari, Adama Dieng yuko nchini Burundi ikiwa ni sehemu ya harakati za Umoja huo za kuepusha mzozo utokanao na udhibiti wa shughuli za kisiasa na ripoti zinazodai kuwepo kwa mpango wa kuwapatia mafunzo na silaha vijana wa chama cha CNDD-FDD Msemaji [...]

10/04/2014 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Fahamu magonjwa ya homa ya ini, Hepatitis A na B.

Kusikiliza / hepatitis testing

WHO inasema mwongozo huo umezingatia tathmini ya kina na ushahidi wa kisayansi kwa hiyo watashirikiana na serikali kujumuisha muongozo huo katika mipango ya tiba ya kitaifa. Kutaka kufahamnu aina za magonjwa ya ini, Joseph Msami wa idhaa hii amefanya amahojino na mtaalamu wa ufuatailiaji na udhibiti wa magonjwa nchini Tanzania Dk Vida Makundi ambaye hapa [...]

10/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban apongeza kuidhinishwa kwa MINUSCA huku akipongeza MISCA

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon akiwa CAR akihutubia wakimbizi wa ndani Bangui wakati wa zaira yake nchini humo mapema mwezi huu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa namba 2149 lililoanzisha ofisi ya kuimarisha ya kuimarisha utulivu huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephen Dujarric amewaeleza waandishi wa habari kuwa Ban anaamini hatua hiyo muhimu itawezesha kuwapelekea wakazi wa [...]

10/04/2014 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakulima Tanzania wawezeshwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

Kusikiliza / Kilimo Tanzania

Mabadiliko ya tabia ya nchi yameleta madhara katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya kilimo ambapo katika kukabiliana na mabadiliko hayo mengi inabidi yafanywe ikiwamo kilimo mbadala. Katika makala ifuatayo Priscilla Lecomte anaangazia kile kinachofanyika nchini Tanzania katika kukabilina na mabadiliko ya tabia nchi katika kilimo

10/04/2014 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

UN wapongeza hatua ya serikali Mynamar kulaani vurugu Sittwe

Kusikiliza / Nembo ya Umoja wa Mataifa

Twapongeza hatua ya serikali ya Myanmar ya kulaani mashambulio dhidi ya ofisi za Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali huko Sitttwe nchini humo, amesema mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Renata Dessallien katika taarifa yake. Amesema hatua hiyo pamoja na ile ya kuunda haraka tume ya Rais ya kuchunguza tukio hilo [...]

10/04/2014 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Njaa na utapiamlo vyaikabili Sudan: FAO

Kusikiliza / Ukulima Sudan Kusini

Wakulima na wafugaji nchini Sudan wanahitaji msaada wa haraka ili kuwaepusha na njaa wakati huu ambapo hali ya usalama wa chakula nchini humo inazidi kuzorota, limesema shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO katika taarifa yake. FAO imeonya kuwa watu Milioni Tatu nukta Tatu nchini Sudan wanakabiliwa na ukosefu wa chakula na [...]

10/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mradi wazinduliwa Tanzania kuinua kipato cha mwananchi kupitia utaliii

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa UNCTAD, Dokta Mukhisa Kituyi

Nchini Tanzania, kumezinduliwa mradi mpya kwa ajili ya kuimarisha maisha ya wananchi kupitia utalii, mradi ambao unafadhiliwa na Uswisi na uzinduzi umefanyika mjini Arusha. Kupitia mradi huo wadau wageni watabadilishana mawazo kuhusu njia bora za kutekeleza mradi kupitia wadau wenyeji. Mkurugenzi Mkuu wa kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD, Dokta Mukhisa [...]

10/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu nusu milioni wameuwawa mwaka 2012: UNODC

Kusikiliza / Jean-Luc Lemahieu

Utafiti mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC inasema takribani watu nusu milioni waliuwawa mwaka 2012 ikiwa ni matokea wa uhalifu wa kimataifa . Utafiti huo uliozinduiwa leo mjini London unaonyesha kuwa watu zaidi ya laki nne walipoteza maisha huku UNODC ikisikitishwa na kukatishwa kwa maisha [...]

10/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha kulinda amani CAR

Kusikiliza / Waziri wa Mambo ya nje wa CAR Toussaint Kongo-Doudou akihutubia baraza baada ya azimio kupitishwa kwa kura zote 15.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuanzisha ofisi ya kusimamia utulivu na ulinzi wa amani Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati huu ambapo hali ya usalama nchini humo inazorota kila uchao na mapigano ya misingi ya kidini yakiendelea. Taarifa kamili na Assumpta Massoi. (Taarifa ya Assumpta) Kikao cha [...]

10/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa utashi wa kisiasa wakwamisha mipango miji nchi zinazoendelea

Kusikiliza / Moja ya mafanikio ya harakati za Kenya kuendeleza makazi mjini Nairobi

Kikwazo kikubwa katika mikakati ya kuendelezea miji miongoni mwa nchi zinazoendelea ni ukosefu wa utashi miongoni mwa viongozi. Akizunguzma katika mahojiano na Joshua Mmali wa idhaa hii mjini Medellin, Colombia kunakofanyika mkutano wa saba kuhusu mipango miji, mwakilishi wa serikali ya Kenya Suzan Araka amesema ukosefu wa utashi umesababaisha nchi zinazoendelea kushindwa kupiga hatua stahili [...]

10/04/2014 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO na wadau waimarisha jitihada za kudhibiti Ebola Guinea-Conakry

Kusikiliza / Harakati za kudhibiti Ebola nchini Guinea-Conakry. Picha @WHO

Jitihada za kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kwenye mji mkuu wa Guinea, Conakry zinaendelea ambapo vifaa zaidi vinaelekezwa eneo hiyo kwa ushirikiano wa shirika la afya ulimwenguni, WHO na wadau wake. Hatua hizo zinachukuliwa wakati hadi sasa watu 101 wamekufa kutokana na ugonjwa huo nchini humo huku 66 kati yao wakithibitishwa kufariki dunia kutokana [...]

10/04/2014 | Jamii: Ebola, Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930